TAI WANAKUSANYIKA PAMOJA

12.06.2021

>>>21-0613 Mfalme Aliyekataliwa <<<

05.06.2021, TNI BARUA KUTOKA MASKANI YA BRANHAM KWA NDUGU JOSEPH BRANHAM.

Wapendwa Watoto wachanga wa Mungu ,

Tumemwona Mungu Mwenye Nguvu akikaa katika Neno lake Mwenyewe, akiwapofusha watu wenye akili, wasomi na wa wakidini wa wakati huu wa sasa; lakini akifunua jambo hilo kwetu, watoto wachanga ambao watakaojifunza, watoto wa changa wa Mungu. Hatuwezi, na hatutasikiliza neno la mtu mwingine yeyote. Hatujali; ni Ujumbe huu, Kanda hizi, ama chochote.

Alipokuja mara ya kwanza, Yeye alikuwa mtu. Alipokuja mara ya pili akiwa na sehemu maradufu, Alikuwa mtu. Alipokuja katika umbo la Yohana Mbatizaji, alikuwa mtu. Alipokuja katika wakati wetu, Alijifunua kwa Mara nyingine tena katika mtu. Yeye SASA HIVI bado anajifunua katika mwili tena katika kila mmoja wetu, Bibi-arusi wake mpenda Neno.

Tumepata hilo katika mioyo yetu. Akili zetu na roho zetu sasa zimelazwa Mbele ya Mwana kuivishwa, kwa sababu kondoo wanataka chakula cha kondoo: “Kondoo Wangu huisikia Sauti Yangu.” Hilo ndilo tunaloishi kwalo, kila Neno. Si tu Neno Sasa hivi na Kisha , lakini KILA Neno ambalo linalotoka kinywani mwa Mungu, hilo ndilo tunaloishi kwalo.

Tumezaliwa wana wa Mungu, tumejazwa na Roho wa Mungu. Daima tulikuwa wana wa Mungu, na daima tutakuwa wana wa Mungu. Hakuna njia ya kutenganisha Jambo hilo sababu tuna Uzima wa Milele. Hatukuanza kamwe, wala hautakwisha kamwe.

Tunalo chujio la mtu mwenye busara: Neno Lake, Ujumbe Wake, Sauti Yake, na imetupa ladha ya mtu mtakatifu. Tumeonja vitu vya Mbinguni na tumepokea Neno hilo mioyoni mwetu. tumeliona likidhihirishwa mbele zetu, na sasa tunaliona likidhihirishwa NDANI YETU, na nafsi yetu yote imefungwa ndani yake.

Kuna wengine ambao wanatafuta mtu mwingine kuwafunulia zaidi, zaidi ya yale yaliyo kwenye kanda, zaidi ya Malaki 4 tu kuwaongoza. Lakini alituambia imeshuka kupitia Luther, kisha kupitia Wesley na hata Wapentekoste, na sasa iko kwenye macho, kinabii, Malaki 4, na hakuna kitu kingine kilichosalia kuja ila Yeye mwenyewe kuja kwa ajili ya Bibi-arusi Wake.

Naye akatazama kule nyuma na akaiona hiyo, akamwona mtu fulani amevaa mavazi meupe, akisonga mbele; na nyuma yake, kasema ilionekana… Kasema, “Ndugu Branham, ilikuwa ni wewe.” Kisha kasema, “Ukasonga mbele kuingia pale,” kasema, “nyuma yako, walikuweko watu wa rangi mbalimbali, wamebaba bendera; Georgia, Alabama, mikoa mbalimbali, wakisonga mbele kwa hatua taratibu,” wakipanda kuja kwenye kichwa ambako Kristo alikuwa akifunuliwa katika lile ono. Loo, haleluya!

Ni Neno lenyewe mioyoni mwetu na linatuvuta kwake. Tunatema kila kitu kinachosema, “Kuna zaidi ya Malaki 4 tu. Kuna makosa katika Ujumbe. Siku za Ujumbe wa mtu-mmoja zimekwisha. Ni udhehebu na ni kupinga-Neno kusikiliza kanda kwa wakati mmoja. Hatulitaki hivyo tu. ” Tunaishi kwa Neno la Mungu tu, kila Neno litokalo kinywani mwa Mungu kwa ajili ya wakati huu, hilo ndilo chujio letu.

Tunaelewa huduma ya kanda si kwa kila mtu. Kwa wahudumu wowote mahali popote, wakati wowote, hii haielekezwi kupuuza mafundisho yako, hii hata haielekezwi kwa kondoo wako. Ujumbe huu, na jumbe zingine zote alizonena zilielekezwa kwetu, kusanyiko lake. Si kwa kusanyiko lako, isipokuwa wawe wanataka kulipokea. Lakini imeelekezewa sisi, kusanyiko lake.

Nimepewa haki ya kuwalisha kondoo Wake. Nami nimejitahidi vizuri tu nijuavyo, katika kutoa kile Chakula ambacho najua chafaa kwa kondoo.

Ningependa kuweka kikamilifu Jambo fulani wazi kabisa mara nyingine tena. Najua wengi wanasema mambo ambayo kikawaida si kweli, na yamesemwa kuwadanganya na kuwaongoza watu vibaya.

• Mimi niko kinyume na huduma ya Waefeso 4:11. Sijawahi KAMWE kusema, ama hata kufikiria hilo. Kinyume chake, nimetawazwa na Ndugu Branham kuwa sehemu ya huduma hiyo, kwa hiyo ningeikanaje.

• Ninapinga kwenda kanisani . Sijawahi KAMWE kusema, kufikiria, au kuamini hilo. Hatukusanyiki katika jengo kuwa na kanisa kwa sababu tunajenga na hatuna mahali pa kukusanyika, lakini Bwana akipenda tutakuwa tunakusanyika wakati ujenzi utakamilika.

• LAZIMA usikilize kanda ile ile kwa wakati mmoja na Jeffersonville kila wiki ili kuwa Bibi-arusi. Sijawahi KAMWE kusema, kuamini ama hata kufikiria jambo kama hilo. Maisha yangu yote nimesema BONYEZA PLAY. Kwa huduma nilisema, mrudishe Ndugu Branham kwenye mimbara na kuzicheza kanda.

Lakini bado wahudumu wengi wanawaambia watu wao mambo kama hayo, WAKIJUA sijawahi kusema au kuandika kitu kama hicho. Wanaweka tu hofu kwa watu na kuwadanganya.

Lazima ujiulize, “Kwanini wahudumu wengi wanapinga kusikiliza Sauti ya Mungu kwa wakati mmoja?” Wanasema ni MAKOSA na ni umadhehebu kwa watu kuzisikia kanda wote kwa wakati mmoja. Je! ilikuwa ni makosa na umadhehebu wakati ndugu Branham alipokuwa hapa na alipofanya hivyo?

Je! Unafikiri kama watu walikuwa wakiunganishwa kusikiliza hewani “wao” wote kwa wakati mmoja wangekuwa wanalipinga hilo na kusema ni kupinga-Neno? Jambo Fulani lina kasoro .

Mungu amempa Bibi-arusi wake chujio, Ni Neno Lake, Ujumbe Wake, Sauti Yake. Neno humjia Nabii Wake. Nabii ni mfasiri wa Neno Lake. Daima imekuwa Ujumbe wa mtu mmoja na kamwe sio kundi. Mungu alimtuma Roho Wake Mtakatifu kumwongoza Bibi-arusi Wake na huyo Roho Mtakatifu atakuelekeza kwa nabii Wake, YULE ALIYEMCHAGUA kuongoza Bibi-arusi Wake kwa Neno Lake. Mungu kamwe hawezi kubadilisha mpango Wake. Daima amewaongoza watu Wake mwenyewe akiwa amejifunika katika mwili wa mwanadamu.

Umealikwa, si kuombwa, kuja kuungana na kundi la watu wanaoamini KILA NENO ni Neno la Mungu lililonenwa kupitia malaika_mjumbe wake wa 7, tunaposikia: Chujio la Mtu Mwenye Busara 65-0822E, saa 8:00 kwa masaa ya Jeffersonville ( ni saa 3:00 Tatu usiku ya Tz).

Ndugu. Joseph Branham

Hesabu 19: 9

Waefeso 5: 22-26

22.05.2021, TNI BARUA KUTOKA MASKANI YA BRANHAM KWA NDUGU JOSEPH BRANHAM.

Mpendwa Bibi-arusi
wa Ujumbe wa Mtu Mmoja,

Ninashukuru sana kwamba Mungu mwenyewe alimchagua nabii kwa wakati wetu kabla ya kuwekwa
misingi ya ulimwengu. Kwamba alichagua Ujumbe Atakaoleta
na hata akachagua tabia ya mtu huyo. Aliweka ndani yake kile kingewavutia watu wa wakati wetu.

Kwa mjumbe wake aliyechaguliwa, alimfunulia Bibi-arusi wake wao ni nani na
mjumbe wao ni nani. Kwa wengine wote, Aliwapofusha macho yao. Hawawezi kamwe kuvuka nyuma ya pazia kuona Mungu akijificha katika mwili wa mwanadamu.

Anatujali sana, hata alimvalisha nabii wetu kwa namna ya mavazi
aliyokuwa: Tabia, shauku, na kila kitu, jinsi tu ilivyompasa kuwa; alimchagua kikamilifu kwa ajili yetu, ili aweze kumwita Bibi-arusi Wake atoke.

Moja ya kikwazo kikubwa adui anachojaribu kukitumia leo ni
Kutenganisha Ujumbe na Bibilia kwa kusema: “kama ilibidi kuchagua
kati ya Biblia na Ujumbe, ungechagua kipi? ”

Ni Ujanja jinsi gani wa shetani kusema jambo kama hilo. Ikiwa mtu atakuuliza
swali la namna hiyo, unaweza kusema mara moja HAWANA ufunuo wa Neno kwa
vyovyote vile. Ujumbe huu ni Kristo Amefunuliwa Katika Neno Lake Mwenyewe.

Maneno yenyewe ya nabii ni haya:

Sasa, tunaona ya kwamba Eliya angeweza kusema hayo kwa sababu Ujumbe wa saa na Neno la Mungu,
ama, mjumbe, Ujumbe _Ujumbe, na Neno, Ilikuwa ni
Kitu kimoja. Nabii, Neno,
ujumbe; mjumbe, Ujumbe, na Ujumbe, vilikuwa kitu kimoja. Yesu
alisema, “Ikiwa sizifanyi kazi nilizoandikiwa mimi, basi msiniamini
Mimi. ” hilo ni sawa. Mtu yeyote na ujumbe wake ni mmoja

Hauwezi kutenganisha Ujumbe na mjumbe, wao ni kitu kimoja .
Pia huwezi kutenganisha Biblia na Ujumbe, ni kitu kile kile.
Ni Mungu Akilifasiri Neno Lake.

Tunao mkataa, yakini, na hiyo ni Neno la Mungu.
Biblia yote si neno la mwanadamu, wala haikuandikwa na mwanadamu, kuletwa na mwanadamu,
au hata hivyo haiwezi kufunuliwa na mwanadamu. Ni Neno la Mungu lililofunuliwa na Mungu
Yeye Mwenyewe, hujifasiria Mwenyewe, Kristo akijifunua katika Neno Lake Mwenyewe.

Neno lake halihitaji kufasiriwa . Analonena kupitia midomo ya Nabii wake ni Neno Lake lililokwisha fasiriwa. Alituonya tusibadilishe kituo kimoja, tamshi moja, kwa sababu ni Mungu. Mungu akidhihirishwa katika mfano wa mwili wa mwanadamu. Mungu mwenyewe katika maumbile ya herufi, sura ya nabii, akidhihirishwa katika
mwili.

Kuandika Biblia Yake, Mungu alituma manabii Wake, ambayo ndiyo njia ambayo alikuwa nayo
kulileta Neno Lake kwa watu, kupitia midomo ya manabii Wake. Wale
manabii waliandika Neno la Mungu lisilokosea.

Walikuwa katika ushirika wa daima na yule Mwandishi. Waliishi daima katika Uwepo wa Yule Mwandishi, kujua vile Kitabu kitakavyokuwa. Wao
walikuwa na kalamu mikononi mwao tayari wakati wowote, kusudi waandike lolote asemalo liandikwe..

Lakini katika siku yetu, Amenena mdomo kwa sikio kwa nabii wetu, kwani wito Wake ulikuwa wa
juu zaidi. Wito wake ulikuwa Ni wa kufunua Neno la Mungu ambalo lilikuwa limeandikwa na kufichwa
katika Biblia yake kutoka Mwanzo hadi Ufunuo.

Kila kitu kiko katika Neno Lake, Biblia, lakini kilikua kimefichwa tangu
kuweka
misingi ya ulimwengu na hakuna mtu aliyejua siri hizi. Isipokuwa uwe na
Ujumbe huu na uamini kuwa ni fasiri ya Biblia, wewe pia hutajua kamwe Neno lote la Mungu.

Kama tukitenganisha Biblia na Ujumbe wa saa, tungekuwa tu kama madhehebu. Tungekuwa tunasoma bali tusingejua kamwe au kuwa na
ufunuo mkamilifu. tusingeweza kamwe kuwa Bibi-arusi Wake. Tungekua tukisubiri
na kusubiri na kusubiri na kamwe bila kupata majibu.

Tungesoma Malaki, Yohana, Luka, Waebrania, Ufunuo kisha tuulize:
“Yuko wapi huyu ambaye Mungu aliahidi atakuja tena katika mwili wa mwanadamu na kugeuza
mioyo ya watoto; kutuambia mambo mengi ambayo hatuwezi kuyavumilia;
Kunena nasi kupitia malaika wake mwenye nguvu na kutufunulia mafumbo yote
Yalioandikwa katika Biblia? Je! Mihuri Saba inamaanisha nini? ni upi Ukweli wa
Uungu, Ngurumo, ufunuo wa kweli Wake mwenyewe? ”

Nabii_mjumbe wetu ndiye mfasiri PEKEE wa kiungu wa Neno la Mungu. Yeye
ndiye ambaye Mungu alimchagua kunena na kufasiri Neno Lake kupitia yeye. Kama
vile
Musa, naye alikuwa Neno lililo hai kwetu lililofunikwa katika mwili wa mwanadamu. Yeye alikuwa ndiye aliyechaguliwa na Mungu kumwita Bibi-arusi Wake atoke.

