All posts by admin5

26-0503 Chakula Cha Kiroho Kwa Wakati Wake

UJUMBE: 65-0718E Chakula Cha Kiroho Kwa Wakati Wake

PDF

BranhamTabernacle.org

Bibi-arusi Kipenzi,

Sauti tunayopenda sote kuisikia itazungumza Jumapili hii, na kutuletea Ujumbe Maalum wa Barua ya Mahaba, kwa ajili ya Bibi-arusi wa Yesu Kristo tu.

Sauti hiyo imetoka kuuambia ulimwengu na kuwaonya, “Msijaribu kunitendea Mimi kazi bila ya kuwa mapenzi Yangu. Ninayo njia kamilifu niliyoiandaa kwa ajili yenu, Bibi-arusi Wangu. Kumbukeni Maneno Yangu, semeni tu yale niliyosema kwenye kanda Zangu, kwa maana mnaingia hukumuni. Rehema imekataliwa. Lakini furahini, na mshukuru, kwa kuwa nimewaandalia na kuwapa Chakula Kilichofichwa, Chakula cha Kiroho, ili mpate kuishi kwa fadhili na rehema za Ufunuo wa Yesu Kristo.

Sasa hivi kuna ukame nchini kwa ajili ya kuisikiliza Sauti Yangu. Wao hawawaelewi ninyi kwa sababu mnasema ninyi ni watu wa Kanda, na mnataka tu kuisikia Sauti Yangu iliyo kwenye Kanda; lakini nimewaita ninyi na kuwafunulia njia Yangu kamilifu iliyoandaliwa kwa ajili ya siku hii.

Ninyi hamjashirikiana na wasioamini katika wakati wa ukame. Nimewapeni ninyi Sauti Yangu ipate kuwalisha. Kwa kuicheza Sauti Yangu, pipa lenu halitapunguka, wala chupa yenu haitaisha kamwe, hata siku ile nitakapokuja na kuwachukueni kama Bibi-arusi Wangu.

Hiyo ndio sababu hasa niliirekodi Sauti Yangu,  Ili mwezekuwa na mahali pa kamilifu pa kwenda, ambapo hamna kosa, hamna haja ya fasiri, ni Sauti Safi ya Mungu tu. Mahali ambapo mnaweza kwenda ili mweze kusikia kile haswa nilichosema: Bwana Asema Hivi.

Nitazungumza nanyi waziwazi Jumapili. Nawatakeni msisahau kamwe kile nitakachowaambia. Kanda hizi ndicho Chakula chenu cha Kiroho cha wakati huu. Ni kinono mno kwa baadhi ya hao; hawawezi tu kukipokea. Hakijafunuliwa kwao, bali Mimi nimewachagua NINYI, na kuwapa Ufunuo wa njia Yangu kamilifu iliyoandaliwa.

Kwenu ninyi, Ni Chakula Kilichofichwa, hata mnaishi kwa fadhili na rehema za Neno Lililo Hai.

Wakati nilipokuwa nikiishi katika mwili ndani ya Mwanangu, wao hawakuweza kabisa kukubali Mimi nilikuwa nani: Mungu na mwanadamu. Kisha niliahidi kwamba ningerudi tena katika siku za mwisho na kuishi katika mwili wa mwanadamu kwa mara nyingine tena kama nilivyofanya mbele ya Ibrahimu, na ningeshuka na kujifanya Mwenyewe katika mwili wa mwanadamu kama nilivyofanya wakati huo.

Hiki ndicho wao walichokosa, wakati huo na sasa hivi, lakini Mimi sitaki kamwe ninyi msahau. Chakula hiki kilichohifadhiwa ninachowalisha ninyi, hicho na mjumbe Wangu, ni kitu kimoja. Huwezi kuwatenganisha. Ujumbe na mjumbe ni kitu kimoja. Niliwaambieni katika Neno Langu kile Mimi ningefanya katika siku hii. Ndiyo maana ni mapenzi Yangu kuiweka Sauti Yangu katika makanisa yenu, majumbani mwenu, kila mahali muendapo; kwa maana ndio Sauti iliyo muhimu zaidi mnayopaswa ninyi kuisikia. Ndio Sauti PEKEE iliyothibitishwa inenayo Bwana Asema Hivi.

Rehema imekataliwa. Sasa ninyi mnaishi kwa Neno Langu. Nimewapa Ufunuo wa Mimi Ni nani na NINYI NI nani. Hakupaswi kuwa na shaka hata chembe mioyoni na akilini mwenu. Ninyi ndio Bibi-arusi Wangu Niliyemchagua, Mteule, Aliyekusudiwa Kimbele. Ninyi ndio Neno Langu Lililonenwa lile lililokuwa ndani Yangu hapo mwanzo.

Ninyi mna ruhusa ya kukikaribia Chakula, Chakula cha Kiroho, ambacho ulimwengu haujui chochote kukihusu.

Mna ruhusa ya kuufikia uponyaji wa miili yetu wakati madaktari wameshindwa; Ni kimoja cha Vyakula Mimi nilichoahidi na nilichowapa ninyi katika siku za mwisho.

Niliahidi kuzifunua siri za mioyo yenu na kuyafanya mambo haya. Mimi niko ndani yenu. Ninyi ni sehemu Yangu, Nami ni sehemu yenu. Ishara hizi zitafuatana na hao waaminio.

Jumapili hii nitakuwa nikimuunganisha Bibi-arusi Wangu kutoka kote ulimwenguni kwa Sauti Yangu. Nitawaambia mwekeane mikono juu ya mmoja kwa mwingine. Msijiombee, mwombee yule mliyemwekea mikono, kwa sababu wao wanawaombea. Tutaomba pamoja, na hakutakuwa na mtu mnyonge popote kote ulimwenguni ikiwa mtaamini.

