UJUMBE: 65-0822M Kristo Amefunuliwa Katika Neno Lake Mwenyewe
- 26-0621 Kristo Amefunuliwa Katika Neno Lake Mwenyewe
- 24-0908 Kristo Amefunuliwa Katika Neno Lake Mwenyewe
- 23-0219 Kristo Amefunuliwa Katika Neno Lake Mwenyewe
- 21-1024 Kristo Amefunuliwa Katika Neno Lake Mwenyewe
- 21-0530 Kristo Amefunuliwa Katika Neno Lake Mwenyewe
- TAI WANAKUSANYIKA PAMOJA
- 19-1013 Kristo Amefunuliwa Katika Neno Lake Mwenyewe – Preliminari
- 17-1112 Kristo Amefunuliwa Katika Neno Lake Mwenyewe
Mpendwa Malkia,
Naye Bibi-arusi leo ametolewa kutoka kwenye mwili wa Kristo, ambao unatenda na kufanya vile vile kabisa na Yeye alivyosema Huo ungetenda kwa siku hii, yule Bibi-arusi, Malkia; Mfalme na Malkia.
Wakati Yesu alipofanyika hilo Neno lote, basi sisi tulikuwa sehemu Yake WAKATI HUO. Hakuna ibilisi, hakuna mamlaka, hakuna kitu kinachoweza kutuondolea hilo. Hiyo ndio nguzo ya kushikiza ya nafsi.
Ni uamsho ulioje Bibi-arusi alionao kwa kila Ujumbe tunaousikia. Yapita maneno ya mwanadamu kuelezea. Hakuna kivuli hata kimoja cha shaka, Mungu ametuchagua sisi na kutupa Ufunuo WA KWELI wa Neno Lake la siku hii. Kwa hivyo, tunajijua sisi ni nani, Malkia Wake.
Sauti ya Mungu inayonena na Bibi-arusi Wake kwenye kanda inamkamilisha Bibi-arusi Wake. Hakuna huduma nyingine, hakuna sauti nyingine; hakuna kitu kinachoweza kumkamilisha Bibi-arusi Wake ila Mungu Mwenyewe akinena kupitia midomo ya mwanadamu moja kwa moja na Bibi-arusi Wake. Wengine wanaweza kutaka kibadala, lakini Bibi-arusi Wake hataridhika na kitu kingine chochote ila SAUTI Yake, barua Yake ya mahaba kwa Bibi-arusi Wake; kwani Kondoo Wake wanataka tu kuisikia Sauti Yake.
Watu wanasema ati tunaweka mkazo sana kwa nabii. Ni ajabu sana kwamba watu hawakubali kwamba Baba Mkuu wa Mbinguni Mwenyewe alimjali sana malaika Wake kiasi kwamba aliuweka umuhimu mkubwa hivi kwa kila kitu kumhusu; jinsi alivyovaa, jinsi alivyotenda, tabia yake, matamshi yake.
Yeye hata alimvalisha namna ya mavazi aliyovaa; tabia yake, shauku yake, kila kitu jinsi tu alivyopaswa kuwa, Yeye alichaguliwa tu kikamilifu na Mungu Mwenyewe kwa ajili yetu sisi…kisha wanasema ati tunamwinua sana nabii.
Kwetu sisi, Sauti iliyo kwenye kanda si neno la mwanadamu, wala halinenwi na mwanadamu, halikuletwa na mwanadamu, wala haliwezi kufunuliwa na mwanadamu. Ni Neno la Mungu lililofunuliwa na Mungu Mwenyewe, Akijifasiria Yeye Mwenyewe, Kristo akijifunua Mwenyewe katika Neno Lake Mwenyewe.
Baadhi wanaweza kusikia, lakini hawatambui kikamilifu. Unaweza kuwaambia, kuwaonyesha, lakini hawawezi tu kuona. Tunawapenda, tunawaombea, bali kile Mungu alichotufunulia sisi ni Ukamilifu Wake.
Hili hapa jaribio la Litimasi kwa huu mgawanyiko mkubwa miongoni mwa Bibi-arusi wa Kristo leo wanaosema wanao Ufunuo wa kweli wa Ujumbe huu mkuu wa wakati wa mwisho.
Fasili ya jaribio la Litimasi: Jambo moja, la kuamua, swali, au tukio ambalo hufichua haraka asili ya kweli, ubora, au nafasi ya kitu fulani(au mtu).
Hebu kwanza niseme kwa mara nyingine tena, Ninaamini katika huduma ya kweli iliyoitwa na Mungu. Kuna haja, na nafasi, kwa kila ofisi. Maandiko yanasema huduma ya watu hawa ni kwa ajili ya kuwakamilisha watakatifu, lakini hayasemi kila huduma-5 itawakamilisha watakatifu. Ndugu Branham anatuambia waziwazi kwamba huduma katika kila wakati hupotoka, kwa hivyo WAO wangewezaje kumkamilisha Bibi-arusi?
