Category Archives: Uncategorized

26-1011 Kimo Cha Mtu Mkamilifu

Ujumbe: 62-1014M Kimo Cha Mtu Mkamilifu

PDF

BranhamTabernacle.org

Mpendwa Kimo cha Mtu Mkamilifu,

Ni mafunzo jinsi gani ambayo tumekuwa nayo. Sauti ya Mungu imekuwa ikinena na kutufundisha, Neno kwa Neno kwa Neno, jinsi ya kumshinda kabisa kila adui. Yeye ametufunulia na kutia nanga mioyoni mwetu, SISI NI NENO. Kwa hivyo, hatuwezi kushindwa.

Wakati adui anapotufuatia, sisi tunampiga tu na kumpiga tena na tena kwa bomu letu la atomiki, Neno Lililonenwa la Mungu, ambalo huishi na kukaa ndani yetu.

Kweli, vita viko tayari, bali sasa hatuna hofu tena; hakuna wasiwasi tena. Hatuzisikilizi dhamiri zetu. Hatuzisikilizi kumbukumbu zetu. Hatuyasikilizi matakwa yetu. Tumezifunga akili zetu kwa mambo haya na kuweka Roho wa Neno Lake mioyoni na rohoni mwetu. Tumekilipua kila kitu kilicho kinyume na Neno Lake.

Kila shaka imetoweka. Kila hofu imetoweka. Kila hisi ya shaka imetoweka. Kila hisi imetoweka. Hakuna kitu kinachosimama hapo ila Neno la Mungu linaloishi na kukaa NDANI YETU, naye Shetani hawezi kupigana na Hilo.

Tunafanyika Maskani iliyo hai ya Mungu aliye hai. Ni Mungu akiishi ndani yetu, akitufanya tufanane na Yeye, akiuakisi Utu Wake ndani yetu.

Tunapachukua mahali pa Kristo, tukiiendeleza huduma Yake. Yeye anaishi katika umbo la mwanadamu kama Yeye anavyojiakisi ndani yetu. Sasa tunayo ibada kamilifu pamoja Naye! Ni Mungu akijidhihirisha ndani yetu, tukiwa Maskani Yake.

Ni upi msingi wetu usiotikisika wa kuyaamini mambo haya? IMANI. Nayo imani yetu haihitaji chochote; kwa maana imani yetu inaliamini Neno la Mungu. Kwa maana imani huja kwa kusikia, na kusikia Neno la Mungu, nalo Neno la Mungu huja kwa nabii peke yake, na tunaweza tu KUMSIKIA nabii kwa Kubonyeza Play…PIGA!!

Kwa kuisikiliza Sauti Yake, tumwekwa kwa mrija Wake wa kutilia Nguvu Zake nasi tumekufa kwa mawazo yetu wenyewe. Imani yetu imekuwa imani halisi, nao Uhai Wake umewekwa ndani yetu. Tumekuwa viumbe hai vya Mungu, makao ambapo Roho Mtakatifu anaweza kutuma miali ya baraka Zake za upendo kupitia humo.

Sauti hiyo iloyo kwenye kanda inafanya nini?

Kristo alinituma kuwajenga watu binafsi wafikie kiwango cha Yesu Kristo, kusudi wapate kuwa kituo cha nguvu na makao ya Roho Mtakatifu, kwa Neno Lake. Kwa Neno Lake, unaona, kumjenga mtu binafsi afikie mahali hapo.

Kwa kuisikia Sauti Yake, na kuamini na kulifuata Neno Lake, imetujenga kufikia vimo vya Yesu Kristo; makao ya Roho Wake. Sisi ni nguvu hai, maarifa hai, saburi hai, utauwa hai, Nguvu iliyo hai, zitokazo kwa Mungu aliye hai, zinatufanya kuwa mtu aliye hai, sanamu hai, katika kimo cha Mungu.

Lakini Mwili uliniwekea tayari,” Mwili ambao Mungu anaweza kuishi ndani yake, Mungu anaweza kutembelea, Mungu anaweza kuona nao, Mungu anaweza kuzungumza humo, Mungu anaweza kufanya nao kazi. Amina! Chombo kilicho hai, Mungu, Mungu akitembea kwa miguu miwili, ndani yako. Utukufu! “Hatua za mwenye haki huongozwa na Mungu,” Mungu akitembea ndani yako. “Kwa maana ninyi ni waraka uliandikwa, unaosomwa na watu wote.”

Utukufu…!!! Kwa hivyo, hatujali kama tunaishi katika hema au kibanda, tuishi ama tufe, tuzame au tufe maji. Jambo hili ndilo tu tunalotaka, UJUMBE HUU, SAUTI HII, NENO LA MUNGU. Ndio Ufalme wa Mungu. Ndio njia ya Mungu iliyoandaliwa ya siku hii. Inajenga Kimo cha Mtu Mkamilifu, ambaye NDIYE SISI!

