21-1107 Edeni ya Shetani

UJUMBE: 65-0829 Edeni ya Shetani

PDF

pakua

BranhamTabernacle.org

Mpendwa Bibi-arusi Aliyeangazwa,

Kama Siku ile iliyokwisha kupita, tulikuwa tumeunganishwa na Yeye akaja katika nyumba zetu na akawa pamoja nasi. Kote katika mataifa, sehemu ya Mwili wa Kristo, Ambayo nabii Wake amepewa haki ya kuilisha, waliketi pamoja katika ulimwengu wa roho Alipokuwa YEYE akisema nasi kupitia malaika Wake mkuu ambaye amemtuma; kuuangaza ulimwengu kwa Roho Wake Mtakatifu kupitia yeye, kumwita Bibi-arusi Wake atoke.

Mungu alituma, katika mlango huu wa 18, malaika mwenye nguvu, baada ya siri hiyo kujulikana, malaika mwenye nguvu, ama, mjumbe….

Mungu alimtuma malaika, mjumbe (kufanya nini?) kuwaita watoke. “Tokeni!” Ujumbe wa Wakati huu!…

Tokeni kwake! Mungu alituma wengi…malaika mkuu, ama, mjumbe. Na Nuru yake haikuwa kwenye maficho, iliangaza duniani kote… Kuiangaza nchi, na kuwaita watu Wake watoke kwake.

Sasa, mnajua jambo hilo ni Kweli. Mjumbe fulani alitumwa kutoka Mbinguni, kuwaita watu wa Mungu watoke Babeli. Na Nuru Yake ikaangaza nchi, Roho Mtakatifu aliye mkuu .

Wiki iliyopita mhudumu fulani aliliambia kusanyiko lake kwamba Mimi nilitaka watu waamini kwamba Ndugu Branham alikuwa ndiye malaika wa Ufunuo 18, lakini akadai kuwa huyo alikuwa ni malaika kutoka Mbinguni, na asingeweza kuwa Ndugu Branham. Kama huyo ndugu angalifanya tu kile nabii ALILOMWAMBIA afanye, kulichunguza jambo hilo kwa Neno, na SI kwa ufahamu wake, ANGESIKIA, KWAMBA KWA KWELI, ALIKUWA NI NDUGU BRANHAM ALIYESEMA YEYE ALIKUWA NDIYE MALAIKA HUYO .

…Angalia, huyu ni malaika wa Nuru, kumbukeni, malaika wa mwisho, ni malaika katika wakati wa kanisa wa Laodikia. Ni mjumbe wa Laodikia, huyo, ni wa mwisho, kwa kuwa mlango unaofuata tu ni mlango wa 19, ambao ni kuja kwa Bibi-Arusi .

Ndugu na dada zangu, NINACHUKIA kusema mambo haya na kuyabainisha. Kama vile Ndugu Branham asemavyo, “Naeleweka vibaya sana ”. Mimi Simaanishi kuwa ni wahudumu wote wanaosema mambo haya, wala siamini wahudumu wote ni wauongo, au hawapaswi kuhudumu. HAPANA, lakini walio wengi sana wanawadanganya watu kwa kuweka umuhimu zaidi katika huduma yao kwa kuhubiri Neno, badala ya kubonyeza play na watu wao na kusikia HASA kile nabii alichosema.

kama umechaguliwa tangu awali, unaliona. Hakuna njia ya kulificha toka kwako. Utaangalia na kusema, “ ni dhahiri sana mbele ya uso wangu! Ninaliangalia moja kwa moja. Ninaliona. Hili hapa, lile Neno; kila Neno, Neno kwa Neno. limedhihirishwa mbele yangu na nafsi yangu yote imefungamanishwa ndani yake.”

Hebu niwape nukuu hii ndugu zangu wahudumu, ambayo inaeleza yale tu mimi, na kanisa ambalo Bwana amenipa kuwa mchungaji, tunaamini kuhusu kucheza kanda kanisani.

Na sasa kumbukeni, kama hili linanaswa…Sijui. Siwezi kumwona ye yote. Naam, naweza, naweza kumwona Ndugu Terry kule kwenye—kwenye chumba cha kurekodia. Na kama hili linanaswa; kwa ajili ya wahudumu wo wote mahali po pote, wakati wo wote, hili halielekezwi kwa madhumuni ya kudharau mafundisho yenu, hili hata halielekezwi kwa kondoo wenu. Ujumbe huu, na Jumbe zote zingine ambazo ninazungumzia, zinaelekezwa kwenye kusanyiko langu. Si kwa ajili ya kusanyiko lako isipokuwa wawe wanataka kulipokea. Bali limeelekezwa kwa watu hawa hapa.

Watu hununua kanda hizi. Watu kila mahali ulimwenguni huzinunua na kuzicheza. Mara nyingi wananiandikia. Na sikuzote mimi huwarejesha, kama wao ni washiriki wa kanisa fulani, “ Mwoneni mchungaji wenu.”

