23-0219 Kristo Amefunuliwa Katika Neno Lake Mwenyewe

Ujume: 65-0822M Kristo Amefunuliwa Katika Neno Lake Mwenyewe

PDF

pakua – m4a

pakua – amr 13MB (use Firefox to download)

BranhamTabernacle.org

Kundi langu Dogo,

Nawasalimu na ninyi mliyo kwenye mfumo huu wa simu, ambao ni mzuri sana, sana. Ninamshukuru sana Bwana mnaweza kuketi moja kwa moja majumbani mwenu, mkusanyike makwenu, makanisani mwenu, na kusikiliza ibada. Kila mahali sauti yangu inapokuja, jalia kundi hilo dogo libarikiwe.

Leo, nataka kuwaandikia barua ndogo ya mapenzi kutoka moyoni mwangu ili kuwatia moyo. Ninyi ndiyo wale ambao Mungu aliyowachagua kuwa Bibi-arusi Wake kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu; ninyi mnaosikiliza kanda hizi. Nimewaambia mara nyingi sana, kanda hizi ni kwa ajili yenu tu, ninyi ndiyo kusanyiko langu. Mimi Siwajibiki na wale ambao Mungu aliowapa wahudumu wengine kuwachunga; Mimi Ninawajibika tu na aina ya Chakula ninachowalisha ninyi. Kanda hizi ni kwa ajili yenu, maskani yangu pekee , wale ambao Mungu amenipa mimi kuwa mchungaji wenu. Ni Mana iliyofichwa, hao wengine hawawezi kuila.

Sasa, kama watu wanataka kutengeneza chakula cha kisasa na kadhalika huko nje, waache wapate ufunuo kutoka kwa Mungu na wafanye yale ambayo Mungu anawaambia wafanye, wale cho chote wanachotaka. Nitafanya jambo lilo hilo. Bali Jumbe hizi ni kwa ajili yenu ninyi tu.

Ninajaribu sana niwezavyo kudumu kwa unyofu na Neno, kwa ajili yenu ninyi ambao mmewekwa mikononi mwangu kutoka kwa Mungu, maana kondoo huhitaji chakula cha kondoo. “Kondoo Wangu huisikia Sauti Yangu.” Na hilo ndilo tunaloishi kwalo, kila Neno litokalo. Si Neno moja mara hii na mara nyingine, bali kila Neno litokalo kinywani mwa Mungu. Hilo ndilo ambalo ninyi watakatifu mnaishi kwalo.

Kila mtu hana budi kuwa na kitu fulani ambacho wanashikilia. Kitu fulani kinapaswa kuwa nguzo ya kushikilia, kwa maneno mengine, Mkataa. Na kila mtu hana budi kuwa na mkataa ama Yakini. Kwangu mimi, na kwa wale ambao ninatumaini ninawaongoza kwa Kristo, na kwa njia ya Kristo, Biblia ndiyo mkataa wetu.

Basi, tunatambua ya kwamba Mungu alitutumia manabii Wake. Hiyo ndiyo njia aliyokuwa nayo yakulileta Neno Lake kwa watu, kwa kinywa cha nabii Wake. Sasa katika siku hizi za mwisho, Yeye ameahidi kujidhihirisha Mwenyewe katika utimilifu tena, wa mwili Wake, katika Roho. Ni Mungu Mwenyewe katika maumbile ya herufi, sura ya nabii, akidhihirishwa katika mwili.

Sina budi kuishi daima katika uwepo wa yule Mwandishi nikiwa na kalamu yangu tayari wakati wo wote kuandika lo lote yeye Analosema. Nimeelekeza nia yangu daima kwenye mawazo Yake; si vile mwanadamu anavyofikiri, vile wakati huu unavyofikiri, vile kanisa linavyofikiri, vile ufalme unavyofikiri. Mawazo ya Mungu tu! Ninatamka tu mawazo ya Mungu kwa Neno.

Wakati Mungu anapoyafunua mawazo Yake Kwangu , mimi ninayatamka katika Neno kwenye kanda, “BWANA ASEMA HIVI.” Si, “ Mimi Nasema Hivi .” Ni, “BWANA ASEMA HIVI!” Ninaweza tu kulifasiri jinsi vile Mwandishi anavyotaka niwafasirie ninyi ; maana ni Neno la Mungu lisilokosea.

