UJUMBE: 65-0718M Kumtendea Mungu Kazi Bila Mapenzi Yake
- 26-0426 Kumtendea Mungu Kazi Bila Mapenzi Yake
- 24-0721 Kumtendea Mungu Kazi Bila Mapenzi Yake
- 23-0101 Kumtendea Mungu Kazi Bila Mapenzi Yake
- 21-0905 Kumtendea Mungu Kazi Bila Mapenzi Yake
- NUKUU YA LEO KWA KISWAHILI
- 18-1007 Kumtendea Mungu Kazi Bila Mapenzi Yake – Preliminari
Mpendwa Bibi-arusi Anayethaminiwa.
Saa imeenda sana. Wakati umekaribia. Maamuzi hayana budi kufanywa. Mungu anawaonya watoto Wake. Bwana Mungu wetu ametutangazia na kututhibitishia Kweli Yake ni ipi kwa Neno Lake, na kwa Roho Wake. Si kwa nguvu, si kwa uweza, bali kwa Roho Wangu, na Neno Lako ni Kweli.
Yeye amemthibitishia Bibi-arusi kikamilifu leo kwamba Yesu Kristo ni yeye yule jana, leo, na hata milele. Yeye ametuonyesha na kutufunulia Ujumbe na mjumbe wa saa hii ni kitu kimoja. Yeye ametufunulia siri Zake zote zilizokuwa zimefichwa katika Neno. Ametuthibitishia hilo kwa Roho Wake Mtakatifu. Hakuna swali akilini mwetu, mioyoni mwetu au rohoni mwetu. Sauti Yake iliyo kwenye kanda ni BWANA ASEMA HIVI KWA BIBI-ARUSI WAKE.
Mungu daima ameruhusu njia nyingi kumjia Yeye. Anayafanya mapenzi Yake ya kuruhusia katika mapenzi Yake Makamilifu. Yeye pia daima ameandaa MAPENZI MAKAMILIFU NA NJIA KAMILIFU KWA AJILI YA WATOTO WAKE. Wengi hujaribu kuja kwa njia tofauti kwa kumtendea Mungu kazi bila ya kuwa mapenzi Yake Makamilifu. Huenda yakaonekana na kusikika kama mapenzi Yake makamilifu, lakini sio kulingana na Neno Lake.
Hata mtu mkuu, aliyepakwa mafuta hivi karibuni, akitoka Uweponi mwa Mungu, akiwa na ufunuo wa kumfanyia Mungu jambo fulani, naye alitaka kulifanya hilo kwa ajili ya Mungu; lakini ufunuo aliokuwa nao ulikuwa si sahihi.
Kila mmoja wetu lazima aipate njia Yake kamilifu iliyoandaliwa. Tutajuaje kwamba tuko katika mapenzi Yake makamilifu Je, ni ikiwa mtu ambaye amepakwa mafuta kweli, yakitoka mapya kutoka uweponi mwa Mungu, akiwa na ufunuo, hayuko katika mapenzi makamilifu ya Mungu?
Kuna NJIA MOJA PEKE YAKE YA KUJUA HAKIKA, naye Mungu ameiandaa njia hiyo kwa Bibi-arusi Wake.
Sauti ya Mungu Mwenyewe imeliambia kanisa hili, na ninyi watu wote mlio kwenye kanda, na watu waliounganishwa kwa redio katika sehemu zingine za dunia, wakati huo na SASA. Alituambia tumsikilize kile yeye alichokuwa akisema kwa makini sana, na ILI TUSIKOSE.
Nasema vivyo hivyo katika Jina la Yesu Kristo: Usiongeze kitu. Usiondoe, kuliwekea mawazo yako. Wewe sema tu yaliyosemwa katika kanda hizo. Tenda sawasawa kabisa na vile Bwana Mungu amekuamuru kutenda; Usiongezee Kwake.
Yeye hakusema, na haimaanishi, kwamba wahubiri hawawezi kulihubiri Neno, waalimu hawawezi kulifundisha Neno, au wachungaji au manabii wafanye kile ambacho tumeitiwa kufanya; yawapasa, Yanipasa. Tumeitiwa na kuteuliwa kufanya hivyo. Yatupasa tuwaelekeze na kuunukuu Ujumbe huu na mjumbe kwa watu, kwa maana Ndilo Neno la siku yetu.
