22-0918 Makao Ya Baadaye Ya Bwana Arusi Wa Mbinguni Na Bibi-Arusi Wa Duniani

UJUMBE: 64-0802 Makao Ya Baadaye Ya Bwana Arusi Wa Mbinguni Na Bibi-Arusi Wa Duniani

PDF

pakua – m4a

pakua – amr

BranhamTabernacle.org

Rafiki wapendwa kwa Nabii ,

Moyo wangu unabubujika kwa furaha ninapowazia kuhusu sisi kukusanyika pamoja Jumapili hii ili kusikia Sauti ya Mungu ikisema nasi. Hakuna furaha kubwa maishani mwangu kuliko kuwa katika uwepo wa Roho Mtakatifu na kumsikia akisema na Bibi-arusi Wake, mdomo kwa sikio.

Hakuna kitu kingine katika ulimwengu huu kinachonipa furaha na amani, ila Neno Lake. Ninaposikia tu, “Habari za Asubuhi Marafiki,” mimi huketi tu, nikastarehe, na kunywa kutoka kwenye Kisima hicho kinachofoka maji kikiniambia Maneno ya Uzima wa Milele. Kuwazia, Mungu alimtuma kwangu MIMI NA WEWE, nasi ni MARAFIKI wa nabii wa Mungu na mjumbe.

Anatupenda sana hivi kwamba Alimtuma nabii Wake atuambie yote yahusuyo Makao yetu ya Baadaye. Alifurahishwa sana kutuambia yote yahusuyo hilo, hata kwa undani zaidi kuliko alivyoambiwa Yohana. Ametufunulia, Si mji wenye umbo la mraba, bali ni mji wenye umbo la piramidi, ambako Mwana-Kondoo atakuwa juu yake na Nuru ya ulimwengu.

Anatujulisha barabara zitajengwa kwa dhahabu na nyumba tutakazoishi zitakuwa za dhahabu safi sana. Yeye anaweka kila kitu kidogo jinsi tunavyopenda hasa, jinsi tungetaka tu. Hajaacha kitu chochote. Mjenzi wa Kiungu ameubuni kwa ajili yetu SISI, Mpendwa wake.

Miti ya Uzima itakuwako kule, nayo itazaa aina kumi na mbili za matunda. Na hayo Malango ya mji hayatafungwa usiku, kwa maana hakuna usiku kule, Yeye atakuwa ndiye Nuru yetu.

Ni nani atakayekuwa kule?

Ni akina nani waliokuja kwenye nchi mpya pamoja na nabii Nuhu? Hao walioingia pamoja naye safinani. Hiyo ni kweli? Hao ndio wanaotoka na kutembea mle. Mnaona? Hao walioingia pamoja na Nuhu, kwa ujumbe wake, hao ndio waliotoka wakatembea juu ya nchi mpya baada ya ubatizo wake wa maji .

Anazungumza kuhusu SISI marafiki zangu! Tuko ndani ya Safina yetu ya siku hii; Neno Lake, Ujumbe Huu, pamoja na Nuhu wetu Nabii . Na huko ng’ambo katika Nchi hiyo, Mji ule ambako Mwana-Kondoo ndiye Nuru, yeye atatujua SISI. Sisi ni watu wake, vito katika taji yake. Tumetoka Mashariki na Magharibi, kuja kwenye mji uliojengwa mraba. Mji ule ambao Ibrahimu alikuwa anautafuta.

Huku nikiona Neno likijidhihirisha Lenyewe , ninajua, bila shaka hata kidogo, vito vya taji yangu vitang’aa kuliko kitu cho chote kile ulimwenguni, katika Siku ile.

Je! twaweza hata kuanza kuwazia… Nabii wa Mungu alisema, ALIJUA, bila shaka hata kidogo , ya kwamba SISI ni vito vya taji yake, na tutang’aa kuliko kitu chochote kile ulimwenguni katika siku ile . Haleluya… Utukufu…Jina la Bwana lisifiwe.

Marafiki, kama tunafikiri ni la ajabu, tukiketi pamoja kutoka kote ulimwenguni, tukisikiliza na kula Neno Lake katika kanda hizi, itakuwaje tutakapoishi katika mji ule pamoja Naye!

Nabii wa Mungu atakuwa jirani yetu wa karibu, na tutakapokula hiyo miti, na tutakapotembea kwenye barabara hizo, tutakapotembea kwenye barabara hizo za dhahabu kwenye chemchemi, kunywa kutoka kwenye chemchemi, kutembea katika paradiso za Mungu, huku Malaika wanarukaruka kuizunguka dunia, wakiimba nyimbo za sifa.

Loo, itakuwa ni Siku ya namna gani! Inastahili kwa vyote. Njia inaonekana inaparuza, wakati mwingine inakuwa ngumu, lakini, loo! itakuwa kitu kidogo sana nitakapomwona Yeye, kidogo sana. Vipi yale majina mabaya na mambo ambayo wao wamesema, hayo yatakuwa nini nitakapomwona Yeye katika Mji ule mzuri, mzuri sana wa Mungu?

Marafiki, siwezi kusubiri kuona, na kuwa katika mji ule. Ninatamani kuwa kule pamoja na Bwana na Mwokozi wetu, nabii Wake, na pamoja na kila mmoja wenu.

Ninaelekea kwenye Mji ule mzuri
Bwana wangu ameuandaa kwa walio Wake ;
Wakati wote Waliokombolewa wa nyakati zote Wataimba “Utukufu!”
Wakikizunguka Kiti Cheupe cha Enzi
Wakati mwingine ninatamani Mbinguni sana, Na utukufu nitakaouona kule
Itakuwa ni furaha jinsi gani nitakapomwona Mwokozi wangu ,
Katika Mji ule mzuri wa dhahabu!

Ninaualika ulimwengu uje kuungana na sisi, marafiki wa nabii, tunapokusanyika kukizunguka Kiti Chake cha Enzi ili kusikia Sauti ya Mungu ikisema nasi saa 6:00 SITA MCHANA , saa za Jeffersonville,( ni Saa 1:00 MOJA JIONI Ya Tanzania) tunapomsikia Yeye akituambia yote kuhusu : Makao Ya Baadaye ya Bwana Arusi wa Mbinguni na Bibi-arusi wa Duniani 64-0802 . Naweza kukuahidi, itakuwa Sikukuu katika maisha yako.

Ndugu. Joseph Branham

Maandiko ya kusoma kabla ya kusikiliza Ujumbe :

Mathayo Mt. 19:28

Yohana Mt. 14:1-3

Waefeso 1:10

2 Petro 2:5-6 / Sura ya 3 yote

Ufunuo 2:7 / 6:14 / 21: 1-14

Mambo ya Walawi 23:36

Isaya Sura ya 4 yote / 28:10 / 65:17-25

Malaki 3:6