Kama unaamini, na huna shaka moyoni mwako, nitatangaza:

Shetani, umeshindwa! Yesu Kristo alikushinda! Yeye alifufuka katika wafu na anasimama miongoni mwetu usiku wa leo, akithibitisha Ujumbe huu wa siku za mwisho. Toka katika watu hawa! Waache, katika Jina la Yesu Kristo! “Katika Jina Langu watatoa pepo,” nawe umetolewa nje. Katika Jina la Yesu Kristo, liache kusanyiko hili!

Kutakuwako na uponyaji ukifanyika kote ulimwenguni kuliko hapo awali.

Kwa nini tungojee tena zaidi, ndugu yangu mpendwa, dada, Huyu hapa, Roho Mtakatifu, Mungu, papa hapa, jambo lenyewe hasa tulilozungumzia.”

Ninauwalika ulimwengu mzima uje uungane nasi Jumapili hii saa 6:00 MCHANA, masaa ya Jeffersonville,(Ni saa 1:00 JIONI ya Afrika Mashariki) na tuusikie Ujumbe na mjumbe Wake atuletee Chakula cha Kiroho kwa Wakati Wake, Chakula Kilichofichwa kwa ajili ya Bibi-arusi.

Ndugu Joseph Branham

 Ujumbe: Chakula cha Kiroho kwa Wakati Wake 65-0718E

 Mjumbe: Kasisi William Marrion Branham

 Maandiko:1 Wafalme 17:1-7 / Amosi 3:7 / Yoeli 2:28

Malaki 4:4 / Luka 17:30 / Yohana Mt. 14:12

26-0426 Kumtendea Mungu Kazi Bila Mapenzi Yake

UJUMBE: 65-0718M Kumtendea Mungu Kazi Bila Mapenzi Yake

PDF

BranhamTabernacle.org

Mpendwa Bibi-arusi Anayethaminiwa.

Saa imeenda sana. Wakati umekaribia. Maamuzi hayana budi kufanywa. Mungu anawaonya watoto Wake. Bwana Mungu wetu ametutangazia na kututhibitishia Kweli Yake ni ipi kwa Neno Lake, na kwa Roho Wake. Si kwa nguvu, si kwa uweza, bali kwa Roho Wangu, na Neno Lako ni Kweli.

Yeye amemthibitishia Bibi-arusi kikamilifu leo kwamba Yesu Kristo ni yeye yule jana, leo, na hata milele. Yeye ametuonyesha na kutufunulia Ujumbe na mjumbe wa saa hii ni kitu kimoja. Yeye ametufunulia siri Zake zote zilizokuwa zimefichwa katika Neno. Ametuthibitishia hilo kwa Roho Wake Mtakatifu. Hakuna swali akilini mwetu, mioyoni mwetu au rohoni mwetu. Sauti Yake iliyo kwenye kanda ni BWANA ASEMA HIVI KWA BIBI-ARUSI WAKE.

Mungu daima ameruhusu njia nyingi kumjia Yeye. Anayafanya mapenzi Yake ya kuruhusia katika mapenzi Yake Makamilifu. Yeye pia daima ameandaa MAPENZI MAKAMILIFU NA NJIA KAMILIFU KWA AJILI YA WATOTO WAKE. Wengi hujaribu kuja kwa njia tofauti kwa kumtendea Mungu kazi bila ya kuwa mapenzi Yake Makamilifu. Huenda yakaonekana na kusikika kama mapenzi Yake makamilifu, lakini sio kulingana na Neno Lake.

Hata mtu mkuu, aliyepakwa mafuta hivi karibuni, akitoka Uweponi mwa Mungu, akiwa na ufunuo wa kumfanyia Mungu jambo fulani, naye alitaka kulifanya hilo kwa ajili ya Mungu; lakini ufunuo aliokuwa nao ulikuwa si sahihi.

Kila mmoja wetu lazima aipate njia Yake kamilifu iliyoandaliwa. Tutajuaje kwamba tuko katika mapenzi Yake makamilifu Je, ni ikiwa mtu ambaye amepakwa mafuta kweli, yakitoka mapya kutoka uweponi mwa Mungu, akiwa na ufunuo, hayuko katika mapenzi makamilifu ya Mungu?

Kuna NJIA MOJA PEKE YAKE YA KUJUA HAKIKA, naye Mungu ameiandaa njia hiyo kwa Bibi-arusi Wake.

Sauti ya Mungu Mwenyewe imeliambia kanisa hili, na ninyi watu wote mlio kwenye kanda, na watu waliounganishwa kwa redio katika sehemu zingine za dunia, wakati huo na SASA. Alituambia tumsikilize kile yeye alichokuwa akisema kwa makini sana, na ILI TUSIKOSE.

Nasema vivyo hivyo katika Jina la Yesu Kristo: Usiongeze kitu. Usiondoe, kuliwekea mawazo yako. Wewe sema tu yaliyosemwa katika kanda hizo. Tenda sawasawa kabisa na vile Bwana Mungu amekuamuru kutenda; Usiongezee Kwake.

Yeye hakusema, na haimaanishi, kwamba wahubiri hawawezi kulihubiri Neno, waalimu hawawezi kulifundisha Neno, au wachungaji au manabii wafanye kile ambacho tumeitiwa kufanya; yawapasa, Yanipasa. Tumeitiwa na kuteuliwa kufanya hivyo. Yatupasa tuwaelekeze na kuunukuu Ujumbe huu na mjumbe kwa watu, kwa maana Ndilo Neno la siku yetu.

Lakini Yeye anatuambia waziwazi kwamba sote tunaweza kupakwa mafuta, kwa upako wa kweli, tujazwe na Roho Wake Mtakatifu, kuwa na ufunuo mpya, na tuwe nje ya mapenzi Yake. Katika siku yetu, Yeye ameiandaa NJIA KAMILIFU ya kujua hakika unaisikia Sauti ya Mungu, kutoka kwa Mungu Mwenyewe. Ndiyo njia PEKEE kamilifu.

