23-0305 Edeni ya Shetani

UJUMBE: 65-0829 Edeni ya Shetani

PDF

pakua – m4a

pakua – amr

BranhamTabernacle.org

Watoto Wangu Wapendwa,

Ninyi ni sifa Yangu, Baba yenu wa Mbinguni. Mlikuwa ndani yangu tangu mwanzo. Hamkumbuki hilo sasa, lakini mlikuwemo humo pamoja Nami . Nilitamani sana kuwajua kwa sababu nilitaka kuwasiliana nanyi, nizungumze nanyi, niwapende, na kuwapa mkono.

Kama mtoto wangu, wewe ni sehemu Yangu, uliyefanyika mwili, kama vile nilivyofanyika mwili, ili tushirikiane mmoja na mwengine kama familia ya Mungu duniani. Hilo ndilo lilikuwa kusudi Langu na ndilo nililotaka tangu mwanzo.

Niliwatengenezea Bustani ya Edeni ili tuweze kuwa na ushirika , lakini adui Yangu akaingia kimya kimya kwa udanganyifu , na kuutawala ulimwengu huu kwa kufasiri vibaya mpango wangu kwenu.

Ni saa danganyifu mnayoishi ndani yake, lakini pia ni wakati mzuri zaidi ya nyakati zote, kwa sababu sasa mnaelekea ule Utawala mkuu wa Miaka Elfu tena; mnaelekea Edeni tena.

Roho wangu si kitu ambacho mmeelimishwa. Ni kitu ambacho Mimi nilikiweka ndani yenu kwa kujua kwangu tangu awali kwa mkono Wangu wenye nguvu. Sasa mwito Wangu wa mwisho unatoka kumshika Bibi-arusi Wangu; “Tokeni kati yao, mkatengwe nao”.

Leo wao hawajaribu kuliimarisha Neno Langu katika mioyo ya watu, wanajaribu kujiimarisha wao wenyewe . Makanisa yanajaribu kuimarisha fundisho la kanisa ndani ya moyo wa mtu. Kila mtu akisema, “Nilitenda hili. Mimi, mie, langu, dhehebu langu, mimi, hili.” Wanajiimarisha wao wenyewe na si Neno Langu lililonenwa kupitia nabii wangu.

Haiwabidi kuelewa yote Nisemayo, inawabidi kuliamini tu kwa sababu nilisema hivyo, na hilo latosha milele.

Roho wangu Mtakatifu anatenda kazi ndani yenu. Ni Uzima uliyo ndani yenu, si msisimko wa mwili ; sio namna fulani ya uhakika wa matendo ya kimwili, Bali ni Mtu, MIMI, Yesu Kristo, Neno la Mungu, lililowekwa mioyoni mwenu, nalo linahuisha kila Neno la wakati huu. Ni Roho Wangu Mtakatifu akitenda kazi ndani yenu kulingana na Neno.

Bibi-arusi wangu wa kwanza alianguka kwa kusikiliza hoja za Shetani, lakini Nimewakomboa ninyi kwa nafsi Yangu, ambalo ni Neno lililofanyika mwili. NINYI HAMTANIANGUSHA. Ninyi ni Bibi-arusi-Neno Bikira Wangu ambao hamtasikiliza hoja za Shetani. Mtakaa na Neno Langu.

Baada ya ule Utawala wa Miaka Elfu kumalizika, basi kutakuweko na Edeni iliyowekwa tena; Ufalme wangu mkuu utarudishwa tena. Niliupigania dhidi ya Shetani katika bustani ya Gethesemane, nami nikainyakua Edeni Yangu. Sasa nimeenda kuiandaa Edeni yenu Mpya huko Mbinguni. Nitarudi tena kuwachukueni hivi karibuni, kwa hivyo msifadhaike mioyoni mwenu.

Hakutakuwa na Bahari tena, kwa maana mbingu za kwanza na nchi ya kwanza zitapita. Nitaifanya upya kwa ubatizo wa Moto ambao utaua kila mdudu mbaya , kila maradhi, kila ugonjwa, na kila uchafu uliowahi kuwa duniani.

Dunia itapasuka, kutatokea Dunia Mpya . Mbingu hii ya kwanza na nchi ya kwanza zitapita. Kutakuwa na Yerusalemu Mpya ikishuka kutoka Kwangu Mimi kutoka Mbinguni. Hapo nitakuwa pamoja nanyi, sifa Zangu za kweli, Wanangu wa kiume na wakike. Tutakuwa na ushirika katika utakatifu, macho yenu yakiwa yametiwa upofu yasione dhambi yo yote.

Nimewajieni tena kama nilivyowaahidi ningefanya. Nimelitimiza Neno langu kwenu. Nililirekodi Neno Langu kwenye kanda ya sumaku ili kusiwe na mkanganyiko, hakuna swali, Neno langu safi tu kwa ajili yenu; kwa kuwa ni Bwana Asema Hivi.

Wekeni dhamiri zenu ziwe safi. Ifunikeni mioyo yenu. macho yenu
yafunikwe yasione mambo ya ulimwengu ya kufanywa mtu mkubwa fulani .

Msisahau kamwe, nitageuka huko magharibi na kurudi tena, mojawapo ya siku hizi. Mpaka wakati huo, peleka Jina Langu ; Litafurahisha moyo, peleka, uendako, kwa Kubonyeza Play.

Msipatane hata kwa Neno moja. Neno Langu kwenye kanda halihitaji kufasiriwa. Ninyi ni sehemu Yangu, sifa Yangu. Ulimwengu huu ni Edeni ya Shetani, lakini nimewafanyia Edeni Mpya ambamo tutaishi milele pamoja. Hadi wakati huo, unganeni kwenye Neno Langu. Pendaneni.

Njoo uungane nao katika Maskani ya Branham Jumapili hii saa 06:00 SITA MCHANA saa za Jeffersonville, ( ni saa 2:00 MBILI USIKU ya Tanzania na Kenya pia ) , na mnisikie mimi Nikinena kupitia nabii Wangu niliyemchagua na kufunua Neno Langu mnaposikia; Edeni ya Shetani 65-0829.

Kwa Niaba Yake,
Ndugu Joseph Branham

Maandiko ya kusoma kabla ya Kusikiliza Ujumbe :

2 Timotheo 3:1-9
Ufunuo 3:14
2 Wathesalonike 2:1-4
Isaya 14:12-14
Mathayo 24:24