Hebu na tukutanike pamoja na kuyachunguza maisha yetu tunapomsikia Mwalimu wetu akitufundisha kile tunachopaswa kufanya, na jinsi gani tunavyopaswa kuishi, ili kufanyika wana na binti za Mungu W-A-K-A-M-I-L-I-F-U

Tutamwahidi Bwana kwamba kwa msaada Wake na kwa neema Yake, tutamwomba na kumtafuta Yeye kila siku bila kukoma, mpaka tutakapojisikia kila moja ya mahitaji Yake yanatiririka katika miili yetu. Tutakaa hapo mpaka tuweze kuwa dhihirisho la Kristo aliye hai.

Kila wiki msisimko na matarajio kwa yale Bwana atakayofanya na kutufunulia sisi yapita maneno kuelezea. Jinsi gani ninavyotaka ulimwengu mzima uungane nasi kwani hakuna kitu kilicho kuu zaidi, au kikamilifu zaidi kuliko kukaa katika uwepo wa Sauti ya Mungu na kuwa Kimo Kikamilifu cha Bibi-arusi Neno Wake Mkamilifu.

Ndugu Joseph Branham

Ujumbe: Kimo cha Mtu Mkamilifu 62-1014M

Muda: saa 6:00 MCHANA Masaa ya Jeffersonville, IN.

Maandiko:

Mathayo Mtakatifu 5:48
Luka Mtakatifu 6:19
Yohana Mtakatifu 1:1 / 3:3 / 3:16 / 5:14 / 14:12
Matendo 2:38 / 7:44–49 / Sura ya 10 / 19:11 / 28:19
Waefeso 4:11-13
Wakolosai Sura ya 3
Waebrania 10:5 / 11:1 / 11:32-40
Yakobo 5:14
2 Petro Mtakatifu 1:1-7
Isaya 28:19

26-1004 Vita Vikuu Sana Vilivyowahi Kupiganwa

Ujumbe: 62-0311 Vita Vikuu Sana Vilivyowahi Kupiganwa

PDF

BranhamTabernacle.org

.

Wapendwa Akina Mikaya,

Vile vita vikuu sana vilivyowahi kupiganwa sasa viko tayari kuanza. Mungu amekuwa akiwachagua wanajeshi Wake wa hali ya juu kwa zaidi ya miaka elfu sita, nawe ulikusudiwa kimbele na kuchaguliwa kuwa katika Jeshi Lake Kuu.

Yeye amekuwa akikuvisha, na kukupa mafunzo, nao uwanja wa vita sasa umewekwa tayari, unajiandaa kuanza. Sio tu kwamba Yeye alikuchagua kuwa katika Jeshi Lake Kuu, bali Yeye amekuteua wewe kuwa Mikaya nabii katika jeshi Lake.

Wakati umefika, siku yenyewe imefika; utapokea mafunzo moja kwa moja kutoka kwa Nguzo ya Moto Mwenyewe ili kumshinda kila adui. Utapokea maagizo maalum, Neno kwa Neno, juu ya nini cha kufanya ili kuangamiza kabisa kila roho mchafu. Itaupeperusha kila ugonjwa na kila pepo anayekuja mbele yako. Hakuna kinachoweza kusimama mbele yako.

Baada ya mafunzo haya maalum, utakuwa umewekewa ngome mno kwa Neno Lake kiasi kwamba utauondoa uovu wote. Tupilia mbali hoja. Tupilia mbali ushirikina. Tupilia mbali wasiwasi. Tupilia mbali magonjwa. Tupilia mbali dhambi. Utaelewa uko juu yake, umefufuka katika Kristo Yesu, umeketi katika ulimwengu wa Roho na kila pepo akiwa chini ya miguu yako. Utaelewa kikamilifu na KUAMINI wewe ni Neno.

Yeye atawapa mafunzo ya lipi la kuwa nalo macho. Atawafundisha kwamba ikiwa adui yako anaweza kukufanya uamini Silaha yako haina nguvu vya kutosha, yeye atakupokonya silaha.

Lakini tutayakumbuka mafunzo yetu, enyi askari, na kumwambia huyo shetani: Sio sisi, sisi si kitu. Silaha yetu ni Neno la Mungu nalo litamshinda KILA PEPO, wakati wowote, mahali popote, kwa sababu ni NENO LAKE, NAYE ALITUPA MAFUNZO NA KUTUFUNULIA KWAMBA SISI SASA NI NENO LAKE LILILOFANYIKA MWILI. HIVYO, hatuwezi kushindwa, sisi ni jeshi LA MUNGU lisiloshindwa.

