Category Archives: Uncategorized

22-0918 Makao Ya Baadaye Ya Bwana Arusi Wa Mbinguni Na Bibi-Arusi Wa Duniani

UJUMBE: 64-0802 Makao Ya Baadaye Ya Bwana Arusi Wa Mbinguni Na Bibi-Arusi Wa Duniani

PDF

pakua – m4a

pakua – amr

BranhamTabernacle.org

Rafiki wapendwa kwa Nabii ,

Moyo wangu unabubujika kwa furaha ninapowazia kuhusu sisi kukusanyika pamoja Jumapili hii ili kusikia Sauti ya Mungu ikisema nasi. Hakuna furaha kubwa maishani mwangu kuliko kuwa katika uwepo wa Roho Mtakatifu na kumsikia akisema na Bibi-arusi Wake, mdomo kwa sikio.

Hakuna kitu kingine katika ulimwengu huu kinachonipa furaha na amani, ila Neno Lake. Ninaposikia tu, “Habari za Asubuhi Marafiki,” mimi huketi tu, nikastarehe, na kunywa kutoka kwenye Kisima hicho kinachofoka maji kikiniambia Maneno ya Uzima wa Milele. Kuwazia, Mungu alimtuma kwangu MIMI NA WEWE, nasi ni MARAFIKI wa nabii wa Mungu na mjumbe.

Anatupenda sana hivi kwamba Alimtuma nabii Wake atuambie yote yahusuyo Makao yetu ya Baadaye. Alifurahishwa sana kutuambia yote yahusuyo hilo, hata kwa undani zaidi kuliko alivyoambiwa Yohana. Ametufunulia, Si mji wenye umbo la mraba, bali ni mji wenye umbo la piramidi, ambako Mwana-Kondoo atakuwa juu yake na Nuru ya ulimwengu.

Anatujulisha barabara zitajengwa kwa dhahabu na nyumba tutakazoishi zitakuwa za dhahabu safi sana. Yeye anaweka kila kitu kidogo jinsi tunavyopenda hasa, jinsi tungetaka tu. Hajaacha kitu chochote. Mjenzi wa Kiungu ameubuni kwa ajili yetu SISI, Mpendwa wake.

Miti ya Uzima itakuwako kule, nayo itazaa aina kumi na mbili za matunda. Na hayo Malango ya mji hayatafungwa usiku, kwa maana hakuna usiku kule, Yeye atakuwa ndiye Nuru yetu.

Ni nani atakayekuwa kule?

Ni akina nani waliokuja kwenye nchi mpya pamoja na nabii Nuhu? Hao walioingia pamoja naye safinani. Hiyo ni kweli? Hao ndio wanaotoka na kutembea mle. Mnaona? Hao walioingia pamoja na Nuhu, kwa ujumbe wake, hao ndio waliotoka wakatembea juu ya nchi mpya baada ya ubatizo wake wa maji .

Anazungumza kuhusu SISI marafiki zangu! Tuko ndani ya Safina yetu ya siku hii; Neno Lake, Ujumbe Huu, pamoja na Nuhu wetu Nabii . Na huko ng’ambo katika Nchi hiyo, Mji ule ambako Mwana-Kondoo ndiye Nuru, yeye atatujua SISI. Sisi ni watu wake, vito katika taji yake. Tumetoka Mashariki na Magharibi, kuja kwenye mji uliojengwa mraba. Mji ule ambao Ibrahimu alikuwa anautafuta.

Huku nikiona Neno likijidhihirisha Lenyewe , ninajua, bila shaka hata kidogo, vito vya taji yangu vitang’aa kuliko kitu cho chote kile ulimwenguni, katika Siku ile.

Je! twaweza hata kuanza kuwazia… Nabii wa Mungu alisema, ALIJUA, bila shaka hata kidogo , ya kwamba SISI ni vito vya taji yake, na tutang’aa kuliko kitu chochote kile ulimwenguni katika siku ile . Haleluya… Utukufu…Jina la Bwana lisifiwe.

Marafiki, kama tunafikiri ni la ajabu, tukiketi pamoja kutoka kote ulimwenguni, tukisikiliza na kula Neno Lake katika kanda hizi, itakuwaje tutakapoishi katika mji ule pamoja Naye!

Nabii wa Mungu atakuwa jirani yetu wa karibu, na tutakapokula hiyo miti, na tutakapotembea kwenye barabara hizo, tutakapotembea kwenye barabara hizo za dhahabu kwenye chemchemi, kunywa kutoka kwenye chemchemi, kutembea katika paradiso za Mungu, huku Malaika wanarukaruka kuizunguka dunia, wakiimba nyimbo za sifa.

Loo, itakuwa ni Siku ya namna gani! Inastahili kwa vyote. Njia inaonekana inaparuza, wakati mwingine inakuwa ngumu, lakini, loo! itakuwa kitu kidogo sana nitakapomwona Yeye, kidogo sana. Vipi yale majina mabaya na mambo ambayo wao wamesema, hayo yatakuwa nini nitakapomwona Yeye katika Mji ule mzuri, mzuri sana wa Mungu?

Marafiki, siwezi kusubiri kuona, na kuwa katika mji ule. Ninatamani kuwa kule pamoja na Bwana na Mwokozi wetu, nabii Wake, na pamoja na kila mmoja wenu.

Ninaelekea kwenye Mji ule mzuri
Bwana wangu ameuandaa kwa walio Wake ;
Wakati wote Waliokombolewa wa nyakati zote Wataimba “Utukufu!”
Wakikizunguka Kiti Cheupe cha Enzi
Wakati mwingine ninatamani Mbinguni sana, Na utukufu nitakaouona kule
Itakuwa ni furaha jinsi gani nitakapomwona Mwokozi wangu ,
Katika Mji ule mzuri wa dhahabu!

Ninaualika ulimwengu uje kuungana na sisi, marafiki wa nabii, tunapokusanyika kukizunguka Kiti Chake cha Enzi ili kusikia Sauti ya Mungu ikisema nasi saa 6:00 SITA MCHANA , saa za Jeffersonville,( ni Saa 1:00 MOJA JIONI Ya Tanzania) tunapomsikia Yeye akituambia yote kuhusu : Makao Ya Baadaye ya Bwana Arusi wa Mbinguni na Bibi-arusi wa Duniani 64-0802 . Naweza kukuahidi, itakuwa Sikukuu katika maisha yako.

