UJUMBE: 65-0829 Edeni Ya Shetani
- 26-0705 Edeni Ya Shetani
- 24-0922 Edeni Ya Shetani
- 23-0305 Edeni ya Shetani
- 21-1107 Edeni ya Shetani
- 17-0118 Edeni Ya Shetani – Preliminari
Mpendwa Bibi-arusi Mkamilifu,
Lakini kuuona udanganyifu wa adui, kamwe hatujawahi kuwa na wakati kama huu tunaoishi sasa, ni wakati wa ujanja sana, udanganyifu kuliko wakati wo wote. Na ninapoona hilo, huniletea hili kwamba Mkristo anapaswa kuwa mwangalifu zaidi siku ya leo, kuliko alivyowahi kuwa katika wakati mwingine wo wote.
Ndugu Branham alimwambia Bibi-arusi maneno haya karibu miaka 61 iliyopita hadi sasa. Udanganyifu wa yule adui miaka 61 iliyopita ulikuwaje ikilinganishwa na sasa? Ili kuliweka hilo katika mtazamo tofauti, teknolojia ya dunia miaka 61 iliyopita ilikuwaje ikilinganishwa na vile ilivyo leo?
Mwaka wa 1961 ulikuwa ndio mwanzo wa Mbio za Anga, kompyuta zilikuwa zenye fremu kuu kubwa zenye ukubwa wa chumba zikifanya kazi kupitia mirija ya utupu na kadi za panchi ambazo zilihitaji wanasayansi maalum kuzipanga. Simu zilifungwa ukutani na zilitegemea waya wa shaba wenye waya na analogia, fremu kuu za Transistor, taipureta za mitambo, mifumo ya kuhifadhi karatasi na vikokotoo vya mwanzoni vya kimitambo.
Lakini leo tuna Intaneti, mifumo ya Akili Mnemba ambayo ina uwezo wa kuunda sanaa, uandishi, na kusaidia kazi kwa wakati halisi. Roketi za kibinafsi zinazokwenda Mars. Simu janja zakuenea mfukoni, saa janja, na vifaa vya kibinafsi vinavyoendeshwa na mitandao ya kimataifa isiyotumia waya ambayo huunganisha mabilioni ya watu mara moja kupitia sauti, maandishi, na video. Wasaidizi wa kiroboti.
Ujanja na udanganyifu wa yule adui ni zaidi ya hapo awali. Uzao mwovu wa Shetani uko katika kukomaa kukamilifu nao umeunda Edeni ya Shetani. Bali wakati huo huo, Mungu anaye Bibi-arusi ambaye yuko katika kukomaa kukamilifu, Uzao Wake wa Kifalme ambao umejiweka wenyewe tayari kwa kukaa katika uwepo wa Mwanawe, Neno Lake, Sauti Yake.
Mungu Yeye alijua ilitakiwa aandae njia ya kumdumisha Bibi-arusi Wake katika wakati huu wa udanganyifu na mwovu. Njia kamilifu ambayo hawangehitaji kushangaa, kukisia, au kuchukua neno la mtu yeyote kwa Neno la kweli lisiloghoshiwa. Yeye alijua wangehitaji kuisikia wao wenyewe Sauti ya Mungu, kwa sababu Yeye alituonya kwamba itafanana sana kiasi kwamba ingewadanganya walio Wateule kama yamkini.
Watu wangeweza kupakwa mafuta, wajazwe na Roho Mtakatifu, na wawe wa uongo. Ilibidi aandae njia. Kwa hivyo, akatengeneza NJIA KAMILIFU kwa ajili ya Bibi-arusi Wake, ambayo ingeonekana haiwezekani wakati Yeye alipoanza kuirekodi Sauti Yake mwaka wa 1947; kwamba kwa ncha ya kidole chao, ulimwengu ungeweza kusikia wao wenyewe kila Neno Yeye alilosema, hata katika lugha yao wenyewe. Hakungekuwa na MASWALI, KUSHANGAA. WAO WANGEWEZA KUISIKIA BWANA ASEMA HIVI WAO WENYEWE.