Aliwaonya watu Jumapili iliyopita:
_
*Neno lake linafunuliwa kwa mmoja. Daima Imekuwa hivyo, Nabii alikuja na Neno
la Bwana, kila kipindi cha wakati, kila wakati, kote katika Maandiko. Neno
Humjia mmoja. Katika kila wakati, vivyo hivyo, hata katika nyakati za kanisa, Tangu wa
Kwanza hadi wa mwisho ._ **Wengine wana mahali pao_ hiyo ni kweli, angalia, **lakini kaeni mbali na hiyo Nguzo ya Moto._

Kaeni mbali na hiyo Nguzo ya Moto. Nguzo hiyo ya Moto ilifanya nini? ILIWAONGOZA WALE WANA . Kiongozi wetu Nguzo ya moto ni Mungu anayenena kupitia Mjumbe wake wa wakati wa saba, akituongoza kwenye Nchi ya Ahadi. Sisi ni wateule wake. Sisi ni wateule wa Mungu. Sisi ni Bibi arusi wake aliyeitwa atoke. Tunao Ufunuo Wa Yeye jana, leo na hata milele. Tunatambua siku yetu na mjumbe wetu. Tunatambua sisi ni nani: Neno lake lililodhihirishwa. Sisi ni Bibi-arusi Wake yule aliyejifanya mwenyewe tayari Kwa Neno lake lililofunuliwa. Njoo usikilize saa 8:00 Mchana, saa za Jeffersonville, (ni saa 3:00 tatu usiku ya TZ) na usikie majibu kwa yote
Yaliyoandikwa na kufichwa katika Biblia. Njoo umuone Kristo Amefunuliwa Katika Neno Lake
Mwenyewe 65-0822M.

Ndugu. Joseph Branham

Maandiko ya kusoma kabla ya kusikia Ujumbe:

Kutoka 4: 10-12

Isaya 53: 1-5

Yeremia 1: 4-9

Malaki: 4: 5

Luka Mtakatifu 17:30

Yohana Mtakatifu 1: 1 / 1:14 / 7: 1-3 / 14:12 / 15:24 / 16:13

Wagalatia 1: 8

2 Timotheo 3: 16-17

Waebrania 1: 1-3 / 4:12 / 13: 8

2 Petro 1: 20-21

Ufunuo 1: 1-3 / 10: 1-7 / 22: 18-19

22.05.2021, TNI BARUA KUTOKA MASKANI YA BRANHAM KWA NDUGU JOSEPH BRANHAM.

15.05.2021, TNI BARUA KUTOKA MASKANI YA BRANHAM KWA NDUGU JOSEPH BRANHAM.

Wapendwa, Enyi Watoto Wadogo.

Tumechukua Maamuzi yetu. Ujumbe umethibitishwa. Mwana wa Adamu amekuja tena katika mwili wa kibinadamu kufunua Neno Lake. Pazia la mapokeo limepasuliwa . Huyu hapa, Nguzo ya Moto, amesimama dhairi kabisa, akidhihirisha Neno la siku hii. Tunaliona, na tunaliamini… KILA NENO !!

Tumesikiliza kila moja ya kanda hizo kama zilivyokuja. Imekuwa wazi na wazi kwetu tunaposikia kila moja . Tumeyachunguza Maandiko. Neno la Mungu limedhihirishwa na kuthibitishwa kwetu. William Marrion Branham alilinena, ndipo Mungu akalitimiza.

Ni kitu gani? Uungu umefunikwa katika mwili wa kibinadamu. Wazieni jambo hilo! Nguzo ile ile ya Moto iliyowashukia hao watu walioiandika Biblia, ndiyo nguzo ile ile ya Moto hapa leo, ikifasiri Biblia. Neno Lake, kanda hizi , zinatufanya tuwe kama yeye zaidi kila siku. Tunaishi katika Uwepo Wake na tunafanana na sura Yake iliyobarikiwa tunapotembea naye na yeye akinena nasi.

Hamko nyuma ya pazia hilo tena, enyi watoto wadogo, Mungu anaonekana wazi kabisa kwenu.

Hatuko nyuma ya pazia hilo, tunaliona wazi kabisa . Ni mkate wa wonyesho ambao tunaoula tunapoungana pamoja kote ulimwenguni kumsikia Mwana wa Adamu akinena nasi na kufunua Neno Lake. Ni Chakula cha waaminio hicho ni Kwa ajili ya mwaminio wa kweli PEKE YAKE.

Wengine wanaweza kutaka chakula tofauti, lakini kwetu Sisi, imefunuliwa, Mungu alituma Neno Lake kwa Mtu Mmoja, si kundi, Mtu mmoja.

Daima imekuwa hivyo , nabii alikuja na Neno la Bwana, kila kipindi cha wakati, kila wakati, kote katika Maandiko. Neno humjia MMOJA. Katika kila wakati, vivyo hivyo, hata katika nyakati za kanisa, Tangu wa kwanza hadi wa mwisho. Wengine wana mahali pao, hiyo ni kweli, angalia, lakini kaeni mbali na hiyo Nguzo ya Moto.

Tunataka Sauti ya Mungu iliyorekodiwa na kuwekwa kwenye kanda, Neno ambalo halihitaji FASIRI YOYOTE, UFAFANUZI WOWOTE, NENO SAFI PEKEE, Mana iliyofichwa.

Kama vile Wayunani walimtaka Mungu; na alikuwa ndiye huyu hapa, lakini hawakuweza kumwona yeye kwa sababu ya ule utaji. Ni jambo lile lile leo, wao hawawezi kumwona kwa sababu ya pazia, limefunika uso wao.

Bwana arusi amekuja katika Mwili wa kibinadamu na anatuunganisha pamoja; Neno na Kanisa Lake, na sasa tunakuwa MMOJA. Ni Dhihirisho la kufunuliwa kwa Mwana wa Adamu, Yesu Kristo katika mwili wa kibinadamu tena. Anatuunganisha na kutupeleka kwenye Karamu ya Harusi ameandaa kwa ajili ya Bibi-arusi Wake.

Sikilizeni enyi watoto wadogo, WEWE NI NENO ambalo lilioandikwa na kudhihirishwa. Baba amekupa Ufunuo Wa Yeye Mwenyewe kwa ajili ya siku hii, na sasa, amekupa Ufunuo wa WEWE MWENYEWE, Bibi-arusi Neno Mkamilifu. Nena Neno, Wewe hauzuiliki.

Ujumbe huu ni huduma kamilifu yake mwenyewe , si mtu fulani, si dhehebu fulani kama vile kote kwenye nyakati hizo, lakini Yeye Mwenyewe, akijidhihirisha mwenyewe: Luka Mtakatifu 17:30, Malaki 4, Ufunuo 10: 7, Waebrania 13: 8.

Ikiwa mnatafuta kitu kingine, au mtu mwingine, kuwafunulia zaidi ya kilicho kwenye kanda, mmelikosa enyi marafiki. Rudini kwenye Neno La Asili. Neno kamilifu. Si mimi, si mchungaji wako, Ni NENO HILI, UJUMBE HUU, KANDA HIZI , kwa kuwa hizo ndizo Sauti PEKEE ya Mungu iliyo hakikishwa na kuthibitishwa.

Njoo umsikilize huyo Sauti Akijifunua mwenyewe Jumapili hii saa 8:00 mchana, saa za Jeffersonville,( ni 3:00 usiku ya TZ) tunapoungana pamoja kumsikia Mungu akinena Ujumbe Wake kwa Bibi-arusi Wake: Kufunuliwa kwa Mungu 64-0614M

Ndugu. Joseph Branham

Maandiko ya kusoma kabla ya kusikia Ujumbe:

Mathayo 24:24
Luka Mtakatifu 17: 28-29
Yohana Mtakatifu 14:14
1 Wakorintho 12:13
2 Wakorintho 3: 6 – 2 Wakorintho 4: 3
Wafilipi 2: 1-8
1 Timotheo 3:16
Waebrania 13: 8
Ufunuo 10: 7 & 19: 13
Kutoka sura ya 19 na 20
Yoeli 2:28
Malaki 4: 5

08.05.2021, TNI BARUA KUTOKA MASKANI YA BRANHAM KWA NDUGU JOSEPH BRANHAM.

Mpendwa Neno,

Bibi-arusi anajiandaa kuwa na uamsho mwingine tena katika nafsi zetu. Roho Mtakatifu atatuunganisha tena kusikia Neno kututhibitishia: sisi ni akina nani, tunatoka wapi na wapi tunaelekea .

yeye huthibitisha Neno lake lote, Neno Lake lote. wazia hilo tu, Neno lake lote! Nawe ulikuwa Neno Lake. Yeye alikuwa Neno, nawe ulikuwa sehemu ya Neno Lake. Na, hiyo ndiyo sababu umetumwa hapa, kuhakikisha mahali pako maishani.

Sisi ni Neno Lake. Sisi ni sifa yake. Alituwaza na kutujua kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu. Tulikuwa katika Mawazo Yake. Tunao uwakilisho Mbinguni kwa kuchaguliwa kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu. Ametupa Ufunuo Wake mwenyewe, jana, leo na hata milele.

Sikiliza kwa makini, kwa kuwa tumefika mwisho. Mungu amelazimisha suala hilo. Wakati umefika wa kuchukua hatua, lazima ufanye uamuzi. Mwana wa Adamu amekuja na kutimiza Maandiko yote yaliyonenwa kumhusu yeye. Amethibitisha kwa Neno. Unasimama wapi?

Swali ambalo unapaswa kujiuliza leo ni: Ni nani alikuwa malaika_mjumbe wa 7 ambaye Mungu alitabiri atamtuma? Je! Yeye, au hakuwa na maneno ya kutokukosea kama vile alivyosema alikuwa nayo? Je! Alitimiza Maandiko yote yaliyonenwa kumhusu yeye? Je! Ujumbe aliounena ulikuwa na makosa?

Je! Imeandikwa katika Neno kwamba tunahitaji zaidi ya kile kilichonenwa na malaika_mjumbe wa 7 wa Mungu? Je! Alisema atatuma mtu kufasiri kile mjumbe wake alisema? Je! Neno linasema atatuma kundi la watu kuongoza na kuunganisha Bibi-arusi Wake? Je! Anasema sio lazima uamini kila Neno?

Ukidai unaamini: Huu ndio ujumbe wa saa. William Marrion Branham alikuwa malaika wa 7 ambaye Mungu alimtuma kufunua siri zote. Ni Mwana wa Adamu akijifunua mwenyewe. Hebu tuone sasa kile malaika_mjumbe huyu kuhusu alisema alikuwa NANI

Sasa, kumbuka, huyo hakuwa Yesu akinena na Ibrahimu pale, ambaye angeyatambua mawazo rohoni mwa Sara nyuma Yake. Huyo hakuwa Yesu, hakuwa amezaliwa bado. Lakini alikuwa Mtu katika mwili, ambaye Ibrahimu alimwita “Elohim, yule Mkuu Mwenyezi ” ikionyesha… Na Yesu alisema, “Kama ilivyokuwa katika siku za Sodoma,” sasa tazama kwa makini, “katika siku za Sodoma, ndivyo itakavyokuwa wakati wa kuja kwake Mwana wa Adamu, wakati Mwana wa Adamu atakapofunuliwa. ” Si tena kama kanisa, unaona, si tena; Bibi-arusi amekwisha kuitwa, mnaona. “katika siku hiyo Mwana wa Adamu atafunuliwa.” Nini? Kuliunganisha Kanisa kwa kile Kichwa, kuliunganisha, Arusi ya Bibi-arusi. wito wa Bwana Arusi utakuja hapa, wakati Mwana wa Adamu atakaposhuka aje katika mwili wa mwanadamu kuunganisha hivyo viwili pamoja.

Wakati NANI atakuja na kuunganisha Bibi-arusi? Kundi la watu? Huduma? Mwana wa Adamu atashuka aje katika mwili wa mwanadamu kuunganisha hivyo wiwili pamoja. Je! Huyu Mwana wa Adamu, mtu aliye katika mwili wa mwanadamu atafanya nini? Ataunganisha Kanisa kwa kile Kichwa, kuunganisha, Arusi ya Bibi-arusi.

Tunajua Mwana wa Adamu ndiye Neno la leo. Lakini mtu huyo alikuwa NANI aliye katika mwili wa mwanadamu ambaye Mwana wa Adamu alijifunua kupitia yeye? Ilibidi awe Nabii; kwa maana Neno humjia Nabii TU na Nabii ndiye mfasiri PEKEE wa Neno LA kiungu la Mungu.

Kanisa halina budi kuwa Neno, Yeye ni Neno, na hivyo viwili vitaungana pamoja, na kufanya hivyo, itachukua dhihirisho la kufunuliwa kwa Mwana wa Adamu. Si kasisi.

Itachukua kitu gani kuunganisha Bibi-arusi kwenye Neno? Si kasisi itachukua:

•Dhihirisho: Webster: Kufanyika mwili kwa kitu fulani au mtu fulani.

•KUFUNULIWA: Webster: Ufunuo wa mwisho wa habari ambayo Iliyohifadhiwa hapo awali.

… Kwa Mwana wa Adamu. Je! Mwana wa Adamu alijifunua kupitia nani? William Marrion Branham.

Je! Unaweza kuona ni kwanini adui anataka utilie shaka kuwa kila Neno lililonenwa si Bwana Asema Hivi? Je! Nukuu hii SIYO Bwana Asema Hivi na mawazo tu ya Ndugu Branham, au wazo lake, au ni Neno la Mungu?

Je! Utaamini kile mtu fulani anafafanua kuwa inamaanisha, au utaamini kile malaika_mjumbe wa 7 aliyethibitishwa na Mungu anachosema? Lazima ujiulize swali hilo.

Si-sijui, mimi… Mnaona lile ninalomaanisha? Mnaona, ni Mwana wa Adamu, Yesu Kristo, atakayeshuka katika mwili wa mwanadamu kati yetu, naye atafanya Neno Lake dhahiri sana hata litaunganisha kanisa pamoja naye kama mmoja, Bibi-arusi, kisha Ataenda Nyumbani kwenye Karamu ya Arusi.

Yesu Kristo, Mwana wa Adamu, akijifunua mwenyewe kupitia mjumbe Wake ataunganisha Kanisa Lake na Yeye mwenyewe kuwa MMOJA na tutaenda Nyumbani kwenye Karamu ya Arusi. Hilo hapo, kwa Kiingereza kilicho wazi.

Si mimi nisemaye hayo, si wazo langu au mawazo yangu, Lisikie mwenyewe. Ni Mungu anayesema na Bibi-arusi Wake kupitia malaika wake wa 7 kama alivyoahidi angefanya katika Neno Lake. Si mwanadamu, MUNGU.

Adui anakuambia, “wanaabudu mtu.” Ninakusahi Shetani, hatuabudu mwanadamu anayesema, Bali BWANA YESU KRISTO anayeongea kupitia yule ALIYECHAGUA kuzungumza kupitia huyo.

Amina. Tayari amekwisha kuunganishwa. unaona, tunaenda kwenye Karamu ya Arusi, si kwenye Arusi. “… jishibisheni… Wenyewe, na nyama zote za watu hodari sababu Arusi ya Mwana_kondoo imekuja.” Lakini, kule kunyakuliwa, ni kuenda kwenye Karamu ya Arusi. Wakati Neno hapa, liunganikapo na mtu, na hao wawili huwa mmoja. Ndiposa linafanya nini basi? Linamdhihirisha Mwana wa Adamu tena, si wanatheolojia wa kanisa. Mwana wa Adamu! Neno na Kanisa wanakuwa mmoja. Lolote afanyalo Mwana wa Adamu, Yeye alikuwa Neno, Kanisa linafanya jambo lile lile.

