NUKUU YA LEO KWA KISWAHILI

23-0530

58-1004 – Imani Ndiyo Ushindi Wetu

Jisalimishe! Kuwa sawa na Mungu! Ama uwe kile ulicho, au usiwe kabisa. Endapo Biblia ya Mungu hailifundishi, basi jiepushe nalo. Kama inalifundisha, dumu Nalo.

Inanikumbusha jambo hili. Kwa mfano, vipi kama tungefunga safari kidogo, katika siku thelathini tangu sasa, kwenda kwenye nchi nyingine? Na katika nchi hii, hali ya hewa ilikuwa nzuri sana, hata hatungerudi tena. Na huko isingetulazimu kufa wala kuzeeka, bali tungekuwa huko milele.

Je, ningeweza kuwazia nikikuona ukienda kwenye duka la mali rahisi, ukinunua vikorokoro vingi kwenda navyo? Ungekuwa ukijaribu kuondoa vikorokoro ulivyo navyo.

Na unapojihangaisha tu, kwa kujiunga na kanisa moja na kisha lingine, utajikusanyia takataka zaidi. Lakini ikiwa utatafakari unakoenda, utaondoa mashaka hayo mengi na upuuzi huo. Utakuwa na imani halisi.

MKATE WA KILA SIKU

…vinavyoonekana ni vya muda tu; bali visivyoonekana ni vya milele: 2 Wakorintho 4:18

23-0529

51-0727 – Kanisa la Mungu Aliye Hai

Ikiwa umechoka na kusononeka na kujisikia kana kwamba kila mtu yuko kinyume chako, “Njooni kwangu ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha.” Hiyo ni mbegu. Ikubali. Na kama wewe ni mgonjwa, “Alijeruhiwa kwa makosa yetu, kwa kupigwa Kwake sisi tumepona.” Likubali. Ni mbegu: itazaa.

Unapopanda mbegu, huichimbui kila asubuhi ili kuona ikiwa imetokeza. Ukifanya hivyo, mbegu yako haitachipuka kamwe. Huna budi kuipanda, ikabidhi kwa ardhi, na kuiacha. Ni juu ya maumbile, Mungu, kuimwagilia maji na kuhakikisha kwamba inazaa. Hiyo ni kweli?

Hivyo ndivyo unavyofanya Neno la Mungu. Lipokee kwa moyo mwema, uliokwisha rutubishwa, na wanyama wote watambaao, na mahali penye miamba, na mashaka ya jiwe yameondolewa, na katika udongo mzuri wa imani, na kuliamini, likabidhi kwa Mungu, na uende zako, ukishuhudia kwamba umepokea kile Mungu alichokuahidi.

Naye ni Kuhani Mkuu wa maungamo yako, ili kukifanya kweli chochote ulichokiri kwamba Yeye amefanya. Hiyo ndiyo Injili.

MKATE WA KILA SIKU

Lakini mimi ningemtafuta Mungu, Ningemwekea Mungu daawa yangu Ayubu 5:8

23-0528

58-0209A – Msikieni Yeye

Sio kanisa takatifu; ni Roho Mtakatifu ndani ya Kanisa ndiye anayelifanya takatifu. Si mtu mtakatifu; ni Roho Mtakatifu ndani ya mtu anayefanya jambo hilo. Si mtu mtakatifu, hakuna kitu kama hicho; ni Roho Mtakatifu. Na Petro alikuwa akiuelezea huu kuwa mlima mtakatifu, kwa sababu Mungu mtakatifu alikutana nao kwenye mlima huu. Ilikuwa ni ardhi takatifu.

Na hebu nisimame hapa alasiri ya leo na kusema hivi: ya kwamba kila mmoja wenu ninyi watu mliozaliwa mara ya pili na Roho Mtakatifu, mnakumbuka saa ile hasa ambapo Roho Mtakatifu, mahali pale alipokutana nanyi. Na mashaka yanapokuja, na woga kuanza kuinuka, daima kuna mahali hapo, ambapo unaweza kurudi kwenye wakati ule ambapo ulipokutana na Mungu, naye ibilisi hawezi kukanyaga mchanga huo mtakatifu.

Ni pale ulipokutana na Mungu na ukazungumza naye. Ingawa hofu na mambo huinuka, hayana uhusiano wowote na jambo hilo. Unajua ulikutana na Mungu kwenye mchanga huo mtakatifu.

MKATE WA KILA SIKU

… Naye Roho ndiye ashuhudiaye, kwa sababu Roho ndiye kweli. 1 Yohana 5:6

23-0527

65-0725E – Nini Kinachovutia Kule Mlimani?

Nadhania, wale watu walipotaka kuangua kicheko, waliondoka wakaenda mbele ya mlango wa ile safina na kucheka. “Vipi, ulisema ingenyesha miaka mia moja iliyopita! Babu yangu aliniambia alikusikia huku juu ukisema ya kwamba itanyesha, nawe ungali unachonga-chonga kipande hiki cha mbao hapa. Mbona huwezi kujitambua mwenyewe?”

Bali ilikuwa Mungu akijitayarisha kuthibitisha ahadi na kutimiza unabii ambao nabii Wake alikuwa ametabiri. Jambo lisilo la kawaida kabisa! Mungu akitimiza ahadi Yake kwa Nuhu, huku wengine wakicheka.

Mungu alikuwa pia akijitayarisha kufanya historia kuonyesha wengine, hata leo, ya kwamba Yeye hutimiza Neno Lake!

Haidhuru lisionekane kuwa la kweli jinsi gani, na lisilo na maana vipi, Yeye hata hivyo hutimiza Neno Lake.

MKATE WA KILA SIKU

Mungu si mtu, aseme uongo; Wala si mwanadamu, ajute;
Iwapo amesema, hatalitenda? Iwapo amenena, hatalifikiliza? Hesabu 23:19

23-0526

62-0117 – Kudhania

Je! ulipata kuwazia ya kwamba Huyo, utasimama Mbele Zake na kutoa hesabu kwa ajili ya Neno hili, na kwa ajili ya Kristo?

Wakati, Mungu ni mtakatifu sana, akikaa huko katika Umilele, wakati majua milioni kumi yangekuwa madoa meusi mbele Zake. Mtakatifu sana, hivi kwamba, hata Malaika wanaonekana wachafu, mbele Zake. Malaika mbele Zake, wao ni wachafu.

Unatarajia wewe na mimi, pamoja na Neno Lake na Damu ya Mwanawe kutusafisha na dhambi, na kukiuka amri Zake moja kwa moja na kuingia moja kwa moja ulimwenguni, na kutarajia kusimama pale bila hatia, wakati ulijua vizuri kuliko kufanya hivyo?

Kanisa bora ujiweke sawa. Usininii, hebu na tusidhanie jambo hili, kwa sababu tu idadi kubwa kuliko tulivyokuwa, na tuko katika hali nzuri kifedha kuliko tulivyokuwa. Tuna majengo mazuri kuliko tuliyokuwa nayo. Tungevalia nguo nzuri kuliko tulizokuwa tukivaa. Tunatumia…Tuna magari mazuri zaidi kuliko tuliyokuwa nayo.

Lakini, loo, ndugu, nashangaa kuhusu Kristo, Yuko pamoja nasi kiasi gani. Mnaona?

MKATE WA KILA SIKU

Bali ninyi ni mzao mteule, ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu wa milki ya Mungu, mpate kuzitangaza fadhili zake yeye aliyewaita mtoke gizani mkaingie katika nuru yake ya ajabu: 1 Petro 2:9

23-0525

65-0801E – Matukio Yakidhihirishwa Na Unabii

Mnaona, Biblia haijipingi Yenyewe; Biblia ni Mungu. Hakuna kuhitilafiana kwa Mungu; Yeye ni mkamilifu.

Lakini watu, kwa ufasiri wao wenyewe! Sasa angalia, hebu niwaonyeshe, enyi marafiki. Makanisa hayawezi kukubaliana juu ya fasiri Yake. Mmethodisti hawezi kukubaliana na Mbatisti, Mbatisti hawezi kukubaliana na Mpresbiteri, Mpresbiteri na Wapentekoste. Na kukiwepo na kama madhehebu arobaini ya Wapentekoste, wao hawawezi kukubaliana wao kwa wao. Kwa hiyo unaona, hiyo ingekuwa ni Babeli tena, mchafuko.

Lakini Mungu hujifasiria Mwenyewe Neno Lake. Yeye aliahidi jambo hili, na halafu analifanya Mwenyewe. Hutoa, Yeye Mwenyewe, fasiri Yake, kwa maana Yeye hujitambulisha Mwenyewe katika saa hiyo.

Ni mbali jinsi gani Mwi—Mwili wa Kristo umekwenda, kutoka miguuni mpaka kichwani!

MKATE WA KILA SIKU

Akawaambia, Enyi msiofahamu, wenye mioyo mizito ya kuamini yote waliyoyasema manabii: Luka 24:25

23-0524

54-0402 – Kipofu Bartimayo

Baadhi ya watu waligusa vazi la Yesu wakapona. Wengine walimpiga kofi usoni na kumpiga kichwani kwa fimbo, na kumtemea mate usoni, wao hawakuwahi kuhisi nguvu zozote hata kidogo. Ilikuwa ni mtazamo wao wa kuliendea jambo hilo. Inategemea ni mtazamo gani unaokuja nao.

Ikiwa unakuja ukiamini kwamba unakuja kupata msaada na una hakika kwamba unamjia Mtu sahihi, Yesu Kristo, nawe unakuja kwa njia yake aliyoiandaa ya kuliendea, utapokea kitu ikiwa unakuja kwa kicho.

Ukija, “Vema, nitakwenda kugusa na kuona kama itanisaidia,” hilo halitasaidia hata kidogo. Unaona? Ni ninii yako—ni jinsi wewe unavyoliendea jambo la Kiungu la Mungu ndiyo linalofanya jambo hilo.

Kama yule nyoka wa shaba. Mbona, nyoka hakuwa na nguvu ndani yake; kilikuwa kipande cha shaba walichokileta kutoka Misri. Wala lile birika halikuwa na nguvu yoyote ndani yake, hata kidogo. Bali ilikuwa ni kutii yale Mungu aliyosema yafanywe, ndicho kilicholeta uweza, kilicholeta nguvu, ni utii kwa Neno la Mungu. Na hilo ndilo jambo lile lile usiku wa leo

MKATE WA KILA SIKU

Na sasa simameni, mkalione jambo hili kubwa, BWANA atakalolitenda mbele ya macho yenu. 1 Samweli 12:16

23-0523

54-0301 – Malaika wa Agano

Unajua, Maandiko Matakatifu yanatolewa kwa uvuvio. Hu—hujifunzi hayo shuleni. Hayana budi kuja kwa ufunuo wa Roho Mtakatifu. Haijalishi wewe ni mwerevu na mjanja kiasi gani, Roho Mtakatifu ndiye hulifunua Neno la Mungu.

Angalia wale Mafarisayo katika siku za Yesu, Masadukayo, na waalimu, watu watakatifu wasio na mawaa, wasomi, walipaswa kuzaliwa katika ukoo fulani, Walawi. Ilibidi kufundishwa tangu ujana na kukua katika Maandiko na kujua kila maana, na hata hivyo wakashindwa kumwona Yesu na kumtambua, wakati Maandiko yote yamejaa jambo hilo, juu ya kuja Kwake. Mnapata ninalomaanisha?

Kwa hiyo usitarajie kumjua Mungu kwa elimu au theolojia; unamjua Mungu kwa kuzaliwa mara ya pili, kuzaliwa upya. Roho Mtakatifu aliliandika Neno la Mungu. Naye amelificha humo ndani; Alisema, “Nimelificha machoni pa wenye hekima na akili, nami nitayafunua kwa watoto wachanga wanaoweza kujifunza.” Kwa hiyo ikiwa unataka kujua jambo lolote, jifanye mtoto mchanga. Usiwe mwerevu sana.

MKATE WA KILA SIKU

Kama watoto wachanga waliozaliwa sasa yatamanini maziwa ya akili yasiyoghoshiwa, ili kwa hayo mpate kuukulia wokovu: 1 Petro 2:2

23-0522

54-0811 – Utuonyeshe Baba

Nchi ikatambua kuwa ni Yeye. Ilitikisika kwa tetemeko kuu la nchi alipokufa. Mwezi na jua vilificha uso wao. Muumba wao mwenyewe alikuwa anakifa pale Kalvari. Jua liliacha kuangaza katikati ya mchana. Namwona akishuka moja kwa moja hadi kwenye milango ya kuzimu. Loo, najisikia wa kidini usiku wa leo.

Angalia ndugu…nimeona…najua ninachozungumzia. Sijapotea katika ukungu. La, bwana. Najua pale ninaposimama. Ndiyo, bwana. Naye akashuka moja kwa moja hadi sehemu za chini za kuzimu, akabisha hodi. [Ndugu Branham anabisha—Mh.] Shetani akaja, akasema, “Ni nani aliyepo hapo?”

Akasema, “Fungua.”

“Wewe ni nani?”

” Fungua.”

Shetani akafungua na kusema, “Oh, kwa hiyo hatimaye umefika, sivyo?” Kasema, “Nilifikiri nilikupata nilipomuua Habili. Nilipomtupa Danieli kwenye tundu la simba, nilifikiri nimekupata. Nilifikiri nilikupata nilipowaweka wale wana wa Kiebrania kwenye tanuru la moto. Nilipomkata kichwa Yohana Mbatizaji, nilifikiri nilikupata, lakini sasa, nimekunasa. Umewasili. Umefika, sivyo?”

“Shetani,” Yesu akasema, “nipe funguo za mauti na kuzimu. Huvimiliki vitu hivyo.”

“loo, ndiyo ninazo. Nimezimiliki, kwa sababu huko nyuma katika bustani ya Edeni, Adamu alitenda dhambi.”

Lakini Yeye akasema, “Mimi ni Mwana wa Mungu aliyezaliwa na bikira. Nimetoka kutoka kifuani mwa Baba. Nimekufa muda huu kule Kalvari, na Damu Yangu ingali inadondoka kutoka msalabani. Nimeshuka kuteka mateka.” Hiyo ni kweli. “Humwogopeshi mtu yeyote kuanzia hivi sasa na kuendelea. Ulishindwa wakati mmoja. Ulikuwa nazo, lakini sasa hauzimiliki tena. Mimi ndiye mmiliki.” Hiyo ni kweli.

“Nitalipa kanisa langu funguo za Ufalme.” Akashika ubavuni mwake, akazinyakua funguo kutoka kwake, akampiga usoni, na kumrudisha ndani, na kuufunga mlango kwa nguvu sana hata kutikisa vigingi vyenye masizi vya kuzimu machoni pake. Haleluya.

MKATE WA KILA SIKU

Hivyo husema, Alipopaa juu aliteka mateka, Akawapa wanadamu vipawa. Waefeso 4:8

23-0521

58-1221E – Umoja Wa Mungu Mmoja Katika Kanisa Moja

Kuna watu wengi sana leo hii wanaosema, kwamba, “Roho Mtakatifu si halisi leo.”

Ingawa makumi ya maelfu yao, na mamilioni, wanasema Sivyo ilivyo, kunao wengi wanaofurahia baraka Zake. Wengi wao ni maskini, watu ambao wamekataliwa na kukataliwa na ulimwengu, watu ambao wametupwa nje ya makanisa kwa sababu waliamini kwamba Mungu ni Mungu, lakini wamejazwa na Roho Wake.

Wana nia moja. Wao ni moyo mmoja. Watu hao ni akina nani? Mmethodisti, mbaptisti, mpresbiteri, mkatoliki, Shahidi wa Yehova, Mworthodoksi, myahudi, wote pamoja, wanakuwa kitu kimoja.

Si mmoja, kwa kanuni ya imani; si mmoja, kwa dhehebu; hiyo ni kazi ya shetani, kupitia mawazo ya kiakili.

Lakini, utendaji wa Roho Mtakatifu, Ufalme wa Mungu ndani yako!

MKATE WA KILA SIKU

…Tazama, ufalme wa Mungu umo ndani yenu. Luka 17:21

23-0520

59-0823 – Tunutu, Nzige, Parare, Madumadu

Kanisa linasonga polepole sana kwa ajili ya saa tunayoishi. Kuna kitu kimeenda vibaya kabisa. Na inatupasa sisi katika siku hii, katika kukaribia kwa Kuja kwa Bwana, kuketi chini na kusoma hili na kuona kuna shida gani, tutafute chanzo chake. Kamwe huwezi kupata tiba mpaka upate chanzo chake.

Kama daktari, kama ukiingia ofisini mwake na kusema, “Ninaumwa na kichwa, na kuumwa na tumbo,” naye akupe aspirini ndogo, ama chochote kile, na kukuachilia, anajaribu tu kukuondosha. Daktari halisi, wa kweli, atakichunguza kisa hicho mpaka agundue ni kiungo gani kina shida, ndipo akishughulikie kiungo hicho.

Hivyo ndivyo ilivyo na Ufalme wa Mungu. Tunapaswa kujua kuna shida gani, kisha tuishughulikie hiyo.

MKATE WA KILA SIKU

Ee Mungu, unichunguze, uujue moyo wangu,
Unijaribu, uyajue mawazo yangu: Zaburi 139:23

23-0519

61-0903 – Vivyo Hivyo Nuru Yenu na Iangaze Mbele ya Watu

Nina mtoto mchanga Utukufuni, ambaye aliwekwa wakfu tu, hakubatizwa.

Kwa sababu, ubatizo ni kwa ajili ya ondoleo la dhambi, unaona, kuonyesha ya kwamba wewe umetubu. Mtoto huyo mchanga hajafanya jambo lo lote la kutubia. Ni mtoto mchanga, ndiyo kwanza tu azaliwe hapa ulimwenguni. Hana nguvu za kujia hapa, unaona, na wala hana dhambi.

Kristo alipokufa Msalabani, alikufa apate kuondoa dhambi ya ulimwengu. Mpaka mtoto huyu mchanga atakapofanya jambo fulani la kutubia, Damu ya Yesu Kristo inamfanyia upatanisho.

Lakini sasa mama na baba, wazazi, wana haki ya kumleta huyo mtoto mdogo, na kumtoa kwa Mungu, huyo mtoto mchanga waliyepewa na Mungu.

MKATE WA KILA SIKU

Kilichozaliwa kwa mwili ni mwili; na kilichozaliwa kwa Roho ni roho. Yohana 3:6

23-0518

60-1125 – Mkutano

Mtu mmoja alisema si muda mrefu uliopita, kasema, “Si—sitaki kumsumbua Mungu. Unajua ni—najua Yeye ana shughuli nyingi sana.” Upuuzi. “Si—sitaki ku…” Vema, huwezi kumaliza baraka Zake zilizo tele. Je, unaweza kuwazia samaki mdogo mwenye urefu wa karibu nusu inchi, huko katikati ya Bahari ya Pasifiki akisema, “Afadhali ninywe maji haya kidogo-kidogo, kwa sababu huenda nikaishiwa”?

Je, unaweza kuwazia maskini panya mwenye ukubwa kiasi chini huko ya ghala kuu za Misri akisema, “Afadhali nile, nijigawie nafaka mbili tu kwa siku msimu huu wa baridi, naweza nikaishiwa kabla ya mavuno yajayo?” Huo ni ujinga. Naam, na ni ujinga mara mbili ya huo, mara elfu zaidi, kuwazia unaweza kumaliza rehema za Mungu mwenye rehema.

Mbona, Yeye anajaribu kuingiza njia Yake ndani yako. “Ombeni kwa wingi ili furaha yenu iwe timilifu.” Hakuna njia ya kummaliza yeye.

Kama vile pampu, unavyosukuma zaidi, ndivyo maji yanavyokuwa safi. Loo, nami nalipenda hilo. Endelea tu kusukuma, ukiishi kwenye kitiririsha maji ambapo utukufu unatokea. Napenda jambo hilo.

MKATE WA KILA SIKU

Waandaa meza mbele yangu, Machoni pa watesi wangu. Umenipaka mafuta kichwani pangu, Na kikombe changu kinafurika. Zaburi 23:5

23-0517

63-0803E – Ushawishi

Nikimwona mtu akitembea, kijana mwenye sura nzuri, katika miaka michache, tazama nywele zake zikigeuka kuwa mvi na kung’oka, mabega yake yanainama. Kijana mwanamke mrembo amesimama, mwenye uso wa kitawa, mcha Mungu, akisimama na kumsifu Mungu; nami narudi katika muda wa miaka michache na kumkuta ana mabega yaliyoinama, huku amebeba watoto wawili watatu.

Vema, jamani, pale, inaonyesha ya kwamba katika mwili huo mna mauti. Haidhuru ni mzuri vipi na unaonekana mrembo vipi, ungali una mauti ndani yake.

Basi natazama kule hiyo roho mle ndani inakoegemea. Ikiwa daima inawakilisha Nuru, inanena kuhusu Nuru, inazungumza habari za Nuru, itaambatana na Nuru. Bali kama kila mara iko upande ule mwingine, wa dunia, wa mambo ya ulimwengu, inashawishiwa na ulimwengu, hamna lingine ila kwake kuingia gizani inapokufa, kuingia katika giza la nje.

Kwa hivyo unaona, tulivyo sisi, hatuna budi kukumbuka ya kwamba sisi tuko jinsi tulivyo kwa neema ya Mungu, na hamna mmoja wetu anayeweza kujivunia hayo. Tunaweza tu kuinama katika kusujudu na kwa unyenyekevu, mbele za Mungu, na kumshukuru kwa wema Wake.

MKATE WA KILA SIKU

Na rehema zake hudumu vizazi hata vizazi Kwa hao wanaomcha. Luka 1:50

23-0516

55-0223 – Ayubu

Huyo hapo, akielekea kule Kalvari.
Anapopanda kilimani, na maskini, bega Lake limechubuliwa, yule nyuki wa kale wa mauti akivuma kumzunguka, “Haitachukua muda mrefu hadi nitakapompata.”

Akivuma pande zote akizunguka, na baada ya muda ilibidi kumchoma. Lakini, rafiki, unajua, kama nyuki akiwahi kumuuma mtu yeyote sana, hawezi kuuma tena. Anauondoa mwiba wake. Kwa hiyo hana mwiba tena.

Nami nawaambia, hiyo ndiyo sababu Mungu alifanyika mwili, hapa duniani, kusudi ahuchukue mwiba wa mauti. Na sasa ki—kifo hakina uchungu tena. Nyuki anaweza kujikusanya na kupiga kelele, lakini hawezi kuuma. “Ee mauti, u wapi uchungu wako? Kaburi, u wapi ushindi wako?”

Lakini Kristo, Mkombozi wa jamaa ya karibu amefanya njia ya kuepukia kwa kila mwamini katika dunia hii leo. Nyuki anaweza kuvuma; nyuki anaweza kupiga kelele; nyuki anaweza kujaribu kukutia hofu. Lakini ninaweza kuelekeza huko Kalvari, ambapo Mungu Mwenyewe alifanyika mwili, wakati aliposhikilia mwiba wa mauti, na kuchukua mahali pangu kama mwenye dhambi, na kulipa gharama.

MKATE WA KILA SIKU

Nitawakomboa na nguvu za kaburi; nitawaokoa na mauti; ewe mauti, ya wapi mapigo yako? Ewe kaburi, ku wapi kuharibu kwako? Kujuta kutafichwa na macho yangu. Hosea 13:14

23-0515

61-1015E – Heshima

Sasa, Nuhu alikuwa na ufunuo kutoka kwa Mungu, hata hivyo ulikuwa kinyume cha cho chote ambacho sayansi ingethibitisha kuwa kweli. Lakini hata hivyo alizungumza na Mungu, na Mungu alikuwa amezungumza naye. Naye aliendelea kujenga safina.

Ambapo, wenye dhihaka na wenye mizaha, kama Biblia ilivyosema kwamba wangelikuwa katika siku za mwisho kama vile walivyokuwa katika siku hizo, kwamba hao wenye dhihaka walimdhihaki Nuhu. Mbona, walifikiria kwamba yeye ni mwenda wazimu kwa sababu alikuwa anajenga safina.

Kwa hiyo, lakini Mungu alileta hukumu juu ya hao wenye dhihaka, kwa sababu wasingemsikiliza mjumbe wa Mungu na kuingia safinani chini ya mahubiri yake, basi Mungu akatuma hukumu Zake duniani. Kwanza Yeye alifanya matayarisho kwa wote ambao wangeliupokea, kuikimbia, na halafu kama hawakuikimbia, kuna jambo moja tu lililobakia.

Kama hawayakubali matayarisho ya Mungu ya kuponea, basi kuna kitu kimoja tu kilichobakia, hiyo ni hukumu ya Mungu.

Unaweza tu kufanya mambo mawili, aidha rehema ama hukumu. Yakubidi ukubali moja au jingine.

MKATE WA KILA SIKU

Ndugu, msinung’unikiane, msije mkahukumiwa. Angalieni, mwamuzi amesimama mbele ya milango. Yakobo 5:9

23-0514

63-0113M – Kutoa Presha

Wakristo, kutoka dhehebu moja hadi lingine, inaonyesha kwamba kamwe hawajapata kuja kwenye kimbilio hilo. Mnaona?

Wanaenda wakati mwingine kwenye seminari. Hilo ni sawa. Nao wanajifunza Neno vizuri tu wawezavyo. Wanakuja nyumbani, na kujaribu kuzungumza Neno hilo vizuri kadiri tu dhehebu lao linavyowaruhusu kulizungumzia. Na hilo ni zuri. Bali hilo silo. Sio kulijua Neno Lake, bali ni kumjua Yeye. Yeye!

Mbona, hakika! Sio kiasi cha Neno ukijuacho, jinsi ulivyo na kanisa zuri, yale dhehebu letu linayomaanisha kwa ulimwengu, ni maachilio mangapi tuliyo nayo kwa hili, na ni ushirika kiasi gani tulio nao pamoja na ulimwengu, ni umati wa namna gani unaokuja. Ni wewe. Je, uko chini ya damu?

Endapo wewe, kama mtu binafsi, sijali kama kila mmoja wa kusanyiko amekosea, wewe ungali salama. Uko chini ya Damu.

MKATE WA KILA SIKU

Kuwaogopa wanadamu huleta mtego; Bali amtumainiye BWANA atakuwa salama Mithali 29:25

23-0513

56-1215 – Msikieni Yeye

Na kila Neno la Mungu ni Mbegu. Na kama Mbegu hiyo inaweza kupandwa kandokando ya Chemchemi ya Uzima isiyokauka, ambayo ni Kristo, mwamini hana budi kunywa kupita mawazo yake, kunywa na kusukuma kutoka nje. Sukuma kutoka nje kila kitu unachohitaji, maana kimo ndani yako unapompokea Kristo. Nasi tumepandwa pamoja katika Kristo. Naye ndiye Chemchemi ya Uzima isiyokauka.

Na usiogope kamwe kuomba mambo makubwa. Mungu anataka uombe mambo makubwa. Hataki wewe kuwa kijitu kidogo kisicho Nathamani na mtoto. Anataka uombe mambo makubwa ili furaha yako iwe timilifu.

Ungeweza kuwazia samaki mdogo wa ukubwa huo, huko chini katika Bahari ya Atlantiki, aseme, “Afadhali ninywe haya maji kidogo-kidogo , huenda nikaishiwa.” Upuuzi.

Ungeweza kuwazia panya mdogo wa ukubwa huo chini huko kwenye maghala makubwa ya Misri, akisema, “Afadhali nile punje mbili kwa siku, maana huenda nikaishiwa kabla ya majira yajayo ya kiangazi.” Naam, huo ni upuuzi. Ikiwa wangekuwa na panya laki kumi wa ukubwa huo, hawangeweza kamwe kuyamaliza. Nao walikuwa na mabilioni mara mabilioni ya tani ya hao samaki, wasingeweza kamwe kuyamaliza hayo maji.

Na ni mara ngapi tungeweza kuzidisha; usingeweza kamwe kummaliza Mungu katika nguvu zake na rehema zake kwa watoto wake. Yeye ndiye Chemchemi isiyokauka ya Uzima. Wewe Kunywa tu, kunywa, kunywa, kunywa.

MKATE WA KILA SIKU

Hata siku ya mwisho, siku ile kubwa ya sikukuu, Yesu akasimama, akapaza sauti yake akisema, Mtu akiona kiu, na aje kwangu anywe.

Aniaminiye mimi, kama vile maandiko yalivyonena, mito ya maji yaliyo hai itatoka ndani yake. Yohana 7:37-38

23-0512

60-0608 – Kuwa na Makongamano

Nilimsikia mtu fulani akisema wakati mmoja ya kwamba uponyaji wa Kiungu ungekuwa katika ule Utawala wa Miaka Elfu. Vema, una mwili uliotukuzwa wakati huo, kwa hiyo unahitaji wa nini uponyaji wo wote wa Kiungu? Ni she—shetani akijaribu kukuweka mbali katika jambo fulani kule, Utawala fulani wa Miaka Elfu utakuwa kitu fulani; ninyi sasa hivi ni wana na binti za Mungu. Amina.

Ikiwa theolojia yako iliyobuniwa na mwanadamu inakupa tu maji baridi kidogo na kukuambia usubiri, wewe endelea. Lakini nilipata karamu ya kozi kamili ya Roho Mtakatifu. Jinsi…Vema, Mungu asifiwe; Hiyo ni kweli.

Wanataka kukuambia usimame kando papa hapa, na kula maganda fulani, au kung’ata mifupa, na kukuambia kuwa kuku ametoweka tangu miaka iliyopita. Usiamini jambo hilo. Mungu ana mlo kamili wa mraba kwa mtu kamili, ambaye ana imani kamili katika Mwana wa Mungu na kuliamini jambo hilo, naye atafuata maagizo.

Menyu inasomeka, “Yeyote atakaye na aje.” Na “Ahadi ni kwa ajili yenu, na kwa watoto wenu, na kwa hao walio mbali; Na kwa wote watakaoitwa na Bwana Mungu wetu wamjie.”

MKATE WA KILA SIKU

Hatawanyima kitu chema
Hao waendao kwa ukamilifu: Zaburi 84:11

23-0511

59-1227M – Ishara Kuu

Ndugu, ninapomwona Mungu, Mungu wa Mbinguni, alivyokiacha kiti Chake cha enzi, uzuri Wake, na yote aliyokuwa; apate kuzaliwa juu ya lundo la samadi, afunikwe nguo za kitoto, adhihakiwe kwa ishara Zake na maajabu Yake, aitwe ibilisi; je, ati nimwonee aibu? La, bwana.

Acha huu ulimwengu maarufu ufanye yale wanayotaka kufanya. Kwangu mimi, Yeye ni ishara kuu. Roho Mtakatifu ndani yangu anapaza sauti. Huenda akanifanya nitende kiajabu na niwe mwenye kichaa, kwa ulimwengu huu, bali siwezi kumkataa Yeye Yule aliyenifanyia mengi sana. Alipachukua mahali pangu katika mauti. Alipachukua mahali pangu pale Kalvari. Alifanya mambo haya yote.

Alijidhili kutoka Mbinguni, kutoka kwenye viti vyeupe vya enzi vya lulu, ili kuwa mwanadamu; apate kuonja mateso yangu, kupitia kwenye majaribu yangu, kujua jinsi ya kuwa mpatanishi anayefaa ndani yangu, kuniongoza na kunielekeza kwenye Uzima wa Milele. Na kupitia kwenye umaskini Wake, ninafanywa tajiri. Kupitia mauti Yake, ninapewa Uzima, Uzima wa Milele.

Usimkatae. Usimwonee aibu. Usimwonee aibu. Lakini mkumbatie, na kusema, “Naam, Mpendwa Bwana wangu, nipe kama walivyofanya kwenye Siku ya Pentekoste, Bwana. Nipe Roho Mtakatifu. Mmwage moyoni mwangu.

Sijali matineja wanasema nini. Sijali walimwengu wanasema nini. Siwaangalii wao. Ninakuangalia Wewe.” Ni kitu gani? Kujiunga na kanisa? La. Ishara kuu, Imanueli, Mungu pamoja nasi.

MKATE WA KILA SIKU

Kwa hiyo Bwana mwenyewe atawapa ishara. Tazama, bikira atachukua mimba, atazaa mtoto mwanamume, naye atamwita jina lake Imanueli. Isaya 7:14

23-0510

63-0606 – Utuonyeshe Baba

Neno, Yesu alisema, ni Mbegu ambayo mpanzi alipanda. Na mbegu yoyote iliyorutubishwa kwenye udongo mzuri itazaa kwa jinsi yake.

Na sasa ninatambua ya kwamba haya yanarekodiwa. Na kanda hizi, tuna huduma ya kanda, kote ulimwenguni. Na watu wengi, hapa tu usiku wa leo, ambapo yapata watu elfu moja wanasikiliza. Kabla kanda hii haijasimama, kutakuwako na watu elfu kumi mara kumi watakaoisikiliza, mnaona, kote ulimwenguni.

Nami ninaingia kwenye kumbukumbu, nasema hili, kuhusu Neno la Mungu kuwa ni Mbegu. Kama unaweza kuchukua msimamo mzuri wa kiakili kuhusu ahadi yoyote ya Kiungu ya Mungu, Yeye ataitimiza, kama unaweza kujiweka mwenyewe katika mahali pa kuamini ya kwamba ahadi hiyo ilikuwa kwa ajili yako.

Lakini ukimwacha riki fulani kuliweka mbali, kwa elimu nyingi kuliko ajuavyo akili za kutosha kujua jinsi ya kuidhibiti, anaweza kuibandika kwenye wakati fulani uliopita, ama wakati fulani ujao, haitakuwa na nguvu kwako. Kama vile Yesu alivyosema, “Mnachukua mapokeo yenu na kuzitangua amri za Mungu,” mnapojaribu kumweka Mungu kuwa Mungu fulani wa kihistoria, ama mtangulizi Mungu ajaye.

“Ni yeye yule jana, leo, na hata milele.” Yeye ni Mungu tu sasa kadiri alivyowahi kuwa. Na laiti ungaliweza kuchukua msimamo huo, kwamba ahadi hiyo ni kwa ajili yako! Yesu alisema, katika Marko Mtakatifu 11:22, “Amini nawaambia, ukiuambia mlima huu, ‘Ng’oka,’ usitie shaka moyoni mwako, bali uamini ya kwamba yale uliyosema yatatimia, yatakuwa yako.

Ninasema, mwombapo, aminini kwamba mnapokea mliyoomba, mtapewa.” Ni ahadi zaidi jinsi gani ingefanywa kuliko Hiyo? Huna budi kuliamini, kwa sababu ni mbegu.

MKATE WA KILA SIKU

Naye aliyepandwa penye udongo mzuri, huyo ndiye alisikiaye lile neno, na kuelewa nalo; yeye ndiye azaaye matunda, huyu mia, na huyu sitini, na huyu thelathini. Mathayo 13:23

23-0509

64-0122 – Kumtazama Yesu

Sasa tunaona ya kwamba Mariamu alipata ufufuo na Uzima. Vivyo hivyo Yairo, maskini kuhani, mwaminio wa kisiri, kwamba alipomwona Yesu na kumwangalia Yeye, alipata ufufuo na Uzima.

Watu wenye njaa walimwangalia Yeye, siku moja, na wakapata mkate wa kudumisha; mfano kwamba wenye njaa leo hii wanaweza kupata Mkate wa Uzima, si kupata kanuni ya imani. Humpati mwanzilishi, humpati mrekebishaji; unapata Uzima unapompata Kristo, Mkate wa Uzima.

Mwizi anayekufa alimwangalia Yeye, katika wakati wa dhiki, naye alipata nini? Alipata msamaha Wake. Ni nani mwingine angalimwangalia? Utawala wa Kirumi usingeweza kumsamehe. Hakuna mwingine yeyote angaliweza kumsamehe. Bali alimwangalia Yesu, katika dhiki yake, ndipo akampata Mtu aliyeweza kumsamehe.

Ndugu yangu, dada, usiku wa leo, ikiwa unaning’inia kama alivyokuwa wakati huo, katika mizani ya hukumu; huku ukijua, kama ungekufa, usiku wa leo, kama mshiriki vuguvugu wa kanisa, ama Mpentekoste vuguvugu, ama chochote kile uwezacho kuwa, unajua unakoelekea.

Mwangalie Yeye, usiku wa leo, Yule awezaye kukuweka huru. Yule, usiku wa leo, kama wewe ni mshiriki tu, na hujui kile ufufuo wa Kristo unamaanisha kuishi katika moyo wa mwanadamu, mwangalie Yeye. Yeye ni Mungu, na Yeye pekee. Utapata msamaha kama vile huyu maskini, mwizi shupavu, aliyelowa dhambi alivyopata, huku amening’inia Msalabani.

MKATE WA KILA SIKU

Kisha akasema, Ee Yesu, nikumbuke utakapoingia katika ufalme wako. Luka 23:42

23-0508

60-0515E – Kufanywa Wana Wenye Mamlaka #1

Lakini katika Mwanzo 2, wakati Yeye alipomuumba mtu, Yeye alisema, “Mimi ni,” Y-a-h-u, J-u-v-u-h, Yahweh, “Yehova.”

Lilimaanisha nini? “Mimi ndimi Yule aishiye peke Yake aliyeumba kitu fulani kutoka kwangu Mwenyewe, kiwe Mwanangu, au mtoto Wangu wa muda, au mdogo.” Utukufu!

Kwa nini? Yeye alimjalia mwanadamu…Yehova maana yake ni kwamba “Yeye alimjalia mwanadamu kuwa mungu mdogo.” Kwa sababu Yeye ni Mungu Baba, na Yeye alimfanya mwanadamu kuwa mungu mdogo, kwa hiyo Yeye si anayeishi peke yake tena, Yeye anaishi na familia Yake.

MKATE WA KILA SIKU

Lakini kwetu sisi Mungu ni mmoja tu, aliye Baba, ambaye vitu vyote vimetoka kwake, nasi tunaishi kwake; yuko na Bwana mmoja Yesu Kristo, ambaye kwake vitu vyote vimekuwapo, na sisi kwa yeye huyo. 1 Wakorintho 8:6

23-0507

51-0729E – Muujiza wa Pili

Baadhi ya watu wana imani kubwa kweli namna hii, lolote laweza kutokea. Anayefuata ana imani ya kina sana, inayochukua muda mrefu kidogo. Anayefuata ana imani yenye kina kirefu, huchukua muda kitambo kidogo.

Wengine wana imani kama punje ya haradali. Lakini ikiwa ni imani ya chembe ya haradali, imani halisi, ishikilie; endelea kuiamini tu; itakuwa imani ya gololi; ndipo itakuwa imani ya tunda la zabibu; na kisha itakuwa imani ya mlima.

Itakuleta nje moja kwa moja ikiwa tu utadumu nayo. Ishikilie; itakuleta moja kwa moja kwenye nuru, ikiwa utakaa nayo.

MKATE WA KILA SIKU

Yesu akajibu, akawaambia, Amin, nawaambia Mkiwa na imani, msipokuwa na shaka, mtafanya si hilo la mtini tu, lakini hata mkiuambia mlima huu, Ng’oka, ukatupwe baharini, litatendeka. Mathayo 21:21

23-0506

58-0720E – Kuweka Mashemasi

Na kanisa letu hapa hujitawala lenyewe. Halina dhehebu lo lote wala cho chote kutuma mashemasi wake, linajichagulia mashemasi wake. Hujichagulia mchungaji wake, linachagua wadhamini wake, linachagua kila kitu kiingiacho na kiondokacho kanisani.

Hakuna mtu mmoja aliye na mamlaka yote juu ya cho chote, ni kanisa.

Na kanisa ni wale wajao na kulisaidia kanisa kwa kuhudhuria kwao, na kwa fungu lao la kumi na sadaka zao, ndio walio na mamlaka halisi katika kuwekwa kwa hao.

MKATE WA KILA SIKU

Vivyo hivyo na sisi tulio wengi tu mwili mmoja katika Kristo, na viungo, kila mmoja kwa mwenzake. Warumi 12:5

23-0505

59-0920 – Kupanda Mzabibu Na Mahali Pa Kuupandia

Yale ibilisi afanyayo ni hadithi ya uongo. Yale Mungu afanyayo ni halisi. Kwa hiyo, ninapenda hili lizame ndani kabisa mioyoni. Mungu anapomwokoa mtu, yeye ameokoka. Usiwe na wasiwasi juu ya kurudi nyuma kamwe; huwezi. Kile Mungu afanyacho ni cha Milele.

Ibilisi anaweza kukuchochea na kukufanya uamini umeokoka. Lakini wakati Mungu anapokuokoa kweli, unao milele, kwa sababu unao Uzima wa Milele. Yesu alisema hivyo.

“Yeye ayasikiaye Maneno Yangu, na kumwamini Yeye aliyenipeleka yuna Uzima wa Milele, wala hataingia hukumuni, bali amepita kutoka mautini kuingia Uzimani.” Huo ni wa Milele kama Mungu Mwenyewe alivyo, kwa sababu ni Neno Lake.

MKATE WA KILA SIKU

… Bali wokovu wangu utakuwa wa milele, na haki yangu haitatanguka. Isaya 51:6

23-0504

63-1130B – Ushawishi

Mungu humwagiza mtu Wake, na huwezi kuchukua mahali pa mwingine. Ukichukua, unafanya tu uigaji wa kimwili, na hatimaye utashindwa. Unaona, huwezi kufanya hivyo. Mungu hukuagiza mahali pako.

Isaya aliona hili, kwamba asingeweza kuweka tumaini lake juu ya mtu yeyote. Hapo alikuwepo mtu mashuhuri kuliko wote waliokuweko duniani, wakati huo, mfalme ambaye ulimwengu wote ulikuwa ukimlipa kodi; lakini kwa sababu alitoka mahali pake, Isaya aliona basi kwamba asingeweza kuegemea mkono wowote wa mwanadamu, na hilo likampeleka nabii hekaluni, kuomba.

Ee Mungu! Laiti kanisa, laiti watu wanaojiita wenyewe Wakristo, wangeweza tu kuona hili leo hii, na lingewasukuma madhabahuni mahali fulani kuomba. Huwezi kuwa kitu usicho.

MKATE WA KILA SIKU

Ila nipendalo ni kwamba watu wote wawe kama mimi nilivyo; walakini kila mtu ana karama yake mwenyewe itokayo kwa Mungu, huyu hivi, na huyu hivi. 1 Wakorintho 7:7

23-0503

60-0308 – Upambanuzi Wa Roho

Wajua, ni—nilikuwa nikiwaambia wavulana muda mfupi uliopita wakati nikija huku, nilisema kuhusu jinsi itupasavyo kuwa wenye furaha kila wakati. Mungu hataki uwe na huzuni. Unajua hasira mbaya kile inachofanya? Na hasira hiyo ya kale, hiyo ni moja ya mambo ya kale ya kutisha. Nayo ni-ndiyo karibu asilimia sitini ya chanzo cha magonjwa yote ni hasira.

Ndiyo, bwana, hizo hasi—hasira unazofungulia, kumbuka, unaendeleza tu saratani, kidonda, au kitu kama hicho, unapofanya jambo hilo. Unapofadhaika kuhusu mtu fulani, “Sitarudi kule tena. Ngoja niwape ukweli Wao.” Vema. Kumbuka, wewe ndiye utakayelilipia jambo hilo. Endelea kuwa mwenye furaha tu.

Hadithi hiyo ndogo, ilisema kulikuwa na robini mdogo asubuhi moja, ameketi juu ya kiungo, akimpigia mluzi mwenzi wake mdogo. Yule mwenziwe mdogo akaruka karibu naye na kusema, “Unajua, nina—nina wasiwasi sana asubuhi ya leo kuhusu jambo moja.” Kasema, “Nini?” Kasema, “Sisi akina Robin hatuna Wasiwasi kamwe.”

“Lakini nashangaa tu ikiwa maskini hao viumbe, wanadamu, wanaokunja nyuso zao, wakitembea, nashangaa, labda hawana Baba wa mbinguni anayewaangalia kama sisi akina robin tuliye naye .”

Ni juu ya jambo hilo. Hujawahi kusikia mmoja wao ana shinikizo kuu la damu, sivyo?

MKATE WA KILA SIKU

Furahini katika Bwana sikuzote; tena nasema, Furahini: Wafilipi 4:4

23-0502

60-0308 – Upambanuzi Wa Roho

Zaburi 105 : Mshukuruni BWANA: liitieni jina lake, Wajulisheni watu matendo yake.

Mwimbieni, mwimbieni kwa Zaburi, Zitafakarini ajabu zake zote. Jisifuni kwa jina lake takatifu, Na ufurahi moyo wao wamtafutao BWANA.

Mtakeni BWANA na nguvu zake, Utafuteni uso wake sikuzote. Zikumbukeni ajabu zake alizozifanya, Miujiza yake na hukumu za kinywa chake.

Enyi wazao wa Ibrahimu, mtumishi wake; na Enyi wana wa Yakobo, wateule wake. Yeye, BWANA, ndiye Mungu wetu; Duniani mwote mna hukumu zake.

MKATE WA KILA SIKU

Ingieni malangoni mwake kwa kushukuru;
Nyuani mwake kwa kusifu;
Mshukuruni, lihimidini jina lake. Zaburi 100:4

23-0501

61-1231M – Huna Budi Kuzaliwa Mara Ya Pili

Na kukukaribia kuzaliwa huku, inakubidi kupitia hatua fulani. Ni kama tu vile chochote kilicho hai, chochote kinachoishi tena, hakina budi kufa kwanza.

Wala huwezi kudumisha roho yako ile ile. Huwezi kudumisha tabia zako zile zile. Huwezi kudumisha mawazo yako yale yale. Huna budi kufa. Huna budi kufa kama Yeye alivyokufa! Huna budi kufa madhabahuni Pake, kama Habili alivyofanya na mwana-kondoo wake. Huna budi kufa pamoja na Mwana-kondoo wako. Huna budi kufa.

Kufia mawazo yako mwenyewe, upate kuzaliwa kwenye mawazo Yake, kuacha nia iliyokuwa ndani ya Kristo iwe ndani yako. Huna budi kuyawaza mawazo Yake.