Kuna wengine wengi wanaojaribu kuniiga, kama makuhani, ama kadhalika. Nao wanafanya nini? Wanachafua tu, hivyo tu. Wasingeweza kufanya jambo hilo. Mungu alinituma mimi, nabii Wake, kumwongoza Bibi-arusi Wake; si mtu mwingine, wala si kundi la watu.

Maneno ninayonena, na vile ninavyotenda, itawapofusha wengine, lakini itayafungua macho ya wengine. Alinivalisha kwa namna ya mavazi ambayo ningevaa, tabia yangu, shauku yangu, kila kitu jinsi tu ilivyonipasa kuwa. Alinichagua kikamilifu kwa ajili yenu. Wengine wangesimama na kuangalia waseme, “Vema, siwezi. Kuna…Si—siwezi kuona.” Wao wamepofushwa.

Yeye atajifunua kwa yule yeye atakayemfunulia Hilo . Amelifanya hivi kwamba anaweza kujificha mwenyewe katika Maandiko, kwa mwanatheolojia mwenye akili sana aliyeko. Yeye Anaweza tu kujificha mwenyewe , akae papo hapo katika Maandiko, nao wanaweza kuyatazama siku nzima na wasiweze kuyaona; wayatazame maishani mwote, na wasiyaone kamwe. Anaweza tu Mwenyewe kujificha, akiketi pale.

Jambo lililopo sasa ni wale wanaoupokea Ujumbe mioyoni mwao, hawana budi kukaa katika Uwepo wa Mwana, wapate kuivishwa. Bonyeza Play halafu umwache Mwana aukaushe ubichi wote ukutoke, awafanye Wakristo waliokomaa.

Wakati yeye alipokuja mara ya kwanza, alikuwa mwanadamu. Alipokuja mara ya pili, akiwa na sehemu maradufu, alikuwa mwanadamu. Alipokuja kama Yohana Mbatizaji, alikuwa mwanadamu. Aliahidi kuja katika siku hii na kuishi na kujidhihirisha kwa mara nyingine tena ndani ya mwanadamu; Mwana wa Adamu akiishi katika mwili wa mwanadamu.

Sasa tuko katika wakati wa jicho, kinabii, ya Malaki 4. Hakuna kitu kingine kilichosalia kuja ila Yeye Mwenyewe kuingia ndani ya kitu hicho, ’ maana hilo ndilo jambo la mwisho lililopo.

Sikilizeni enyi wana-kondoo wangu wadogo, ninyi ambao Mungu amenipa kuwa mchungaji wenu. Wakati umeenda sana . Anakuja upesi kuwachukua ninyi , Bibi-arusi Wake. Kaeni na hizo kanda, hazihitaji kufasiriwa.

Ninawaalika ninyi Tai wadogo mje kuungana nami kwenye jambo pekee litakalomleta Bibi-arusi Wake pamoja Jumapili hii, saa 6:00 SITA MCHANA , saa za Jeffersonville.( Ni saa 2:00 MBILI USIKU ya Tanzania na Kenya pia ) Mtasikia Bwana Asema Hivi wakati Mungu anaponena kupitia mimi na kufunua: Kristo Amefunuliwa Katika Neno Lake Mwenyewe 65-0822M.

Kumbuka, KAENI NA HUDUMA YA KANDA . BONYEZA PLAY KILA SIKU.

Ndugu Branham

Maandiko ya kusoma kabla ya kusikiliza Ujumbe:

Kutoka 4:10-12
Isaya 53:1-5
Yeremia 1:4-9
Malaki 4:5
Luka Mtakatifu 17:30
Yohana Mtakatifu 1:1 / 1:14 / 7:1-3 / 14:12 / 15:24 / 16:13
Wagalatia 1:8
2 Timotheo 3:16-17
Waebrania 1:1-3 / 4:12 / 13:8
2 Petro 1:20-21
Ufunuo 1:1-3 / 10:1-7 / 22:18-19