Hili hapa tena, Mungu akituambia Kile YEYE anachofanya sasa hivi, ANATUUNGANISHA NA NENO LAKE LILILONENWA KUPITIA MWANA WA ADAMU. Neno na Kanisa (SISI) wanakuwa kitu kimoja.

Lazima uamini kila Neno. Usimsikilize mwanadamu au mawazo ya mwanadamu.

Nanyi mnoketi papa hapa sasa, mkitaka nitaje majina yenu, imekuwa, Shetani amejaribu kwa muda mrefu kuwafanya mnishuku. Msifanye hivyo. Dada, ukifanya hivyo, vema, wewe… ama, si mimi, bali kutilia shaka tu. Amini tu hili Neno. Silazima uniamini mimi, bali uliamini Hili. Mnaona? Nikisema Neno hili, si langu, ni Lake. Mnaona? Neno langu ni tofauti, bali Hili ni Neno Lake.

Sio Neno la William Marrion Branham, ni Neno la Mungu, na Shetani anataka utilie shaka Neno moja tu.

Na kukiwapo neno linalotiliwa shaka, sharti lijaribiwe hata utakapotambua ukweli. Kisha utakapopata lililo kweli, lilisema, “Lishikilieni.” Kwa maneno mengine, “Likamateni Sana, msiliachilie. Lishikilie!” Kwa maneno mengine, “Lishikeni kwa dhati, Lisije likaponyoka.” Lishikeni lililo jema, baada ya kuthibitishwa kuwa “Kweli” Na lolote Lililothibitishwa kuwa “si Kweli,” basi Liachilie upesi uwezavyo, ikimbie.

Njoo uungane nasi Jumapili saa 8:00 mchana, saa za Jeffersonville,(Ni saa 3:00 usiku ya TZ) kumsikia Baba akinena kupitia mjumbe wake Aliyemchagua kutuunganisha kwa ajili ya Unyakuo kwani Yeye anatuambia Anathibitisha Neno Lake 64-0816.

Ndugu Joseph Branham

Maandiko ya kusoma kabla ya Ibada:

Marko 5: 21-43
I Wafalme 10: 1-3
I Wathesalonike 5:21
Waebrania 4:12

01.05.2021, TNI BARUA KUTOKA MASKANI YA BRANHAM KWA NDUGU JOSEPH BRANHAM.

10/04/2021

Mpendwa Ulimwengu Usioonekana wa Kanda,

Sisi ni wale watu wa Ulimwengu usioonekana wa kanda ambao wameshikamanishwa kisumaku kwa kila Neno lililonenwa kwenye kanda ya sumaku. Tunajivunia kusema, “NDIYO, tunaamini kila Neno. Tunaamini ni kutimizwa kwa: Malaki 4: 5, Luka 17:30, Waebrania 13: 8, Ufunuo 10: 7. Tunaamini ni Sauti Ya Mungu kwaajili ya siku yetu. Tunaamini Ni Bwana Asema Hivi. ”

Loo, wakati sisi sote tunakusanyika pamoja, sehemu hizi ndogo tukija pamoja, inapendeza. Hakuna dhehebu; hakuna kufungwa na chochote, lakini ni kwa Yesu Kristo pekee, hilo tu, unaona, “kukaa tu pamoja katika makao ya kimbinguni.”

Ni wikendi maalum ya barua ya kipekee ya Pasaka jinsi gani Bwana aliyotupatia alipomshikamanisha kisumaku bibi_arusi na Sauti yake. Alituleta pamoja kutoka kote ulimwenguni, na kutuweka katika makao ya kimbinguni, na kisha akatufunulia Neno Lake kwa kutuambia, “Shalom. Usiogope, yote ni sawa. Ninakuja kwaajili yako hivi karibuni. Haitakuwa muda mrefu sasa. Wewe ni uakisi wa Neno Langu. ”

Ilikuwa ni ajabu jinsi gani wakati sisi sote tulipokusanyika kila siku na kumwabudu Yeye, kumsifu na kumshukuru kwa uponyaji wetu, kujazwa tena Roho wake Mtakatifu, na muhimu zaidi, kutupa Ufunuo wa Kweli wa Yeye mwenyewe katika siku yetu.

Tunafurahi zaidi ya hapo awali. Uamsho mkuu umekuja miongoni mwa Kanisa Lake. Hakuwezi kuwa na kosa,hakuna shaka; tumemtambua Yeye kwa siku yetu, na sasa tumejitambua sisi ni nani, Bibi-arusi wake kipenzi.

Wakati Tai wanapokusanyika, tunaweka wakfu upya maisha yetu kwake na tukimwambia kutoka ndani ya mioyo yetu:

Mimi ni Wako, Bwana. Ninajilaza juu ya madhabahu hii, nikijiweka wakfu tu kama nijuavyo. uondoe ulimwengu kutoka kwangu, Bwana. Viondoe vitu viharibikavyo kutoka kwangu ; nipe vitu visivyoharibika, Neno la Mungu. Na niweze kuliishi Neno hilo kwa karibu sana, mpaka Neno litakuwa ndani yangu, na mimi ndani ya Neno. Lijalie, Bwana. Naomba kamwe nisikengeuke kutoka Kwake. Naomba niushike Upanga huo wa yule Mfalme kwa nguvu sana, na kuushika kwa karibu sana. Lijalie, Bwana.

Kwa kweli haya ni maombi ya kila mwamini. Tusikengeuke kamwe kutoka kwenye hili. tusiongeze kamwe mawazo yetu au mafikara yetu kwenye hili, lakini tukae na njia ya Mungu iliyotolewa kwaajili ya siku yetu, Ujumbe huu.

Ametupatia kila kitu tunachohitaji: mwana-kondoo wa dhabihu, Nguzo ya Moto, nabii, Sauti ya Mungu kwenye kanda ya sumaku. Ujumbe wa saa hii umeendana na kila kitu ambacho ilichosema Biblia.

Kama ilivyokuwa juu ya Mlima wa Kubadilika sura siku ile, wakati walipopewa agizo la “Msikieni Yeye ,” tu, huo ndio ushuhuda wetu leo, kwa maana Bibi-arusi anataka “msikieni Yeye.” TU.

Tunataka kuenda nje ya kambi. Haijalishi inatugharimu kitu gani, tutachukua msalaba wetu na kuubeba kila siku. Haijalishi watu wanasema nini juu yetu, kushindwa kutuelewa, au kutufanyia mzaa, tunataka kumfuata nje ya kambi.

Mpendwa bibi_arusi, kuna NJIA MOJA TU PEKEE YA UHAKIKA, BONYEZA PLAY NA MSIKIENI YEYE. Nabii alisema watu wanaweza kweli kutiwa mafuta na Mungu, wakiwa na ufunuo sahihi kutoka kwa Mungu, na bado wawe wamekosea, lakini Kanda HAZIWEZI KUKOSEA KABISA.

Njoo na ujishikamanishe kisumaku na Neno Lake pamoja nasi Jumapili hii saa 8:00 mchana, saa za Jeffersonville,(ni saa 3:00 usiku ya TZ), tunapo : kuenda nje ya Kambi 64-0719E, na usikie Sauti ya Mungu ikinena kwa Bibi-arusi Wake.

Ndugu. Joseph Branham

Maandiko ya kusoma kabla ya ibada:

Waebrania 13: 10-14
Mathayo 17: 4-8

31/03/2021

Mpendwa Mgeni Mwalikwa,

Ni kwa matarajio makubwa kukaribisha kila mmoja wenu kwenye pasaka yetu ya kimataifa ya tai wanakusanyika. Wikendi tukufu iliyojaa maombi,kuabudu, uponyaji, kumwagwa na kujazwa tena kwa Roho Mtakatifu. Wikendi ambayo Ni kama haujawahi kupitia hapo awali.

Sio tu ibada za kimsingi za Ijumaa, Jumamosi na za Jumapili na wanenaji wachache walioalikwa, ni kukusanyika kwa Bibi-arusi wa Kristo kutoka kote ulimwenguni anayeweka wakfu wikendi nzima ya Pasaka kwaajili yake wakati tunapovumisha mbingu kwa maombi yetu, tukisikia Sauti ya Mungu ikinena nasi moja kwa moja kupitia mjumbe wake aliyechaguliwa, na kumwabudu Mfalme wetu aliyefufuka.

Tunafungia nje ulimwengu wote, simu zetu, kazi yetu, marafiki zetu, kila na vizubaishi vyote. Tunafunga milango yetu na kumwalika katika nyumba zetu kwa wikendi iliyojaa ibada isiyoisha na kumtafakari yeye, na Yeye peke yake. Tunayo fursa iliyoje.

Tutamshukuru kwa wakati mzuri tuliokuwa nao majira haya ya baridi wakati Yeye ametufunulia Neno Lake zaidi ya hapo awali, kama tulivyosikia: Mihuri Saba, Kile kipeo na Baragumu Saba. Amekuwa akituandaa na kutukamilisha kwa kuja kwake kwaajili ya hivi karibuni. Na sasa ana kitu Fulani alichotunza maalum kwaajili yetu kwa wikendi hii ya Pasaka.

Tunasikia ulimwengu sasa ukisema, “Tumemaliza, na tunataka kurudi katika hali ya kawaida, jinsi mambo yalivyokuwa zamani. Kila kitu ni sawa sasa, tumepiga kitu hiki. Tuliogopa kwa muda, kwamba kunaweza kuwa na kitu katika jambo hili, kwa hivyo tukashikamana kwenye Safina kwa muda, lakini haijanyesha, hebu tuendelee na maisha yetu. “

Lakini Bibi-arusi anapaaza sauti kinyume chake, “MVUA ITANYESHA, TUPO KATIKA SAFINA BWANA kama vile Neno lako lilivyoamuru. Njoo umchukue Bibi-arusi wako, hii sio nyumba yetu. Tuko tayari kuja kwenye nyumba yetu mpya ambayo umekuwa ukitutayarishia. Hatuwezi kuwa kamwe wale wale ”

Tumejionea siku kuu za maisha yetu. Sasa, anatupa nafasi nyingine tena ya kujaza wikendi nzima si chochote ila Yeye. Siku ambazo tumezitamani. Siku ambazo tulizoomba. Wakati maalum ambapo tunaweza kumwambia, “Bwana Yesu, Umesema Unakuja kwaajili ya Bibi-arusi ambaye amejifanya mwenyewe tayari. Bwana, tunaamini sisi ni yule Bibi-arusi ambaye umekuwa ukimsubiri. Bibi-arusi Neno anayependa na kuamini kila Neno. Ninataka kukusanyika na Bibi-arusi wako kutoka kote ulimwenguni, na kwa umoja, kukuabudu na kukusifu, na kujiweka wenyewe tayari kwaajili ya kuja kwako kwa hivi karibuni.”

Ni nini kitakachomleta kwenye eneo La tukio? Kukata tamaa. Lazima tuwe wenye kukata tamaa.

Sasa, naamini kwamba tunaishi katika siku ambazo sisi ni… Au, vinginevyo, siku ambazo tunaishi zinapaswa kulifanya Kanisa kwenda kabisa katika kukata tamaa. Ninaamini, tangu ujumbe asubuhi ya leo kutoka kwa Mungu, sio mimi, naamini inapaswa kulitupa kusanyiko hili zima katika kukata tamaa, kwamba tumecheza kwa muda mrefu vya kutosha. Tumeenda kanisani kwa muda mrefu vya kutosha. Tunapaswa kufanya kitu.

Tunayo fursa iliyoje yakukata tamaa wikendi hii na kumwita Yesu kwenye eneo la tukio. Njoo ukusanyike na Bibi-arusi Ijumaa hii, Jumamosi na Jumapili. Tumecheza kwa muda mrefu, tumekwenda kanisani kwa muda mrefu vya kutosha, tunapaswa kufanya kitu.

Ningependa sisi sote tuungane wikendi hii kwa majira ya saa za Mashariki ya Kati (EDT) kwa ratiba ifuatayo.

IJUMAA
Hebu tuianze wikendi yetu ya Pasaka saa 9:00 asubuhi, (ni saa 10:00 jioni ya TZ) halafu tena saa 6:00 mchana, (ni saa 1:00 jioni ya TZ) kwa kuungana katika maombi na kumwalika Bwana kuwa nasi na Bibi-arusi Wake kutoka kote ulimwenguni katika wikendi hii maalum, na kujaza nyumba zetu na Roho wake Mtakatifu wakati tumejiweka wakfu kwa kumwabudu Yeye.

Kisha hebu tuungane tena katika maombi saa 9:00 alhasiri.(ni saa 4:00 usiku ya TZ). katika ukumbusho wa kusulubiwa kwa Bwana wetu. Mawazo yetu na yarudi siku hiyo zaidi ya miaka 2000 iliyopita, hadi Kalvari, na tumuone Mwokozi wetu akining’inia juu ya msalaba huo, halafu tusome jina letu ndani pale:

Wakati unaweza kulisoma jina lako ndani mle,”Alijeruhiwa kwa makosa ya William Branham; Alichubuliwa kwa uovu wa William Branham,” hapo wakati amani inapokuja. Sio tu kwamba ilikuwa tu jambo la uuzaji wa jumla; ilikuwa kwa ajili yangu. Ni mtu binafsi. Nilijumuishwa katika hilo. “Kwa kupigwa kwake William Branham aliponywa.” Ndipo ni tofauti.

Halafu saa 1:00 jioni (ni saa 8:00 usiku ya TZ), hebu tusikilize kesi ya mahakamani muhimu zaidi ya wakati wote inakuja kuamuru, tunapokusanyika kwenye Kiti Chake cha enzi kusikia Ujumbe: Kesi 64-0419.

JUMAMOSI
Jumamosi: saa 3:00 Asubuhi (ni saa 10:00 jioni ya TZ) ,6:00 mchana (Ni saa 1:00 jioni ya TZ), na 9:00 alhasiri (ni 4:00 usiku ya TZ), hebu tuungane wote tena katika maombi.

Halafu Jumamosi jioni saa 1:00 , (ni saa 8:00 usiku ya Tz )sisi sote tutakusanyika pamoja kusikia NENO: Siku Hiyo pale Kalvari 60-0925. Hii itakuwa siku njema sana.

JUMAPILI
Kwenye asubuhi hiyo kuu na ya ajabu ya ufufuo, hebu tuamke mapema kama Ndugu Branham alivyofanya, saa 11:00 alfajiri, (ni saa 6:00 mchana ya TZ) na tu mshukuru Bwana kwa kumfufua Yesu kutoka kwa wafu:

“Saa kumi na moja Alfajiri ya leo, rafiki yangu mdogo aliye na kifua chekundu akaruka dirishani na kuniamsha. Ilionekana kama moyo wake mdogo ungepasuka, ukisema, “Amefufuka.”