Kuna wahubiri wengi, wengi sana waalimu, mitume na manabii ambao wamehubiri kwamba wanauamini Ujumbe huu wa wakati wa mwisho na kwamba Ndugu Branham alikuwa ndiye Sauti ya Ufunuo 10:7, ambao sasa wanasema ati ni uongo, yeye ni mdanganyifu, sisi tu dhehebu.
Hawa walikuwa wahudumu wanaoheshimika mno wenye makusanyiko makubwa ambao walisafiri ulimwenguni na kuhudumu. Walichukuliwa kama viongozi wakuu katika huduma-5, wakihubiri katika mikutano na makanisani kote Marekani. Wao walikuwa na huduma kuu machoni pa watu, nao waliwafuata na kuwaamini kuwa watu wakuu wa Mungu.
Kisha wapo wahudumu leo ambao wanaotambulikana vilivyo kama wahudumu wa huduma-5 ya kweli wanaodai kuuamini Ujumbe huu kwa kuunukuu na kuuhubiri, lakini pia wao wanasema Ujumbe huu sio Yakini. Siku za Ujumbe wa mtu mmoja zimekwisha. Huduma-5 hivi sasa ndio ya kumkamilisha Bibi-arusi, na ni makosa kuzicheza kanda kanisani, nikinukuu kauli zao chache.
Tunajua kutakuwako na watiwa-mafuta wa uongo katika wakati wa mwisho; nabii alituonya tuwaangalie. Huduma yao itatiwa mafuta. Watakuwa na Roho Mtakatifu, kwa hivyo wao wataunukuu Ujumbe wa Saa. Wao WATAFANANA SANA kiasi kwamba wangewadanganya walio wateule kama yamkini.
Hao SI madhehebu. Wao hawangeweza kuanza kuwadanganya wateule. Kwa hivyo, lazima iwe inafanana sana kuliko hiyo. Hii haimaanishi kwamba KILA mhudumu amepotoka, hata kidogo. Kuna watu wakuu wa Mungu wanaohubiri na kufundisha ukweli, bali kuna jambo ambalo kila mwaminio lazima atambue na kujiuliza:
Je, mhudumu unayemfuata wewe anaweza kukosea?
Je, unaweza kusema amina kwa kila Neno yeye analohubiri?
Je, unaamini kila Neno yeye analofundisha ni Bwana Asema Hivi?
Je, sauti yake ndio Sauti iliyo muhimu zaidi unayopaswa wewe kuisikia?
Je, anaweza kuhubiri jambo lisilo sahihi?
Je, anaweza kukosea hata baada ya yeye kuuhubiri Ujumbe kwa miaka 30?
Je, anaweza kushindwa?
Je, anaweza kukuambia mambo yasiyo sahihi?
Je, anaweza kudanganywa?
Sasa jiulize maswali yayo hayo kuhusu Sauti ya Mungu iliyothibitishwa unayoweza kuisikia kwenye kanda.
Je, Ujumbe ulio kwenye kanda unaweza kukosea: HAPANA
Je, unaweza kuamini na kusema AMINA kwa kila Neno yeye asemalo? NDIYO
Je, Hiyo inaweza kushindwa? HAPANA
Je, yeye anaweza kuhubiri mambo yasiyo sahihi? HAPANA
Je, Hiyo inaweza kukuambia jambo lisilo sahihi? HAPANA
Je, unaweza kukiweka kikomo chako cha milele kwenye kila Neno unalosikia… NDIYO!!!
Je, Ni Sauti ya Mungu: NDIYO
Kwa nini nayasema mambo haya? Ili kuonyesha kwamba watu WOTE wanaweza, na hufanya, makosa, bali SAUTI YA MUNGU iliyo kwenye kanda haiwezi kukosea. Ndiyo maana ni SAUTI ILIYO MUHIMU ZAIDI UNAYOPASWA KUISIKIA. Ndiyo maana wahudumu hawanabudi wayachezee makanisa yao kanda. Ndio NJIA KAMILIFU ya Mungu ILIYOANDALIWA ambayo Yeye amemfanyia Bibi-arusi Wake.
Hakika, Mimi ninaamini unaweza kuwasikia wengine, bali Sauti pekee UNAYOPASWA KUISIKIA na kuamini kila Neno ni Sauti iliyo kwenye kanda. Sauti hiyo ndiyo MOJA TU tunayoweza kusema AMINA kwa kila Neno.
Hiyo ndiyo amri ya Mungu, lazima uamini kila Neno, nalo Neno unalolisikia kwenye kanda ndilo NENO PEKEE lililothibitishwa na Nguzo ya Moto kuwa ndio kweli. Mungu alisema William Marrion Branham ndiye mfasiri PEKEE wa kiungu wa Neno Lake, kwa sababu Hilo si neno lake, Ni Neno la Mungu.