Wahudumu hawapaswi tu kuunukuu na kuuhubiri Ujumbe huu, inatubidi tuwachezee watu Sauti ya Mungu iliyo kwenye kanda. Hakuna UPAKO MKUU kuliko kuisikia Sauti ya Mungu. Hakuna njia nyingine ya kujua bila shaka kwamba kile tunachokisikia ndicho HASA kile Mungu alichosema.

Katika siku hii, tofauti na siku nyingine yoyote ile katika historia ya ulimwengu, Mungu ameiandaa njia ambayo inalifanya kuwa vigumu kulikosa, ikiwa wewe ni Bibi-arusi Wake Aliyechaguliwa Kimbele. Limethibitishwa na kufunuliwa na Nguzo ya Moto Mwenyewe kuwa Sauti ya Mungu Yeye Mwenyewe akizungumza moja kwa moja na Kanisa Lake.

Kote kote katika tawala elfu za miaka, watoto wa Mungu wamekuwa wakitamani na kuonea njaa kuisikia Sauti ya Mungu wao wenyewe. Jinsi gani wao walivyotamani wangekuwa pale siku ile Yesu alipowahubiria maelfu kule mlimani. Kusikia jinsi Yeye alivyolinena Neno Lake kwa upendo na huruma. Kusikia jinsi Yeye alivyoliwekea msisitizo kila Neno. Jinsi ambavyo lingezungumza na kuitia moyo mioyo yao.

Tuko hai sasa na katika Uwepo wa Mungu tukiisikia Sauti ya Mungu.

Siku moja hivi karibuni hatutarudi katika maisha kama haya tena. Tutarudi kama kiumbe kisichokufa. Dhambi itaondolewa. Shetani atafungwa kwa miaka elfu moja nasi tutaishi katika nchi hii ambayo Bwana Mungu wetu ametupa.

Tumekamilika asilimia 100%. Hatujawahi kuwa wenye furaha zaidi hivi au kutokuwa na shaka zaidi hivi katika maisha yetu. Sisi ni Mmoja Naye na Neno Lake. Sisi tu Neno Lake. TUKO KATIKA MAPENZI YAKE MAKAMILIFU KWA SISI KUDUMU NA SAUTI YAKE, NENO LAKE. Atarudi siku yoyote sasa kutuchukua twende pamoja Naye.

Asante Bwana Yesu!

Bwana Mungu wako amekutangazia yaliyo Kweli. Bwana Mungu Wako amethibitisha Kweli ni nini kwa Neno Lake na kwa Roho Wake. “Si kwa uweza, wala si kwa nguvu, bali ni kwa Roho Yangu.” Na Roho, “Mungu anawatafuta wale ambao wanamwabudu katika Roho na Kweli.” “Neno Lake ni Kweli.” Na amethibitisha vizuri kabisa kwamba Yesu Kristo ni yeye yule jana, leo, na hata milele. Amewaonyesha ninyi Mbegu za jioni. Ameifunua kwenu katika Neno. Amethibitisha hilo kwenu kwa Roho Wake.

Kwa moyo wangu wote ninawaalika kila mmoja wenu aje aungane na sehemu ya Bibi-arusi Wake tunapoungana kutoka kote ulimwenguni saa 6:00 MCHANA, masaa ya Jeffersonville,(ni saa 1:00 JIONI ya Afrika Mashariki) kuisikia Sauti Yake ikinena kupitia malaika-mjumbe Wake wa saba na kutuletea Ujumbe: Kujaribu Kumtendea Mungu Kazi Bila Ya Kuwa Mapenzi Ya Mungu 65-0718M.

Ndugu. Joseph Branham

Maandiko ya kusoma kabla ya kuusikiliza Ujumbe:
Kumbukumbu la Torati 4:1-4 / 4:25-26
1 Nyakati 13
1 Nyakati 15:15
Zaburi 22
Marko Mt. 7:7
Yoeli 2:28
Amosi 3:7
Malaki 3
Mathayo Mt.11:1-15
1 Wakorintho 13:1

26-0419 Kuchagua Bibi-Arusi

UJUMBE: 65-0429E Kuchagua Bibi-Arusi

PDF

BranhamTabernacle.org

Mpendwa Bibi-arusi Aliyechaguliwa,

Wakati tunapousikiliza Ujumbe huu, Kuchagua Bibi-arusi, wengine wanafikiri kwamba nabii anazungumza tu na kutufundisha kuhusu tabia na kimo ambacho mwanamume anapaswa kuangalia wakati anapomchagua mwanamke anayemtaka awe mke wake. Hiyo ni kweli, anafanya hivyo, lakini hapo kuna barua ya mahaba halisi iliyofichwa katika Maneno Yake. Kile Yeye anachomfunulia Bibi-arusi Wake ni cha kina zaidi. Mungu anazungumza na Yeye(Bibi-arusi) moja kwa moja, akimwambia kile Yeye alichokuwa akikitafuta ndani Yake, na kwa nini Yeye alimchagua tangu mwanzo. Yeye alimtaka Yeye(Bibi-arusi) ajue kwamba Yeye amemchagua awe BIBI-ARUSI WAKE KIPENZI WA KUPENDEZA, ambaye Yeye alitaka ashiriki naye Umilele Wake.

Hapo mwanzo, Mungu alikuwa akimtafuta Bibi-arusi ambaye angekuwa na Tabia ile ile ya Kwake. Roho Wake yule yule angedhihirishwa ndani Yake(Bibi-arusi). Yeye alimtaka Bibi-arusi ambaye alikuwa amejitolea kabisa-kabisa Kwake, na Neno Lake lililoahidiwa, mpaka Nia ile ile iliyokuwamo ndani Yake iwe ndani yake Yeye(Bibi-arusi). Lazima afinyangwe kama Yeye alivyo.

