23-0319 Kuchagua Bibi-Arusi

Ujumbe: 65-0429e Kuchagua Bibi-Arusi

PDF

pakua – m4a

pakua – amr

BranhamTabernacle.org

Mpendwa, Mmoja Katika Milioni Moja,

Nimekuwa nikikusubiri kwa muda mrefu sana. Wewe ni Kipenzi changu wa moyo, na ninakupenda sana. Kama nilivyokuahidi, nimekuwa nikikutengenezea Makao mapya ambapo tutaishi pamoja katika Milele yote. Nimeweka kila kitu jinsi kabisa unavyovipenda.

Sasa Ninaweza kukutazama na kuona, wewe ni picha halisi yangu mimi . Una tabia Yangu hasa, Mwili Wangu, Mifupa Yangu, Roho Wangu yeye yule, kila kitu Changu jinsi ile ile , sawa kabisa. Umekuwa mmoja na Mimi.

Nilimtuma malaika Wangu mwenye nguvu duniani kukuita wewe kutoka katika Edeni ya Shetani. Nilimtuma ili aweze kueleza mawazo Yangu, sifa Zangu, na kuwaambia kuhusu mambo yajayo. Nilitumia kinywa chake na sauti yake kujieleza. Baada ya yeye kuyasema, naliyatimiza, kwa maana Mbingu na nchi zitapita, bali Neno Langu kwenu halitashindwa kamwe.

Nilijua uliponisikia nikizungumza, kwa kutumia sauti ya malaika Wangu, ungejua ndani kabisa ya moyo wako, huyo hakuwa yeye, ilikuwa ni Mimi nikizungumza nawe. Ilikuwa ni Mimi nikikutumia barua ya mapenzi, nikikuambia, Nimekuchagua kuwa Bibi-arusi Wangu kipenzi.

Machoni Mwangu, hakuna aliye kama wewe. Hakuna anayeweza kupachukua mahali pako. Umebaki mkweli na mwaminifu Kwangu. Ninapokutazama, Moyo Wangu unachangamka kwa furaha.

Wakati Nilipokuambia, kuwa mwangalifu sana kipenzi , kile unachosikiliza, kutakuwa na wapakwa mafuta wengi wanaotumia Maneno Yangu, lakini ni wa uwongo. Nawe ulielewa onyo Langu kwa Ufunuo na ukakaa mkweli na mwaminifu kwa Sauti Yangu.

Nilijisikia vizuri sana mlipoomba kwa bidii kuhusu ni kanisa la aina gani mnaloshiriki. Niliwaambia mfanye chaguo sahihi, na nikawapa mifano ya jinsi kanisa kamilifu lilivyo. Mlikumbuka niliposema hayo huwa yana roho, na mchague kanisa kamilifu.

Hata niliwaambia kuwa wangalifu sana ni nani aliye mchungaji wako. Kwa hiyo mnaweza kufikiria jinsi moyo Wangu ulivyoruka kwa furaha nilipowaona mmekaa na mchungaji Niliyemtuma kuwaleta ninyi Kwangu. Mlijua ni Roho Wangu Mtakatifu akiishi ndani ya nabii Wangu kuwaongoza ninyi Kwangu.

Nakumbuka siku mliyokuwa na furaha sana, na kuchangamshwa kweli, wakati nilipomwita malaika Wangu mahali pa juu ili niweze kumwonyesha ninyi mkikaguliwa Kimbele . Tulikuwa tumesimama hapo tukiwatazama mkipiga hatua taratibu ya Twendeni Askari wa Kristo mbele Yetu.

Alipenda jinsi nyote mlivyokuwa mmevalia vazi lenu la taifa mlikotoka ; kama Uswisi , Ujerumani, na kutoka kote ulimwenguni. Kila mmoja mkiwa na nywele zenu ndefu zilizotengenezwa vizuri. Sketi zenu zilikuwa ndefu nadhifu. Nilijisikia vizuri na kufurahi sana kuwaonyesha ninyi nyote kwake, ili aweze kurudi na kuwatia moyo na kuwaambia aliwaona Kule.

Kila jicho lilitutazama Sisi. Wakati wasichana wachache, nyuma ya mstari, walianza kuangalia huku na huko mahali pengine, yeye alipiga kelele , “Msifanye hivyo! Msiache hatua hizo!”

Wakati Nilipowaambia Ninawahifadhia chakula ninyi mpate kula, mlijua kabisa nilichokuwa nazungumzia. Mlitaka kuwa Bibi-arusi-Neno Bikira Wangu . Sijawahi kuwapata mkitaniana na mtu mwingine yeyote. Daima imekuwa ni Mimi, Neno Langu. Hilo lilinifurahisha sana Mimi.

Nimewachagua , NINYI , kuwa Bibi-arusi Wangu. Ninawapenda sana, kama vile ninyi mnavyonipenda Mimi. Msivunjike moyo, jipeni ​​moyo, iweni wenye furaha , Shangilieni, siku ile inakaribia upesi nitakapokuja kuwachukua. Ni Wakati mzuri vipi Tutakaokuwa nao .

Ninyi Wengine, TUBUNI, dunia inanguruma. Siku moja Los Angeles itazama chini ya bahari, Kama vile nilivyowaambia ingekuwa. Ghadhabu yangu inakokomoa papa hapa chini yake. Sitazuia ufuko huo muda zaidi tena. Utatiririka ndani ya bahari kina cha maili moja, kote kote mpaka kwenye Bahari ya Salton. Itakuwa mbaya zaidi kuliko siku ya mwisho wa Pompeii.

Naenda kuisafisha dunia hii kwa moto hivi karibuni. Nitaua kila kitu Kilicho juu yake na chini yake. Mnayaona yale yanayoendelea ulimwenguni kote, kama nilivyowaambia. Mnamwona Bibi-arusi Wangu akiungana pamoja kulizunguka Neno Langu, kama vile nilivyowaambia.

Sasa huu ndiyo wakati Wenyewe . Sasa haya ndiyo majira yenyewe. Jiandaeni!

Ile saa ya ghadhabu Yake iko juu ya nchi. Kimbieni wakati kungali na wakati wa kukimbia, na mwingie ndani ya Kristo.


Mmealikwa kuja kuungana nasi, sehemu ya Bibi-arusi Wake, tunapojiweka wenyewe tayari kwa ajili ya Kuja Kwake, kwa kusikia Sauti ya Mungu ikisema nasi na kutuletea Ujumbe: Kuchagua Bibi-arusi 65-0429E Jumapili hii saa 06:00 SITA MCHANA saa za Jeffersonville.( Ni saa 1:00 MOJA JIONI ya Tanzania na Kenya pia )

Ndugu. Joseph Branham

Maandiko ya Kusoma Kabla ya Kusikiliza Ujumbe :

Mwanzo 24:12-14
Isaya 53:2
Ufunuo 21:9