Usibadilishe yodi moja au nukta moja. Hakuna mtu aliye mkamilifu hivyo; ni Sauti ya Mungu peke yake ndiyo iliyo kamilifu hivyo. Hata tusipoelewa kile tunachosikia, tunapaswa tu kuamini kwamba hiyo ni Sauti ya Mungu iliyothibitishwa kwa Bibi-arusi Wake.
Kwa kweli, Roho Mtakatifu anawaongoza watu wa Mungu. Kwa kweli, Roho Mtakatifu amewaita wao kuwa wachungaji, wahubiri na waalimu; hiyo ni kweli, bali wao si wakamilifu. Bali Mungu ametengeneza njia ambayo mnaweza kulisikia NENO KAMILIFU kila wakati mnapokusanyika.
Watu, vivyo hivyo na wahudumu, wanataka vibadala leo. Je, unaweza kuwazia mtu fulani kumfanyia mhudumu kile wao wanachomfanyia Ndugu Branham?… “Nitakupa dakika 30 kisha yakubidi usitishe, nina ujumbe ninaotaka kuuleta.
Mnaweza kuzisikia kanda wakati wowote. Mimi ninajua kile ambacho kusanyiko hili linachohitaji kusikia ambacho ni cha sasa hivi kwa ajili siku hii.” Wengi wao hawatacheza hata sehemu ya kanda, na wanasema ati ni vibaya kuicheza Sauti ya Mungu makanisani mwao.
Je, kuna mtu yeyote mwenye akili timamu anaweza kuwazia kwamba mhudumu ambaye angetoa udhuru, udhuru wowote, ili kutoicheza Sauti ya Mungu kanisani mwao kwa sababu wao wanaamini wanapaswa kuhubiri? Wanaisema, bali hawaiamini kuwa ni Sauti ya Mungu, vinginevyo wasingetoa kamwe udhuru wowote wa kutozicheza kanda.
Mtu anawezaje kudai kwamba anaamini hii ni Sauti ya Mungu naye hangetaka kuicheza kanisani mwao? Watu wanawezaje kudai kwamba wanaamini hiyo ni Sauti ya Mungu inayonena na huku hawawadai wachungaji wao wazicheze kanda makanisani mwao? Kwa sababu wao wana roho ile ile.
Usiwe Nikodemo na kusema, “Ninaliona na ninaliamini. Ni Mwana wa Adamu akijifunua katika mwili wa mwanadamu. Ni Bwana Asema Hivi. Ni Ujumbe mkamilifu. Ni Sauti ya Mungu iliyo kwenye kanda, bali siwezi tu kuishusha huduma yangu na kusema Sauti hiyo ndio muhimu zaidi kwa kanisa langu kuisikia.”
Ndugu na dada, huenda msikubaliane nami hasa kabisa kabisa kwenye hili. Siwaombi mkubaliane nami. Jambo pekee, ninyi lifikirieni tu. Lile mtakaloniambia, nitalifikiria. Ikiwa wachungaji wanaliambia kanisa lao kwamba wao hawaamini katika kuzicheza kanda makanisani mwao, hiyo ni sawa, ndugu yangu. Wewe walishe chochote unachotaka.
Mimi ninajaribu niwezavyo kudumu sawasawa na Neno, kwa sababu kondoo hawahitaji kitu kingine chochote ila chakula cha kondoo nasi tunaamini Sauti iliyo kwenye Kanda ndio Chakula chetu cha Kondoo. Hiyo ndio tunayoishi kwayo: kila Neno litokalo…Si Neno moja mara hii na mara nyingine; bali kila Neno litokalo kinywani mwa Mungu lisemwalo kwenye kanda; hilo ndilo tunaloishi kwalo.
Mungu nisamehe na mnisamehe ikiwa niliwaudhi au nilisema jambo fulani baya. Hili ndilo tu sisi tunaloliamini na kuona kuwa Kweli tunayoishi kwayo. Mungu ametupa NJIA KAMILIFU ya kuisikia Sauti Yake nasi tunaipenda.
Kama kawaida, ninamwalika kila mtu anayetaka kuungana nasi kuisikia Sauti Hiyo kwa wakati mmoja, kuungana nasi saa 6:00 MCHANA, masaa ya Jeffersonville,(Ni saa 1 JIONI ya Afrika Mashariki) ambapo tutaungana kama Jamii Moja kusikia: 65-0822M Kristo Amefunuliwa Katika Neno Lake Mwenyewe.
Ndugu. Joseph Branham
Maandiko ya kusoma kabla ya kuusikia Ujumbe:
Kutoka 4:10-12
Isaya 53:1-5
Yeremia 1:4-9
Malaki 4:5
Luka Mt. 17:30
Yohana Mt. 1:1 / 1:14 / 7:1-3 / 14:12 / 15:24 / 16:13
Wagalatia 1:8
2 Timotheo 3:16-17
Waebrania 1:1-3 / 4:12 / 13:8
2 Petro 1:20-21
Ufunuo 1:1-3 / 10:1-7 / 22:18-19