Yeye alimtaka awe mwili Wake ule ule, mifupa ile ile, Roho yule yule, kila kitu kile kile, kama tu Yeye hasa. Wawili hao wangekuwa MMOJA.

Yeye hangekuwa na namna fulani ya macho jeuri. Yeye hangebembana huko na sauti nyingine yoyote. Yeye angekuwa mwaminifu na mkweli Kwake, haijalishi mtu yeyote angesema nini. Yeye angemkubali kwa Neno Lake. Chochote Yeye alichosema, YEYE ANGEAMINI KILA NENO, haijalishi ingechukua muda gani hilo kutimia, yeye angeliamini. Yeye angedumu na Neno Lake.

Yeye(Bibi-arusi) angempenda Yeye, na Yeye peke yake. Haikumlazimu Yeye kumpa utajiri mwingi, yeye alikuwa na Lulu ya thamani kuu, ule Ufunuo wa kweli wa Yeye( Bwana-Arusi). Yeye(Bibi-arusi) angejua, wao walikuwa MMOJA na kitu kimoja. Roho Wake angekaa ndani Yake. Chochote Yeye (Bibi-arusi) alichokihitaji, Yeye angempa; kitu tu Yeye(Bibi-arusi) alichopaswa kufanya ni kuomba na kuamini, na Yeye angekifanya.

Yeye(Bibi-arusi) alijua Yeye(Bwana-Arusi) angeondoka kwa muda mrefu kwenda kumjengea Yeye nyumba ambayo ingekuwa na kila kitu jinsi tu vile Yeye apendavyo kiwe na atakavyo. Yeye alikuwa akiijenga jinsi ambavyo Yeye (Bibi-arusi) angeipenda. Yeye (Bibi-arusi) alijua siku moja Yeye (Bwana-Arusi) angerudi kumchukua Yeye, kama Yeye alivyoahidi, kisha wangekuwa na Karamu Kuu ya Harusi kwa miaka elfu. Ndipo, wao wangeenda pamoja kwenye Makao hayo mazuri Yeye aliyomjengea waishi milele.

Hakuna kitu kingine ambacho kingekuwa muhimu kwake Yeye. Yeye asingetaka kitu kingine chochote. Yeye angeridhika mno na kutosheka na Ufunuo kujua Yeye (Bwana-Arusi) ni nani, na Yeye (Bibi-arusi) ni nani. Yeye (Bibi-arusi) angejua kwamba Yeye(Bwana-Arusi) angelitimiza Neno Lake. YEYE ANGETIMIZWA, AKIJUA YEYE NDIYE YULE AMBAYE YEYE ALIYEMCHAGUA KUWA BIBI-ARUSI WAKE.

Ndugu na dada zangu, Mungu mwenye nguvu wa Mbingu na nchi alitazama kote katika Umilele na AKAWACHAGUA NYINYI… NYINYI KUWA BIBI-ARUSI WAKE KIPENZI ALIYOWACHAGUA.

Ninawaalika mje muungane nami na sehemu ya Bibi-arusi Wake Jumapili hii, wakati Yeye anapozungumza kupitia malaika Wake Mwenye nguvu na kutuambia sisi ndio Bibi-arusi Wake Aliyowachagua.

Ndugu Joseph Branham

Ujumbe: 65-0429E / Kuchagua Bibi-arusi
Muda: saa 06:00 MCHANA, masaa ya Jeffersonville(Ni saa 1:00 JIONI ya Afrika Mashariki)

Maandiko Matakatifu:
Mwanzo 24:12-14
Isaya 53:2
Ufunuo 21:9

26-0412 Je! Mungu Hubadilisha Nia Yake Kuhusu Neno Lake?

UJUMBE: 65-0418E Je! Mungu Hubadilisha Nia Yake Kuhusu Neno Lake?

PDF

BranhamTabernacle.org

Wapendwa Waliohuishwa,

Jinsi gani mioyo yetu ilivyoinuka kama Tai wikendi hii ya Pasaka. Siku baada ya siku, upako Wake ulizidi kuwa mkubwa. Ushirika, Kuzikwa, Ukamilifu, kisha kile kilele kikuu Alichotujengea: Ni Kuchomoza kwa Jua…UTUKUFU, AMEFUFUKA na Yuko hai ndani ya kila mmoja wetu. Yeye alikuwa akilifunua Neno Lake kwa kila mmoja wetu jinsi tusivyowahi kusikia hapo awali. Ule upako uliifurika mioyo yetu, uwepo Wake uliitanda hewa; ilionekana kana kwamba Unyakuo ulikuwa umekaribia.

Yeye alituambia yale yaliyotukia miaka 2000 iliyopita, na kisha yale yaliyokuwa yakitukia sasa mwaka wa 2026. Yesu alikuwa Chembe ya kwanza ya Ngano ya Mungu iliyofufuka kutoka kwa wafu. Yeye alikuwa amefufuliwa na Nguvu za Mungu za kuhuisha. Mungu alikuwa ameyahuisha maisha Yake, akamfufua kutoka kwa wafu, Naye alikuwa malimbuko ya kwanza ya wale waliolala. Yeye alikuwa wa kwanza kukomaa, Mganda wa Mungu uliotikiswa kama ukumbusho wa kutoa shukrani kwa Mungu, akiamini kwamba sisi wengine tungekuja. Ilikuwa ishara.

KISHA YEYE AKATUFUNULIA KILE KILICHOTUKIA LEO. Kama vile Yeye alivyotikiswa siku ya Pentekoste wakati sauti kutoka Mbinguni iliposikika kama upepo wa nguvu ukienda kasi ukitikiswa juu ya watu. Ulikuwa ukitikiswa tena mbele ya watu kama alivyoahidi katika Luka 17:30 na Malaki 4, wakati Mwana wa Adamu atakapofunuliwa na kutikiswa tena juu ya watu.