Wananitazama Mimi kama mchungaji wao Wa mahali hapa , ndiomana ninawaambia, “NINAAMINI KUZIPOKEA KANDA NA KUBONYEZA PLAY . Ndugu Branham ndiye mchungaji wetu. Sisi ni sehemu ya Kusanyiko lake ”.

Sasa, ewe mchungaji , nataka ujue jambo hilo, ya kwamba, ninazungumza haya kwa ajili ya kusanyiko langu peke yake. Nami nina haki ya kutenda jambo hilo, kwa maana nimewekwa na Roho Mtakatifu kuwachunga kondoo hawa. Na ole wangu kama siwaambii ninayofikiria ni Kweli, na jinsi ninavyofikiri linakuja. Bali si kwa ajili ya ulimwengu wala kwa makanisa mengine. Ninyi fanyeni lo lote ambalo Mungu anawaambia mtende. Siwezi kuwajibieni, wala ninyi hamwezi kunijibia .
Lakini kila mmoja wetu hana budi kujibu mbele za Mungu, kwa ajili ya huduma yetu

Sina budi kujibu kwa Mungu kwa ajili ya huduma aliyonipa. Kwa kila hali ya utu wangu naamini ni lazima ucheze Sauti ya Mungu katika kanisa lako kwa njia ya Jumbe zilizorekodiwa . Ni njia iliyoandaliwa na Mungu kwa ajili ya siku hii kuivisha Bibi-arusi Wake. Ndiyo njia PEKEE kwa Bibi-arusi kuunganishwa na kukamilishwa.

Ujumbe tutakaosikia Jumapili ulinenwa na kurekodiwa kwa ajili ya LEO HII. Ni Chakula Cha Kiroho Kwa Wakati wake. Hebu na tufungue mioyo yetu ili Roho Mtakatifu aweze kututia mafuta ili tusikie kile alichokuwa anatuonya tutazamie katika siku hizi za mwisho.

Alitueleza roho zote mbili zitadhihirishwa kikamilifu katika siku hii ya mwisho. Alitueleza ingefanana sana hata ingewadanganya wateule kama yamkini. Siku hiyo ndiyo hii.

Angalia, wakati Yesu alipokuja—unaona, Shetani alikuwemo katika kundi lile la waalimu wa Kiyaudi na marabi na makuhani, akijaribu kuwaambia washike Torati ya Musa, ambapo Neno lenyewe lilisema—kwamba katika siku hiyo, Mwana wa Adamu angefunuliwa. Unaona? Kwamba angejifunua Mwenyewe . Kwa hiyo walikuwa wakijaribu…kadiri ambavyo waliwaweka wa kidini, na katika Torati ya Musa…unaona alilotenda ? Alikuwa akijaribu kuwaambia, “Sehemu hiyo ya Neno ni sawa kabisa, lakini mtu huyu siye mtu yule.” Unaona jinsi alivyo mdanganyifu ? Hiyo ndiyo hiyo siku yenyewe hasa ya udanganyifu.

HATUWEZI kudanganywa, sisi ni Bibi-arusi. Sisi NI watoto wa Mungu. Sisi NI sehemu ya sifa ya Mungu iliyokuwa ndani Yake, tulifanyika mwili kama vile Yeye alivyofanyika mwili, ili tuweze kuwa na ushirika sisi kwa sisi kama familia ya Mungu duniani. Hatulikumbuki jambo hilo kwa sasa, lakini tulikuwa huko. Alijua jambo hilo. Na alitaka tuwe hivyo ili aweze kuwasiliana nasi, aseme nasi na kutupenda, na kupeana nasi mikono,
UTUKUFU!!!

Hakuna tena, “NADHANI MIMI ni Bibi-arusi Wake. NATUMAI MIMI ni Bibi-arusi Wake.” TUNAJUA SISI NI BIBI-ARUSI WAKE .

Roho Mtakatifu anatenda kazi ndani yetu . Ni Uzima. Si msisimko wa mwili; sio namna fulani ya uhakika wa matendo ya kimwili, bali ni Mtu, Yesu Kristo, Neno la Mungu lililowekwa katika mioyo yetu kuhuisha kila neno la wakati huu.

Unakaribishwa kuungana nasi kwa kuunganishwa Jumapili saa nane 8:00 mchana , saa Jeffersonville, ( ni saa nne 4:00 usiku ya Tanzania), Roho Mtakatifu anapotuangazia kwa Neno Lake lililonenwa kupitia malaika Wake, na kutuletea Ujumbe: Edeni ya Shetani 65-0829

Ndugu. Joseph Branham.

Maandiko ya kusoma

2 Timotheo 3:1-9

Ufunuo 3:14

2 Wathesalonike 2:1-4

Isaya 14:12-14

Mathayo 24:24