22-0925 Kuthibitisha Neno Lake

UJUMBE: 64-0816 Kuthibitisha Neno Lake

PDF

BranhamTabernacle.org

Mpendwa Chumvi ya Dunia ,

Wakati tu inaonekana kana kwamba haiwezi kuwa bora zaidi, Yeye anatupa Mzigo mwingine wa Kanda wa mafunuo. Tuna uwakilisho kwa kuchaguliwa tangu awali. Hiyo ndiyo sababu tunatoka mashariki na magharibi, kaskazini na kusini, ili kusikia Neno lililo hai likidhihirishwa.

Mungu alipoumba ulimwengu, tulikuwa katika mawazo yake. Wakati mshitaki wetu anapoendelea kutunyooshea kidole na kumwambia Baba, “walifanya hivi, walifanya hivi, walifanya hivi,” Damu ya Bwana wetu Yesu inatufunika. Tunapoomba, Mungu hatuoni, Yeye husikia tu sauti zetu kupitia Damu ya Yesu.

Shetani hawezi kusumbua; ama, anaweza kukujaribu, bali hawezi kumpata Mkristo aliyezaliwa mara ya pili. Kwa maana, Mungu, tangu kuwekwa misingi ya ulimwengu, alitangulia kumwona, na akamtuma Yesu kumkomboa, nayo ile Damu inanena kwa niaba yake. Anawezaje kufanya dhambi wakati, hata, haiwezi kuonekana na Mungu? Yeye hata haninii…Kitu pekee anachosikia ni sauti yako. Yeye huona uwakilisho wako. Amina! Hiyo ni kweli. Mnaona?

Nabii wa Mungu alituambia mambo haya. Hakuwa yeye aliyekuwa Akinena ; alionyesha tu mawazo ya Mungu, sifa Zake za mambo ambayo hayana budi kutendeka . Anatumia mdomo wake kuyaeleza. Na baada ya yeye kuyaeleza ,  lazima yatimie . “Mbingu na nchi zitapita, bali Neno Langu halitashindwa kamwe.”

Amethibitisha Neno Lake kwetu tena na tena. Je, hajatuthibitishia kuwa: Mwana wa Adamu aliyefanyika mwili kati yetu? Je! hajatuthibitishia: Nabii wetu anatimiza kila andiko linalomuhusu ? Je, hajatuthibitishia: Sisi ni Bibi-arusi Wake? Je, hajatuthibitishia: Tunao ushahidi wa kweli wa Roho Mtakatifu?

Tuna wasiwasi wa nini basi? Ametuthibitishia, ikiwa tutamshindania Naye, Atatushindania . Neno Lake haliwezi kushindwa kamwe.

Wote wanaoamini Ujumbe huu na mjumbe wa wakati huu wataokolewa. Wote wasiouamini Ujumbe na Mjumbe, wataangamia pamoja na ulimwengu .

Sikilizeni kwa makini enyi kanisa. Wengi sana hawaelewi, ama hawana Ufunuo wa Neno. Wanahisi tunamtukuza sana mtu huyu. Ikiwa kweli unaamini Ndugu Branham ni nabii wa Mungu, basi fungua moyo wako na nafsi yako na usikilize kile isemacho Bwana Asema Hivi .

Ni kitu gani kitakachomleta Bibi-arusi pamoja? Ni nini kitakachomuunganisha Bibi-arusi kuwa Mmoja na Mungu?

“ Katika siku hiyo Mwana wa Adamu atafunuliwa.” Nini? Kuliunganisha Kanisa kwa kile Kichwa, kuliunganisha, arusi ya Bibi-arusi. Wito wa Bwana Arusi utakuja hapa , wakati Mwana wa Adamu atakaposhuka aje katika mwili wa mwanadamu kuunganisha hivyo viwili pamoja. Kanisa halina budi kuwa Neno, Yeye ni Neno, na hivyo viwili vitaungana pamoja, na kufanya hivyo, itachukua dhihirisho la kufunuliwa kwa Mwana wa Adamu.

Itachukua dhihirisho la kufunuliwa kwa Mwana wa Adamu. Si wazo lako, si uelewa wako, si mawazo yako wala mahubiri yako. Mwana wa Adamu atamuunganisha Bibi-arusi pamoja na Bwana-arusi, nalo linatendeka HIVI SASA .

Hivi sasa tuko kwenye Karamu ya Harusi na Bwana Harusi na hivi karibuni tutaondoka kwenda kwenye Karamu yetu ya Arusi na Fungate.

Neno na Kanisa wanakuwa mmoja. Lo lote afanyalo Mwana wa Adamu, Yeye alikuwa Neno, Kanisa linafanya jambo lile lile .

Tunaweza tu kuishi kwa kila Neno litokalo katika Kinywa cha Mungu! Mungu amethibitisha kwamba nabii wetu ndiye Mnenaji wa Mungu kwa ajili ya wakati huu. Tunajuaje kuwa ni Neno la Mungu? Yeye amesema hivyo, ndipo akalithibitisha kwa Neno Lake.

Sisi ndio Kanisa-Bibi-arusi Aliye tayari katika siku za mwisho. Aliyeitwa kutoka katika mengine yote; yule ndege mwenye madoadoa kwa Damu Yake.

Baba, mioyo yetu inarukaruka, na moyo wangu unapigapiga, ninapowazia hayo na kujua ya kwamba maneno yako ni kweli, hamna hata moja linaloweza kushindwa .

Hii ndiyo njia pekee iliyoandaliwa na Mungu kwa siku hii. Ndiyo njia PEKEE ya kutobadilisha Neno moja. Kumbuka, Roho Mtakatifu anaweza kuja na kumtia mtu mafuta, na bado ni nje ya Mapenzi ya Mungu. NI LAZIMA TUDUMU NA NENO LA ASALI LILILOLITHIBITISHWA.

Ikiwa ungependa kudumu na Neno hilo na kusikia Sauti ya Mungu pamoja nasi, ninakualika uungane nasi Jumapili hii saa 6:00 SITA MCHANA , saa za Jeffersonville,(ni Saa 1 :00 MOJA JIONI Ya Tanzania),tunaposikia: Kuthibitisha Neno Lake  64-0816 .

Si lazima uungane nasi au hata kusikia kanda ile ile kwa wakati mmoja pamoja nasi, lakini ninakusihi, msikie nabii wa Mungu.

Ndugu. Joseph Branham

Maandiko ya kusoma kabla ya ibada:

Mathayo Mt 24:24

Marko Mt 5:21-43 / 16:15

Luka Mt 17:30 / 24:49

Yohana Mt 1:1 / 5:19 / 14:12

Warumi 4:20-22

I Wathesalonike 5:21

Waebrania 4:12-16 / 6:4-6 /13:8

1 Wafalme 10:1-3

Yoeli 2:28

Isaya 9:6

Malaki 4