Sasa, Mwana wa Adamu ni Nani? “Hapo mwanzo alikuwako Neno, naye Neno alikuwa kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu. Naye Neno akafanyika mwili, akakaa kwetu.” Na iwapo mafundisho yote tuliyo nayo, na thibitisho la Neno la Mungu; kwa Neno la Mungu, kwa ishara, kwa maajabu, tunaona leo, ya kwamba katika Kitabu cha—cha Luka hapa, ya kwamba kama tulivyonukuu hicho hivi punde, ama Lu—Luka mlango wa 17 na kifungu cha 30; na Malaki 4, na Maandiko mbalimbali ambayo tunayajua, ya kwamba hilo Neno tena linatikiswa juu ya watu, ya kwamba mapokeo yaliyokufa ya mwanadamu yamekufa, na Mwana wa Mungu yu hai tena na ubatizo wa Roho Mtakatifu moja kwa moja miongoni mwetu, naye anatupa Uzima.

Roho Mtakatifu aliendelea kutikisa na kutikisa juu yetu, akifunua na kufunua Neno Lake… Nguvu za utendaji, mitambo, Nguvu za kuhuisha…

Ndipo, ilipoonekana kana kwamba Haiwezi kuwa kuu zaidi, Yeye alituambia:

Naye akaniruhusu niangalie ng’ambo ya pazia, nami nikawaona ninyi nyote kule ng’ambo… Wote uliowahi kupenda, na wote waliowahi kukupenda, umepewa wewe.” Mnaona? Niliwaona hao kila mahali pale namna hiyo. Ilikuwa nini? Nguvu za kuhuisha.

YEYE ALITUONA SISI KULE!! Ng’ambo ya pazia la wakati….tulikuwa KULE pamoja naye; wapendwa wetu wote waliotutangulia…akina baba, mama, watoto. Tulikuwa kule pamoja nao na wale wote ambao hatujawahi kukutana nao: Musa, Eliya, Petro, Paulo….tulikuwa sote kule pamoja.

Kisha, kama vile Roho Mtakatifu alivyo mzuri, Yeye hakutaka kutusahau sisi tulio wagonjwa, wenye huzuni na waliopigwa, kwa hivyo Yeye alijitikisa Mwenyewe juu yetu tena ili kila mtu aponywe chochote kile tulichokuwa na haja nacho.

Watu hawa, ambao ni raia wenza wa Ufalme, mmiliki wa Nguvu za kuhuisha, lihuishe kwao, Bwana, sasa hivi. Pia naomba Roho aende kutoka tai hadi tai, kutoka kwenye Neno hadi Neno, mpaka utimilifu wa Yesu Kristo udhihirishwe katika kila mmoja wa hiyo miili, kwa ajili ya haja za kimwili, za kiroho, ama haja zozote walizo nazo, tunapowekeana mikono sisi kwa sisi. Katika Jina la Yesu Kristo.

Neno Hilo. Sauti Hiyo. KILA KITU tunachokihitaji kiko kwenye kanda, Ewe, Bibi-arusi. Mungu habadilishi nia Yake kuhusu Neno Lake. Hakuna nukta moja au yodi moja inayoweza kubadilishwa, kwa hivyo Yeye alitengeneza njia ambayo Bibi-arusi Wake angeweza kusikia kwa masikio yao wenyewe kile hasa Yeye alichotaka kuwaambia.

Mungu amenena na Bibi-arusi Wake na kufunua KILA KITU. Kimerekodiwa. Bibi-arusi lazima aje kwa Bwana Arusi; hiyo ndio Njia Yake kamilifu iliyoandaliwa ambayo imetengenezwa kwa ajili ya siku hii. Ni BWANA ASEMA HIVI.

Je! Mungu hubadilisha Nia Yake kuhusu Neno Lake? HAPANA. Yeye anayo MAPENZI MAKAMILIFU NA MAPENZI YAKURUHUSIA.  Bibi-arusi yambidi awe katika MAPENZI YAKE MAKAMILIFU. Hakuna Mapenzi yaliyo makamilifu zaidi, au mahali pakamilifu, kuliko kuisikia Sauti ya Mungu moja kwa moja kutoka kwa Mungu Mwenyewe.

Mwaliko wangu kwa kila mmoja wenu ni muungane nasi Jumapili saa 6:00 MCHANA, masaa ya Jeffersonville(ni saa 1:00 JIONI ya Afrika Mashariki), kuisikia Sauti ya Mungu ikituletea Neno Safi. Hakuna haja ya kubahatisha, wewe keti tu na useme AMINA KWA KILA NENO….hakuna mahali pengine hilo linaweza kufanywa, ila kwa KUBONYEZA PLAY.

Ndugu Joseph Branham.

Ujumbe: 65-0418E — Je! Mungu Hubadilisha Nia Yake Kuhusu Neno Lake?

Tutaanzia kwenye aya ya 61.

Maandiko ya kusoma kabla ya kuusikia Ujumbe:

Kutoka sura ya 19

Hesabu 22:31

Mathayo Mt. 28:19

Luka 17:30

Ufunuo sura ya 17

PASAKA 2026 – Ibada Maalum ya Ushirika na Kutawadhana MIGUU

Wapendwa Raia Wenza Wa Ufalme,

Pasaka hii inaahidi kuwa Pasaka iliyo kuu kuliko ambayo Bibi-arusi amewahi kuwa nayo. Tumekuwa tukiketi katika Uwepo wa Mwana, tukiivishwa, tukijitambua sisi ni nani. Ule utimilifu wa Yesu Kristo unadhihirishwa ndani ya kila mmoja wetu huku Neno Lake, Sauti Yake, ikipiga kelele, Tai kwa tai, ikituita kutoka kwenda kwenye Karamu yetu ya Arusi.

