UJUMBE: 65-0725M Watiwa Mafuta Katika Wakati Wa Mwisho
- 26-0517 Watiwa Mafuta Katika Wakati Wa Mwisho
- 24-0804 Watiwa Mafuta Katika Wakati Wa Mwisho
- 23-0115 Watiwa Mafuta Katika Wakati Wa Mwisho
- 21-0919 Watiwa Mafuta Katika Wakati Wa Mwisho
- NUKUU YA LEO KWA KISWAHILI
- 20-0405 Watiwa Mafuta Katika Wakati Wa Mwisho
- 18-1021 Watiwa Mafuta Katika Wakati Wa Mwisho
- 17-0115 Watiwa Mafuta Katika Wakati Wa Mwisho – Preliminari
Wapendwa Tai Wanaokusanyika,
Kichwa pekee cha Ujumbe wa wiki hii kinafunua kule kumhisi Roho Mtakatifu kwa Bibiarusi. Kuwazia kutakuwa na wanaume watiwa mafuta wa kweli watakaoinuka katika siku hii, wakiwa na upako wa kweli wa Roho Mtakatifu yule yule aliyekuwa juu ya nabii wetu, bali wawe wa uongo.
Neno linatuambia watafanya ishara na maajabu, wanapokea mvua ile ile, baraka zile zile kama nabii wa kweli. Watu wangegeukia mbali kutoka kwenye Neno la kweli lililothibitishwa la siku hii na kuzifuata nia zao wenyewe, wakijipatia waalimu makundi makundi, wenye masikio ya utafiti. Hilo litafanana sana na Neno la kweli hata karibu litawadanganya Walioteuliwa.
Hivi upako huo utafanana sana kiasi gani? Je, itakuwa rahisi kupambanua kilicho kweli na cha uongo? Nabii alituambia kwamba Mfalme Daudi, mtu anayeupendeza moyo wa Mungu, akiwa na upako juu yake, alipata ufunuo wa kweli; bali ilikuwa makosani.
ATI NINI!! Hebu hilo lizame ndani kwa muda. Mfalme aliyechaguliwa na Mungu alikuwa na upako wa kweli na ufunuo wa kweli, bali alikuwa makosani! Kondoo wa Mungu watatakiwa kuwa macho sana ili kujua kile wanachokisikia ni upako wa kweli au wa uongo; kwani kikomo chao cha milele kinategemea maamuzi haya.
Tunajua Mungu ameweka wahudumu wengi wa kweli waliotiwa mafuta ili kusaidia kuongoza na kumweka Bibi-arusi Wake katika Neno. Neno Lake linasema hivyo, nasi tunamshukuru sana Bwana kwa ajili ya kila mmoja wao. Wameitwa kuwa wachungaji kuyaangalia makundi yao. Wapo kwa ajili ya kuwaweka wao katika Neno. Kwa kufanya hivyo, hawapaswi kushindwa kuicheza Sauti PEKEE ya Mungu iliyothibitishwa kwa makundi yao.
Kama tulivyotoka kusikia jinsi ambavyo kila mtu anavyoweza kukosea, hata pamoja na upako wa kweli na ufunuo wa kweli. Bali Bibi-arusi wanaweza kuwa na uhakika, kwa sababu Mungu ameiandaa njia kamilifu ambayo daima wanaweza kuusikia UPAKO WA KWELI, UFUNUO WA KWELI, BWANA ASEMA HIVI YA KWELI; BONYEZA PLAY TU.
“Palipo na Mzoga,” palipo na Mana, palipo na Neno, “ndipo watakapokusanyika tai.”
Palipo na Mzoga, hapo ndipo sisi Tai tutakapokusanyika. Mahali palipo na Nyama mbichi, Neno la wakati huu, Ujumbe wa saa hii. Na hakuna mahali pazuri pa kuila Mana hiyo kuliko kuisikia Sauti ya Mungu akinena Yeye Mwenyewe.
Hilo ni Neno Lake. “Mtu hataishi kwa mkate tu, bali kwa kila Neno.” Mnaona? Waliochaguliwa tangu awali wanajua jambo hili. “Neno geni, ama sauti ngeni,
hawataifuata.”
Sababu ya sisi kutofanya hivyo, na hatuwezi kudanganywa, ni kwa sababu sisi ni Neno wenye Ufunuo huu. Hatuwezi kuwa kitu kingine. Hatuwezi kusikia kitu kingine. Hatujui kitu kingine.
“MIMI NIKO!” Si “Nilikuwa, wala Nitakuwa.” “MIMI NIKO,” wakati uliopo, Neno sasa hivi. Si Neno lililokuwa, wala Neno litakalokuja; Neno lililopo sasa. Mnaona? Mnalifahamu? “MIMI NIKO!” “MIMI NIKO” ni Neno. “Hapo mwanzo alikuwapo Neno, Naye Neno alikuwako pamoja na Mungu.” Hiyo ni kweli? “MIMI NIKO.” “Mungu alinituma kama nabii Wake, kuthibitisha jambo hili kuwa ni kweli. Mimi ndiye jibu la Neno hili, kwa hiyo, wakati Yeye anaposhuka huku na kufanya jambo hili.”
Na alipofanya jambo hilo, Farao akasema, “Vema, tuna vijana wengi sana katika kundi letu wanaoweza kufanya jambo hilo, pia,” waigaji.
Yesu alisema, “Naam, hiyo itajirudia tena katika siku za mwisho,” mnaona, wakidai jambo lile lile.
Bwana asifiwe. Nena kuhusu hakikisho kwa Bibi-arusi. Kama unao Ufunuo huu, basi utajua wewe ndiye Bibi-arusi Wake kipenzi mteule, aliyechaguliwa tangu zamani.
Kwa kuisikiliza Sauti ya Mungu iliyo kwenye kanda, tunamsikiliza Mwana wa Adamu, ambaye ni Kristo. Yeye ndiye tunayejilisha. Hatujilishi mwanadamu; mwanadamu, maneno yake yatashindwa. Bali tunakula Mwili-Neno lisiloshindwa la Mwana wa Adamu.
Ikiwa unataka kuwa na uhakika wa asilimia 100 kwamba unasikiliza Bwana Asema Hivi, njoo uungane na sehemu ya Bibi-arusi Jumapili hii saa 06:00 MCHANA, masaa ya
Jeffersonville,(Ni saa 1:00 JIONI ya Afrika Mashariki) tunapoisikia Sauti ya Mungu ikitufunulia yote kuhusu watiwa mafuta katika wakati wa mwisho.
Ndugu Joseph Branham
Ujumbe: Watiwa Mafuta Katika Wakati Wa Mwisho 65-0725M
Maandiko:
Mathayo Mt. 5:44-45 / 7:21 / 24:15-28
Luka Mt. 17:30 / 18:1-8
Yohana Mt. 14:12
Waefeso 1:5
II Timotheo 3:1-8
Waebrania 6:1-8 / 11:4
Ufunuo 10:1-7 / 16:13-14
Malaki 4:5
I Wafalme 22:1-28
Yeremia: Sura ya 27 na 28