Na sasa, ndugu, dada, hebu niseme hili kwa akili kadiri nijuavyo kulisema. Unawezaje kuyawaza mawazo Yake kisha ulikane Neno Lake, na hata hivyo udai umezaliwa mara ya pili? Hebu jiulize tu swali hilo. Unawezaje? Huwezi.

Kama umezaliwa mara ya pili, unayo mawazo Yake. Endapo nia ya Kristo iko ndani yako, basi wewe ni kiumbe kipya.

MKATE WA KILA SIKU

Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita tazama! Yamekuwa mapya. 2 Wakorintho 5:17

23-0430

65-1207 – Uongozi

Na kama mtoto mchanga aliyeumbika tumboni mwa mamaye. Mtoto anapoingia tu—tumboni mwa mamaye, ile chembechembe dogo, inatambaa hata kwenye yai. Haifanyi chembechembe moja mwanadamu, nyingine mbwa, na nyingine paka, na nyingine farasi. Zote ni chembechembe za binadamu kwa sababu zinafanyika kutoka chembechembe yenye asili ya binadamu.

Na mtu anapozaliwa mara ya pili na Neno la Mungu, akachaguliwa tangu awali Uzima wa Milele, akaitwa “Aliye Mteule,” itakuwa Neno la Mungu juu ya Neno, Neno kwa Neno!

Si kanuni za imani za kidhehebu kisha Neno, na kanuni ya imani; nayo haiwezekani. Hauwezi kuwa na hiyo chachu ndani yake! Mna Uzima wa Milele mmoja tu, Yesu Kristo aliye Neno:

MKATE WA KILA SIKU

Mkavae utu mpya, ulioumbwa kwa namna ya Mungu katika haki na utakatifu wa kweli. Waefeso 4:24

23-0429

61-0216 – Alama Ya Mnyama Na Muhuri Wa Mungu #1

Kaini akawaza mambo haya, “Nitatoa sadaka vitu hivi.” Lakini nadhani sadaka ya Habili ​​haikuwa yakupendeza sana. Huenda hakukuwa na katani yoyote katika siku hiyo, yaweza kuwa mzabibu ulishungushiwa shingoni pa yule maskani mwana-kondoo, akampeleka pale na kumlaza juu ya mwamba.

Hakuwa na mkuki wala kisu wakati huo, kwa hiyo itakuwa alichukua ki—kipande cha jiwe, akakirudisha kichwa chake kidogo nyuma, na kuanza kuikata shingo yake ndogo. Na alipoanza kulia na kupiga mateke, na damu ikipita kote juu yake, akitoka damu, akilia, akifa juu ya mwamba…Iliwakilisha nini? Miaka elfu nne baadaye, Mwana-Kondoo wa Mungu alikatwakatwa hadi kufa juu ya mwamba wenye imara, akilowa damu, akilia, akinena kwa lugha alipokuwa akifa pale Kalvari.

“Loo, Mwana-Kondoo mpendwa anayekufa, Damu Yako ya thamani haitapoteza nguvu zake kamwe mpaka Kanisa lote la Mungu lililokombolewa litakapookolewa lisitende dhambi tena.”

Mipango yetu ya kielimu, mipango ya kimadhehebu haitamaanisha jambo hilo[Ndugu Branham analiza vidole vyake—Mh.]; itachukua Damu ya Yesu Kristo na si kitu kingine cha kufanya jambo hilo. Ndiyo.

MKATE WA KILA SIKU

Nao wakamshinda kwa damu ya Mwana-Kondoo, na kwa neno la ushuhuda wao; ambao hawakupenda maisha yao hata kufa. Ufunuo 12:11

23-0428

62-0128A – Kitendawili

Yesu alipokuwa hapa duniani, alitembea juu ya maji, nielezee hilo. Niambie kisayansi jinsi mtu anavyoweza kutembea juu ya maji,ni kitendawili. Siku moja alichukua biskuti tano na samaki wawili na kuwalisha elfu tano.

Ni aina gani ya atomi aliyoifungua? Sasa, huyo hakuwa hata samaki aliye hai. Wakati alipoumega mkate huo, akaumega kutoka kwenye kipande cha biskuti, alipoutoa, wakati aliporudisha mkono Wake tena, kulikuwa na biskuti nyingine pale, tayari imeinuliwa, ngano shambani, tayari imepikwa, mafuta yote ndani yake, yaliowekwa. Hiki hapa kipande cha samaki, akakimega, na kipande kingine cha samaki aliyepikwa. Amina. Haleluya!

Kipengele hicho kimetolewa kwetu, ikiwa tu tutadumu katika Neno. Baki hapo, naamini tuko mbioni kuliona likitokea. Ishi mkweli kwa Neno.

MKATE WA KILA SIKU

Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake: Yohana 1:12

23-0427

55-0311 – Muhuri Wa Mpinga Kristo

Sasa, ninyi wahubiri, na ninyi wanaume, vivyo hivyo. Hiyo ni kweli. Ni ukweli. Tunachohitaji leo, ni mahubiri mazuri ya mtindo wa kale, makali, ya Injili. akina john wasamawati wakapuao wakale wa kutosha, hadi kitu hicho kiwake. Tunachohitaji, ni kurudi Azusa, kurudi mwanzo, kurudi Pentekoste. Hiyo ni kweli. Amina.

Mungu turehemu. Loo, mnajua kwa nini hatuna utukufu kanisani, mnajua kwa nini jambo hilo liko jinsi hii? Kwa sababu tumeingia kwenye kitu kingine. Loo, “Siionei haya Injili ya Yesu Kristo, kwa maana ni uweza wa Mungu uletao wokovu.”

Si kitu fulani kitakachokufanya kuwa mshupavu wa dini. Ni jambo ambalo litakufanya uwe na akili timamu na halisi, kulifanya kuwa halisi sana kwa watu, mpaka watakuwa na kiu ya kuwa kama wewe. Hiyo ni kweli.

Ulimwengu mzima utatazama na kusema, “Jamani, kama ningeweza tu kutenda kama mwanamke yule. Kama ningeweza kuishi maisha anayoishi.” Na sasa, hilo ndilo tunalohitaji.

MKATE WA KILA SIKU

Heri wenye njaa na kiu ya haki; Maana hao watashibishwa. Mathayo 5:6

23-0426

51-0508 – Imani Ni Kuwa na Hakika

Sasa, nataka kufikia, kwa muda kidogo tu, kutokushindwa kwa Neno, unaona, kwenu. Kwanza, nataka mjue kwamba Mungu hana kikomo. Yeye ni mkamilifu sana hivi kwamba alijua kila kitu ambacho kingekuwako. Je,Unaamini jambo hilo ?

Yeye Alijua jambo hilo kabla ulimwengu haujaumbwa, ya kwamba tungekuwa tumeketi hapa usiku wa leo ikiwa Yeye hana kikomo. Kama Yeye ana kikomo, basi Yeye si Mungu. Kwa hivyo ikiwa Yeye ana kikomo, Yeye yu kama sisi. Lakini kutokuwa na kikomo, hakuna njia ya kulielezea. Na lolote asemalo Mungu ni kamilifu; Hawezi kuliboresha au kulighairi. Ni kamilifu, kwa kuwa Mungu ni mkamilifu, na Maneno Yake ni makamilifu. Ahadi zake haziwezi kushindwa kamwe.

Sasa, Yakupasa uwe na imani ya namna hiyo kwa Mungu unaposoma Biblia ili kuziamini ahadi zake. Yakubidi ukumbuke Yeye ni mkamilifu. Maneno yake ni makamilifu; hayawezi kushindwa kamwe; hayawezi kuboreshwa kamwe; ni makamilifu kwanza Kabisa.

MKATE WA KILA SIKU

Mungu njia yake ni kamilifu; Ahadi ya BWANA imehakikishwa; Yeye ndiye ngao yao Wote wanaomkimbilia. 2 Samweli 22:31

23-0425

63-0126 – Uwekezaji

Sasa, nataka kufikia, kwa muda kidogo tu, kutokushindwa kwa Neno, unaona, kwenu. Kwanza, nataka mjue kwamba Mungu hana kikomo. Yeye ni mkamilifu sana hivi kwamba alijua kila kitu ambacho kingekuwako. Je,Unaamini jambo hilo ?

Yeye Alijua jambo hilo kabla ulimwengu haujaumbwa, ya kwamba tungekuwa tumeketi hapa usiku wa leo ikiwa Yeye hana kikomo. Kama Yeye ana kikomo, basi Yeye si Mungu. Kwa hivyo ikiwa Yeye ana kikomo, Yeye yu kama sisi. Lakini kutokuwa na kikomo, hakuna njia ya kulielezea. Na lolote asemalo Mungu ni kamilifu; Hawezi kuliboresha au kulighairi. Ni kamilifu, kwa kuwa Mungu ni mkamilifu, na Maneno Yake ni makamilifu. Ahadi zake haziwezi kushindwa kamwe.

Sasa, Yakupasa uwe na imani ya namna hiyo kwa Mungu unaposoma Biblia ili kuziamini ahadi zake. Yakubidi ukumbuke Yeye ni mkamilifu. Maneno yake ni makamilifu; hayawezi kushindwa kamwe; hayawezi kuboreshwa kamwe; ni makamilifu kwanza Kabisa.

MKATE WA KILA SIKU

Mungu njia yake ni kamilifu; Ahadi ya BWANA imehakikishwa; Yeye ndiye ngao yao Wote wanaomkimbilia. 2 Samweli 22:31

23-0424

63-0126 – Uwekezaji

Danieli alikusudia moyoni mwake ya kwamba hatajichafua na ulimwengu. Alikuwa anaenda kudumisha utaratibu ambao Mungu alikuwa ameandaa, zile amri za Mungu.

Kwa nini ninyi wanawake na wanaume msiweze kufanya jambo lile lile? Lakini Marilyn Monroe ama mtu fulani walizikata nywele zao, halafu mke wa mhubiri fulani akafanya jambo lile lile, nanyi mnafikiri mna haki ya kufanya hivyo. Hilo haliwaachilii kutoka kwa Neno la Mungu.

Nanyi wahubiri mnawaacha wake zenu wawaongoze. Ni aibu jinsi gani! Ni—ni—ni neno la jinsi gani, la kuwa mwanamume. “Mtumishi wa Kristo asiyeweza kuiongoza nyumba yake mwenyewe, ataongozaje nyumba ya Mungu?”

“Vema,” mnasema, “Ndugu Branham, hayo, hayo ni mambo madogo tu.” Vema.

Hebu na tuyanyoshe mambo yaliyo madogo, ndipo tuliendee jambo kubwa. Mnaona? Ndipo tutazungumza juu ya Roho Mtakatifu, na ma—na mambo ya jinsi ya kupokea karama za Kiungu.

MKATE WA KILA SIKU

Jitakaseni basi, iweni watakatifu: Mambo ya Walawi 20:7

23-0423

57-0908E – Waebrania, Mlango Wa Sita #2

Je! unaghadhabika sana? Wewe ni mgonjwa? Unatilia shaka? Una mvurugiko wa akili hapa na pale? Hivi unashangaa kama ni kweli ama si kweli? Unapomjia Kristo, je! unakuja kwa uhakika kabisa, moyo uliojaa upendo? Je! unamwendea bila woga wowote, ukisema, “Ninajua kwamba Yeye ni Baba yangu”?

Wala hakuna hukumu, umepita kutoka mautini ukaingia Uzimani. Unajua jambo hilo. Na unayaona maisha yako: ni mwenye upendo, mwenye kusamehe, wewe una utu wema, una amani, ni mpole. Matunda yote haya ya Roho yanaambatana na maisha yako, kila siku.

Na mara unapofanya jambo lolote baya, “Loo, jamani.” Mara tu linapokuja niani mwako, “umefanya jambo baya,” upesi unaliweka sawa, papo hapo. Usingojee dakika nyingine, nenda papo hapo na ukaliweke sawa. Usipoliweka sawa, vema, huna Roho wa Kristo.

MKATE WA KILA SIKU

Tukiishi kwa Roho, na tuenende kwa Roho. Wagalatia 5:25

23-0422

63-0119 – Mapito Ya Nabii Wa Kweli

Ningesema jambo hili katika Jina la Bwana: Mungu yeye yule ambaye taifa hili linadhaniwa linamwakilisha ataliangamiza taifa hili. Atayaangamiza makanisa haya. Mungu wa Mbinguni ataishusha ghadhabu Yake katika hukumu na kuyaangamiza makanisa haya, yanayojiita makanisa. Kumbukeni, ninyi lishikeni neno langu.

Hakuna mtu anayeweza kujiunga na Kanisa. Unajiunga na chama. Hujiungi na Kanisa. Unazaliwa katika Kanisa. Unaona? Unajiunga na chama cha Kimethodisti, chama cha Kibaptisti, chama cha Kikatoliki, chama cha Kipentekoste. Bali unazaliwa katika Kanisa la Mungu aliye hai; na hilo ndilo analolijia, Kanisa hilo.

Kwa hiyo, tuna vyama, sio Makanisa. Chochote kinaweza kukusanyika kwenye chama hicho, wanafiki na kila kitu kingine.

Lakini nitawafahamisha hili sasa hivi, kulingana na Neno, hakuna mnafiki hata mmoja katika Kanisa la Mungu aliye hai. Hakuna kitu Mle ila watakatifu.

MKATE WA KILA SIKU

Ole wenu waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnawafungia watu ufalme wa mbinguni; ninyi wenyewe hamwingii, wala wanaoingia hamwaachi waingie. Mathayo 23:13

23-0421

53-0906A – Je, Unasadiki Hayo?

Na kama wanawake, kama ungetambua ni mamia ngapi ya mabilioni ya dola kila mwaka ambayo wanawake wanatumia Marekani kwa ajili ya vipodozi, kila unachoweka pajani mwako—midomoni. Sijui mambo hayo ni kitu gani. Hata hivyo, ni mamilioni ngapi ya dola wanazotengeneza watu hawa kwa vitu hivyo wanajipaka usoni mwao na kujipodoa namna hiyo…

Na wakati maskini watoto wadogo kule na wamishenari wanaoketi hapa kitako kwa sababu hawawezi kwenda. Hawana pesa za kutosha kuendelea. Mungu atakuwajibisha siku ya hukumu. Hiyo ni kweli. Ni ukweli.

Ndio, Wakristo, mnajiita Wakristo, mkija mkiwa mmejiremba na kujipodoa. Kulikuwa na mwanamke mmoja tu katika Biblia ambaye aliyewahi kujipaka rangi usoni mwake na huyo alikuwa Yezebeli. Unajua Mungu alimfanya nini? Alimlisha kwa mbwa. Hiyo ni kweli.

Na unapomwona mwanamke akitenda namna hiyo na kujiita mwenyewe Mkristo, wewe sema, “Unaendeleaje, Ewe bibi nyama ya mbwa?” Hivyo ndivyo yeye alivyo: nyama ya mbwa. Mungu akamtoa kwa mbwa. Ndiyo, bwana.

Loo, tunachohitaji leo ni Roho Mtakatifu mwema wa mtindo wa kale kuchangamsha kati ya watu kuwarudisha wanaume na wanawake kwa Mungu aliye hai tena.

MKATE WA KILA SIKU

Kwa kuwa nia ya mwili ni mauti; bali nia ya roho ni uzima na amani. Warumi 8:6

23-0420

56-0427 – Imani

Hapa wakati fulani uliopita nilisimama Mlima Wilson huko nje ambapo ungeweza kuona kupitia chumba hiki kikubwa cha uchunguzi, kioo kikubwa, kuona miaka milioni mia moja na ishirini ya upeo wa Nuru Angani.

Kwa nini, hiyo ingechukua tisa ngapi kuigawanya kwa maili? Miaka milioni mia na ishirini ya upeo wa nuru angani, na zaidi ya hapo bado kulikuwa na miezi na nyota na kuendelea na kuendelea, mfumo mkuu wa jua. Nami nikasimama pale nikishangaa. Nikasema, “Wazia jambo hilo. Baba yangu wa Mbinguni tu, “Whew.”

Akazipuliza kutoka mkononi Wake namna hiyo, akaziweka mahali, nazo zinamtii. Alikuwa mkubwa vya kutosha kufanya jambo hilo na Yeye alikuja mdogo vya kutosha ili kuniokoa. Akawa mimi ili nipate kuwa Yeye. Kristo alifanyika mwenye dhambi, ili kwa umaskini wake tupate utajiri wake na kuwa wana na binti za Mungu. Amina.

MKATE WA KILA SIKU

… kwani kuna mungu gani mbinguni au duniani awezaye kufanya mfano wa kazi zako, na mfano wa matendo yako yenye nguvu? Kumbukumbu la Torati 3:24

23-0419

61-0205M – Tarajio

Dhehebu fulani, hivi majuzi, kwa sababu kwamba nilimruhusu mhudumu mwingine aketi jukwaani ambaye hakuwa mfuasi wa shirika lao, yeye alisema, “Tumechora mstari. Tumekuweka nje yake, Ndugu Branham, nje ya—nje ya kundi letu.”

Nikasema, “Ninachora mwingine, mkubwa sana, kuwarudisha ndani tena.” Nikasema, “Kwa hiyo ha—hamwezi kunilazimisha nitoke nje.” Hiyo ni kweli. “Nitachora mstari moja kwa moja juu ya huo wenu na kuwaingiza ndani moja kwa moja.” Mnaona?

Hiyo ni kwa ajili ya…Sisi ni ndugu. “Hatujagawanyika; sisi sote ni mwili mmoja.” Kweli. Sisi ni Wakristo, waliozaliwa kwa Roho Wake, tukaoshwa kwa Damu Yake. Sisi ni Wakristo. Inatupasa kutenda kama Wakristo; inatupasa kuenenda kama Wakristo. Wanaume na wanawake, hebu niwaambie hilo ni jambo moja sisi, kanisa limepungukiwa nalo siku hizi, ni kuenenda kama Wakristo.

MKATE WA KILA SIKU

Na kama mnavyotaka watu wawatendee ninyi, watendeeni vivyo hivyo. Luka 6:31

23-0418

54-0103M – Maswali na Majibu #1

Nitawapa makadirio yangu ya yale nadhani kuwa ndiyo yanayokaribia sana ishara, ya kwamba mtu ni Mkristo, kuliko cho chote nikijuacho. Mwajua ni nini? Ni utungu wa nafsi.

Mtu ambaye kila mara ana njaa na kiu cha Mungu. Wao…mchana na usiku, wao—wao hawawezi kujizuia. Yawapasa wamtendee Mungu jambo fulani. Wa—wamejawa na upendo nao…utungu wa nafsi zao, kuwa na utungu wakati wote.

Biblia ilisema, “Yeye aendaye akipanda kwa machozi hakika atarudi tena, kwa kelele za furaha, aichukuapo miganda yake ya thamani.” Sivyo? Mambo hayo yote.

MKATE WA KILA SIKU

Ingawa mtu anakwenda zake akilia,
Azichukuapo mbegu za kupanda.
Hakika atarudi kwa kelele za furaha,
Aichukuapo miganda yake. Zaburi 126:6

23-0416

62-0601 – Kuchagua Upande wa Yesu

Mnakumbuka ile ndoto niliyopata tafsiri yake ilivyokuwa. “Rudi ukakihifadhi chakula.” Ghala lilikuwa wapi?—maskani haya.

Ni mahali gani nchini palipo kama hapa ambapo pangelinganishwa na ujumbe tulio nao? (Sasa, bila shaka, ndugu zetu hapa walio karibu hapa, makanisa haya mengine madogo, ni sisi. Sisi ni mmoja). Ungeenda wapi, kuupata? Onyesha mahali po pote panapoweza kulinganishwa napo. Ukienda moja kwa moja katika kanuni za kidhehebu, utaenda mbali sana na Jina la Bwana Yesu; utaenda mbali na mambo haya mengine. Ona?

Na hapa ndipo chakula kimehifadhiwa.

Vema Ujumbe mmoja niliowahubiria ninyi nyote…Tazama, nimekuwa nikiwahubiria kutoka saa moja hata masaa sita kwa Ujumbe mmoja. Vema, kama ingalinipasa kutumia mmoja wa Jumbe hizo, ningechukua juma moja kuchukua kidogo hapa na kidogo pale (ona?) kwa sababu umehifadhiwa.

Uko kwenye kanda; utaenda ulimwengu mzima katika kanda ambapo watu manyumbani mwao…Hizo kanda zitaangukia mikononi mwa wale waliochaguliwa tangu awali wa Mungu.

Yeye anaweza kuliongoza Neno; yeye ataelekeza kila kitu kuelekea njia yake hasa. Hiyo ndiyo sababu Yeye alinituma nirudi nikafanye hivi. “Kihifadhi chakula hapa.”

MKATE WA KILA SIKU

Na hicho chakula kitakuwa akiba ya nchi kwa ajili ya miaka hiyo saba ya njaa, itakayokuwa katika nchi ya Misri, nchi isiharibike kwa njaa. Mwanzo 41:36

23-0415

56-0108 – Mungu Ana Njia Iliyoandaliwa

Lo, jinsi lipendezavyo! Unajua, labda sisi sote ni watoto wa chupa za Mungu, labda tungesema. Na Mungu alikuwa ametoa chupa mbili tu, Agano Jipya na la Kale, na Yeye ndiye aliyedondosha vitamini vyote ndani yake. Na pindi tunapomshika yeye, kwenda kunyonya, haturidhiki tu, bali tunaponywa, wakati huo huo. Tunapata vitamini vya kiroho.

Inaendelea tu kutujenga, kutufanya kuwa na nguvu zaidi, na zaidi. Ni nzuri. Inayo kalsiamu kwa ajili ya mifupa. Ndiyo. Inayo ya vitamini B ngumu kwa ajili ya mishipa. Lo, ina kila kitu ndani yake. Kabati lote la dawa la Mungu lilishushwa ndani yake. Yote yalikuwa kwenye chupa, iliyowekwa kwenye chupa, na Yeye aliifungua pale Kalvari. Kwa hiyo, kupitia Kalvari, tunaweza kurudisha baraka zozote zilizokombolewa ambazo Yesu alizozifia.

MKATE WA KILA SIKU

WANA ni nguvu za watu wake, Naye ni ngome ya wokovu kwa masihi wake. Zaburi 28:8

23-0414

62-0610E – Kushawishika Kisha Kuhusika

Sasa, Biblia ilisema, “Katika siku za mwisho, mpinga Kristo atakuwa wa kidini sana, na kufanana sana na kitu kilicho halisi, hata ingewadanganya walio Wateule kama yamkini.” Lakini, haiwezekani. Hiyo ni kweli. Na, “Wote.” “Angewadanganya wote, walio juu ya nchi, ambao majina yao hayakuandikwa katika Kitabu cha Uzima cha Mwana-kondoo.” Tangu ule uamsho wa mwisho? Hilo halisikiki kama Biblia, sivyo? [Kusanyiko linasema, “La.”—Mh.] “ Tangu kuwekwa msingi wa ulimwengu.”

Hutawadanganya, maana wao wamekaa moja kwa moja katika Neno hilo. Wanapoyaona mambo hayo yakitokea, [Ndugu Branham anadata vidole vyake.] Ni Uzima, wanaushika sasa hivi.

Wengine watatembea huku na huku, wakisema, “Aa, hakuna kitu katika Hilo. Huh!” Mnaona? Hawajashawishika. Hakuna kitu pale cha kuwashawishi. Hakuna kitu ndani yao, cha kuaminia.

Mama alizoea kusema, “Unawezaje kupata damu kutoka kwa mboga nyekundu wakati hamna damu yoyote mle?” Kweli.

“Kondoo Wangu huisikia Sauti Yangu.” Wanalijua Neno. Sauti Yake ni nini? Hii hapa. Kanuni hizi za imani hawazifuati. “Bali, wanaisikia Sauti Yangu, wanaifuata.”

MKATE WA KILA SIKU

Hao walio pamoja naye ndio walioitwa, na wateule, na waaminifu. Yohana 17:14

23-0413

64-0306 – Aliye Mkuu Kuliko Sulemani Yupo Hapa Sasa

Na wakati mtu aigizapo kitu fulani, kamwe hakijawahi kufanikiwa. Lakini kama tu unaweza kushikilia kitu Fulani, na kitu Fulani hicho kinakushikilia, litatukia.

Kama ukija hapa usiku wa leo kwa ajili ya uponyaji, na umwache Roho Mtakatifu akushikilie, nawe umshikilie Yeye, utapata kile unachoomba. Hakuna njia ya kukutenganisha Nacho.

Ukija ukiamini ya kwamba Yesu Kristo huokoa, na kuna nguvu ya kuokoa inakushikilia, nawe unaishikilia Hiyo, utaokoka.

Kama unaamini katika ubatizo wa Roho Mtakatifu, naye Roho Mtakatifu anakushikilia, Naye atakubatiza, nawe umshike Yeye; haitakulazimu kuondoka kwenye kiti chako, Yeye atakujaza na Uwepo Wake papo hapo ulipo. Kama tu alivyokwisha fanya Yeye, “Petro alipokuwa angali akinena maneno haya, Roho mtakatifu akawashukia hao waliolisikia.” Kitu Fulani kilishikilia!

MKATE WA KILA SIKU

Kwa sababu hiyo nawaambia, Yo yote myaombayo mkisali, aminini ya kwamba mnayapokea, nayo yatakuwa yenu. Marko 11:24

23-0412

53-0325 – Israeli na Kanisa #1

Unasema, “Vema, Mungu atukuzwe, nimeokolewa kwa sababu niliacha kunywa pombe. Utukufu kwa Mungu, nilipatwa na mtetemo ukipitia mgongoni mwangu. Nilipatwa na upepo wa nguvu ukienda kasi uliyonipiga usoni. Je,unaamini jambo hilo, Ndugu Branham?” Hakika. Lakini nataka kuona huo upepo wa nguvu ukienda kasi unatoka wapi, kwanza. Unaona? Hiyo ni kweli . Kweli kabisa.

Hiyo mitetemo, sawa, lakini sijaokolewa kwa sababu nilikuwa na kutetemeka, na wala si kwa sababu nilipatwa na upepo wa nguvu ukienda kasi. “Huamini katika jambo hilo, Ndugu ?” Ndiyo, Naamini. Lakini Hebu kidogo, hebu tuyaweke sawa hapa kidogo tu. Ibilisi anazo bidhaa bandia huko.

Mimi Nimeokolewa kwa sababu nilitimiza masharti ya Mungu. Aliniita, nami nilijua yeye aliniita. Nilimkubali yeye kwenye Neno Lake, kwa hiyo basi naweza kumwambia Shetani, “BWANA ASEMA HIVI!”

Wakati Yesu alipokuwa hapa duniani, yeye alikuwa Mungu, alikuwa Imanueli. Mungu alikuwa ndani ya Kristo, akiupatanisha ulimwengu kwa nafsi Yake. Hakutumia kamwe moja wapo ya karama Zake kuu, wakati alipokutana na Shetani. Alisema, “Imeandikwa, ‘Mtu hataishi kwa mkate tu.’ Imeandikwa, ‘Usimjaribu Bwana Mungu wako.’” Akamshinda.

Hilo ndilo lenyewe, kujua Maandiko. Shetani anayajua, pia, lakini unapaswa kujua jinsi ya kuligawanya Neno la Mungu kwa usahihi. Unaona?

MKATE WA KILA SIKU

Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu: Waefeso 2:8

23-0411

64-0121 – Neno La Mungu Linahitaji Utengano Mkamilifu Kutokana Na Kutokuamini

Unatoa lundo la chenji. Kuna mapeni, vijisenti, mashilingi, robo, nusu dola, dola, zote zikiwa ni sarafu. Sasa, hivyo ndivyo ulimwengu ulivyo, katika mkono wa Mungu. Kuna watu wengine ambao wanaweza tu kuwa na thamani yake ya peni moja, na Mungu anaweza tu kuwatumia kwa njia ya peni. Hayo tu ndiyo wanayoweza kununua. Usiwakatae.

Ikiwa hawawezi kuamini Kweli halisi, usiwakatae, usiwatupe nje na kusema hawako ndani ya Hilo, kwa sababu Mungu hutumia mapeni wakati mwingine.

Lutu alikuwa ni peni tu, Ibrahimu alikuwa ni dola ya fedha, kwa hiyo ilihitaji Lutu mia moja kufanya Ibrahimu mmoja. Na vivyo hivyo inahitaji…Waaminio mia moja wa kimwili hawatasimama uweponi mwa Mkristo halisi aliyetenganishwa na mambo ya kimwili ya ulimwenguni, anayeishi ndani ya Kristo Yesu, ambapo Neno linaweza kufanya kazi kupitia yeye.

Anaweza tu kuchukua thamani ya peni moja; hiyo ndiyo tu aliyo nayo.

MKATE WA KILA SIKU

… mwenende kama inavyoustahili wito wenu mlioitiwa;

kwa unyenyekevu wote na upole, kwa uvumilivu, mkichukuliana katika upendo;

Waefeso 4:1-2

23-0410

56-0115 – Njia Panda Ya Wakati

Usingekunywa supu iliyo na nzi ndani yake. La, bwana. U—usingeinywa. Usingekuwa…Ungeogopa kula chakula ambacho hakikuonekana sawa kabisa, na kilikuwa kimechafuliwa. Kwa sababu, unajua, kinaweza kukupa sumu ya chakula ama chochote kile, na kingekuua baada ya muda mfupi. Na wewe unautunza mwili huu.

Lakini, hiyo nafsi, unaiacha ijifurahishe na mambo ya ulimwengu, ambayo unajua yamechafuka na yanaweza tu kufanya jambo moja, kukupeleka kwenye maangamizi. Haijalishi jinsi unavyoutendea vizuri mwili huu, na jinsi chakula kilivyo kizuri, ama jinsi unavyoishi, hauna budi kuingia katika mavumbi ya nchi.

Lakini nafsi hiyo itaishi milele, mahali fulani. Afadhali ninywe supu iliyochafuliwa kuliko kuichafua nafsi yangu na mambo ya ulimwengu, wakati wowote.

MKATE WA KILA SIKU

Maana Mungu hakutuitia uchafu, bali tuwe katika utakaso. 1 Wathesalonike 4:7

23-0404

63-0728 – Kristo Ni Siri Ya Mungu Iliyofunuliwa

Kwa hiyo, ni Neno, ama si chochote. Hiyo ni kweli. Yeye, Neno! Unajuaje kuwa ni sawa? Yeye, Neno, amethibitishwa. Unaona?
Yeye, Neno, linapothibitishwa ipasavyo, ndiye Uongozi, Kichwa cha Kanisa. Yeye ni Neno, Uongozi. Yeye anatambulishwa ipasavyo, ametambulishwa, amethibitishwa, na Roho Wake Mwenyewe akiwa ndani ya Kanisa Lenyewe, huyo mtu. Akijidhihirisha Mwenyewe, katika uthibitisho, ndio uthibitisho wa moja kwa moja kwa huo Mwili mzima. Huhitaji kanuni za imani, basi.

Madhehebu yameangamia. Lakini Uongozi Wenyewe, unatambulika katika Mwili kwa vitambulisho vya kibinafsi, unaona, akijitambulisha Mwenyewe, unathibitisha Uongozi kwa Mwili. Basi, tumeunganishwa chini ya Uongozi Mmoja uliothibitishwa, yaani, Kristo, Neno la Mungu si chini ya kanisa lolote.

Basi, Uongozi wetu ni Ufalme. “Ufalme wa Mungu uko ndani yenu,” ilisema Biblia, Yesu. Ufalme! Sisi si dhehebu. Sisi ni raia wa Ufalme, nao huo Ufalme ni Neno la Mungu lililofanyika Roho na Uzima katika maisha yetu wenyewe, likitimiza kila ahadi katika siku hii, kama ilivyokuwa katika siku ile wakati Neno na Mungu walikuwa Mmoja.

MKATE WA KILA SIKU

Mungu aliyeufanya ulimwengu na vitu vyote vilivyomo, yeye, kwa kuwa ni Bwana wa mbingu na nchi, hakai katika hekalu zilizojengwa kwa mikono. Matendo 17:24

23-0401

52-0713A – Uzoefu wa Mwanzoni wa Kiroho

Mungu wa Agano la Kale alikuwa Yesu wa lile Jipya, na Roho Mtakatifu wa leo. Unajua jambo hilo. Je, huamini jambo hilo?

Kumkufuru Roho Mtakatifu leo, ni adhabu sawa tu, au mbaya zaidi, kuliko kumkufuru Yesu Kristo, au Mungu Baba. Je, huamini jambo hilo?

Sasa, nini zaidi? Sasa, tazama. Ikiwa ulimwengu unatuita wendawazimu. Ikiwa ulimwengu unafikiri kwamba tuko karibu nusu tu hapa…Angalia. Kwa sababu ishara hizo zilitokea mahali nilipo, na huyu Malaika wa Bwana, na kadhalika, hiyo haimaanishi ya kwamba huyo ni mimi tu, enyi marafiki.

Hilo lina maana gani? Mungu anajaribu kuwaleteeni kitu gani? Anajaribu kuwaleta kwenye jambo hili, kwamba mimi ninawaambieni kweli.

MKATE WA KILA SIKU

Kisha akawaambia,
Sikizeni basi maneno yangu; Akiwapo nabii kati yenu,
Mimi, BWANA, nitajifunua kwake katika maono,
Nitasema naye katika ndoto. Hesabu 12:6

23-0331

53-0405E – Mashahidi

Hiyo ndiyo sababu, usiku wa leo, kwamba wengi wa Wakristo hawajapata ushindi, ni kwa sababu dhambi zao zimewatenga na baraka; wamekatiliwa mbali, huko nyikani mahali fulani, peke yao. Nayo mioyo yetu inaning’inia kwenye mwerebi uliao, kwa sababu hatuwezi kuzifurahia nyimbo za kanisa.

Nakumbuka zamani sana, tulipozoea kuingia humu. Wangekuwa wakicheza Pale Chini Msalabani, kwenye piano, kengele ilipokuwa ikipigwa, nao wakaingia. Kusingekuwa na angalau jicho moja kavu kanisani, kila mtu akilia, polepole, mtulivu. Ninapenda tu njia ya mtindo wa kale; Nguvu tulivu, tamu, za Roho Mtakatifu, zikitokea.

Kabla hatujaweza kupata ufanisi wowote, hatuna budi kuvunjika, kwanza. Unajua, kama vile mfinyanzi, nabii alikuwa akishuka kwenye nyumba ya Mfinyanzi, akavunjwe, ili kufinyangwa tena. Nanyi mwajua, ikiwa hakuna kuvunjika, hakuna kufanywa upya tena. Inakubidi uvunjwe kwanza.

MKATE WA KILA SIKU

Lakini sasa, Ee BWANA, wewe u baba yetu; sisi tu udongo, nawe u mfinyanzi wetu; sisi sote tu kazi ya mikono yako. Isaya 64:8

23-0330

57-0908M – Waebrania, Mlango Wa Tano Na Wa Sita #1

Baba wa Mbinguni, wanakuja kwa imani, kwa njia ya neema. Kuna kama dazani moja ya mikono iliyoinuliwa. Ni matunda ya Ujumbe huu. Wanakuja Kwako. Wanaamini. Ninawaamini, pia, Bwana. Ninaamini ya kwamba, hakika, Roho Mtakatifu alinena nao. Na kwa imani wanapanda moja kwa moja kwenye ngazi ya Yakobo sasa, moja kwa moja mpaka chini ya msalaba, hapo wanaweka dhambi zao zote chini, na kusema, “Bwana, zimenilemea mno. Siwezi tu kuzivumilia tena. Na nakusihi uondoe mzigo wangu wa dhambi, na utoe tamaa ya kufanya jambo hilo moyoni mwangu?

Na nijalie, kwa imani, leo hii, nikupokee Wewe kama Mwokozi wangu binafsi. Na tangu sasa, nitakufuata kila maili ya njia, hata mwisho wa safari yangu.

Nimetupia jicho kile inachomaanisha ‘kukaza mwendo kuufikilia utimilifu,’ si kwenda kanisani, na mashina ya matendo mafu kama mabatizo na kadhalika. Lakini ninataka kuendelea, mpaka isiwe tena ni mimi, na Kristo anaweza kuishi ndani yangu.”

MKATE WA KILA SIKU

Lakini sisi tulio wa mchana, tuwe na kiasi, hali tukijivika kifuani imani na upendo, na chapeo yetu iwe tumaini la wokovu. 1 Wathesalonike 5:8

23-0329

59-1216 – Roho Mtakatifu Ni Nini?

Nikasema, “Shetani, wewe unayezungumza na dhamira yangu, ningetaka kukuuliza mambo machache. Ni nani ambaye wale manabii wa Kiebrani walinena kwamba Yeye angekuja? Ni nani aliyekuwa Masihi mtiwa mafuta? Ni nini kilikuwa juu ya watu hao waliomwona Yeye hapo awali na kusema habari za maisha Yake, maelfu ya miaka kabla Yeye hajafika hapa? Ni nani aliyetabiri jambo hilo kwa usahihi kabisa?

Na hapo alipokuja, wao walisema, ‘Alihesabiwa pamoja na wakosaji,’ Naye alihesabiwa. ‘Alijeruhiwa kwa makosa yetu,’ na alijeruhiwa. ‘Alifanya kaburi Lake pamoja na matajiri, lakini Yeye angefufuka, siku ya tatu,’ Naye akafufuka. Kisha aliahidi Roho Mtakatifu, nami ninaye Huyo.

Kwa hiyo ni afadhali uliondokee jambo Hilo, kwa kuwa imeandikwa katika Neno, na kila Neno ni kweli.” Ndipo akaondoka. Mpe tu Neno; hilo linatosha. Yeye hawezi kuvumilia Neno hilo, kwa kuwa limevuviwa.

MKATE WA KILA SIKU

Naye akajibu akasema, Imeandikwa, Mtu hataishi kwa mkate tu, ila kwa kila neno litokalo katika kinywa cha Mungu. Mathayo 4:4

23-0328

62-0401 – Hekima Dhidi Ya Imani

Mungu asingeweza kumbariki Sethi mpaka Yeye alipomtenga na Kaini. Alimtia alama Kaini na kumtuma kwenye nchi ya Nodi. Ndipo Kaini, kwa hekima yake ya kielimu, akawa wanasayansi na kila kitu kingine, akakuza zao la hiyo. Naye Sethi, chini ya haki yake, na upendo na imani katika Neno la Mungu, yeye alikuza zao lililomzaa nabii aliyetoa onyo kwa siku za mwisho, hiyo ni kweli, akamwokoa kila mwaminio.

Nayo hekima ikamwangamiza kila mmoja wao. Wao, kila mmoja, akafa. Kila mmoja, haijalishi walikuwa na digrii ngapi na saikolojia, kila kitu kingine, waliangamia katika hukumu za Mungu.

Na kila kitu nje ya watu wa kweli, waliozaliwa upya kwa Roho wa Mungu, wanaoamini kila Neno la Hilo na wanalitetea, wataangamia katika hukumu za Mungu.

Mnaona maskini hawa wanaojinengua wakishuka kwenda mtaani, na vurugu hizi zote, na kuendelea namna hiyo, kumbukeni, si kitu ulimwenguni ila chakula cha ile hukumu. Itaoza. Haina budi kuoza. Itaibidi tu kuoza. Enyi wanawake, amkeni.

MKATE WA KILA SIKU

Na mataifa yote watakusanyika mbele zake; naye atawabagua kama vile mchungaji abaguavyo kondoo na mbuzi Mathayo 25:32

23-0327

53-0613 -Njia ya Mungu iliyoandaliwa

Mungu hutufananisha sisi na kondoo. Ninashangaa kwa nini. Mtu yeyote hapa amekwishawahi kufuga kondoo wowote? Naam, unajua kwamba kondoo ni kitu kisicho na msaada duniani wakati Kimepotea. Hawezi kufahamu njia ya kurudi nyumbani hata kidogo. Je, hiyo ni Kweli, enyi wafugaji wa kondoo? Nami nimesaidia kuwafuga mimi mwenyewe nje huko ya msitu wa Magharibi, na kuwapakia wengi.

Lakini angalia, kondoo anapopotea …wakati amepotea, atasimama tu na kulia baa. Ni hayo tu. Mbwa mwitu watakuja kumkamata (ni hayo tu.), ‘Ikiwa Mchungaji hamwendei. Na ndivyo ilivyo na sisi, tunapopotea, hatuna tumaini kabisa isipokuwa mchungaji Aje na kutuchukua.

Kwa hiyo, nafurahi usiku wa leo Mungu anaye mchungaji wake kuwaangalia kondoo wake, Nawe je, Hauna furaha? Kwamba tunapoita, yeye husikia kila wakati…

MKATE WA KILA SIKU

Atalilisha kundi lake kama mchungaji, Atawakusanya wana-kondoo mikononi mwake; Na kuwachukua kifuani mwake. Isaya 40:11

23-0326

61-0903 – Vivyo Hivyo Nuru Yenu na Iangaze Mbele ya Watu

Sasa, njia pekee ambayo ulimwengu utapata kumwona Kristo ni wakati mtu, watu, watakapomwona ndani yako na ndani yangu. Hiyo ndiyo njia watakayoweza kumwona Kristo.

Dhamiri ya—yao imekufa isifahamu kutua kwa jua, mlio wa ndege, majani, na—na nyasi, na maua; na muziki, na Ujumbe na kadhalika, ambavyo tunafurahia baada ya kumpata Kristo. Lakini, mpaka tutakapofikia mahali ambapo tunamwonyesha Kristo wazi!

Sasa, kumbukeni jambo hilo. Kila mmoja wenu, tangu usiku huu na kuendelea, kumbukeni, ninyi ni vibao vya Mungu vya kuwekea matangazo. Nanyi—nanyi ni maajenti wa Mungu wa kutangazia. Sasa, ulimwengu utakutazama, waone kwamba Kristo ni kitu gani.

Kwa hiyo hatutaki kupaka takataka chungu mbovu hapo, ambazo zinashuhudia kuhusu mambo ambayo kweli hayapo. Hebu kwanza tuwe hivyo. Ndipo basi tutakapokuwa hivyo, ndipo ulimwengu utakapomwona Kristo ndani yako na ndani yangu.

MKATE WA KILA SIKU

Ninyi ndinyi barua yetu, iliyoandikwa mioyoni mwetu, inajulikana na kusomwa na watu wote. 2 Wakorintho 3:2

23-0325

55-1110 – Maisha Yaliyofichwa Katika Kristo

Sasa, usiku wa leo tutazungumza juu ya Patakatifu pa patakatifu, mahali pa kukaa ambapo Mungu Mwenyewe alikaa. Siku hizo, alikaa katika maskani Yake. Na leo hii yeye anakaa ndani yako kama maskani yake.

Lakini ni lazima tufanye mahali hapa kuwa makao, si mahali pa ua wa nje, au mahali patakatifu pa kwanza. Lakini ni lazima tuishi na Mungu katika Patakatifu pa patakatifu, maisha yaliyowekwa wakfu, yaliyofichwa, peke yake, tulivu na Mungu.

Tunachochewa sana, tunakasirika, kuhusu mambo mengi sana. Inaonyesha kuna kitu fulani kinakosekana. Kanisa linapaswa kuwa maili milioni moja juu ya jinsi lilivyo sasa. Bado tumerudi chini katika enzi za utoto, tukigombana, na kupigana, na kuzozana, na kuchukiana, wakati inatupasa kujiweka wakfu, kufichwa katika Patakatifu pa patakatifu pamoja na Mungu.

MKATE WA KILA SIKU

Bali kama yeye aliyewaita alivyo mtakatifu, ninyi nanyi iweni watakatifu katika mwenendo wenu wote. 1 Petro 1:15

23-0324

65-1128M – Mahali Pekee Palipowekwa Na Mungu Pa Kuabudia

Angalieni, sasa, kwamba Daudi akiisha kutiwa mafuta, hata hivyo kwa upako alifanya, alitoka kwenye mapenzi ya Bwana akiwa na upako huo; ndipo watu wote, bila kuchukua mwelekeo wa Maandiko ama ufunguo wa ufunuo huu, wote wakiwa wametiwa mafuta pia, hao wote, pamoja, wakipiga makelele na kumsifu Mungu kwa ajili ya jambo lililoonekana ni sawa kabisa: kulirudisha Neno la Mungu kwenye nyumba ya Mungu.

Lakini Daudi alikuwa ni mfalme, sio nabii. Mnaona? Yeye…Kulikuwako na nabii nchini wa kufanyia jambo hilo, ndipo Mungu akadharau mwenendo huo wote kwa sababu kamwe hawakutumia ufunguo unaofaa.

Mlango huo haukufunguka. Na sasa hatuna budi kukumbuka jambo hilo, na kuliweka hilo niani. Kuna ninii…Kila kitu cha Mungu, njia moja ya hakika kinavyopaswa kufanywa, na hiyo yatosha.

MKATE WA KILA SIKU

Zishikeni kwa bidii sheria za BWANA, Mungu wenu, na mashuhudizo yake, na amri zake alizokuagiza. Kumbukumbu la Torati 6:17

23-0323

65-0725E – Nini Kinachovutia Kule Mlimani?

Bali katikati ya hayo yote, kupitia kila wakati na kila nabii ambaye alikuwako ama ambaye angekuwako, kutakuweko kiasi fulani cha watu ambao wamechaguliwa tangu asili kusikia Ujumbe huo, nao wataufuata.

Hao hawajali umati wa watu. Hawajali lawama za wasioamini. Wao—wao hawabishani nao.

Wana wajibu mmoja, huo ni kuamini na kupata kila sehemu Yake wawezayo, waiingize ndani kama Mariamu aliyeketi miguuni pa Yesu.

MKATE WA KILA SIKU

Kondoo wangu waisikia sauti yangu; nami nawajua, nao wanifuata. Yohana 10:27

23-0322

52-0810E – Yesu Kristo Yeye Yule Jana, Leo, Na Milele

… katika bustani ya Edeni, kuna miti miwili; mmoja ulikuwa maarifa na huo mwingine imani. Mmoja ilikuwa Uzima. Mmoja ulikuwa kifo cha maarifa, mwingine ulikuwa uzima kwa imani. Na mradi tu walavyo kwa imani ya mti huu, vema, waliishi. Bali alipofika kwenye mti huu, alikufa.