Saa 2:30 Asubuhi (ni saa 9:30 jioni ya TZ) tuungane kwa dhati tena katika mnyororo wetu wa maombi, tukiombeana na kujitayarisha kuisikia Sauti ya Mungu.

Saa 3:00 Asubuhi ( ni saa 10:00 jioni ya TZ) tutakuja pamoja kusikia Ujumbe wetu wa Pasaka: Shtaka 63-0707M.

Saa 6:00 mchana.(ni saa 1:00 jioni ya TZ) Hebu tuungane tena katika maombi, tukimshukuru kwa WIKIENDI YA AJABU AMBAYO AMETUPA PAMOJA NAE NA BIBI_ARUSI WAKE.

Kwa ndugu na dada zangu wa nchi za ng’ambo, napenda kuwakaribisha kuungana nasi kwa masaa ya Jeffersonville, kwa masaa yote ya maombi kwenye ratiba hii na kwa kanda itakayochezwa Jumapili asubuhi. Natambua, hata hivyo, kwamba kucheza kanda Ijumaa na Jumamosi jioni saa za Jeffersonville itakuwa ngumu sana kwa wengi wenu, kwa hivyo tafadhali jisikie huru kucheza jumbe hizo wakati wowote wa siku unaofaa kwako. Ningependa, hata hivyo, sisi sote tuungane pamoja Jumapili saa 3:00 Asubuhi, saa ya Jeffersonville,(ni saa 10:00 jioni ya TZ) kusikia Ujumbe wetu wa Jumapili pamoja.

Bofya hapa kwa Ratiba inayoweza kuchapishwa iliyo katika mfumo wa PDF.

Napenda pia kukualika wewe na watoto wako kuwa sehemu ya karatasi za kazi za uundaji na maelekezo, na majaribio ya YF, ambayo familia yako yote inaweza kufurahia pamoja. Tunafikiri utayapenda kwani yote yanalenga NENO ambalo tutasikia wikendi hii.

Bofya hapa kuona nyenzo utakazohitaji kwaajili ya kazi za Uundaji. Kazi zenyewe zinaweza kutazamwa hapa.

Bofya hapa kwa majaribio ya kanda ya Wiki ya Pasaka.

Ni heshima kubwa kwangu kukualika wewe na familia yako kuungana pamoja na Bibi-arusi kote ulimwenguni kwa wikendi iliyojaa KUABUDU, KUSIFU NA UPONYAJI. Ni wikendi ambayo itabadilisha maisha yako.

Ndugu. Joseph Branham

27/03/2021

Mpendwa Hawa wa Pili,

Tutakumbuka daima siku ile ambayo Bwana aliunganisha Bibi-arusi Wake pamoja, kutoka mataifa yote ya ulimwengu, kutuambia, “wewe ni familia Yangu kuu ya kile kipeo, Hawa Wangu wa Pili. Sasa uko tayari kwa ile bustani, utawala wa miaka elfu. ”

Kile kipeo na Bibi-arusi, naye ni kipande Chake, ambacho lazima kiwe utimilifu wa Neno. Neno limetimizwa, na tuko tayari kwaajili ya Kuja kwa Bwana.

Je! Bibi-arusi huyu atafanyaje jambo hili? Je! Ngano hii itafanyaje jambo hili? Alituambia kwamba Malaki 4, na Ufunuo 10: 1-7 ingemkamilisha Bibi-arusi Wake. Sio mfumo, sio kundi la watu, lakini malaika_mjumbe wa 7 atairudisha, kama ilivyokuwa hapo mwanzo, kurudi kwenye Neno la Asili.

Angalia Ufunuo 10: 1 hadi 7, siri zote zitafunuliwa kwa Bibi-arusi, na mjumbe wa Kanisa la Laodikia.

Ikiwa siri ZOTE zitafunuliwa na mjumbe, basi hakuna njia bora ya kupokea siri zote kuliko njia iliyotolewa na Mungu, “BONYEZA PLAY,” na kusikia Sauti ya Mungu ikinena moja kwa moja kupitia nabii Wake na kufunua siri Zake zote.

Nimefurahi sana na nimeridhika sana. Hakuna kitu kingine chochote katika ulimwengu huu kinachojalisha ila Ujumbe huu, Neno Lake, Sauti hiyo. Najua kila mmoja wenu anahisi vivyo hivyo. Kila mmoja akishiriki Neno alilosikia tu mmoja kwa mwengine kwa kupiga au kutuma ujumbe mfupi wa nukuu zao pendwa.

Je! Umelikamata hili… wow… namaanisha WOW!
Sikuwahi KAMWE kusikia Ujumbe kama huo hapo awali, KAMWE.
Nimeikosaje nukuu hii miaka hii yote?
Aliniambia tu mimi nilikuwa Kipeo chake, UTUKUFU.
Ni Barua ya kimapenzi jinsi gani. Kito baada ya kito baada ya kito.
Haiwezi kuwa wazi zaidi ya hapo.
Je! Mtu yeyote anawezaje kutoona hili … Hayo ndio yote asemayo.
Kwa hivyo sasa ningependa kufanya jambo lile lile na kila mmoja wenu. Baada ya Ujumbe wa kesho mtakuwa mnatuma meseji na kupiga simu na kuzungumza kama kichaa. Yeye hukonga msumari na kuifunga yote pamoja kwaajili Hawa Wake.

Mimi pia nataka kukutia moyo. Ikiwa unaamini huyu ni Malaika_Mjumbe wa saba wa Mungu. Ikiwa unaamini Ujumbe huu ni Neno kwaajili ya siku hii. Unaamini kila Neno. Ikiwa unafuata UJUMBE WA MTU MMOJA, BASI NUKUU HIZI NI KWA AJILI YAKO.

Tumewasilii ! Tuko mwisho. Hilo si jambo la kijinga tu la mwanadamu. Hiyo ni BWANA ASEMA HIVI.
Nabii wa Mungu ni mfasiri wa Kiungu wa Neno la Mungu.
Huwezi kuongeza jambo moja Kwake, au kuondoa Neno moja kutoka Kwake.
Mtu katika mwili wa kibinadamu, kama nabii, lakini alikuwa Elohim akitambua mawazo yaliokuwa moyoni mwa Sara, nyuma Yake.
Mungu, katika umbo la mwanadamu, ambaye angeweza kutambua mawazo ya watu; mtu mmoja, sio dazeni; mtu mmoja, haijalishi kuna kuiga kungapi. Walikuwa na Mmoja.
Je! Ushahidi wa kweli ni nini? Yesu alisema, “Ili muamini ya kuwa mimi ndiye.” Naye ni Neno.
Nabii haimaanishi tu “mwonaji au mtabiri;” inamaanisha “mfunuzi wa Neno lililoandikwa … Neno lililoahidiwa kwa wakati huo.
Ndipo Mungu anamtuma nabii Wake, kwa … na nabii ni Neno la Mungu lililo hai, lililodhihirishwa.
Yesu, Mwana wa Mungu, akijifunua mwenyewe kwa Maandiko, akifanya Maandiko hayo (ambayo yamekusudiwa kwaajili ya siku hii, kama ilivyokuwa kwaajili ya siku hiyo, na siku zingine zote) yaishi. Na kuiamini, ni ushahidi wa Roho Mtakatifu.
Na unajuaje ikiwa ni Neno? Kila mmoja anasema hivi? Ni ahadi ya Biblia ikidhibitishwa kwa wakati huo.
Huu ni ufunuo mkamilifu wa Yesu Kristo. [Ndugu Branham anapapasa Biblia yake — Mh.] Na ile Mihuri Saba ilikuwa na siri zilizofichwa, za yote yalikuwa kitu gani.
Na jinsi gani Masihi… watu wanaomwamini wataijua isipokuwa ikiwa wako katika Neno kila wakati, kujua Yeye ni nini!
Ujumbe huu, Sauti hii, Kanda hizi, ni NENO PEKEE , lililothibitishwa na Mungu, kuwa Neno la wakati huu. NI KILA KITU KWETU. Hatujui kitu kingine chochote, hatutaki kitu kingine chochote, na hatuwezi kusikia kitu kingine chochote. Hatupingani na mtu mwingine yeyote, sisi tupo tu kwaajili ya, KUBONYEZA PLAY.

Kweli. Watoto wa Nuru, kubalini Neno Lake, endeleeni kutembea na kutazama likifunuka zaidi. Usiliache, haijalishi mtu mwingine anasema nini. Kaa moja kwa moja katika Hilo na endelea tu kutembea nalo, litazame ikijiweka wazi na Kujifunua. Neno ni Mbegu; mbegu katika aina sahihi ya udongo itazaa kwa jinsi yake.

Njoo ulisikie Neno la Mungu likijiweka wazi na kujifunua lenyewe kwa mataifa ya ulimwengu, Hawa wake wa pili,Jumapili saa 2:00 mchana, saa za Jeffersonville ,( SAA 21:00 usiku ya TZ) tunaposikia : Sikukuu ya Baragumu 64-0719M.

Ndugu. Joseph Branham

Maandiko ya kusoma kabla ya kusikia Ujumbe:

Mambo ya walawi 16
Mambo ya walawi 23: 23-27
Isaya 18: 1-3
Isaya 27: 12-13
Ufunuo 10: 1-7
Ufunuo 9: 13-14
Ufunuo 17: 8

20/03/2021

Mpendwa kipeo Kilichorejeshwa cha Mungu ,

Msimu huu wa Baridi umekuwa wakati waajabu mno na kipekee wa maisha yetu. Tumejifunza, na ametufunulia kitabu cha Ufunuo. Umekuwa wakati ambao hatutasahau kamwe.

Tunaweza kuona dalili tayari za kuleta Kanisa katika Uwepo wa Kristo. Bibi-arusi anachukua umbo. Tunavaa vazi la harusi, tukijifanya wenyewe tayari. Tunaweza kuona vimulimuli vikimemetesha. Tunajua kwamba tuko mwishoni. Tumefika. Tumewasili. Anakuja KWA AJILI YANGU NA WEWE !!

Uzao wa Kifalme sasa unakusanyika, tayari kwa ufufuo, tayari kwa mavuno. Alfa imekuwa Omega. Mbegu ile isiyokamilika iliyoanguka katika bustani ya Edeni sasa imerudi kwa Uzao mkamilifu, Hawa wa Pili, Bibi-arusi Neno Wake wa kweli tena. WEWE NDIYE HUYO BIBI_ARUSI NENO RAFIKI YANGU.

Ni furaha iliyoje kujua kwamba sisi ni Bibi-arusi Wake mkamilifu, katika mapenzi Yake makamilifu. Amesema na mioyo yetu kwa Ufunuo, na kufunua kwamba sisi ni Kipeo Chake kilichorejeshwa kikamilifu.

Ilimchukua Baba miaka elfu nne kutengeneza Kipeo Chake cha kwanza. Sasa amekuwa kwa miaka elfu mbili mingine akitengeneza Kipeo kingine, SISI, Bibi_arusi Wake, kwa ajili ya Kristo. Amefanya hivyo kwa njia Yake isiyobadilika kamwe, njia ile ile aliyokifanya Kipeo Chake cha kwanza, Neno Lake.

Hiyo ndiyo njia pekee Anayotengeneza vipeo vyake, kwa sababu Yeye anaweza tu kuwa Kipeo Kikamilifu wakati Ni Neno kamilifu, na Ujumbe huu ni NENO LAKE KAMILIFU, likimfanya Bibi-arusi Wake Mkamilifu.

Ikiwa Alichukua kutoka Kwake, uumbaji wa asili, kujitengenezea Bibi-arusi, Yeye hakufanya kiumbe kingine. Alichukua sehemu ya uumbaji wa asili. Halafu, kama Yeye alikuwa Neno, lazima Bibi-arusi awe kitu gani? Haina budi kuwa Neno la asili, Mungu akiishi katika Neno.

Je! Tunaweza kutambua, sisi ni Neno la asili lisilo na waa wala kunyanzi. Sisi ndio kile kipande kilichopigwa kutoka Kwake, kilichorejeshwa. Shetani hawezi kutudanganya tena. Sisi sio bibi-arusi fulani aliyebuniwa na wanadamu, sisi ni Neno lililo hai likitenda kazi.

Mavuno yamefika. Tumekufa nakuiva. Tuko tayari sasa kwa huo ujio. Huduma ya kwanza na ile ya mwisho ni sawa. Ujumbe wa kwanza na Ujumbe wa mwisho (wa pili) ni kitu kimoja. “Mimi, nilikuwa katika Alpha; Niko katika Omega. “

Familia ya Kile kipeo imekuja tena, Kristo na Bibi-arusi Wake, tayari kurudi Nyumbani kwao.

Bibi-arusi anasubiri kwa Hamu kuona yote ambayo ametuwekea wakati huu wa kuchipua. Tuko chini ya matarajio na matazamiyo makubwa. Njoo uungane nasi Jumapili saa 2:00 mchana, saa za Jeffersonville,( SAA 21:00 usiku ya TZ) wakati Roho Mtakatifu akiingia majumbani mwetu na kunena kupitia kinywa Chake alichokichagua, na kutuletea Ujumbe: Kile Kipeo 64-0705.

Ndugu. Joseph Branham

Maandiko ya kusoma kabla ya ibada:

Isaya 53: 1-12
Malaki 3: 6
Mtakatifu Mathayo 24:24
Mtakatifu Marko 9: 7
Mtakatifu Yohana 12:24
Mtakatifu Yohana 14: 9
Ufunuo 3:20

13/03/2021

Mpendwa Kundi dogo.

Je! Tunajua nini sasa, bila kivuli cha shaka, imefunuliwa kwetu?

SISI NDIO BIBI_ARUSI !!

Ninaweza kusikia utukufu, haleluya, kusifu na kupaaza sauti kutoka kwa Bibi-arusi kote ulimwenguni. Mpango mkuu wa baba sasa umekamilika. Hakuna swali zaidi. Hakuna kushangaa zaidi. Ufunuo tumepewa sisi. Sisi ni wateule Wake, waliochaguliwa kimbele, kipenzi ; SISI NDIO BIBI_ARUSI !!

Umoja wa Bibi-arusi Wake haujawahi kuwa mkubwa zaidi kama ilivyo siku hii. Bibi-arusi hajawahi kutokuwa na swali zaidi katika kujua wao ni nani, kama ilivyo leo. Hatujawahi kuwa na furaha zaidi, kuridhika zaidi, au kutosheka kuliko ilivyo leo. SISI NDIO Bibi harusi !!

Wengine wanaamini na kupumzika juu ya huduma tano kuwafunulia zaidi. Sisi hapana. Tunaamini Neno Lake halihitaji tafsiri yoyote. Tunaamini Alinena kupitia Sauti Yake iliyochaguliwa, aliirekodi ili tuweze kuisikia, na tunapumzika na kuamini kila Neno lililonenwa.