Kila mwaka wakati huu Bibi-arusi anaisubiri kwa hamu kubwa wikendi ijayo ya Pasaka. Wakati ambapo Yeye atatuunganisha kutoka kote ulimwenguni kwa siku nne mfululizo, tukimwabudu Yeye, tukimshukuru Yeye, tukimsifu Yeye; kwa maana Yeye amefufuka na anaishi ndani ya kila mmoja wetu. Bwana Arusi na Bibi-arusi wanakuwa MMOJA.

Yeye anatupa sisi wakati huu maalum wa kufungia nje vitu vyote vya kilimwengu vinavyotuzunguka na kuutumia tu muda pamoja Naye. Hakuna vizubaishi vya kilimwengu huu, huku tunapouumba ulimwengu wetu wenyewe pamoja Naye. Tufunge milango yetu, tuvizime vifaa vyetu vyote vya kielektroniki na chochote kinachotukengeusha kutoka Kwake.

Haja iliyo kuu ambayo kila mmoja wetu aliyonayo ni kuwa karibu Naye. Tunataka kuishi maisha yaliyowekwa wakfu zaidi kwa ajili Yake; kuwa daima katika mapenzi Yake makamilifu. Kuwa tayari kwa ajili ya Kuja Kwake. Hakuna chochote katika ulimwengu huu, au katika maisha yetu, kilicho muhimu zaidi kuliko hili.

Yeye ametupa sisi fursa hii maalum ya kuutumia tu muda pamoja Naye, kuzungumza na kumtafakari Yeye. Kuingia katika uwepo Wake na kuifungua mioyo yetu Kwake. ITAKUWA IBADILISHAYO MAISHA KWA BIBI-ARUSI WAKE!

Yeye anajua yaweza kuwa vigumu kwa baadhi yenu wenye watoto, familia, na majukumu mengine tuliyo nayo, lakini tukiitumia kila sekunde huru tuliyonayo kuzungumza Naye, kumkaribia Yeye, kumfungulia Yeye mioyo yetu, kutakuwako na badiliko kubwa katika kutembea kwetu pamoja Naye, hata hatutakuwa vile tulivyokuwa.

Kama vile Yeye alivyofanya katika ile siku ya Musa alipowaleta watoto Wake majumbani mwao, damu ilikuwa imepakwa nao walikuwa wakijiandaa kwa ajili ya kule Kutoka kwao; itakuwa vivyo hivyo na wikendi hii maalum ya Pasaka ambayo Yeye ameiandaa kwa kila mmoja wetu.

ALHAMISI

Ilikuwa ni Alhamisi usiku ambapo Bwana Yesu aliila Karamu ya Mwisho pamoja na wanafunzi Wake, katika ukumbusho wa Pasaka kabla ya kule kutoka kwa wana wa Israeli. Tunayo fursa iliyoje ya kufanya ushirika na Bwana majumbani mwetu, kabla ya wikendi yetu takatifu, na kumwomba Yeye atusamehe dhambi zetu, na atupe yote tunayohitaji katika safari yetu.

Baba wa Mbinguni, tunashukuru kwa ajili ya jambo hili, wakati mwingine wa kukusanyika pamoja, upande huu wa Umilele. Na tunatarajia asubuhi ya leo kuhuishwa upya kwa nguvu kuja kutoka Kwako, zipate kututia moyo kwa ajili ya safari iliyoko mbele. Tumekusanyika kama wana wa Kiebrania walivyofanya asubuhi na mapema, kuokota mana iliyokuwa imetolewa kwa ajili yao usiku kucha, kuwapa nguvu kwa ajili ya siku ijayo. Tunakusanyika kwa ajili ya Mana ya kiroho, asubuhi ya leo, ipate kutupa nguvu kwa ajili ya safari.

Hebu sote tuanze saa 12:00 KUMI NA MBILI JIONI. masaa ya eneo unaloishi ili kusikiliza Ushirika 62-0204, na kisha nabii atatupeleka kwenye ibada yetu maalum ya Ushirika na Kutawadhana Miguu baada ya kanda kukamilika, ambayo itachezwa kwenye app ya Lifeline (kwa Kiingereza), au unaweza kuipakua ibada hiyo kwa Kiingereza au lugha zingine kwa kubofya anuani iliyo hapa chini.

IJUMAA

Hebu na twende katika maombi pamoja na familia zetu saa 3:00 TATU ASUBUHI,(Ni saa 10:00 KUMI JIONI ya Afrika Mashariki) na kisha tena saa 06:00 SITA MCHANA,(Ni saa 1:00 MOJA JIONI ya Afrika Mashariki), tukimwalika Bwana awe pamoja nasi na kuzijaza nyumba zetu kwa Roho Mtakatifu tunapojiweka wakfu Kwake.

Hebu akili zetu na zirudi huko nyuma hadi kwenye siku ile pale Kalvari, yapata miaka 2000 iliyopita, na kumwona Mwokozi wetu akining’inia msalabani. Na tukumbuke ile gharama kuu Yeye aliyoilipa kwa ajili yetu. Yeye alikuwa Mwana wa Mungu asiye na dhambi, lakini ilibidi ateseke kuliko mtu mwingine angeweza kuteseka, kwa sababu dhambi zetu sisi ziliwekwa juu Yake.

Ilibidi amtume Yeye kuzimu akiwa amehukumiwa (Unaona?), kwa sababu Yeye alizichukua dhambi zetu. Naye Kristo alikufa, si mwenye haki; Kristo alikufa mwenye dhambi. Unaona? Kristo mwenyewe hakutenda dhambi, bali alizichukua dhambi zetu juu Yake.