Yeye hata ametengeneza njia ambayo angeweza kumuunganisha Bibi-arusi Wake kote ulimwenguni ili kuisikia Sauti Yake, wote kwa wakati mmoja, ili waweze kuwa katika nia moja, kwa umoja, wakimsikia Yeye akinena.
Ilimbidi Yeye amchukue mjumbe Wake, bali Yeye aliiacha Sauti Yake, Neno Lake kamilifu kwa ajili ya Bibi-arusi Wake Mkamilifu. Kwa kuisikia na kudumu na Sauti Yake, angejua wao hawawezi kudanganywa.
Na ndilo hili hapa: Hivyo ndivyo ambavyo Mungu huliimarisha Kanisa Lake. Kila Neno kwa jinsi yake. “Mtu hataishi kwa mkate tu, bali kwa kila Neno linalotoka kinywani mwa Mungu.”
Tunajua huku ni kuamini kila Neno ambalo Roho Mtakatifu asemalo, bali kwangu mimi, ninayo heshima kubwa zaidi ambayo mwanadamu amewahi kupewa. Ninaweza kusikia, kwa masikio yangu, SAUTI halisi IKINENA kila Neno linalotoka kinywani mwa Mungu.
Hakuna njia nyingine kwangu mimi. Mungu ametoa njia nyingi za kuwaokoa watoto Wake, bali kwangu mimi, Mungu ameiandaa NJIA KAMILIFU YA KUMKAMILISHA BIBI-ARUSI WAKE.
Leo, Shetani anafasiri vibaya sehemu ya Andiko linalohusu siku hii. Yeye atakuacha ujue yote yale Yesu aliyotenda yalikuwa sawa kabisa. Atakuacha ujue yote yale Ndugu Branham aliyotenda yalikuwa sawa kabisa, na alikuwa nabii wa Mungu. Bali linapokuja suala la kuicheza Sauti halisi Ya Mungu iliyothibitishwa katika kanisa lao, wao watasema hilo halitumiki leo hii, ni wahudumu.
Hilo ndilo tu lote linalompasa kufanya, unaona, ni kuwafanya watu kuamini hilo namna hiyo, na ni hilo tu. Kwani huwezi kuondoa neno moja Kwalo, au kuongeza neno moja Kwalo, lakini hilo ndilo afanyalo.
Kiongozi wako wa kiroho anawekea mkazo nini kanisani mwako? Ni Sauti gani iliyo muhimu zaidi ambayo Bibi-arusi hana budi kuisikia leo? Unaweza tu kuwa na 1 Kikuu.
A: Sauti ya wahudumu?
B: Sauti ya Mungu iliyo kwenye kanda?
“Kila mbegu lazima izae kwa jinsi yake! Hivyo ndivyo ambavyo Mungu aliimarisha Edeni Yake.
Mimi sipingi wahudumu kuhudumu. Najua, na ninaamini, Mungu amewaita. Lakini kwangu mimi, huduma ya kweli itawaambia kusanyiko lake kwamba Sauti iliyo kwenye kanda ndiyo Sauti iliyo muhimu zaidi ambayo HAWANA BUDI kuisikia, kwa hivyo yawabidi wazicheze kanda kanisani mwao, kwani ndio SAUTI KUU.
Mimi na nyumba yangu, na Maskani ya Branham, tutadumu na NJIA KAMILIFU YA Mungu ILIYOANDALIWA. Tuta BONYEZA PLAY na kuisikia Sauti ya Mungu.
Ningependa kuualika ulimwengu mzima uje kuungana nasi kuisikia Sauti hiyo Jumapili hii saa 6:00 MCHANA, masaa ya Jeffersonville,(ni saa 1 JIONI ya Afrika Mashariki) tunapoungana kwa mara nyingine tena kwenye njia Yake iliyoandaliwa aliyoichagua kwa ajili ya siku hii.
Ndugu Joseph Branham
Ujumbe: Edeni ya Shetani 65-0829
Maandiko ya kusoma kabla ya kuusikia Ujumbe:
2 Timotheo 3:1-9
Ufunuo 3:14
2 Wathesalonike 2:1-4
Isaya 14:12-14
Mathayo 24:24