Hakuna mhubiri, mwalimu, mtume, nabii au mchungaji ambaye anaweza kumuunganisha Bibi-arusi; tunaweza kukuelekeza kwenye JAMBO MOJA PEKEE LITAKALO MKAMILISHA NA KULETA Bibi-arusi WOTE PAMOJA. Mungu mwenyewe akinena kupitia Malaika_mjumbe wake wa 7.

Hiyo ni ” William Branham asema hivi?” Hiyo ni “BWANA ASEMA HIVI!” Walakini, Yeye ni mtu tofauti na mimi, lakini njia pekee Anayotambulishwa ni kupitia mimi.

Haya yalikuwa maagizo kwa maskani yake. Labda usiwe sehemu ya maskani yake; hivyo, haingekuhusu. SISI TU. Alimwagiza mchungaji wake nini cha kufanya wakati hayupo hapa … na tunafanya hivyo.

Sasa, na tuna mchungaji mzuri, mtu halisi wa Mungu, na ninashukuru sana kwaajili ya jambo hilo. Ikiwa utakumbuka, lile ono, mwaka mmoja uliopita, Chakula hicho kilihifadhiwa mahali hapo. Na hiyo ni kweli kabisa.

Sauti ya Mungu inamvuta Bibi-arusi Wake pamoja zaidi ya hapo awali. Tunakaa pamoja katika makao ya kimbinguni wakati malaika wa 7 wa Mungu anapofunua Muhuri wa 7, Ngurumo Saba, Mvuto wa Tatu, na chochote tunachohitaji kwaajili ya kwenda kwenye unyakuo.

Ufalme wa Mungu unakuja. Tunakuwa zaidi kutoka hasi hadi chanya. Tunakuwa na uamsho kukusanyika kwenye Neno. Njoo uungane nasi Jumapili hii saa 2:00 Mchana, saa za Jeffersonville,( SAA 22:00 usiku ya TZ) tunaposikia yaliyofichwa tangu kuwekwa misingi ya ulimwengu, na sasa yanafunuliwa kwa Bibi-arusi Wake, tunaposikia: Muhuri wa Saba 63-0324E.

Ndugu. Joseph Branham.

Maandiko ya kusoma kabla ya kusikia Ujumbe:

Kumbukumbu la Torati 29: 16-19
I Wafalme 12: 25-30
Ezekieli 48: 1-7, 23-29
Mathayo 24: 31-32
Ufunuo 7
Ufunuo 8: 1
Ufunuo 10: 1-7
Ufunuo 14

20/02/2021

Mpendwa Moja ya Mia ya Asilimia mia Moja,

Hebu fikiria tu, tunamkaribisha Mfalme wa wafalme na Bwana wa mabwana katika nyumba zetu ndogo nyenyekevu kote ulimwenguni kila wiki. Hahitaji mazulia yatandazwe ili kumkaribisha; Anataka tu mioyo minyenyekevu iwekwe hapo, ili Yeye achukue mioyo yetu iliyo minyenyekevu na atufunulie mambo mazuri ambayo amewawekea wale wote wanaompenda.

Lakini sio tu nyumba yoyote au kwa watu wowote, lakini kwa kundi dogo la watu aliowachagua. Kundi la watu ambao amebisha hodi kwenye mlango wao, na wamefungua.

Sasa, tunatukuzwa tu sana,na tunashukuru kweli_kweli kwa Aliyotutendea, mkono mkuu wa ajabu wa Mungu aliye hai! Ni jambo gani kubwa zaidi lingekuwa, tungeweza kuwa watu wenye majaliwa zaidi jinsi gani, kuliko kuwa na Mfalme wa wafalme, Bwana wa mabwana kati yetu?

Tumefurahi sana na tunashukuru sana, hatujui tu la kufanya! SISI ndio moja ya mia ya asilimia mia moja ambayo inasikiliza na kuamini KILA NENO Yeye analonena na kutuambia.

“Mimi ni Neno aliyefanyika mwili. Nitakufunulia Ngurumo Saba, na Itakupa imani ya kunyakuliwa. Kwa sababu unaamini kila Neno, Wewe ni Malkia Wangu aliyehesabiwa haki na nitakupa Jina Jipya. Nitakufunulia mvuto wa Tatu. Unaweza Kunena Neno, kwa kuwa wewe ni Neno. Nimerejesha vitu vyote kwako. ”

“Sasa nina tu jambo fulani la kukuambia ambalo ni zuri sana, linawaka tu moyoni mwangu. Natumahi hutalisahau. Nilimruhusu malaika_mjumbe wangu awaone ninyi nyote mmevaa mavazi meupe. Ninyi akina dada mlikuwa kule na nywele zenu zikining’inia chini viunoni mwenu, bila viatu, nyote mlienda mbio_ mbio kuelekea kwake. ”

“Ndipo nikamruhusu aangalie upande ule mwingine na hapo linakuja kundi la ninyi wanaume. Nyote mlikuwa jamaa vijana, wapatao umri wa miaka ishirini. Mlikuwa na nywele nyeusi, na nywele za Shaba. Ninyi pia wote mlikuwa mmevaa mavazi meupe, na mkamkimbilia na kuanza kumkumbatia, mkipaza sauti, “Ndugu Mpendwa!”

“Nilimtwaa na kumweka juu, juu ya kitu kirefu sana, kwa sababu duniani alikuwa kiongozi wako. Ulimfuata yeye kama alivyonifuata MIMI. ”

“Ujumbe ambao alipaswa aunene kwako ulikuwa mkamilifu sana hivi kwamba sikuweza kuutumainia kumpa Malaika wa mbinguni, kwa hivyo nimempa Yeye, nabii_mjumbe malaika wangu wa duniani, William Marrion Branham. Nilimfunulia Kitabu hiki chote cha Ufunuo na nikamwambia akupe. ”

“Yeye ni nabii_tai Wangu. Kumbuka, hakuna nguvu tena zitakazotokea baada ya yule tai mkuu kunena. Nimempa siri zote akupe wewe, kama nilivyokuambia nitafanya. Kila kitu unachohitaji kipo ndani ya Jumbe hizo Zilizorekodiwa alizonena, kwa maana sio maneno yake, bali ni MANENO YANGU KWAKO. ”

“Usisahau kamwe, na kumbuka kile ulichomwambia wakati alipokuona kule:”

Kwa nini siwezi kumwona Yesu? ” Ikasema, “Vema, sasa, Yeye atakuja ataninii — Yeye atakuja siku moja. Naye atakuja kwako, kwanza, na ndipo utahukumiwa. ” Ikasema, “Watu hawa ni waongofu wako ambao umewaongoza.”

Nami nikasema, “Unamaanisha, mimi kuwa kiongozi,ni kwamba mimi…ni kwamba atanihukumu mimi?” Ikasema, “Ndiyo.” Ndipo nikasema, “Je! Kila kiongozi atapaswa kuhukumiwa namna hiyo?” Ikasema, “Ndiyo.”

Nikasema, “na Paulo je?” Akasema, “Itambidi kuhukumiwa pamoja na lake.”

“Vema,” nikasema, “Kama kundi lake likiingia, na langu pia, maana nimehubiri Neno lile lile kabisa.” Ndio Hivyo. Nikasema, “Pale alipobatiza katika Jina la Yesu, na mimi pia nilibatiza. Nilihubiri… ”

Na mamilioni wakapaza sauti, wote mara moja, wakasema, “Tunategemea jambo Hilo!”

Kuna NJIA MOJA tu ya kuwa kule rafiki yangu, kwa Kubonyeza Play, na kutegemea kila Neno linalonenwa na Tai nabii_mjumbe wa Mungu.

Njoo utegemee kila Neno pamoja nasi na uwe Ile moja ya mia ya asilimia mia moja, Jumapili saa 2:00 Mchana, saa ya Jeffersonville(SAA 22:00 Usiku ya TZ) tunaposikia: Muhuri wa Tano 63-0322

Ndugu. Joseph Branham

Maandiko ya kusoma kabla ya kusikia Ujumbe:

Danieli 9: 20-27
Matendo 15: 13-14
Warumi 11: 25-26
Ufunuo 6: 9-11
Ufunuo 11: 7-8
Ufunuo 22: 8-9

13.02.2021

Wapendwa Tai Wanao kusanyika,

Nasubiri kwa hamu kubwa kuungana nanyi na kusikia Sauti ya Mungu ikinena nasi moja kwa moja kupitia malaika Wake mwenye nguvu, anapouvunja Muhuri Wake wa 4 kwetu na kumwambia kila mmoja wetu, “Umezaliwa na Mimi, kwa hiyo huwezi kutenda dhambi . Kitakasaji cha damu Yangu kinasimama kwaajili yako. Ninaivunja na kuituma tena kwa yule aliyeipotosha. ”

Wakati Shetani anaponiambia, “Wana hatia!”, Ninamwambia, “Sio, wote ni safi. Siwezi hata kuikumbuka tena. Hawana dhambi kabisa. Wao ni Wangu. Ikiwa wakiuambia mlima ‘ng’oka,’ na wasitilie shaka moyoni mwao, lakini waamini kile nilichosema, KITATIMIA na watapokea kile walichoomba. Hao ni Wana_Tai Wangu waliokombolewa ”.

“Ninyi subirini tu Enyi wana tai wangu mpaka hizo Ngurumo Saba zitoe sauti zao kwako. Unaweza kuchukua Neno la Mungu na kulipeleka hapo. Utakata na kukata. Unaweza kufunga mbingu. Unaweza kufunga hili, au kufanya lile, chochote unachotaka. Adui atauawa na Neno linalotoka kinywani mwako kwa maana ni kali kuliko upanga wenye makali kuwili. Unaweza kuwaita nzi tani bilioni mia moja ikiwa ungetaka. Chochote unachonena, kitatokea, kwa sababu ni Neno la Mungu linalotoka kinywani mwa Mungu na nimekuwa nikimtumia mwanadamu kufanya kazi ya Neno Langu ”.

Kabla ya kuwa Neno, ni mawazo. Na wazo lazima liumbwe. Vema. Kwa hiyo, mawazo ya Mungu yakawa uumbaji wakati yaliponenwa, kwa Neno. Hapo ndipo Anapoliwasilisha kwako – kwako kama wazo, wazo Lake, na Limefunuliwa kwako. Halafu, bado ni wazo mpaka ulinene.

Ongea juu ya Changamko kwa Ufunuo. Mioyo yetu, akili zetu, roho zetu zinasifu na kupiga kelele, “utukufu, haleluya.” Amewasilisha Mawazo yake kwetu. Sasa yamefunuliwa kwetu. Tunaweza kuyanena.

Msiogope chochote Wana tai, Neno lake linakaa ndani yetu. Shetani hawezi kutudhuru, yeye ni mpumbavu tu, nena Neno. Alituchagua tangu mwanzo. Alitutumia mjumbe_tai wake wa mwisho ili kujifunua na kumwita Bibi-arusi Wake atoke. Tumemtambua. Tumejitambua sisi ni nani. Endelea kushikilia, haitachukua muda mrefu sasa, Anakuja kwaajili yetu.

Ikiwa ungependa kupata Changamko hili kwa Ufunuo, njoo usikie Sauti ya Mungu ikinena Jumapili saa 2:00 mchana, saa ya Jeffersonville,(SAA 22:00 Usk yaTZ) na umsikie Akifunua Muhuri Wake wa Nne kwa Bibi-arusi Wake.

Ndugu. Joseph Branham

Maandiko ya kusoma kwa kujiandaa kusikia mahubiri “Muhuri wa Nne” 63-0321.

Mtakatifu Mathayo 4
Mtakatifu Luka 24:49
Mtakatifu Yohana 6:63
Matendo 2:38
Ufunuo 2: 18-23, 6: 7-8, 10: 1-7, 12:13, 13: 1-14, 16: 12-16, 19: 15-17
Mwanzo 1: 1
Zaburi 16: 8-11
II Samweli 6:14
Yeremia 32
Yoeli 2:28
Amosi 3: 7
Malaki 4

30.01.2021

Mpendwa Malkia wa Mbinguni,

Tunawezaje kuanza kuelezea kile kinachofanyika. Kila siku, maandiko baada ya maandiko, unabii baada ya unabii unatimizwa. Mungu anaunganisha Malkia wake karibu na Neno Lake.

Ndege wa paradiso wameanza kuimba mioyoni mwetu. Tunajua kuwa haitakua muda mrefu kutoka sasa. Kitu fulani kinaenda kutokea. Wakati umefika. Bibi-arusi amejiweka tayari kwa kumsikiliza malaika_mjumbe wa 7 wa Mungu Anguruma Neno Lake.

Kila wiki tunakusanyika pamoja na chini ya matarajio makubwa kama tunavyohesabu, 5,4,3,2,1 … BONYEZA PLAY. Mara hiyo tu, Bibi-arusi ameunganishwa kutoka ulimwenguni kote. Kisha Mjumbe wake anasema nasi hapa duniani. Wakati huo huo, Mungu anaunga kitu kimoja kutoka Mbinguni. Ni Sauti ya Mungu ikiongea na Uzao Wake uliochaguliwa awali ikisema, “Wewe ni Bibi-arusi Wangu. Nakupenda Malkia wangu. Wakati umefika. Furahini, nimeandaa kila kitu tayari kwa Karamu ya Harusi yetu. ”

Sasa ni saa ya ufunuo. Vitu vyote vinafunuliwa tu wakati wa kuja kwake. Ni wakati wa mwisho kumaliza. Mioyo yetu huruka kwa furaha kila wiki Anapotupatia zawadi zaidi za harusi.

Nilimwona mwanamke mzuri akisimama, mrembo, amevaa mavazi ya rangi ya zambarau. Na nina mabano madogo hapa chini, “(Alikuwa mtawala mkuu huko Marekani; labda kanisa Katoliki.)” Mwanamke, mwanamke fulani; Sijui litakuwa kanisa Katoliki. Sijui. Siwezi kusema. Kitu pekee nilichoona, nilimwona yule mwanamke, hilo lilikuwa yote.

Wakati Bibi-arusi alikuwa akisikiliza Mihuri Saba ikifunuliwa, Kamala Harris alikuwa akiapishwa, kuwa mwanamke Makamu wa Rais wa kwanza wa Marekani. Sisemi kwamba huu ni unabii Ndugu Branham aliona ukitimizwa, lakini hakika inaonekana kama inaweza kuwa ni wenyewe.

Kamala Harris ameandika historia leo, kuwa mwanamke wa kwanza na mweusi wa kwanza na Makamu wa Rais wa Asia ya Amerika kusini. Katika sherehe ya uzinduzi wa 59, alikuwa amevaa mavazi ya zambarau na mkoti unaofanana kutoka kwa mbuni anayeibuka Christopher John Rogers. Alipata pia mkusanyiko wake na mkufu wa lulu kutoka kwa Wilfredo Rosado.