Moja ya siku zilizo kuu mno katika historia ya ulimwengu inaenda kutukia Jumapili hii. Akina Mikaya Wake wataungana pamoja kutoka kote ulimwenguni chini ya Sauti ya Jenerali wao mkuu, ambapo tutaungana pamoja hasa kwa nia moja, bila hata chembe moja ya shaka popote.

Kisha, ikiwa tu tutaamini, NASI TUNAAMINI, hakutakuwa na mtu dhaifu ulimwenguni kote. Ikiwa tukiweza tu kurekebisha jambo hilo fulani, hakutakuwa na mtu anayemtamani Roho Mtakatifu ila yule ambaye angempokea, nako kutakuwa na uponyaji wa ghafla wa roho na mwili, ikiwa tutashikilia tu nafasi zetu. Huu ndio wakati wenyewe. Sisi ndio watu hao. Roho wa Mungu ameinua beramu dhidi ya kila pepo; sisi ni MMOJA WAO na hakuna kinachotuzuia!!

Tumekufa kwa dhamiri zetu, tumekufa kwa hoja zetu, tumekufa kwa mambo yote hayo. Maisha yetu yamefichwa nasi tumezikwa katika Jina la Yesu Kristo, na kufufuliwa pamoja Naye. Na po pote alipo Yeye, hapo ndipo nasi tulipo pia.

Tumedonoa tukatoka, ewe shetani, kwa kukulipua kwa, “BWANA ASEMA HIVI. BWANA ASEMA HIVI. BWANA ASEMA HIVI.” Hatimaye tunainusa hewa safi. “BWANA ASEMA HIVI.” Sisi hawa hapa tunakuja shetani, tumetokeza vichwa vyetu nje. “BWANA ASEMA HIVI, UMESHINDWA.”

Tunamshinda shetani kwa kitu gani?

Neno!
Hebu na tuseme; Neno! Neno! NENO!!

MAAGIZO ZAIDI YA MAFUNZO

Sasa wakati adui anaposhambulia na kujaribu kusema ati unapaswa kufanya hivi, unapaswa kufanya vile, wewe hufai, hustahili, hujapona, bado ungali una matatizo yako yale yale. Utafanya nini?

Ondoka kwangu.” Mpige dharuba! Kisha umkate kwa Neno. Iwe ni pepo; iwe ni adui; iwe ni maradhi; iwe ni ugonjwa; cho chote kile; chukua hilo Neno ulivute kwa Upanga, na kama ukilipiga dharuba mara ya kwanza nalo halielekei kusogea, lipige dharuba tena, na ulipige dharuba tena, na ulipige dharuba tena!

Tunalikubali tu Neno kwa msingi wa, “Mungu alisema hivyo,” na hilo linafanya kijito kati yetu na Yeye. Kila mkondo umefunguka kati yetu. Tunasema, “Sijui ni lini nitalipata, bali nitalipata. MUNGU ALISEMA HIVYO. Kila shaka IMETOWEKA…hata tunatilia shaka mashaka yetu.”

Tunampinga shetani na kulichukua Neno la Mungu. Ikiwa najisikia hisi fulani, au bila hisi, haijalishi kinatokea nini, Mungu alisema hivyo. Hilo latosha.

Yafuateni maagizo haya, enyi askari, kwa kina. Yarudieni Maneno haya wakati adui anaposhambulia. Si Maneno yenu, ni MANENO YAKE YEYE, NA MANENO YAKE HAYAWEZI KUSHINDWA. Yeye ametupa uwezo wa kulitumia Neno Lake kwa kutufanya sisi kuwa Neno Lake. Wakati Shetani anaposhambulia, msomeeni maagizo yenu.

MAAGIZO YA JENERALI WETU

Hiki ndicho hasa ninachowataka mfanye.

Rudia kiapo hiki na uamini kila Neno kwa ajili ya ukombozi mkamilifu.

Shetani, simile; ninatoka humu ndani; silali hapa tena; sikai hapa tena; siko kwenye ardhi hii ya ibilisi ya kale tena; ninadonoa nipate njia ya kutoka asubuhi hii! Amina! Mimi ni tai!” Amina! Haleluya!

Kisha nakutaka ufanye hivi:

Kulilipua na BWANA ASEMA HIVI. BWANA ASEMA HIVI. BWANA ASEMA HIVI.”

Fungua akili yako, useme, “Neno Lako ni Kweli.”

Bwana, sitajali jinsi ninavyojisikia, jambo mtu mwingine asemalo; ninafunga, ninasafisha kila moja ya njia zangu. Mahangaiko yote, na mashaka, na kutokuamini ambako nimepata kuwa nako; kila kuhisi ulikowahi kuwa nako; maradhi yote niliyowahi kuwa nayo; kila kitu kingine nilichopata kuwa nacho; ninavitupilia vyote nje; ninavipuuza vyote na kuja moja kwa moja kwa Roho yangu.

