23-0312 Makao Ya Baadaye Ya Bwana Arusi Wa Mbinguni Na Bibi-Arusi Wa Duniani

UJUMBE: 64-0802 Makao Ya Baadaye Ya Bwana Arusi Wa Mbinguni Na Bibi-Arusi Wa Duniani

PDF

pakua – m4a

pakua – amr

BranhamTabernacle.org

Mpendwa Bibi-arusi wa Duniani,

Malaki 4 ni Neno la Mungu, nayo imezaa kwa jinsi yake, SISI, Bibi-arusi Wake. Ni Roho Mtakatifu, Utu wa Yesu Kristo, katika matendo , aliyewekwa ndani ya mioyo yetu. Tumehuishwa kwa KILA Neno alilonena, kwa kuwa “Kondoo Wangu huisikia Sauti Yangu; mgeni hawatamfuata.”

Imekuwa ya ajabu jinsi gani miezi hii iliyopita , kumfuata nabii huko Jeffersonville. Mungu amekuwa akizungumza kupitia malaika wake mwenye nguvu na kutulisha kwa Chakula chake kilichohifadhiwa Ghalani kutoka kwenye GHALA LAKE MOJA DOGO katika nchi yote. Ni Mana Iliyofichwa, ni kwa ajili ya Bibi-arusi Wake tu.

Kwa kila Ujumbe tunaousikia, tunashiriki na kufurahi pamoja; “Najua nimezisikia Jumbe hizi mara nyingi sana hapo awali, lakini KAMWE sijawahi kuzisikia kama hivi sasa”. Hakika ni chemchemi ya Maji yaliyo Hai yanayobubujika ndani yetu. Hatuwezi kujizuia. Ndiyo yote tunayotaka kuzungumzia. Hatukuwahi kuwa na uhakika katika maisha yetu, wakujua sisi ni nani na wapi tunaelekea.

Hakuna kujiuliza tena:
“ Mimi Sijui tu. Nimefanya mambo mengi ya kutisha maishani mwangu. Nimemkosea Bwana mara nyingi sana. Inaonekana DAIMA mimi hujichafua.”

Hakuna kutumai tena :
“Natumai kweli kuwa mimi ni mtoto wa Mungu. NINATAKA kuwa. Naomba niwe.”

Siku hizo ZIMEKWISHA . Sasa TUNAJUA . Utukufu kwa Mungu!!

Tunajuaje? Mungu amekuwa akizungumza nasi moja kwa moja kwa Sauti Yake iliyo kwenye kanda, akituambia tena na tena, “Mimi niko ndani yenu, ninyi mko ndani Yangu. Sisi ni MMOJA. Niliwachagua NINYI kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu. Ninyi ni nyama ya Nyama Yangu , mfupa wa Mfupa Wangu”.

Ni Ujumbe mkamilifu jinsi gani Mungu aliyotuzungumzia siku ya Jumapili kutuambia yote kuhusu jinsi ulimwengu huu tunaoishi si wetu, ni Edeni ya Shetani. Jinsi alivyomdanganya Hawa hapo mwanzo kuhoji na kutilia shaka NENO MOJA tu. Alivua utaji mtakatifu wa Mungu, na kujivika utaji wa maarifa, ndipo macho yake yakafumbuliwa naye akajua alikuwa yu uchi.

Shetani alipotosha Neno la asili, na sasa amempofusha kwamba bado yu uchi wala hajui. Amekuwa malkia wa Shetani na dunia hii ndiyo Edeni ya ufalme wake.

Jumapili, Bwana-arusi wetu wa Mbinguni anataka kumkumbusha Bibi-arusi Wake wa duniani mahali Makao yetu ya baadaye yalipo na vile yatakavyokuwa. “Mpendwa Kipenzi , kwa kuwa sasa nimekwisha kuambia yote kuhusu ulimwengu huu na jinsi Edeni ya Shetani ilivyo, ninataka kukuambia KWA MARA NYINGINE TENA kuhusu Makao YAKO ya Baadaye na mimi .