Mego moja ya kwanza aliyokula, alijitenga mwenyewe na Mungu. Na mwanadamu daima amekuwa aking’ata kutoka kwenye mti huo. Na kila wakati anapong’ata kwa maarifa, anajiangamiza mwenyewe. Mungu haangamizi chochote. Mwanadamu hujiangamiza yeye mwenyewe kwa maarifa.

Angalia, aling’ata yeye mwenyewe Kwenye baruti, anawaua wenzake. Aling’ata kutoka kwenye motokaa kutoka kwenye mti huo, unaua zaidi ya vita vyote vikiwekwa pamoja. Je, hiyo ni kweli? Maarifa, maarifa, kula kutoka kwenye mti huo. Amejipatia bomu la hidrojeni sasa; Nashangaa atafanya nini nalo. Unaona?

Lakini shida yake ni kwamba, watu hawa, wanafikiri sana, juu ya mti huu wa maarifa , basi wasipoweza kujua jambo hilo tena, wanasema, “Yote ni upuuzi .”

Sikilizeni , katika Jina la Bwana, sikilizeni: Wakati huwezi kujua zaidi, huo ndio wakati wa kuamini.

MKATE WA KILA SIKU

Lakini matunda ya mti ulio katikati ya bustani Mungu amesema, Msiyale wala msiyaguse, msije mkafa. Mwanzo 3:3

23-0321

62-0518 – Kutoa Presha

Na Mwakilishi wa Mungu duniani leo ni Roho Mtakatifu. Na unapokuwa katika Uwepo Wake, unamwona Yeye akikubariki, unawezaje kujenga presha kama hiyo ya kumchukia jirani yako? Unawezaje kujenga tofauti ya kimadhehebu moyoni mwako? Unasema, “Kama hawakuwa Wapentekoste, kama alikuwa wa Umoja, au kama alikuwa wa Utatu, kama alikuwa, alikuwa mfuasi wa Assemblies, kama alikuwa mfuasi wa church of God , ningeweza kushirikiana naye.”

Unawezaje kufanya jambo hilo katika Uwepo wa Mwenyezi Mungu? Roho Mtakatifu anawezaje kuwa anashuka juu ya kusanyiko, na kisha kuleta tofauti za kimadhehebu? Inawezaje kutenda jambo hilo? Toa presha .

Shida, tuliongeza presha , kwa sababu tuna nia ya kimadhehebu sana. Loo, Marekani imeoza pamoja nayo, madhehebu, kujizungushia uzio, kanuni za imani. Unajalije kuhusu kanuni hizo za imani na uzio? Ingia katika Uwepo wa Mungu, ingia katika Uwepo wa Roho Mtakatifu, toa presha basi.

MKATE WA KILA SIKU

Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu Wagalatia 5:22

23-0320

53-0508 – Mungu Akimwagiza Musa

Sasa, unataka kuzungumza kuhusu jambo fulani la kipuuzi, hebu tuangalie tukishuka kwenye kilima hapa sasa. Asubuhi moja yenye kupendeza, jua linachomoza, ndege wanapiga miluzi, huyu hapa mzee mmoja, mwenye umri wa miaka themanini anakuja, sharubu zikiruka huku na huko, na nywele nyeupe zikibubujika nyuma yake, huku akimwongoza nyumbu mzee na mke wake akiwa ameketi kwa kushikilia na mtoto mchanga mapajani, kijiti kilichopinda mkononi mwake.

Huyu Hapa anaenda. “Unaenda wapi Musa?” “Nashuka kwenda Misri kuiteka!” Uvamizi wa mtu mmoja, kwenda Misri. Mbona, Misri ingekuwa kama tu kuvuka na kwenda kuiteka Urusi. Vitengo vilivyo bora kabisa ulimwenguni vilikuwepo huko, lakini Mungu akamwambia, “Nitakutuma chini kule ukaiteke.” “vema, unamaanisha kuwa unaenda kuiteka?” “Hakika.” “Kwa nini? Kwa ninii yako…” “Ndiyo, Mungu alisema hivyo.” Hiyo ni kweli. Unasema, “Je, utaitwaa?”

“Hakika, tunaenda kuiteka sasa. Ni hayo tu. Mungu alisema hivyo.” Hiyo ni kweli. Maadamu Mungu alisema hivyo, amina. Hilo—hilo latosha.

Kama Mungu amesema hivyo, unaweza kufanya jambo hilo . Je, hiyo ni kweli? Vema, basi hebu na tukateke sasa hivi, na kumwambia Ibilisi, ya kwamba hatakuwa na uhusiano wowote nasi. Kila mgonjwa ataponywa; kila jicho lililopofushwa litafunguliwa; kila kiziwi atasikia; kila ulimi uliyo bubu utanena; kila mwenye dhambi ataanguka jukwaani na kutoa mioyo yao kwa Kristo. Tunakwenda kuteka. Unaona? Mungu tupe jambo hilo . Nenda ukateke.

MKATE WA KILA SIKU

Tazama, nimewapa amri ya kukanyaga nyoka na nge, na nguvu zote za yule adui, wala hakuna kitu kitakachowadhuru. Luka 10:19

23-0319

50-0115 – Je, Unasadiki Hayo?

Si muda mrefu uliopita, nilikuwa nimesimama karibu na jumba la makumbusho. Kuna picha ya mtu hapo, Ratili mia na hamsini. Nayo-inatoa uchambuzi wa kemikali za mwili wake. Ana thamani ya senti themanini na nne. Hiyo ndio thamani yote ya Mtu Mwenye Ratili mia na hamsini, ni senti themanini na nne .

Lakini atahakikisha Anaweka kofia ya dola kumi kwenye senti hiyo themanini na nne na kufikiria yeye ni kitu fulani kikubwa. Hiyo ni kweli. Mwanamke atafunika senti hiyo themanini na nne kwa koti la manyoya la dola mia moja na hatazungumza na nusu ya majirani zake.

Kuna nini? Upendo wa Mungu unakupeleka mahali fulani. Hiyo ni kweli .

Ni Kitu gani? Bado ni ile senti themanini na nne. Utaishughulikia hiyo ni sawa. Lakini nafsi hiyo ina thamani ya Dunia elfu kumi, nawe utaacha kitu chochote kishushwe ndani yake. Hiyo ni kweli. Huo ni ukweli .

MKATE WA KILA SIKU

Vivyo hivyo wanawake na wajipambe kwa mavazi ya kujisitiri, pamoja na adabu nzuri, na moyo wa kiasi; si kwa kusuka nywele, wala kwa dhahabu na lulu, wala kwa nguo za thamani; 1 Timotheo 2:9

23-0318

64-0205 – Mungu Ndiye Anayejifasiria

Lutu ni mfano wa kanisa la kidhehebu lililoko kule chini katika Sodoma bado. Angalia, Biblia ilisema kwamba, “Dhambi za Sodoma ziliitesa roho yake yenye haki kila siku.” Kwa nini hakuthubutu kuzipinga? Wapo watu wengi wazuri wanaoketi kanisani leo, wanaowaona wanawake wamevaa kaptura na wanaume wakifanya mambo haya, na wafuasi wao wakienda, wakicheza mpira wa ving’oe Jumapili, na karamu za mandari, na kuogelea na mambo, badala ya kuhudhuria kanisa.

Wakikaa nyumbani Jumatano usiku, wakiangalia televisheni, badala ya kuhudhuria kanisa. Wanajihisi kusema kitu kuhusu hilo, lakini halmashauri itawatupa nje. Kuna nini? Ni Lutu tena, akiangalia kwenye dirisha lake na kuona hiyo dhambi, na kuogopa kuita dhambi “dhambi”!

Ibrahimu hakuwa katika vurugu yao, alikuwa nje yake. Alikuwa mfano wa Kanisa la kiroho. Sasa hebu angalieni tu lilitukia mwishoni mwa wakati, kabla tu ya moto kuanguka.

Na hao walikuwa watu wa Mataifa. Ilionyesha kivuli cha moto ukivangukia ulimwengu wa Kimataifa leo. Wakati falme zitakapovunjika na zitaunguzwa. “Mbingu zitashika moto,” asema Bwana, “nazo zitateketezwa.” Hicho kilikuwa kivuli chake.

MKATE WA KILA SIKU

Lakini kama mkiendelea kutenda mabaya, mtaangamia. 1 Samweli 12:25

23-0317

56-0121 – Ndani ya Pazia

Unapokuwa umepandwa katika Kristo Yesu, kila kitu unachohitaji katika safari ya duniani kiko ndani yako unapompokea Roho Mtakatifu. Na jambo pekee unalopaswa kufanya ni kunywa, kunywa, na usukume utokeze, sukuma utokeze . Kunywa tu mpaka utosheke.

Kama unahitaji uponyaji wa Kiungu, nenda kwenye Neno la Mungu na unywe kutoka Kwake, mpaka utokeze. Ikiwa una haja ya Mungu zaidi, endelea tu kunywa, jisukume utokeze. Na Kristo ndiye Chemchemi ya Uzima isiyokauka. Na kama umepandwa ndani Yake, jambo pekee unalopaswa kufanya, ni kunywa wema Wake na utokeze chochote unachohitaji katika safari hii ya duniani. Yote ni kunywa, kupumzika, amani.

Si kile unachohangaikia na kujitahidi na kuvuta, wewe—unalishinda kusudi hasa ambalo unaloliwakilisha unapofanya jambo hilo. Ukristo si kitu fulani , Mungu si Mtu unayepaswa kumsihi-sihi,na kulia, na kusihi, na kufunga,na kujinyima kwa njaa, na kila kitu kama hicho ili kumfikia.

MKATE WA KILA SIKU

Naye atakuwa kama mti uliopandwa Kandokando ya vijito vya maji, Uzaao matunda yake kwa majira yake, Wala jani lake halinyauki; Na kila alitendalo litafanikiwa. Zaburi 1:3

23-0316

56-0726 – Upendo

Nadhani upendo ndio nguvu iliyo kuu zaidi duniani. Hakuna kitu chenye nguvu zaidi kuliko upendo. Kama ningekuwa na chaguo usiku wa leo, na nilikuwa mwenye dhambi, na nilikuwa nimesimama hapa mbele za Mungu, Naye aseme, “Sasa, kijana, nitakupa karama zote tisa za kiroho.

Nitakuacha utabiri, nitakupa roho ya unabii. Nitakufanya kuwa mhubiri hodari, nikupe neno la hekima na ufahamu. Nitakupa karama ya kunena kwa lugha na kufasiri. Nitakupa karama ya uponyaji ambayo utakuwa na imani kuu kwa wagonjwa. Nami nitakufanyia mambo haya yote.

Nitakupa yote hayo, au sitakuruhusu uwe na lolote la vitu hivyo, lakini hebu uwe na upendo halisi moyoni mwako.” Ningesema, “Mungu nipe upendo.” Hiyo ni kweli . “Kwa maana palipo na lugha, zitakoma. Ambapo kuna unabii utashindwa. Ambapo kuna maarifa, yatatoweka. Lakini palipo na upendo, utadumu milele. Hilo ndilo lililousukuma moyo wa Mungu kumtuma Kristo duniani.

MKATE WA KILA SIKU

Jilindeni katika upendo wa Mungu, huku mkingojea rehema ya Bwana wetu Yesu Kristo, hata mpate uzima wa milele. Yuda 1:21

23-0315

56-0527 – Pale Kadesh-Barnea

Sasa, Mungu akiwa mwenye enzi, na kama tu nilivyokuwa nikifundisha leo, katika nyumba ambayo nilialikwa huko kwa chakula cha jioni. Walitaka kujua ikiwa wangewajua wapendwa wao, pindi watakapokutana nao Utukufuni.

“Vema,” nikasema, “hakika tutawajua.” Unaona, sisi—tuko katika… Tuna miili mitatu tofauti tunayoishi ndani yake . Mmoja ni Wa kibinadamu, mwingine ni wa kimbinguni, na mwingine ni ule uliotukuzwa. Na Basi ikiwa tunajuana tukiwa katika mwili wa kibinadamu, mwili upatikanao na mauti, ni zaidi sana vipi, tutajua jambo hilo, mmoja kwa mwengine tukiwa katika mwili wa utukufu!

Inafanana na kwamba, ikiwa sheria inaweza kuzaa kitu kizuri, ni zaidi jinsi gani neema inaweza kuzaa kitu kikubwa ? , kwa maana ni kubwa kuliko sheria!

Na ikiwa mwezi unaweza kutoa sehemu fulani ya mwanga, je! jua litauzidi zaidi vipi litakapokuja! Na hakika tutajuana mmoja kwa mwingine.

MKATE WA KILA SIKU

Yesu akawaambia, Njoni mfungue kinywa. Wala hakuna mtu katika wale wanafunzi aliyethubutu kumwuliza, U nani wewe? Wakijua ya kuwa ni Bwana. Yohana 21:12

23-0314

63-0428 – Tazama

Wakati mwingine hatuwezi kungoja kutoka usiku mmoja hadi mwingine. Wakati mwingine hatuwezi kungoja kutoka uamsho mmoja hadi mwingine. Inatubidi kutoka nje na kujitatanisha na mambo ya ulimwengu. Jinsi inavyotupasa kujionea aibu.

Kabla hatujaja hapa kukiri na kuingia ndani ya hiyo Damu ya Yesu inayotusafisha na dhambi yote, inatupasa kujilenga kikamilifu, tupate kumwona yule Mungu mmoja aliye hai amesimama pale, Yeye aliyefanya ahadi, ya kwamba, “Mbingu na nchi zitapita, bali Neno Lake haliwezi kushindwa.” Kaa papo hapo juu ya Hilo, ndipo hutatupwa huku na huko kwa pepo za mafundisho, ukichukuliwa mahali mahali, huku na huku.

Lakini, unajua mahali unaposimama, kwa maana umelengwa shabaha pamoja na Mungu. Unayaona maisha yako mwenyewe yakipiga ile shabaha, kama tu wale mitume walivyofanya. Unaishi jinsi walivyoishi. Ulibatizwa jinsi walivyobatizwa. Unaona matokeo yale yale waliyoona. Unaona likitenda kazi ndani yako. Umelengwa kikamilifu.

Sijali yale kampuni isemayo na yale madhehebu yasemayo. Umelengwa kikamilifu, kwa sababu unajua ya kwamba unapiga shabaha. Amina.

MKATE WA KILA SIKU

Mwe na kiasi na kukesha; kwa kuwa mshitaki wenu Ibilisi, kama simba angurumaye, huzunguka-zunguka, akitafuta mtu ammeze. 1 Petro 5:8

23-0313

49-1225 – Uungu Wa Yesu Kristo

Na halafu, tena, nawatakeni muone jambo lingine, mojawapo ya yanayotimia. Watu hawa ambao ni baridi katika makanisa haya baridi, wanainuka dhidi ya hii Huduma.

Nayo Biblia ilisema, “Wangekuwa na mfano wa utauwa, lakini wakikana Nguvu zake; hao nao mjiepushe nao.” Na wanachukua msimamo wao.

Ukomunisti unachukua msimamo wake.

Mungu asifiwe, Roho Mtakatifu anachukua msimamo Wake.

Naam. “Adui atakapokuja kama mafuriko, basi nitainua bendera dhidi yake.” Hiyo ni kweli. Nalo Kanisa limechukua msimamo Wake, ninamaanisha Kanisa la Roho Mtakatifu.

Sasa hayo ndiyo tu yanayonivutia, enyi marafiki, nami niko hapa. Huko nje, nitawaombea wagonjwa. Lakini hapa ndani ninavutiwa na jambo moja, na hilo ni Kanisa la Mungu lililozaliwa mara ya pili. Hiyo ni kweli. Hilo ndilo linalonivutia, kwa vyovyote vile.

Sivutiwi na sheria ndogo, na mashemasi, na kadhalika, namna hiyo, ama taratibu za makanisa. Ninavutiwa na ubatizo wa Roho Mtakatifu juu ya Kanisa, kwa siku hizi tunazoishi. Hiyo ndiyo sehemu ya kimsingi, na hiyo ndiyo tunayotafuta.

MKATE WA KILA SIKU

Basi, wataliogopa jina la BWANA toka magharibi, na utukufu wake toka maawio ya jua; maana yeye atakuja kama mkondo wa mto ufurikao, uendeshwaokwa pumzi ya BWANA. Isaya 59:19

23-0312

62-0628 – Aliye Mkuu Kuliko Sulemani Yupo Hapa

Mungu hulitimiza Neno lake, sijali ni wakosoaji wangapi wanasema! Na kama ilivyokuwa katika siku za Nuhu, “Mvua haitanyesha.” Mvua ilinyesha hata hivyo, Mungu alisema hivyo. Na anayosema Mungu, Mungu anaweza kuyafanya.

Lile yeye Asemalo, Ibrahimu aliliamini jinsi hiyo, na watoto wote wa Ibrahimu huamini jinsi hiyo. Na kama tuko ndani ya Kristo, sisi ni Uzao wa Ibrahimu na warithi pamoja naye, pamoja na ahadi. Ndipo tunapaswa kuwa na imani ambayo Ibrahimu alikuwa nayo katika Neno la Mungu. Hakika. Hilo ndilo linaloleta mambo kutimia, ni imani katika yale yeye aliyosema.

Hautawahi kulisogeza kwa njia nyingine ila kuwa na imani katika yale Mungu aliyosema. Unapaswa kulichukua Neno Lake juu ya kila kitu kingine. “Neno la kila mtu na liwe uongo, na la Mungu liwe kweli.” Alichosema Mungu, liamini tu. Huwezi kuliamini jinsi hiyo, kamwe hutafika popote na Mungu.

Unaweza kujiunga na kanisa mahali fulani, lakini ninamaanisha kufika mahali fulani na Mungu. Unaona? Hiyo ni—hiyo ni tofauti sana .

MKATE WA KILA SIKU

Jumla ya neno lako ni kweli, Na kila hukumu ya haki yako ni ya milele. Zaburi 119:160

23-0311

57-0901M – Waebrania, Mlango Wa Tatu

Kuna kitu fulani kuhusu ninii…mahali unakoenda, kanisa gani unalohudhuria, na mwalimu gani anayekufundisha. Je! ulijua jambo hilo? Hilo, kuna jambo fulani kwake.

Kwa hiyo inatupasa kutafuta yaliyo bora sana tunayoweza kupata, ili kwamba tuwe tunapata yaliyo bora sana; si kwa sababu eti ni mambo yanayopendwa na watu wengi na kadhalika, bali ni mafundisho halisi la Biblia.

Angalia, wakati mmoja wakati Israeli walipokuwa wametoka wakaenda jangwani pamoja na majeshi yao, nao walikuwa wamepiga kambi siku saba, ndipo wakaishiwa na maji. Nao walikuwa karibu kuangamia, wakasema, “Loo, laiti kungalikuwa na nabii karibu!”

Ndipo mmoja wao akasema, “Tuna Elisha, hapa chini. Alimimina maji kwenye mikono ya Eliya.” Unaona wenzake? Kwa maneno mengine, “Huyu hapa Elisha ambaye amekuwa na uhusiano na Eliya. Neno la Bwana liko pamoja naye.” Unalipata? Alikuwa amefundishwa vizuri.

MKATE WA KILA SIKU

Niletewe nuru yako na kweli yako ziniongoze, Zinifikishe kwenye mlima wako mtakatifu na hata maskani yako. Zaburi 43:3

23-0310

50-0115 – Je! Unasadiki Hayo?

Siku moja nilipokuwa na mkutano wangu wa kwanza na watu wa Holiness . Nilikuwa huko St. Louis, na nikakutana na kasisi Robert Daugherty. Naye alikuwa katika mkutano wa hema. Nami nilienda kule usiku huo, na msichana wake mdogo alikuwa ametoka kuponywa. Ushuhuda wake ulitokea pale. Naye akanipeleka kwenye mkutano walipokuwa wakiufanyia.

Alisimama pale, naye akaanza kuhubiri, na ndiyo mara ya kwanza nilipopata kumsikia mhubiri wa Kipentekoste akihubiri. Mvulana huyo alihubiri mpaka magoti yake yakagongana pamoja . Alienda mpaka sakafuni, naye angevuta pumzi . Ungeweza kumsikia miraba miwili huko. Akiendelea kuhubiri. Mtu fulani alisema, “Je, wewe ni mhubiri?” Nikasema, “La, bwana.” La, La. Njia zangu za kale za polepole za Kibaptisti hazifikirii jambo hilo haraka jinsi hiyo. Ni hayo tu.

Nili ninii tu…Sikuwa mhubiri basi baada ya mimi kusikia hayo. Kwa hiyo nilinyamaza tangu wakati huo na kuendelea karibu na watu wa Full Gospel kuhusu kuwa mhubiri. Niliiacha tu. Nikasema, “La, nitawaombea wagonjwa.” Acha liende namna hiyo.

Lakini ninafurahia kuja siku hii namna hii, kujaribu kusoma baadhi ya Neno na kulieleza vizuri zaidi nijuavyo; kwa sababu yote…ninaamini ya kwamba ni Kweli. Kila Neno la Mungu ni Kweli.

MKATE WA KILA SIKU

Lakini tumekataa mambo ya aibu yaliyositirika, wala hatuenendi kwa hila, wala kulichanganya neno la Mungu na uongo; bali kwa kuidhihirisha iliyo kweli twajionyesha kuwa na haki, dhamiri za watu zikitushuhudia mbele za Mungu. 2 Wakorintho 4:2

23-0309

62-0909E – Katika Uwepo Wake

Kama tumekiri ya kwamba Yeye ndiye, tumekuwa katika Uwepo Wake, na tumetubu dhambi zetu, zimeondolewa kwenye kitabu cha kumbukumbu Lake. Hakuna mtu anayeweza kufanya jambo hilo ila Mungu.

Sasa, unaweza kunifanyia jambo lolote, nitakusamehe, bali nitalikumbuka. Kama ningekufanyia jambo lolote, ungenisamehe, bali utalikumbuka. Bali Mungu anaweza kusamehe na kusahau hilo. Wazia jambo hilo, “hata halikumbuki!” Amina.

Hilo linanifanya nijisikie vizuri. Wakati ambapo hata halikumbukwi tena, hakuna kitu kinachoweza kufanya hivyo ila Mungu. Hakuna kitu kinachoweza kufanya hivyo ila Mungu. Alisema angelifutilia mbali kutoka kwenye kitabu Chake cha kumbukumbu. Mimi siwezi kufanya hivyo, wewe huwezi kufanya, kwa sababu tuna hisi hizi ndogo tu zenye kikomo. Bali Yeye hana kikomo, Mungu, Yeye anaweza kusahau kabisa kwamba lilipata kufanywa kamwe. Amina.

MKATE WA KILA SIKU

Kama mashariki ilivyo mbali na magharibi, Ndivyo alivyoweka dhambi zetu mbali nasi. Zaburi 103:12

23-0308

64-0112 – Shalom

Wakati mwingine nimeuliza, “Mbona?” Kwa nini, nilipokuwa tu mhudumu kijana, nilipoanza, Mungu alimtwaa mke wangu, chini yangu, akamchukua mtoto wangu chini yangu, chini ya moyo wangu? Mbona Yeye alifanya hilo? Sikujua. Najua sasa. Niliuweka tu mkono wangu ndani ya Wake na kuendelea kumtumai.

Yeye ajua kila njia panda. Yeye ajua mdundo hauna budi…unapopaswa kuchezwa. Yeye ajua kile kihitajikacho kukufinyanga wewe, Yeye ajua vifaa atakavyotumia. Waona? Huko upande wa nyuma wa jangwa wakati mwingine, ambapo Mungu huwafinyanga watu wenye haki wakawa wenye hekima nyingi na manabii. Mwaona? Mwaona? Hapo ndipo watu wanapoundiwa.

Watu huundwa, katika Neno. Wanapokuwa na kila namna ya kanuni za imani na mengineyo ndani yao, hebu na walijie Neno na Mungu anayatwanga kuyaondoa kwao, na kuwaunda wawe Hili, kuwaingiza katika Tarabu, ya Neno Lake. Mwaona? Ndiposa wao huona Neno likiendelea.

Mungu ajua wakati mdundo wake huna budi ubadilike. Yeye ajua jinsi mdundo unavyoendelea. Sijui jinsi unavyoendelea, lakini Yeye ajua.

MKATE WA KILA SIKU

Nasi twajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hufanya kazi pamoja na wale wampendao katika kuwapatia mema, yaani, wale walioitwa kwa kusudi lake. Warumi 8:28

23-0307

55-1115 – Bartimayo Kipofu

Yatafakari mambo yaliyo mema. Kamwe usiruhusu mawazo mabaya yapite; ninii tu, ama, usiliache lisimame, kwa vyovyote vile, kama likianza. Dumisha mawazo yako kuwa mazuri: Yesu.

Usifikiri, ukiketi hapa kwenye kiti cha magurudumu, wewe, kwamba huna tumaini, hujiwezi. Sivyo ulivyo. Usiruhusu wazo hilo hasi lipite kamwe, au, usiliache likolee. Huwezi kulizuia lisipitie akilini mwako (Hiyo ni kweli.), lakini usiliache lisimame.

Kama vile yule mkulima wa kale alivyosema, “Siwezi kuwazuia ndege kuruka juu ya eneo langu.” Lakini alikuwa na bunduki ya mitutu miwili, kasema, “Hakika ninaweza kuwazuia kutua.” Kwa hiyo fanya jambo lile lile, nawe pia. Unaona? Usiwaache watue. Waache wapite moja kwa moja.

MKATE WA KILA SIKU

Kwa wanadamu haiwezekani, bali kwa Mungu sivyo; maana yote yawezekana kwa Mungu. Marko 10:27

23-0306

60-0308 – Upambanuzi Wa Roho

Haidhuru yeye ni mwalimu mkuu jinsi gani, jinsi alivyo na nguvu, jinsi alivyo mwenye akili, au karama yake inavyotenda kazi, ikiwa hajaribu kufanikisha jambo fulani kwa faida ya Mwili wa Kristo, upambanuzi wako wa kiroho ungekwambia ya kwamba hilo ni kosa.

Haidhuru jinsi ilivyo sahihi, jinsi ilivyo kamilifu, jinsi ilivyo, ni makosa ikiwa haitumiwi kwa ajili ya Mwili wa Yesu Kristo.

Kupata kitu, huenda ikawa ana karama kuu ambayo anaweza kuwavutia watu pamoja kwa akili kuu au kwa nguvu za kiroho, ambazo kwazo angeweza kuwavuta watu pamoja, na huenda ikawa anajaribu kutwaa karama hiyo na kujifanya mwenyewe mashuhuri, ili kwamba atakuwa na jina kubwa, hivi kwamba ndugu wale wengine watamtazama yeye kama mtu fulani mkubwa. Basi hilo ni kosa.

Huenda ikawa yeye anajaribu ku—kujenga jambo fulani hapa ambapo anataka kila mtu aondoke kwenye picha na kumwachilia yeye na kundi lake wawe ndio picha. Hilo bado ni kosa, mwaona.

Lakini iwapo ana karama ya Mungu naye anajaribu kuujenga Mwili wa Kristo, basi sijali anatokana na nini. Wewe humpambanui huyo mtu, unapambanua roho, uhai ulio ndani ya huyo mtu. Na hivyo ndivyo Mungu alituambia tufanye.

MKATE WA KILA SIKU

Wapenzi, msiiamini kila roho, bali zijaribuni hizo roho, kwamba zimetokana na Mungu; kwa sababu manabii wa uongo wengi wametokea duniani. 1 Yohana 4:1

23-0305

51-0729E – Muujiza wa Pili

Kataa kusaini lolote analoleta shetani. Atalazimika kukirudisha. Sema, “Ninakataa kukipokea. Siwezi kukipokea, la, bwana.” Itabidi akirudishe kwa Jina la Bwana.

Kama unaamini jambo hilo , na kukikiri, na kusema, “Nimemkubali Yesu Kristo kama Mponyaji wangu,” hakuna mateso au ugonjwa unaoweza kukaa juu yako. Dumu moja kwa moja nalo. Lakini mara ya kwanza unapodhoofika na kusema, “Vema, ndio, bado ninao.” Ndipo Basi unaporomoka hadi pale ulipokuwa.

Ulisaini jambo hilo, kisha ukalirudisha tena. Kusema, “Ndiyo, Bwana. Ibilisi, ni—nitaurudisha.” Loo, ndugu. Simama papo hapo ilimradi kuna pumzi mwilini mwako, sema, “ Ninakataa kuwa nao. Ninakataa kuwa nao.” Je, unajisikiaje? “Vizuri Sana , haleluya.” Hivyo ndivyo. Hiyo ni kweli .

Mwonyeshe shetani umeumbwa kwa kitu gani; umezaliwa mara ya pili kwa Roho wa Mungu, wala huna haja ya kuziinamia sanamu zake. Kaa papo hapo, useme, “Sitaki vitu vyako.” “Mbona, hili hapa jina lako, daktari alisema…” “Sijali alichosema. Najua Alichosema Mungu. Ondoka nalo hapa.” Hiyo ni kweli, hiyo ndiyo njia ya kumkabili; kirudishe .

Yeye ndiye aliyekupa kitu hicho , itabidi awe ndiye atakayekirudisha .

MKATE WA KILA SIKU

Basi mtiini Mungu. Mpingeni Shetani, naye atawakimbia. Yakobo 4:7

23-0304

64-1227 – Mnasema Huyu Eti Kuwa Ni Nani?

Sasa kumbukeni, watu hawa walifurahia hizo baraka. Walifurahia mahubiri ya nabii huyu, huyu mtiwa mafuta. Walimwamini. Walimfuata. Lakini kulitokea huko jangwani, mtu jina la—lake Dathani, na mwingine jina lake Kora. Nao wakasema, “Hii haina budi kuwa ni kazi ya mtu mmoja. Musa anafikiri yeye ndiye pekee aliyeitwa na Mungu.”

Huo Ujumbe wa mtu mmoja, hawakuutaka. La, hawakuutaka. Wala Mungu kamwe hakushughulika ila na mtu mmoja kwa wakati mmoja. Daima ni Ujumbe wa mtu mmoja. Ni wakati gani alipopata kushughulika na watu, nje ya mtu mmoja tu? Ni mtu binafsi. Si kundi.

Wewe unawajibika kwa Mungu, kila mmoja wenu. Unasema, “Loo, ninaamini jambo Hilo.” Unaninii tu…Unachofanya, unalifurahia tu. Unafurahia wazo fulani.

MKATE WA KILA SIKU

Yule mwanamke akamwambia, Bwana, naona ya kuwa u nabii! Yohana 4:19

23-0303

58-0510 – Mwaminini Mungu

Dhambi iko kwenye maandamano. Huwezi kuwaambia, kwa sababu shetani ameliteka taifa. Alitujia miaka michache iliyopita; Yeye aliishi Paris, shetani na malaika zake. Nao walikuwa na vita vya kwanza vya dunia, na Ujerumani ingalizamisha taifa hili ardhini , lakini tulienda kuwasaidia.

Na mara vilipokwisha, ilirudi tena, mvinyo, wanawake, na wakati mkuu. Ndipo Shetani akatuma mtindo wake hapa, akawavua wanawake wetu, akaleta fedheha kwa taifa letu, kupitia staili na mitindo. Kisha akachukua tu jeshi lake na kutua Hollywood.

Wengi wenu enyi watu hamngewaruhusu watoto wenu kwenda kwenye maonyesho ya sinema na kuona vitu kama hivyo. Ibilisi ni mtu mwerevu; yeye hulileta moja kwa moja kwenye televisheni, ili ahakikishe umelipata.

MKATE WA KILA SIKU

Wala msiifuatishe namna ya dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu. Warumi 12:2

23-0302

61-0108 – Ufunuo, Mlango Wa Nne Sehemu Ya III

Adamu na Hawa walishona nguo nzuri tu kama Mmethodisti, Mbaptisti, Mpresbiteri, ama Mpentekoste yeyote angeweza kushona, iliufunika uchi wao. Lakini Mungu angeweza kuona kupitia hiyo, kwa hiyo akaua kitu fulani na kuzichukua hizo ngozi zilizokufa za—ngozi za mnyama aliyekufa na kuufunika.

Ilibidi damu ichukue mahali pake. Hiyo iliizuia hasira Yake, Yeye aliiona hiyo damu ndipo akarudi nyuma, kwa sababu kitu fulani kilikuwa kimeumwaga uhai wake. Ee Mungu!

Wazia hilo! Kitu pekee kitakachomzuia Mungu ni Damu. Na kuna Damu moja tu ambayo itamfanya arudi nyuma, na hiyo ni Mwana Wake Mwenyewe. Akiona hiyo ni Damu ya Mwana Wake Mwenyewe, atarudi nyuma.

Maana hiyo ndiyo karama ambayo…Mungu amempa Mwanawe, kuwakomboa wale aliowajua tangu zamani, nayo inamrudisha Mungu kutoka kwenye hukumu Yake.

Lakini hiyo Damu ikiondolewa, na wote waliojulikana tangu zamani wameletwa wakaingia kwenye huo Mwili wa thamani, Kanisa Lake limefanywa tayari na kunyakuliwa, basi hasira ya Mungu iko juu ya watu. Loo, ndugu, kamwe usipende kusimama hapo!

MKATE WA KILA SIKU

Kwa ajili hii Yesu naye, ili awatakase watu kwa damu yake mwenyewe, aliteswa nje ya lango. Waebrania 13:12

23-0301

62-1123 – Njia ya Kurudi

Sasa, tunaona ya kwamba wakati mwanadamu anapojaribu kutafuta seramu, daktari, kumpa mgonjwa wake, kumchanja kutokana na ugonjwa, yeye huijaribu kwanza kwa nguruwe, na kuona kama itafanya kazi. Lakini Mungu hakufanya hivyo, Yeye kamwe hakuchukua nguruwe, Aliitumia kwake yeye Mwenyewe. Daktari mzuri anayetaka kujaribu seramu, ikiwa hajui kama itaua au kuponya, anapaswa kuitumia yeye mwenyewe kwanza ili kujua, kabla hajaiweka kwa mtu mwingine.

Naye Mungu, ili, aitumie Seramu hii, ilimbidi kufanyika mwili na kukaa kati yetu, Mkombozi aliye wa Jamaa ya Karibu. Amina. Ilibidi Mungu afanyike mwanadamu, ili aweze kuitumia Seramu. Naye alichanjwa kule Yordani, amina, alipotoka mtoni kwa Yohana na kubatizwa, ndipo chanjo ikashuka. Dawa ikaanguka kutoka Mbinguni kama hua, ikisema, “Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu, ninayependezwa kukaa ndani yake. Alichanjwa.

Na mara baada ya chanjo kuja, jaribio likaja. Na kila mtu, mara tu unapompokea Roho Mtakatifu na kuchanjwa, kila pepo kutoka kuzimu atakugeukia wewe.

Hata familia yako mwenyewe, wakati mwingine itakukataa: mume wako, mke wako, mchungaji wako; unafukuzwa kanisani, unachekwa, unadhihakiwa; ni jaribio . Amina.

MKATE WA KILA SIKU

Yesu akajibu akasema, Hamjui mnaloliomba. Je! Mwaweza kunywea kikombe nitakachonywea mimi? Mathayo 20:22

23-0228

55-1111 – Ambapo Nadhani Pentekoste Iliposhindwa

Musa aliwaongoza watu milioni mbili jangwani. Naye akawaongoza kwa muda wa miaka 40, na alipotoka upande mwingine, hapakuwa na mtu dhaifu kati yao .

Je! ninyi madaktari hapa usiku wa leo, ama baadhi yenu, mngependa kujua daktari Musa alikuwa na maagizo gani ya daktari ? Aliwapa nini watu hao? Ni watoto wangapi waliozaliwa kila usiku? Ni wazee wangapi na kadhalika? Wangapi wachechemeao na vilema? Na je, alipatwa na maradhi mangapi, na mengineyo katika usiku mmoja?

Na Daktari Musa alitatua kila moja ya hayo .

Je, ungependa kuangalia katika mkoba wake wa dawa na kujua ni aina gani ya Maagizo ya taktari alitoa ?
Je, ungependa kujua ni kitu gani ?

Hebu tuone ilikuwa ni nini. Hii hapa: “Mimi ni Bwana nikuponyaye magonjwa yako yote . ” Amina.

Hiyo ndiyo dawa pekee aliyokuwa nayo, na ilifanya kazi kwa watu milioni mbili .

MKATE WA KILA SIKU

… kama yule nabii angalikuambia kutenda jambo kubwa, usingalilitenda? 2 Wafalme 5:13

23-0227

58-0126 – Msikieni Yeye

Kanisa ni wakala wa Mungu. Alisema sehemu moja katika Injili, “Mimi ni Mzabibu, ninyi ni matawi.” Mzabibu hauzai matunda; hutoa tawi, na tawi huzaa matunda. Kwa hiyo Kanisa ni Tawi ambalo Roho Mtakatifu analifanyia kazi.

Ananena kupitia midomo ya mchungaji. Anafanya kazi kupitia mikono yake. Na kupitia karama za Kiungu anaweka mwili wake katika hisia, akiongozwa na Roho Mtakatifu kwa kujiondoa mwenyewe na kumwacha Roho Mtakatifu atawale.

Analeta jumbe; anaona maono. Na mambo makuu, haidhuru yaweza kuwa kitu gani Mungu amemchagua kufanya, kama atajisalimisha kwa Roho, Mungu atafanya kazi kupitia kwake, ama mshiriki yeyote wa Kanisa Lake.

MKATE WA KILA SIKU

Wazee watawalao vema na wahesabiwe kustahili heshima maradufu; hasa wao wajitaabishao kwa kuhutubu na kufundisha. 1 Timotheo 5:17

23-0226

55-1116 – Kuitwa kwa Ibrahimu

Ungeweza kuwazia kwenda hapa na kumwambia nguruwe, kusema, “Sasa, angalia hapa, bwana Nguruwe, nitakuambia, umekosea.” Mbona, ungeweza kumwosha na kumvika koti rasmi, kama ungetaka. Hilo lisingefaa kitu; angerudi moja kwa moja kwenye dimbwi la matope na kugaagaa tena. Ndiyo asili yake. Kwanza Kabisa Yeye ni nguruwe.

Na kila mtu, kila mtu ambaye hajazaliwa upya, haijalishi unajaribu kuwa mzuri kiasi gani, unajiona kuwa ni mzuri vipi , wewe ni mwenye dhambi kwa asili, mpaka Mungu abadilishe asili yako. Amina.

Sasa, hiyo ni kweli. Hatupendi kusema jambo hilo. “Lo,” unasema, “mimi huvaa nguo nzuri zaidi katika ujirani wangu . Ninalo gari zuri zaidi. Nina bora zaidi…” Hilo halihusiani na jambo hilo. Ikiwa asili sio …”Sijawahi kusema uwongo. Si…” Hilo bado halina uhusiano wowote nalo. Si kwa ustahilifu wako mwenyewe, bali ni uchaguzi usio na masharti na wito wa Mungu.

Na wokovu ni ustahilifu wa matendo ya Yesu Kristo, na hakuna kitu ambacho mtu yeyote angeweza kufanya. Mungu, kwa upendo wake alimwokoa mwanadamu.

MKATE WA KILA SIKU

Lakini kwa neema ya Mungu nimekuwa hivi nilivyo. 1 Wakorintho 15:10

23-0225

63-0126 – Uwekezaji

Danieli alikusudia moyoni mwake ya kwamba hatajichafua na ulimwengu. Alikuwa anaenda kudumisha utaratibu ambao Mungu alikuwa ameandaa, zile amri za Mungu.

Kwa nini ninyi wanawake na wanaume msiweze kufanya jambo lile lile? Lakini Marilyn Monroe ama mtu fulani walizikata nywele zao, halafu mke wa mhubiri fulani akafanya jambo lile lile, nanyi mnafikiri mna haki ya kufanya hivyo. Hilo haliwaachilii kutoka kwa Neno la Mungu.

Nanyi wahubiri mnawaacha wake zenu wawaongoze. Ni aibu jinsi gani! Ni—ni—ni neno la jinsi gani, la kuwa mwanamume. “Mtumishi wa Kristo asiyeweza kuiongoza nyumba yake mwenyewe, ataongozaje nyumba ya Mungu?”

“Vema,” mnasema, “Ndugu Branham, hayo, hayo ni mambo madogo tu.” Vema.

Hebu na tuyanyoshe mambo yaliyo madogo, ndipo tuliendee jambo kubwa. Mnaona? Ndipo tutazungumza juu ya Roho Mtakatifu, na ma—na mambo ya jinsi ya kupokea karama za Kiungu.

MKATE WA KILA SIKU

Jitakaseni basi, iweni watakatifu, kwa kuwa mimi ndimi BWANA, Mungu wenu. Mambo ya Walawi 20:7

23-0224

59-0708M – Kuweka Jengo Wakfu, Kwa Bwana

Si ajabu kwamba kanisa la kawaida leo hii haliwezi kuamini miujiza. Hawajawahi kamwe kuingia katika mahali panapotendeka miujiza ambapo wamepumzika na Mungu. Hapo ndipo fimbo ya Haruni ilipochipuka, kitu ambacho kilikuwa kimekufa. Fimbo kuukuu iliyokauka kutoka jangwani katika mahali hapo patakatifu pa patakatifu ilitwaa uhai mpya, na kuchanua maua, na kuchipua, na kutoa majani.

Namna gani? Ilikuwa imekaa katika patakatifu pa patakatifu. Unaweza kumchukua mwenye dhambi aliyekufa, aliyeoza, wa kimwili akilini mwake na katika kufikiri kwake ni mkosoaji wa nguvu za Mungu, na kumleta katika Uwepo wa Roho Mtakatifu, kutakuwa na jambo fulani litakalompata. Hakika. Kuingia katika eneo hilo pweke na Mungu…

“Yeye huketi,” asema Musa katika sura inayofuata, “kati ya giza kuu.” Hapo ndipo Mungu hukaa. Hapo ndipo uhai hukaa. Ni katikati ya upotovu uliooza. Je, uhai hukaa wapi? Katika mbegu baada ya kuoza. Inapojifia yenyewe huleta uhai mpya.

Mungu hukaa wapi? Yeye Atakaa nawe ikiwa uko tayari kujifia mwenyewe na kumpa yeye nafasi: huduma: mwili. kiakili: roho, mawazo; na nafsi , imani yako kwa Mungu: nyumba yenye vyumba vitatu.

MKATE WA KILA SIKU

Mkaribieni Mungu, naye atawakaribia ninyi. Itakaseni mikono yenu, enyi wenye dhambi, na kuisafisha mioyo yenu, enyi wenye nia mbili. Yakobo 4:8

23-0223

53-0614A – Kuishindania Imani Waliyokabidhiwa Watakatifu mara Moja

Sasa, Mungu ni mwenye enzi. Bila shaka, Yeye—Yeye anajua, “Hapendi yeyote apotee bali wote wafikie toba.” Lakini ili awe Mungu, hana budi kujua, na Yeye anajua kabla jambo hilo halijatokea, ni nani angeokolewa na nani hangeokolewa. Hiyo ni kweli.

Basi kuna baadhi ya watu hawataokolewa, na Mungu alijua jambo hilo hapo mwanzo hawangeweza.

Na hata alimwinua Farao na kuufanya moyo wake kuwa mgumu kwa sababu hiyo hiyo, ili apate kuonyesha uweza wake. Na Esau na Yakobo, ili kuonyesha uchaguzi wa Mungu ungeweza kusimama hakika… Hiyo ni kweli. Kabla…

Unaona, wewe ni Mkristo kwa sababu Mungu alikukusudia kwamba lazima uwe Mkristo. Sasa, unaweza kuligeuzia kando. Baadhi…Mungu atamweka mtu fulani mahali pako. Lakini mahali pako papo pale. Kama Mungu akikuita, nenda kapatwae na udumu napo.

MKATE WA KILA SIKU

Kwa hiyo ndugu, jitahidini zaidi kufanya imara kuitwa kwenu na uteule wenu; maana mkitenda hayo hamtajikwaa kamwe. 2 Petro 1:10

23-0222

56-0610 – Ukamilifu

Hebu tuchore picha ya wakati. Hebu tuone duara kamilifu, milele, milele. Na basi, mara, dhambi ikaingia, na kuweka ninii—ninii ndogo…Kama mke wangu anavyoiita, “kovu” dogo, ama tone dogo kwenye mnyororo. Kwa hiyo, inashuka chini sasa. Milele inaendelea, bali haiko katika hali yake kamilifu.

Hili hapa pengo dogo linaloshuka, linavunja upande huu, linatokea upande huu. Ilimbidi Mungu kufanya jambo hilo kwa sababu Shetani alisababisha jambo hilo. Nayo ikashuka ikaingia katika muda wa wakati, kwa ajili ya kujaribiwa, na kukamilishwa, na kwa kuwatakasa waliopotoea.

Kwamba, Mungu kwa neema yake ya mamlaka Yake, huenda siku moja ikainua kovu hilo dogo, ama pengo, na kulirudisha kwenye duara kamilifu, ndipo itavingirika namna ile ile. Mnaona jambo hilo?

MKATE WA KILA SIKU

Binadamu amefanana na ubatili,
Siku zake ni kama kivuli kipitacho. Zaburi 144:4

23-0221

63-0412M – Ulimwengu Unaporomoka

Tumejenga madhehebu yetu juu ya ishara fulani, kama vile tunavyochukua kunena kwa lugha. Ninaamini katika kunena kwa lugha, hakika, bali kila kitu kinachonena kwa lugha hakina Roho Mtakatifu.

Mimi ni mmishenari. Nimeona wachawi wakinena kwa lugha na kufasiri, na kutoa tafsiri ya kweli ya lugha hiyo, na kunywa damu kutoka katika fuvu la kichwa cha mwanadamu, na kumwita Ibilisi. Kweli.

Rudini kwenye Neno la Mungu ambako ndiko kwenu. Yakimbieni mambo haya. Maisha ndiyo yanayonena ndani ya binadamu, Maisha ya Kristo. Unawezaje uwe wa Kristo na ushikilie taratibu hizi? Basi angalia mahali tulipofikia?