Ndugu. Joseph Branham

Maandiko ya kusoma kabla ya kusikiliza Ujumbe :

Mathayo Mt. 19:28

Yohana Mt. 14:1-3

Waefeso 1:10

2 Petro 2:5-6 / Sura ya 3 yote

Ufunuo 2:7 / 6:14 / 21: 1-14

Mambo ya Walawi 23:36

Isaya Sura ya 4 yote / 28:10 / 65:17-25

Malaki 3:6

22-0911 Mabirika Yavujayo

UJUMBE: 64-0726E Mabirika Yavujayo

PDF

pakua – m4a

pakua – amr

BranhamTabernacle.org

Wapendwa Wanywaji wa Maji ya Kisima Kinachofoka Maji.

Hatukupandikizwa, sisi ni sehemu ya uzao asili wa Neno. Roho Mtakatifu Mwenyewe, ameivisha, amethibitisha, na kujidhihirisha Mwenyewe kwetu. Tumelikubali kwa utimilifu Wake, kwa uwezo wa thibitisho lake na Ufunuo wa kile lilicho, nasi tumekuwa sehemu Yake. Ni zaidi ya uhai kwetu.

Roho Mtakatifu Mwenyewe alinena kupitia chombo kinyenyekevu, kisichostahili na kusema, “Hii hapa Fimbo Yangu ya kifalme , Neno Langu, lichukue, uende zako, na uupeleke Ujumbe.” Alichukua Neno Lake na kutubangua, kutufanya kuwa Bibi-arusi Wake.

Imewasumbua makasisi kuona watu wakitoka makanisani na kwenda kucheza kanda. Walisema, “Ikiwa yeyote wenu atahudhuria hiyo mikutano, utatupwa nje , tutakuweka nje ya shirika letu”.

Jibu lao ni: Mnaweza pia kutuachilia, tutaendelea hata hivyo! Tuko safarini pamoja na Bwana Yesu, Mwamba wetu uliopigwa, tukila Chakula cha malaika, mana iliyohifadhiwa ghalani kutoka juu, na kunywa kutoka kwenye Mwamba huo. Hatupaswi kamwe kuhangaikia kile tunachokunywa, Si chochote ila NENO SAFI.

Daima tumekuwa na uamsho unaoendelea. Chemchemi yetu daima inabubujika tena na tena, na tena na tena. Hakuna mwisho wake.
Tunapata kinywaji safi na baridi cha maji kila tunapobonyeza Play. Tunakitegemea na tunaishi kwacho. Jambo likupasalo kufanya tu ni kwenda kule na Unywe.

Tunaishi kwa chemchemi hiyo kila siku! Haitubidi kuvuta, kuchimba, kuvuta kwa mashine, au chochote kile; tunashiriki tu katika njia aliyoiandaa yeye , bure . Unaweza kuchukua taratibu zako zote zakujitengenezea unazotaka, visima vyako vyote vya kale vya maji yanayooza; kwetu sisi, tumekuja kwenye Chemchemi yake safi. Ni Furaha yetu. Ni Nuru na Nguvu zetu.

Yeye ndiye furaha yangu. Yeye ndiye Nuru yangu. Yeye ni—Yeye ni nguvu zangu. Yeye ni Maji yangu. Yeye ni Uzima wangu. Yeye ni Mponya wangu. Yeye ni Mwokozi wangu. Yeye ni Mfalme wangu. Kila ninachohitaji kinapatikana Kwake. Kwa nini niwe na hamu ya kukiendea kitu kingine?

Kwetu sisi hakuna mahali pengine pa kwenda ila moja kwa moja kwenye Chemchemi iliyotolewa na Mungu. Hatuna hofu kamwe tutakunywa nini. Haitulazimu kuweka kitambaa cha kale cha kuchujia ambacho kinaweza kutoa vitu vikubwa, lakini huacha juisi mbaya. TUNAPATA TU MAJI SAFI YA KISIMA KINACHOFOKA MAJI YENYE MADINI NA VIRUTUBISHO VYOTE TUNAVYOHITAJI.

Ametuhakikishia: Watoto wangu wachanga , msiwe na wasiwasi tena, mnao ushahidi wa kweli wa Roho Mtakatifu. Mmenithibitishia Mimi ya kwamba mnaamini kila Neno. Mmelipokea, NINYI NI WANGU. SISI NI KITU KIMOJA. MUME NA MKE.

Ninakuja kwa ajili yenu katika muda mfupi, katika kufumba na kufumbua jicho. Ninawaandalia Makao mapya. Mtapenda jinsi nilivyoyafanya.
Najua ni ngumu sana kwenu sasa, na mna mitihani mingi na majaribu na mizigo yenu ni mizito. Lakini msisahau, hamna chochote cha kuhofia , Nimewapa Neno Langu. Ninyi ni Neno Langu . Tayari nimefanya kila kitu kwa ajili yenu. Nena Neno na msiwe na shaka. Mnayo Imani yenu, pamoja na nabii Wangu aliwapa Imani yake.

Ningependa uungane nasi Jumapili hii saa 06:00 SITA MCHANA , saa za Jeffersonville, ( Ni saa 1:00 MOJA JIONI Ya Tanzania) kusikia 64-0726E Mabirika Yavujayo , na kunywa kutoka kwenye Chemchemi hii inayofoka maji inapobubujisha Neno Safi ambalo halihitaji chujio.

Ndugu. Joseph Branham

Maandiko ya kusoma kabla ya kusikiliza ibada

Zaburi 36:9
Yeremia 2:12-13
Yohana Mtakatifu 3:16
Ufunuo Sura ya 13 yote.

22-0904 Kutambua Siku Yako Na Ujumbe Wake

UJUMBE: 64-0726M Kutambua Siku Yako Na Ujumbe Wake

PDF

pakua – m4a

pakua – amr

BranhamTabernacle.org

Wapendwa Waliokatwa Watoke,

Nataka kila mtu ajue kwanini tunafuraha sana jinsi hii!!

Tumelikubali Neno la Bwana. Neno lililofunuliwa lililonenwa, na nabii wa Mungu wa Malaki 4. Sisi ni Bibi-arusi wa Yesu Kristo. Sisi Ndio ambao tumedumu waaminifu kwa Sauti Yake iliyothibitishwa. Sisi ndio ambao Aliyowapa Lulu ya thamani kuu, Ufunuo wa kweli wa Ujumbe Wake na mjumbe Wake.

Mungu amechukua Neno la nabii Wake na kumbangua Bibi-arusi anayeamini kila nukta na kila yodi. Ametukata, kama alivyoahidi atafanya. Sisi ni kondoo wa Mungu, na tunaisikia tu Sauti ya Mungu! “Kondoo Wangu huisikia Sauti Yangu,” tunapobonyeza Play.