Nataka kuwaambieni kinaganaga. Najua mmenisikia nikiwaambia juu Yake mara nyingi, lakini ngojeni tu, wakati huu itakuwa kana kwamba hamjawahi kunisikia nikiwaambieni hapo kabla.

Nataka kuingia kwa undani sana. Ninataka kuwafunulia Ninyi mko katika Mapenzi yangu Makamilifu kwa kukaa na Neno langu na nabii Wangu. Ninataka kuwapa mfano wa kile mnachofanya leo hii kama mfano mkamilifu wa ule mji mpya mtakaoishi ndani yake.

Tutaingilia jambo fulani hakika. Nitawadondoshea kitu fulani kidogo; Naamini mtalikamata. Mtaishi katika Mji huo pamoja Nami. Nabii wangu ataishi karibu nanyi . Atakuwa jirani yako. Mtatembea kwenye barabara hizo za dhahabu na kunywa kutoka kwenye Chemchemi Yangu. Mtatembea katika paradiso za Mungu, huku Malaika wakirukaruka na kuimba nyimbo za sifa.

Ninyi mtakuwa vito kwenye taji ya nabii Wangu. Mtang’aa kuliko kitu chochote kile ulimwenguni, katika Siku ile. Kuna mengi nataka kuwafunulieni Jumapili. Ni siku ya ajabu iliyoje tutakayokuwa nayo pamoja”.

Anayo mengi sana ambayo ametuwekea akiba katika wiki chache zijazo, kama hatakuja na kutuchukua kabla ya wakati huo. Wiki baada ya wiki, akituambia, sisi ni akina nani, tunakoelekea, jinsi kutakavyokuwa kule. Atakuwa akituongoza hadi kwenye wiki iliyo tukufu sana ya Pasaka ambayo hatujawahi kamwe kuwa nayo, iliyojawa na si kingine ila kumsifu na kumwabudu yeye.

Ni wakati wa kusisimua jinsi gani . Tunaona unabii ukitimia mbele ya macho yetu. Tunaona Neno likidhihirishwa NDANI YETU. Kuja Kwake kunaweza kutokea wakati wowote. Tunasimama mlangoni tukiwa na shada la maua mikononi mwetu. Tunaweza kusikia farasi wakienda shoti na mchanga ukivingirishwa chini ya magurudumu.

Lile gari la Kale la Farasi litasimama hivi karibuni. Tutaruka kutoka kwenye mlango wa mwili huu mzee na kurukia mikononi Mwake. Atatutazama na kusema, “Yote yamekwisha sasa, mpenzi, nitakupeleka sasa kwenye Makao yako ya Baadaye.”

Unaalikwa kuwa sehemu ya siku zilizo kuu ambazo ulimwengu haujawahi kuona. Wana tai watakusanyika kutoka ulimwenguni kote ili kusikia Sauti ya Mungu ikizungumza na Bibi-arusi Wake na kumwambia yote kuhusu: Makao Ya Baadaye ya Bwana-arusi Wa Mbinguni na Bibi-arusi wa Duniani 64-0802 , saa 06:00 SITA Mchana , saa za Jeffersonville. ( Ni saa 1:00 MOJA JIONI Ya Tanzania na Kenya pia ).

Ndugu. Joseph Branham

Ukumbusho: Msisahau kuhusu badiliko la saa ya Akiba ya mchana.

Maandiko ya kusoma kabla ya kusikia Ujumbe:

Mathayo 19:28
Yohana 14:1-3
Waefeso 1:10
2 Petro 2:5-6 /Sura ya 3 yote.
Ufunuo 2:7 / 6:14 /21:1-14
Walawi 23:36
Isaya Sura ya 4 yote / 28:10 / 65:17-25
Malaki 3:6