Kanisa la Pentekoste, wakati lilipoanza, miaka hamsini iliyopita, na Roho Mtakatifu akaanza kushuka na watu wakapokea karama ya kunena kwa lugha, ndipo mkaanza kuingiza kila kitu ndani yake, mkifanya hiki madhehebu, na kile, na kile kingine. Basi angalieni mahali mlipo leo, mpaka kitu hicho chote kimeoza. Hiyo ni kweli.

Mfumo wote umepotoka, na unaporomoka tu pamoja na ulimwengu wote. Kila kitu hakina budi kufanya hivyo. “Bali tumepokea Ufalme usioweza kutikiswa.”

MKATE WA KILA SIKU

Roho ndiyo itiayo uzima, mwili haufai kitu; maneno hayo niliyowaambia ni roho. Yohana 6:63

23-0220

59-0510E – Ni Nani Huyu?

Ufunuo mmoja juu ya mchanga huo mtakatifu, wakati mmoja juu ya mahali hapo, mtu hawezi kuwa vile vile. Mtu, kabla hajajiita Mkristo, kabla hajaweza kujitambulisha, kwanza anapaswa kuwa na tukio hilo la upande-wa-nyuma-ya-jangwa, ambapo alikutana na Mungu, uso kwa uso.

Kwa kuwa, siku hizi, unaweza kuwa na aina yoyote ya jibu. Unaweza kumwona Bwana akifanya vile hasa Yeye alivyosema ufanye, na wanatheolojia werevu watalielezea vinginevyo. Watasema, “Hiyo ilikuwa ni kwa ajili ya siku nyingine. Ilikuwa kwa ajili ya hii. Ama, ni kwa ajili ya wakati mwingine. Au, ni makosa.” Kama walivyosema juu ya Yesu, “Yeye ni Beelzebuli, ibilisi. Yeye ni mpiga ramli.” Na mambo hayo yote, wana jibu.

Lakini wakati mtu amewahi kamwe kukutana na Kristo, na kumwona kama Paulo alivyomwona, ama kupata tukio Naye, hakuna wanatheolojia wa kutosha ulimwenguni kuweza kuelezea tukio hilo vinginevyo kwa mtu.

Hiyo ndiyo sababu, siku hizi, hawana tukio. Hiyo ndiyo sababu hawawezi kusema…wote wanasema, “Ni nani Huyu? Ni nini Hii? Inatoka wapi?” Hawana jibu. Kwa nini? Kwa sababu, yote wajuayo ni thiolojia ambayo kanisa fulani limeunda. Sio “kuijua thiolojia” ni Uzima. Sio “kuijua Biblia” ni Uzima.

Bali “kumjua Yeye” ni Uzima. “Kumjua Yeye” kama Mwokozi wako binafsi, kama Yule ambaye amekujaza na Uwepo Wake. Ulikuwepo wakati ilipototendeka. Hakuna mtu anayeweza kuliondoa kwako. Hakuna mtu anayeweza kukuelezea Hilo vinginevyo. Wakati tukio hilo linapokutokea, unajua Yeye ni Nani. Kwangu mimi, Yeye ni Yesu Kristo yeye yule jana, leo, na hata milele.

MKATE WA KILA SIKU

Kwa kuwa nia ya mwili ni mauti; bali nia ya roho ni uzima na amani. Warumi 8:6

23-0219

55-1008 – Matokeo ya Maamuzi

Akasema, “Lakini ni amri juu ya amri, na kanuni juu ya kanuni. huku kidogo na huku kidogo, na ushikilie sana lililo jema. La, bali kwa midomo ya watu wageni na kwa lugha nyingine nitasema na watu hawa, na hii ndiyo Sabato.” Amina.

Waebrania 4 ilisema, “Basi, Imesalia raha ya Sabato kwa watu wa Mungu, kwa maana sisi tulioingia katika raha yake, tumepumzika katika kazi zetu, kama vile Mungu alivyopumzika katika kazi zake; Mungu alifanya kazi siku sita, na siku ya saba akapumzika, naye hakurudi tena. Na mtu anaweza kufanya kazi duniani hapa mpaka awe na umri wa miaka ishirini, thelathini, arobaini, sabini, lakini anapoacha kazi zake za kilimwengu, anaingia katika pumziko la milele pamoja na Mungu, kama vile Mungu alivyofanya hapo mwanzo.

Loo, ndugu, kama unaishi mpakani usiku wa leo, njoo huku. Vuka Yordani. Ni ajabu. Kuna zabibu kubwa kubwa huku. Tunao ushahidi wa awali, tuna…Haleluya. Tuna baadhi ya akina Yoshua na Kalebu ambao wamevuka mpaka na kurudisha ushahidi kwamba ni Nchi nzuri.

Kila ahadi ambayo Mungu ametoa iko hapa. Injili yote, Biblia yote , uponyaji wa Kiungu, shangwe, furaha, amani, kila kitu ambacho Biblia iliahidi, kila tunda lipo katika nchi hii. Amina.

MKATE WA KILA SIKU

Kwa maana ni amri juu ya amri, amri juu ya amri; kanuni juu ya kanuni, kanuni juu ya kanuni; huku kidogo na huku kidogo.

La, bali kwa midomo ya watu wageni, na kwa lugha nyingine atasema na watu hawa. Isaya 28:10-11

23-0218

55-1006A – Maisha Yaliyofichika

Je, ninamtazama Henry Groat. Mungu akubariki, Ndugu Henry, sijakuona kwa muda mrefu na ndugu. Nilitokea tu kutazama nyuma na kumuona baba na kumtambua. Nilipovunjika moyo sana au nilipotoka hudumani kwa yapata miezi minane, walikuwa ndugu na baba halisi kwangu. Walikaa nami wakati wote.

Sitasahau kamwe siku ambayo Ndugu Groat pale, tulienda kwenye shamba la mahindi kuomba. Nilikuwa na wasiwasi sana; Nilikaa katika ono muda mrefu sana sikuweza kujua kama nilikuwa ndani au nje. Sitamsahau kamwe Ndugu Groat alipopiga magoti kuomba pamoja nami. Alinikumbatia, kirahisi tu kama kusema “Sasa, Baba Mungu, je, utakuja kumsaidia Ndugu Branham? Baba Mungu, utakuja kumsaidia Ndugu Branham?” Hilo limedumu nami daima, Ndugu Groat.

Loo, itakuwaje, Ndugu Groat, siku moja ninatumaini kukukumbatia kwa mkono wangu na kuketi karibu na miti ya kijani kibichi ambapo chemchemi za maji ya Uzima zinatiririka kutoka chini ya kile kiti cha enzi. Tutakuwa katika Uwepo wa Baba Mungu wetu basi milele na milele kuishi katika Uwepo wake.

MKATE WA KILA SIKU

Kwa maana huyo Mwana-Kondoo, aliye katikati ya kiti cha enzi, atawachunga, naye atawaongoza kwenye chemchemi za maji yenye uhai, na Mungu atayafuta machozi yote katika macho yao. Ufunuo 7:17

23-0217

51-0729A – Kufufuliwa Kwa Lazaro

Ninapenda jambo fulani lenye ujasiri. Namdharau tu mwoga. Nawe je? Mtu anayeogopa…Simama papo hapo . Ikiwa una mambo yaliyo sahihi nyuma yako; simama kwa unachojua ni kweli. Usiwe tu tayari kuliishia, lifie, ama chochote kile. Kama ni kweli, ni kweli.

Watu wengine wamefia yaliyo kweli. Na hivyo ndivyo ilivyo kwa Injili. Ikiwa sikufikiri ilikuwa ni kweli, na sikuamini Yeye alikuwa Mwana wa Mungu, ningekuwa kinyume Naye. Ningekuwa nje huku nikisema kila niwezalo dhidi Yake, kwa sababu singefikiri ilikuwa kweli. Lakini najua Yeye yuko sahihi.

Na hivyo basi mimi…ninaamini jambo hilo kwa moyo wangu wote. Na kama—na kama sehemu tu ya hili ni Kweli , na mengine yote si kweli, basi si— yote si kweli. Ni aidha kweli ama uwongo . Na kila neno ni kweli. Unaweza kuning’iniza nafsi yako kwenye fungu lolote la Injili na kuliamini; kwa sababu kila sehemu yake ni kweli.

MKATE WA KILA SIKU

Msiogope , lakini mikono yenu na iwe hodari. Zekaria 8:13

23-0216

61-0217 – Alama Ya Mnyama Na Muhuri Wa Mungu #2

Angalia, “Mtu asipozaliwa mara ya pili, hawezi kamwe kuingia katika Ufalme.” Hiyo ni kweli . Ni Lazima uje. Haijalishi wewe ni wa kidini jinsi gani, yote ufanyayo, hilo halina uhusiano wowote na jambo hilo .
Jambo Hilo linakufanya kuwa raia mzuri sana, lakini si raia wa ule Ufalme kule , labda wa ufalme huu hapa.

Bali Ufalme wa Mungu umo ndani yenu; umezaliwa katika Ufalme. Ufalme unaingia…Ufalme wa Mungu ni Roho Mtakatifu; wewe ni wa Ufalme huo.

Hiyo ndiyo sababu wanawake hawakati nywele zao, hawavai nguo fupi. Hiyo ndiyo sababu wanaume hawavuti sigara na mambo kama hayo. Wao Wanatoka juu, Roho wao huwafundisha haki, utakatifu. Hawa—hawaapi; wao—hawatumii lugha mbaya na kadhalika, kwa nini? Wamezaliwa kutoka juu. Wao ni tofauti. Wao wanatoka—ni raia kutoka juu.

MKATE WA KILA SIKU

Yesu akajibu, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa kwa maji na kwa Roho, hawezi kuuingia ufalme wa Mungu.

Kilichozaliwa kwa mwili ni mwili; na kilichozaliwa kwa Roho ni roho.

  Yohana 3:5-6

23-0215

52-0720A – Hadithi ya Maisha

Na sisi kila mmoja wetu ana maisha ambayo Mungu ametupa, nasi hatunabudi kuyaishi.

Nami…Kwa maoni yangu manyenyekevu, ikiwa utayapata haya, ninafikiri maisha yaliyo bora zaidi ulimwenguni, haidhuru ni ya juu ama chini, kama tutaipata njia ya Mungu na kutembea ndani yake ambapo Mungu ametuwekea sisi kutembea.

MKATE WA KILA SIKU

Katika njia zako zote mkiri yeye,
Naye atayanyosha mapito yako. Mithali 3:6

23-0214

64-1227 – Mnasema Huyu Eti Kuwa Ni Nani?

Mtu atashuka aende hapa kwenye hii—kwenye hii…kula. Na kama ungeona buibui kwenye bakuli lako la supu, ungetaka kuishtaki kampuni hiyo ama mkahawa huo. Mbona, usingekula hiyo supu, ingekuwa na sumu. U—u—u—usingeinywa hata kidogo, mende mkubwa ama kitu fulani kilichochemshwa katika bakuli la supu. Mbona, usingeinywa hata kidogo. Ingekuchefua kuwazia jambo hilo.

Lakini hata hivyo, utaruhusu kundi la wanateolojia waingize kitu fulani ndani ya koo lako kitakachokupeleka maili milioni moja kutoka kwa Mungu, na unakimeza. Wakati, “Mtu ataishi kwa kila Neno litokalo katika kinywa cha Mungu.” Ni nyororo ambayo nafsi yako inaning’inia juu ya kuzimu nayo.

Na kama nilivyosema hapo awali, “Nyororo ni imara sana kwenye sehemu yake iliyo dhaifu sana.” Kiungo kimoja kuvunjika…hilo tu ndilo linalokupasa kufanya ni kuvunja kimoja; hivyo tu. Vingine vyote vinaachilia pamoja nacho. Ina nguvu tu kadiri ya kiungo chake kilicho dhaifu sana.

MKATE WA KILA SIKU

Ila mlicho nacho kishikeni sana, hata nitakapokuja. Ufunuo 2:25

23-0211

53-0405E – Mashahidi

Nawazia, usiku kucha kulikuwa na mkutano wa maombi ukiendelea. Unajua, ikiwa unakuja kwenye jaribio…

Hili hapa. Hiyo ndiyo shida ya kanisa siku hizi; unategemea hisia na uwezo wako mwenyewe, badala ya kulipeleka kwa Bwana katika maombi. Hiyo ni kweli. Siku hizi tunaanza kumtuma mtu fulani mahali fulani, vema, unasema, tunashuka na kuwa na mashauri kidogo, na kukutana na kusema, “Tunapaswa kufanya hivi, au kwenda hapa, au kufanya vile.”

Lakini Biblia, katika zile siku kabla hawajawatuma mitume, walikusanyika pamoja na kufunga na kuomba. Ndipo Roho Mtakatifu akasema, “Nitengeeni Paulo na Barnaba.” Roho Mtakatifu! Mnaona, si maoni ya mwanadamu; bali Roho Mtakatifu akiongoza, akiongoza. Amina. Tazama.

Sasa, mkutano wa maombi, usiku kucha, kwa hiyo iliwabidi waonyeshe walichoumbwa kwacho. Na, ndugu, kila mtu anayedai kuwa Mkristo, wakati mmoja ama mwingine huna budi kuonyesha umeumbwa kwa kitu gani. Ibilisi atakupa changamoto.

MKATE WA KILA SIKU

Nami maombi yangu nakuomba Wewe, BWANA,
Wakati ukupendezao; Ee Mungu,
Kwa wingi wa fadhili zako unijibu,
Katika kweli ya wokovu wako.

Zaburi 69:13

23-0210

63-1114 – Ushawishi

Tunapaswa kuheshimiana mmoja na mwenzake, kuheshimiana mmoja na mwenzake, kama ndugu, dada. Na kupendana mmoja na mwenzake, kwa upendo usiopungua.

Unasema, “Vema, siwezi kabisa.” Vema, bakia tu hapa muda mrefu kidogo, na ndipo utawapenda watu, pia. Utawapenda wale wasiokupenda. Hiyo kweli ni ishara nzuri ya Ukristo: wakati unapoweza, kutoka moyoni mwako, kuwapenda wale ambao hawakupendi. Wapende wasiopendeka.

Yesu alisema, “Ukiwafanyia fadhili wale tu ambao hukufadhili, vema, watoza ushuru hufanya jambo lilo hilo.” Bali, unaona, lazima uwahurumie wale wasiokuhurumia. Watendee wema wale ambao wangekutendea uovu. Daima kumbuka hilo. Weka hilo mbele zako, kwamba Mungu anakutazama.

Kumbuka, Mungu alikuwa mwema kwako wakati ulipokuwa mwovu Kwake. “Wakati mlipokuwa mngali wenye dhambi, Kristo alikufa kwa ajili yenu.”

MKATE WA KILA SIKU

Maana, hii ndiyo habari mliyoisikia tangu mwanzo, kwamba tupendane sisi kwa sisi. 1 Yohana 3:11

23-0209

62-0119 – Bendera

Sasa, mtu ameumbwa kiumbe chenye asili tatu: nafsi, mwili, roho.

Sasa, nje ni mwili. Kuna milango mitano ya kuingia kwenye mwili huo, na naam hiyo ni zile hisi tano, hakika: kuona, kuonja, kugusa, kunusa, na kusikia.

Mle ndani, kama mbegu iliyopandwa, ndani yake ni kitu chororo cha mbegu, ambacho ni nafsi. Kuna milango mitano ya kuingia humo, unayoingilia: dhamira, na kumbukumbu, na kadhalika .

Lakini basi ndani ya chumba hicho kidogo kuna chumba cha tatu, ambacho ni roho. Na hiyo ndiyo inayoongoza hizo zingine. Kuna njia moja tu ya kuingia humo, na hiyo ni hiari ya mtu. Unaweza kuikubali ama kuikataa, na hiyo ndiyo njia pekee ya kuingia humo.

Kama ukiyakubali mapenzi ya Mungu kupitia roho huyo, Roho wa Mungu anachukua nafasi Yake ndani ya moyo wako na kukutawala wewe mzima. Na usipokubali jambo Hilo, basi adui anashika hatamu na kukutawala wewe mzima.

MKATE WA KILA SIKU

Kwa kuwa wote wanaoongozwa na Roho wa Mungu, hao ndio wana wa Mungu. Warumi 8:14

23-0208

57-0828 – Waebrania, Mlango Wa Pili #3

Mungu asingeweza kuteseka katika Roho. Ilibidi afanyike mwili, apate kusikia uchungu wa magonjwa, apate kusikia jaribio la tamaa mbaya, kusikia jaribio la kupungukiwa, kusikia jaribio la njaa, kusikia nguvu za mauti. Apate kutwaa juu Yake jukumu la kusimama Mbele ya Roho Yehova mkuu, yule Roho, si Mwanadamu; Roho, kufanya upatanisho kwa ajili ya maisha haya.

Basi Yesu alichukua hayo, kusudi apate kutupatanisha, kwa maana anajua jinsi hali ya mambo ilivyo. Unapokuwa mgonjwa, Yeye anajua unavyojisikia. Unapojaribiwa, Yeye anajua unavyojisikia.

MKATE WA KILA SIKU

Maana mmejua neema ya Bwana wetu Yesu Kristo, jinsi alivyokuwa maskini kwa ajili yenu, ingawa alikuwa tajiri, ili kwamba ninyi mpate kuwa matajiri kwa umaskini wake. 2 Wakorintho 8:9

23-0207

63-0802 – Mng’ang’anizi

Watu hawang’ang’anii.
Kama Roho Mtakatifu, kama Yesu Kristo, akithibitisha kwamba Yeye yuko hapa miongoni mwetu, basi kazana mpaka umfikie Yeye. Kama maskini yule mwanamke aliyekuwa anatokwa na damu, na mambo yote mbalimbali yaliyotukia, na maadui njiani mwake, , moja kwa moja mpaka akamgusa Yeye.

Ikiwa kanisa hili, usiku wa leo, lingefanya jambo lile lile, lingekazana kupenya kupitia kila kiwango cha kutokuamini, lingeshikamanisha panga na ibilisi na kutokuamini kwake, na lijitahidi kujua kwamba wewe ni mwana wa Mungu na mrithi wa mambo haya, na Yesu Kristo akiwepo kuwaonyesheni ya kwamba Yeye yuko pamoja nanyi, kulitimiza Neno Lake. Ng’ang’ania, usiache chochote kikuzuie.

Ninashangaa tu. Kama imani kweli ikitia nanga, kitu chochote kingeweza kukuzuia? Hamlipati. Kama kweli mliipata, hilo lingetosha. Hivyo tu. Unaona?

MKATE WA KILA SIKU

Kwani hao wote walitaka kutuogofisha, wakisema, Italegea mikono yao katika kazi, isifanyike. Lakini sasa nitaitia mikono yangu nguvu. Nehemia 6:9

23-0206

62-1223 – Dhihaka Kwa Sababu Ya Neno

Na Mungu huweka wakati na ana kusudi kwa ajili ya kila kitu afanyacho. Hakuna kitu kinachotukia kwa bahati mbaya tu kwa wale wampendao Bwana na wameitwa kulingana na wito Wake. Mnaona?

Tumechaguliwa tangu zamani. Na kila kitu hufanya kazi vizuri tu, kwa ajili ya jambo hilo, kwa kuwa Yeye hawezi kusema uongo. Naye alisema hiyo ilikuwa ndivyo, ya kwamba kila kitu kina wakati wake, majira yake, na kina njia yake.

Na Mungu yuko nyuma ya kila msogeo. Na wakati mwingine unafikiri kwamba kila kitu kinaenda mrama. Ni juu yetu. Mambo hayo yanawekwa juu yetu, majaribu na fadhaa. Ni kujaribiwa, kuona vile tutakavyotenda kwa tukio fulani.

MKATE WA KILA SIKU

Maana ghadhabu zake ni za kitambo kidogo,
Katika radhi yake mna uhai.
Huenda kilio huja kukaa usiku,
Lakini asubuhi huwa furaha.

Zaburi 30:5

23-0205

62-0513M – Mwenendo Wa Nabii Wa Kweli Wa Mungu

Na wakati Neno la Bwana linapomjia mtumishi wa kweli, hana budi kwenda, haidhuru hali ya mambo ikoje, ama haidhuru kuna shida gani. Hana budi kwenda, kwa vyovyote vile. Kama yeye yuko tayari, kama anajisikia kwenda, kama anataka kwenda, kama chochote kile; hana budi kwenda, haidhuru.

Ni Mungu anayenena, naye hana budi kuubeba Ujumbe huu. Kwa sababu, ni…Haendei upuuzi. Haendi kwa ajili ya kupata fedha. Haendi kwa ajili ya kupendwa na watu. Yeye huenda tu katika Jina la Bwana, kwa ajili ya jambo moja .

Ana hu—huduma, naye ametumwa na Bwana. Naye ni Neno la Mungu, kwa sababu anabeba Neno la Bwana. Huyo ni nabii wa kweli wa Bwana.

MKATE WA KILA SIKU

Maana, ingawa nimekuwa huru kwa watu wote, nalijifanya mtumwa wa wote, ili nipate watu wengi zaidi. 1 Wakorintho 9:19

23-0204

64-0418E – Yesu Hutimiza Miadi Yake Yote

Ulimwengu mzima umechafuliwa. Yote yaliyo kwenye televisheni na kadhalika ni maskini upuuzi mchafu, wa kishenzi. Nanyi mnajaribu kuuiga namna hiyo. Hivi hutachukua mfano wa Yesu? Hivi huta—hutamruhusu? Hutalisikiliza Neno Lake? Hutafanya mambo haya yaliyo haki?

Ni wangapi humu ndani watakaosema kwa uaminifu kwamba unajua hujampokea Roho Mtakatifu? Jiangalie mwenyewe, kwenye kioo, na kujua hujampokea. Ujue, na uyaangalie tu maisha yako mwenyewe, na vile ufanyavyo.

Si kwa sababu wewe ni mfuasi wa kanisa, “Mimi ni Mmethodisti, Mbaptisti, Mpres-…Mimi…” Hiyo ni sawa. Sisemi kitu dhidi ya hilo. Lakini ninakuuliza, hivi unamjua Kristo Yesu? Yeye anaishi ndani yako? Kama anaishi, Yeye atajitambulisha mle. Kama yuko mle, itambidi kujitambulisha. Huwezi kumficha, Yeye huonekana wazi.

MKATE WA KILA SIKU

Endeni njia yote aliyowaagiza BWANA, Mungu wenu, mpate kuwa hai, na kufanikiwa, mkafanye siku zenu kuwa nyingi katika nchi mtakayoimiliki. Kumbukumbu la Torati 5:33

23-0203

53-0601 – Lo lote Atakalowaambia, Fanyeni

Kama wewe—ikiwa hakuna vita, basi hakuna ushindi. Lakini lazima uwe na vita ili kupata ushindi.

Kama ungepewa hilo tu, haingekuwa—isingekuwa na—usingekuwa ushindi. Bali yeye ashindaye ndiye aliye na ushindi .

Basi Yesu akaja duniani; Alikuwa na vita; Yeye Alishinda. Na usiku wa leo tunayo vita, na tukiwa na Kristo, tunaweza kupata ushindi.

MKATE WA KILA SIKU

Mwimbieni BWANA wimbo mpya,
Kwa maana ametenda mambo ya ajabu.
Mkono wa kuume wake mwenyewe,
Mkono wake mtakatifu umemtendea wokovu.

Zaburi 98:1

23-0202

55-1007 – Nguvu ya Maamuzi

Musa akaenda mbele, akiwa amebeba fimbo. Nasi tunaona kwamba Bahari ya Shamu ilifunguka, kwa sababu upepo mkali ulifuata Moto huo, Nuru ya Mungu. Wakati watu wanapotembea katika Nuru, ndipo upepo hufuata.

Yesu alisema, “Kaeni katika mji wa Yerusalemu hata mvikwe uwezo utokao juu. Nao wakangoja mpaka ikaja sauti ya upepo wa nguvu ukienda kasi kutoka mbinguni. Walitembea katika Nuru, mpaka upepo ukaanza kuvuma. Amina.

Ingia tu Nuruni usiku wa leo, ninyi mlio nje ya Kristo; pepo zitarudi tena kama zilivyokuwa katika siku ya Pentekoste. Endelea tu kutembea katika Nuru; itatenganisha kitu hicho kilichokuwa kinakuzuia kutoka upande mmoja hadi mwingine.

MKATE WA KILA SIKU

Na waende kwa sheria na ushuhuda; ikiwa hawasemi sawasawa na neno hili, bila shaka kwa hao hapana asubuhi. Isaya 8:20

23-0201

63-1226 – Utaratibu Wa Kanisa

Sasa, sijaribu kuchukua mamlaka au kitu kama hicho, lakini, mwaona, mtu au cho chote kilicho na vichwa viwili, haki—hakijui jinsi ya kuenenda.

Mungu hajapata kuwa na vichwa viwili kamwe kwa Kanisa Lake, Yeye hakufanya hivyo kamwe, ni kichwa kimoja. Yeye kila mara alitenda hivyo katika kila kizazi vile tumesoma Maandiko kote, kila mara kuna mtu mmoja ambaye Yeye humshughulikia. Kwa sababu ukiwa na watu wawili, una maoni mawili.

Yapasa kuwe na Yakini moja ya mwisho, na yakini yangu ni Neno, Biblia. Kama mchungaji hapa wa kanisa, Yakini yangu ni Neno, nami nataka…Najua ninyi ni Ndugu, mnanichukua mimi kama Yakini yenu kwa yale…mradi ninamfuata Mungu kama Paulo alivyosema katika

MKATE WA KILA SIKU

Basi, nawasihi mnifuate mimi . 1 Wakorintho 4:16

23-0131

59-0920 – Kupanda Mzabibu Na Mahali Pa Kuupandia

Wakati Roho wa kweli wa Mungu anapotenda kazi juu ya mwaminio, lolote Maandiko yasemalo, atasema, “Amina.” Mbona? Roho Mtakatifu ndiye aliyeiandika Biblia, yuko ndani yake, akiyapigapiga maisha yake. Yeye hajali ni nani anayeketi karibu, ama yale mtu mwingine yeyote asemayo. Sikuzote litaendana na Neno.

Kuna ya uongo. Ni matango. Yametoka kwenye mzabibu mwitu. Ni mzabibu mkubwa, unaifunika dunia nzima, bali ni mauti. Mengi ya hayo yametupwa miongoni mwa watu.

Lakini, kumbukeni, “Unga” unayapa Uzima tena, unayang’oa na kuyaweka mahali pazuri, ambapo ni Kristo Yesu. Chochote Neno Lake lilicho, na liwe “amina,” kwako. Ndipo Roho wa Mungu, basi, furaha ya kiroho itatiririka kama mto. “Atakuwa kama mtu, mti, uliopandwa kando ya mito ya maji. Majani yake hatanyauka. Hataketi kwenye kiti cha wenye mizaha ama cha asiyeamini, ama mtu mwovu anayeishi kwa kufuata mambo ya ulimwengu, bali atazaa matunda katika majira yake.”

Ni tunda la aina gani? Kama umepandwa katika Kristo, utazaa matunda ya kiroho, matunda ya kiroho ya Roho Mtakatifu. Roho Mtakatifu anaishi ndani yako.

MKATE WA KILA SIKU

Naye atakuwa kama mti uliopandwa
Kandokando ya vijito vya maji,
Uzaao matunda yake kwa majira yake,
Wala jani lake halinyauki;
Na kila alitendalo litafanikiwa. Zaburi 1:3

23-0130

65-1207 – Uongoz

Una chaguo la mwenendo. Jinsi unavyoenenda, hiyo ni shauri lako.
Una chaguo la mke. Unaondoka na kuoa mke wako. Ukitaka kuoa mke, unataka kuoa yule anayeambatana na…jinsi unavyotaka unavyopanga nyumba yako ya usoni iwe.

Je, ungewazia mwanamume, mwanamume Mkristo, akiondoka na kutwaa mmoja wa hawa Vipusa wa kisasa kama mke? Waona? Ungewazia hayo? Je, mtu huyo anafikiri nini? Atakuwa na nyumba ya namna gani kama akichukua mwenda uchi, mcheshi mwigizaji kutoka barabarani hapa, kahaba wa barabarani?

“Lo,” mnasema, “sasa, ngoja kidogo.” Je, anajivalishaje? Mwaona? Mwaona? Kuvaa suruali fupi na kadhalika, yeye ni kahaba wa barabarani. “Lo,” mnasema, “sasa, Ndugu Branham!” Jamani, maskini rinda hizo zenye kubana, yaonekana kama kwamba umemwagiliwa mle, kahaba wa barabarani.

Yesu alisema, “Kila mtu amtazamaye mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini naye moyoni mwake.” Basi hana budi kuhukumiwa kwa ajili ya hilo. Naye alifanyaje? Alijionyesha mwenyewe. Ni nani aliye na hatia? Wazia hilo.

MKATE WA KILA SIKU

…Watu watendao mambo ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa Mungu Wagalatia 5:21

23-0129

58-0326 Kuungana chini ya Kichwa kimoja

Unaweza kuwa umejazwa na rundo la kanuni za imani. Unaweza kuwa umejazwa na rundo la madhehebu. Lakini Mungu hataki ujazwe na hayo. Mungu aliweka mahali humo ndani pa kujiweka mwenyewe . Mungu anataka ujazwe na yeye mwenyewe.

Nini kinachotokea unapojazwa na Mungu? Unapojazwa na Mungu, unajazwa na Roho Mtakatifu, unajazwa na nguvu, unajazwa na upendo, furaha, amani, uvumilivu, wema, upole, utauwa, na kuabudu. Umejawa na furaha.

Daudi akasema, Kikombe changu kinafurika. Na kama Daudi alikuwa na kikombe kinachofurika kabla Roho Mtakatifu hajaja, ingekuwaje hivi sasa? Umejazwa kitu fulani .

MKATE WA KILA SIKU

Lakini mtu awaye yote asipokuwa na Roho wa Kristo, huyo si wake. Warumi 8:9

23-0128

64-0614M – Kufunuliwa Kwa Mungu

Neno Lake linafunuliwa kwa mmoja. Daima imekuwa hivyo, nabii alikuja na Neno la Bwana, kila kipindi cha wakati, kila wakati, kote katika Maandiko. Neno humjia mmoja. Katika kila wakati, vivyo hivyo, hata katika nyakati za kanisa, tangu wa kwanza hadi wa mwisho. Wengine wana mahali pao, hiyo ni kweli, angalia, lakini kaeni mbali na hiyo Nguzo ya Moto. Unaona?

Ni somo la jinsi gani tunalosoma hapa! Unaona, kila mtu akitaka kuwa Musa, na kila mtu…Mnakumbuka yale Dathani na hao wengine waliyosema kule njiani? Walisema, “Sasa, Musa, hebu ngoja hapa kidogo tu! Unajitukuza sana, unaona. Sasa, wapo watu wengine hapa ambao Mungu amewaita.”

Hiyo ni kweli. Wao, kila mmoja, walikuwa wakifuata vizuri mradi tu waliendelea mbele, lakini wakati mmoja alipojaribu kuinuka na kuchukua nafasi ya Mungu ambayo alikuwa amempa Musa, ambaye alikuwa amekusudiwa tangu zamani na kuchagulia kwa ajili ya kazi hiyo, alipojaribu kupachukua, moto ulishuka na ukaifunua nchi na kuwameza moja kwa moja ndani yake. Unaona? Unaona?

Kuwa mwangalifu. Unaona? Kuwa mwema tu, Mkristo wa Mungu mcha Mungu, ukiliamini Neno. Unaona? Kaa mbali na hiyo Nguzo. Ni somo la jinsi gani!

MKATE WA KILA SIKU

Kwake nitanena mdomo kwa mdomo,
Maana, waziwazi wala si kwa mafumbo;
Na umbo la BWANA yeye ataliona.
Mbona basi ninyi hamkuogopa
Kumnenea mtumishi wangu, huyo Musa?

Hesabu 12:8

23-0127

65-0725M – Watiwa Mafuta Katika Wakati Wa Mwisho

Roho Mtakatifu ndiye Nabii wa wakati huu; Yeye analihakikisha Neno Lake, akilithibitisha.

Roho Mtakatifu alikuwa ndiye Nabii wa wakati wa Musa.

Roho Mtakatifu alikuwa Nabii wa wakati wa Mikaya.

Roho Mtakatifu, aliyeliandika Neno, anakuja na kulithibitisha Neno.

Sasa ni nini kilitukia wakati wa Mikaya? Ahabu aliuawa, kisha mbwa wakairamba damu yake, kulingana na Neno la Mungu.

Enyi waalimu wa uongo nyote, ndivyo anavyosema Mungu, siku moja mtavuna mnayopanda, enyi viongozi vipofu wa vipofu! Sina hasira. Ninawaambieni tu Kweli.

Na nisingelisema jambo hili kama hapa, kwenye kile chumba, kama Roho Mtakatifu hakusema, “Liseme kwa njinsi hiyo.”

Je! nimepata kuwaambia jambo lo lote lisilo kweli ila lile Mungu alilothibitisha kuwa ni kweli? Amkeni, ndugu zangu, kabla ya kuchelewa sana!

MKATE WA KILA SIKU

Msidanganyike, Mungu hadhihakiwi; kwa kuwa cho chote apandacho mtu, ndicho atakachovuna. Wagalatia 6:7

23-0126

61-1224 – Mabwana, Sisi Tunataka Kumwona Yes

Kama ukimgusia mwanafunzi, “Ningependa kumjua Bwana Yesu.”

“Vema, sasa angalia, sisi ni wafuasi wa kanisa fulani-fulani, shuka ukaungane na hilo, uungane nasi.” Mnaona? Ama, “Tulikuwa…Sisi ni wanachama wa shirika fulani hili, basi njoo ukajiunge na hilo.” Na hayo ndiyo unayosikia.

Lakini Kristo Mwenyewe aliwaelekeza watu kwa mauti Yake, na akasema, “Punje ya ngano isipoanguka ardhini, inakaa peke yake.”

Loo, jinsi ilivyo tofauti! Naam, bwana. Jinsi ilivyo tofauti! Bali maisha yako na Uzima Wake hupatana, sio kanisani, sio katika jengo, sio katika kanuni ya imani, sio katika matendo mema, bali msalabani ambapo unasulubiwa pamoja na Yeye. Hapo ndipo unapompata Kristo.

Humpati Yeye kwa kufanya vema zaidi, kufungua ukurasa mpya. Kuanza maisha mapya, humpati Kristo. Unampata Kristo katika mauti pekee; sio katika hori, sio katika kuungama. Kuamini katika kanuni fulani za imani na hekaya, humpati Kristo huko.

Mtumishi wa kweli hukupeleka Kwake, na Yeye ni Neno.

MKATE WA KILA SIKU

Amin, amin, nawaambia, Chembe ya ngano isipoanguka katika nchi, ikafa, hukaa hali iyo hiyo peke yake; bali ikifa, hutoa mazao mengi. Yohana 12:24

23-0125

58-0126 – Msikieni Yeye

Ni kosa kwa mwanamke kukata nywele zake. Biblia ilisema hivyo. Naye anamwaibisha mumewe anapofanya jambo hilo . Na Kanisa lilikuwa halifanyi hivyo, lakini leo, kwa sababu mimbara ni dhaifu, wanafanya hivyo.

Na wanawake wanavaa nguo hizi ndogo ndogo zinazoonekana kama nguo za mwanamume, suruali, ama kitu fulani , wanavyoziita.

Je, unajua Biblia ilisema hayo ni uchafu na chukizo mbele za Mungu. Roho Mtakatifu anafikiri nini anapoleta jambo hilo mbele za Mungu Baba, jinsi binti za Kanisa wanavyofanya?

MKATE WA KILA SIKU

Lakini mwanamke akiwa na nywele ndefu ni fahari kwake. Kwa sababu amepewa zile nywele ndefu ili ziwe badala ya mavazi. 1 Wakorintho 11:15

23-0124

64-0125 – Washa Taa

Mng’ao ni nuru danganyifu.

Ni kama tu mazigazi barabarani. Tunashuka kwenda barabarani na kuona mazigazi. Ni picha ya bandia ya jua. Na unapofika pale, haijadhihirisha kitu ila kitu cha uongo. Kwa sababu, huwezi kutembea katika mmweko wa jua, kwa sababu ni mazigazi, daima yakikuonyesha kitu fulani ambacho ni uongo mtupu.

Na wakati watu wanapojaribu kukwambia ya kwamba Yesu Kristo si yeye yule jana, leo, na hata milele, wanakuongoza kukuingiza katika mazigazi. Hivyo tu.

Na wakati unapoingia katika kanisa na kujiunga na kanisa, kanuni fulani baridi ama kitu kama hicho, hakuna kitu hapo, si zaidi ya yale uliyokuwa nayo duniani.

Hebu nikwambie.

Usiikatae Nuru ya Injili ya Yesu Kristo, ambayo inaleta miali inayotia joto ya Roho Mtakatifu juu yako, inakufanya kiumbe kipya katika Kristo Yesu. Usijaribu kutembea katika mng’ao fulani wa wakati mwingine.

MKATE WA KILA SIKU

Hawa ni visima visivyo na maji, na mawingu yachukuliwayo na tufani, ambao weusi wa giza ni akiba waliyowekewa. 2 Petro 2:17

23-0123

62-0218 – Kung’ang’ania

Wasema, “Vema, Ndugu Branham, daktari aliniambia ya kwamba nilikuwa ninakufa. Nina kansa.” Huenda hilo likawa ni kweli. Huyo mtu anakwambia yote ajuayo. Lakini, jambo pekee analoweza kufanya, yeye yuna hisi tano za kufanyia kazi, mbili za hizo anaweza kuzitumia. Ni kitu gani?

Hisi moja ni ya kugusa, mahali hapo pengine ni—ni kuona. Kuona na kugusa, anaweza kugusa kitu fulani, ama kuona kitu fulani kwa eksi-rei. Hizo tu ndizo mtu huyo alizo nazo za kutumia. Hayo tu ndiyo ajuayo, bali anafanya vizuri awezavyo. Bali usiangalie hayo, yeye amefikia mwisho wake.

Angalia hapa juu yale Hili liliyoahidi! Useme, “Inaweza kutendwaje?” Mungu alisema hivyo. Hilo linatosha hapo Mungu alipolisema. Hilo linatosha, liko imara Milele daima Mbinguni, Neno Lake liko imara. Nayo Maneno Yake yalifanyika mwili, Nayo ni mwili leo hii ndani yako, kama utaliacha Hilo lifanyike mwili.

“Mkikaa ndani Yangu nayo Maneno Yangu yakae ndani yenu, basi ombeni mtakayo nayo yatafanywa,” Yohana Mtakatifu 15. Mnaona, tunataka tu kuyaacha Maneno hayo yakae humu ndani. Liaminini, ni la kweli. Ni mbegu, nayo ita—itatimiza kila kitu Yeye alichoahidi.

MKATE WA KILA SIKU

Mkiniomba neno lo lote kwa jina langu, nitalifanya. Yohana 14:14

23-0122

55-1118 – Ile Imani ya Ibrahimu

Naweza kuwasikia watakatifu wote wa Agano la Kale wakisema, “Inueni, enyi malango ya milele, inukeni, Mfalme wa Utukufu apate kuingia. Ninaweza kuwasikia Malaika wakiimba kutoka kule nyuma, “Ni nani huyu Mfalme wa Utukufu?” Wakasema, Bwana wa majeshi, hodari wa vita. Huyo ndiye , Mungu, Yehova-yire.

Malango yatafunguliwa vipi? Kitufe kilibonyezwa, na malango ya lulu yakafunguka; huyu hapa Yesu anakuja, ameteka mateka. Huyu hapa akishuka kama Mshindi, akishuka katika miji ya Mbingu mpya, na akaenda mbele za Baba, na kusema, “Baba, hawa hapa. Wote walikufa chini ya nia njema chini ya dhabihu ya mwana-kondoo, bali Ninawakabidhi kwako.”

” Vema. Panda hapa, uketi mkono Wangu wa kuume, kwa maana nitamtuma Roho Mtakatifu ashuke. Nawe uketi hapo mpaka kila adui awekwe chini ya miguu yako.” Utukufu kwa Mungu.

Tunamtazamia aje tena siku moja katika Utukufu. Na wale walio katika mavumbi ya ardhi watainuka na kubadilishwa kwa dakika moja katika kufumba na kufumbua, na kufanana naye …“Watamiliki malango ya adui.”

MKATE WA KILA SIKU

Inueni vichwa vyenu, enyi malango,
Naam, viinueni, enyi malango ya milele,
Mfalme wa utukufu apate kuingia.

Ni nani huyu Mfalme wa utukufu?
BWANA wa majeshi,
Yeye ndiye Mfalme wa utukufu.

Zaburi 24:9-10

23-0121

58-0209A – Msikieni Yeye

Katika mikataba yako ya biashara, neno lako ndicho kifungo chako; ushuhuda wako unapaswa kuwa wa kweli. Mungu aijaalie siku ile ambayo watu watakapokuwa kile walicho, kile wasemacho.

Kama nisingekuwa upande wa Kristo alasiri hii, ningekuwa kinyume chake. Ningekuwa nazunguka huko nikiaribu mambo. Bali ninamwamini, nami ni—niko tayari ku…hata kutoa maisha yangu kwa ajili Yake, kwa maana ninamwamini, ya kwamba ni kweli.

Na ikiwa Neno lake haliko sahihi , basi Yeye hayuko sahihi . Na ikiwa Neno Lake haliwezi kuaminiwa, Yeye hawezi kuaminiwa. Lakini nina furaha sana kujua ya kwamba mimi…Unaweza kuining’iniza nafsi yako kwenye Neno lolote fulani katika Biblia hiyo, na ni kweli; kila Neno Lake ni kweli. Mungu anaishi katika Neno lake.

MKATE WA KILA SIKU

BWANA ni mwema, ni ngome siku ya taabu; naye huwajua hao wamkimbiliao. Nahumu 1:7

23-0120

53-0613 – Njia ya Mungu Iliyoandaliwa

Sio—sio lazima kwamba mwanadamu yeyote Angeenda kuzimu. Na Mungu hampeleki mtu yeyote kuzimu. Unajipeleka mwenyewe kuzimu. Mungu amefanya kila kitu katika ulimwengu anachoweza ili kukuzuia wewe usiende kuzimu. Na bado, unaazimia kabisa kwenda kuzimu.

Unapambana kuvuka kila kizuizi ambacho Mungu anaweka njiani kukuzuia; wewe unakivuka tu moja kwa moja. “Siamini hili. Na siamini hilo. Na siamini hili.” ukiendelea tu…

Sasa, kuna taa nyekundu hapa jijini. Nazo hubadilika nyekundu na kijani. Hizo hukuambia wakati gani unaweza kusimama na kwenda. Ikiwa unapitiliza, vyema , usilaumu jiji. Wao Wameziweka hizo taa juu hapo kwa ulinzi wako. Lakini ikiwa utazipitiliza, hiyo ni juu yako. Ni wewe—wewe—umejiletea hukumu yako mwenyewe.

MKATE WA KILA SIKU

Mbele za BWANA, kwa maana anakuja,
Kwa maana anakuja aihukumu nchi.
Atauhukumu ulimwengu kwa haki,
Na mataifa kwa uaminifu wake.

Zaburi 96:13

23-0119

60-0609 – Msiogope

Hebu niwaambieni enyi watu wa kimadhehebu mlioko hapa, Wamethodisti, Wapresbiteri. Wakati watu hawa hapa wanajiita wenyewe Wapentekoste, hiyo haimaanishi kuwa ni dhehebu. Huwezi kuifanya Pentekoste dhehebu .

Unaweza kuwa na dhehebu, lakini Pentekoste ni tukio kwa ye yote atakaye na aje, awe ni Mbaptisti, Mpresbiteri, Mmethodisti, mweusi, manjano, kahawia, au mweupe. Haileti tofauti yoyote yeye ni wa rangi gani, ni mkubwa kiasi gani, ni mdogo jinsi gani, yuko chini kiasi gani, jinsi alivyo mbaya, haileti tofauti hata kidogo; ni kwa yeyote atakaye. Ni mchakato wa Utakaso wa Mungu kwa Kanisa Lake.

Si lazima uwe mwenye bongo; si lazima uwe uliyeelimika . Hakukuwa ila na mmoja tu katika kundi Lake lote aliyepata kuwa na elimu yo yote, na huyo alikuwa ni Paulo. Naye Paulo alisema ilimbidi kusahau kila kitu alichojua ili ampate Kristo. Mungu hajulikani kwa uwezo wa kiakili; Mungu anajulikana kwa tukio kupitia Roho Mtakatifu.

MKATE WA KILA SIKU

Kukaja ghafula toka mbinguni uvumi kama uvumi wa upepo wa nguvu ukienda kasi, ukaijaza nyumba yote waliyokuwa wameketi. Matendo 2:2

23-0118

55-0410S – Mteteaji Wangu Yu Hai

Sasa leo, wazia tu kwamba Uwepo Wake ukiwa hapa leo. Bwana Yesu yuko katika ulimwengu mwingine, ama kiwango kingine, papa hapa leo katika umbo la Roho. Roho wake anaunganika pamoja na roho zetu.

Macho yetu hayawezi kumwona, kwa sababu bado ni ya kimwili, isipokuwa kingetukia jambo fulani ambacho tungeweza kuona ono. Lakini Yeye yuko hapa anaonekana tu, halisi tu kama alivyokuwa siku ile alipozungumza na Mariamu, pale kaburini, ama Yeye alipokutana na Kleopa akiwa njiani Akienda Emau. Uwepo wake uko hapa.

Inaweza kuhisiwa na hilo, kuhisiwa na msukumo wa ndani uliyo ndani ya mwili wa mwanadamu, unaoitwa Kuzaliwa upya. Nafsi imekwishatiwa sumaku Kwake. Na mara tu, mnaporuhusu nia zenu ziwe juu Yake, kwa kumwamini; baada ya muda kidogo, Kitu fulani, uhalisia, unaweza kuhisi Kitu fulani kikipitia juu ya utu wako. Hilo ndilo thibitisho la kufufuka kwake.