Tuna Washiriki kutoka kote nchini; kutoka New York, kutoka Massachusetts, hadi Boston, Maine, Tennessee, Georgia, Alabama, na kote nchini. Kutoka Afrika hadi Mexico, Ulaya hadi Australia, tunakusanyika pamoja, chini ya Ujumbe Mmoja, Sauti Moja, nayo inamuunganisha Bibi-arusi kwa ajili ya Kunyakuliwa.

Nabii wetu, mjumbe wa Mungu, Mwana wa Adamu akijifunua Mwenyewe katika mwili, anapaza sauti, “Shetani, ondoka njiani, nina Ujumbe wa Mfalme. Mimi ni Mjumbe wa Mfalme. Nina Neno lililothibitishwa la siku hii. Nimekusudiwa kumwita Bibi-arusi Wake atoke na Kumwongoza.”

“Ninajaribu kuwavuta watu fulani, kuwakata niwaondoe kwenye mambo haya. kuwavuta watoke; kuwaonyesha, kwa Maandiko, ya kwamba Mungu amesimama hapa; pamoja na thibitisho la Nguzo ya Moto”

Mungu ametambua ya kwamba kuna watu fulani ulimwenguni ambao aliwakusudia Uzima. Alitambua ulikuwa ni wakati wa kumtuma mjumbe Wake kumwita Bibi-arusi Wake atoke, Hivyo Yeye Akamtuma . Sisi Ndio wale Waliotambua jambo hilo. Sisi ndio wale Aliojua tungeamini kila Neno.

Ibrahimu alitambua ya kwamba Mungu alikuwa akisema naye katika mwili wa Kibinadamu. Alitambua ishara Yake na kumwita B-W-A-N-A, Elohim, na akabarikiwa na Bwana. Tumetambua ya kwamba kama ilivyokuwa katika siku hiyo, ndivyo itakavyokuwa wakati Mwana wa Adamu atakapodhihirishwa, Elohim, akinena katika mwili wa kibinadamu.

Sisi ni sehemu yake, na Mwanawe, na tutadumu naye milele. Si kwa wito wetu au uchaguzi wetu, bali kwa uchaguzi wake. Hatukuwa na uhusiano wowote nalo. Yeye ndiye aliyetuchagua kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu.

Haidhuru utahubiri namna gani, hata ufanye nini, haliwezi kuivishwa, haliwezi kudhihirishwa, haliwezi kuthibitishwa; ila tu na Yeye aliyesema, “Mimi Ndimi Nuru ya ulimwengu,” lile Neno. Kwa hiyo hakuna budi kutokee Nguvu fu—fu—fulani, Roho Mtakatifu Mwenyewe, kuivisha, ama kuthibitisha, ama kuhakikisha, ama kudhihirisha ya kwamba yale ambayo Yeye amebashiri yangetukia katika siku hii. Nuru ya jioni inaleta hilo. Ni wakati wa jinsi gani!

Alituona katika lile ono tulipokuwa tukipita mbele yake. Tulipitia mahali pale pale alipopitia Bibi-arusi wakati alipopitia hapo mwanzo, Alfa na Omega. Alikuwa akiangalia wengine wakitoka mstarini, na alikuwa akijaribu kumvuta , lakini sisi ndio Wale tuliopaza Sauti, “Tunategemea jambo Hilo.”

Angalia, “Kama vile Yane na Yambre pia walivyompinga Musa,” yeye atakuja moja kwa moja, baadhi yao . Si , sasa, yeye hazungumzi kuhusu Mmethodisti, Mbaptisti, hapa; wao wako nje ya picha . Unaona? “Lakini kama vile Yane na Yambre walivyoshindana na Musa na Haruni, vivyo hivyo hao nao; watu walioharibikiwa na akili zao kuhusu ile Kweli.” wamepotoka wakaingia katika mafundisho ya sharti na mafundisho ya kanisa, badala ya Biblia.

Jinsi inavyotupasa kuwa waangalifu sana kudumu na Neno la kweli, lililothibitishwa la siku yetu. Ni lazima kila wakati tukumbuke na kutambua Neno humjia nani. Ni nani aliye mfasiri pekee wa kiungu wa Neno? Ni nani Aliye Neno la siku yetu ?

Roho wa Mungu, ambaye ni Neno la Mungu, “Neno Langu ni Roho na Uzima,” litamweka Bibi-arusi mahali Pake. Kwa maana, Yeye Atatambua nafasi yake katika Neno, ndipo anakuwa ndani ya Kristo, litamweka kwenye nafasi yake .

Umealikwa kuja kusikiliza Sauti pekee ya Mungu iliyothibitishwa ya siku yetu, na kutambua nafasi yako katika Neno na kuwekwa mahali pako tunapomsikia Elohim akisema kupitia nabii Wake na kutuletea Ujumbe: Kutambua Siku Yako na Ujumbe Wake 64-0726M , saa 06:00 MCHANA , saa za Jeffersonville (Ni Saa 1:00 MOJA JIONI Ya Tanzania.)

Ndugu. Joseph Branham

Maandiko ya kusoma kabla ya kusikia Ujumbe:

Hosea: Sura ya 6 yote

Ezekieli: Sura ya 37 yote

Malaki: 3:1 / 4:5-6

2 Timotheo: 3:1-9

Ufunuo: Sura ya 11 yote

Mungu, umba ufufuo ndani yangu! Jalia niwe huo ufufuo. Jalia kila mmoja wetu awe huo ufufuo, ufufuo ndani yangu. Nifanye mimi, Bwana, nipate njaa, nifanye nione kiu. Umba ndani yangu, Bwana, kile ambacho kinahitajika ndani yangu. Nijalie, tangu saa hii na kuendelea, niwe wako; mtumishi aliyewekwa wakfu zaidi, mtumishi bora, aliyebarikiwa zaidi na Wewe; mwenye uwezo zaidi, mnyenyekevu zaidi, mwema zaidi, mwenye kupenda kufanya kazi zaidi; mwenye kuangalia zaidi mambo ambayo ni ya kweli, na kusahau mambo yaliyo nyuma, na mambo yasiyo ya kujenga. Jalia nikaze mwendo kuelekea kwenye mede ya wito mkuu wa Kristo. Amina.