IMANI yako itaanza kupanda juu zaidi na zaidi. Kisha mwambie Yeye, “Ee Bwana, shuka; Wewe ulisema, Wewe ulinifanya mimi mtu mwenye hiari.”

“Ndivyo ulivyo, Mwanangu.”

Sawa, ninafungua moyo wangu na akili yangu.

“Karibu, Bwana Yesu.”

Uinyakue ile imani, Upanga wa Roho, BWANA ASEMA HIVI!

Piga kelele, Haleluya! Amina!

Kisha katilia mbali kila adui aliye mbele yako. Amina. Jambo ndilo hilo. Kata kila adui. Iwapo pe—pepo mchafu wa kale anakufanya ujisikie…Katilia mbali kitu hicho kwa Neno la Bwana.

MAAGIZO YAKO YA MWISHO EWE ASKARI.
MWAMBIE ADUI:

“Ondoka kwangu.” Mpige dharuba!

Kisha umkate kwa Neno.
Iwe ni pepo; iwe ni adui; iwe ni maradhi; iwe ni ugonjwa; cho chote kile; chukua hilo Neno ulivute kwa Upanga: na kama—kama ukilipiga dharuba mara ya kwanza nalo halielekei kusogea, lipige dharuba tena, na ulipige dharuba tena, na ulipige dharuba tena! Na ulipige dharuba mpaka umetoboa tundu, kama kifaranga mdogo akijitokeza mwenyewe nje; au tai, ndivyo ulivyo. Jitokeze moja kwa moja kutoka hilo gamba la kale la maradhi, fyeka upate njia ya kutokea, kisha useme, “Haleluya! yuko wapi mwingine?” Amina! Hivyo ndivyo vita; huyo ndiye askari. Huyo ndiye askari wa msalaba. Ndiyo, bwana!
Mtupilie nje kila adui. Kwa nini? Kwa nini?

Sisi ni Mzao wa Kifalme wa Ibrahimu uliochaguliwa tangu awali.

Utukufu, kila adui ameshindwa. Hakuna kitu CHOCHOTE kinachoweza kusimama mbele ya Neno la Mungu, nasi ni Neno la Mungu. Sisi ndio Uzao Wake wa Kifalme na kila ahadi ni YETU.

Siku hiyo imefika, Bibi-arusi anaamini kila Neno naye analitendea kazi. Tumejiweka wenyewe tayari kwa kulisikia na kuliamini Neno Lake.

Kama unahitaji chochote, kama unataka kujazwa na Roho Mtakatifu, kama unataka kuponywa, kama unataka kila pepo atolewe, kama unataka kuwa Bibi-arusi wa Kristo, huu ndio wakati, kuisikia na kuiamini Sauti Yake ndio mahali penyewe.

Ikiwa una haja ya mambo haya na unataka kuwa katika uwepo wa Bwana, karibu zaidi kuliko ulivyowahi kuwa, njoo uungane nasi Jumapili saa 06:00 MCHANA, masaa ya Jeffersonville, [ni saa 1:00 JIONI ya Afrika mashariki–Mh] wakati Jenerali wetu mwenye nyota nne anapomwelekeza Bibi-arusi Mikaya Wake mwenye nguvu jinsi ya kumshinda kila pepo, kila adui, kuwekwa huru, na kujazwa na Roho Wake Mtakatifu, na kuwa tayari kwa ajili ya Kuja Kwake hivi karibuni.

Ndugu Joseph Branham

Ujumbe: Vita Vikuu Sana Vilivyowahi Kupiganwa. 62-0311

Maandiko:
1 Petro 5: 8-10
Waefeso 6:10-17
Danieli 12: 1-7

26-0927 Mungu Aliye Mwingi Wa Rehema

Ujumbe: 65-0119 Mungu Aliye Mwingi Wa Rehema

PDF

BranhamTabernacle.org

.

Wapendwa Mawazo Ya Mungu,

Ninyi ni Neno la Mungu lililodhihirishwa lile lililoahidiwa kwa ajili ya siku hii. Daima mlikuwa. Si kwamba mtakuwa, bali ninyi sasa hivi ni wana na binti za Mungu;, kwa maana Mungu, aliye mwingi wa rehema, alikuwa na wewe katika mawazo Yake hapo mwanzo kabisa.

Kabla hata Yeye hajafanyika mwili hapa duniani; kabla hapajakuweko chochote, wewe ulikuwa mojawapo ya mawazo Yake. Yeye alijua jina lako lingekuwa lipi. Yeye alijua rangi ya nywele ambazo wewe ungekuwa nazo. Alijua kila kitu kukuhusu wewe.