Haki ya Ubatili

Tulipokuwa tunasikiliza Nyakati saba za Kanisa , malaika_mjumbe wa 7 wa Mungu alitabiri na kutuambia baada ya Kennedy kutakuwa na Rais mwingine Mkatoliki wa Marekani.

Baada ya sherehe ya kuapishwa, Biden anakuwa mkatoliki wa pili kuongoza Marekani, tangu wa kwanza John F. Kennedy mnamo 1961

Leo

Hakuna wakati zaidi katika historia ya ulimwengu kuishi ndani yake. Msimu huu wa Baridi , unabii huu unatimizwa mbele ya macho yetu.

Na hatimaye itaishia, (ninatabiri), mwanamke atamdhibiti. Kumbuka, hiyo ilikuwa miaka thelathini iliyopita, nilisema. Na — na — yale mambo saba ambayo nilitabiri, matano kati yao yametimia. Nao wamempata yule mtu pale sasa kumleta ndani. Na mnalipigia kura, kupitia siasa zenu huko.

Neno la Mungu ni lisilokosea. Neno Lake haliwezi kushindwa, halina budi kutukia. Ana kiwango. Kiwango hicho ni Neno Lake. Mungu pia ana njia ya kufunua Neno Lake: “Sitafanya lolote, hata, mpaka nimfunulie kwanza mtumishi Wangu, nabii Wangu.” Kabla hajafanya chochote, Yeye hulifunua kwa nabii Wake. Naye anapolifunua, kuna jambo liko njiani.

Ngurumo saba zitampa Bibi-arusi imani ya kunyakuliwa .

.Imani huja kwa kusikia.
.Kusikia Neno la Mungu.
.Neno la Mungu humjia nabii.

Kuna SAUTI MOJA YA MUNGU.

“Kondoo wangu wanaijua Sauti Yangu.” Sauti, bila shaka, ni Neno Lake, wakati Yeye anazungumza. “Kondoo Wangu wanaijua Sauti Yangu. Sauti yangu imethibitishwa kwao, kuwa kweli. Imethibitishwa kuwa hiyo ni Sauti Yangu. ” Sasa, sasa angalia, hawatafuata sauti nyingine yoyote. Hawatafanya hivyo. “Kondoo wangu wanaijua Sauti Yangu, na mgeni hawatamfuata.”

Tunaijua Sauti hiyo na tunaipenda. Hatutakiwi kufuata sauti nyingine yoyote, bali Sauti Yake iliyo kwenye Kanda. Ni Bwana harusi wetu anayetuita Malkia wake.

Ah, Malkia wa Mungu, ni nini kinachokusubiria kila siku. Zawadi baada ya zawadi, baraka baada ya baraka, furaha baada ya furaha, ufunuo baada ya ufunuo.

Hebu na tuhesabu tena kinyume_nyume Jumapili hii saa 2:00 mchana, saa ya Jeffersonville, kusikia Sauti ya Mungu ikinguruma kwa Malkia Wake, tunaposikia: Muhuri wa Pili 63_0319.

Ndugu. Joseph Branham

Maandiko ya kusoma kabla ya kusikia ujumbe:

Mathayo 4:8/11:25_26/24:6
Marko 16:16
Yohana 14:12
2Wathessalonike 2:3
Waebrania 4:12
Ufunuo 2:6/6:3_4/sura ya 17/ 19:11_16
Yoeli 2:25
Amos 3:6_7

27.01.2021

Wapendwa Wateule,

Bibi-arusi bado anafurahi katika utukufu wa Neno lililosikiwa Jumapili. Mioyo yetu inafurahi, roho zetu zimeinuka; utambuzi kwamba sisi ni wateule wake unazidi kuwa wazi na halisi kila siku tunaposikia Ujumbe wa Ngurumo na kutuambia, “Tazama, nitakutumia Eliya nabii. Atakuwa Sauti Yangu kwako. Atakufunulia siri zangu zote. Itakupa imani ya Kunyakuliwa unayohitaji kuwa Bibi-arusi Wangu. ”

Yote tunayohitaji kipo katika hicho CHAKULA KILICHOHIFADHIWA. Alisema “Sitafanya chochote isipokuwa nitakapomfunulia nabii Wangu. Nimemfunulia na atakufunulia. ” Kwa hivyo, tunachohitaji kipo KWENYE KANDA.

Lakini alituonya, lazima tuwe tayari kwa ujio wake kila wakati. Lazima tuwe katika Neno kila wakati. Vita vinaendelea na kuna njia moja tu ya kumshinda adui, NENO.

Ninajaribu kusema nini? Sijaribu kukutisha, kukupa wasiwasi . Mimi-nataka uwe kwenye vidole vyako. Kuwa tayari, ukiangalia, kila dakika. Acha upuuzi wako. Nenda tu kwenye shughuli na Mungu, kwa sababu ni mwisho kuliko unavyofikiria.

Lazima tuingie kwenye shughuli. Neno lake linapaswa kuwa akilini mwetu na mioyoni mwetu kila dakika ya kila siku. Tunapoamka kila asubuhi, tukiwa kazini, kusafisha nyumba, kuwafundisha watoto, kuendesha gari, dukani, chochote tunachofanya, tunahitaji kutafakari Neno na kushirikiana naye kwa siku nzima.

Tuko karibu bibi_arusi, karibu kabisa. Anadhihirisha Neno Lake mbele yetu kila siku. Tunazidi kufanana naye kila siku inayopita. Hasi inakuwa chanya, kama vile alivyosema ingekuwa.

Hebu na tuombe vya kutosha leo, kesho, na kila siku. Usiruhusu Shetani akupigie chini, acha Neno hilo likuinue. Acha Baba akukumbushe unaposhirikiana Naye. USIWE NA HOFU, NIKO PAMOJA NAWE DAIMA. SEMA NENO TU, MAANA WEWE NI NENO LANGU.

Wakati umekaribia, Bwana Arusi anakuja kwa Bibi-arusi Wake anayengojewa kwa muda mrefu. Maelezo yote ya dakika ya mwisho yanatunzwa. Tunasikia gurudumu la gari linakuja. Kuwa tayari na chini ya matarajio makubwa. Atafanya nini na kunifunulia leo?

Ndugu. Joseph Branham

23.01.2021

Mpendwa Bibi_arusi Dhahabu Safi,

Je! Ungependa kusoma barua ya kipekee sana ya mapenzi kutoka kwa Bwana wetu Yesu kwako tu? Je! Ungependa kumsikia akikuambia anachofikiria juu yako?

“Kwangu wewe umefananishwa na Dhahabu safi; haki yako ni haki YANGU. Sifa zako ni sifa ZANGU zenye utukufu. Utambulisho wako unapatikana ndani YANGU. Kile nilicho, mnaakisi. Kile NILICHOKUWA, kinadhihirika ndani yako. Hamna kosa ndani yako. Wewe wote ni mtukufu, ndani na nje. Kuanzia mwanzo hadi mwisho wewe ni kazi YANGU, na kazi ZANGU zote ni kamilifu. Kwa kweli, ndani yako imejumlishwa na kudhihirishwa hekima ya milele na kusudi LANGU MWENYEWE. ”

Mtu anawezaje kulifahamu? Mtu anawezaje kulielewa? Ingawa hatuwezi kufanya hivyo, tunaweza kulipokea kwa imani, kwa maana Mungu amelinena.

Yeye anatupenda sana hata na zaidi hivi kwamba alituchagua sisi Atufunulie siri zake kuu zote.

Biblia iliandikwa kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu. Na Kristo, akiwa Mwana-Kondoo, alichinjwa kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu. Na wewe, Bibi-arusi Wake, jina lako liliwekwa katika Kitabu cha Uzima cha Mwana-Kondoo kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu.

Lakini, siri hizi zote zimefungwa kwa wakati wote. Tulihitaji Mkombozi Aliye Jamaa wa karibu ajitokeze na kufanya madai Yake, lakini hapakuwa na mtu ambaye angefanya hivyo; hakuna mtu Mbinguni, hakuna mtu duniani, hakuna mtu chini ya nchi. Hakukuwa na mtu anayestahili hata kukitazama Kitabu hicho.

Ndipo Mwana-Kondoo akashuka kutoka kwenye Kiti cha Enzi, na Damu kote juu yake. Yeye ndiye aliyeonekana anayestahili. Lakini ili mpango mkuu wa Mungu ukamilike, ilimbidi awe na mtu ambaye alihisi anastahili kufunua siri zake zote kuu, na watu ambao aliotaka kuwafunulia hilo.

Alikuwa tayari amemchagua malaika Wake mkuu kufunua hilo kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu, na Kundi maalum la watu Aliowaita Bibi-arusi Wake. Jina la malaika huyo mkuu lilikuwa William Marrion Branham. Kundi hilo maalum la watu ni WEWE, Bibi-arusi Wake aliyechaguliwa tangu zamani.

Naye akakitwaa kile Kitabu, (utukufu!) Akakifungua Kitabu, na kuing’oa Mihuri; na Akakituma chini duniani, kwa malaika Wake wa saba, kukifunua kwa watu Wake!

Jinsi gani tunavyoshukuru kujua sisi ni watu Wake ambao malaika_mjumbe wake wa saba anaowafunulia.

Ni Siri gani kuu zingine ambazo zimefichwa tangu kuwekwa misingi ya ulimwengu zitakazofunuliwa kwetu msimu huu wa baridi?

Na halafu kunakuja Ngurumo saba za siri ambazo hata hazijaandikwa. Hiyo ni kweli. Nami naamini ya kwamba, kupitia hizo Ngurumo Saba, zitafunuliwa katika siku za mwisho ili kumleta Bibi-arusi pamoja kwaajili ya imani ya kunyakuliwa.

Siri zote zimefunuliwa kwa malaika_mjumbe wa 7. Yeye peke yake ndiye anayeweza kuifunua kwa Bibi-arusi. Basi siri ya Ngurumo Saba iko katika Ujumbe huu. Ninaamini sasa inafunuliwa ili kumleta Bibi-arusi pamoja kwaajili ya imani ya kunyakuliwa.

Lakini ninawazia, wakati siri hizo zinapoanza kutokea, Mungu alisema, “Ishikilie sasa. Subiri kidogo. Nitaifunua katika siku hiyo. Usiiandike, hata kidogo, Yohana, kwa sababu watayumba juu Yake. Tu — acha tu, unaona. Lakini nitaifunua katika siku hiyo wakati itakapohitajika kufanywa. “

Tunaamini hii ndio siku hiyo. Mungu ana njia moja tu ya kulifunua kwa watu Wake: Nabii Wake. Kwa hiyo ikiwa ungependa kupokea Ufunuo wa Mihuri, Ngurumo Saba, na Siri zote zilizokuwa zimefichwa, njoo uungane nasi tunapomsikia yule ambae Mungu alimchagua kumfunulia, Atufunulie, Jumapili saa 2:00 mchana, saa ya Jeffersonville, tunaposikia
Muhuri wa Kwanza 63-0318.

Ndugu. Joseph Branham

Maandiko ya kusoma kwa kujiandaa kwa usikilizaji wa Ujumbe:

Mtakatifu Mathayo 10: 1/11: 1-14 / 24: 6 / 28:19
Mtakatifu Yohana 12: 23-28
Matendo 2:38
2 Wathesalonike 2: 3-12
Waebrania 4:12
Ufunuo 6: 1-2 / 10: 1-7 / 12: 7-9 / 13:16 / 19: 11-16
Malaki Sura ya 3 na 4
Danieli 8: 23-25 ​​/ 11:21 / 9: 25-27

16.1.2021

Wapendwa Waliokombolewa,

Huu utakuwa msimu wa baridi mkuu zaidi katika maisha yetu. Kwa kila siku mpya, Yeye atatupa Ufunuo mkuu wa yeye ALIKUWA Nani, ni nani SASA, na SISI TUMEKUWA nani.

Atatuambia jinsi anavyotupenda na amekuwa akingojea msimu huu wa baridi Ufike, ili aweze kutufunulia mpango wake kamili wa ukombozi katika Mihuri Saba hii. Itakuwa moja ya siku tukufu na muhimu sana ambayo ulimwengu uliwahi kujua.

Sikia yale yatakayotokea msimu huu wa baridi.

Yote ambayo Kristo atakayofanya mwishoni yatafunuliwa kwetu wiki hii, katika Mihuri Saba, ikiwa Mungu ataturuhusu. Unaona? Vema. Itafunuliwa. Na kufunuliwa, wakati Mihuri inavunjwa na kutolewa kwetu, ndipo tunaweza kuona mpango huu mkuu wa ukombozi ni kitu gani , na lini na jinsi gani utakavyofanyika.

Imani yetu itaongezeka kimo hata na zaidi wakati anapoelezea kile ukombozi wetu unachomaanisha kwetu. Atatuambia kuwa tunayo hati miliki ya Uzima wa Milele, ambayo inamaanisha kuwa tunamiliki kila kitu ambacho Adamu na Hawa walipoteza. Tutakuwa na utimilifu ,wa utawala mkuu, kama mungu mdogo, kwa sababu sisi ni wana na binti zake. Tutatawala kama wafalme na makuhani juu ya dunia milele yote na yeye.

Jinsi tutakavyobarikiwa wakati malaika_mjumbe wake anapotuambia jinsi Mungu alivyompeleka milimani mapema asubuhi moja na kuweka upanga wa Yule Mfalme, Neno Lake, mikononi mwake, na ulitosha mkono wake kikamilifu.

Atatufunulia kile kilichoendelea mbinguni wakati Mwana-Kondoo alipotembea na kukichukua Kitabu kutoka mkono wa kuume wa Yeye aketiye juu ya kiti cha enzi. Kisha Jinsi alivyokifungua , kuivunja ile Mihuri na kukipeleka chini duniani, kwa malaika_mjumbe Wake wa saba, na kisha yeye Akifunue kwetu, Bibi-arusi Wake.

Tutakuwa kama Yohana siku hiyo; kila kitu Mbinguni, kila kitu duniani, kila kitu chini ya dunia, kila kiumbe, kila kitu kingine kitatusikia tukisema, “Amina! Baraka, na utukufu, na hekima, na nguvu, na uweza, na utajiri, ni vyake yeye. ”

Hivi sasa tunatawala pamoja na Kristo, tukitawala dhambi, ulimwengu, mwili, na Ibilisi. Ni Kristo ndani yetu, anayependa na kufanya mapenzi Yake mema. Sasa tumeketi katika makao ya kimbinguni katika Kristo Yesu, tukimsikiliza akisema nasi kupitia malaika wake mkuu.

Msimu huu ujao wa baridi utakuwa wa baraka sana. Wakati ambao ulimwengu haujawahi kujua. Ni wakati wa Mavuno, na hivi Punde kila mmoja wetu anaweza kukaa chini ya mtini wake mwenyewe na kucheka na kufurahi na kuishi milele katika uwepo Wake na Furaha Timilifu.