Rev. William Marrion Branham

22-0828 Kuenda Nje Ya Kambi

UJUMBE: 64-0719E Kuenda Nje Ya Kambi

PDF

pakua – m4a

pakua – amr

BranhamTabernacle.org

Wapendwa Wana Tai ,

Hebu na tukusanyike pamoja Sote na kusikia Ujumbe 64-0719E Kwenda Nje ya Kambi Jumapili hii saa 06:00 SITA MCHANA , saa za Jeffersonville. ( Ni saa 1:00 MOJA JIONI Ya Tanzania)

Ndugu Joseph Branham

22-0821 Sikukuu Ya Baragumu

UJUMBE: 64-0719M Sikukuu Ya Baragumu

PDF

pakua – m4a

pakua – amr

BranhamTabernacle.org

Mpendwa Bibi-arusi wa Kubonyeza Play,

Kila Jumapili tunakusanyika na kusikiliza Huduma kuu iliyo hai katika historia ya ulimwengu. Tunapata wakati mtukufu zaidi tunapokutana pamoja ili kusikia Sauti ya Mungu! Ni Yesu, Mwana wa Mungu, akijifunua Mwenyewe kwa Maandiko, akilifanya andiko hilo ambalo limechaguliwa tangu zamani kwa ajili ya Siku siku hii, kama ilivyokuwa katika siku Yake, na siku Zingine zote, LIISHI. Na Kuamini Hilo, ndio Dhihirisho la kuwa una Roho Mtakatifu .

Dhihirisho la kweli la kuwa na Roho Mtakatifu sio ati kwenda kanisani kila Jumapili; Ni kwamba unaamini ya kwamba “Mimi Ndiye ,” Neno la Siku yako. Neno la Siku hii ni nini? Nabii wa Mungu ndiye Neno la Siku hii naye anapaswa kuwarudisha watu kwenye Neno, ili kwamba Bibi-arusi amjue Mumewe, amjue Mwenziwe, Neno lililofunuliwa.

Maisha yake mwenyewe, kazi zake mwenyewe, hufunua na kulithibitisha Neno la Siku hii.

Ni Roho Mtakatifu aliyerudi tena Kanisani; Kristo, Mwenyewe, aliyefunuliwa katika mwili wa mwanadamu, wakati wa jioni, kama tu alivyoahidi angefanya. Ninajua kwa namna fulani hilo linawakaba wao kidogo, lakini lazima usome katikati ya mistari na kuona, hiyo inafanya ile picha ije.

Sisi ni Uzao wa Kifalme wa Ibrahimu, Bibi-arusi. Ishara ya mwisho ambayo Ibrahimu aliwahi kuona kabla ya mwana aliyeahidiwa kuja ilikuwa ni nani? Mungu, katika umbo la mwanadamu, ambaye aliweza kuyatambua mawazo ya watu. Mtu mmoja, sio dazani, mtu mmoja.

Najua watu wengi hawakubaliani na jambo hilo, bali najua ndilo hili. Najua jambo hilo. Si kwa sababu ninasema mnalisema; kwa sababu, sikulitoa kwangu mimi. Ma—mawazo yangu si yangu mwenyewe . Cho chote kile kilichoniambia jambo hilo, kama kimekosea, basi kimekosea. Bali sisemi jambo hili kwa nafsi yangu, ninasema yale Mtu mwingine amesema. Mtu huyo mwingine ni Mungu aliyenena nasi na kufanya mambo haya yote ambayo amefanya, na akajitokeza, mnaona, kwa hiyo mimi najua ya kwamba ni kweli.

Tunasikiliza wazo lenyewe la Mungu; si mawazo ya mwanadamu, bali ya Mungu. Nabii wetu ndiye mfunuzi wa Neno lililoandikwa.

Tunaelewa kwamba kuzicheza kanda majumbani mwenu ama makanisani mwenu si kwa kila mtu, bali ni kwa ajili Yetu , Ndiyo NJIA PEKEE. Tunapenda kusikia Sauti ya Mungu ikizungumza nasi moja kwa moja. Hatuhitaji fasiri au ufafanuzi wowote; ni Mungu akisema Nasi mdomo kwa sikio .

Jumapili hii tutakuwa tukimsikia Mungu akisema na kutuambia jinsi alivyomwonyesha nabii wake sisi katika onyesho la awali ng’ambo ya pili. Jinsi Bibi-arusi huyo alivyokuwa akimtazama yeye moja kwa moja, akizungumza naye, nasi tulikuwa tumesimama pamoja naye. Tulikuwa tukitembea kikamilifu mbele za Bwana.

Kisha Mungu anazungumza kupitia nabii wake na kutabiri kwa mara nyingine tena na kusema:

Yawezekana kuwe na baadhi huko nje katika mataifa, ulimwenguni kote, ambao hata kanda hii ingewakuta manyumbani mwao au makanisani mwao. Tungeomba, Bwana, kwamba wakati ibada inaendelea, pale—pale…au kanda inachezwa, au nafasi yo yote tunayoweza kuwamo, au—au hali, yule Mungu mkuu wa Mbinguni na aheshimu huu unyofu wa mioyo yetu asubuhi hii, na kuponya wahitaji, kuwapa wao yale wanayohitaji.

Kama unazisikiliza hizo Kanda, na kuamini kwamba ndizo
Sauti ya Mungu kwa ajili ya wakati wetu, basi chochote unachoweza kuwa unakihitaji, Mungu atakuwa akizungumza kupitia mjumbe Wake na kusema, “ Wape chochote tunachohitaji .

Hilo linaweza kutukia tu kwa KUBONYEZA PLAY rafiki yangu.
Ikiwa ungependa kumsikia Mungu akinema na kufasiri Neno Lake Mwenyewe, akijifunua Mwenyewe kupitia mwili wa mwanadamu, na upokee chochote unachohitaji, njoo uungane nasi Jumapili saa 06:00 SITA MCHANA , saa Jeffersonville,( Ni Saa 1:00 MOJA JIONI Ya Tanzania) tunapomsikia Mungu akisema nasi tunaposikia: Sikukuu ya Baragumu 64-0719M .

Ndugu. Joseph Branham

Maandiko ya kusoma kabla ya kusikiliza Ujumbe:

Mambo ya Walawi Sura ya16 yote

Mambo ya Walawi 23:23-27

Isaya 18:1-3

Isaya 27:12-13

Ufunuo 10:1-7

Ufunuo 9:13-14

Ufunuo 17:8

22-0814 Kile Kipeo

UJUMBE: 64-0705 Kile Kipeo

PDF

pakua – m4a

pakua – amr

BranhamTabernacle.org

Mpendwa Kipeo,

Nawezaje kuwaandikia leo bila kuwakumbusha kile ambacho mchungaji wetu alichosema kuhusu kila mmoja wetu Jumapili iliyopita?

Bali kujua ya kwamba mahali po pote niwezapo kwenda…sina ku—kundi fulani ulimwenguni , nilijualo, linaloshikamana nami kama kundi hili. Mungu na—na ajalie tuwe wasioweza kutengana sana, hata, katika Ufalme ujao, naomba kwamba tuwe huko pamoja; ombi langu.