Kisha, ulipoisikia Sauti Yake ikimulika mbele yako, kulikuwa na kitu fulani ndani yako kilichopaza tu sauti; unajua wapi unakotoka nawe ukakijia. Ulijua hiyo ilikuwa Kweli. Ulijua hiyo ilikuwa njia ya Mungu iliyoandaliwa kwa ajili ya leo hii kwa sababu Mbegu hiyo daima ilikuwa ndani yako.

Yeye sasa anatubeba juu ya mbawa za tai. Neno linatuambia Yeye huwafananisha manabii Wake na tai kila wakati. William Marrion Branham ndiye mjumbe tai wa Mungu aliyethibitishwa kwa ajili ya siku hii. Hizo ndizo mbawa za tai tunazopaswa kubebwa nazo hadi kwenye Nchi ya ahadi, kwa sababu yeye,; nabii tai wa Mungu, anaubeba ujumbe wa Mungu, akiita kutoka na kulinena Neno Lake, akimkamilisha Bibi-arusi Wake.

Sisi tunamfuata Mungu tunapomfuata William Marrion Branham mwenye ujumbe Wake wa ukombozi. Na Biblia inasema kwamba, “…Yeye, hawakuangamia pamoja na wale ambao hawakuamini.” Kwa maana, Mungu alikuwa mwingi wa rehema kwao;, kwa sababu walikuwa wakifuata amri Zake.

Mungu anatutaka tufuate amri Zake, nazo amri Zake zilisema:; Mimi ni Sauti ya Mungu kwenu. Semeni TU kile kilicho kwenye hizo kanda. Sauti Yangu ndio Sauti pekee inenayo Maneno ya kutokukosea. Yamenenwa kikamilifu nanyi mnayapokea kikamilifu kutoka kwenye Sauti Yangu. Kwa hivyo, ni Sauti ya Mungu iliyo kwenye kanda ndiyo tu mnayohitaji, kwa kuwa Mimi, Mungu niliye mwingi wa rehema Zangu, nimeiandaa hiyo kwa ajili yenu. Ndiyo Njia Yangu iliyoandaliwa kwa ajili ya siku hii.

Mungu aliye mwingi wa rehema alikuchagua wewe na kukukusudia kimbele ili uwe na Ufunuo huo ili uisikie Sauti hiyo. Mungu aliye mwingi wa rehema alijua katika wakati huu wa mwisho, Wakati kungekuwa na mitazamo mingi potofu, sauti nyingi na fasiri tofauti za Ujumbe, kiasi kwamba tulihitaji Sauti iliyo Kamilifu, na Njia Kamilifu, ambayo tungeweza kwenda kwake ili tuweze kuisikia sisi wenyewe, Neno, kwa Neno, kwa Neno, kile hasa Yeye alichotaka kumwambia Bibi-arusi Wake.

Huwezi kupokea alichosema mtu mwingine. Inakupasa kupokea aliyosema Mungu. Yeye alisema, “Na neno la kila mtu na liwe uongo, na Langu kweli.”

Kwa hivyo, Mungu, aliye mwingi wa rehema Zake, ameiandaa njia ambayo Bibi-arusi Wake angeweza Kuisikia Sauti Yake masaa 24/siku 7 za wiki, siku 365 za mwaka, kwa Kubonyeza Play, na kuhuishwa kwa kuisikia Sauti ya Mungu ikinena mdomo kwa sikio na mioyo yao.

Sisi ni Neno Lake lililofanyika mwili. Hatuna nguvu yoyote, lakini Yeye ametupa mamlaka Yake. Kila mmoja wetu anayo. Ukiyakataa, utakaa mahali ulipo. Lakini tukiyakubali, yatafanya yapitayo ufahamu, kwa sababu Mungu ni mwingi wa rehema Zake.

Na wakati mwanamume au mwanamke, si hoja uko katika hali gani, unayo mamlaka kutoka kwa Mungu, kwa ahadi, kwa sababu Yeye ni tajiri na ametuahidi kutufanyia mengi mno. “Kama ukiuambia mlima huu ‘Ng’oka’ na usione shaka moyoni mwako, bali uamini kwamba hayo usemayo yametukia, yatakuwa yako.” Huna uweza wowote, bali unayo mamlaka.

Bibi-arusi anaweza tu kukamilishwa na kuunganishwa kwa kulisikia Neno Lake kamilifu lililoandaliwa kwa ajili ya leo hii:; Sauti Yake. Ndio Sauti pekee inayoweza kumuunganisha na kumkamilisha Bibi-arusi. Ndio Sauti pekee ambayo Mungu alituambia yatupasa kuisikia na KUIFUATA. Kama Musa, Ndugu Branham alijua kwamba yeye ndiye aliyechaguliwa kutuchukua sisi watoto kutuingiza kwenye Nchi ya ahadi kwa sababu hiyo ahadi alipewa yeye. Naye yampasa atupeleke kwenye Nchi ya ahadi.