MKATE WA KILA SIKU

Lakini, ikiwa Roho yake yeye aliyemfufua Yesu katika wafu anakaa ndani yenu, yeye aliyemfufua Kristo Yesu katika wafu ataihuisha na miili yenu iliyo katika hali ya kufa, kwa Roho wake anayekaa ndani yenu. Warumi 8:11

23-0117

61-0224 – Msiogope3

Sasa, kama ungemwendea Yeye, na Yeye alikuwa amevaa suti hii ambayo alinipa naye Angesema—ungesema, “Yesu, utaniponya?” Unajua angekuambia nini? “vema, mwanangu, nilikwishafanya jambo hilo.” Yeye Hawezi kulitenda tena.

Ikiwa umekombolewa kutoka kwenye duka la Rehani, unawezaje kukombolewa mara ya pili? Yeye Alikutoa . Alijeruhiwa kwa makosa yako na kwa kupigwa kwake Uliponywa. Unaona ninachomaanisha?

Uponyaji wako tayari umekamilika. Wokovu wako umekamilika. Kitu pekee unachopaswa kufanya ni kuupokea tu. Je, inaleta tofauti gani yeyote anayekuwekelea mikono, huyu anafanya nini, kile au kinginecho? Mahali popote ulipo, Liamini tu. Ni hayo tu. Lipokee. Ni Mungu apasaye kukupa wewe jambo hilo.

MKATE WA KILA SIKU

Yeye mwenyewe alizichukua dhambi zetu katika mwili wake juu ya mti, tukiwa wafu kwa mambo ya dhambi, tuwe hai kwa mambo ya haki; na kwa kupigwa kwake mliponywa. 1 Petro 2:24

23-0116

60-0522M – Kufanywa Wana Wenye Mamlaka #3

Baba wa kweli, kweli kabisa hatampiga mtoto wake anapojaribu kutembea, kama akianguka sakafuni. Huinama na mkono mkubwa wenye nguvu na kumwinua, anachukua mikono yote miwili na kumshika, kusema, “Hivi ndivyo unavyofanya jambo hilo, mwanangu. Tembea namna hii.”

Hivyo ndivyo Mungu anavyolifanya Kanisa Lake! Huinama na kumshika kwa mkono Wake, anamwinua na kusema, “Tembea namna hii, mwanangu. Angalia huku, usi—usi—usiliseme namna hiyo, namna Hii. Sasa, sijali linavyosema kanisa, kile huyu asemacho, kile yule asemacho, wewe liseme kama Hivi. Namna Hii, hili Ndilo!

Kama Neno Langu linalihubiri, wewe dumu nalo, enenda katika Hilo. Dumu nalo kabisa. Sijali analosema kila mtu, ling’ang’anie. Tembea namna Hii. Hivi ndivyo unavyopiga hatua zako.”

MKATE WA KILA SIKU

Ninyi, watoto wadogo, mwatokana na Mungu nanyi mmewashinda, kwa sababu yeye aliye ndani yenu ni mkuu kuliko yeye aliye katika dunia. 1 Yohana 4:4

23-0115

55-0817 – Yehova-Yire

Na ndugu yangu, ambaye tayari ametolewa katika Yesu Kristo, Mwana-Kondoo aliyechinjwa tangu kuwekwa misingi ya ulimwengu, ametolewa kwa ajili ya ugonjwa wako usiku wa leo .

Ameliandika hilo katika Kitabu. Amemtuma Roho Mtakatifu. Ameziweka karama katika Kanisa. Sasa, sio kosa la Mungu; itakuwa ni kutokuamini kwetu sisi wenyewe. Je! hiyo si ni kweli?

Tusipolipokea, sio kosa la Mungu. Je! unaamini hilo kwa moyo wako wote, kwamba Yesu Kristo ametolewa kama Mwana-Kondoo aliyechinjwa tangu kuwekwa misingi ya ulimwengu kwa ajili ya—kwa ajili ya wokovu wako na uponyaji.

Je, unaamini jambo hilo?
Inua mkono wako .

MKATE WA KILA SIKU

Hakuna aliye na upendo mwingi kuliko huu, wa mtu kuutoa uhai wake kwa ajili ya rafiki zake . Yohana 15:13

23-0114

50-0227 – Mungu Katika Watu Wake

Kuna chemchemi wazi iliyofunguliwa, inayotiririka bure kila mahali. Kunywa tu mpaka utosheke . Mti, kama ungekunywa tu kama yale ulivyogawiwa, mbona, ungekuwa tu daima, ungali kwenye ukame. Hiyo ndiyo shida ya Wakristo. Hawanywi vya kutosha. Unataka kunywa hadi ueneze tu na kuruhusu mtu mwingine aone jambo hilo . Unaona? Sukuma nje . Pata ushuhuda. Likabidhi kwa Mungu. Liamini . Simamia juu yake. Dai ahadi ya Mungu. Jitoe tu—likabidhi kwa Mungu. Liamini.

Umkabidhi Bwana njia zako. Atafanya yote unayotaka. Lakini Yeye hawezi kufanya jambo hilo mpaka…mradi tu umelishikilia. Kusema, “Sasa, nitaona ikiwa mimi ni mzima hata hivyo, na nione ikiwa hili litatenda kazi. Wewe likabidhi Kwake; sahau kuhusu hayo mengine. Nenda ukashuhudie mambo hata usioyaona. Unaliamini. Sio kile unachokiona; ni kile unachoamini. Si kile unachohisi.

Yeye kamwe Hakuwahi kusema, “unalihisi?” Alisema, “unaliamini?” Ndivyo unavyookolewa ni kwa imani. Ndivyo unavyoponywa ni kwa imani. Na imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo usiyoyaona, kuonja, kuhisi, kunusa, au kusikia. Wewe liamini tu. Litendee kazi kana kwamba ndivyo ilivyokuwa. Amina.

MKATE WA KILA SIKU

Umkabidhi BWANA njia yako,
Pia umtumaini, naye atafanya.

Zaburi 37:5

23-0113

60-0723 – Uambie Mwamba Nao Utatoa Maji Yake

Kanisa ni kiti cha hukumu, ambapo Mbingu ni Kiti kikuu cha Hukumu cha Mungu. Na vile visima vidogo vinawakilisha makanisa madogo yote nje, nayo hukumu uanzia katika nyumba ya Mungu. Unaona? Hapa ndipo hukumu uanzia.

Ndiyo maana…Sioni ni kwa nini wengi wanalalamika kwamba mimi huzungumza kwa bidii sana, na kujaribu kuwanyoosha watu, na kuwaambia jinsi wanavyoishi, jinsi wanavyovaa, na kuniambia ati naidhuru huduma yangu, wakati kiti cha hukumu ni nyumba ya Mungu. Hiyo ni kweli. Hapa ndipo inapopaswa kuanzia, papa hapa ambapo haki, na utauwa , na hukumu ya Mungu inapotokea kutoka mimbarani.

MKATE WA KILA SIKU

Kwa maana wakati umefika wa hukumu kuanza katika nyumba ya Mungu; na ikianza kwetu sisi, mwisho wao wasioitii injili ya Mungu utakuwaje? 1 Petro 4:17

23-0112

63-0804A – Mara Nyingine Tena

Tumepata nini, watu wa Kipentekoste leo hii? Kina Riki wengi kupita kiasi. Neno hilo, Elvis na Ricky, kamwe hukusikia kuhusu hilo katika siku zingine. Ni neno, ndilo jina kwa ajili ya siku hii. Huambatana na hili. Linamaanisha jambo fulani.

Unasema, “Jina halimaanishi chochote.” Basi ni kwa nini Yeye alibadilisha jina la Abramu, kuwa Ibrahimu? Ni kwa nini Yeye alibadilisha jina la Sauli kuwa Paulo? Jina la Simoni kuwa Petro? Ni kwa nini Yeye alibadilisha Jina Lake Mwenyewe?

Ni kwa nini Yeye alibadilisha Yakobo kuwa Israeli? Si mpaka alipopigana mwereka na Bwana, si mpaka aliposhinda. Basi wakati Yesu aliposhinda kifo, kuzimu na kaburi, Biblia ilisema, “Alikuwa na Jina jipya.” Pia wakati Yakobo aliposhinda.

Na iwapo Kanisa linaweza kushinda, ataacha kusema, “Mimi ni Mmethodisti, Mbaptisti, na Mpresbiteri.” Wakati anapoweza kushinda kanuni zake za imani na ulimwengu ambao umemvuta humo ndani, atarudi kuwa Bibi-arusi wa Yesu Kristo, Bibi Yesu Kristo. Amina.

MKATE WA KILA SIKU

Na tufurahi, tukashangilie, tukampe utukufu wake; kwa kuwa arusi ya Mwana-Kondoo imekuja, na mkewe amejiweka tayari. Ufunuo 19:7

23-0111

60-0329 – Ni Mimi, Msiogope

Mashua hiyo ndogo ilipokuwa ikienda mbio kuvuka ziwa. Haina budi kuwa karibu wakati huo ambapo Shetani aliinuka na kusema, “Loo, nimewashika peke yao bila Yeye. Sasa ni wakati wangu wa kuwafanya walipie jambo hilo, kwa kuwa walikuwa wakitoa pepo wangu na kadhalika. Kwa hivyo nawaadhibu leo kwa jambo hilo.” Hapo ndipo Shetani anapoweza kukuadhibu anapogundua kuwa umetoka bila Yesu.

Hapo ndipo Shetani anapolipata kanisa. Unapopendelea sana jambo lingine zaidi ya mikutano ya maombi, unapopendelea sana hata—kwamba unataka kuwa na ukuaji wa kimwili badala ya ukuaji wa kiroho, basi kumbuka, Shetani yuko njiani. Amekushika bila Yeye.

Ee Mungu, ni maombi yangu, liamshe kanisa tena kwenye mtindo wa kale, mikutano ya maombi ya usiku kucha. Waamshe watu kwenye ma—mazingira ya kiroho. Loo, i—inahitaji hilo kuwaleta watoto katika Ufalme. Inahitaji mazingira .

MKATE WA KILA SIKU

… maana pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya neno lo lote. Yohana 15:5

23-0110

61-0214 – Msingi Wa Ushirika

Lakini sasa, tunaona ya kwamba kile kinachomfanya mwanadamu kuwa na shauku ya ushirika ni kwa sababu wakati mmoja alikuwa na ushirika. Na ushirika wake ulikuwa pamoja na Mungu.

Mwanadamu siku hizi anajaribu awezavyo, haidhuru yeye ni nani, kama ni Mhindi; wakati tulipokuja hapa tulimkuta Mhindi akiabudu jua, akiabudi mti wa mizimu. Tukienda Afrika tunawakuta chini ya maskini sanamu ndogo na kadhalika. Kuna mahali fulani anapojaribu kupata njia yake ya kurudi, kwa sababu asili yake ilikuwa ni kufanya ushirika na Mungu. Hapo ndipo ilipotokea.

Yeye anajua ya kwamba alitoka mahali fulani nyuma ya pazia, naye anajaribu tu kuangalia nyuma kule kuona mahali alipotoka na mahali amefikia wakati akirudi. Hiyo ndiyo sababu mambo ya kimbinguni huvutia usikivu wa watu kwa nguvu sana ni kwa sababu wanadamu wanaangalia mahali walipotoka na ni njia gani wanayopitia.

Kuna Kitabu kimoja tu ulimwenguni kinachoweza kukwambia hivyo, hicho ni Biblia, kwamba wewe ni nani, mahali ulipotoka, na mahali unakoenda. Hiyo ni kweli kabisa; kinakwambia kikomo chako papa hapa katika Biblia na unakotoka na kwamba wewe ni nani.

MKATE WA KILA SIKU

Kila mmoja aliyeitwa kwa jina langu, niliyemwumba kwa ajili ya utukufu wangu; mimi nimemwumba, naam, mimi nimemfanya. Isaya 43:7

23-0109

Nilikuwa na msalaba mdogo ulioning’inia mbele ya motokaa yangu, na mtu fulani akaniambia, kasema, “Billy, unajua hiyo ni alama ya Kikatoliki?”

Nikasema, “Lini Wakatoliki walipata haki ya kutumia msalaba?” Hasha! Hiyo si alama ya imani ya Kikatoliki; hiyo ni alama ya imani ya Kikristo. Imani ya Kikatoliki ni maskini mtakatifu aliyekufa, ya Mariamu au—au mtu fulani aliyekufa ambaye wanamwabudu. Sisi hatuwaabudu watu waliokufa. Hatumwabudu Mtakatifu Cecelia na watakatifu hao wote mbalimbali. Huo ni Ukatoliki, ambao ni ibada ya hali ya juu ya mizimu. Bali msalaba unamwakilisha Yeye Ambaye alikufa na akafufuka tena.

Nami nikasema, “Nauweka huo hapo, nikiangalia barabarani. Miaka ishirini na mitano iliyopita, au thelathini, nilipokuwa karibu kipofu, nilimwahidi Mungu iwapo Yeye angeyaponya macho yangu ningetazama jambo lililo halali.” Kisha nikasema, “Kila mahali unapoangalia, ni uovu mwingi, wanawake nusu uchi, na wanawake walio uchi wamelala viwanjani na kila mahali. Naangalia msalaba badala ya kuangalia, nakumbuka ambalo Kristo alinitendea, kisha nalipa kisogo jambo hilo…ambalo ni la Ibilisi.” Haleluya!

MKATE WA KILA SIKU

Nimekuinulia macho yangu,
Wewe uketiye mbinguni .

Zaburi 123:1

23-0108

61-0122 – Kama Tai Ataharikishavyo Kiota Chake

Kama mtu akitoka…akasema, Ufalme wa Mungu…akatupa nyavu baharini. Na alipozitoa, alikuwa na kasa, samaki wa kamba, mijusi, na kila kitu kingine.” Akawavuta nje ufuoni. Hiyo ndiyo kazi ya mhubiri.

Hatujui yupi ni yupi. Baadhi yao ni samaki; baadhi yao ni mijusi; baadhi yao ni nyoka; baadhi yao ni samaki wa kamba . Tazama samaki wa kale wa kamba anapokuwa hapo. Mtu fulani anasema, “Utukufu, haleluya. Bwana asifiwe.” anasema, nundu, nundu, nundu, nundu, nundu, nundu. Siwezi kuamini hilo,” huyo moja kwa moja anarudi zake majini. Yule mzee nyoka anainua tu kichwa chake, kusema, “Nilifikiri nilikuwa kanisani, kumbe ni watakatifu wanaojiviringisha.” Na hapa huyo anaenda zake.

Alikuwa kitu gani? nyoka tangu mwanzo, samaki wa kamba tangu mwanzo . Bibi kizee buibui, mtupu, akirudi moja kwa moja kwenye shimo la matope tena, ametoka moja kwa moja, akivaa kaptura, akikata nywele zake. Naam, lakini…“Kama nguruwe aendavyo kwenye uchafu wake, na mbwa kwenye matapiko yake,” haya basi. Usikasirike; wewe tulia tu.

MKATE WA KILA SIKU

Kama vile mbwa arudiavyo matapiko yake;
Kadhalika mpumbavu afanya upumbavu tena.

Mithali 26:11

23-0107

54-0514 – Muhuri Ya Mungu

Vema, mlipata kuona mwana reli akipakia mabehewa? Yeye atatoka aende na ataweka kiasi fulani hapa, na kiasi fulani hapa. Mkaguzi anapita pale, anaangalia ndani; na iwapo hili limelegea kidogo, linatikisika, “La. Mimi sitalitia muhuri. Sina budi kulifungua na kulirudia tena.” Basi, atajaribu kulipakia tena; atakosea hili. Mkaguzi anapita pale, “Ni makosa. Fanya tena.”

Na hivyo ndivyo Mungu amekuwa akifanya na kanisa Lake kwa muda mrefu. Utapakiwa, nawe unaenda Mbinguni; unachukua kila kitu. Karata zako, a-ha, kila kitu kingine unachoweza kupakia kwenye kanisa, unajaribu kwenda nacho. Mungu anahukumu jambo hilo; huko tayari kwa kutiwa mhuri.

Lakini wakati Mungu anapomwona mtu, mwenye roho iliyopondeka, iliyovunjika, moyo mwaminifu, kwenye madhabahu, Mungu hufunga mlango wa ulimwengu kwake, na kumtia muhuri mle kwa ubatizo wa Roho Mtakatifu, na unadumu mpaka Yesu atakapokuja; si kutoka ufufuo mmoja hata mwingine, lakini, “hata siku ya ukombozi wako.”

MKATE WA KILA SIKU

Lakini msingi wa Mungu ulio imara umesimama, wenye muhuri hii,
Bwana awajua walio wake… 2 Timotheo 2:19

23-0106

61-0426 – Nabii Mikaya

Sasa, ilikuwa imepita muda mrefu tangu Eliya atoe unabii huu. Alikuwa ameenda Utukufuni kwa muda mrefu. Lakini ali—alitoa unabii huu, naye alijua ulikuwa utatimia.

Ndipo Mikaya akajua ya kwamba Eliya alikuwa mtu wa Mungu, na huyu hapa Mungu juu Mbinguni akifanya baraza huko juu jinsi ya kulitimiza neno la Eliya. Na kama una Neno la Bwana, nawe utanena Neno la Bwana, na usitilie shaka Neno la Bwana, Mungu atafanya mkutano wa baraza kufanya Neno lako litimie; kwa sababu si Neno lako; ni Neno Lake.

Ni Neno Lake, kama ni BWANA ASEMA HIVI, kama kweli ni BWANA ASEMA HIVI.

MKATE WA KILA SIKU

Mbingu na nchi zitapita; lakini maneno yangu hayatapita kamwe. Mathayo 24:35

23-0105

62-0722 – Utuonyeshe Baba Itatutosha

Sasa, mti hutakiwa kufanyaje? Unapoupanda, jambo pekee unalopaswa kufanya ni kuumwagilia maji, na kisha unapaswa kunywa maji; majani yamo ndani yake, matofaa yamo ndani yake, kile…kila kitu kiko humo ndani ya mti, lakini hauna budi kunywa, hauna budi kunywa zaidi ya sehemu yake. Na jinsi unapokunywa, unatoa , unatoa majani, unatoa maua, unatoa matofaa; bali ni lazima uendelee kunywa, kunywa, kunywa, ili kuyatoa hayo .

Na tunapochukua ahadi ya Mungu, tuidondoshe ndani ya mioyo yetu, tukiendelea kuitia maji kwa imani, na inaendelea kusukuma , kusukuma. Haleluya! Kristo anapopandwa moyoni, Roho Mtakatifu, jambo pekee tunalofanya ni kunywa katika Neno hili la Mungu, nalo linatoa wokovu, Linatoa uponyaji wa Kiungu, Linatoa utukufu, Linasukuma. Kila kitu tunachohitaji kimo tayari ndani yetu tunapopandwa ndani ya Kristo Yesu.

Hii hapa fasiri yangu kwake, kuhusu kuwa yale Maji: Yeye ndiye Chemchemi ya Uzima isiyokauka. Hutawahi kumuomba yeye sana. Wewe Kamwe huwezi kumwamini yeye kwa mambo makubwa , anafurahia wewe kumwamini yeye kwa mambo makubwa, huwezi kamwe kuzidisha.

MKATE WA KILA SIKU

Walakini ye yote atakayekunywa maji yale nitakayompa mimi hataona kiu milele; bali yale maji nitakayompa yatakuwa ndani yake chemchemi ya maji, yakibubujikia uzima wa milele. Yohana 4:14

23-0104

60-0302 – Tangu Wakati Huo

Mambo hubadilika wakati mwanadamu anapokutana na Mungu.

Mwanadamu hawezi kamwe kukutana na Mungu na kubali vile alivyokuwa . Utakuwa aidha mtu bora au mtu mbaya zaidi. Utakuwa bora zaidi, au mbaya zaidi baada ya wewe kukutana na Mungu. Inategemea unataka kufanya nini kuhusu jambo hilo. Lakini mwanadamu hawezi kamwe kukutana na Mungu na kubali kamwe vile alivyokuwa .

Vyovyote mtazamo wako ulivyo kumhusu Mungu, unaweka muhuri kikomo chako cha milele. Unaweza kuvuka mstari kati ya neema, rehema, na hukumu; na unapoikataa neema mara nyingi sana unaweza kujitenga milele kutoka Uwepo wa Mungu, au unaweza kumkubali na kuwa na Uzima wa Milele, na usife kamwe, bali ufufuliwe tena katika siku ya mwisho katika ule ufufuo mkuu.

MKATE WA KILA SIKU

Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu . Warumi 6:23

23-0103

55-0225 – Yesu Aliyetukuzwa

Tuna wito wa madhabahuni na kuwaleta watu kuizunguka madhabahu. Hayo ni ma—mapokeo mazuri ya kanisa, lakini katika wakati wa Biblia, “Wote waliomwamini Bwana…” walimkubali tu, popote pale alipokuwa. “Wote walioamini, waliokolewa. Hawakuwa na miito ya madhabahuni.

Hilo lilianzia Methodisti, karibu na kanisa la kwanza la Methodisti huja madhabahuni. Ni jambo jema. Hatupaswi kamwe kuliacha. Endeleeni nalo. Nadhani ni jambo jema. Kuja huko, kuumimina moyo wako mbele za Mungu. Hiyo ndiyo njia ya kufanya jambo hilo. Lakini kwa kweli, hilo silo linalokuokoa.

Unaweza kukaa hapo madhabahuni, na kuomba usiku kucha, kulia, kutembea huku na huku madhabahuni. Unaweza kufanya kila kitubio unachoweza. Unaweza kuuza kila kitu ulicho nacho na kuwapa maskini. Unaweza kuendelea na mfungo kwa siku arobaini na uchoke sana—hivyo kwa kufunga mpaka usiweze hata kutembea, na kamwe isikusaidie chochote, mpaka kwanza, ukubali…hilo ndilo. Ni sehemu yako.

Mungu alifanya sehemu yake. Sasa, wewe fanya sehemu yako, jambo rahisi tu la kuliamini hilo. Na unapoliamini, hilo linatatua jambo hilo milele.

MKATE WA KILA SIKU

Na kwa yeye kila amwaminiye huhesabiwa haki katika mambo yale yote asiyoweza kuhesabiwa haki kwa torati ya Musa. Matendo 13:39

23-0102

60-0911E – Vitambulisho Vitano Dhahiri Vya Kanisa La Kweli La Mungu Aliye Hai

Hivyo ndivyo Kanisa la Mungu aliye hai lilivyo siku hizi. Halijaunda dhehebu, kadiri mambo ya ulimwenguni yanavyohusika. Bali limeunganishwa pamoja, si kwa vifungo vya kimadhehebu, bali kwa nguvu na Roho wa Yesu Kristo, kwa vifungo vya upendo.

Inamfanya Mmethodisti na Mbaptisti kupigana kikofi cha mgongoni, na kusema, “Ndugu yangu mpenzi,” wakati wanapoona hawawezi kutembea pamoja wasipopatana. Watu husema, “Je! wewe ni Mkristo?”
“ Mimi ni Mbaptisti.” Hilo halijibu swali, hata kidogo. “Mimi ni Mkristo? Mimi ni Mpentekoste.” Hilo halijibu swali hilo.

Endapo wewe ni Mkristo, wewe ni kiumbe kilichozaliwa mara ya pili. Umo katika—katika Ufalme wa kisiri wa Mungu. Macho yako hayako kwenye mambo ya ulimwengu huu, bali kwenye mambo ya huko juu. Na hapo ni wakati uwapo katika Kanisa hilo. Hilo ndilo Kanisa. Si dhehebu. Kamwe haliwezi kuwa ni dhehebu.

Nishuhudieni hadharani. Kanisa la Mungu aliye hai haliwezi kamwe kuwa ni kundi lolote lile. Haliwezi kuwa ni dhehebu.

MKATE WA KILA SIKU

Na alipoulizwa na Mafarisayo, Ufalme wa Mungu utakuja lini? Aliwajibu akawaambia, ufalme wa Mungu hauji kwa kuuchunguza. Luka 17:20

23-0101

63-0707E – Ushirika

Naomba nilete jambo hilo: tunapohukumiwa kwa Neno, ambalo ni Kristo, tunarudiwa. Ikiwa tunafanya makosa, hatuishi kulingana na Neno hili, tunarudiwa na Bwana. Na Bwana anapoturudi maana yake ni “kutusahihisha” ili isije ikatupata hukumu pamoja na ulimwengu.

Sisi si wa ulimwengu. Sisi tu tofauti na ulimwengu, tunaishi maisha tofauti, maisha yaliyotengwa. Hatupaswi kamwe kuishi maisha ya ulimwengu na kuwa Mkristo. Tunapaswa kuishi ma-maisha masafi, maisha tofauti. Si, simaanishi, katika viwango hivyo vya kijamii, bali namaanisha tuishi maisha ya utakatifu wa kweli ili matunda ya Roho yaonekane ndani yetu: ya upole; na utu wema ; na saburi; uvumilivu; imani: tunda la Roho.

MKATE WA KILA SIKU

Maana yeye ambaye Bwana ampenda, humrudi,
Naye humpiga kila mwana amkubaliye.

Waebrania 12:6

22-1231

54-0103E – Maswali na Majibu #2

Pia, nataka kujua nini maana ya “yasiyo na maana.” “Yasiyo na maana—jiepushe na maneno yasiyo na maana, kwa kuwa wataendelea zaidi katika maovu.”

Sasa, jambo la kwanza ni “maneno yasiyo na maana kwa kuwa wataendelea.” Sasa, cho chote kilicho cha kale—kinaendelea tu kupayuka. Biblia ilisema—Yesu alisema, “Bali ‘ndiyo’ yetu iwe ‘ndiyo’ na ‘siyo’ yetu iwe ‘siyo’ kwa kuwa yazidiyo hayo yataleta dhambi. ”

Haiwapasi hata kufanya mizaha na kuchekeshana ninyi kwa ninyi. Mungu atakuhukumia kila neno lisilo maana unalonena. Mwajua hilo? Biblia ilisema kuwa itakupasa uhukumiwe kwa kila neno lisilo maana. Kwa hivyo yatupasa tuwe watu wa jinsi gani? Watu wanyofu, thabiti, wanaopendana, wakarimu, na wala si kundi la wapumbavu, kila mara kuendelea…

MKATE WA KILA SIKU

Jiepushe na maneno yasiyo na maana, ambayo si ya dini; kwa kuwa wataendelea zaidi katika maovu ,

2 Timotheo 2:16

22-1228

60-1204E – Ono La Patimo

Sasa nataka kuwaulizeni jambo lingine. Ni kitu gani kilicho kitamu zaidi kwa mtu aliyetia nanga, amelala huko chini ya mti usiokauka, kusikia kijito cha kiwimbi-wimbi?

Loo! Hilo ni Kanisa limeketi katika mahali pa mbinguni huku Sauti ya Mungu ikilia vizuri kama mawimbi na kuwazungumzia basi.

Mnaona ni kitu gani? Ni hukumu kwa mwenye dhambi, na baraka kwa aliyeokoka. Mtu ambaye ametia nanga salama mashua yake juu ya Mwamba Kristo Yesu, naye anakaa tu na kusikiliza, jinsi anavyoweza kustarehe! Kuingia katika raha hiyo.

MKATE WA KILA SIKU

Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha .

Mathayo 11:28

22-1227

63-0728 – Kristo Ni Siri Ya Mungu Iliyofunuliwa

Kuzaliwa upya ni Kristo, ni ufunuo. Mungu amekufunulia siri hii kuu, na huko ndiko Kuzaliwa upya. Sasa utafanya nini ukishakusanya kundi hilo lote Pamoja? ambapo ufunuo unapatana kikamilifu, na Mungu akiudhihirisha kupitia Neno Lake kwa matendo yale yale, mambo yale yale aliyofanya, akilidhihirisha Neno.

Laiti Kanisa lingejua mahali pake! Litajua, siku moja. Ndipo, Litaenda katika Kunyakuliwa wakati litakapojua ni kitu gani. Sasa angalia.

Unasema, “Ndugu Branham, lakini hiyo—hiyo sio…” Loo, naam, ni hivyo, pia. Ni Kweli .

MKATE WA KILA SIKU

Hata walipokwisha kumwomba Mungu, mahali pale walipokusanyika pakatikiswa, wote wakajaa Roho Mtakatifu, wakanena neno la Mungu kwa ujasiri.

Na jamii ya watu walioamini walikuwa na moyo mmoja na roho moja; wala hapana mmoja aliyesema ya kuwa kitu cho chote alicho nacho ni mali yake mwenyewe; bali walikuwa na vitu vyote shirika.

Matendo 4:31-32

22-1226

56-0715 – Alama Ya Mnyama

Sikiliza. Unaweza kuishi bila chakula kwa muda mrefu, lakini huwezi kuishi bila kunywa. Asilimia themanini ya mwili wako umetengenezwa kwa maji. Jambo la kwanza Mungu alilopata kukaa juu yake, Roho wa Mungu alilowahi kukaa juu yake, ilikuwa ni maji. Wala huwezi kuishi bila maji. Na ikiwa nafsi yako inaonea njaa kuabudu; sikiliza, bwana, Pentekoste, na Pilgrim Holiness, na Mpresbiteri, Mbaptisti, ye yote uliye. Unaona?

Ikiwa unaonea njaa, na unaonea kiu, ridhisha kiu yako kwa Kristo, na mfanye Kristo kuwa Mungu wako. Usigeuke na kunywa kutoka kwenye mabirika haya ya kale yaliyotuama. Jambo la kwanza wajua, unaweza kutenda kidini sana, lakini masikio yako yametiwa muhuri kutoisikia Kweli. Na je, unakumbuka?

“Watafanana sana hata itawapoteza walio wateule…” Na kukataa Injili, ni kutiwa muhuri kwa alama ya mnyama. Mungu anakutia alama.

MKATE WA KILA SIKU

Walakini ye yote atakayekunywa maji yale nitakayompa mimi hataona kiu milele; bali yale maji nitakayompa yatakuwa ndani yake chemchemi ya maji, yakibubujikia uzima wa milele.

Yohana 4:14

22-1225

56-0223 – Agano la Mungu pamoja na Ibrahimu na Uzao Wake

Basi, katika bustani ya Edeni palikuwa na miti miwili. Mmoja wao anasema, upande wa kuume, ulikuwa ni Mti wa Uzima; upande wa kushoto ulikuwa mti wa maarifa . Na mradi tu mtu anakula kutoka kwenye Mti wa Uzima ambao ni imani, anaishi. Lakini mego ya kwanza aliomega kwenye mti wa ujuzi, alijitenga na ushirika wake na Mungu. Unaliona hilo ?

Na angalia basi, katika kujitenga, yeye mara kwa mara anamega kutoka kwenye mti huo, akila kutoka kwenye mti huo. Ndipo anaileta mpaka anajaribu kuchanganya maarifa hayo na ushirika na Mungu. Na Mungu kamwe hakumfanya mtu kwa ujuzi wake amjue Yeye. Na maarifa yote tuliyo nayo kamwe hayatamwelewa Mungu. Mungu anajulikana kwa kipengele kimoja; hicho ni imani.

MKATE WA KILA SIKU

Walakini matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya usile, kwa maana siku utakapokula matunda ya mti huo utakufa hakika.

Mwanzo 2:17

22-1224

62-0719B – Uzima

Unaona, mfumo wa jua unadhibiti maisha ya mimea, jua, j-u-a. Na mara tu jua hilo lenye joto linapozunguka kutoka nyuma ya dunia, na kurejea hapa, kuna chembechembe ya uhai mahali fulani mle ndani ambayo hakuna mwanasayansi anayeweza kuipata, bali ua hilo dogo linaishi tena. Limetimiza kusudi lake, linaishi tena, kwa sababu ni uzima.

Vema, kama Mungu alitengeneza njia kwa mfumo wa jua kuinua tena uhai ambao ulimtumikia Yeye, vipi kuhusu M-w-a-n-a atakapokuja na Uzima wa Milele? Nasi tuna Uzima wa Milele, tutafufuka tena moja ya siku hizi. Hebu na tutumikie kusudi letu vyema , chochote tulicho, tulitumikie. Mahali popote Mungu amekuweka, hebu tuitumikie, kwa maana M-w-a-n-a atainuka moja ya siku hizi na uponyaji katika mbawa Zake. Ninataka kujitokeza wakati huo, katika mwangaza na utukufu wa kufufuka Kwake. Ninataka kutembea nimeshikana mikono na kila mmoja wenu, mbele ya Uwepo Wake.

MKATE WA KILA SIKU

Mtu akinitumikia, na anifuate; nami nilipo, ndipo na mtumishi wangu atakapokuwapo. Tena mtu akinitumikia, Baba atamheshimu.

Yohana 12:26

22-1223

63-0901M – Ile Ishara

Yeye hatatambua cho chote ila hilo Agano, la Roho Mtakatifu. Nawe hauwezi kupokea hilo Agano isipokuwa umeokolewa, ukatakaswa, kisha ukabatizwa kuwa katika ule Mwili. Yeye hawezi.

Huenda ukawa na maigizo, huenda ukajisikia vizuri, ukaruka juu chini, na kunena kwa lugha, na kucheza katika Roho. Hilo halihusiani nalo kamwe.

Sikizeni, katika Jina la Bwana! Mungu hatambui hayo. Makafiri hufanya hivyo. Wachawi hufanya hivyo.

Unasema, “Mimi ni mwanachuoni. Mimi hufanya hili, lile au lingine.” Yeye hajali wewe ni mwanachuoni namna gani. Shetani ndivyo alivyo, pia, waona .

Yeye hutambua tu I—Ishara. Huo ndio Ujumbe wa wakati huu! Huo ndio Ujumbe wa siku hizi! Huo ndio Ujumbe wa wakati huu! Katika Jina la Yesu Kristo, upokeeni!

MKATE WA KILA SIKU

Na ile damu itakuwa ishara kwenu katika zile nyumba mtakazokuwamo; nami nitakapoiona ile damu, nitapita juu yenu, lisiwapate pigo lo lote likawaharibu, nitakapoipiga nchi ya Misri.

Kutoka 12:13

22-1222

63-0115 – Kuikubali Njia Ya Mungu Iliyowekwa Katika Wakati Wa Mwisho

Hivi uliwahi kuona maskini kifaranga anapotoka kwenye ganda? Anacho cha ziada, maskini kidomo kwenye ganda lake, kikwaruzio kidogo cheupe. Naye jamaa huyo mdogo humo ndani, mara uhai unapoanza kuja, anaanza kukitikisa maskini kichwa chake. Huko kunafanya nini? Kikwaruzio hicho kidogo hulikwaruza hilo ganda, na kulifanya jembamba. Anapopata uhai mwingi zaidi kidogo, anaanza kugonga kwa kitu hicho kidogo. Basi akiisha kutoka kwenye ganda, hakihitaji tena, kwa hiyo kinaanguka tu chini.

Nacho kitu kinachosababisha hilo, ni kinga ya ncha ya kidomo chake. Isingalikuwa hivyo, angekuwa na kidomo kilichoumbuka, wala asingeweza kuidonoa nafaka yake. Loo, jamani!

Njia ya Mungu iliyowekwa ya kuishi! Mungu humwandaa, njia tu ya kutoka humo. Hakuna njia iliyo bora zaidi. Kitu kingine chochote kingemwua. Hana budi kupitia kwenye njia ya Mungu iliyowekwa. Sasa, kama ukijaribu kutengeneza njia nyingine ama kuwazia njia nyingine, utamwua.

Hiyo ndiyo shida ya kanisa la Kikristo siku hizi. Limejaribu kukubali njia fulani iliyotengenezwa, badala ya kupiga na kutoboa njia yake, kuingia kwenye Ufalme wa Mungu.

MKATE WA KILA SIKU

Mungu njia yake ni kamilifu;
Ahadi ya BWANA imehakikishwa;
Yeye ndiye ngao yao
Wote wanaomkimbilia.

2 Samweli 22:31

22-1221

53-0507 – Matarajio

Sikilizeni jambo hili enyi watoto. Neno la Mungu litamshinda Shetani popote, mahali popote, kwa hali yoyote, wakati wowote. Yesu alipokuwa hapa alikuwa Mungu. Mungu alikuwa ndani ya Kristo akiupatanisha ulimwengu kwa nafsi Yake, lakini hakutumia kamwe karama Zake zozote. Alipokutana na Shetani, aliushusha sana Ufalme wa Mungu, hata Mkristo aliye dhaifu sana anaweza kuutumia. Wakati Shetani alipomjia na kusema, “Ikiwa wewe ni Mwana wa Mungu, yaamuru mawe haya…” Alisema, “Imeandikwa.” Neno.

Akamchukua, akajaribu kumpigia Neno msasa . Na Yesu akasema, “Na pia imeandikwa.” Akampeleka juu ya kilele cha mlima, akasema, ilimbidi atazame falme hizi zote, “Nitakupa wewe hizo kama ukiniabudu.” Akasema, Imeandikwa. Hilo hapo.

Na imeandikwa, “Yo yote myaombayo mkisali, aminini kwamba mnayapokea; yatakuwa yenu .” Kisha mshinde Shetani kwa Neno la Mungu.

MKATE WA KILA SIKU

Amin, nawaambieni, Ye yote asiyeukubali ufalme wa Mungu kama mtoto mdogo hatauingia kabisa.

Marko 10:15

22-1220

62-0720 – Ushuhuda Baharini

Mungu alimfanya mwanadamu awe na kiu. Alipoufanya moyo wake, alimfanya awe na kiu kwa sababu alimfanya awe na kiu ya kumfuata. Na kuthubutu mtu ye yote kujaribu ku—kuridhisha kile kiu kitakatifu kwa mambo ya ulimwengu! Hilo liliwekwa ndani yako ili kumwonea kiu, “Kama ayala aioneavyo shauku mito ya maji, nafsi yangu inakuonea kiu, Ee Mungu.”

Siyo kwamba nina hasira na Kanisa, ninalipenda Kanisa. Nami ninajua ya kwamba—kwamba jambo fulani liko karibu kutukia. Na ndiyo maana nasema, “Jitayarisheni, enyi watu. Huwezi kufanya mambo hayo, mwonekano wako wa nje unaonyesha kazi ya neema humo ndani haijafanyika bado.”

Haidhuru ulipaza sauti kiasi gani, ulinena kwa lugha kiasi gani, ulicheza katika Roho, cho chote ambacho huenda ungeita misisimko yako, isipokuwa maisha hayo yakubiliane na Neno hili… Nawe Unasikia Neno hilo kisha ulipe kisogo? Kuna kitu fulani kasoro . Roho Mtakatifu ndani yako daima ataliitikia Neno kwa, “Amina. Ni kweli.” Unaona? Hiyo ni kweli

MKATE WA KILA SIKU

Yesu akawaambia, Mimi ndimi chakula cha uzima; yeye ajaye kwangu hataona njaa kabisa, naye aniaminiye hataona kiu kamwe.

    Yohana 6:35

22-1219

62-0128A – Kitendawili

Inashangaza kwamba Yeye alichagua kundi la watu wasio na elimu, na kuwatuma kule juu wakiwa na agizo kwenye Pentekoste—si kwenda kwenye seminari fulani, bali kungoja mpaka walipovikwa uwezo utokao juu.

Kama mtu huyo Petro, na Yohana na hao wengine, walitaka kuhubiri nao walikuwa wajinga na wasio na elimu, inaonekana kama Yeye angesema, “Vijana, kuna shule nzuri papa hapa. Enendeni hadi mjifunze ABC zenu. Kisha baada ya ninyi kufanya jambo hilo, mtachukua shule yenu ya sarufi. Pateni yote, pitieni hayo vizuri kabisa . Kisha mtachukua miaka minne ya shule ya upili, kisha miaka minne ya chuo kikuu, na kisha miaka minne au mitano hivi ya chuo cha Biblia. Kisha mnaweza kutoka kwenda.”

Lakini yeye alisema, Kaeni katika mji wa Yerusalemu, kwa maana nitawaletea juu yenu ahadi ya Baba yangu. Nanyi mtakuwa mashahidi Wangu (Luka 24:49), mashahidi Wangu katika Yerusalemu, Uyahudi, Samaria, na hata mwisho wa nchi. Hicho bado ni kigezo chake.

MKATE WA KILA SIKU

Luka 24:49

Na tazama, nawaletea juu yenu ahadi ya Baba yangu; lakini kaeni humu mjini, hata mvikwe uwezo utokao juu.

22-1218

60-0723 – Uambie Mwamba Nao Utatoa Maji Yake

Walikuwa njiani mwao wakitembea wakati huo, wakitoka, kulikuwa na Nguzo ya Moto mbele yao, nao wakasonga mbele hadi kwenye Bahari ya Shamu. Na walipofika pale, moja kwa moja wakiwa katika wajibu wao kizuizi kikainuka. Na jambo la kwanza unajua, hofu iliwashika, nao hawakujua la kufanya. Hivyo ndivyo watu wanavyofanya leo hii.

Hofu inapowapata wanapokuwa moja kwa moja katika mkondo wa wajibu wao…Sikilizeni, ndugu, hebu niseme hivi: Ikiwa unatembea katika nuru, ukiwa na ushirika na Mungu, na watu wake, na Roho Mtakatifu yuko juu yako. , na unakutana na kizuizi moja kwa moja katika wajibu wako, usisimame, endelea tu kusonga mbele . Mungu atafanya njia ya kupita jambo hilo.

Hilo ni mojawapo ya uzoefu mkuu sana katika maisha yangu, ni kumuona Mungu. Wakati siwezi kulivuka, kupita chini yake, kulizunguka kando , au vyovyote vile, Mungu hufungua njia nami hulivuka. Kwa namna fulani au nyingine neema yake inatosha kutuvusha katika jambo hilo.

MKATE WA KILA SIKU

Hayo nimewaambieni mpate kuwa na amani ndani yangu. Ulimwenguni mnayo dhiki; lakini jipeni moyo; mimi nimeushinda ulimwengu.

Yohana 16:33

22-1217

58-1004 – Imani Ndiyo Ushindi Wetu

Sasa hebu chukua kijito, kama kijito cha maisha, na mbao nyingi sana zinazopwelewa zikining’inia kwenye kila lundo la takataka. Na, hata hivyo, mashua inakuja, iliyotengenezwa kwa mbao, pia.

Lakini ukiangalia, hizo mbao zimetengenezwa na kuchongwa na bingwa ambaye ameijenga hiyo mashua. Si kwamba tu imechongwa, bali inaongozwa na nahodha, na inasukumwa na nguvu fulani.

Na sote tumeumbwa kwa vitu vile vile. Inategemea tu kule shauku yako imeelekezwa. Je, uko tayari kuruhusu Fundi mkuu atengeneze, kutoka kwako, kile ambacho angeweza kutumia, na kile ambacho angeweza kudhibiti, na kile ambacho angeweza kutia nguvu?

MKATE WA KILA SIKU

Lakini sasa, Ee BWANA, wewe u baba yetu; sisi tu udongo, nawe u mfinyanzi wetu; sisi sote tu kazi ya mikono yako.

Isaya 64:8

22-1216

63-1114 – Ushawishi

Jambo ni kwamba, watu, ndugu yangu, dada, na marafiki, ni kutambua udogo wako. Unaona? Usione jinsi ulivyo mkubwa. Tambua jinsi ulivyo mdogo. Wewe ni—wewe ni mdogo. Sote tuko hivyo. Mungu anaweza kufanya bila ya sisi, bali sisi hatuwezi bila Yeye. Unaona? Unaona? Sisi, sisi hatuwezi bila Yeye, lakini Yeye anaweza bila ya sisi.

Mungu anajaribu tu kumpata mtu mmoja ambaye Yeye anaweza kumshika mikononi Mwake. Daima amejaribu kufanya hivyo. Unatambua, kote katika Biblia, wakati Yeye alipompata Isaya, wakati Yeye alipompata Yeremia. Na Yeye alimpata—Yeye alimpata Samsoni, siku moja; bali Samsoni alimpatia Mungu nguvu zake, lakini akampa Delila moyo wake. Unaona, yeye…

Inakubidi kutoa yote uliyo nayo kwa Mungu; kicho chako, heshima zako, kila kitu ulicho wewe. Usiwe chochote, uone tu jinsi ulivyo mdogo, na hilo ndilo Mungu anatutaka tufanye.

MKATE WA KILA SIKU

Maana sijui sababu ya kujishitaki nafsi yangu, lakini sihesabiwi haki kwa ajili hiyo; ila anihukumuye mimi ni Bwana.

1 Wakorintho 4:4

22-1215

57-0915E – Waebrania, Mlango Wa Saba #1

Kama nikizurura na wanawake kila siku, na kisha nirudi nyumbani, nimwambie mke wangu kwamba nilimpenda, yeye angejua kwamba mimi nilikuwa mwongo. Matendo yangu yangenena kwa sauti kubwa zaidi kuliko maneno yangu. Hakika. Ninamthibitishia ya kwamba sikumpenda, kwa sababu sikuwa mwaminifu kwake.

Kama angaliniambia ananipenda, na kila wakati nikiwa sipo, angetoka na mwanamume mwingine, ingethibitisha ya kwamba hakunipenda. Kweli. Matendo yake yanathibitisha jambo hilo. Sijali angejaribu kuniambia kiasi gani, “Bill, ninakupenda, wala hakuna mtu mwingine duniani ila wewe,” ningejua alikuwa mwongo.

Na unapojaribu kusema, “Bwana, ninakupenda,” na unaishi katika mambo ya ulimwengu, Mungu anajua kwanza kabisa, wewe ni mwongo. Kwa hiyo ni kwa nini? Ya nini kukubali tukio la nusu-nusu, na kitu kingine kama hicho, wakati anga kuu za Mbinguni zimejaa jambo lililo halisi? Kwa nini unataka kuwa Mkristo mnyonge, wa kujifanya, nusu-nusu, usiye na busara?

Wakati, unaweza kuwa mtoto halisi wa Mungu aliyezaliwa mara ya pili, huku kengele za furaha za Mbinguni zikilia moyoni mwako, ukifurahi, na kumsifu Mungu, na ukiishi maisha ya ushindi kwa Yesu Kristo.

