21-1031 Chujio La Mtu Mwenye Busara

Ujume: 65-0822e Chujio La Mtu Mwenye Busara

PDF

pakua – m4a

pakua – amr

BranhamTabernacle.org

Wapendwa Waamini wa Biblia,

Ni siku tukufu jinsi gani tunayoishi. Mioyo yetu inawaka ndani yetu anapozungumza nasi kila siku njiani. Kristo amefunuliwa kwetu kwa Neno Lake. Ni Ufunuo wa Yesu Kristo, Neno Mwenyewe aliyedhihirishwa katika mwili. Ni Sauti ya Mungu ikimwita Bibi-arusi Wake atoke.

Tunao Mkataa, neno la mwisho, Yakini yetu; ni Neno Lake, Biblia. Sasa kama “Biblia” ndiyo Yakini yetu, hebu na tuone kile nabii alichosema Biblia ilichokuwa .

Yeye Alisema Mungu aliandika Biblia kwa kutumia manabii pekee yao. Hiyo ndiyo ilikuwa njia Yake ya kufanya jambo hilo. Hiyo ndiyo njia Aliyokuwa nayo ya kuleta Neno Lake kwa watu: kupitia midomo ya manabii Wake. Neno Lake lilimjia nabii peke yake .

Nabii alikuwa ameelekeza nia yake daima kwenye yale Mungu aliyosema; si vile mwanadamu alivyofikiri, vile huo wakati ulivyofikiri, vile kanisa lilivyofikiri, vile ufalme ulivyofikiri. Bali Vile Mungu alivyofikiri, yeye alitamka tu mawazo ya Mungu kwa Neno, wakati Mungu alipoyafunua mawazo Yake kwake, yeye aliyatamka kwa Neno lililoandikwa.

Kwa hiyo, Biblia nzima si maneno ya mwanadamu, wala haikuandikwa na mwanadamu, kuletwa na mwanadamu, ama wala haiwezi kufunuliwa na mwanadamu. Ni Neno la Mungu hufunuliwa na Mungu Mwenyewe, Hujifasiria Mwenyewe. Neno Lake.

Sasa manabii hawa walisema, “Si mimi. Sina uhusiano wowote nalo, bali ni BWANA ASEMA HIVI.” Kwa hivyo, Biblia ni BWANA ASEMA HIVI kupitia manabii. Manabii hawa hawakunena tu na kuandika Neno, lakini pia alikuwa Mfasiri wa Kiungu wa Neno hilo lililoandikwa.

Kwa hiyo, Biblia ni mawazo hasa ya Mungu yaliyoandikwa na manabii. Nabii ndiye mfasiri pekee wa kiungu wa Biblia. Ujumbe, Neno, Biblia na mjumbe ni kitu kimoja . Hivyo, tutahukumiwa kwa fasiri ya Biblia iliyonenwa na nabii.

” Wewe ulitumwa kuwa kiongozi na Mungu atakuja, na atakapokuja, Yeye atakuhukumu kulingana na yale uliyowafundisha, kwanza; kama wataingia ama hawataingia. Tutaingia kulingana na mafundisho yako .”

Je hivi yeye amesema NINI? Atahukumiwa kwanza kwa yale YEYE aliyotufundisha. Tunaweza TU kuingia kulingana na mafundisho YAKE. Kwa hiyo ni jinsi gani ilivyo muhimu kusema tu yale yaliyo kwenye kanda kwani tutahukumiwa kwa NENO LAKE KWENYE KANDA; ambayo ni fasiri ya Biblia.
Je, utaamini kikomo chako cha Milele juu ya kile mtu fulani anachosema? Sio Bibi arusi!! Sisi Tutafanya na kusema nini?

Ndipo hao wote wakapaza sauti kwa pamoja, “Tunajua hilo! Tunastarehe kwa uhakika.”

Kwa hiyo, Bibi-arusi anastarehe juu ya kila Neno ambalo nabii alilonena, ambayo ilikuwa ni fasiri ya mawazo ya Mungu yaliyoandikwa na manabii, na katika siku hizi za mwisho yamenenwa na Mungu Mwenyewe kupitia midomo ya nabii Wake.

“Wewe utatukabidhi Kwake, na ndipo tutarudi duniani tena, tukaishi milele.”