Kisha saa 06:30 SITA NA NUSU MCHANA,(Ni saa 1:30 MOJA NA NUSU JIONI ya Afrika Mashariki) na tuungane pamoja majumbani mwetu kusikia: 57-0419 Ukamilifu.

Kisha na tuungane tena katika maombi mara tu baada ya ibada, katika ukumbusho wa kusulubiwa kwa Bwana wetu.

JUMAMOSI

Hebu na tuungane tena sote katika maombi saa 3:00 ASUBUHI (Ni saa KUMI JIONI ya Afrika Mashariki) na saa 06:00 SITA MCHANA,(Ni saa 1:00 MOJA JIONI ya Afrika Mashariki) na tuiandae mioyo yetu kwa ajili ya mambo makuu Yeye atakayotutendea sisi miongoni mwetu.

Ninaweza kumsikia akisema, “Shetani, njoo hapa!” Yeye ni Bosi sasa. Ananyosha mkono, anaunyakua ule ufunguo wa mauti na kuzimu kutoka ubavuni mwake, akauning’iniza ubavuni Mwake Mwenyewe. “Ninataka kukupa notisi. Umekuwa laghai muda mrefu kutosha. Mimi ni Mwana wa Mungu aliye hai niliyezaliwa na bikira. Damu Yangu ingali imelowa msalabani, na deni kamili limelipwa! Huna haki tena. Umenyang’anywa zote. Nipe funguo hizo!”

Kisha saa 06:30 SITA NA NUSU MCHANA,(Ni saa 1:30 MOJA NA NUSU JIONI ya Afrika Mashariki) sote tutakusanyika pamoja kulisikiliza NENO: 57-0420 Kuzikwa.

Hii itakuwa SIKU ILIYO MAALUM vipi kwa Bibi-arusi Wake kote ulimwenguni.

Kisha hebu na tuungane tena pamoja katika maombi mara tu baada ya ibada.

JUMAPILI

Hebu kwanza na tuamke mapema kama vile Ndugu Branham alivyofanya asubuhi ile wakati rafiki yake mdogo, robini, alipomwamsha saa 11:00 Alfajiri. Natumshukuru tu Bwana kwa kumfufua Yesu kutoka kwa wafu:

Saa kumi na moja asubuhi ya leo, maskini rafiki yangu mwenye kifua chekundu aliruka dirishani akaniamsha. Ilionekana kana kwamba moyo wake mdogo ungepasuka, akisema, “Amefufuka.”

Saa 3:00 TATU ASUBUHI, (Ni saa KUMI JIONI ya Afrika Mashariki) tuungane tena katika mnyororo wetu wa maombi, tukiombeana na kujiandaa kuisikia Sauti ya Mungu.

Saa 3:30 TATU NA NUSU ASUBUHI, (Ni saa KUMI NA NUSU JIONI ya Afrika Mashariki) tutakusanyika pamoja kuusikiliza Ujumbe wetu wa Pasaka: 65-0418M Ni Kuchomoza kwa Jua.

Saa 06:00 SITA MCHANA. (Ni saa 1:00 MOJA JIONI ya Afrika Mashariki) tutaziinua sauti zetu Kwake tukimshukuru kwa ajili ya Nguvu za Kuhuisha.

Saa 9:00 TISA ALASIRI.(Ni saa 4:00 NNE USIKU ya Afrika Mashariki), Hebu na tuungane tena katika maombi, tukimshukuru Yeye kwa ajili ya WIKENDI YA KUPENDEZA ALIYOTUPA SISI PAMOJA NAYE NA BIBI-ARUSI WAKE KOTE ULIMWENGUNI.

Kwa ndugu na dada zangu walio nchi za ng’ambo, kama vile mwaka jana, ningependa kuwaalika muungane nasi katika masaa ya Jeffersonville, kwa masaa yote ya maombi katika ratiba hii. Hata hivyo, ninatambua kwamba kuzicheza Kanda Alhamisi, Ijumaa, na Jumamosi alasiri kwa masaa ya Jeffersonville itakuwa vigumu sana kwa wengi wenu, kwa hivyo tafadhali jisikieni huru kuzicheza Jumbe hizo kwa masaa yafaayo kwenu. Hata hivyo, ningependa sote tuungane pamoja Jumapili saa 3:30 TATU NA NUSU ASUBUHI masaa ya Jeffersonville (Ni saa 10:30 KUMI NA NUSU JIONI ya Afrika Mashariki), kuusikia Ujumbe wetu wa Jumapili pamoja.

Pia ningependa kukualika wewe na watoto wako kuwa sehemu ya vipindi vya Creations, Journaling na mapishi, ambayo familia yako yote inaweza kufurahia pamoja. Tunafikiri mtayapenda kwani yote yanalenga NENO tutakalolisikia wikendi hii.

Kwa ajili ya ratiba ya wikendi, taarifa kuhusu jinsi ya kujiandaa kwa ajili ya ibada ya Ushirika, nyenzo zitakazohitajika Kwa ajili ya vipindi vya Creations, na taarifa nyinginezo, tazama anuani zilizo hapa chini.

Hebu tuzifunge simu zetu kwa ajili ya wikendi ya Pasaka isipokuwa kupiga picha, kusikiliza Nukuu ya Siku, na kucheza kanda kutoka kwenye app ya The Table, app ya Lifeline, au kwenye anuani ya kupakulia.

Ni heshima kubwa kwangu kukualika wewe na familia yako kuja pamoja na Bibi-arusi ulimwenguni kote katika wikendi iliyojaa KUABUDU, KUSIFU NA UPONYAJI. Ninaamini kweli hii ni wikendi ambayo itayabadilisha maisha yako milele.

Ndugu Joseph Branham

26-0329 Huyu Melkizedeki Ni Nani?