Sio kujaribu kufanya jambo hilo wewe mwenyewe, kwa sababu utashindwa, kwanza. Lakini mchukue Yeye, ni swala la Neno Lake, na utulie kwenye yale aliyosema yalikuwa ni Kweli. Na umwamini, na umpende, Naye atafanya kila kitu kifanyike kinaganaga vizuri kwako. Jambo ndilo hilo. Wazo ndilo hilo.

MKATE WA KILA SIKU

Afadhali maskini aendaye katika unyofu wake,
Kuliko mpotofu wa njia angawa ni tajiri.

Mithali 28:6

22-1214

57-0818 – Kumbukumbu za wakati za Mungu zilizojaribiwa

Naamini, moja ya siku hizi wakati lile Kanisa kuu…

Wakati, sayansi inaposema, “Inawezaje kuachia? Nguvu ya uvutano inakushikilia duniani.”

Sasa najisikia wa kidini. Hebu nikuambie. Kanisa hilo la wakati lililojaribiwa litakuja kuwepo siku moja. Kunaweza kuwa na nusu yao wamelala katika mavumbi ya ardhi. Sijui walipo, lakini Mungu amevijaribu vitu vyake vyote.

Siku moja Anakuja kukaa mstari wa mbele: “Nifuateni!” Moja kwa moja kupitia angahewa na anga za juu, na sayari na sayari, hadi kwenye Uwepo wa Mwenyezi Mungu Ataenda, pamoja na Kanisa la wakati lililojaribiwa .

MKATE WA KILA SIKU

Umenijaribu moyo wangu, umenijilia usiku,
Umenihakikisha usione neno; Nimenuia kinywa changu kisikose.

Zaburi 17:3

22-1213

Siku zote nilimhurumia kuku wa kiangulio. Kuku aliyezaliwa ndani ya kiangulio, analia, na hana mama wa kumwendea. Hilo linaniweka katika mawazo ya mhubiri wa seminari ambaye hajui zaidi kuhusu Neno la Mungu kuliko vile seminari ilivyosema; hulia, na hamna Mama wa kumwendea

Lakini unapozaliwa kweli chini ya mbawa za neema na nguvu Zake, utakubaliana na kila Neno alilosema, ni Kweli. Na wakati Mungu anaposonga katika mambo ya kimbinguni, moyo wako utakuwa na njaa moja kwa moja Kwake.

Hutashuka kando na kusema, “Telepathia ya kiakili! Shetani! Beelzebuli! Siamini Hilo. Kanisa langu halifundishi Jambo Hilo.”

Utasema, “Mungu asifiwe milele,” kwa maana umejazwa .

MKATE WA KILA SIKU

Kwa manyoya yake atakufunika,
Chini ya mbawa zake utapata kimbilio ;
Uaminifu wake ni ngao na kigao .

Zaburi 91:4

22-1212

50-0819 – Utuonyeshe Baba Inatosha

Yesu alikuwa na sifa zote nzuri za Mungu ndani Yake. Je, unaamini jambo hilo ? Alikuwa na mamlaka juu ya mamlaka. Lakini alipokutana na Shetani, Yeye kamwe hakutumia nguvu Zake. Anatoa mfano kwa Wakristo walio dhaifu zaidi. Alipokutana na Shetani, Yeye alisema, “Imeandikwa. Mtu hataishi kwa mkate tu, bali kwa kila Neno litokalo katika kinywa cha Mungu.” Mkristo dhaifu zaidi anaweza kuchukua msimamo huo. Lishikilie. Hakika, Mungu yu katika Neno Lake.

Kila wakati alipokutana na adui, alisema: Imeandikwa. Ninaamini alikuwa na uwezo wa kufanya jambo hilo. Lakini alikutana na Shetani kwenye misingi ile ile na Neno lile lile unaloweza kukutana naye kwalo, kila mmoja, “Imeandikwa.” mnaamini jambo hilo? Kwa nini, imeandikwa.

“Yo yote myaombayo mkisali, aminini ya kwamba mnayapokea.” Angalia mpangilio wa Neno. Amini sasa hivi (wakati uliopo) unalipokea, nawe utalipata . Utapewa jambo hilo baadaye, lakini liamini sasa hivi.

MKATE WA KILA SIKU

Kwa ajili ya hayo BWANA atangoja, ili awaonee huruma, na kwa ajili ya hayo atatukuzwa, ili awarehemu; kwa maana BWANA ni Mungu wa hukumu; heri wote wamngojao.

Isaya 30:18

22-1211

60-0608 – Kuwa na Makongamano

Na sasa, kuna mafundisho mengi tofauti na mambo leo hii, nyoka wenye ndimi laini, mpaka wanaweza kuelezea mambo yote kutoka katika Biblia, kuyaweka kando katika siku nyingine. Nyoka, wala siombi radhi hata kidogo kwa jambo hilo . Hivyo ndivyo ilivyokuwa hasa.

Mgongo wenye Mafuta, anayeng’aa kote, aliyenakshiwa kwa nywele zilizotiwa mawimbi na mwenye kuvalia suti nzuri; hivyo ndivyo shetani anavyoonekana. Yeye si mzee john Barleycorn, mwenye whiski ikitoka kinywani mwake; yeye ni shetani aliyenakshiwa siku hizi, nakuambia.

Biblia ilisema kwamba “Yeye alikuwa mjanja sana hata angewadanganya walio wateule kama yamkini.” Hiyo ni kweli . Loo, yeye ni mwanafunzi wa Biblia, mwanachuoni. Alipokutana na Yesu, alimnukulia Maandiko moja baada ya nyingine. Yesu alisema, “Lakini pia imeandikwa…” Amina? Alikuwa ni jamaa fulani.

MKATE WA KILA SIKU

Lakini nachelea; kama yule nyoka alivyomdanganya Hawa kwa hila yake, asije akawaharibu fikira zenu, mkauacha unyofu na usafi kwa Kristo.

2 Wakorintho 11:3

22-1210

53-0508 – Mungu Akimpa Musa agizo

Mtu fulani hivi majuzi, akifundisha, alisema, akinena juu ya Apolo, juu kule, yule mhubiri mzuri wa Kibaptisti. Paulo alimwendea akasema, “Loo, ndiyo, wewe ni mtu mzuri, lakini je, ulimpokea Roho Mtakatifu tangu ulipoamini?”

Akasema, Loo, loo, nili—nilifikiri nilimpokea Roho Mtakatifu wakati nilipoamini. Bado wanafundisha hivyo, lakini ni makosa. Imani ni sawa. Imani ni nzuri sana. Imani ina…Ibrahimu alimwamini Mungu, nayo ikahesabiwa kwake na, au, kuwa haki, lakini Mungu akampa muhuri wa tohara kuwa muhuri wa imani yake.

Ndugu zanguni, unapokuwa na imani halisi na ya kweli katika Mungu, Mungu atakupa ubatizo wa Roho Mtakatifu kama muhuri wa ahadi, ambao ni muhuri, kwamba una imani. Unaweza kufanya—a—aina fulani ya stuko, ama kuwafanya watu waamini, ama unaweza kusema una imani, lakini unapokuwa na imani halisi isiyoghoshiwa, Mungu atakupa ubatizo wa Roho Mtakatifu kama muhuri wa ahadi. Amina. Hayo si maziwa ya mtindi sasa, enyi watoto.

Sasa kumbuka, lichukue, liamini. Weka imani yako na uiachie kule na Mungu, na Roho Mtakatifu atakuja juu yako. Aliahidi hilo. Kisha , ndugu, Ibilisi anaonekana kama jamaa mdogo.

MKATE WA KILA SIKU

Naye aliipokea dalili hii ya kutahiriwa, muhuri ya ile haki ya imani aliyokuwa nayo kabla hajatahiriwa; apate kuwa baba yao wote waaminio, ijapokuwa hawakutahiriwa, ili na wao pia wahesabiwe haki.

Warumi 4:11

22-1209

64-0125 – Washa Taa

Na leo kuna Mti wa Bibi-arusi; ulianza huko nyuma hapo mwanzo, huko nyuma kabisa katika Siku ya Pentekoste.

Sikilizeni, ninyi watu ambao ni washiriki wa kanisa! Kanisa kamwe halikuanzia huko Nikea, Rumi. Lilianzia huko Yerusalemu, kwenye Siku ya Pentekoste, kanisa lilianza. Ndipo walifanya nini? Waliendelea tu kuunda madhehebu; na Mungu anaendelea kukata matawi. Ndipo wakaunda la Kilutheri; akakata matawi. Wesley; akakata matawi. Pentekoste; akakata matawi. Mpaka imefikia …

Lakini Mungu atakuwa na Mti wa Bibi-arusi! “Yote yaliyoliwa na parare na madumadu wamekula, nitayarudisha,” asema Bwana. Malaki 4 inatwambia tutarudishwa kwenye Imani ya mwanzoni kama ilivyokuwa kwenye Siku ya Pentekoste, “Imani ya baba.” Tunaamini kwamba itakuja. Ninaamini wakati wake umewadia sasa. Matawi yamenyauka na kukauka.

MKATE WA KILA SIKU

Na asubuhi, mwasema, Leo kutakuwa na dhoruba; kwa maana mbingu ni nyekundu, tena kumetanda. Enyi wanafiki, mwajua kuutambua uso wa mbingu; lakini, je! Ishara za zamani hizi hamwezi kuzitambua?

Mathayo 16:3

22-1208

61-1231M – Huna Budi Kuzaliwa Mara Ya Pili

Sasa, ninyi watu mnaozungumza kuhusu kumpokea Roho Mtakatifu na jinsi inawabidi kungoja kwa muda mrefu sana, hili hapa. Mpaka Mungu atakapoipokea dhabihu hiyo, mpaka iwekwe juu ya hukumu Zake pale, mpaka hukumu Yake imeua hisi zako! Unaweza kusema, “Vema, nitafungua ukurasa mpya.” Hilo silo. “Vema, najua nilikuwa nikivuta sigara, nitaacha kuvuta sigara.” Hilo bado silo. Mpaka Mungu atakapoipokea dhabihu hiyo kwenye madhabahu yake ya shaba, madhabahu yake ni hukumu. Hukumu yake ni ipi? Kifo. Hiyo ndiyo adhabu.

“Roho itendayo dhambi,” inadumu katika hiyo, “itakufa.” sijali ulichofanya.

Yesu alisema, “Wengi watakuja Kwangu katika siku hiyo, na kusema, ‘Bwana, hatukutenda hili na lile? Anasema , ” ondokeni Kwangu Ninyi Mtendao Maovu.” unaona?

Wakati dhabihu hiyo inapokelewa kwa moto, na kupaa juu namna hiyo, na moshi ukipanda juu, unapanda pamoja na dhabihu yako kwenda mbinguni, na unatiwa muhuri kutoka kwa mambo ya ulimwengu basi. Nafsi zetu ziko juu ya madhabahu yake.

MKATE WA KILA SIKU

Usistaajabu kwa kuwa nilikuambia, Hamna budi kuzaliwa mara ya pili.

Yohana 3:7

22-1207

57-0126B – Ripoti ya Safari ya India

Lakini nina matumaini bora kwenu ninyi ndugu hapa asubuhi ya leo, ya kwamba mtakuwa watumishi wa Mungu mnaodumu na Neno la Mungu. acha kila kitu kingine kianguke kulia na kushoto, bali dumu moja kwa moja na hilo Neno. Usisogee. Haijalishi kama wewe ni kanyagio la mlangoni nje hapo, wewe kuwa kanyagio bora la mlangoni. Usijaribu kushindana na mtu mwingine au kufanya hivi. Ingia tu moja kwa moja katika Neno, na udumu papo hapo, naye Mungu atakuweka mahali pako katika Ufalme Wake, ambapo unaweza kuwa bora zaidi.

Inakuaje ikiwa kidole changu kingepata wazo, kwa sababu hakikuwa jicho, hakitakuwa kidole tena? Ningechukia kupoteza kidole hicho. Ingaweje jicho langu linaweza kuwa la thamani zaidi, lakini ninakipenda kidole hicho. Ni sehemu yangu. Mnaelewa ninachomaanisha? Nina hakika mnaelewa.

Kwa hivyo ofisi yoyote, chochote kile kiwezacho kuwa, kuwa kile ulicho. Na mahali pako ambapo Mungu amekuweka, kaa hapo na uwe mwaminifu kwa Neno hilo jinsi unavyojua kuwa. Mungu atabariki jambo hilo . Akichukua dhana ya kitu kingine, Yeye atakuweka mahali pale anapohitaji.

MKATE WA KILA SIKU

Lakini kama vyote vingekuwa kiungo kimoja, mwili ungekuwa wapi?

Na jicho haliwezi kuuambia mkono, Sina haja na wewe; wala tena kichwa hakiwezi kuiambia miguu, Sina haja na ninyi.

1 Wakorintho 12:19,21

22-1206

61-0428 – Kuingia Katika Roho

Sijali ikiwa mtu huyo amekosea. Kama yeye yuko makosani na mwaminifu moyoni mwake na wewe uko sahihi katika imani yako na—na uko makosani katika—kutenda jinsi unavyotenda. Ningependa kuwa katika nafasi yake kuliko kuwa katika yako. Hiyo ni kweli.

Ni afadhali niwe nimekosea katika mafundisho yangu na niwe sahihi moyoni mwangu. Mungu ataliheshimu jambo hilo zaidi. Kwa hivyo ikiwa mtu yuko makosani, iweje ? Msaidie. Anahitaji msaada. Mpende. Ikiwa huwezi kumpenda adui yako kama vile unavyowapenda wale wanaokupenda, wewe si bora kuliko watoza ushuru. Hiyo ni kweli.

Hicho ndicho Kanisa limeshindwa kukipata. Natumaini utakipata usiku wa leo. Natumaini mtaona ninachozungumzia.

Nikurudi kwenye upendo, upendo wa ukombozi. Mambo mengine yote ni sawa, lakini hatuna budi kurudi kwenye ushirika wa mmoja kwa mwingine . Na watu walisema ninapinga mashirika. mimi siyapinga. Napinga huo mfumo uliomo humo ndani unaovunja undugu. Siku zote nimefanya hivyo . Na nitafanya hivyo kila wakati. Hiyo ni kweli.

MKATE WA KILA SIKU

Lakini mimi nawaambia, Wapendeni adui zenu, waombeeni wanaowaudhi.

Mathayo 5:44

22-1205

62-0607 – Kuzivaa Silaha Zote za Mungu

Kwa hiyo tunamjua adui yetu kwa mashambulizi yake. Labda hukulipata tu sawasawa, jinsi nilivyosema jambo hilo . Tunamjua adui yetu: Wakati mtu yeyote, roho yoyote, mtu yeyote anapojaribu kutokubaliana na Neno la Mungu, kumbuka, huyo ndiye adui yako, huyo ndiye adui yako. Tunajua mashambulizi yake ya kale , hilo ndilo alilovunjia jamii ya wanadamu, na hivyo ndivyo anavyoivunja hata leo, na hivyo ndivyo anavyokuweka mbali na Mungu, ni kutoliamini Neno Lake.

Na njia pekee ya kuweza kukaa katika ushirika na Mungu, na kuongea Naye wakati wa jua kutua, ni kukaa umeimarishwa katika Neno pande zote mbili, acha pazia la Neno la Mungu likufunike pande zote, nawe ushushwe moja kwa moja katikati Yake. Hiyo ni kweli. Ndipo umeimarishwa. Utukufu!

MKATE WA KILA SIKU

Vaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kuzipinga hila za Shetani.

Waefeso 6:11

22-1203

53-1205 – Ufufuo

Hakuna kitu kama imani ya mitume. Kama kuna kanuni ya imani ya mitume katika Biblia, inapatikana katika Matendo ambapo Yeye alisema, “Tubuni kila mmoja wenu, mkabatizwe katika Jina la Yesu Kristo mpate ondoleo la dhambi zenu. Nanyi Mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu kwa kuwa ahadi hii ni kwa ajili yenu, na watoto wa watoto wenu, kwa hao walio mbali, na wote watakaoitwa na Bwana Mungu wetu wamjie.”

Hilo linasikika zaidi kama imani ya mitume, sivyo, “Naamini katika Kanisa takatifu la Kirumi. Naamini katika ushirika wa watakatifu.” Yeyote anayeamini katika ushirika wa watakatifu ni mwabudu mizimu. Hiyo ni kweli kabisa.

Watakatifu wamekufa; wako katika Uwepo wa Mungu. Hakuna mpatanishi kati ya Mungu na mwanadamu ila Yesu Kristo. Amina. Hiyo ni kweli. Loo, jinsi mnavyojipotosha. Jamani, ni aibu…

Ona, sitaki kuwalaumu ninyi watu; ni mimbarani ndipo ilipoanzia. Si ajabu hiyo ndiyo hukumu ya nchi, wakati Shetani alipoingia mimbarani. Ni ukweli. Kushindwa kuhubiri Neno la Mungu lisiloghoshiwa, nalo Neno la Mungu litazaa yale ambayo lilisema lingefanya.

MKATE WA KILA SIKU

Wanakiri ya kwamba wanamjua Mungu, bali kwa matendo yao wanamkana; ni wenye machukizo, waasi, wala kwa kila tendo jema hawafai .

Tito 1:16

22-1202

56-0129 – Ya Kimbinguni

Na ni mazingira yanayoleta miujiza, na maajabu, na nguvu za Mungu kati ya watu. Ni hali ya watu. Na watu wanapofika mahali wanajadiliana, na kustaajabu, na kuzozana, na kuwaza, na wote wamegawanyika, na hawajui wanasimama wapi, nusu yao hata hawajafundishwa Maandiko, unawezaje kutarajia hali kuwa sawa?

Huwezi kufanya jambo hilo; haitakuwa sawa. Ni lazima iwe kwa roho moja, mahali pamoja, na kuwekwa kwa nia moja, jambo moja, ndipo utaona jambo fulani likitendeka.

MKATE WA KILA SIKU

Ijalizeni furaha yangu, ili mwe na nia moja, wenye mapenzi mamoja, wenye roho moja, mkinia mamoja.

Wafilipi 2:2

22-1201

62-0422 – Kurudishwa Kwa Mti Wa Bibi-Arusi

Kwa hiyo, unaona, kanisa la Kiprotestanti lisilolichukua Neno la Mungu ni binti kwa kanisa la Kirumi. Mungu kamwe, katika wakati wowote, hakuliundia kanisa dhehebu. Kanisa Katoliki la Kirumi ndilo lililokuwa dhehebu la kwanza. Na kila mmoja wao, aliyeunda dhehebu, ni binti kwake.

Wanakufa pamoja naye. Biblia ilisema, ya kwamba, “Atawateketeza watoto wake kwa moto.” Ni wangapi wanaojua jambo hilo? [Kusanyiko linasema, “Amina.”—Mh.] Biblia ilisema hivyo.

Vema, Biblia ilisema ya kwamba ngano na magugu vitakua pamoja mpaka siku ya mwisho, ndipo atayafunga magugu (hiyo ni kweli?), kwanza, na kuyateketeza kwa moto. [“Amina.”] Na ngano itawekwa ghalani. Hiyo ni kweli? [“Amina.”] Magugu yanajifunga pamoja katika dhehebu, Muungano wa Makanisa, kwa ajili ya kuchomwa na atomu. Kweli kabisa. Bali Kanisa linajiandaa tayari kwenda kwenye ghala, hakika kabisa, katika Unyakuo, kwa maana mwanamke huru hatarithi pamoja na mjakazi.

22-1130

65-0123 – Mabirika Yavujayo

Sasa Neno la Mungu ni kama mnyororo, unavuka jehanamu Nao; na mnyororo wake uko tu katika kipeo cha ubora wake kwenye kiungo chake kilicho dhaifu sana, naye Mungu anatutaka sisi tudumishe kila Neno Lake. Sasa hiyo ilikuwa ni mwanzoni mwa Biblia; kuvunja tu Neno moja, kuliitumbukiza jamii ya binadamu katika giza la mauti.

Yesu alikuja katikati ya Biblia, na akasema kwamba, “Mtu hataishi kwa mkate tu, bali kwa kila Neno.” Si sehemu tu ya Maneno, ama tisini na tisa kwa mia; bali kwa kila Neno, kama tu vile Hawa na Adamu walivyokuwa.

Na mwishoni mwa Biblia, Ufunuo 22:18, akasema kwamba, “Mtu yeyote atakayeondoa Neno moja kutoka Kwake, ama kuongeza Neno moja Kwake!”

Basi kwa nini tunahitaji kuingiza Hapa wazo la mambo ya mtu fulani, wakati hili ndilo Wazo la Mungu Mwenyewe kulihusu?

22-1129

63-0120M – Sauti Ya Mungu Katika Siku Hizi Za Mwisho

Kama wewe ni mwaminio vuguvugu tu, Sauti ya Mungu inapaza sauti moyoni mwako asubuhi ya leo, “wewe ni mwaminio vuguvugu,” afadhali utubu!

Wewe mwanaume, wanawake, wavulana ama msichana, ambao hammwishii Kristo, na Sauti ya Mungu inasema nanyi kupitia kwenye Neno Lake na kusema “acha kufanya jambo hilo,” afadhali ufanye hivyo. Kwa sababu utaisikia tena siku moja, Nayo itakuhukumu. Huwezi kuikana, inazungumza nawe sasa. Na, kumbuka, inarekodiwa.

Na wale wanaotenda mema na kuisikia Sauti Yake, watafufuka katika haki, kwa Utukufu, waende Mbinguni.

22-1128

64-0411 – Usahaulifu Wa Kiroho

Bali ninapenda uzao bora na halisi. Loo, yeye ni mpole. Unaweza kuzungumza naye. Yeye anajua baba yake alikuwa ni nani, mama yake alikuwa ni nani, babu na nyanya yake walikuwa ni nani. Ana makaratasi ya ukoo safi kuonyesha alikotoka.

Nami nampenda Mkristo wa ukoo safi, ambaye anaweza kurejea huko nyuma kabisa kwenye Neno la Mungu, kwenye siku ya Pentekoste, na kujitambulisha wenyewe kule pamoja na watakatifu, ambapo Nguvu za Roho Mtakatifu ziliwashukia. Huyo ni Mkristo wa ukoo safi. Anajua anakotoka .

Hajitambulishi na Methodisti, Baptisti, wala chochote kile. Yeye anajitambulisha katika Neno la Mungu. Anajua mahali anaposimama hasa. Damu ya kifalme ya Baba yake inatiririka ndani yake; Damu ya Yesu Kristo. Anajua kile inachofanya! Anaamini kila Neno. Mungu anatenda kazi kupitia kwake na anathibitisha hilo kwa ishara alizoahidi zitafuata. Hana usahaulifu wa kiroho. Yeye ni ukoo safi. Ninapenda hilo

22-1127

55-0118 – Huyu Shujaa Mkuu , Daudi

Kila Daudi anayeketi hapa usiku wa leo, umewekwa mahali pako katika Kristo. Mungu amethibitisha hilo. Uchaguzi, kuita, kutia mafuta, kuweka: Alikuchagua na kukuita. Alikuchagua na kukuita. Kisha Yeye aliwatia mafuta kwa Roho Mtakatifu, na sasa, amewaweka katika mwili wa Kristo, kila mmoja wenu ni akina Daudi.

Goliathi yuko wapi? “Ndugu Branham, Goliathi ni nani?” Hiyo kansa inayokula (hiyo ni kweli.), huo uvimbe unaoning’inia juu yako, hao watoto wa jicho waliomo machoni mwako, huo mkono ulio lemaa. Kila kitu hukiangaliacho na kusema, “Haiwezekani.” Ibilisi anasema, “Ni vema ukaacha kuamini. Ni vema ukatulia, kwa sababu huwezi kamwe kupona tena.

Daktari wako alisema hivyo; wengine wote walisema hivyo. Hauwezi kupona.” Lakini Kristo aliyekufanya uache kunywa pombe, kuvuta sigara, kusema uwongo, kuiba, aliyekuokoa na maisha ya ulevi, uropokaji, dhambi na kaburi la shetani, Ikiwa Mungu anaweza kukufanyia namna hiyo, anaweza kukuokoa na TB yako na kutokana na saratani yako. Yeye ni Goliathi; usichukue fahari yake. Simama katika Jina la Bwana Yesu na umpe changamoto kwenye shindano la kuamua. Amina. Haleluya. Najisikia wa kidini.

22-1126

61-0217 – Alama Ya Mnyama Na Muhuri Wa Mungu #2

Loo, ni Muhuri wa Roho Mtakatifu, ndugu; huo ni Muhuri wa Mungu. Hiyo ni kweli, kuweka muhuri.

Sasa, Wayahudi ndio wanaofuata kuupokea. Wapentekoste wamekuwa nao, Wamethodisti, Wabaptisti, hao wote wametoka katika madhehebu mbalimbali wameketi papa hapa usiku wa leo. Mimi mwenyewe ni Mbaptisti, ama nilikuwa. Mimi bado ni Mbaptisti, lakini mimi ni Mbaptisti wa Kipentekoste nikiwa na Roho Mtakatifu. Mimi ni Mnazarayo, Mpentekoste, Mpresbiteri, Mbaptisti. Loo, mwajua ninalomaanisha, yote katika hilo.

Ni nini, ni Roho Mtakatifu ndiye aliyeleta tofauti, kwamba ndiye aliyenitia muhuri katika Ufalme wa Mungu. Hilo ndilo lililomtia muhuri kila Mmethodisti, kila Mkatoliki, kila Mpresbiteri. Sisi sote ni wanadamu, na kwa Roho mmoja, sisi sote hatujaunganishwa katika kanisa moja, kwa mkono mmoja sote tumetikiswa, kwa maji mamoja; lakini kwa Roho mmoja sisi sote tumebatizwa kuwa mwili mmoja kwa Roho Mtakatifu na kutiwa muhuri hadi siku ya ukombozi wetu. Amina. Huyo ndiye Roho Mtakatifu.

22-1125

64-0620B – Yesu Ni Nani?

Mungu peke yake, hapo mwanzo, Alikuwa Mungu tu…Hata hakuwa Mungu, hapo mwanzo. Je, ulijua jambo hilo? Hasingekuwa. Mungu ni “kitu cha kuabudiwa,” neno la Kiingereza. Unaona?

Kama Yeye alivyokuwa Elohim, Yeye aishiye peke yake ; Hakuwa hata Mungu. Lakini ndani Yake kulikuwa na sifa, kama vile wazo lako . Unaona? Wazo lako, sina budi kuona jambo fulani, halafu…naliwazia, na kisha kulizungumza. Na neno ni wazo lililodhihirishwa. Kwa hiyo, “Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alidhihirishwa,” unaona, kuonyeshwa.

Na sasa yote ni mamoja. Jinsi ile ile tulivyo, kuzaliwa mara ya pili, tunao Uzima wa Milele. Kama tuna Uzima wa Milele, kuna aina moja tu ya Uzima wa Milele, huo ni Mungu. Na sisi ni sifa zake. Sasa naweza kuzungumza na Wakristo kwa njia hii. Sisi ni sifa. Na Yesu alikuja kama Mkombozi. Ni wangapi wanaoamini jambo hilo?

Kukomboa, sio kuumba kitu kipya. Kukomboa ni kurudisha kile ambacho kimekuwako tayari . Unaona? Kwa hiyo unaogopa nini? Unaona? Yote—yote yako mikononi Mwake, saa haizunguki vibaya. Kila kitu kilipaswa kiwe namna hii , na kutufikisha mahali hapa.

22-1124

53-0607A – Huduma Ya Kristo

Petro alisema…Walipoanza kuyumbayumba na kupiga kelele , ulimwengu wa nje wa kikanisa wa Injili yote , ama ulimwengu wa kishupavu ulimjia na kusema, “Watu hawa wamelewa.” Je, unaweza kuwazia?

Na sikilizeni, enyi marafiki Wakatoliki, na ninyi wengine. Bikira Mariamu aliyebarikiwa alikuwa miongoni mwao. Na kama Mungu hata asingemruhusu mama wa Mungu Mwana, aingie katika Ufalme wa Mungu mpaka ajazwe kabisa na Roho Mtakatifu mpaka akatenda kama mwanamke mlevi, utaingiaje, basi kwa kitu kingine pungufu? itakuwaje? Wazia jambo hilo mwenyewe.

Biblia ilisema Mariamu alikuwa mle ndani. Mama mwenyewe wa Kristo ilimbidi kwenda kule Pentekoste na kukaa kule katika jiji la Yerusalemu mpaka alipokuwa amejazwa Roho Mtakatifu hata akayumbayumba kama vile alikuwa amelewa. Amina. Huo ni ukweli. Hiyo ni Biblia.

22-1123

53-0219 – Kubali Karama ya Mungu

Nakumbuka siku moja nilipotazama kule juu na kuona kile alichonifanyia, nilitambaa kwa unyenyekevu kwake. Jina langu lilikuwa pale juu ya kitabu, na, loo, kile kilichoandikwa chini yake. Nikasema, “Bwana, utanisamehe?”

Na inaonekana, akashika mikono yake, akaichovya ubavuni mwake, akasema, “Ndiyo.” Naye akaandika kote katika kile kitabu, “Amesamehewa,” akakifunga, na kukirejesha katika bahari ya usahaulifu. Nimekuwa na furaha tangu wakati huo.

Ninajaribu niwezavyo katika njia yangu nyenyekevu kumwambia kila mwanadamu duniani: “Yesu Kristo anakupenda, na Yeye ndiye kitu pekee kinachozuia ghadhabu ya Mungu kutoka kwako. Mpokee Yeye kama Mwokozi wako binafsi.” Na ukishafanya hivyo, sasa, Yeye ambaye—pia alipigwa mijeledi mgongoni Mwake, “kwa kupigwa Kwake sisi tumepona,” ama “tulipona,” sio tutakuwa, tumepona tayari.

Kila mtu amepona. Na sasa, jambo pekee unalopaswa kufanya, ni kuamini jambo hilo kwanza moyoni mwako kabla hujalisema. Ikiwa unalisema tu kutoka kwa midomo yako, haitakufaa chochote.

22-1122

63-0412E – Mungu Akijificha Katika Urahisi

Mungu hafanyi mambo kuwa magumu, ya rozari kadhaa, na vitu vingi hivi, na kujiunga na hili, na elimu kubwa mno, thiolojia kubwa mno. Mbona, tunazidi kujipeleka mbali zaidi na zaidi na Mungu, wakati wote, kwa kufanya hivyo.

Leo, sisi ni wa kisayansi sana hata tunaweza kusema inachukua molekuli ngapi kufanya atomu moja, ni elektroni ngapi, na kadhalika; na kuipasua hiyo atomu, na kuwaambia jinsi ya kufanya hivyo; kuunda bomu la atomiki, na halafu tungeweza kuelezea jinsi tulivyolitengeneza; lakini tunatembea juu ya jani la nyasi ambalo hatuwezi kulielezea.

Mungu, katika urahisi. Mungu alijidhihirisha katika urahisi. Yeye hujifanya wa kawaida. Ni kusudi kwamba wenye hekima wasifahamu. Yesu alisema, “Nakushukuru, Baba, umeficha jambo Hili wenye hekima na akili, na utalifunua kwa watoto wachanga ambao watajifunza.”

Kamwe usijaribu kujielimisha umfahamu Mungu. Unapofanya hivyo, unajielimisha kwenda mbali na Mungu. Unaona?

Mungu hajulikani kwa elimu. Mungu, ni wa kujulikana kwa imani. Na pigo la kwanza ambalo Ibilisi alipiga nalo lilikuwa ni kwenye mpango wa elimu, ndipo mwanadamu akapoteza ushirika wake na Mungu. Hiyo ni kweli kabisa. Hana budi kumjua Mungu kwa imani, si yale anayoweza kuelezea; kwa yale anayoamini, ambayo hawezi kuelezea.

22-1121

60-0417S – Najua

Imeandikwa, katika mojawapo ya Maandiko katika Biblia, kwamba, “Majaribu yanayoletwa kwetu, yana thamani zaidi kwetu kuliko dhahabu yenyewe, kwa kuwa ni Mungu anayetupa majaribu haya.”

Baada ya sisi kuwa mali yake, maungamo yetu na ubatizo wetu, na ahadi yetu kutembea maishani kwa ajili Yake, basi kila jaribu linalotujia ni kutukamilisha kwa ajili ya utukufu Wake. Ni la kutuleta mahali ambapo Mungu anaweza kujifanya Mwenyewe halisi zaidi kwetu kuliko alivyokuwa kabla ya jaribu kuja.

Ninataka kuungana asubuhi ya leo na Ayubu, kusema ya kwamba nimeishi muda mrefu kutosha kujua kuwa hiyo ni Kweli. Nimeiona katika maisha yangu mwenyewe, kwamba kila mara hali ngumu inapoinuka, ambayo siwezi kuizunguka, ama kupita chini yake au juu yake, Mungu hufanya njia, na hutokea kwa utukufu. Nashangaa tu jinsi neema Yake huifanya kamwe, bali Yeye huifanya.

22-1120

59-0823 – Tunutu, Nzige, Parare, Madumadu

Na kama Mungu hana kikomo, hana kikomo, wala hawezi kubadilika, Kanisa Lake halina budi kubaki kama lilivyokuwa hapo mwanzo. Je, mnakubali hilo? [Kusanyiko linasema, “Amina.”—Mh.]
Kanisa halina budi kubaki kama lilivyokuwa.

Bali mwanadamu ameliingilia ovyoovyo, wakaweka tafsiri zao wenyewe ndani Yake. Kamwe usijaribu kulifasiri Neno la Mungu. Sema tu kile Hilo lisemacho. Haijalishi jinsi lilivyo, kwa hiyo ambatana tu na Hilo, hivyo tu. Usilibadilishe Neno.

Biblia ilisema, kwamba, “Maandiko si ya kutafsiriwa apendavyo mtu kibinafsi.” Hatuna haki ya kusema mambo haya; inatubidi tu kulisoma na kusema jinsi tu lisemavyo, na kuliamini vivyo hivyo. Sijali jinsi linavyoonekana la kijinga; liamini, kwa vyovyote vile.

22-1119

59-1220M – Kongamano Pamoja Na Mungu

Labda wewe ni mwenye dhambi, na umetenda dhambi nyingi sana. Labda ulivuta sigara mpaka huwezi kuzivuta tena, wala huwezi kuachana nazo. Labda umekunywa pombe hata huwezi kuinywa tena, wala huwezi kuiacha. Labda umefikia mahali ambapo umejaa dhambi sana na tamaa mbaya, mpaka inakubidi kumtazama kila mwanamke unayemwona, vibaya.

Ama, labda hata umepotosha asili yako mwenyewe. Labda umefika mwisho. Sijali mahali ulipo, Mungu angali yuko tayari kuja kwako, katika kongamano, na kulizungumzia pamoja nawe.

22-1118

56-0128 – Uvuvio

Watu wanajua hilo wakati umetiwa mafuta na Roho Mtakatifu. Huenda mioyoni mwao, ama katika—katika hoja zao, kusema, “Loo, hapo, jamaa huyo ana kichaa. Loo, mimi—mimi…” Lakini ndani moyoni mwao wanakukubali (hiyo ni kweli.), ndani ya mioyo yao.

Wanaweza kubishana nawe, kwa sababu wanajaribu kukubaliana na hoja zao; lakini ndani ya mioyo yao wanakubali, isipokuwa nafsi zao zimeungua mpaka hawana kitu ila hoja .

Kwa maana kama wewe ni Mkristo halisi, unaishi maisha ya kweli, na unaishi Neno na Mungu yu pamoja nawe, kila mtu atalithamini, ikiwa nafsi yake ingali ina mawasiliano na Mungu. Amina. Hiyo ndiyo sababu ninafikiri kubishana kuhusu madhehebu hakufai. Hakika hakufai.

22-1117

63-0120M – Sauti Ya Mungu Katika Siku Hizi Za Mwisho

Mbali na kuiga huku kote, sauti za uongo, manabii wa uongo, mambo haya mengine yote yanayoibuka, Yesu angali alisema, mbali na mambo haya yote, “Kama mtu yeyote atasikia Sauti Yangu na kunifuata Mimi.” Yeye ni Neno.

Sikilizeni, agizo Lake kwetu leo, katika sauti hizi zote. Ambazo, nilisema ingechukua saa nyingi kuzielezea sauti hizi zote. Nazo zinawakanganya watu, ni jambo la kusikitisha .

Na, hata hivyo, hupati nafasi ya pili, inakupasa kulichukua sasa. Huenda usipate nafasi usiku wa leo. Huenda usipate nafasi kesho. Ni sasa!

“Unapoisikia Sauti Yangu, usiufanye mgumu moyo wako, kama wakati wa kukasirisha. Wakati ndio huu. Huu ndio wakati uliokubalika kwamba kama mtu yeyote ataisikia Sauti Yangu.”

22-1116

60-0329 – Ni Mimi, Msiogope

Hayo Ni mazingira yanayofanya hivyo.

Unaweza kuchukua yai la kuku na kuliweka kwenye kiangulio na kuweka mazingira sawa yataangua kuku sio Kiangulio. Waona? Kwa sababu ni hayo Mazingira yanayojalisha. Weka yai la kuku chini ya m—mbwa. Yataangua kuku. Ni Mazingira.

Na hivyo ndivyo inavyopaswa kuwa kanisani leo hii, si kanuni nyingi za imani na theolojia, bali Roho wa Mungu aliye hai akishuka juu ya watu Wake kuleta hali ya kiroho. Sio mmoja akisema, “Ninaamini ni hili,” na mwingine, “Ninaamini ni lile .” Ni vigumu kwa Roho Mtakatifu kufanya kazi.

Je, unajua Roho Mtakatifu alipokuja mara ya kwanza? Ilikuwa siku ya Pentekoste, walipokuwa wote mahali pamoja na moyo mmoja. Ndipo sauti ikatoka mbinguni kama upepo wa nguvu ukienda kasi. Walipaswa kuweka mazingira sawa.

Na hivyo ndivyo tunavyohitaji leo hii, ndugu. Tuko nyuma sana. Kanisa linapaswa kuwa maili milioni moja juu ya barabara.

22-1115

57-0825E – Waebrania, Mlango Wa Pili #2

Maskini nabii huyo thabiti, mzee, alimwangalia mwanamke huyo usoni. Akasema, “Nenda, kaniokee mimi keki kwanza.” Ni amri ya jinsi gani, kwa mwanamume kumwambia mwanamke mjane, anayekufa kwa njaa, ati amlishe yeye kwanza. Yeye alisema nini? “Kwa kuwa BWANA ASEMA HIVI, lile pipa halitapunguka, wala chupa haitaisha, mpaka Mungu atakapoleta mvua juu ya nchi.”

Kwanza, Mungu. Aliingia ndani na akamwokea mkate huo mdogo, kisha akaja akampa nabii. Akarudi moja kwa moja na kuoka mwingine, na mwingine, na mwingine, na mwingine. Wala lile pipa halikupunguka, wala chupa haikuisha, mpaka Mungu alipotuma mvua juu ya nchi. Yeye alimweka Mungu mbele ya watoto wake. Alimweka Mungu mbele ya kitu kingine chochote. Aliuchukua Ufalme wa Mungu, kwanza.

Mungu hana budi kuchukua nafasi ya kwanza moyoni mwako, nafasi ya kwanza maishani mwako, mahali pa kwanza katika kila kitu ufanyacho ama chochote ulicho. Mungu hana budi kuwa ni wa kwanza. Yeye hataki nafasi ya pili. Hastahili nafasi ya pili. Yeye anastahili kilicho bora sana, na cha kwanza, na yote tuliyo nayo. Anastahili. Jina Lake takatifu litukuzwe!

22-1114

61-0216 – Alama Ya Mnyama Na Muhuri Wa Mungu #1

Na kumbukeni, wakati ule ule ambapo yule bikira aliyelala alipoenda kununua mafuta, hapo ndipo Bwana-arusi alipokuja. Utukufu .

Hamwoni jambo hilo? Kama Wapresbiteri na Waiskopalia na hao wengine, wamekuja wakimtafuta Roho Mtakatifu, ni afadhali uitengeneze taa yako. Imetengenezwa, imetengenezwa, ndio, inahitaji kutengenezwa. Pentekoste, ni bora utengeneze taa kadhaa . Amina.

Yaondoe mengi ya huu ulimwengu kutoka kwako. Umeota kutu. Utambi umeingia katika hali mbaya. Unajua kwamba utambi ni jambo kuu. Mimi Hutazama. Utambi halisi wa Mungu ni kitu gani m—mwamini, ni utambi. Tazama, ana moto upande mmoja, hapa juu, na upande mwingine umechovya kwenye mafuta, ukichota mafuta na kuwasha moto. Ni—ni kanisa la jinsi gani, ni nguvu ya namna gani. Ni Mahali pa jinsi gani pa kuwa. Haleluya.

Kuangaza nuru ile ile ya Injili inayoangaza mashariki, inaangaza magharibi. Kutakuwa na nuru wakati wa jioni. Inuka, Pentekoste, tengeneza taa yako. Uondoe ulimwengu; iondoe mitindo ya ulimwengu; Yaondoe mambo ya ulimwengu. Jiweke Tayari; Ile saa imekaribia.

22-1113

60-0925 – Siku Hiyo Pale Kalvari

Hatimaye siku moja—hiyo ni ile siku pale Kalvari—Mtu mmoja akashuka akaja kutoka Utukufuni— Mtu mmoja aliyeitwa Yesu Kristo, Mwana wa Mungu Yeye aliyetoka Utukufuni, kisha Kalvari ikatengenezwa.

Hiyo ndiyo siku ambayo ile gharama ililipwa, na swali la dhambi likatatuliwa milele, naye akafungua njia ya kitu hiki tunachokionea njaa na kukionea kiu. Ilileta mahali pa utoshelevu. Hakuna mtu aliyepata kutembelea Kalvari na kuona jinsi ilivyokuwa, anayeweza kubaki alivyokuwa.

Kila alichoonea shauku au kutamani sana kinapatikana anapofika mahali hapo. Ilikuwa siku muhimu sana na jambo muhimu sana, hata ikaitikisa dunia. Iliitikisa dunia jinsi ambavyo haijatikiswa hapo awali, Yesu alipokufa pale Kalvari naye akalilipia swali la dhambi.

Dunia hii yenye dhambi ilitiwa giza kabisa. Jua lilitua mchana nalo likazimia roho kwa wasiwasi. Miamba ikatikisika. Milima ikapasuka. Miili ya waliokufa ikafufuka ghafla kutoka kaburini.

22-1112

55-0109E – Mwanzo na Mwisho wa Miliki ya Mataifa

Daniel alikuwa amechoma madaraja yote nyuma yake. Hakuwa na mpango wa kurudi, tena. Hakuwa akiangalia njia yake ya nyuma. Alikuwa akitazamia, akiyasahau mambo yale yaliyokwishakupita. Alikaza mwendo kuiendea mede ya wito mkuu. Hicho ndicho tunachopaswa kufanya. Hivyo ndivyo Kanisa linapaswa kufanya.

Na kama ninavyoona, basi, Mungu alimruhusu Shetani kumpa jaribio. Na, loo, waliwajaribu, kwa moto. Wakawajaribu, pia, penye tundu la simba. Na kwa kila hali , Mungu akawatoa, zaidi ya washindi .

” Majaribu ya mwenye haki ni mengi, lakini Mungu humponya nayo yote.” Hilo ni la kustaajabisha jinsi gani ! Jinsi tunavyothamini jambo hilo. Majaribu, dhiki, mitihani, yote yakitenda kazi kwa manufaa! Baada ya muda, Mungu anaweza kuona wakati huo kwamba anaweza kukuamini , na kisha atakufanyia mambo makuu.

22-1111

58-0517E – Dhambi ya Kutokuamini

Ina faida gani kuhubiri Biblia ikiwa Mungu ni bubu na hatajibu ahadi yake? Ingefaa nini kumlisha kurumbizi wako vitamini B, vitamini A ili kufanya mabawa yake kuwa na nguvu na kisha kumweka kwenye kizimba wakati wote? Humruhusu atoke. Vitamini vyako vina faida gani?

Semina zetu zote na shule za theolojia zina faida gani, na wahubiri wetu wakuu wenye D.D., Ph.D., na L D maradufu? Hilo lina faida gani, ikiwa yote yanatokana na Mungu wa kihistoria ambaye haishi na kutenda vivyo hivyo leo kama wanavyofundisha juu ya jambo hilo kwamba lilitendeka?

Biblia ilisema ni yeye yule jana, leo na hata milele. Yeye Si mfu; Amefufuka kutoka kwa wafu na yuko hai milele na milele, yuko kila mahali milele. Huyo ndiye Mungu ambaye tunataka kusikia habari zake. Huyo ndiye Mungu ambaye kila mwana wa kweli aliyechaguliwa wa Ibrahimu anataka kusikia habari zake na anataka kumjua.

22-1110

50-0716 – Je, Unasaki Hayo?

Ukiupenda ulimwengu, mambo ya ulimwengu , kumpenda Baba hakumo ndani yako. Hilo linaweza kuwa gumu kidogo kulifundisha hapa, lakini ni kweli; hebu niwaambieni.
Sina vijiti vya kupimia kanisani. La, hata kidogo. La, bwana.

Mti wa mwaloni wa zamani sana mlio nao hapa unashikilia majani yake wakati wote wa majira ya baridi kali. Majira ya kuchipua ya mwaka yajapo, huna haja ya kwenda kuchuma majani ya kale kuyaondoa, acha tu uhai mpya uingie, jani kuukuu huanguka. Ndivyo ilivyo. Hebu Kristo aingie moyoni; hayo mengine yatajishughulikia yenyewe. Hiyo ni kweli .

Mwingize tu Kristo moyoni; itashughulikia mengine yote .

22-1109

56-0814 – Upendo wa Kiungu na Neema kuu

Sasa walikuwa wanafanya nini? Kuonyesha upendo, upendo wa Kiungu wa Mungu. Na neema kuu italazimika kuchukua hatua badala yake. Unaona jambo hilo ? Nini kilitokea? Mungu akamwambia Musa, “Waambie wasimame kimya

Wao…[Sehemu tupu kwenye kanda—Mh.]…?…nami nitawaonyesheni neema Yangu ni kitu gani. Simameni tu kimya sasa. Msishtushwe. Kila hatua ya mwenye haki huongozwa na Bwana.” Haijalishi kipi kijacho au kuondoka, Mungu anakiamuru. Labda kupitia majaribu na labda kupitia taabu na dhiki, lakini ilimradi tu ni Mungu aongozaye inaleta tofauti gani?