Ee wandugu na wadada, amkeni kabla hamjachelewa. Huu ni wito Wake wa mwisho. Fungua moyo wako na uone jinsi unavyopaswa kusikiliza Sauti ya Mungu kwenye kanda. Ikiwa tutahukumiwa kwa Ujumbe ambao Mungu alinena kupitia mjumbe Wake kwenye kanda, unawezaje kutokuona jinsi ilivyo muhimu, na njia pekee ya kuwa sahihi na kuwa mstari mmoja na Neno Lake, ni kwa kusikia Sauti ya Mungu kwenye kanda.

Ndiyo, Mungu ameita huduma tano , lakini hawana budi kuweka umuhimu wa kuzisikiliza kanda zaidi ya huduma yao. Sisemi kwamba mchungaji wako hawezi kuhubiri au kufundisha. Sisemi kuacha kwenda kanisani; unapaswa kwenda kanisani, lakini wakati mchungaji wako haweki kanda, Sauti ya Mungu ambayo utahukumiwa kwayo, kuchukua nafasi ya kwanza na kuwapa hiyo kusikiliza, una chujio mbaya.

Hebu Jiulize, wakati mhudumu anapokuambia, unapaswa kucheza kanda tu nyumbani kwako na sio kanisani, je! Hilo linaingia akilini? Hakika, hujadanganganywa kiasi hicho . Sauti ile ile na Neno utakayohukumiwa kwayo inapaswa TU kusikilizwa majumbani mwenu na si kanisani? Ndugu Branham kamwe hakusema kucheza kanda kanisani, lakini unapaswa kunisikiliza mimi tu kama mchungaji wako unapokuja kanisani. hivi una hata chembe ya ufunuo kweli ?

Ni jambo gani linaloweza kuwa muhimu zaidi mnapokutanika pamoja katika kanisa lenu kumwabudu Bwana, kukua katika ufahamu wa Neno, kumkaribia Mungu zaidi, kuliko kuivishwa kwa kusikia sauti PEKEE…PEKEE iliyothibitishwa ya Mungu.

Je, ungeweza kuwazia Yoshua akiwaambia Israeli wote, najua tunayo maneno halisi ambayo Musa aliyonena, lakini Musa hakuwahi kusema tunapokutanika pamoja kwamba tunapaswa kusoma maandishi yake. Ninawaongoza sasa na mimi nitawaambia maneno ya Musa.

Kisha akasoma maneno yote ya torati, baraka na laana, sawasawa na yote yaliyoandikwa katika kitabu cha torati .

Wala Hapakuwa na neno lo lote katika yote aliyoamuru Musa, ambalo Yoshua hakulisoma mbele ya mkutano wote wa Israeli, pamoja na wanawake, na watoto, na wageni waliokaa kati yao .

Kwa maneno mengine, kama Yoshua angekuwa na kinasa sauti katika siku zake, alipowakusanya watu pamoja ange BONYEZA PLAY.

Malaki 4 amekuja na BWANA ASEMA HIVI, nawe utahukumiwa kwa kila neno lililonenwa kwenye hizo kanda . Ujumbe huu ni chujio lako. Sikiliza na uishi, kataa na ufe.

Je, tunawezaje kuchukua nafasi wakati kikomo chetu cha Milele kina uwalakini? Tunahitaji kuwa daima tunasikia Neno; katika nyumba zetu, katika magari yetu, wakati wakufua nguo, tunapofundisha watoto wetu, tunapoosha magari yetu, tunapokuwa matembezi, na muhimu zaidi, tunapokusanyika katika makanisa yetu.

Unakaribishwa kuungana na sehemu ya Bibi-arusi Wake, inayoamini KILA NENO kwenye kanda, tunaposikia Ujumbe: Chujio la Mtu Mwenye Busara 65-0822E , Jumapili saa 8:00 nane mchana , saa za Jeffersonville ( ni saa 3:00 tatu Usiku ya Tanzania) . Au mtie moyo mchungaji wako acheze kanda kanisani mwako ili wewe pia uweze kusikia Sauti ile ile itakayokutambulisha kwa Bwana wetu Yesu Kristo, na kisha tutarudi duniani tena ili kuishi milele. HAIWEZEKANI KUWA BORA ZAIDI YA HIYO.

Ndugu. Joseph Branham