Hakuna kundi duniani linaloshikamana na nabii wa Mungu, na Ujumbe ambao Mungu alionena kwenye kanda, kama sisi. Na kwa sababu tunafanya hivyo, tutakuwa tusioweza kutengana katika Ufalme ule mpya pamoja naye na Bwana wetu Yesu Kristo. Haiwi bora zaidi ya hapo!

Hizi ni siku kuu sana za maisha yetu. Tumeridhika kabisa kuwa mpumbavu wa Kristo na Ujumbe Wake wa wakati wa mwisho. Kuitwa nati kwa sababu tunaamini kila Neno kwenye kanda hizo na kusema, BONYEZA PLAY.

Sisi ni Washiriki wa Lile Kanisa Moja la Pekee. Hatukujiunga Nalo, tulizaliwa ndani Yake. Kila wiki tunakusanyika pamoja kutoka ulimwenguni kote na kuendeleza mapenzi na Kristo na kusema, “Loo, jinsi ninavyokupenda ‘Jesu!’”

Tunaweza kuwa nati kwa ulimwengu, lakini Baba ametupa Ufunuo Wa yeye Mwenyewe katika wakati wetu, Mungu mwenye ngozi, na imetuvuta, Bibi-arusi Wake, Kwake.

Tunapenda tu jinsi lilivyo rahisi, lakini wakati huo huo, jinsi tu lilivyo la Kilindi. Lakini yakupasa uwe na Ufunuo upate kuliona, Nasi TUNAO.

Alijificha Mwenyewe katika utaji wa binadamu, katika Kanisa Lake, akijifunua Mwenyewe kwa imani yako na imani yangu, pamoja, kutuunganisha pamoja, tukifanya umoja wa Mungu. Mimi siwezi kufanya kitu bila ninyi; ninyi hamwezi kufanya kitu bila mimi; hakuna anayeweza kufanya kitu bila Mungu. Kwa hiyo, sote pamoja linafanya kitu kimoja, ule muungano. Mungu alinituma kwa kusudi hilo; mnaamini jambo hilo; na hapa linatendeka. Ndilo hilo hasa, mnaona, limehakikishwa kikamilifu.

Sisi ni Kama wale watu wakitembea barabarani kutoka Emau siku ile. Tunamsikiliza Yeye akizungumza nasi sote wakati wa mchana. Kisha tunamwalika ndani ya nyumba zetu ili tuweze kujifungia pamoja Naye peke yake. Ndipo anafanya jambo fulani awezalo yeye tu kulifanya, kuumega Mkate wa Uzima wa Milele. Tunamtambua papo hapo. Kisha tunasema, je mioyo yetu haikuwaka ndani yetu alipokuwa akisema nasi njiani.

Kila Wiki tunakusanyika kwa matarajio makubwa, tukijiuliza, “Atatuambia na kutufunulia nini wiki hii”. Tutatumiana nukuu mmoja kwa mwingine na kuzungumzia hilo wiki nzima. “Je, ulimsikia aliposema”:

“Ilinichukua miaka elfu nne kukitengeneza Kipeo Changu; lakini sasa imenichukua karibu miaka elfu mbili kutengeneza Kipeo kingine, Wewe, Bibi-arusi Wangu. Ninakitengeneza kwa njia Yake isiyobadilika , namna ile ile nilivyokitengeneza Kipeo Changu cha kwanza, Neno Langu. Hivyo ndivyo ninavyojitengenezea Vipeo Vyangu , kwa kuwa unaweza tu kuwa Kipeo kikamilifu wakati linapokuwa ni Neno kamilifu.”

Ndugu yangu, usione hili kuwa baya, lakini waza kwa dakika moja. Kama Yeye alitoa Kwake, kile kiumbe cha asili, ili amtengenezee Bibi-arusi, Yeye hakuumba kiumbe kingine; Yeye alichukua sehemu ya ule uumbaji asili. Basi kama Yeye alikuwa Neno, Bibi-arusi anapaswa kuwa nini? Hana budi kuwa Neno la asili, Mungu Aliye Hai katika Neno.

Nena kuhusu yubile ya mlo bora. Sisi ni sehemu ya uumbaji wa asili. Sisi ni sehemu ya Neno la asili. Mungu anaishi ndani yetu. Sisi ni Kipeo Chake. Sisi ndio kundi lile linaloshikamana na nabii Wake. Sisi ni wasioweza kutengana na nabii Wake na Bwana Yesu Kristo. Sisi ni MMOJA Na Yeye.

Kama nawe pia ungependa moyo wako uwake ndani yako kama unavyowaka ndani yetu, njoo uungane nasi Jumapili hii saa 06:00 SITA MCHANA , saa za Jeffersonville,( ni Saa 1:00 MOJA JIONI Ya Tanzania), Wakati sehemu ya Bibi-arusi inapokusanyika Pamoja na kumwalika Yeye Majumbani mwetu, na katika makanisa yetu, tunapomsikia Mungu akisema Nasi na kutufunulia Maneno ya Uzima wa Milele, anapotuletea Ujumbe: Kile Kipeo 64-0705 .

Ndugu. Joseph Branham

Maandiko ya kusoma kabla ya ibada:

Isaya 53:1-12
Malaki 3:6
Mathayo Mt 24:24
Marko Mt 9:7
Yohana Mt 12:24 / 14:19

22-0807 Wa Kipekee

UJUMBE: 64-0614E Wa Kipekee

PDF

pakua – m4a

pakua – amr

BranhamTabernacle.org

Mpendwa Bibi-arusi wa Utukufu wa Shekina,

Jinsi gani mioyo na nafsi zetu zilivyoinuliwa hadi kufikia viwango vipya tulipokuwa tumekusanyika pamoja kutoka duniani kote, tukisikiliza Sauti ya Mungu ikizungumza kupitia mjumbe Wake na kutuhakikishia kwa mara nyingine tena, sisi ni nani.

Naye Anajifunika leo, katika vyombo vya udongo, pamoja na Shekina. Nje wanaonekana kana kwamba ni kundi la watakatifu wanaojifingirisha, ngozi za kale za pomboo, lakini ndani yake zinaficha Utukufu wa Shekina.

Utukufu kwa Mungu! Ndani yetu unajificha Utukufu wa Shekina. Tumeenda nyuma ya pazia nasi tunaweza kumwona Kristo waziwazi.

Leo hii, Mungu hatendi kazi akiwa ndani ya mwanadamu, Anatenda kazi kupitia mwanadamu. Yeye Alikuwa akitenda kazi akiwa katika mwanadamu wakati huo, Yesu. Sasa, Yeye anatenda Kazi kupitia mwanadamu ambaye yeye amemchagua kwa kusudi hili. Mungu, katika umbo la mwanadamu; Yeye Alijibadilisha kutoka katika umbo la Mungu, akawa katika umbo la mwanadamu.