Kasema, “Sasa, waambie wasimame kimya. Wananipenda, na wananionyesha Mimi kwa kuthibitisha ya kwamba wananiamini Mimi kusonga na Neno Langu, na wanaliamini. Na sasa wako mwisho wa njia. Upendo umewachukua kadri uwezavyo, kwa hiyo sasa nitawaonyesha. Walionyesha upendo Kwangu. Nami Nitawaonyesha neema Yangu ya Kimungu na uweza wangu.”

Kasema, “Waambie ya kwamba wako mwishoni; hawawezi kufanya kitu zaidi . Lakini bado wananipenda Mimi na wananiamini Mimi. Kwa hiyo neema Yangu itafanya kazi sasa katika Kesi hii.”

Nayo Itafanya kazi usiku wa leo katika kesi yako. Itafanya kazi katika Kila kesi . Mtazame yeye .

22-1108

58-1221M – Yuko Wapi Yeye , Mfalme wa Wayahudi?

Ni Krismasi. Hivyo Vitu vyote vya mapambo, juu-chini mtaani, vya Santa Claus, hadithi ya kubuniwa ya Kijerumani, fundisho la sharti la Kikatoliki, hakuna hata chembe moja yake ya ukweli. Na inachukua mahali pa Yesu Kristo, katika mioyo ya Wamarekani wengi sana. Krismasi haimaanishi Santa Claus. Krismasi inamaanisha Kristo. Sio mtu fulani aliye na bomba mdomoni mwake, na akishuka kwenye bomba la moshi! Unapowafundisha watoto wako kitu kama hicho, unatarajia wakue wawe namna gani?

Waambie Ukweli, sio hadithi za uwongo. Waambie, “Kuna Mungu wa Mbinguni Aliyemtuma Mwanawe, na hicho ndicho Krismasi inachomaanisha. Naye yuko karibu kuja tena.”

Na presha inapoanza kuja duniani, shetani ametoa vitu vyake, kwa macho, vile unavyoweza kuona, mapambo na kadhalika. Mungu ametoa kitu chake, ambaye ni Roho, ambaye huwezi kumwona, bali unaamini.

22-1107

62-0603 – Uinjilisti Wa Wakati Wa Mwisho

Hiyo ndiyo sababu ninaamini ya kwamba Neno ni Kweli. Ikiwa kanuni zetu za imani na madhehebu yetu hayaambatani kabisa na Neno, basi yamekosea.

Na ikiwa Mungu hataruhusu, nalo Neno Lake lilikuwa ni muhimu sana, kunukuu tu vibaya neno moja Lake kulisababisha yote, kila kifo kilichopata kutokea, kila mateso, kila mtoto mchanga anayelia, kila msafara wa mazishi, kila kaburi ubavuni mwa kilima, kila gari la kuchukulia wagonjwa lililowahi kupiga makelele, kila damu iliyowahi kumwagwa, uzee wote na kufa kwa njaa na matatizo ambayo tumekuwa nayo, kwa sababu tu Neno la Mungu lilikosewa, kulisababisha haya yote, hivi Yeye atalisamehe wakati wa mwisho iwapo tutalikosea Hilo tena?

22-1105

62-0117 – Kudhania

Siku ya Pentekoste, walingojea mpaka wakapata mamlaka ya Kimaandiko. Hiyo ni kweli, kabla hawajadai chochote, walijua walikuwa nayo. Hawakusema—kusema, “Vema, ni—nilisikia mhemuko mdogo.” Waliihisi, wakaiona, chochote kile. Walijua walikuwa nayo. Waliiona ikitenda kazi ndani yao, ikitenda kazi ndani yao, ikizungumza kupitia kwao, kila kitu. Ilikuwa pale. Haikuwabidi kudhania chochote. Ilikuwa pale, ikijielezea .

Na mtu, anapozaliwa mara ya pili kwa Roho wa Mungu, ni jambo lile lile leo. Hudhanii .

“Ni—ninaamini tunampokea Roho Mtakatifu tunapoamini.” La. Hamkumpokea. Hamumpo-…Wengine, mngeweza kumpokea. Lakini kwa sababu tu ati uliamini, kama Mungu hakukujaza na Roho Mtakatifu, basi Yeye hajakuthibitisha bado. Hujampata. Unaona? Hiyo ni kweli .

Usidhanie unaye. Kuwa na hakika na kitu hicho. Hutaki kubahatisha juu ya jambo hilo, la, maana utapotea. Usibahatishe tu. Kaa tu, nenda, kaa mpaka jambo hilo limetimizwa kwako.

22-1104

65-0801M – Mungu Wa Wakati Huu Mwovu

Kuasi maana yake “uhalifu.” Nililiangalia hilo kwenye kamusi, nipate kuwa na hakika. Maasi, maasi dhidi ya nini (kitu gani?) Neno la Mungu lililofunuliwa. Kama Kaini alivyofunua…alivyoasi dhidi ya ufunuo aliofunuliwa Habili, uliothibitishwa na Mungu kwamba ni wa haki. Naye Kaini akauasi huo, na kumwua ndugu yake.

Mafarisayo, wakiwa na maarifa yao wenyewe ya kimadhehebu kuhusu Neno la Mungu lilivyokuwa, waliwachagua watu wa kujichagulia wenyewe, wakaliasi Neno la Mungu lililothibitishwa na kudhihirishwa kwa ajili ya siku hiyo, Yesu Kristo, na wakamwua. Hiyo ni kweli?

Hicho ndicho “wana wa kuasi walicho,” ni maasi dhidi ya Neno la Mungu .

Sasa unaona mahali walipo?”Loo, siku za miujiza zimepita. Yesu Kristo si yeye yule bado. Hakuna kitu kama ubatizo wa Roho Mtakatifu. Takataka zote hizo ni upuuzi!” Unaona, maasi!
Si lazima waseme mambo mawili; inawapasa tu kusema jambo moja, yatosha. Hayo ni maasi, papo hapo .

22-1103

55-0114 – Daktari Musa

Jambo lile lile kuhusu Roho Mtakatifu. Unasema, “Nimekuwa nikimtafuta Roho Mtakatifu kwa miaka mingi.” Sikukemei. Huenda umefundishwa vibaya , au kuna jambo fulani lina kasoro , ama huelewi.

Mungu yuko chini ya wajibu kwa Neno lake. Petro alisema katika Siku ya Pentekoste, “Tubuni mkabatizwe kila mmoja wenu katika Jina la Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu.” Hayo ni Maandiko, wazi tu kama jinsi nijuavyo kuyasoma.

Kama ulitubu na kubatizwa, basi Mungu yuko chini ya wajibu, kama imani yako ni sahihi kwa Mungu kukupa Roho Mtakatifu dakika tu unapotii Neno Lake. Amini hilo. Mungu atalithibitisha jambo hilo kwako.

Kama moyo wako kweli uko sawa mbele za Mungu, nawe umefundishwa sahihi , na kuliamini, na uende kule ukiwa na uhakika, jambo fulani litatukia, maana Mungu yuko tayari kukupa Roho Mtakatifu kuliko vile wewe ulivyo tayari kumkubali.

22-1102

64-0629 – Mungu Aliye Mkuu Akifunuliwa Mbele Zetu

Na hivyo ndivyo Mungu alivyofanya. Yeye alijigeuza kutoka kwa Yehova Mungu akawa mmoja wetu, apate kuteseka, apate kuonja mauti, apate kujua jinsi uchungu wa mauti ulivyokuwa, na achukue adhabu ya kifo juu Yake .

Yeye aliweka kando taji Ya—Yake na joho Lake na akawa mmoja wetu. Yeye alitawadhana miguu na—na—na watu wa kawaida. Yeye aliishi katika hema na watu maskini. Alilala m—mstuni na barabarani za mji pamoja na makabwela. Yeye akawa mmoja wetu apate kutufahamu vizuri zaidi. Nasi tukapate kumfahamu Yeye vizuri zaidi.

22-1101

61-0205M – Tarajio

Nilisoma kuhusu Abraham Lincoln, mkusini mashuhuri, aliyeshuka kwenye mtumbwi kule New Orleans, naye akawaona kwenye shimo la watumwa kule, wakimpiga mnada Mnegro mkubwa mno, shupavu. Naye maskini mke wake amesimama huko nje pamoja na watoto wawili, wakilia, kwa kuwa walikuwa wakienda kumwuza wapate kumzalisha kwa wanawake wakubwa zaidi, wenye afya wapate kuwazaa watumwa wakubwa zaidi. Abraham Lincoln akakunja ngumi yake namna hiyo, na kusema, “Hiyo si haki. Siku moja nitalipiga, hata ikinigharimu maisha yangu.” Ilimgharimu maisha, bali aliipiga. Akaivunja, pia.

Hebu nikwambie, ndugu, kutokuamini ni kwa ibilisi. Hebu nikupige, Bwana. Sijali kama kukinigharimu maisha yangu. Nijalie kukivunjilia mbali kitu hicho juu ya kanisa, hiyo mipaka, na kadhalika, tupate kuona, sisi, kwa Roho mmoja, sote tumebatizwa kuwa mwili mmoja, nasi ni Wakristo. Sisi ni ndugu.

Haidhuru kama huyo mtu ni mfuasi wa Church of God nami ni wa Assemblies, naye huyu ni Mbaptisti, ama Mpresbiteri; sisi ni ndugu, hivyo ndivyo tulivyo, sisi ni ndugu katika Kristo. Hebu tukivunje. Tuivunjilie mbali mipaka hii. Tunaweza kumnyoshea mikono yetu kila ndugu.

22-1031

53-0601 – Lo lote Atakalowaambia, Fanyeni

Kama wewe—ikiwa hakuna vita, basi hakuna ushindi. Lakini lazima uwe na vita ili kupata ushindi.

Kama ungepewa hilo tu, haingekuwa—isingekuwa na—usingekuwa ushindi. Bali yeye ashindaye ndiye aliye na ushindi .

Basi Yesu akaja duniani; Alikuwa na vita; Yeye Alishinda. Na usiku wa leo tunayo vita, na tukiwa na Kristo, tunaweza kupata ushindi.

22-1030

51-0508 – Imani Ni Kuwa na Hakika

Si muda mrefu uliopita, msichana wangu mdogo aliniita, nilipokuwa hapa wakati ule. Kwa namna fulani imenipa wazo. Alisema, “Baba, nataka urudi nyumbani.” Ndipo nikasema, “Mpenzi, kutoka Texas nilikutumia m—mdoli mdogo.” Akasema- yeye ana umri wa miaka minne tu. Nikasema, “Nilikutumia mdoli mdogo, mpenzi.” Akasema, “Niliupata Baba.” Nami nikasema—Akasema, “Nataka uje nyumbani, baba.” Ndipo nikasema, “Vema, mpenzi, nilikutumia sungura mdogo kutoka Chattanooga.” Akasema, “Nilimpata, baba.” Lakini akasema, “Nataka urudi nyumbani.” Unaona? Nami nikasema, “Vema, mpenzi, mimi—baba…” Akasema, “Baba, nakupenda, na ninapenda zawadi unazonipa, lakini namtaka baba.”

Hilo ndilo. Karama zake zote ni za ajabu, lakini namtaka Baba. Ninapenda karama Zake, kumsikia katika madhihirisho, huko Kumsifu Mungu ,na kupaza sauti, na uponyaji, na kunena kwa lugha, na tafsiri za lugha, na karama zote mbalimbali.

Ninapenda kuketi na kuzitazama. Sina hizo, lakini ninapenda kuzitazama zikitenda kazi Kanisani. Lakini baada ya hayo yote, namtaka Yesu. Na—nataka hilo . Karama zake ni nzuri, lakini namtaka huyo mtoa karama humu ndani. Unaona? Hiyo ni kweli.

22-1028

61-0213 – Na Uzao Wako Utamiliki Lango la Adui Zake

Mungu anapenda kuonyesha mkono wake wenye nguvu. Ndiyo, anapenda kufanya hivyo. Anapenda kuonyesha nguvu zake. Anangoja usiku wa leo ili azionyeshe ndani yako; kumchukua huyo mwenye dhambi na kumgeuza, kumchukua mwanamke huyo mwenye sifa mbaya na kumbadilisha kuwa mwanamke mtakatifu mcha Mungu, kumchukua msichana huyo ambaye ameshika njia mbaya, mvulana huyo njia mbaya, kuwarudisha mahali na kuwafanya wana na binti za Mungu kutoka kwao.

Yuko tayari kumchukua mtu huyo anayekufa kwa kansa, huyo mwenye shida ya moyo, huyo aliye kipofu, huyo anayeteseka, akiweka tu imani yake huko itamgeuza kutoka mautini kuingia uzimani, amwanzishe upya na ushuhuda. Anasubiri kufanya jambo hilo. Anakuweka moja kwa moja kwenye mtego ili kuona utafanya nini. Aliwaweka moja kwa moja kwenye mtego ule pale. Ilionekana kana kwamba maumbile yenyewe yalikuwa yanaficha uso wake. Ndiyo.

Mwandishi mmoja alisema wakati mmoja, kwamba walipofika mahali pale, walishangaa Musa angefanya nini. Alikuwa na amri moja, “Songa mbele.” Ikiwa uko kwenye jukumu, haijalishi ni kitu gani kinachosimama njiani …

Matukio makubwa zaidi ambayo nimewahi kuwa nayo ni kukabili jambo ambalo nisingeweza kuvuka juu, au chini yake, na kusimama tu pale na kumwangalia Mungu akifanya njia kulivuka. Hiyo ndiyo njia ya kufanya jambo hilo. Wewe songa tu. Endelea kusonga mbele. Kabili pua yako dhidi yake. Endelea tu songa. Endelea tu kusonga mbele . Mungu atafanya njia.

22-1027

58-0324 – Msikieni Yeye

Kondoo wanapenda chakula cha kondoo. Na ndege Wala mizoga hupenda chakula cha ndege Wala mizoga. Koho hula chakula cha koho. Na ikiwa unayapenda mambo ya ulimwengu , hiyo inaonyesha kwamba kumpenda Mungu hakumo hata ndani yako .

Na mnafiki mkubwa aliyepo duniani ni kunguru. Hua na kunguru, waliketi kwenye nguzo moja, labda, ndani ya safina. Sasa, hua anaweza tu kula aina moja ya chakula, kwa sababu hua ni ndege mmoja ambaye hana nyongo. Hawezi kusaga vitu vilivyooza.

Na mtakatifu halisi wa Mungu aliyezaliwa mara ya pili hana uhusiano wo wote na mambo ya ulimwengu, maana yeye hana nyongo tena. Yeye haendi kuzunguka kubishana na kuwa mkali kwa sababu ya kujiona amedharauliwa, akitaka kujadiliana na kuhojiana juu ya jambo fulani .

Lakini mzee kunguru anaweza kuketi juu ya mzoga wa kale na kuula kwa masaa mawili na kuruka huko nje shambani na kula ngano pamoja na hua. Lakini hua hawezi kula ngano na kisha ale mzoga. Mnamwona mnafiki? Hapo ndipo kanisa limefikia. Ni kweli kabisa. Ni yapi Baba anayowazia…

22-1026

59-1216 – Roho Mtakatifu Ni Nini?

Nikasema, “Shetani, wewe unayezungumza na dhamira yangu, ningetaka kukuuliza mambo machache. Ni nani ambaye wale manabii wa Kiebrani walinena kwamba Yeye angekuja? Ni nani aliyekuwa Masihi mtiwa mafuta?

Ni nini kilikuwa juu ya watu hao waliomwona Yeye hapo awali na kusema habari za maisha Yake, maelfu ya miaka kabla Yeye hajafika hapa? Ni nani aliyetabiri jambo hilo kwa usahihi kabisa? Na hapo alipokuja, wao walisema, ‘Alihesabiwa pamoja na wakosaji,’ Naye alihesabiwa. ‘Alijeruhiwa kwa makosa yetu,’ na alijeruhiwa. ‘Alifanya kaburi Lake pamoja na matajiri, lakini Yeye angefufuka, siku ya tatu,’ Naye akafufuka. Kisha aliahidi Roho Mtakatifu, nami ninaye Huyo.

Kwa hiyo ni afadhali uliondokee jambo Hilo, kwa kuwa imeandikwa katika Neno, na kila Neno ni kweli.” Ndipo akaondoka. Mpe tu Neno; hilo linatosha. Yeye hawezi kuvumilia Neno hilo, kwa kuwa limevuviwa.

22-1025

57-0302 – Ndipo Yesu Akaja

Nataka kusema hivi, marafiki. Mimi si mponyaji. Siwezi kuponya watu. Siamini kwamba kuna mwanamume yeyote, daktari, au hospitali, au dawa zinazoweza kuponya watu. Ninaamini kwamba uponyaji upo kwa Mungu pekee.

Sasa, daktari anaweza kuondoa kizuizi; anaweza kurekebisha mfupa, kuondoa jino, kuondoa kivimbe. Lakini hilo haliponyi. Hilo linaondoa tu kizuizi.

Mungu ndiye huponya. Uponyaji ni uumbaji. Ni kuumba na kujenga upya. Na hakuna dawa inayoweza kujenga mwili wako upya . Mungu pekee ndiye anayeweza kujenga upya. Hiyo ni kweli. Mungu ndiye anayeponya .

22-1024

58-0609 – Ujumbe kwa Kanisa la Laodikia

Nami ninawazia jambo hili kwa undani, ya kwamba mara nyingi kanisa ndani yake ni ulegevu huanza kufanya mambo, na kuwazia mambo, na—na kuchukua mambo jinsi tu yalivyo, wakati inatupasa kupima kile tunachofanya na kusema. Tunapaswa kulitafakari kabla ya kulizungumza.

Mama yangu mzee wa kusini alizoea kuniambia, “Fikiria mara mbili na uzungumze mara moja.”

Ni mambo madogo, wakati mwingine, ambayo tunaacha bila kufanywa, hayo yana maana sana kwetu. Tunakuwa na haraka sana ya kushindana na mambo katika wakati huu wa neva tunaoishi. Ingetubidi sisi, kama kanisa la Mungu usiku wa leo, kusimama na kungoja kidogo, tuone mahali tulipo.

22-1023

54-0718A – Ufufuo Mkuu Ujao Na Kumwagwa Kwa Roho

“Kutakuweko Nuru yapata wakati wa jioni.” Mawingu yamerudi nyuma. Madhehebu yamevunjwa, Haleluya, na watu wameingia katika ubatizo wa Roho Mtakatifu kwa ishara na maajabu kama tu walivyokuwa nao hapo mwanzo. “Kutakuweko nuru wakati wa jioni.”

Na kumbukeni, ilikuwa ni wakati wa jioni wakati Bibi-arusi alipochaguliwa. Rebeka alichukuliwa wakati wa jioni. Ilikuwa ni wakati wa jioni alipokutana na Isaka; alikuwa nje shambani. Ni wakati wa jioni.

Ufufuo wetu wa Mataifa unakwisha hivi karibuni. Wayahudi wanaenda kuchukua ufufuo. Mara tu wanapoweza kuona nguvu za Mungu zikidhihirisha na kumpokea Roho Mtakatifu, wataipokea Injili. Siku zetu za Mataifa zinakwisha.

Ingia katika Ufalme wakati una—una nafasi ya kuingia katika Ufalme.

22-1022

62-0513M – Mwenendo Wa Nabii Wa Kweli Wa Mungu

Ee Simba, wa kabila la Yuda, simama na ungurume!

Wewe unanguruma katika siku hii ya mwisho. Macho yako yamefinyaa. Unaangalia chini. Unaona dhambi za taifa hili na ulimwengu unaojiita wa Kikristo. Unaona dhambi ya taifa hili, wakati limenunuliwa kwa Damu ya thamani. Unaona jinsi madhehebu yanavyogaagaa juu ya Neno Lako. Unaona jinsi manabii wa uongo wanavyosema uongo. Wanaukana Ukweli wa Mungu .

Nguruma, Ee Simba wa Yuda! Jalia manabii wako wapaze sauti .

“Mungu anaponena, ni nani awezaye neno ila kutabiri?” Ni Neno la Mungu likitoka katika Biblia, likipitia kwa nabii. Anawezaje kutulia? Kama angetulia, angepasuka vipande-vipande.

Ee Mungu, jalia nabii Wako angurume, Bwana. Nguruma Ujumbe Wako, Mungu, na jalia kila kiumbe cha Ufalme Wako kisikilize .

Jalia wakome. Jalia wanawake wasimame na kujichunguza wenyewe. Jalia wanaume wasimame na wajichunguze wenyewe.

Jalia kila mhubiri anayesikiliza kanda hii, asimame na kujichunguza mwenyewe, kwa maana Simba wa kabila la Yuda ananguruma. Na Neno la kweli linawajia manabii, wanene, waseme kwa sauti kuu, “Tubuni mkageuke kabla ya kuchelewa sana.”

22-1021

64-1221 – Kwa Nini Ilibidi Iwe Ni Mchungaji Wa Kondoo

Naam, hiyo ndiyo sababu Musa alijua Sauti hii iliyokuwa imesema naye, ilikuwa ni Sauti ya Neno. Yeye alijua ya kwamba Mungu alikuwa amemwambia Ibrahimu, “Uzao wako utakuwa mgeni kwa muda wa miaka mia nne, bali nitawakomboa.” Naye alijua hiyo miaka mia nne ilikuwa imekwisha na alikuwa ameitwa kufanya hivyo.

Enyi wanaume kwa wanawake, Mungu aliahidi katika siku hizi za mwisho ya kwamba Yeye angewamwagia watu wote Roho Yake. Aliahidi angetuma Ubatizo wa Roho Mtakatifu, Naye angemwita Bibi-arusi bila waa wala kunyanzi. Aliahidi kufanya hivyo, Yeye atafanya. Usiwasikilize hawa wachungaji wa kukodishwa, watakupoteza.

Roho Mtakatifu ndiye Mchungaji wa kukulisha chakula cha kondoo kutoka kwenye Neno hili. Daima linakuja kwa Mchungaji. Yeye ndiye Mchungaji wetu. Msikieni, ninyi ni kondoo wa zizi Lake; kama ndivyo mlivyo, mnaisikia Sauti Yake. Si yale mtu mwingine yeyote asemayo, mnasikia yale asemayo. Sauti ngeni, hamna habari nayo.

22-1020

61-0224 – Msiogope

Sasa, kama ungemwendea Yeye, na Yeye alikuwa amevaa suti hii ambayo alinipa naye Angesema—ungesema, “Yesu, utaniponya?” Unajua angekuambia nini? “vema, mwanangu, nilikwishafanya jambo hilo.” Yeye Hawezi kulitenda tena.

Ikiwa umekombolewa kutoka kwenye duka la Rehani, unawezaje kukombolewa mara ya pili? Yeye Alikutoa . Alijeruhiwa kwa makosa yako na kwa kupigwa kwake Uliponywa. Unaona ninachomaanisha?

Uponyaji wako tayari umekamilika. Wokovu wako umekamilika. Kitu pekee unachopaswa kufanya ni kuupokea tu. Je, inaleta tofauti gani yeyote anayekuwekelea mikono, huyu anafanya nini, kile au kinginecho? Mahali popote ulipo, Liamini tu. Ni hayo tu. Lipokee. Ni Mungu apasaye kukupa wewe jambo hilo.

22-1019

64-0719M – Sikukuu Ya Baragumu

Na Biblia ilisema Yeye angefukuzwa kanisani, katika Wakati wa Saba wa Kanisa. Yeye angefukuzwa kanisani. Litakuwa jeusi kabisa, na liende…Linakuwa jeusi wapi? Linaingia katika utaratibu huu wa kidini, likaingia kwenye baraza hili la ekumenia, Baraza la Makanisa Ulimwenguni. Hilo…Yeye anatolewa nje kabisa.

Neno Lake, wao hata hawawezi kukubaliana Nalo. Mnajua hawawezi. Hawawezi kukubaliana katika makundi yao madogo ya mtaa; wao watakubalianaje katika jambo Hilo? Kwa hiyo, wao wanachukua alama nyingine ya mnyama, sanamu ya mnyama. Kumbukeni, Biblia ilisema, “Kulikuweko na sanamu iliyofanyiwa yule mnyama.”

Na Marekani hii daima imekuwa namba kumi na tatu. Ilianza na mikoa kumi na mitatu, koloni kumi na tatu; nyota kumi na tatu, milia kumi na mitatu; namba kumi na tatu, na daima ni mwanamke. Inatokea katika sura ya kumi na tatu ya Ufunuo.

Na, kwanza, ni mwana-kondoo; upole, uhuru wa kunena, uhuru wa dini, na kadhalika; halafu wanapokea mamlaka, na kunena kwa uwezo wote aliokuwa nao yule joka mbele yake. Ni nini? Yule joka alikuwa nini? Rumi. Mnaona, alikuwa na alama, sanamu ya mnyama, iliyoinuka dhidi ya Kanisa halisi la Mungu. Chini ya hayo madhehebu, watakitesa kitu hiki! Lakini, watakapoanza kufanya jambo hilo:

Mwana-Kondoo atamchukua Bibi-arusi Wake awe daima karibu Naye .

22-1018

61-0207 – Matarajio

Lakini mjapo pamoja, loo, jamani, ndivyo ilivyo, mtakapomtii Mungu kikamilifu. “Hivyo watu wote watatambua ya kuwa ninyi mmekuwa wanafunzi Wangu, mkiwa na upendo ninyi kwa ninyi.”

Unapotoa sehemu ya theolojia na kupata upendo mdogo mle ndani, itafanya kazi, na maajabu, na—na miujiza. Lakini tunapaswa kuwa na hilo. Kwa nani? Kwa kila mtu.

“Loo, kwa kundi lile la kale la Assemblies of God, ama lile kundi la kale la Church of God, ama la Kale la Umoja, au la Utatu, ama la Utano, ama cho chote kile walicho nacho? Ati Mimi niwapende? Siwezi kuwapenda; wao ni wapinga Kristo.” Umejipoteza mwenyewe, ndugu, unapofikiri hivyo. Hiyo ni kweli.

Hauko sawa na Mungu. Kama huwezi kuinua mkono kwa adui mkali zaidi uliye naye na kujaribu kumvuta kwa Kristo, basi Roho wa Kristo hayumo ndani yako. “Kwa maana alikuja kwa Walio Wake, wala Walio Wake hawakumpokea.” Hata hivyo alitoa maisha yake kwa ajili ya adui yake. Alifanya hivyo. Ni kweli jinsi gani.

Na huyo Roho wa Mungu ndani yako anakufanya ujisikie vivyo hivyo juu ya kila mtu .

22-1017

62-0122 -Thibitisho La Agizo

Biblia ilisema, “Injili haikutujia kwa neno tu, bali Katika Nguvu , madhihirisho ya Roho Mtakatifu.” Kwa maneno mengine, “Ni Roho Mtakatifu akichukua Neno la Mungu na kulidhihirisha.” Unaona? Na, vinginevyo, njia pekee ambayo ishara za Marko 16 zinaweza kumfuata mwamini ni kwamba Roho Mtakatifu Mwenyewe kuchukua Neno la Mungu na kulidhihirisha kwa watu. Ndivyo ilivyo. Sasa, imani hulifanya Neno hilo kuwa hai. Unaona?

Neno ni Mungu. “Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu.” Ndipo Yesu akasema, “Ninyi mkikaa ndani Yangu, na Neno Langu ndani yenu, ombeni mtakalo lote, mtatendewa.” Unaona?

Huko ni kukaa na Kristo katika Neno. Usiende kulia au kushoto. Kaa moja kwa moja nalo. Unaona? Na kisha kwa kweli si Neno lako, basi. Ni Neno Lake, na Neno Lake lina nguvu na mamlaka nyuma Yake .

22-1016

64-0830M – Maswali na Majibu #3

Ee, ni—ninampenda Yeye. Moyoni mwangu ninampenda, kama naujua moyo wangu. Naamini hata nanyi pia. Kwa hivyo pamoja sisi tu watoto Wake. Tunapendana. Sasa, siwezi kumpenda Yeye pasipo kuwapenda ninyi.

Na kama nikisema kuwa ninampenda Yeye nami siwapendi ninyi, Biblia ilisema, mimi ni mwongo. Ona?

Na kama nina… Kama mnataka—kama mlitaka kunipenda mimi au kupenda jamaa yangu…Chaguo lilikuwa, ninalotaka ninyi mfanye, mnipende au mpende jamaa yangu; mpende jamaa yangu, ningefurahiwa kama mngalimpenda Billy Paul kuliko kunipenda mimi. Kama ikifikia chaguo la kuamua la namna hiyo, ningefurahiwa mkifanya hivyo.

Nawatakeni mnisikize, kwa sababu Billy si mhudumu. Lakini nataka mnisikize mimi, yale ninayowaambia; lakini wakati—ukitaka kumpenda mtu fulani, kuwapenda sana, useme, “Nataka nimpende mmoja wenu, wewe au Billy,” mpende Billy. Ona?
Mungu ajisikia vivyo hivyo kutuhusu sisi. Nasi hatuwezi…Ndipo najua kuwa huwezi kumpenda Billy pasipo kunipenda mimi, kwa sababu yeye ni sehemu yangu. Ona? Kwa hivyo siwezi kumpenda Mungu pasipo kuwapenda ninyi, kwa sababu ninyi ni sehemu ya Mungu. Nasi tunapendana.

22-1015

53-0508 – Mungu Akimwagiza Musa

Akasema, Loo, loo, nili—nilidhani nilimpata Roho Mtakatifu nilipoamini. Bado wanafundisha hivyo, lakini ni makosa. Imani ni sawa. Imani ni nzuri sana. Imani ina…Ibrahimu alimwamini Mungu, nayo ikahesabiwa kwake na, au, kuwa haki, lakini Mungu akampa muhuri wa tohara kuwa muhuri wa imani yake.

Ndugu zanguni , unapokuwa na imani halisi na ya kweli katika Mungu, Mungu atakupa ubatizo wa Roho Mtakatifu kama muhuri wa ahadi, ambao ni muhuri, kwamba unayo imani. Unaweza kufanya—a—aina fulani ya hisia, ama kuwafanya watu waamini, ama unaweza kusema una imani, lakini unapokuwa na imani halisi isiyoghoshiwa, Mungu atakupa ubatizo wa Roho Mtakatifu kama muhuri wa ile ahadi. Amina. Hayo sio maziwa ya mtindi sasa, Enyi watoto .

Sasa kumbuka, Lichukue, Liamini. Weka imani yako kwake na lifungue huko na Mungu, na Roho Mtakatifu atakuja juu yako. Aliahidi hilo. Basi Ndipo, ndugu, Ibilisi anaonekana kama jamaa mdogo.

22-1014

56-0726 – Upendo

Si Kingine ila nafsi zilizopotea, ndicho kitu pekee ambacho kina thamani yoyote ile ndani yake.

Pesa hupita. Nyumba zinaharibika na kutoweka. Kila kitu kilicho katika nchi Huondoka.

Thamani pekee, thamani ya kudumu, ni afadhali niwe na nafsi moja katika utukufu, ambayo niliyompelekea Kristo, kujua na kuona kwamba Nuru hiyo ya Mungu inaizunguka nafsi hiyo, milele yote, jina langu lihusishwe nayo; kuliko kuwa na kila senti ya pesa katika dunia yote, maana nitaipoteza yote. Lakini Unayoyapeleka huko juu ni ya Milele .

22-1013

56-1207 – Karama

Sasa, angalia kwa makini. Sasa, Mungu akikaa ndani ya Kristo alitumia sauti yake kunenea. Yesu alisema katika muujiza wake, “Amin, amin, nawaambia, Mwana hawezi kufanya neno mwenyewe, ila lile analomwona Baba akifanya, ndilo hufanya Mwana vivyo hivyo. Je, hiyo ni kweli? Yohana Mtakatifu 5:19.

Basi hakufanya neno lolote kwa yeye mwenyewe. Hakuna nabii aliyewahi kamwe kufanya lolote kwa yeye mwenyewe , mpaka kwanza Mungu alipoonyesha la kufanya. Ni kosa la namna gani Musa alilofanya alipotoka bila ono la Mungu na kumuua yule Mmisri, akafikiri angewakomboa kwa mikono yake, kwa maana alifikiri alikuwa na imani nyingi na angeweza kufanya hivyo, kwa maana aliitwa kwa ajili ya kazi hiyo .

Haijalishi umeitwa kwa kazi hiyo jinsi gani, Inabidi Mungu aongoze. Unaona? Alishindwa kwa kisomo chake chote na akili yake ya kijeshi na mafunzo yake kama kiongozi mkuu wa Misri. Lakini hata hivyo ilishindikana, kwa sababu Mungu alikuwa na mpango nasi hatuna budi kufanya kazi kulingana na mpango wa Mungu.

Haijalishi tunafanya nini, sisi ni werevu kiasi gani, tunatakiwa kujinyenyekeza na kufanya kazi kulingana na mpango wa Mungu. Amina.

22-1012

50-0115 – Je, Unasadiki Hayo?

Na watu wakipita barabarani, walizoea, mbona, tungeshikana mikono na kupeana mikono namna hiyo, tukisema, “Habari yako, ndugu?” Na leo hii wanapopita barabarani, wanatoa tabasamu la kipuuzi kidogo, wanaweka vichwa vyao juu hewani. Loo, jamani. Si ajabu kwamba Upendo Umekwisha.

Nadharau Huko kujisikia kwa kale kwa Mtu fulani kuwa ni mkuu kuliko mtu mwingine. Hata Hivyo, wewe ni futi sita za dunia. Hayo ndiyo yote uliyo. Hiyo ni kweli, kila mtu.

Si muda mrefu uliopita, nilikuwa nimesimama karibu na jumba la makumbusho. Kuna picha ya mtu hapo, Ratili mia na hamsini. Nayo-inatoa uchambuzi wa kemikali za mwili wake. Ana thamani ya senti themanini na nne. Hiyo ndio thamani yote ya Mtu Mwenye Ratili mia na hamsini, ni senti themanini na nne .

Lakini atahakikisha Anaweka kofia ya dola kumi kwenye senti hiyo themanini na nne na kufikiria yeye ni kitu fulani kikubwa. Hiyo ni kweli. Mwanamke atafunika senti hiyo themanini na nne kwa koti la manyoya la dola mia moja na hatazungumza na nusu ya majirani zake.

Kuna nini? Upendo wa Mungu unakupeleka mahali fulani. Hiyo ni kweli .

Ni Kitu gani? Bado ni ile senti themanini na nne. Utaishughulikia hiyo ni sawa. Lakini nafsi hiyo ina thamani ya Dunia elfu kumi, nawe utaacha chochote kishushwe ndani yake. Hiyo ni kweli. Huo ni ukweli .

22-1011

50-0115 – Je, Unasadiki Hayo?

Sasa, nataka uangalie tofauti kati ya Mariamu na Zakaria. Zakaria, yule mhudumu, mhudumu wa Injili, au mhubiri, kama ilivyokuwa katika siku hiyo, kuhani katika hekalu, alikuwa amejua kila namna ya mambo yaliyotukia hapo awali kuhusu miujiza ya nguvu ya Mungu, lakini alimtilia shaka Malaika katika kesi yake. Ambapo Mariamu alisema, Tazama, mimi ni mjakazi wa Bwana .
Hakujiuliza ni nini kingekuwa kuwa au kadhalika. Na kutazama ni kiasi gani alipaswa kuamini zaidi ya kile ambacho alipaswa kuamini.

Hana alikuwa amepata mtoto hapo kabla , alipokuwa amepita umri. Sara alikuwa amepata mtoto kabla baada ya yeye kupita umri. Na hilo lilikuwa tayari limetukia mara nyingi.

Lakini Mariamu alipaswa kuamini jambo ambalo halikuwahi kamwe kutokea . Hakuna mwanamke aliyewahi kuleta mtoto duniani namna hiyo bila kumjua mwanamume.
Lakini alikuwa na mengi ya kuamini kuliko yale Zakaria aliyofanya. Kwa hiyo, yeye hakumswali Mungu; alimchukua tu Mungu kwenye Neno Lake. Amina. Nalipenda hilo.

Mchukue Mungu kwenye Neno lake. Liamini hata hivyo. Haijalishi jinsi gani Linavyoonekana kuwa haliwezekani, mwamini Mungu, Naye atalitimiza.

22-1010

63-0428 – Tazama

Wakati mwingine hatuwezi kungoja kutoka uamsho mmoja hadi mwingine. Inatubidi kutoka nje na kujitatanisha na mambo ya ulimwengu. Jinsi inavyotupasa kujionea aibu.

Kabla hatujaja hapa kukiri na kuingia ndani ya hiyo Damu ya Yesu inayotusafisha na dhambi yote, inatupasa kujilenga kikamilifu, tupate kumwona yule Mungu mmoja aliye hai amesimama pale, Yeye aliyefanya ahadi, ya kwamba, “Mbingu na nchi zitapita, bali Neno Lake haliwezi kushindwa.” Kaa papo hapo juu ya Hilo, ndipo hutatupwa huku na huko kwa pepo za mafundisho, ukichukuliwa mahali mahali, huku na huku .

Lakini, unajua mahali unaposimama, kwa maana umelengwa shabaha pamoja na Mungu. Unayaona maisha yako mwenyewe yakipiga ile shabaha, kama tu wale mitume walivyofanya. Unaishi jinsi walivyoishi. Ulibatizwa jinsi walivyobatizwa. Unaona matokeo yale yale waliyoona. Unaona likitenda kazi ndani yako. Umelengwa kikamilifu.

Sijali yale kampuni isemayo na yale madhehebu yasemayo. Umelengwa kikamilifu, kwa sababu unajua ya kwamba unapiga shabaha. Amina.

22-1009

54-0404M – Kuishindania Imani kwa Bidii

Loh, Mungu anataka kurejesha imani ile Waliokabidhiwa watakatifu mara moja. Unasema, “Ndugu Branham, hiyo ndiyo imani?” Usichukue taratibu za dini la Me—Methodisti, taratibu za dini la Kibaptisti, au taratibu za dini la Kipentekoste; chukua Biblia.

Hebu tuone walichofanya. Wote walikuwa katika chumba cha juu kwa nia moja, na kwa ghafula, upepo uleule wa nguvu ukienda kasi ukaja kutoka Mbinguni, ukaijaza nyumba yote walimokuwa wameketi.

Ulisema nini? Wakasema, “Looh, sijui nifanye hivi au la. Nikienda nje, watanifanyia mzaha . Nikisema chochote, ‘Kwa nini , alisema kuenda nje.’” La, bwana.

Roho Mtakatifu alikutana nao, kundi lile la jamaa waoga. Walipata uzima na wakapitia madirishani na milangoni, wakaingia barabarani, na wakatenda kama kundi la wendawazimu, na kujikongoja na kupiga mayowe na kupiga makelele na kila kitu, kama kundi la watu walevi; mpaka kanisa la kitamaduni la siku hizo likasema, “Watu hawa wamejawa na divai mpya.”

Na sikiliza, dada, wewe uliye na heshima sana kwenye kundi la kushona nguo kanisani kwako, na kadhalika, na una hadhi ya kijamii huko Louisville, New Albany, na Jeffersonville, bikira Mariamu aliyebarikiwa alikuwa mle ndani.

Na kama Mungu Mwenyezi alihitaji bikira Mariamu aliyebarikiwa, na hangemruhusu aje Mbinguni hadi apate tukio hilo, utawezaje basi kufika huko kwa kitu pungufu ya hilo?

22-1008

59-1108 – Kumiliki Malango Ya Adui

Mungu huleta mvutano kanisani, “Maana kila mwana ajaye kwa Mungu lazima ajaribiwe na athibitishwe, na ahakikishwe.”

Yeye huruhusu upatwe na ugonjwa. Yeye huachilia magonjwa yakujie, kukujaribu na kukuthibitisha, kuuonyesha ulimwengu ya kwamba wewe hakika u uzao wa Ibrahimu. Yeye huruhusu hayo kwa mapenzi Yake Mwenyewe.

Yeye huruhusu msiba, huruhusu marafiki kuwa kinyume chako. Huruhusu mambo hayo yote, na kumwachilia Shetani akujaribu, naye atafanya yote ila kuutwaa uhai wako.

Yeye angekutupa katika kitanda cha dhiki, angeruhusu jirani zako wakuchukie, angeruhusu kanisa likuchukie, anaweza kufanya karibu kila kitu, na ni mapenzi ya Mungu Kwake kufanya hilo. Tunafundishwa lina thamani zaidi kwetu kuliko dhahabu.

22-1007

65-0725M – Watiwa Mafuta Katika Wakati Wa Mwisho

Roho Mtakatifu ndiye Nabii wa wakati huu; Yeye analihakikisha Neno Lake, akilithibitisha. Roho Mtakatifu alikuwa ndiye Nabii wa wakati wa Musa. Roho Mtakatifu alikuwa Nabii wa wakati wa Mikaya. Roho Mtakatifu, aliyeliandika Neno, anakuja na kulithibitisha Neno.

Sasa ni nini kilitukia wakati wa Mikaya? Ahabu aliuawa, kisha mbwa wakairamba damu yake, kulingana na Neno la Mungu.

Enyi waalimu wa uongo nyote, ndivyo anavyosema Mungu, siku moja mtavuna mnayopanda, enyi viongozi vipofu wa vipofu! Sina hasira. Ninawaambieni tu Kweli.

Na nisingelisema jambo hili kama hapa, kwenye kile chumba, kama Roho Mtakatifu hakusema, “Liseme kwa njinsi hiyo.” Je! nimepata kuwaambia jambo lo lote lisilo kweli ila lile Mungu alilothibitisha kuwa ni kweli? Amkeni, ndugu zangu, kabla ya kuchelewa sana!

22-1006

63-1116B – Uwekezaji

Katika Ufunuo 3, tunasoma hili, kwamba Kanisa la Laodikia, tumechorwa mojawapo ya picha zenye huzuni kuliko picha zote za Biblia nzima, Ufunuo 3, kwenye Kanisa la Laodikia.

Makanisa mengine yote, kupitia Wakati wa Luther, na Nyakati Saba za Kanisa, kila mmoja, haikuninii, kasema kuhusu Yesu kuwa ndani ya kanisa, “Yeye aliye ndani ya kanisa .”

Lakini katika Laodikia, Yeye alikuwa nje, akibisha, akijaribu kurudi ndani. Ni kitu cha kusikitisha namna gani kuwazia, kwamba, “Mwana wa Mungu, akibisha katika kanisa Lake Mwenyewe, akijaribu kurudi ndani.”

Lakini utajiri wa ulimwengu huu umepofusha macho yao. Si tu tajiri wa pesa, bali tajiri katika umaarufu, tajiri katika mambo ya ulimwengu, mahangaiko ya maisha, mpaka mmechangamana, na watu wenye elimu wameingia ndani na kuondolea mbali hiyo Punje, ile—ile Lulu yenye thamani kubwa.

Lakini Mungu aliwachagua watu kimbele kuwa huko; mtu fulani anaenda kuwepo huko. Bali wao wanaikataa Hiyo. Si wote watakaofanya hivyo; baadhi yao wataipokea Hiyo.

22-1005

64-0719E – Kuenda Nje Ya Kambi

Kutoka nabii mmoja hadi mwingine, Yeye alisafiri, hata nabii wa mwisho alikuwa Malaki, ndipo hapakuwepo na nabii mwingine kwa miaka mia nne.

Ndipo Mungu akajitokeza tena. Siku moja Yeye akatembea miongoni mwao tena, bali mapokeo yao yalikuwa yamepachukua mahali Pake sana miongoni mwao, alikuwa mgeni kwao .

Mapokeo ya baba zao, walikuwa na kusafisha vyombo, na—na jinsi ya kutengeneza nywele zao, na kutia vifungo fulani kwenye makoti yao, na majoho ya makuhani—ya makuhani; na mmoja ni Mfarisayo shupavu, na mwingine ni Msadukayo .

Na jambo hilo lilikuwa limepachukua mahali pa Neno miongoni mwa hao watu, hata, Mungu alipowazuru, alikuwa mgeni.

Hebu niseme jambo hili kwa upendo na heshima, lakini kulisisitiza. Ni jambo lilo hilo leo hii. Haijabadilika hata kidogo.

22-1004

62-0204 – Ushirika

Sasa, tunataka kufikiria kumhusu Yesu na kumhusisha Yeye, kile alichokuwa Yeye. Mwili Wake ni nini? Mwili wa Kristo ni nini? Ni kundi la waamini ambao wanashirikiana na Yeye katika Roho Mtakatifu .

Si sanamu, si kipande cha mkate, bali Roho ambaye yuko ndani ya moyo wa mwamini, nao wanashirikiana pamoja, kwamba wakati mwanadamu na Mungu wanaweza kuzungumza mmoja kwa mwingine, wana na binti za Mungu.

Binadamu asiyedumu, kwa kumwaga Damu ilileta ondoleo la dhambi, na mtu huyu na mwanamke huyu, mvulana au msichana, ambaye ana ushirika pamoja na Kristo, anashirikiana Naye, mwili.

22-1003

56-0527 – Pale Kadesh-Barnea

Nilipokuwa nikifundisha leo, katika nyumba ambayo nilialikwa nje kwa chakula cha jioni. Walitaka kujua kama wangewajua wapendwa wao, watakapokutana nao Utukufuni.

“Vema,” nikasema, “hakika, tutawajua.” Unaona, tu—tuko katika…

Tuna miili mitatu tofauti tunayoishi ndani yake. Mmoja ni wa kibinadamu, mwingine ni wa kimbinguni, na mwingine ni wenye utukufu. Na kisha ikiwa tunajuana mmoja kwa mwengine katika mwili wa kibinadamu, mwili uwezao kufa, ni zaidi vipi tutajuana sisi kwa sisi katika mwili wenye utukufu!

Ni kama, kama sheria inaweza kuzaa kitu kizuri, neema inaweza kuzaa kitu kikubwa zaidi, kwa sababu ni kuu kuliko sheria!