Nabii tai wetu alitufundisha kwa mifano. Agano la Kale lilikuwa kivuli cha Agano Jipya. Alituambia jinsi gani tunavyopaswa kuwa waangalifu na kipi cha kuwa nacho macho katika wakati huu wa mwisho. Yeye alituonya kuhusu roho ya Kora, na kuhusu Dathani, na kundi lao la watu wasioamini, walipojaribu kuiga. Wao walijaribu kuingiza kitu fulani katika mpango wa Mungu.

Hawakutaka mpango wa mtu mmoja. Hawakutaka hayo. Iliwapasa wapate jambo la kutenda. Kora alisema, “Mbona, kuna watu watakatifu kuliko wewe, Musa. Unajifanya kama kwamba wewe tu ndiye pwani kwenye…au ndiwe pekee kijiwe katika pwani, hasa.” Akasema, “Mimi—Mimi…haukupaswa kufanya hivyo. Na kuna watu wengine hapa.”

Ndugu na dada, Mimi sijaribu kuyatenganisha makanisa kwa kuyasema na kuyanukuu mambo haya, Roho Mtakatifu ndiye anayetenganisha. Usikilizeni Ujumbe huu tunaoenda kuusikia, Nabii ndiye anayemwonya Bibi-arusi ni kipi cha kuwa nacho macho. Yeye anatuambia kile hiyo roho ilichofanya wakati huo, na kile itakachofanya tena katika siku yetu.

Kwa kweli, sijaribu kuwakusanya watu katika huduma tano, wao hawawezi kabisa kumuunganisha Bibi-arusi. Mimi ninajaribu kuwaunganisha kwenye Neno la Mungu lililo safi, lisiloghoshiwa, Sauti pekee inayoweza kumuunganisha Bibi-arusi.

Tunasikia mambo yayo hayo leo,, ati Ndugu Branham si mtu pekee anayeweza kuuhubiri Ujumbe, tumeitwa kuuhubiri Ujumbe. Kwa kweli wameitwa, bali kisha, wanashindwa kutambua umuhimu wa kuisikia Sauti hiyo na kuamini Ni Ujumbe wa mtu mmoja, kwa kutoa visingizio VYA KUTOICHEZA Sauti ya Mungu katika makanisa yao, na kuiweka huduma yao kuwa muhimu zaidi.

Nayo Biblia ilisema, “Walikwenda njia ya Balaamu, na kuangamia katika maasi ya Kora.” Kuangamia katika maasi! Je maasi ya Kora yalikuwa nini? “Je, unadhani wewe tu ndiye mtu aliye mtakatifu peke yako? Kwa nini, wa Mungu…Sisi sote tu watakatifu. Kanisa lote ndivyo lilivyo. Kila…Sote tukusanyike, ndivyo inavyotupasa kuwa.” Hivyo ndivyo walivyoangamia, katika hilo. Na tulistahili hayo kabisa. Tulistahili hayo.

Ujumbe huu, Sauti Yake, ndio Sauti pekee inenayo waziwazi na inapokelewa wazi na Bibi-arusi. Huduma aminifu ni kuwatia moyo watu wadumu na Sauti Hiyo kwa kuuhubiri na kuunukuu Ujumbe. Lakini si tu kuuhubiri, bali LAZIMA waucheze makanisani mwao, na kuwaambia watu wao Hiyo ndio SAUTI ILIYO MUHIMU ZAIDI, ili Bibi-arusi aweze kuisikia Sauti ya Mungu, kutoka kwa Mungu Mwenyewe.

Hakuna kilicho kikubwa zaidi kuliko kuisikia Sauti ya Mungu. Hakuna upako ulio mkuu zaidi kuliko upako ulio kwenye kanda. Hakuna njia nyingine ya kumuunganisha Bibi-arusi ila kwa Sauti ya Mungu ilio kwenye kanda. Hakuna NJIA nyingine KAMILIFU isipokuwa kwa KUBONYEZA PLAY NA KUAMINI KILA NENO UNALOSIKIA. Kweli ni Mungu, Aliye mwingi wa rehema Zake kwa Bibi-arusi Wake. Ndio njia Yake KAMILIFU iliyoandaliwa ya leo hii.