Mungu Mwenyewe alijitokeza katika umbo la mwanadamu , kwa uzao wa kawaida wa Ibrahimu, kabla ya yale maangamizi, na Yesu alisema litakuwa ni jambo lile lile kwa Uzao huu wa kifalme kabla ya kurudi kwa Mwana aliyeahidiwa.

Mungu amejitokeza kwa mara nyingine tena katika umbo la mwanadamu, kama alivyoahidi angefanya. Ni Mungu aliyefichwa nyuma ya pazia la mwili uitwao William Marrion Branham. Isipokuwa uende nyuma ya pazia hilo na kuona Mungu, na si mwanadamu, umeukosa mpango wote wa Mungu.

Baadhi ya watu husema, “Ninyi watu mnamfanya Ndugu Branham kuwa mungu”. Vema, jambo hilo liko sawa kwa Namna fulani . Tunajua wanajaribu tu kutulaumu. Tunajua sisi hatukufanya hivyo. Bali pia tunajua hawalifahamu hilo, kwa maana wao wako upande wa pili wa ngozi, hawajaja nyuma ya pazia.

Tunaweza kusema waziwazi, “Vema, jambo hilo haliko mbali sana na Neno la Mungu sivyo? Tunawataka tu wajue kwamba hatujapotea. Tunajua tunaposimama. Tunajua tumetweka matanga ya namna gani, Na ni upepo wa namna gani unaoyavumia. Tunajua Hesi zetu zilivyo, na Nati yetu ni ipi . Nasi tunajua jinsi tunavyosimama.

Mungu alipodhihirishwa ulimwenguni, Yeye alikuwa amejificha nyuma ya pazia, nyuma ya ngozi ya Mtu aliyeitwa Yesu. Yeye alikuwa ametiwa utaji na kujificha nyuma ya ngozi ya mtu aliyeitwa Musa, nao walikuwa miungu, si Mungu ; bali walikuwa Mungu, yule Mungu mmoja, akibadilisha kinyago Chake tu, akifanya jambo lile lile kila wakati, akileta Neno hili.

Tumeingizwa kwenye Neno, Ujumbe na nabii wa wakati huu, na unatuvuta na kutupeleka kwenye Makao yetu ya Mbinguni. Sisi ni Wa Kipekee kwa ulimwengu, lakini Mungu ametutumia Nati ambayo inamtoa Bibi-arusi Wake atoke katika mchafuko huu, imwingize katika Uwepo wa Mungu. Sisi ni nati tuliyotiwa hesi kwa Neno.

Mungu, aliye na ngozi! Linaweza likasikika kama nati, kwa ulimwengu, bali linawavuta watu wote Kwake.

Ujumbe huu ni Mana itokayo Mbinguni, Chakula cha waamini ambacho ni kwa ajili yetu tu, nacho Kinamvuta Bibi-arusi Wake Kwake. Utukufu wa Shekina, juu ya Mkate wa Wonyesho, uliufanya usiharibike.

Mungu ameandaa Njia kwa ajili ya siku hii, Ujumbe huu na mjumbe wake; Mungu aliyefunikwa Aliye na ngozi . Sasa ni Mungu akijificha Mwenyewe ndani yetu, Bibi-arusi Wake, anayeweza tu kujilisha Sauti safi ya Mungu iliyothibitishwa na Nguzo ya Moto.

Sisi Hatupingani na huduma tano, Mungu apishe mbali, Mungu amewaita kuhudumu. Wanafuata na kufanya jinsi Roho Mtakatifu anavyowaongoza. Na sisi Tunafanya tu jinsi Roho Mtakatifu anavyotuongoza kufanya naye anatuongoza na kutuelekeza kushikilia hizo kanda peke yake.

Kwa hiyo, sasa , sikiliza kila Neno . Likamate. Na—na iwapo mnaunasa Huo kwenye kanda, ama cho chote kile , basi shikilieni kabisa Mafundisho hayo ya kanda . Msiseme kitu ila kile kanda hiyo inachosema. Semeni tu yale hasa kanda inayosema .

Kwetu sisi, NJIA PEKEE YA KUSIKIA: “KILA NENO,” “ SI KINGINECHO BALI YALE KANDA ZINACHOSEMA,” “ YALE HASA KANDA ZINACHOSEMA,” NI KUBONYEZA PLAY NA KUZISIKILIZA KANDA.

Kwa hiyo tunakualika uje kusikiliza yale hasa kanda zinachosema Jumapili saa 06:00 SITA MCHANA , saa za Jeffersonville, ( Ni saa 1:00 MOJA JIONI Ya Tanzania) na uwe Wa Kipekee pamoja nasi tunaposikia Ujumbe: Wa Kipekee 64-0614E .

Ndugu. Joseph Branham

Maandiko ya kusoma kabla ya kusikiliza Ujumbe :

I Wakorintho 1:18-25
2 Wakorintho 12:11

22-0731 Kufunuliwa Kwa Mungu

UJUMBE: 64-0614M Kufunuliwa Kwa Mungu

PDF

pakua – m4a

pakua – amr

BranhamTabernacle.org

Mpendwa Neno lililoandikwa,

Kila wiki inakua kuu zaidi na zaidi. Jumapili, tulipata fursa ya kutazama, na kuamua, TULIONA NINI? Je, tuliona mhudumu , HAPANA! Je, tuliona mchungaji wetu, HAPANA! Tulipotazama nyuma ya pazia la mwili wa mwanadamu tulimwona Yesu Kristo akijifunua Mwenyewe na kujidhihirisha Mwenyewe.

Wakati tumekuwa tukizisikiliza hizo kanda kama zijavyo, Imekuwa dhahiri zaidi na zaidi, kama unayo masikio ya kusikia na macho ya kuona. Sasa tunamwona Mungu waziwazi. Pazia limepasuka, nasi tunamwona Mungu akisimama waziwazi mbele zetu, Yule Nguzo ya Moto Akijidhihirisha Mwenyewe waziwazi.

Imewapofusha wengine, Lakini kwetu sisi, Imefunua ile Kweli. Mungu amemtukuza mjumbe wake mbele zetu, kama alivyomtukuza Musa.

Hamko nyuma ya pazia hilo tena, enyi Watoto wadogo. Mungu anaonekana wazi kabisa kwenu.

Ni kitu gani? Uungu uliofunikwa katika mwili wa mwanadamu. Mungu, katika umbo la mwanadamu, akijificha Mwenyewe wasimwone. Wanaweza tu kumwona mwanadamu na kusema Nabii wa Mungu anakosea, hata alisema hivyo yeye mwenyewe, akijaribu kuwafundisha watu ya kwamba kuna makosa kwenye hizi kanda . Lakini kwetu sisi, Bibi-arusi Wake Aliyechaguliwa tangu Awali, tunamwona Mungu na kumsikia na hakuna makosa.