Na ikiwa mwezi unaweza kutokeza kiasi fulani cha nuru, je! Ni zaidi vipi jua litauzidi litakapokuja! Nasi hakika tutajuana.

22-1001

64-0214 – Sauti Ya Ile Ishara

… Mwaminio yeyote wa Biblia, mwaminio halisi wa Biblia, huitikia kila moja ya ahadi hizi za Mungu kwa “amina.” Hiyo ni kweli.

Kama huwezi kuliamini lote…Unasema, “Vema, ninaamini hili, bali sijui kuhusu Lile.” Una mfasiri yule yule ambaye Hawa alikuwa naye. Alijaribu…Alijaribu kulifasiri kwa Hawa, “Loo, hili ni kweli, na lile ni kweli, na, loo, hilo kweli ndilo, lakini hakika Mungu…”

Mungu alisema hivyo, na kila Neno! Hakuna hata Neno moja wala sehemu Yake moja inayoweza kukosekana, kutokubalika. Usipolikubali kwa moyo wako wote, kila sehemu yake, basi afadhali usianze hata kidogo. Unaona?

Kumbuka, ilikuwa ni kifungu Chake kimoja kidogo cha maneno, kilichopinduliwa tu, ambacho kilisababisha kila ugonjwa, kila huzuni ya moyoni, kila kifo, kila kitu. Kilisababisha yote.

Kwa kutokuamini tu kifungu kimoja kidogo cha maneno, kulisababisha yote haya, je! unafikiri kukiuka tu maksudi kifungu kimoja kidogo cha maneno kutakurudisha? Wakati, watu hawakubali nusu Yake, mara nyingine, halafu wanajiita Wakristo. Unaona? Unaona?

Ni sawa, kila sehemu Yake ndogo, linapaswa tu kuwekwa pamoja. Na kuna Mmoja pekee anayeweza kufanya jambo hilo, huyo ni Roho Mtakatifu, kwa kulifasiri kwa kutimiza Kwake Mwenyewe kile alichosema angefanya .

22-0930

53-0831 – Mungu Alinena na Musa

Makanisa siku hizi, mengi yao, yanatafuta wachanganyishaji. Mtu fulani anayeweza kuchanganya na labda kufanya kidogo cha hili na lile, na tafrija ndogo, na kucheza gofu, na labda karamu chache na kadhalika.

Sasa, ulimwengu unatafuta wachanganyishaji wazuri, lakini Mungu anatafuta watenganishaji, wale ambao watakaojitenga wenyewe. “Tokeni kati yao, enyi watu wangu, msishiriki dhambi zao.” Jitengeni…

Katika Misri, wakati mwana-kondoo alipotolewa, Mungu alifanya utofauti. Aliwatenga—Waisraeli kutoka kwa—kutoka kwa Mataifa, na kuleta tofauti ndani yao.

Na watu wa Mungu ni watu waliotengwa, taifa takatifu, watu wa kipekee, wasio wa kawaida, wenye kutenda kiajabu .

Kwa hivyo ulimwengu hautakuelewa kamwe. Kwa hivyo usiwazie juu ya ulimwengu; waza juu ya Mungu. Hilo ndilo jambo kuu .

22-0929

55-0118 – Huyu Shujaa mkuu wa Vita , Daudi

Na kama Mungu hakukuchagua wewe kuwa Mkristo, usigekuwa Mkristo. Ni chaguo la Mungu, si lako .

Hakuna mtu amtafutaye Mungu. Hakuna mwanadamu amtafutaye Mungu wakati wowote. Wewe Hukumtafuta Mungu, lakini Mungu ndiye Aliyekutafuta. Si wewe uliyemwita Mungu; ni Mungu aliyekuita.

Ndipo Basi Mungu alipokuita, ilionyesha kuwa alikuchagua. Ukakubali wito, ilikuwa ni kuhesabiwa haki. Kisha ukatoa moyo wako kwa Kristo na ukajazwa na Roho Mtakatifu. Na sasa umewekwa mahali pako katika mwili wa Kristo .

Sasa, kama ilikufanya uache tabia zako za kale na kutenda kama Mkristo anavyopaswa kutenda, kama itakufanyia jambo hilo, itauponya mwili wako, maana ni ahadi. Amina. Haya basi.

22-0927

62-0909E – Katika Uwepo Wake

Kama tumekiri ya kwamba Yeye ndiye, tumekuwa katika Uwepo Wake, na tumetubu dhambi zetu, zimeondolewa kwenye kitabu cha kumbukumbu Lake. Hakuna mtu anayeweza kufanya jambo hilo ila Mungu .

Sasa, unaweza kunifanyia jambo lolote, nitakusamehe, bali nitalikumbuka. Kama ningekufanyia jambo lolote, ungenisamehe, bali utalikumbuka. Bali Mungu anaweza kusamehe na kusahau hilo. Wazia jambo hilo , “ hata halikumbuki !” Amina .

Hilo linanifanya nijisikie vizuri. Wakati ambapo hata halikumbukwi tena, hakuna kitu kinachoweza kufanya hivyo ila Mungu. Hakuna kitu kinachoweza kufanya hivyo ila Mungu.

Alisema angelifutilia mbali kutoka kwenye kitabu Chake cha kumbukumbu. Mimi siwezi kufanya hivyo, wewe huwezi kufanya, kwa sababu tuna hisi hizi ndogo tu zenye kikomo .

Bali Yeye hana kikomo, Mungu, Yeye anaweza kusahau kabisa kwamba lilipata kufanywa kamwe. Amina.

22-0926

62-0117 – Kudhania

Mtu fulani alisema, hivi majuzi, kasema, “Ndugu Branham, watu wanakuthamini wewe kama nabii. Kwa nini sana sana huwafundishi watu hao jinsi ya kupata karama za kiroho? Uachane na vile hao wanawake wanavyovaa nguo na jinsi hao wanaume wanavyotenda. Achana nao. Si kazi yako kuyasema hayo. Wafundishe mambo makuu, ya kiroho, yenye kilindi.”

Nikasema, “Ninawezaje kuwafundisha aljebra, wakati hawajui ABC?”
Unawezaje kuwapa elimu ya chuoni; hata hawajatoka kwenye shule ya chekechea? Hata hamna adabu ya kawaida kujisafisha na kutenda kama Wakristo, na kuvaa kama Wakristo, na kuishi kama Wakristo, na halafu kuzungumza juu ya karama za kiroho .

Tokeni kwenye shule ya chekechea. Wanadhani hayo ni sawa, bali ni makosa. Hampaswi kufanya jambo hilo . Mama zenu hawakufanya jambo hilo, hilo lilikuwa katika miaka ya Kipentekoste. Bali wanalifanya.

Na ninyi wanaume, jinsi mnavyoishi, mnawaacha wake zenu kufanya hivyo? Mngali mko katika shule ya chekechea. Mnaona? Hiyo ni kweli. Mnadhani ni sawa, bali si sawa .

22-0925

64-0215 – Vishawishi

Kumbukeni, Biblia ilisema, “Ninyi ni nyaraka zilizo hai, zilizoandikwa, zinazosomwa na watu wote.” Sasa, watu wengi hawatasoma Biblia, bali Mungu amekufanya wewe mwakilishi aliye hai. Wewe ni barua inayotembea, unapaswa kuwa Biblia inayotembea, Kristo ndani yako. Unapaswa kuwa Neno la Mungu linalotembea.

Na kama ukikiri kuwa Mkristo, nawe sivyo ulivyo, ushawishi wako, ninii yako…Kile unachoshawishi, kitakufanya uwajibike kwa nafsi za wengi ambao umewakengeusha, mbali na Kristo, katika Siku hiyo ya Hukumu .

Nafikiri inatupasa, usiku wa leo, kuwazia jambo hilo, kwa kuwa kila mwanamume, mwanamke, mvulana na msichana, anajua kwamba unakuja Hukumuni.

Huenda ukaepuka hili, lile, ama linginelo. Huenda ukaepa kodi ya mapato, na huenda ukaepa Mapato ya Ndani ya nchi. Huenda ukafanya jambo moja ama lingine. Huenda uliendesha gari kupita mwendo ulioruhusiwa na polisi wasikushike. Lakini, siku moja, Hukumu itakushika. Hiyo ni hakika!

22-0924

63-0721 – Yeye Hujali. Je! Wewe Unajali?

Nasi tunaamini ya kwamba madaktari huwasaidia watu. Ninaamini ya kwamba Mungu huponya kwa dawa. Mungu huponya kwa upasuaji. Mungu huponya kwa kuhurumiana. Mungu huponya kwa upendo.
Upendo kidogo tu huenda umbali mkubwa .

Hebu mtu awe amefadhaika sana, na hebu uwaonyeshe unawajali. Unaona? Mungu huponya kwa upendo. Mungu huponya kwa maombi. Mungu huponya kwa miujiza . Mungu huponya kwa Neno Lake. Mungu huponya! Hata chanzo chake kiwe ni kipi, Mungu huponya kwa hicho .

Mungu Ndiye aponyaye, kwa kuwa Yeye alisema, “Mimi ni Bwana akuponyaye magonjwa yako yote.” Kwa hiyo yote yanapaswa kutenda kazi pamoja, na watu katika huduma mbalimbali wanapaswa kufanya kazi pamoja kwa ajili ya jambo hilo. Unaona?

Sasa, bali hawafanyi hivyo, kwa sababu wakati mwingine wanakatazwa kuchukua misimamo fulani juu ya Neno la Mungu, kwa sababu madhehebu yao fulani hayawaruhusu kufanya hivyo. Bali hilo haliizuii ile Kweli, ni vile vile tu, Mungu anaendelea kuponya vivyo hivyo .

22-0923

56-0122 – Wakati wa Makutano

Siku moja, Biblia inasema, mambo yatatokea katika dunia hii na magonjwa na kadhalika, na watu wote watapata tauni, hata miili yao itaoza na kadhalika.

Lakini Biblia inasema, “Usimkaribie yeyote kati ya hao walio na Muhuri wa Mungu katika vipaji vya nyuso zao.”

Na Muhuri wa Mungu ni ubatizo wa Roho Mtakatifu. Sasa, ninyi ndugu wa sabato, sitaki kutokubaliana nanyi katika kuwa siku ya saba; hakuna Maandiko kwa jambo hilo. Lakini Biblia Waefeso 4:30 inasema, “Msimhuzunishe Roho Mtakatifu wa Mungu ambaye kwa yeye mlitiwa muhuri hata siku ya ukombozi wenu.”

Na alama ya mpinga-Kristo ni kumkataa huyo Roho Mtakatifu. Ambapo umetiwa muhuri nje ya Ufalme milele, bila, hakuna njia ambayo watasamehewa. Yeye anenaye vibaya kuhusu Roho Mtakatifu hatasamehewa kamwe katika ulimwengu huu au ulimwengu ujao. Hiyo hapo alama yako ya mnyama na muhuri wa Mungu katika konzi moja ndogo.

Muhuri wa Mungu ni ubatizo wa Roho Mtakatifu. Na alama ya mpinga Kristo ni kukana jambo hilo. Sasa, umetiwa alama kwa njia moja au nyingine. Je, hutaki kuwa na Roho Mtakatifu leo?

22-0922

51-0727 – Kanisa la Mungu Aliye Hai

Ikiwa umechoka na kusononeka na kujisikia kama kila mtu anakupinga, “Njooni kwangu ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha.” Hiyo ni mbegu .
Ikubali.

Na kama wewe ni mgonjwa, “Yeye Alijeruhiwa kwa makosa yetu, kwa kupigwa kwake sisi tumepona.” Ikubali. Ni mbegu: itazaa.

Unapopanda mbegu, huichimbui kila asubuhi ili kuona ikiwa imejitokeza. Ukifanya hivyo, mbegu yako haitajitokeza kamwe. Huna budi kuipanda, kuikabidhi ardhi, na kuiacha. Ni juu ya maumbile, Mungu, kuimwagilia maji na kuona kwamba inazaa. Hiyo Ni kweli ?

Hivyo ndivyo unavyofanya Neno la Mungu. Lipokee kwa moyo mzuri, uliokwisha rutubishwa, na wanyama wote watambaao, na mahali penye miamba, na mashaka ya jiwe yameondolewa, na katika udongo mzuri wa imani, na kuliamini, mkabidhi Mungu, na uende zako, Ukishuhudia kwamba umepokea kile ambacho Mungu alikuahidi. Naye ni Kuhani Mkuu wa maungamo yako, kutimiliza chochote ulichokiri kwamba amekwishafanya. Hiyo ndiyo Injili .

22-0921

63-0120E – Mara Nyingine Moja Tu, Bwana

Mungu aliliinua kanisa lipate kuwa ni mnara wa taa, kuziachilia nguvu Zake, kuwaponya wagonjwa, kuwafufua wafu, kuwatoa pepo, kuishi kitakatifu, kuihubiri Injili yote, kuidhihirisha, bali tunaanza kujipenyeza ndani na kushusha viwango .

Tulichukua mifano mibaya. Wanawake walimwiga mke wa mchungaji. Yeye alimwachilia aingie wazimu, kukata nywele zake, kuvaa namna yoyote ya nguo za kizinifu, kamwe hakumkemea.

Nao hao wanawake wengine wanasema, “Kama Dada Nanii anaweza kufanya hivyo, mimi pia ningeweza.” Usimfanye huyo mfano wako . Unaona? Mungu alikwambia jambo la kufanya, dumu na Hilo .

22-0919

55-1003 – Imani Katika Matendo

Nguzo ile ile ya Moto iliyowaongoza wana wa Israeli jangwani , Malaika yule yule wa Mungu aliyekuja kwenye—mahali pale na kumkomboa Petro kutoka kwenye nguzo, Bwana Yesu yeye yule aliyesimama mbele ya Paulo na kutuma ile nuru inayong’aa iliyompofusha macho yake. Na wale wanaume waliokuwa karibu naye hawakuweza kuona Nuru yoyote hata kidogo.

Lakini Paulo; ilimtoa macho . Naye alikuwa kipofu na ilimbidi aongozwe kwa mikono hadi mjini, nuru ilikuwa kali sana kumzunguka. Nuru iyo hiyo, Bwana Yesu Kristo yuko hapa usiku wa leo katika Utu Wake Uliofufuka na akijithibitisha Mwenyewe kwa ishara na maajabu yasiyoweza kushindwa kwamba Yeye yuko hapa .

Loo, Enyi watu, wekeni imani yenu katika matendo. Usiogope. Kwa nini, aibu kwako; usiogope. Simama imara katika uhuru ndani ya Kristo amekuweka huru. Usijitie kwenye kizimba cha ndege tena. Toka ndani yake. Vunja kuta hizo. Kristo alivivunjilia mbali viambaza vya katikati, akatuweka huru. Tuko tayari kuruka. Amina. Napenda jambo hilo .

22-0918

55-1110 – Maisha Yaliyofichwa Katika Kristo

Asubuhi moja, je, uliwahi kuamka mapema sana, kutoka nje mapema sana na kunusa hewa hiyo safi, jinsi ilivyo na jinsi kila kitu kinavyoburudisha?

Umande umeshuka. Loo, ndugu, dada, kama jambo pekee unalojua ni kwenda kanisani, kama jambo pekee unalojua kwamba ulijiunga au ulibatizwa, ama kitu kama hicho, kwa nini usifiche maisha yako pamoja na Kristo. Kaa peke yako katika utulivu, mbali na ulimwengu na mahangaiko yake yote, na kutulia na kutazama kuburudika jinsi kutakavyokuja .

Unajua, Isaya alinena habari zake wakati mmoja. Alisema, “ amri juu ya amri kanuni juu ya kanuni; huku kidogo, na huku kidogo: shikilia sana yale yaliyo mema .
bali kwa midomo ya watu wageni, na kwa lugha nyingine nitasema na watu hawa;
Na hii ndiyo Sabato (ama kuburudika) ambakl kunapaswa kutoka katika Uwepo wa Bwana.”

22-0917

51-0729E – Muujiza wa Pili

Kataa kusaini lolote analoleta shetani. Atalazimika kukirudisha. Sema, “Ninakataa kukipokea. Siwezi kukipokea, la, bwana.” Itabidi akirudishe kwa Jina la Bwana.

Kama unaamini jambo hilo , na kukikiri, na kusema, “Nimemkubali Yesu Kristo kama Mponyaji wangu,” hakuna mateso au ugonjwa unaoweza kukaa juu yako. Dumu moja kwa moja nalo. Lakini mara ya kwanza unapodhoofika na kusema, “Vema, ndio, bado ninao.” Ndipo Basi unaporomoka hadi pale ulipokuwa.

Ulisaini jambo hilo, kisha ukalirudisha tena. Kusema, “Ndiyo, Bwana. Ibilisi, ni—nitaurudisha.” Loo, ndugu. Simama papo hapo ilimradi kuna pumzi mwilini mwako, sema, “ Ninakataa kuwa nao. Ninakataa kuwa nao.” Je, unajisikiaje? “Vizuri Sana , haleluya.” Hivyo ndivyo. Hiyo ni kweli .

Mwonyeshe shetani umeumbwa kwa kitu gani; umezaliwa mara ya pili kwa Roho wa Mungu, wala huna haja ya kuziinamia sanamu zake. Kaa papo hapo, useme, “Sitaki vitu vyako.” “Mbona, hili hapa jina lako, daktari alisema…” “Sijali alichosema. Najua Alichosema Mungu. Ondoka nalo hapa.” Hiyo ni kweli, hiyo ndiyo njia ya kumkabili; kirudishe .

Yeye ndiye aliyekupa kitu hicho , itabidi awe ndiye atakayekirudisha .

22-0916

61-0903 – Vivyo Hivyo Nuru Yenu na Iangaze Mbele ya Watu

Lakini ni kama vile mtu ungalikuwa na gari kuu kuu na ulikuwa unapanda mlima, nami nilijua wakati ulipoanza kuteremka upande wa pili hukuwa na breki. Mimi nisingekuwa na kitu dhidi ya mtu huyo, ninayepigia makelele. Si yeye. Ni lile gari alilopanda. Ataumia .

Na hivyo ndivyo ilivyo kuhusu madhehebu. Ninafikiri watu wanaoshikilia madhehebu hayo, kana kwamba yalikuwa ni Mungu Mwenyewe, nao wanaliacha Neno la Mungu, wapate tu kushikilia madhehebu .

Vema, wanapofanya jambo hilo, ninasikitika watafanya kosa baya sana.

Si kwamba mimi nina jambo lo lote dhidi ya mtu huyo, bali ni huo mtumbwi aliopanda, unaona, nina hakika hatamaliza safari. Madhehebu hayatafaulu kamwe, bali Kristo atafaulu.

Kwa hiyo toka tu kwenye—kwenye huo mtumbwi unaovuja wa umadhehebu, uingie kwenye Meli ya salama ya Sayuni, ile Meli ya kale ambayo bado haijashindwa kamwe kutua pwani mapema, Kristo.

22-0915

63-0112 – Ushawishi

Sikuzote sikilizeni. Tambua udogo wako .

U nani wewe? Ingiza kidole chako kwenye ndoo ya maji na kukitoa, kisha tafuta shimo ulimoingiza kidole chako. Kisha useme, “Huyo alikuwa ni mimi.” Wewe si kitu.

Hutakumbukwa baada ya, muda mfupi baada ya wewe kuondoka. Wana msafara wa mazishi hapa nje, na ni hayo tu. Lakini ushawishi wako utaendelea kuishi, na kuendelea, na kuendelea.

Hiyo ndiyo sababu leo hii, katikati ya makafiri, kamwe hawajawahi kuelezea na kupata njia ya kuuondokea ushawishi wa Mtu mmoja, Yesu Kristo, Yule aliyekuwa ni Mungu aliyefanyika mwili.

Wakati alipoutoa uhai Wake huku chini duniani, ulifanya mahali pa kufyonza ambapo huwavuta watu wote Kwake, katika ule mzunguko mkuu wa maisha Yake yaliyokuwa duniani wakati mmoja. Huwezi kuukaribia pasipo kuingizwa ndani yake.

Lakini, mimi na wewe, sisi si kitu. Sisi si kitu .

22-0914

54-0306 – Agano lisilo na Masharti Ambalo Mungu Alilofanya na Watu Wake

Huwezi kamwe kujifanya kitu usicho. Ikiwa unaiga tu Ukristo, haijalishi kama unahubiri Injili, unahitaji wito wa madhabahuni katika nafsi yako. Hiyo ni kweli .

Ikiwa unajaribu tu kutenda kama mtu huyo ambaye ni Mkristo, wewe mwenyewe ni mwenye Mashaka, ukijua moyoni mwako mwenyewe hauko hivyo .

Na kama matunda ya Roho hayakufuati: uvumilivu , wema, upole, utu wema, saburi, basi unahitaji wito wa madhabahuni moyoni mwako.

Uliogopa tu kuzimu na ukaanza kujaribu kuwa Mkristo. Mungu hana budi kukuita kuwa Mkristo. Mungu alimwita Ibrahimu. Akampa…Alimteua .

22-0912

57-0303E – Mwaonaje Katika Habari za Kristo?

Mwingine aliandika.

Maishani, alinipenda, kufani, akaniokoa
Alipozikwa, akaondolea mbali dhambi zangu ;
Alipofufuka , akanihesabia haki bure milele: Yuaja siku moja, Ee, siku tukufu !

Mwaonaje katika habari za Kristo na ni Mwana wa Nani? Mna maoni gani juu yake? Mwaonaje kumhusu yeye?

“ William Branham, una maoni gani?” Loo, jamani. Kama ningekuwa na lugha milioni kumi za kunena nazo, nisingeweza kamwe kueleza mawazo yangu Kwake. Nikiwa nimelala kule kitandani, kutoka katika familia yenye dhambi, nao madaktari wakanitazama na kusema, “Una dakika tatu za kuishi.” Na ghafla Kitu fulani kikanijia ; alikuwa ni Mwana wa Mungu aliyebarikiwa ambaye aliniokoa kutoka katika dhambi, na kuponya macho yangu yaliyopofushwa, na kuniweka nje kuhubiri Injili .

Loo , jinsi ninavyompenda, jinsi ninavyomwabudu. Nisingeweza kueleza naonaje katika habari Zake. Tunapaswa kuwa watu wa namna gani?

22-0911

53-0325 – Israeli na Kanisa #1

Alipokea ile ahadi kabla ya kutahiriwa. Kisha alipewa tohara kama muhuri wa utii wake wa imani.

Sasa tunaposema…Hiyo ndiyo sababu Billy Graham, Charles Fuller, na Billings na hao wote, kwa nini wanazungumza juu yao, hao ndugu Wabaptisti. Niliwaambia wengi wao hivyo, Rufus Mosley na kundi hilo lolote. Nilisema…

Akasema, “Vema, tulikuwa na waongofu elfu ishirini katika majuma mawili. Hawakuweza kupata watu ishirini.” Nikasema, “Hawakuongoka.” “Loo,” akasema, “walimkubali Kristo kama Mwokozi wao kibinafsi.”

Nikasema, “Hata hivyo, hawajaongoka.” Hiyo ni kweli . Hujaongoka mpaka…Kuongoa maana yake ni “kubadilishwa.” Na mtazame, Paulo…

Petro alikuwa amemwamini Bwana, alikuwa amebatizwa, akapewa uwezo wa kuponya wagonjwa, kutoa pepo, kufufua wafu. Na Yesu akamwambia, usiku kabla ya kusulubishwa, “Baada ya wewe kuongoka, mwimarishe ndugu yako.” Hiyo ni kweli? alikuwa ameokolewa na kutakaswa pia, na hata hivyo hakuwa ameongoka. Hayo ni Maandiko.

22-0910

63-0707M – Lile Shtaka

Walimshtakije? Kwa sababu kanuni zao za imani hazingalimkubali. Na ndani mioyoni mwao walijua tofauti .

Je, si Nikodemo, katika sura ya 3 ya Injili ya Yohana, alieleza vema? “Rabi, sisi, Mafarisayo, wahubiri, waalimu, twajua ya kuwa Wewe u mwalimu, kutoka kwa Mungu; kwa maana hakuna mtu awezaye kufanya ishara hizi uzifanyazo Wewe, isipokuwa Mungu yu pamoja naye.” Mwaona?

Wao waliishuhudia hadharani kupitia kwa mmoja kati ya watu wao mashuhuri. Ingawaje, kwa ajili ya kanuni za imani zao wao walimsulubisha Kristo .

Na leo hakuna msomaji ambaye hawezi kusoma Matendo 2:38 kama vile mimi niwezavyo kuisoma, na mengineyo jinsi mimi niwezavyo kuyasoma. Lakini kwa ajili ya kanuni za imani zao na kwa ajili ya—ya tikiti zao za kidhehebu walizo nazo mifukoni mwao (ile chapa ya mnyama wanayoibeba kama kadi ya ushirika )…

Na kwa kuchukua mambo hayo, wao humsulubisha Yesu Kristo upya kwao wenyewe, na kumsulubisha kwa umma; na kukufuru Mungu yule yule aliyeahidi kutenda hili, wakileta laana juu ya kizazi hiki.

22-0909

53-0405S – Nenda, Uwaambie Wanafunzi Wangu

Ilikuwa asubuhi na Mapema moja. Waliuweka mwili Wake ardhini, kwenye Sabato, ambayo ilikuwa desturi kwamba hawakufanya lolote siku ya Sabato . Kwa hiyo Alikufa Ijumaa alasiri, saa tisa, na akafufuka kweli Jumapili asubuhi na mapema .

Sasa nataka kusuluhisha swali hili, mkiwapo hapa asubuhi ya leo katika ibada hii ya mapambazuko. Watu wengi husema, “Inakuwaje basi kwamba Yeye alisema ya kwamba angelala…Alikuwa kaburini, siku tatu mchana na usiku?” Hakusema kamwe kwamba angefanya hivyo.

Alisema, Katika siku hizi tatu nitaufufua mwili wangu. Unaona? Sasa, sababu ya Yeye kufanya hivyo ni kwa sababu Daudi alikuwa amesema, mahali pamoja katika Maandiko, “Sitaiacha nafsi Yake kuzimu, wala sitamwacha Mtakatifu Wangu aone uharibifu.” Naye alijua ya kwamba uharibifu uingia katika mwili wa mwanadamu baada ya masaa sabini na mawili, siku tatu mchana na usiku. Na mnamo wakati fulani ndani ya siku hizo tatu mchana na usiku, Mungu alikuwa anaenda kumfufua.

Kwa hiyo alikufa siku ya Ijumaa alasiri saa tisa, na akafufuka Jumapili asubuhi na mapema .

22-0908

56-0115 – Makutano ya Nyakati

Huwezi kula supu iliyo na nzi ndani yake. La, bwana. U—usingefanya jambo hilo. Usingekuwa…Ungeogopa kula chakula ambacho hakionekani sawa, na kilikuwa kimeambukizwa. Kwa sababu, unajua, kinaweza kukupa sumu ya uozo au kitu fulani, na kingekuua baada ya muda mfupi.

Nawe unahujali mwili huu. Lakini, nafsi hiyo, unaiacha ifurahie mambo ya dunia, ambayo unajua kwamba yameambukizwa na yanaweza tu kufanya jambo moja, kukupeleka kwenye maangamizi.

Haijalishi jinsi gani unavyoutendea mwili huu vizuri, na chakula kizuri jinsi gani , au jinsi unavyoishi, hauna budi kwenda kwenye mavumbi ya ardhi. Lakini nafsi hiyo itaishi milele, mahali fulani .

Afadhali nile supu iliyoambukizwa kuliko kuiambukiza nafsi yangu kwa mambo ya ulimwengu, wakati wowote .

22-0907

53-0729 – Maswali na Majibu Juu ya Kitabu Cha Mwanzo

Kama nilienda mezani kwako na kuketi pale, nawe ukasema, “Mhubiri karibu ule pamoja nami,” naamini unanipenda. Na una maharagwe na viazi na karoti na kuku iliyokaangwa na sambusa ya boga na maziwa ya mtindi, kila kitu kimewekwa pale.

Basi, naamini ningekaribishwa tu viazi jinsi ningalikaribishwa maharagwe. Jambo ni kwamba, naamini ningekaribishwa kuku kama nilivyokaribishwa sambusa. Vyote viko mezani. Na kitu pekee kinipasacho kufanya ni kusema, “Waweza nisogezea sambusa tafadhali?”

Nami naamini kwa moyo mzuri na mkunjufu, upendo wako kwangu, ungesema, “Naam, ndugu yangu, chukua kipande kikubwa kitamu.” Sivyo? Kama ningesema, “Tafadhali nisogezee viazi?” “Naam, hakika, ndugu yangu, hivi hapa”

Na kila baraka ya ukombozi ambayo Yesu Kristo aliifia na kuinunua katika utakaso Wake Kalvari, iko mezani na kila mwamini anaketi mbele yake . Haleluya!

Kama nahitaji uponyaji, nitasema, “Baba, nisogezee uponyaji,” nami naumwaga kwenye sahani yangu na kula kikubwa …Naam, ukitaka kufa kwa njaa, endelea .

22-0906

53-0906A – Je, Unayasadiki Hayo?

Mungu atanena, na hakuna kitu kinachoweza kuliondoa Neno la Mungu. Neno la Mungu hudumu milele. Wakati Mungu anapolinena, limethibitishwa mbinguni milele. Liko tayari papo hapo, sawa tu na limekwisha tendeka, wakati Mungu anapolinena .

Loo, ili sisi wanadamu tuweze kusema, “BWANA ASEMA HIVI; imetatuliwa,” kumchukua Mungu kwenye Neno Lake na kusimama pale haidhuru ni nini kitakachokuja, ni njia ngapi zinazosukuma kando. Tunadumu sawa na Neno la Mungu .

Mungu alisema hivyo. Ninaliamini. Hilo latosha.” Amina.

22-0905

52-0713A – Uzoefu wa Kiroho wa Mwanzoni

Mungu wa Agano la Kale alikuwa ni Yesu wa agano Jipya, na Roho Mtakatifu wa leo. Mnajua jambo hilo. Je, hamuamini jambo hilo ? Kumkufuru Roho Mtakatifu leo, ni adhabu ile ile tu, au mbaya zaidi, kuliko kumkufuru Yesu Kristo, au Mungu Baba. Je, hamuamini jambo hilo?

Sasa, nini zaidi? Sasa, tazama. Ikiwa ulimwengu unatuita wendawazimu . Ikiwa ulimwengu unafikiri kwamba tuko karibu nusu tu hapa…Angalia. Kwa sababu ishara hizo zilionekana mahali nilipo, na Malaika huyu wa Bwana, na kadhalika, hiyo haimaanishi kwamba ni mimi tu, marafiki .

Hiyo ina maana gani? Mungu anajaribu kuwaleta wapi? Anajaribu kuwaleta kwenye jambo hili, kwamba mimi ninawaambia ukweli.

22-0904

62-0128M – Kutokuamini hakumzuii Mungu

Kutokuamini ni kwa Kale tu kama Edeni. Hapo ndipo kulipozaliwa, ilikuwa Edeni. Na kutokuamini ni kutilia shaka yale aliyoyasema Mungu .

Sasa, je! uliona mahali ambapo kutokuamini kulipozaliwa, kulikuwa na Neno kubwa la Mungu lililozingatiwa, kwa maana Shetani alimwambia Hawa…Aliposema, “Mungu amesema,” yeye hakukana jambo hilo, ya kwamba Mungu alikuwa amesema, “hivi -na-vile”; lakini akasema: “Hakika Mungu hatafanya jambo kama hilo.”

Unaona, huko kulikuwa kuzaliwa kwa kutoamini: kubadilisha hata chembe moja kutoka kwa Neno kamilifu la Mungu. Hatuna budi kudumu nalo moja kwa moja, haidhuru ni wapi, ama nini, ama vipi, maisha yetu na kadhalika lazima yalingane na, BWANA ASEMA HIVI.

22-0903

57-0922E – Waebrania, Mlango Wa Saba #2

Lakini, sasa, ninaamini ya kwamba Biblia inafundisha habari za jehanamu halisi inayowaka moto. Biblia inafundisha jambo hilo, ya kwamba dhambi na uovu hayo yataadhibiwa, milele na milele. Hiyo si Umilele, sasa.

Hiyo huenda ikawa ni kwa miaka bilioni kumi. Huenda ikawa ni kwa miaka bilioni mia moja, lakini wakati fulani haina budi kukoma. Kwa kuwa, kila kitu kilichokuwa na mwanzo, kina mwisho. Ni vitu vile visivyo na mwanzo, havina mwisho .

Mnakumbuka somo hilo sasa ? [Kusanyiko linasema, “Amina.”—Mh.] Jinsi tulivyorudi nyuma na kupata ya kwamba kila kitu kilichokuwa na mwanzo kilikuwa kimepotoshwa, unaona, kupotoshwa kutokana na kitu chenyewe cha kwanza. Na, hatimaye, ni jambo linaloishia katika Umilele. Ndipo basi kuzimu yote, mateso yote, na kumbukumbu lote la hayo, vitatoweka Milele. Kila kitu kinachoanza, hukoma .

22-0902

57-0301 – Kipofu Bartimayo

Unajua kuna kitu kuhusu kuwa peke yako .

Watu wengi hawaombi mpaka waje kanisani. Watu wengi wanafikiri kwamba mahali pekee pa kusali ni kanisani, lakini Biblia ilisema wanaume wasalishe kila mahali, huku wakiinua mikono iliyotakata .

Na kisha tunapokuwa peke yetu, kwa kawaida tutaomba tofauti na vile tungeomba ikiwa tungeomba kanisani .

Ni maombi ya siri ambayo Yesu alizungumza, akisema, “Ingieni katika chumba cha ndani, na mfunge mlango, na mkiisha kufanya hivyo, mwombeni Baba yenu aonaye sirini; na aonaye sirini atakujazi .”

Na tunapoomba namna hiyo, inaonekana kuna kitu kwenye maombi ambacho huondoa unafiki wote ndani yake. Inaonekana kwamba tunapata muunganiko bora zaidi na Mungu, kuwa peke yetu .

Na kumekuwa na mara nyingi maishani mwangu, kama pengine katika maisha yako, kwamba inakupasa tu kuwa peke yako na Yesu mara moja kwa muda.

22-0901

62-0610E – Kushawishika Kisha Kuhusika

Nimeshawishika kwamba Yeye ni yeye yule jana, leo, na hata milele .

Nimeshawishika, katika hii huduma na huu Ujumbe, ninaohubiri, nimeshawishika kwamba ni Kweli .

Nimeshawishika ya kwamba maono haya yanatoka kwa Mungu .

Nimeshawishika tunaishi katika siku za mwisho .

Nimeshawishika ya kwamba Roho yuyu huyu aliye juu yangu ni Roho Mtakatifu . Utukufu!

Nimeshawishika kabisa. Nimeshawishika kwamba njia ya Roho Mtakatifu ni ya kweli .

Nimeshawishika ya kwamba njia ya Biblia ni ya Kweli .

Nimeshawishika ya kwamba Huyu ni Yesu Kristo hapa sasa .

Nimeshawishika. Kama tukimwamini dakika hii, nimeshawishika kwamba Yeye angeponya kila mtu mgonjwa katika dakika moja, kufumba na kufumbua jicho .

Nimeshawishika Yeye angemwaga Roho Mtakatifu juu ya mahali hapa, mpaka kungekuwako na kelele kubwa mno, hata ingekuwa ni vigumu kujua yale yangetukia .

Nimeshawishika. Ninaliamini kwa moyo wangu wote …

22-0831

62-1124E – Mambo Yote

Tangu Adamu mpaka sasa, mwanadamu amejaribu kujifanyia Kibadala chake yeye mwenyewe . Mwanadamu amejaribu mara kwa mara kufanya jambo hilo, kutoka kwenye majani ya mtini hadi kwenye elimu . Amejaribu kujifanyia Kibadala .

Adamu alionyesha yaliyokuwa ndani ya mwanadamu, alipojaribu kurudi kwenye majani ya mtini .

Tangu wakati huo, walijenga minara, wakajenga miji, wakajenga sanamu, wakajenga ustaarabu, wakajenga madhehebu, wakajenga tawala za kisayansi, na mambo haya yote, lakini bado yanabaki vile vile: Damu pekee ndiyo Mungu atakayokubali .

Mungu humkubali mtu kupitia Damu iliyomwagika tu .

22-0830

52-0720A – Hadithi ya Maisha

Na sisi kila mmoja wetu ana maisha ambayo Mungu ametupa, na ni lazima tuyaishi. Nami…Kwa maoni yangu Manyenyekevu, ikiwa utapata haya, nafikiri maisha bora zaidi duniani, haijalishi kama yako juu au chini, ikiwa tutapata njia ya Mungu na kutembea ndani yake ambapo Mungu ametuagiza tuenende .

22-0829

61-0215 – Ewe Mwana Wa Daudi, Unirehemu

Mungu aliwaambia huko chini kabisa Misri, “Nimewapa nchi hiyo.” Bali Yeye hakusema, “Nitaenda huko nje na kuwafagilia mbali, na kuzipamba nyumba, na kuweka mapazia, na kila kitu. Nyote mwingie tu.” La, la .

Iliwabidi kupigania kila inchi ya ardhi waliyoiteka . Hiyo ni kweli, kupiga vita, na kuiteka kwa kila…kupiga vita kila inchi. Bali Yeye alisema, “Kila mahali nyayo za miguu yenu zitakapokanyaga, huo ni umiliki.” Nyayo za miguu ni umiliki.

Hilo ndilo jambo lile lile siku hizi. Uponyaji wa Kiungu ni wetu. Roho Mtakatifu ni wetu. Ni mali yetu, bali itakubidi kupigania kila inchi yake . Naam, bwana. Lakini ndugu, nyayo za miguu ni umiliki. Endelea tu kupiga vita. Iteke. Ibilisi anasema, “Siku za miujiza zimepita.”

Sema, “Unadanganya. Mungu alisema Yeye ni yule yule jana, leo, na hata milele.” Iteke. Kila mahali mguu wako utakapokanyaga, huo ni umiliki . Hiyo ni kweli.

22-0828

54-1212 – Aliapa kwa nafsi yake

Tembea bila kuwazia woga. Tembea bila kuwazia ukosoaji . Tembea bila kuwazia ulimwenguni . Tembea, kama unavyoenenda katika Kristo, tembea pamoja naye. Bila kujali, mkono wa kulia au wa kushoto; wewe endelea tu .

Kama kuna jambo likitokea kanisani; tembea pamoja na Mungu . Haleluya!

Ugonjwa ukikupata; tembea pamoja na Mungu . Ikiwa jirani hakupendi; tembea pamoja na Mungu. Endelea tu kutembea pamoja na Mungu .

Enoko, siku moja, alitembea namna hiyo. Unajua alichofanya ? Alitembea njia yote kwenda Nyumbani, pamoja na Mungu; alifika mbali sana barabarani, hakutaka kurudi tena . Amina.

Tembea pamoja na Mungu!

Daktari anasema utakufa; tembea pamoja na Mungu. Ndiyo. Daktari anasema huwezi…Vema, tembea pamoja na Mungu. Wewe tembea tu Pamoja na Mungu, ni hayo tu .

Kwa maana Mungu amekuahidi, “Sitakuacha kamwe wala sitakupungukia. nitakuwa pamoja nawe hata mwisho wa dahari.” Naye aliapa, kwa lile agano alilokupa, ya kwamba atalithibitisha. Tembea tu pamoja na Mungu, basi .

Utakuwa na mema na mabaya yako. Usijali. Huna budi kupitia sehemu zenye michongoma, juu ya miamba mikali, juu ya mawe, chini ya vilima, juu ya milima, juu ya maji; bali tembea pamoja na Mungu . Ndiyo, bwana.

” Kuna vilima vingi vya kupanda, kwenda juu,” umeusikia wimbo huo wa kale , ” lakini itaonekana ndogo jinsi gani ufikapo mwisho wa njia.”

jamani, jamani! Angalia tu pale, yote ambayo yamekuwa, angalia nyuma kwenye nyayo zako; haitakuwa nyingi .

22-0827

63-0601 – Njoo, Unifuate

Enyi watoto, ninyi, kila mmoja, mnaonekana kama wangu. Ninyi, kila mmoja, mnaonekana kama tu wana na binti zangu. Kwa njia moja, ndivyo mlivyo, mnaona, tukinena kiroho . Hiyo ni kweli.

Bwana Mungu ame—ameziweka nafsi zenu katika ulinzi wangu, kwa sababu mnakuja, kunisikiliza. Mnaniamini mimi. Mnaona?

Na katika maana moja ya neno hilo, ninyi ni wana na binti zangu . Hiyo ni kweli.

Daima kumbukeni, kuzishika amri za Mungu ni jambo kuu. Kulelewa katika nyumba nzuri ni urithi kutoka kwa Mungu. Na kuwa watoto wazuri wenye haiba kama mlivyo nazo , vema. Vizuri sana, kuwa na elimu . Ni vizuri sana hata kuishi katika nchi hii huru. Tuna mambo mengi ya kutolea shukrani .

Ila kuna kitu kimoja ambacho hukirithi. Inakubidi kukikubali. Hicho ni Uzima wa Milele. Nawe utafanya hivyo tu kwa kumfuata Yesu, kwa ujuzi wa kuzaliwa mara ya pili. Usipuuze hilo .

22-0826

64-0312 – Macho Yao Yalipofumbuliwa, Walimtambua

Ibrahimu alitambuaje hilo? Sasa, Ibrahimu alimwita, “Elohimu.” Ni wangapi wanaojua hiyo ni kweli, wasomaji wa Biblia? Naam, bwana. Elohimu ni Yule ajitoshelezaye kwa yote, yule Muumba mkuu Mwenyewe. Ni kwa nini alimwita Elohimu? Kwa sababu Yeye aliweza kutambua mawazo yaliyokuwako moyoni. Hilo ni Neno.

Waebrania 4, ilisema—ilisema, “Neno la Mungu ni kali kuliko upanga ukatao kuwili, lachoma hata kugawanya viungo na mafuta yaliyomo ndani yake, na huyatambua mawazo na makusudi ya moyo .”

Hivyo ndivyo, manabii, Yesu aliwaita, “miungu.” Hivyo ndivyo Yesu alivyojitambulisha Mwenyewe, ndipo mwanamke huyo alijua Yeye alikuwa ni Neno, Yeye angeweza kutambua mawazo. Naye Yesu alisema, “Kama ilivyokuwa katika siku za Sodoma, ndivyo itakavyokuwa katika kuja kwake Mwana wa Adamu, anapofunuliwa Mwana wa Adamu .”

Limefanyia nini macho yako? Je! anaweza kuingia ndani, usiku wa leo? Ninatumai anaweza .

22-0825

65-0410 – Muhuri Wa Pasaka

Ninashangaa, leo. Ni yale yanayotendeka. Je! hivi kweli sisi tunawapeleka watu kwa Mungu, ama tunawapeleka tu kwenye kanisa ?

Hatuna budi kuwapeleka kwa Kristo, ambako kuna nguvu hizi za kuhuisha. Ni vizuri kwenda kanisani. Hakika. Kama huo ndio umbali tunaofikia, si umbali wa kutosha .

Unapokuja kanisani, hilo ni jambo zuri; bali nenda hadi kwa Kristo, unapotoka kanisani, kwa kuwa hatuna budi kupokea nguvu hizi za kuhuisha, ikiwa tunatarajia kuwa kwenye ule ufufuo wa watu wote, kwa sababu ndicho kitu pekee kitakachotufufua kutoka kwa wafu .

“ Kwa kuwa ikiwa Roho huyu aliyemfufua Yesu toka kwa wafu anakaa ndani yenu, pia ataihuisha, ataifanya, ataifufua miili yenu iliyo katika hali ya kufa .” Ni ahadi ya jinsi gani kwetu !

22-0824

57-0420 – Kuzikw

Na kila kitu duniani, uzuri, utamu, uzuri wa dunia, si kitu kingine ulimwenguni ila ni jibu la kilicho bora kuliko hicho, ambacho kinatungojea tunapouacha ulimwengu huu.

Kwa maana, kila kitu duniani ni mfano tu wa kile kilicho Mbinguni. Kila kitu kizuri, kila kitu ambacho ni cha haki, kila kitu kinachovutia, miti, ndege, kila kitu, ni mfano tu wa kile kilicho Mbinguni .

Maisha yetu yenyewe ni mfano tu. Ni kivuli tu, wala sio kitu halisi. Ni upande hasi. Inahitaji kifo kuisafisha hiyo picha, kuturudisha katika thiofania tulimotoka .

Ndipo katika ufufuo tunakuja katika sura Yake, mwili uliofufuliwa. Ni mzuri jinsi gani; sio tu mzuri, bali ni halisi, Ukweli mnyofu wa Neno la Mungu la Milele, kwamba tutakuwa kama Yeye.

22-0823

51-0729A – Kufufuliwa kwa Lazaro

Angalia. Uungu…Mimi ni sehemu ya Charles Branham, kwa sababu nilizaliwa kutoka kwa Charlie Branham, baba yangu. Mimi ni sehemu yake. Nina paji la uso kama yeye. Nywele zangu zilikuwa kama yeye. Mimi ni mtu mdogo kama yeye. Mimi niko katika asili kama yeye, kwa sababu yeye ni baba yangu.

Na tukifanyika katika roho wana wa Mungu, Uungu hukaa ndani ya mwanadamu. Haleluya! Basi Nena macho ya vipofu kufunguliwa .

Walisema Hakuna neno lisilowezekana kwa Mungu . Mungu Alisema Hakuna neno lisilowezekana kwako, kama utaamini, si kwa Mungu, bali wewe. Uungu uko ndani ya mwanadamu.

Mungu yule yule aliyesimama kule nyuma kwenye jukwaa la umilele alilobuni, na kuziondoa dunia kutoka mikononi Mwake, na kuumba vitu hivi anakupa majaliwa ya kuwa mwanawe, nawe ni sehemu Yake. Na Mungu anakaa ndani ya wanadamu, na mwanadamu mwenyewe ni mungu. Haleluya!

Haya Basi. Laweza kukukaba, lakini jifunze juu ya hilo kwa muda kidogo . Unaona?

An Independent Church of the WORD