Ninawaalika mje na muungane chini ya ule upako mkuu zaidi wa siku yetu Jumapili hii saa 6:00 MCHANA, masaa ya Jeffersonville, [ni saa 1:00 JIONI ya Afrika mashariki–Mh] tunapomsikia Mungu akinena na kuwafundisha watoto Wake Neno kamilifu kwa kuuleta Ujumbe:; Mungu Aliye Mwingi Wa Rehema 65-0119

Ndugu Joseph Branham

Maandiko ya kusoma: Waefeso 2:1-5

26-0920 Mbegu Ya Hitilafu

Ujumbe: 65-0118 Mbegu Ya Hitilafu

PDF

BranhamTabernacle.org

Mpendwa 1 WAO, [ 1 of TM inamaanisha pia 1 of Tape Ministry- 1 wa Huduma ya Kanda—Mh.]

Watu wanapotuuliza:

S: Je, wewe ni mmoja wao “Bonyeza Play” watu wa kanda wale wanaoamini kwamba Mungu alimtuma William Marrion Branham kumwita Bibi-arusi wa Mungu atoke?

J: NDIYO, Mimi Ni Mmoja Wao.

S: Je, Unaamini kila Neno lililonenwa kwenye hizo Kanda?

J: Bwana asifiwe, Mimi Ni Mmoja Wao.

S: Basi lazima unaamini pia kwamba yakulazimu Kubonyeza Play na kuisikia Sauti Yake ili uwezekuwa Bibi-arusi wa Kristo?

J: Utukufu, huyo ndiye hasa Mimi niliye, huyo ni mimi kindakindaki…Mimi Ni Mmoja Wao.

S: Unaniambia, unaamini kweli kwamba wewe ni aliyechaguliwa, mteule, Uzao wa Kifalme ambao umekusudiwa kimbele tangu misingi ya ulimwengu kuliamini Neno Lake, kuwa Bibi-arusi Wake, na ni mkamilifu machoni Pake, bila dhambi yoyote, na huwezi kabisa kudanganywa?

J: Haleluya, umeelewa, huyo ni mimi kabisa kabisa, MIMI NI Mmoja Wao.

Kulingana na Yesu Mwenyewe, sisi ndio fasiri ya Neno Lake. Wana wa Ufalme. Dhihirisho la Roho Mtakatifu. Ule Uzao wa Ufalme wa wakati huu.

Unajua nini? Ni wakati wa kila mtu kujua sisi ni nani hasa ili kusiwe na kutatanika. Tutamwacha Mungu azungumze kupitia nabii Wake na ayaweke yote pamoja kwa ajili yenu.

Nguvu zizo hizo zilizounena ulimwengu ukawa ziko katika wale watu walio na Roho Mtakatifu. Hiyo ni kweli. Wanaume kwa wanawake, wakati umewadia kwetu kujua wewe ni nani. Ibilisi anajaribu kukuficha, kukwambia ya kwamba wewe ni maskini kitu kidogo kilichodhalilishwa. Sivyo ulivyo. Ninyi ni wana na binti za Mungu.

Uungu hauko Mbinguni; uko ndani yenu. Haleluya!

J: Uungu hauko Mbinguni, unaishi na kukaa ndani ya kila mmoja wetu!

Kwa kila siku mpya, kwa kila pumzi tunayotwaa, ule Ufunuo Yeye aliotupa wa sisi ni nani unakuwa mkubwa zaidi na zaidi. Sisi ni Neno lililo hai linalokaa katika mwili.

Tunalijua hili kwa sababu Yeye ametupa sisi Ufunuo ni nani Yeye aliyemtuma katika siku yetu; ni yupi ambaye Mungu Yeye Mwenyewe alisema angemtuma kuhubiri na kulifundisha Neno Lake katika Ufunuo 22.

Mimi Yesu nimemtuma malaika wangu kuwashuhudia ninyi mambo hayo katika makanisa.

Yeye alimtuma malaika Wake: William Marrion Branham, kunena katika MAKANISA YAKE…Hilo ewe rafiki linamaanisha ZICHEZENI KANDA KATIKA MAKANISA YENU. Hilo hata halihitaji ufunuo, unatakiwa tu kusoma.

Kulingana na Neno, huu ndio wakati wa udanganyifu zaidi kuliko katika historia ya ulimwengu. Ile roho ya kweli na ya uongo itafanana sana kiasi kwamba ingewadanganya walio wateule kama yamkini.

Mungu alimtuma MALAIKA WAKE kwa makanisa. Tunayo Sauti Yake viganjani mwetu. Tunaweza kusikia kabisa Neno kwa Neno kile hasa Yeye alichosema. Haihitaji ufafanuzi au fasiri, kile tu Bibi-arusi anachopaswa kufanya ni KUBONYEZA PLAY na KUAMINI.

Yeye alituonya, msibadilishe nukta moja au yodi moja kwenye kanda. Usiweke uelewa wako au mawazo yako, isikieni tu Sauti Yangu na muamini. Hadi leo hii, hilo halijawezekana; bali leo ni kwa sababu Ndio njia ya Mungu iliyoandaliwa ya siku hii.