Mmoja aliona mwanadamu, huyo mwingine alimwona Mungu. Unaona? Na ilikuwa ni Mungu nyuma ya pazia la mwanadamu, ikiwafanya wote wawili kuwa sahihi, lakini imani yako katika yale usiyoyaona.

Kwetu sisi, tutaamini na kufuata makosa ya nabii wa Mungu aliyethibitishwa, kama kungekuwepo na yoyote , kabla hatujachukua na kuamini Bwana Asema hivi yao.

Musa hakupaswa kuupiga Mwamba mara ya pili. Roho yuleyule angalisema katika siku hiyo, “Ona, Musa anakosea.” Lakini maji yalitoka hata hivyo, na ikiwa hukunywa kutoka kwenye kile kinachoitwa kosa la musa, ulikufa. Ndivyo ilivyo leo hii. Mashtaka mengi sana.

Musa alikuwa na Neno. Sasa kumbukeni, baada ya Neno kudhihirishwa, Musa alikuwa ni Musa tena. Mnaona? Lakini wakati Neno hilo lilipokuwa ndani Yake lipate kutolewa, yeye alikuwa ni Mungu; vema, yeye hakuwa ni Musa tena.

Ndugu Branham alikuwa na Neno. Baada ya Neno kudhihirishwa, Ndugu Branham alikuwa Ndugu Branham tena, Lakini wakati Neno hilo lilipokuwa ndani yake lipate kutolewa kwa watu kwenye kanda, yeye alikuwa ni Mungu; hakuwa Ndugu Branham. Hivyo tunajifunza, yaliyo kwenye hizi kanda ni Maneno ya Mungu, na hakuna makosa katika Maneno ya Mungu.

Sisi sio tu kwamba tunaliamini, bali tunaliishi. Wakati hao wengine wote wanaliondokea, sisi tunadumu Nalo! Tunaliamini! Haijalishi kile mtu ye yote anachofanya ama anachosema , sisi tunaliamini na kisha tunalitendea kazi. Kama wewe hufanyi hivyo, basi huliamini.

Nasema vivyo hivyo katika Jina la Yesu Kristo. Usiongeze kitu. Usiondoe—kuliwekea mawazo yako. Wewe sema tu yaliyosemwa katika kanda hizo. Tenda sawasawa kabisa na vile Bwana Mungu amekuamuru kutenda. Usiongezee Kwake!

Bonyeza play na uamini KILA NENO kama vile Mungu alivyotuamuru kutenda. Ni Mungu akinena mdomo kwa sikio na Bibi-arusi Wake.

Mbele za watu, Mungu alijitia utaji tena na kumthibitisha Musa, kwa utaji, kwa kujitia utaji kwa Moto ule ule, Nguzo ile ile ya Moto ilishuka. Tangu—tangu wakati huo…Kutoka kwao, kwa hiyo wangeweza tu kusikia Neno la Mungu. Mnalipata? Neno pekee, waliisikia Sauti Yake. Kwa kuwa, Musa alikuwa, kwao, Neno lililo hai .

Mungu habadilishi, na hawezi kubadilisha mpango Wake. Yeye Ni Yesu Kristo yeye yule jana, leo na hata milele. Kwa hiyo, kwetu sisi, nabii Wake aliyethibitishwa, William Marrion Branham ndiye Sauti yetu ya Mungu, na Neno lililo Hai la wakati wetu.

Sasa si Neno tu lililoandikwa kwetu, ni kitu halisi. Tuko ndani Yake. Sasa tunafurahia. Sasa tunamwona Yeye. Sasa tunamwona, lile Neno, akijidhihirisha Mwenyewe. Limefichwa, huko nje, kwa sababu (kwa nini?) Limetiwa utaji katika mwili wa binadamu. Mnaona?

Haidhuru nini, wao hawalioni. Kwa nini? Haikutumwa kwao .

Kwa sababu unaliona, je, uko tayari kumsikia yeye akikuambia kwa mara nyingine tena WEWE NI NANI? Anapotazama chini kutoka kwenye ngome za Utukufu na kukuona, Yeye Anamwona nani?

* Ninaona Neno likidhihirishwa. Yale aliyosema angeyafanya katika siku hizi za mwisho, ninaliona likikua. Ninaona watoto wakila huo Mkate wa Shekina unaotoka kwenye kule kuiva kwa hilo Neno, ambao wanaliamini. Amina!

* Basi, sisi, ndipo tunakuwa sehemu Yake, kwa kuwa wewe ni utaji unaomficha Yeye. Wewe ni sehemu Yake, mradi Kristo yumo ndani yako, kama vile Kristo alivyokuwa wa Mungu. Kwa kuwa Mungu alikuwa ndani Yake, ilimfanya Mungu. Na kwa kuwa Kristo yumo ndani yako, tumaini la Utukufu, unakuwa sehemu ya Kristo.

* “Ninyi,” Hilo lilisema, “ninyi ni nyaraka zilizoandikwa,” ama, “ninyi ni Neno, ambalo limeandikwa, lililodhihirishwa,” hakuna kitu kinachoweza kuongezewa Kwake. Huwezi kusema, “Mimi ni waraka ulioandikwa,” na kuishi namna nyingine mbali na vile Hii imeandika tayari, kwa maana hakuna kitu kinachoweza kuongezwa wala kuondolewa .

Jina la Bwana Yesu Kristo litukuzwe. YEYE ANATUONA SISI. SISI TUNAMWONA YEYE. Sisi ni Neno Lake lililodhihirishwa leo hii.

Njoo uungane nasi Jumapili saa 06:00 SITA MCHANA , saa za Jeffersonville, (Ni Saa 1:00 MOJA JIONI Ya Tanzania), Mungu akisimama mbele zetu; ile Nguzo ya Moto ikiwa imefichwa katika mwili wa mwanadamu, nayo inazungumza nasi Neno tunalopaswa kuishi kwalo katika siku hii. Ni Utukufu wa Shekina unaotuivisha. Mkate wa Wonyesho kwa mwamini.