Lakini Yeye anatuambia waziwazi kwamba sote tunaweza kupakwa mafuta, kwa upako wa kweli, tujazwe na Roho Wake Mtakatifu, kuwa na ufunuo mpya, na tuwe nje ya mapenzi Yake. Katika siku yetu, Yeye ameiandaa NJIA KAMILIFU ya kujua hakika unaisikia Sauti ya Mungu, kutoka kwa Mungu Mwenyewe. Ndiyo njia PEKEE kamilifu.
Wahudumu hawapaswi tu kuunukuu na kuuhubiri Ujumbe huu, inatubidi tuwachezee watu Sauti ya Mungu iliyo kwenye kanda. Hakuna UPAKO MKUU kuliko kuisikia Sauti ya Mungu. Hakuna njia nyingine ya kujua bila shaka kwamba kile tunachokisikia ndicho HASA kile Mungu alichosema.
Katika siku hii, tofauti na siku nyingine yoyote ile katika historia ya ulimwengu, Mungu ameiandaa njia ambayo inalifanya kuwa vigumu kulikosa, ikiwa wewe ni Bibi-arusi Wake Aliyechaguliwa Kimbele. Limethibitishwa na kufunuliwa na Nguzo ya Moto Mwenyewe kuwa Sauti ya Mungu Yeye Mwenyewe akizungumza moja kwa moja na Kanisa Lake.
Kote kote katika tawala elfu za miaka, watoto wa Mungu wamekuwa wakitamani na kuonea njaa kuisikia Sauti ya Mungu wao wenyewe. Jinsi gani wao walivyotamani wangekuwa pale siku ile Yesu alipowahubiria maelfu kule mlimani. Kusikia jinsi Yeye alivyolinena Neno Lake kwa upendo na huruma. Kusikia jinsi Yeye alivyoliwekea msisitizo kila Neno. Jinsi ambavyo lingezungumza na kuitia moyo mioyo yao.
Tuko hai sasa na katika Uwepo wa Mungu tukiisikia Sauti ya Mungu.
Siku moja hivi karibuni hatutarudi katika maisha kama haya tena. Tutarudi kama kiumbe kisichokufa. Dhambi itaondolewa. Shetani atafungwa kwa miaka elfu moja nasi tutaishi katika nchi hii ambayo Bwana Mungu wetu ametupa.
Tumekamilika asilimia 100%. Hatujawahi kuwa wenye furaha zaidi hivi au kutokuwa na shaka zaidi hivi katika maisha yetu. Sisi ni Mmoja Naye na Neno Lake. Sisi tu Neno Lake. TUKO KATIKA MAPENZI YAKE MAKAMILIFU KWA SISI KUDUMU NA SAUTI YAKE, NENO LAKE. Atarudi siku yoyote sasa kutuchukua twende pamoja Naye.
Asante Bwana Yesu!
Bwana Mungu wako amekutangazia yaliyo Kweli. Bwana Mungu Wako amethibitisha Kweli ni nini kwa Neno Lake na kwa Roho Wake. “Si kwa uweza, wala si kwa nguvu, bali ni kwa Roho Yangu.” Na Roho, “Mungu anawatafuta wale ambao wanamwabudu katika Roho na Kweli.” “Neno Lake ni Kweli.” Na amethibitisha vizuri kabisa kwamba Yesu Kristo ni yeye yule jana, leo, na hata milele. Amewaonyesha ninyi Mbegu za jioni. Ameifunua kwenu katika Neno. Amethibitisha hilo kwenu kwa Roho Wake.
Kwa moyo wangu wote ninawaalika kila mmoja wenu aje aungane na sehemu ya Bibi-arusi Wake tunapoungana kutoka kote ulimwenguni saa 6:00 MCHANA, masaa ya Jeffersonville,(ni saa 1:00 JIONI ya Afrika Mashariki) kuisikia Sauti Yake ikinena kupitia malaika-mjumbe Wake wa saba na kutuletea Ujumbe: Kujaribu Kumtendea Mungu Kazi Bila Ya Kuwa Mapenzi Ya Mungu 65-0718M.
Ndugu. Joseph Branham
Maandiko ya kusoma kabla ya kuusikiliza Ujumbe:
Kumbukumbu la Torati 4:1-4 / 4:25-26
1 Nyakati 13
1 Nyakati 15:15
Zaburi 22
Marko Mt. 7:7
Yoeli 2:28
Amosi 3:7
Malaki 3
Mathayo Mt.11:1-15
1 Wakorintho 13:1