Tumetoka kuzisikia Nyakati Saba za Kanisa na jinsi ambavyo katika kila wakati, roho hizo ziliinuka ili kuwatoa watu kutoka kwenye Neno la kweli. Jinsi ambavyo katika kila wakati, baada ya mjumbe kuondoka, vile walivyofanya ili kuwapeleka watu kwenye kanuni ya imani au fundisho la sharti; kwao wenyewe na kwenye wazo la mwanadamu.

Leo wao wanajaribu kuuua ushawishi wetu na kusema, “Loo, wanaamini kanda ndiyo Sauti iliyo muhimu zaidi unayopaswa kuisikia. Yakupasa ucheze kanda kanisani mwako… huo ni upuuzi. Ndugu Branham hakusema kuzicheza kanda kanisani. Hivi sasa ni sauti ya wahudumu ndiyo mnayopaswa kuisikia.”

Kwangu mimi, hiyo ndiyo mbegu ya hitilafu! NI LAZIMA MBONYEZE PLAY na muisikie Sauti ya Mungu makanisani mwenu kwani Ndiyo Sauti PEKEE iliyothibitishwa na Mungu Mwenyewe. Lazima mtii kila Neno alilonena Mungu.

Mimi Yesu nimemtuma malaika wangu kuwashuhudia ninyi mambo hayo katika makanisa.

Malaika huyo aliyethibitishwa ananena katika Kanisa letu, kwa hivyo Mimi ninawaalika mje muungane nasi kuisikia Sauti hiyo pamoja na Bibi-arusi Wake kutoka kote ulimwenguni kwenye mawasiliano ya simu saa 6:00 MCHANA, masaa ya Jeffersonville,(ni saa 1:00 JIONI ya Afrika mashariki) na kusikia: 65-0118 – “Mbegu Ya Hitilafu”.

Ndugu Joseph Branham

26-0913 Wakati wa Kanisa La Laodikia

Ujumbe: 60-1211E Wakati wa Kanisa La Laodikia

PDF

BranhamTabernacle.org

Mpendwa Bibi-arusi wa Kristo, hebu na tukutanike pamoja Jumapili saa 06:00 MCHANA, masaa ya Jeffersonville,(ni saa 1 JIONI ya Afrika Mashariki) kusikiliza 60-1211E Wakati wa Kanisa la Laodikia.

Ndugu Joseph Branham

26-0906 Wale Wanawali Kumi, Na Wayahudi Mia Na Arobaini Na Nne Elfu

Ujumbe: 60-1211M Wale Wanawali Kumi, Na Wayahudi Mia Na Arobaini Na Nne Elfu

PDF

BranhamTabernacle.org

Mpendwa Bibi-arusi wa Kristo, hebu na tukutanike Jumapili saa 06:00 MCHANA, masaa ya Jeffersonville,(ni saa 1:00 JIONI ya Afrika Mashariki) ili kusikia 60-1211M Wale Wanawali Kumi, Na Wayahudi Mia na Arobaini na Nne Elfu.

Ndugu Joseph Branham

26-0830 Wakati Wa Kanisa La Filadelfia

Ujumbe: 60-1210 Wakati Wa Kanisa La Filadelfia

PDF

BranhamTabernacle.org

Mpendwa Bibi-arusi wa Kristo, hebu na tukutanike pamoja Jumapili saa 6:00 MCHANA, masaa ya Jeffersonville,(Ni saa 1 JIONI ya Afrika Mashariki) kusikiliza 60-1210 Wakati Wa Kanisa La Filadelfia.

Ndugu Joseph Branham

26-0823 Wakati Wa Kanisa La Sardi

UJUMBE: 60-1209 Wakati Wa Kanisa La Sardi

PDF

BranhamTabernacle.org

Mpendwa Bibi-arusi wa Kristo, hebu na tukutanike pamoja Jumapili saa 6:00 MCHANA, masaa ya Jeffersonville,(ni saa 1:00 JIONI ya Afrika Mashariki) kusikiliza 60-1209 Wakati Wa Kanisa la Sardi.

Ndugu Joseph Branham

26-0809 Wakati Wa Kanisa La Pergamo

UJUMBE: 60-1207 Wakati Wa Kanisa La Pergamo

PDF

BranhamTabernacle.org

Mpendwa Bibi-arusi wa Kristo, hebu na tukutanike pamoja Jumapili saa 06:00 MCHANA, masaa ya Jeffersonville,(ni saa 1 JIONI ya Afrika Mashariki) kusikiliza 60-1207 Wakati wa Kanisa la Pergamo.

Ndugu Joseph Branham