26-0524 Nini Kinachovutia Kule Mlimani?

UJUMBE: 65-0725E Nini Kinachovutia Kule Mlimani?

PDF

BranhamTabernacle.org

Wapendwa Tai Wanaokusanyika,

Huu mvuto mkubwa ni wa nini unaotendeka kote ulimwenguni? Watu kutoka kote ulimwenguni wanakusanyika saa 6:00 MCHANA masaa ya Jeffersonville, wakiketi majumbani mwao na makanisani mwao kwa matarajio makubwa, wakingojea kuisikia Sauti ya Mungu izungumze nao.

Ni jambo la ajabu mno na lisilo na mantiki kwa ulimwengu kuzisikiliza Kanda tu. Wao wanasema sisi tunaweza kuzisikia kanda wakati wowote. Hakuna lolote kusikiliza kwa wakati mmoja. Lazima uisikilize huduma iliyo mubashara, mhubiri, Si ati kanda tu. Wao wamekwama katika mapokeo yao.

Hakuna kitu kama hiki kimewahi kutokea katika historia ya ulimwengu. Ni nini kimewavutia watu hawa kuungana wote kwa wakati mmoja kuisikia Sauti hiyo ikimwita Bibi-arusi Wake atoke? Ni Mungu akitimiza Luka 17:30. Ni Mungu akitimiza Ufunuo 10:7. Ni Mungu akifunua Waebrania 13:8, Melkizedeki katika mwili wa mwanadamu, kama vile alivyofanya kwa Ibrahimu.

Wanasubiri na kujiuliza, Hivi Yeye atasema nini? Nini kitatokea wakati Yeye atakapoanza kunena? Wao wanataka kuwa pale kwenye mawasiliano ya simu ili kupata chochote kile Yeye asemacho. Wanakitaka. Wanataka kukisikia wote kwa wakati mmoja pamoja na Bibi-arusi kote ulimwenguni. Kwa maana wanaamini yeye ndiye sauti ambayo Mungu aliichagua kuwa Sauti Yake kumwita atoke na kumwongoza Bibi-arusi Wake.

Ingawa wako umbali wa masaa mengi, bali wao wote wako pamoja kama JAMII MOJA, wameunganishwa, wakiisikiliza Sauti hiyo ikizungumza nao kutokea Kanisa lao la Nyumbani. Wamekaa katika uwepo wa Mwana, wakiivishwa na kungojea Kuja kwa Masihi.

Mioyo yao inaenda mbio. Roho Mtakatifu anawafunulia wao kile kinachotendeka. Mungu amesubiri kufikia leo hii kulidhihirisha Neno Lake na kumkusanya Bibi-arusi Wake. Linatendeka, nao ni sehemu ya hilo. Uhalisia wa kile kinachotendeka unaingia mioyoni mwao. Wamesoma kulihusu hilo katika Maandiko kwa karne nyingi, bali sasa hivi ni uhalisia. Ufunuo wa Neno unadhihirishwa kupitia wao. Unabii wa nabii unatimizwa.

Wakati wanapoketi chini ya upako huo mkuu wa Sauti Yake yenye nguvu, Yeye anawatangazia wajiandae; Kwa maana usiku wa leo atawaombea kila mmoja wao. Yeye anatuambia wakati anapoanza kuomba, wawekeeni mikono walio wagonjwa, kwa maana uwepo wa Mungu aliye kila mahali uko kila mahali pamoja nao, haijalishi wako wapi: Texas, kule juu California, juu kule Arizona, Amerika Kusini, hata kwenye vibanda vilivyopo msituni ule upande mwingine wa dunia. Mahali popote pale wanaposikiliza hewani kwa simu, wawekeane mikono tunapoanza kuomba na Mungu atamponya kila mmoja wao, ikiwa wanaamini, kwa maana Ni Bwana Asema Hivi.

Wao sasa wanaelewa kwamba kupitia kila kizazi na kila nabii ambaye alikuwako au ambaye angekuwako, kutakuweko na kiasi fulani cha watu ambao wamechaguliwa tangu asili kuusikia Ujumbe huo, nao wataufuata. Hao hawatajali umati wa watu. Wao hawajali ukosoaji wa asiyeamini anayesema ati ni makosa au sio njia ya Mungu iliyoandaliwa. Wao hawabishani nao. Wana Wajibu mmoja WANAOPASWA KUFANYA, huo ni kuamini na kupata kila sehemu Yake wawezayo, waiingize ndani kama Mariamu aliyeketi Miguuni pa Yesu. Wao hawaonei haya, wanajivunia kusema wao ni kijana wa kanda au binti wa kanda anayebonyeza play.

Sauti hiyo tayari imekwisha kuwaonya wao kwamba kutakuwako na watiwa mafuta katika wakati wa mwisho ambao watakuwa na upako mkubwa, Roho Mtakatifu. Watamnukuu nabii na Ujumbe wa saa hii; wanadai kuwa waaminio, bali ni watiwa mafuta wa uongo.

Wao wangefanana sana na upako halisi kiasi kwamba ingewadanganya kama yamkini walio wateule, bali wao wanajua hawawezi kudanganywa, kwa maana wao NI NENO. Wao ndio Bibi-arusi wa kweli aliyedumu na Sauti ya Mungu.
Sauti hiyo inawatangazia kwamba katika siku hii haitakuwa limau, au balungi. Hiyo ingekuwa rahisi kutofautisha. Lakini itakuwa tangelo, nusu limau, nusu chungwa, uzao uliochanganyikana. Itaonekana kabisa kama chungwa, lakini haitakuwa, kwa maana tawi hilo jipya litakuwa asilimia 100% kama lile la asili. Wao WATADUMU na Neno hilo la asili la Sauti. Hawatabahatisha. Wao watadumu na yule, ambaye Mungu Mwenyewe alimtangaza kuwa ndiye SAUTI YAKE, NENO LAKE, aliyethibitishwa kwa Nguzo ya Moto.

Ni nini kinachotendeka?

Uzao wa Mungu uliochaguliwa tangu asili hauwezi kutenda chochote bali kuifuata na kuisikiliza Sauti hiyo, kwa maana ni zaidi ya maisha kwao. Unaweza kuyatwaa maisha yao, bali huwezi kuichukua Sauti hiyo.

Je, ni mvuto gani?

Mungu, kama kawaida, akitimiza Neno Lake.

Njoo uungane nasi na uwe sehemu ya unabii wa nabii unaotimizwa Jumapili hii saa 6:00 MCHANA, masaa ya Jeffersonville,(Ni saa 1:00 JIONI ya Afrika Mashariki) tunapoyasikia Maandiko yakidhihirishwa.

Ndugu Joseph Branham

Ujumbe: 65-0725E “Nini Kinachovutia Kule Mlimani?”

Maandiko:
Mathayo Mt 21:1-4
Zekaria 9:9 / 14:4-9
Isaya 29:6
Ufunuo 16:9
Malaki 3:1 / Sura ya 4
Yohana Mt 14:12 / 15:1-8
Luka Mt 17:22-30