Mungu anaandaa Mlima wake Mtakatifu, Bustani Yake mpya ya Edeni kwaajili ya Bibi-arusi na Wake na wahudumu wake, kwa fungate ya mwaka wa Elfu moja duniani. Kama vile Adamu na Hawa walivyokuwa katika bustani na hawakumaliza miaka elfu moja, sasa Yesu, Adamu wetu wa mwisho, na Hawa wake, SISI, Bibi-arusi wake, tutatimiza mpango wote wa Mungu.

Njoo ukae katika uwepo wa Roho Mtakatifu kwa Kubonyeza Play, Jumapili saa 2:00 Mchana, saa ya Jeffersonville, tunaposikia Malaika Wake wa saba akileta: Pengo kati ya Nyakati Saba za Kanisa Na ile Mihuri Saba 63-0317E.

Tutakuwa tukipiga kelele na kufurahi na kusema haleluya.

Ndugu. Joseph Branham

Maandiko ya kusoma kwa kujiandaa kwa usikilizaji wa Ujumbe:

Mambo ya Walawi: 25: 47-55
Yeremia: 32: 1-15
Zekaria: 3: 8-9 / 4:10
Warumi: 8: 22-23
Waefeso: 1: 13-14 / 4:30
Ufunuo: 1: 12-18/
Sura ya 5/ 10: 1-7 / 11:18

13.1.2021

Wapendwa wa Furahio,

Jinsi tunavyobubujika leo ndani ya mioyo yetu tunapotafakari na kumwabudu Bwana, kumshukuru kwa Ufunuo ambao ametupatia. Ufunuo Wake Mwenyewe katika siku yetu.

Ni Mungu, akiongea kupitia Malaika_Mjumbe wake mkuu; mchungaji wetu, nabii wetu, ambaye maisha yake yalizama ndani ya Kristo. Taa yake ilikuwa ikivuta uzima na Nuru kutoka kwenye rasilimali ya bakuli kuu, maisha halisi ya Kristo. Ni Mungu Akijificha Mwenyewe katika Urahisi, Kisha Akijifunua kwa jinsi hiyo kwa Bibi-arusi Wake.

Kwa sababu ametupa Ufunuo huo, sasa SOTE tunachota kutoka kwenye Chanzo kimoja. Sisi sote tumelowekwa kwenye bakuli moja. Wenyewe Tumekufa na maisha yetu yamefichwa pamoja na Kristo katika Mungu.

Tumetiwa muhuri na Roho Mtakatifu. Hakuna mtu awezaye kutunyakua kutoka mkononi mwake. Maisha yetu hayawezi kuchezewa. Maisha yake dhairi yanawaka na kuangaza ndani yetu, yakitoa Nuru na Madhihirisho ya Roho Mtakatifu kwa ulimwengu.

Shetani hawezi kutugusa. Hata kifo hakiwezi kutugusa, kwani kifo kimepoteza uchungu wake; kaburi limepoteza ushindi wake.

Msikilize Bwana akizungumza na kututia moyo leo.

Neno Hilo halijawahi kushindwa vinywani mwa Wakristo wanaoamini. Na katika wakati huu wa mwisho hapa lina nguvu na kuu kuliko wakati wowote katika bibi-arusi Neno wa kweli. Loo, kundi dogo, enyi wachache, shikilieni Neno, jazeni kinywa na moyo kwa hilo, na siku Moja Mungu atawapa ufalme.

Furahi na kumsifu Bwana leo kwa yote aliyoyafanya, yale atakayoyafanya, na bila kusahau kile anachotufanyia leo.

Ndugu. Joseph Branham

9.1.2021

Wapendwa Wakipekee,

Sisi ni tofauti na mwenendo wa ustaharabu wa kisasa. Tumekuwa wasio wa kawaida, wa ajabu, na hata wa juu zaidi kati ya ndugu na dada zetu.

Sisi ni watu wa pekee, ukuhani wa kiroho, taifa la kifalme, tunatoa sadaka za kiroho kwa Mungu, na tunda la midomo yetu, tukilisifu Jina Lake kwa kusema tunaamini kila Neno Alilolinena kupitia Malaika_Mjumbe wake wa saba. Tunaitwa Wakipekee: Watu Wa Kanda, na tunafurahi sana kuitwa MMOJA WAO.

Kwa nini tunaamini namna hii? Tumeamriwa na Malaika_Mjumbe wa 7 aliyethibitishwa na Mungu kufanya hivyo.

Kwa hiyo, sasa, sikiliza kila Neno. Lipate hilo. Na — na ikiwa unalichukua kwenye kanda, au kitu chochote kile, basi kaa sawa sawa na Mafundisho ya hizo kanda. Usiseme chochote isipokuwa kile kanda inachosema. Sema tu haswa kile kanda inachosema. Unaona? Sasa, kwa sababu, baadhi ya mambo hayo, tutaelewa mengi kabisa kuhusu hili sasa, kwa nini halieleweki. Unaona? Na uwe na hakika, sema tu yale ambayo kanda inachosema. Usiseme kitu kingine chochote. Unaona? Maana, sisemi Hilo mwenyewe. Ni Yeye anayesema hilo, unaona. Na mara nyingi sana, kuchanganyikiwa, watu huinuka na kusema, “Vema, fulani-na Fulani-alisema Ilimaanisha hivi-na-hivi.” Hebu-liache tu jinsi lilivyo. Tazama, ndivyo tunavyoitaka Biblia. Jinsi tu Biblia inavyolisema, ndivyo tunavyolitaka, tu — kama hivyo tu. Usiweke tafsiri yako mwenyewe. Imetafsiriwa tayari, unaona.

Ni pumziko jinsi gani, ni amani iliyoje Bibi-arusi aliyo nayo. Imefunuliwa kuwa kuna njia moja tu pekee ya kutochanganyikiwa kwa hili na lile wanalosema kuwa inamaanisha hivi. Kuna njia moja tu pekee ya kusema haswa kile Kanda zinachosema, BONYEZA PLAY, kwani haiitaji tafsiri.

Tumeamini Ujumbe huu wakati wote, lakini sasa kuna kitu cha tofauti, kuna badiliko Linalofanyika ndani ya Bibi-arusi Wake. Tumekuwa tukikaa katika uwepo wa Mwana na tunaiva. Ni njia pekee ambayo Bibi-arusi anaweza kujifanya tayari kwa mavuno, KUBONYEZA PLAY NA KUTII.

Itatokea tu kama tulivyosema. Watu wa Mungu wanafanywa tayari kwa Neno la Kweli kutoka kwa mjumbe hadi wakati huu. Ndani yake kutakuwa na utimilifu wa Pentekoste kwa kuwa Roho atawarudisha watu pale pale walipokuwa hapo mwanzo. Hiyo ni “Bwana asema hivi.”

Hiyo inasisimua tu roho zetu. Tunataka kupiga kelele na kupaaza sauti. Hatupaswi kushangaa, au kukisia, au hata kutumaini tuko katika Mapenzi yake makamilifu tuna “Bwana Asema Hivi”. Tunafanywa tayari kwa Neno la kweli kwa KUBONYEZA PLAY.

Hata wakati hasa wa kusikia zile Nyakati Saba za Kanisa umekuwa mkamilifu. Tumeona unabii ukitimizwa hivi leo.

  • Tumekuwa na rais mmoja Mkatoliki na bila shaka tutakuwa na mwingine

Leo, wakati tunasikiliza Ujumbe huu, unabii huu ulitimizwa.

Tumeona matukio ya ulimwengu yakijipanga kikamilifu na Neno.

  • Kanisa na serikali, dini na siasa zinaungana pamoja.
  • Laodikia, “haki za watu,” au “haki ya watu.”
  • Mataifa yote yanainuka na kudai usawa, kijamii na kifedha.
  • Kahaba ataharibu mfumo wa sasa wa pesa

Inathibitisha kwetu kwamba wakati wa Mungu ni mkamilifu kila wakati.

“Wakati umekaribia.” Wakati haukuwa umekaribia hapo awali. Katika hekima na uchumi wa Mungu ufunuo huu wenye nguvu (ingawa ulijulikana kabisa na Mungu) haungeweza kutokea ila sasa. Kwa hivyo tunajifunza kanuni mara moja – ufunuo wa Mungu kwa kila kizazi unaweza kuja katika wakati huo uliokusudiwa tu, na kwa wakati maalum. Angalia historia ya Israeli. Ufunuo wa Mungu kwa Musa ulikuja tu wakati maalum wa historia, na haswa ulikuja wakati watu walipomlilia Mungu. Yesu, Mwenyewe, alikuja wakati Mkamilifu, Yeye ndiye Ufunuo kamili wa Uungu. Na katika wakati huu (Laodikia) ufunuo wa Mungu utakuja kwa wakati wake. Hautayumba, wala hautawahi . Fikiria juu ya hili na ulizingatie vizuri, kwani tuko katika wakati wa mwisho leo.

Kama nyinyi, nimebarikiwa sana wakati nikisikiliza na kusoma Zile Nyakati Saba za Kanisa, nikijua ni wakati muafaka wa Mungu.

Bwana ameweka moyoni mwangu kwa sisi kuendelea na kitabu cha Ufunuo wakati wote wa msimu wa baridi.

  • Laiti tungekuwa nayo wakati wote wa baridi tu, kwa hivyo tungeweza tu kuchukua Kitabu chote cha Ufunuo na kukipitia tu. “Ono La Patmo” na Ile Mihuri itafunguliwa katika kipindi hiki cha wakati wakanisa, na zile siri saba za Mungu zitafahamika,
  • Lo, ningependa kuiweka tu wakati wote wa baridi na kuupitia. “Wakati wa Kanisa la Efeso”
  • Ni mwisho wa wakati, na kila kitu kinaangukia hapa mahali pamoja, kwa hiyo ndipo tunapaswa kuwa na pumziko msimu wa baridi tu kutoa hili, lakini sisi… kuwa na Kitabu cha Ufunuo, kuona jinsi Inavyoungana pamoja . “Wanawali Kumi, na Wayahudi mia na Arobaini na Nne Elfu”
  • Halafu tunapomaliza na huo, kuinua huo juu, kuvuta huo mwingine chini kama hivi na kuanza juu ya hiyo, na kuufundisha. Loo, hiyo ingekuwa kama mbingu ndogo, sivyo? Kukaa tu majira ya baridi kikamilifu, kukaa tu na Bwana. “Ufunuo, Sura ya Nne # 2”

Siwezi kusubiri kukaa tu wakati kamili wa msimu wa baridi na Bwana anapotufunulia kitabu cha Ufunuo. Tutaona Neno likitimizwa na kudhihirishwa mbele ya macho yetu. Utakuwa wakati mtukufu sana kwa Bibi-arusi Wake.

Itahitaji utendaji wa Roho Mtakatifu kwa sababu haiwezi kufunuliwa kwa mtu yeyote isipokuwa jamii maalum ya watu. Itahitaji mmoja mwenye ufahamu wa kinabii. Itahitaji uwezo wa kusikia kutoka kwa Mungu. Itahitaji maagizo ya yakimbinguni .

Ninyi ni jamii hiyo ya watu. Una ufahamu huo wa kinabii. Una uwezo wa kusikia kutoka kwa Mungu. Unaamini kila Neno la maagizo ya yakimbinguni yako.

Njoo, uungane pamoja nasi kulizunguka Neno Lake, Jumapili, saa 2:00 Mchana, saa ya Jeffersonville( saa 22:00 usiku ya Tz), na usikie maagizo ya Mungu ya ngurumo ya Yakimbinguni , tunaposikiliza; 63-0317A – Mungu Akijificha katika Urahisi, Kisha Akijifunua mwenyewe kwa jinsi hiyo hiyo.

Ningependa tuanzie kwenye aya ya # 94, baada ya ibada ya kuweka wakfu. Ikiwa Bwana Akipenda , na bado tuko hapa, ningependa kucheza sehemu hiyo ya Ujumbe kwaajili ya ibada yetu ya kuweka wakfu baada ya ujenzi upya wa jengo letu .

Wakati Bwana aliweka moyoni mwangu kuendelea msimu huu wa baridi na kitabu cha Ufunuo, nilikwenda kwenye kalenda yangu ili kuona ni lini siku hizi zitaangukia. Tunaposikiliza Muhuri wa Saba, itakuwa wikendi ya mwisho ya msimu wa baridi na wikendi inayofuata ikiwa siku ya kwanza ya kuchipua, UTUKUFU !!

Ndugu. Joseph Branham

Maandiko ya kusoma kabla ya Ujumbe:

1 Mambo ya Nyakati 17: 1-8
Isaya 35: 8/40: 1-5 / 53: 1
Malaki Sura ya 3
Mathayo Mtakatifu 11:10, 11: 25-26
Yohana Mtakatifu 14: 1-6
1 Wakorintho Sura ya 13
Ufunuo Sura ya 21

30.12.2020

Ndama Wapendwa Katika Banda,

Tazama, nitawatumia Eliya nabii kabla haijaja Siku ile ya Bwana iliyo kuu na ya kuogofya.

Ametimiza Neno Lake kama alivyoahidi na kumtuma Nabii Wake mkuu Eliya kuigeuza mioyo ya watoto iwaelekee baba zao. Yule atakayeinuka na uponyaji katika mbawa zake (kampeni za uponyaji) na Bibi-arusi atakua kama ndama katika zizi (kula tu chakula kilichohifadhiwa). Yule ambaye ilikuwa arudishe vitu vyote, kufunua Siri zote zilizofichwa na kumwita Bibi-arusi atoke.

Tumemtambua malaika_mjumbe huyu mkuu , na jina lake ni William Marrion Branham, na sisi ni yule Bibi-arusi Neno ambaye alitumwa kumwita atoke.

Wakati anapo Nena, ni barua ya Mapenzi kwetu. Ni Mafuta ya Dhahabu ya Roho; Inamwagika moyoni mwako, kwa maana si maneno ya mwanadamu, bali ni Maneno kabisa ya Bwana wetu Yesu Kristo , anapoongea mdomo kwa sikio na nabii Wake Mwenye nguvu kusema na Bibi-arusi Wake.

Wengi hawamtambui yeye ni nani, au hawaelewi jinsi wanavyopaswa kuwa waangalifu kusema tu kile anachosema. Sio kuongeza au kuondoa kutoka kwenye Ujumbe wake.

Alituambia kutakuwa na wengi watakaoinuka na kuamini kuwa wao pia walichaguliwa kuongoza Bibi-arusi, lakini bibi huyo aliyechaguliwa hatadanganywa, kwani wanaamini haswa kile nabii anasema.