Kufunuliwa Kwa Mungu 64-0614M

Ndugu. Joseph Branham

Maandiko ya kusoma kabla ya kusikia Ujumbe:

Mathayo 24:24
Luka Mtakatifu 17:28-29
Yohana Mtakatifu 14:14
1 Wakorintho 12:13
2 Wakorintho 3:6 – 2 Wakorintho 4:3
Wafilipi 2:1-8
1 Timotheo 3:16
Waebrania 13:8
Ufunuo 10:7 & 19:13
Kutoka sura ya 19 yote & sura ya 20 yote
Yoeli 2:28
Malaki 4:5

22-0724 Tazama Aliko Yesu

UJUMBE: 63-1229E Tazama Aliko Yesu

PDF

pakua – m4a

pakua – amr

BranhamTabernacle.org

Wapendwa Nuru Zilizodhihirishwa,

Hebu sote na tukusanyike pamoja na kusikiliza Ujumbe 63-1229E Tazama Aliko Yesu Jumapili hii saa 6:00 SITA Mchana , saa za Jeffersonville.( Ni saa 1:00 MOJA jioni ya Tanzania).

Ndugu Joseph Branham

Maandiko ya kusoma ili kujitayarisha kusikia ujumbe :

Hesabu 21:5-19

Isaya 45:22

Zekaria 12:10

Yohana Mtakatifu 14:12

22-0717 Yupo Mtu Hapa Anayeweza Kuiwasha Taa

UJUMBE: 63-1229M Yupo Mtu Hapa Anayeweza Kuiwasha Taa

PDF

BranhamTabernacle.org

Mpendwa Sura ya Yesu Kristo,

Kama yule mvulana mdogo aliyejitazama kwenye kioo na asitambue kwamba alikuwa akijiangalia mwenyewe, sasa tunatazama katika Kioo cha Mungu, Neno Lake, na tunatambua, BABA, HUYO NI MIMI, Mimi ni Sura ya Neno Lako. Mimi ni Neno Lako lililodhihirishwa. Mimi ni mwamini, mimi ndiye Bibi-arusi Wako!

Kila Ujumbe tunaosikia huinua Imani yetu hadi viwango vipya. Alituambia lazima tujitokeze katika mojawapo ya makundi matatu: Waamini, waamini wakujifanya au wasioamini. Tulipotazama kwenye kioo Chake tulipaza sauti, “Naona, bila kivuli cha shaka, sisi ndio Waamini. Hakika Mwamini ndiye atakayeamini kila nukta na kila yodi; BABA, HUYO NI MIMI.”

Hakuna kitu kinachoweza kuturidhisha na kutupa Uzima ila Neno la Mungu lililonenwa kwenye kanda. Ndiyo njia pekee Uzima unapoweza kuja, kupitia Neno Lake lililonenwa, Sauti ya Mungu kwa ajili ya wakati wetu.

Jitayarishe, kuna mengi zaidi yajayo Jumapili hii, Julai 17, 2022. Kuna mtu hapa ambaye atakaye iwasha Taa, na atakapofanya hivyo, sote tutakuwa na maumivu ya koo kwa kupiga kelele na kupaza sauti, Amina, Haleluya, Jina la Bwana lisifiwe, Utukufu kwa Mungu, kwa sababu Mungu Mwenyewe atakuwa akizungumza nasi moja kwa moja na kulifunua zaidi Neno Lake.

Kama vile lile jua linaloangaza leo litaivisha nafaka kwa ajili ya mavuno mwezi wa Julai. Mwaona ninayomaanisha? Bali Nuru ya leo haitafaa lolote kule nyuma Julai . Ina nguvu zaidi ; ngano imeendelea zaidi. Iko tayari kulipokea. Amina! Hakika iko hivyo .

Mavuno yameiva! Tumeendelea zaidi na tayari zaidi kulipokea. Yesu ana meza iliyotandazwa, ambapo watakatifu wa Mungu wanalishwa kwa Chakula kilichoiva cha siku hii. Nuru ya Injili ikithibitisha na kuhakikisha kwamba Yeye yuko hapa leo pamoja nasi. Watakatifu wanakula Chakula cha kiroho ambacho kimehifadhiwa, wakijiandaa kwa ajili ya Unyakuo.

Wakati Mchungaji wetu, Roho Mtakatifu anapozungumza kupitia kwa nabii Wake aliyethibitishwa, anabonyeza swichi hiyo na kuwasha nuru ya Ufunuo, Yeye atatuambia Yeye ni nani hasa katika wakati wetu. Atapaza sauti na kutuonya,
Natumaini hamjalala.

Nuhu alikuwa Nuru katika siku yake. Musa alikuwa ni Nuru ya saa yake, sasa Nimewatumia nabii mwenye Nguvu katika Wakati wenu, nami ninalidhihirisha Neno Langu lililoahidiwa kupitia kwake. Yeye ni Neno la Mungu lililodhihirishwa katika siku yenu. Yeye ndiye Nuru ya Wakati huu.

Nilipokuwa hapa duniani katika mwili mara ya mwisho, nilichukua ile mikate mitano ya shayiri na kuanza kuimega ile mikate. Kutoka ile ya asili, nilitengeneza mikate na kuwalisha elfu tano.

Kisha nikapata samaki, na kutoka kwa samaki huyo, nikafanya samaki mwingine na samaki mwingine, nikawalisha elfu tano.

Lakini Katika wakati wako, sikuwa na kitu. Nilinena tu na kusema , “Sema itakuwepo,” na ilikuwa pale, bila kuwa na kitu. Yeye alinena tu na kusema, “Sema itakuwapo!” na ilikuwa pale bila kuwa na kitu. Sikuwa na kindi; hapakuwa na mmoja pale. Yeye alisema tu, “Wawepo!” wakawa! Neno Langu haliwezi kukosea na Lazima litimie.
.

Kama wana wa Israeli, walipokuwa safarini, walikuwa wakila mana mpya kila siku. Walikuwa wakitembea katika Nuru ya Nguzo ya Moto. Hiyo Nguzo ya Moto ilikuwa ni Yesu Kristo.

Leo yuko pamoja nasi kwa mara nyingine tena, Nguzo ile ile ya Moto, akifanya mambo yale yale ambayo Yeye alifanya alipokuwa hapa duniani akilitimiza Neno Lake.

Tunakualika uungane nasi Jumapili saa 06:00 SITA MCHANA, saa za Jeffersonville, ( ni saa 1:00 MOJA JIONI ya Tanzania) wakati mchungaji wetu, Roho Mtakatifu, ile Nguzo ya Moto, anapowasha Nuru Yake ya Ufunuo, tunaposikia : 63-1229M “Yupo Mtu hapa Anayeweza Kuiwasha Taa “.

Ndugu. Joseph Branham

Maandiko ya kusoma kabla ya ibada ni:

Mwanzo 1:3, Sura ya 2 yote

Zaburi 22 yote
Yoeli 2:28
Isaya 7:14, 9:6, 28:10, 42:1-7

Mathayo 4:12-17, Sura ya 24 yote na Sura ya 28 yote

Marko Mtakatifu Sura ya 16 yote.

Ufunuo Sura ya 3 yote