UJUMBE: 65-0221E Huyu Melkizedeki Ni Nani?

PDF

BranhamTabernacle.org

Mpendwa Bibi-arusi Wa Uzima Wa Milele,

Sauti hiyo ni nani inayozungumza nasi kwenye kanda?

Tunaweza tu kujua jibu la swali hilo kwa Ufunuo kutoka kwa Mungu. Ni Bibi-arusi Wake aliyechaguliwa tangu zamani peke yake ndiye atakayekuwa na Ufunuo huo. Kwa hivyo, lazima tutafute Neno Lake ili kuelewa alisema Yeye alikuwa ni nani: Mfasiri pekee wa Neno Lake. Ni nani angeivunja na kuifunua ile Mihuri Saba? Ni nani angezifunua siri zote zilizofichwa za Biblia? Ni nani atakayemwita atoke na kumwongoza Bibi-arusi Wake? Ni nani atakayekuwa na ile Sauti ya kutokukosea?

Kulingana na Neno, si mwingine ila Melkizedeki, Yeye Mwenyewe. Mtu asiye na baba wala mama, Ambaye hakuwa na mwanzo wala mwisho wa siku Zake. Mungu, Ambaye alifanyika mwili na akala nyama na mkate wa mahindi, akanywa maziwa ya siagi, na akanena na Ibrahimu. Yeye alikuwa Mtu mwenye utu, akiishi katika mwili wa mwanadamu.

Neno lilo hilo lililosema kwamba Melkizedeki, Mtu huyo, utu huo, angeishi na kujifunua Mwenyewe tena katika mwili wa mwanadamu kama vile alivyofanya kwa Ibrahimu, kisha tena katika Yesu Kristo; bali leo, katika malaika-mjumbe Wake wa saba wa Ufunuo 10:7.

Roho Wake angeiteketeza hiyo maskani ya duniani ili Yeye aweze kuzungumza na kujifunua Mwenyewe kwa Bibi-arusi Wake. Mungu Mwenyewe akiishi na kuzungumza katika mwili wa mwanadamu. Mbegu Yake ya kwanza iliyorejeshwa kikamilifu ilikuwa imefikia kukomaa kabisa. Ule mpango kamili wa Mungu ulikuwa umewasili; Mungu na mwanadamu walikuwa Mmoja. Mungu alikuwa akizungumza mdomo kwa mdomo na Bibi-arusi Wake kama alivyofanya kwa Ibrahimu.

Akaingia na kuishi katika huo, katika Utu wa Melkizedeki. Ndipo baadaye hatukusikia tena habari za Melkizedeki, kwa sababu Yeye alifanyika Yesu Kristo. Melkizedeki alikuwa yule Kuhani, bali akafanyika Yesu Kristo, Basi, wewe uliruka hilo, kwa kuwa katika umbo hilo Yeye alijua yote, Nawe haujapata kujua hayo bado.

BADO…!! Basi sisi ni nani?

Macho yetu, kimo chetu, chochote kile tulichokuwa, tulikuwa katika mawazo Yake hapo mwanzo. Kabla hajakuwepo Malaika, nyota, Kerubi, au chochote kile. Yeye aliliwazia, Akalinena, nasi hawa hapa.

Hiyo ni isiyo kikomo. Hatuwezi kuelewa kwa akili zetu. Bali huyo ni Mungu. Mungu, asiye kikomo.

Kwa kuwa tulikuwa ndani Yake hapo mwanzo, nini kinachotokea kwetu sisi baada ya maisha haya yapatikanayo na mauti hapa duniani kwisha?

Joho hili la mwili linapobwagwa chini, kunao mwili wa kawaida, mwili wa kiungu, mwili ambao haukujengwa kwa mikono, wala kuzaliwa na mwanamke, ambamo tunaingia. Ndipo huo mwili unarudi huku na kuchukua mwili uliotukuzwa.

Ni mambo ya kupendeza vipi aliyowekewa Bibi-arusi Wake. Angalia yale yanayoendelea sasa hivi wakati Yeye akitufunulia Neno Lake zaidi ya wakati wowote ule. Nena kuhusu barua ya mahaba kwa Bibi-arusi Wake! Ni siku iliyoje tunayoishi.

Tuna Ufunuo na tunajua ni Melkizedeki, Sauti ya Mungu, anayezungumza nasi kwenye kanda. Tuna Ufunuo ndio mapenzi ya Mungu yaliyoandaliwa na makamilifu kwa ajili ya siku hii. Hivyo, tunamjua YEYE NI NANI NASI NDIYE BIBI-ARUSI WAKE.

Ufunuo huo unazidi kuwa mkubwa zaidi na zaidi kila siku. Kila siku ipitayo hutuletea furaha zaidi, Ufunuo zaidi. Bibi-arusi anajiweka mwenyewe tayari kwa kuketi katika uwepo wa Sauti Yake, Yeye anapotuambia Sisi ni nani, jinsi gani Yeye anavyotupenda Sisi, jinsi ambavyo Yeye anavyosubiri kwa hamu kuwa pamoja Nasi!!!

Njooni, mjiweke tayari saa 06:00 MCHANA, masaa ya Jeffersonville,(Ni saa 1:00 JIONI ya Afrika Mashariki) kwa ajili ya kile kinachokaribia kutukia, tunapoisikiliza Sauti ya Melkizedeki.

Ndugu Joseph Branham

Ujumbe: 65-0221E “Huyu Melkizedeki Ni Nani?”

Maandiko ya kusoma:
Mwanzo Sura ya 18
Kutoka 33:12-23
Yohana Mt. 1:1
Warumi 8:1
2 Wakorintho 5:1
1 Wathesalonike 4:13-18
Timotheo wa Kwanza 3:16 / 6:15
Waebrania 7:1-3 /13:8
Ufunuo 10:1-7 / 21:16