Tutakuwa tukimtazamia yule mtu mkuu ainuke. Anaweza kuja katika siku yangu, anaweza kuja siku ndogo, sijui. Anaweza kuwa yupo hapa kati yetu sasa, hatuwezi kueleza. Roho Mtakatifu yuko hapa kutuongoza hadi wakati huo, basi wakati kiongozi huyu atatuongoza, atakuwa bado amepakwa mafuta na Roho Mtakatifu; Yule_Yule Eliya atafanya hivyo, kwa kweli, yeye atakayekuja.

Roho Mtakatifu aliyemwagwa na kupewa kila mmoja wetu siku ya Pentekoste atatupeleka kwa kiongozi huyu mkuu wa Roho Mtakatifu aliyepakwa mafuta, naye atatuongoza … UTUKUFU !!

Tuko katika siku za mwisho za kufunga za mwaka 2020, lakini pia tuko katika siku za mwisho za kufunga za ulimwengu na kuja kwa Bwana wetu Yesu, kutupeleka kwenye karamu yetu kuu ya Harusi.

Je! Tumekuwa sehemu ya nini na kuona yakifanyika mwaka huu, zaidi ya wakati mwingine wowote katika historia ya ulimwengu?

Mungu anamuunganisha Bibi-arusi Wake. Anakuja pamoja, kutoka Mashariki na Magharibi, na Kaskazini na Kusini. Kuna wakati wa kuungana, na huyo upo sasa hivi. Anaungana kwaajili gani? Unyakuo. Amina! Mungu anamtayarisha. Ndio bwana, kuungana! Anaungana na nini? Pamoja na Neno! “Kwa maana mbingu na Nchi zitapita, lakini Neno Langu halitapita kamwe.” Anajiunganisha mwenyewe na BWANA ASEMA HIVI bila kujali madhehebu yoyote au mtu mwingine yeyote anasema nini. Anajiunganisha. Anajifanya tayari. Kwa nini? Yeye ndiye Bibi-arusi. Hiyo ni kweli . Naye anajiunganisha Mwenyewe na Bwana Arusi Wake, unaona, na Bwana Arusi ni Neno. “Hapo mwanzo alikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu. Naye Neno alifanyika mwili akakaa kwetu. ”

Tunaweza kuona kwa kusoma Maandiko na kusikia Neno kwamba tuko mwisho. Tunaishi katika siku za mwisho, kizazi ambacho kitamwona Yesu Kristo akirudi duniani. Watakatifu wa kabla yetu walitamani kuiona siku hii, walingojea siku hii, lakini sasa imewadia, na sisi ni sehemu Yake.

Hebu tuweke kando kila kitu mwaka huu ujao na tuzidi kukata tamaa na tujiandae kwa kuja kwake.

  • Ni wajibu wako, kujiandaa. “Bibi-arusi amejifanya mwenyewe tayari.” Mavazi yamelipiwa. Wako tayari, lakini lazima uwe tayari kuvaa nguo hizo.
  • Anakuja kwa ajili ya Bibi-arusi, ambaye hajipumbazi na ulimwengu au vitu vya ulimwengu. Ameoshwa katika Damu ya Mwanakondoo. Amemuahidi-Upendo wake kwake yeye tu. Upendo wa ulimwengu umekwenda na umekufa kwake. “Ndoa ya Mwana-Kondoo imekuja, na Bibi-arusi Wake amejifanya mwenyewe tayari.”

Ningependa tusikilize jumbe Zifuatazo kwani mwaka 2020 unamalizika, na tunajiandaa kwa yote ambayo ametuwekea mwaka huu ujao.

Alhamisi jioni, Tarehe 31 Decemba, Saa utakayochagua wewe, hebu tusikie Ujumbe wa Hawa wa Mwaka Mpya: Ufunuo, Sura ya Nne #1 60-1231

Ijumaa asubuhi, Tarehe 01 Januari , Saa utakayochagua wewe, hebu tusikie Ujumbe wa Mwaka Mpya: Ufunuo Sura ya Nne #2 61-0101

Jumapili, Tarehe 03 Januari , tuungane Pamoja Saa 2:00 Mchana Majira ya Jeffersonville ( SAA 22:00 usiku ya Tz.) Kusikia ujumbe :Ufunuo sura ya Nne #3. 61_0108

Ndugu , Joseph Branham

26.12.2020

Mpendwa Bibi-arusi Neno Mkamilifu,

 Bibi-arusi anafurahi sana na mwenye Matarajio makuu  tunapojiandaa kusikia Ujumbe wa jiwe la kifuniko wa wakati wa mwisho wa kanisa, Laodikia.  Ni wakati mkuu zaidi wa nyakati Zote , na Mjumbe mkuu zaidi wa nyakati zote, ambaye anakusanya watu wakuu zaidi wa nyakati zote.

Hakujawahi kuwa na siku kama siku tunayoishi. Ulimwengu unaweza kusikia Sauti ya Mungu kama vile andiko lilivyotabiri katika Neno Lake.  Ufunuo 10: 7, Katika siku za SAUTI.  Angalia, SI MASAUTI(sauti nyingi), BALI SAUTI.

 Mungu aliahidi kumtuma malaika mwenye nguvu katika wakati huu wa mwisho kufunua siri zote ambazo alikuwa amezificha tangu kuwekwa misingi ya ulimwengu.  Atakuwa malaika_mjumbe aliyethibitishwa kuliko mwingine yeyote, kwa maana amechaguliwa kumwita Bibi-arusi Wake Atoke.

Wengi watamkataa.  Wengine watasema huwezi kuamini yote anayosema;  Ila tu anaposema Bwana asema hivi. Kuna makosa katika ujumbe wake.  Sio yeye tu, kuna wengine walioitwa na kupakwa mafuta kumuongoza Bibi-arusi na kufunua kweli.

Neno linasema kutakuwa na kundi teule la watu ambao wataamini kila Neno mjumbe huyu kutoka kwa Mungu alilosema;  kwa kuwa agizo lake lilikuwa “Wafanye watu WAKUAMINI”.

 Kwa hiyo, ni lazima tuamini baadhi tu ya yale aliyosema?  Je! Neno linasema, “Nitakutumia Eliya nabii kisha tena nitakutumia watu wengine kukuambia lipi ni Neno na lipi sio Neno?”

Maneno yangu yatashindwa, lakini Maneno ya Mungu hayawezi kushindwa. Hebu na tusome ni Mamlaka gani MUNGU ATAKAYOMPA Malaika wake wa Saba.

Ni nani basi atakayekuwa na nguvu ya kutokushindwa ambayo itarejeshwa katika wakati huu wa mwisho, kwani wakati huu wa mwisho utarejea kudhihirisha Bibi-arusi Neno Safi?  Hiyo inamaanisha tutakuwa na Neno mara nyingine tena kama lilivyotolewa kikamilifu, na kueleweka kikamilifu katika siku za Paulo.  Nitakuambia ni nani atakayekuwa nalo. Atakuwa nabii aliyethibitishwa kabisa, au hata na zaidi amethibitishwa kabisa kuliko nabii yeyote katika nyakati zote tangu Enoko hadi leo hii, kwa sababu mtu huyu atakuwa na huduma kuu ya  kinabii ya jiwe La kifuniko, na Mungu atamweka wazi.  Hataitaji kuongea mwenyewe, Mungu ataongea kwaajili yake kwa sauti ya ishara.  Amina.

Utukufu !!  Haleluya !!  Sauti tunayoisikiliza tunapo BONYEZA PLAY, imetolewa kikamilifu, na inaeleweka kikamilifu, NA INAONGEA MANENO YASIOSHINDWA.  (Webster: isioweza kukosea.)

Ni pumziko la jinsi gani Bibi_arusi alilonalo tunaposikiliza Neno safi la Mungu.  Hakuna kubashiri, hakuna kushangaa, hakuna haja ya kwenda kumsikia huyu, au kwenda kumsikia yule;  tunayo yote KATIKA SAUTI MOJA KWENYE KANDA.

hebu na tuende kutafuta na kung’asha vitu muhimu zaidi na tuone kile Mungu anachosema juu ya malaika wetu.

-Yeye atasikia tu kutoka kwa Mungu na
-Atakuwa na “Bwana asema hivi” na kunena kwa niaba ya Mungu. Yeye
-Atakuwa kinywa cha Mungu.
-Atawarudisha wateule wa siku za mwisho.
-Atairudisha kweli.

Sasa na tuang’aizie  baadhi ya vitu muhimu wakati anapozungumza kutuhusu sisi, kundi hilo maalum aliloita, aliloteua na kuchagua kuamini kila Neno;  Bibi_arusi wake.

-Na hao wateule walio pomoja  naye katika siku hiyo watakuwa ndio wanaomdhihirisha Bwana kwa kweli na watakuwa ndio Mwili wake na kuwa sauti yake na kutenda kazi zake.  Haleluya!  Je! Unaliona hilo?
-Katika wakati huu wa mwisho kuna watu wengine nchini, ambao chini ya mjumbe wao watakuwa ndio sauti ya mwisho kwa wakati wa mwisho.
-Kanisa si  “kinywa” cha Mungu tena.  Ni kinywa chake lenyewe
-Sauti ya Mungu itakuwa ndani ya bibi_arusi.  Ndio Iko, kwa maana inasema katika sura ya mwisho ya Ufunuo mstari wa 17, “Roho na bibi_arusi wasema, Njoo.”
-Amempa bibi_arusi Sauti.
-Wateule hawawezi kudanganywa

Ongea juu ya kupumzika, ametupa Sauti yake na hatuwezi kudanganywa, sisi ni MMOJA na yeye.

Sasa, thawabu yetu ya kukaa wa kweli kwa nabii huyo na kuamini kila Neno kwa kusikiliza Sauti hiyo.

-Hao wanaompokea nabii huyo katika jina lake mwenyewe watapokea matokeo mema ya huduma ya nabii huyo.  Na hao wanaomsikia watabarikiwa na kuwa sehemu ya bibi-arusi wa siku  ya mwisho anayetajwa katika Ufunuo 22:17, “Roho na bibi_arusi wanasema, Njoo.”

Ikiwa ungependa kupokea thawabu hiyo, njoo uungane nasi Jumapili hii saa 2:00 mchana saa ya Jeffersonville ( saa 22:usiku ya TZ), kusikia: Wakati wa Kanisa la Laodikia 60-1211e, au vile Napenda kuuita, Hadithi ya Maisha yangu.

Ndugu.  Joseph Branham

Malaki 4: 1-6
Mtakatifu Mathayo 2: 14-15, 17: 9-13
Mtakatifu Luka 1: 14-17
Warumi 11: 15-27
Ufunuo 3: 14-22

23.12.2020

JUMATANO, DESEMBA 23, 2020
Mpendwa Bibi_arusi Kipenzi,

Jinsi tumekuwa tukifurahiya dhamana ya wokovu wetu, ambayo ni malipo yetu ya chini tu. Ikiwa dhamana ni ya ajabu hivi, itakuwaje tukipata bei kamili. Itakuwa tukufu!

Ningependa kuchukua fursa hii kumtakia kila mmoja wenu na familia yako baraka nyingi za Bwana wakati huu wa msimu wa sikukuu.

Na tukumbuke kile Nabii wetu alichotufundisha. Sio juu ya Santa Claus na kumpa mtu zawadi, hilo ni fundisho la sharti la Kikatoliki. Wala sio juu ya mtoto aliye kwenye hori. Tunamwabudu Yesu Kristo aliyefufuka, Mungu Mwenyezi, katika Uungu wa Mwanawe.

Katika Siku hii ya Krismasi, kwa wakati wako utakaochagua , Natufarahie zawadi kuu zaidi ambayo mwanadamu aliyowahi kupewa ; Roho wake Mtakatifu, Anapozungumza kupitia Nabii wake kwa Bibi-arusi wake mpendwa na kutuletea ujumbe, Zawadi ya Mungu iliyofungwa 60-1225.

Ndugu. Joseph Branham

branhamtabernacle.org

19.12.2020

16.12.2020

Mpendwa Kanisa Lisilo na Waa Wala kunyanzi,

Jinsi gani Tulivyo na shukrani leo kwa yote aliyoyatenda, na yote anayotutendea. Tunapoenda kwake katika maombi, na kujaribu kuelezea kile kilicho ndani ya mioyo yetu, haiwezekani. Kwa hivyo, kama kila kitu kingine tunachofanya, tunageukia kwenye Neno, kwani ni KILA KITU KWETU.

Loo, Hebu na tuinamishe vichwa vyetu na kusema: “Baba, tunakupenda. Tunakupenda. Loo, jinsi tunavyokupenda! Tunakushukuru tu, sana, Bwana. Loo, yetu — mioyo yetu duni ya kibinadamu haiwezi kuelezea kile tunachohisi ndani yetu, kwa jinsi ulivyotuosha katika Damu Yako Mwenyewe. Tulikuwa wageni, Bwana. Sisi-tulipenda vitu vya ulimwengu, na sote tulikuwa-wote tumechanganyikana huko nje katika vitu vya ulimwengu, na Wewe unashuka chini kwa neema Yako na kufikia mikono Yako mitakatifu ya thamani chini kwenye matope ya dhambi ambayo tulikuwa, ukatutoa, ukatuchagua, ukatuosha, ukatusafisha, ukaweka Roho Mpya ndani yetu, na kuweka Mapenzi yetu kwa vitu vilivyo juu. Jinsi gani Tunavyokupenda, Bwana! ”

NEEMA YAKO YA AJABU Baba. kufikiria UMEtuchagua, UMEtuosha, halafu UMEweka Roho Wako ndani yetu. Ndio Bwana, Tunakupenda!

Katika Wakati huu uliodanganywa, hakuna kitu kingine ulimwenguni kilichobaki kwaajili yetu, Bwana. Hakuna kilichobaki kwa ulimwengu, ni-ni-ni katika wakati wa mwisho. Tunaona kupitia Biblia, kila wakati umekwenda. Sasa tuko mwishoni, tunatoka haraka. Haitakuwa mbali na Yesu atakuja. Ee Mungu, weka mioyo yetu moto, usituache tusimame tuli.

Ee Bwana, jinsi gani tunashukuru kwamba Unawasha mioyo yetu moto kwa kutufunulia Neno lako ni kama zaidi ya hapo Awali . Tunaweza kuona, kwa kusikia Neno lako, kwamba tuko mwisho. Maandiko yanatimizwa mbele ya macho yetu kila siku.

Bwana, kutoka kwenye kina cha mioyo yetu, haya ni maombi yetu:

Na sasa, Bwana, ninaomba kwamba utachukua roho zetu mkononi mwako,tuoshe, tupige pasi, kwa sababu ilisemwa ulikuwa “unakuja kwaajili ya Kanisa lisilo na waa wala kunyazi.” Hebu pasi ya moto wa Roho Mtakatifu na ibonyeze kabisa kunyanzi zote kutoka kwetu, na tunakaa tayari kwa ujio wa Mwana wa Adamu.

Amina na amina.

Ndugu Joseph
branhamtabernacle.org

An Independent Church of the WORD,