23-0115 Watiwa Mafuta Katika Wakati Wa Mwisho

Ujume: 65-0725M Watiwa Mafuta Katika Wakati Wa Mwisho

PDF

Server S
Server G

pakua – m4a

pakua – amr 18MB (use Firefox to download)

Wapendwa Wakusanyikao Katika Zizi La Kondoo,

Nimeridhishwa na kumshukuru sana Bwana kwa kukusanyika pamoja na kila mmoja wenu katika zizi la Kondoo wa Mungu kila wiki, ambapo tumefichwa mahali petu pa siri, tukijilisha na kuishi kwa Chakula hicho Kilichofichwa. Ni Ufunuo wa Yesu Kristo, akijithibitisha na kujidhihirisha Mwenyewe kwetu.

Amejificha ili kwamba wengine waliangalie moja kwa moja na bado wasilione, bali kwetu sisi, Bibi-arusi Wake mteule, tunaliona waziwazi na kuamini kila Neno. Tumekaa na Neno Lake na nabii Wake kwani wao ni Mmoja na kitu kile kile .

Na iwapo wewe ni mwana wa Mungu, utakaa pamoja na nabii wa Biblia hii. Ni Neno.

Manabii wengi waliotiwa mafuta siku hizi wanasema “Ni Roho Mtakatifu ndiye unayepaswa kukaa naye, si nabii.” Kama manabii wa kale, kama tuna swali, inabidi kuwe na jibu sahihi. Ni lazima twende KWENYE NENO kuona kile nabii aliyetutangulia alichosema.

Lakini kuna Kristo mmoja aliye halisi, Roho, na huyo ni Neno lililofanyika mwili kama alivyoahidi kufanya.

Kristo MMOJA aliye halisi, Roho, ambaye Yeye aliahidi, Malaki 4, Luka 17, Mwana wa Adamu akijifunua Mwenyewe katika mwili wa mwanadamu.

Ndiyo, kuna watu waliotiwa mafuta. Ndiyo, wana wito. Ndiyo, wana Roho Mtakatifu halisi. Ndiyo, wana nia na makusudi sahihi.

Basi tutajuaje wa kweli na wa uongo?

Angalia, wanafanana. Wametiwa mafuta namna ile ile. Lakini angalia, “Kwa matunda yao…”

Sipendi kusema mambo haya lakini saa imechelewa sana na wakati unaenda. Hili ndilo linalosemwa na kuhubiriwa leo na wale mbwa-mwitu wakali Paulo alilionya kanisa kuwahusu, na wale wapakwa mafuta wa uongo ambao Ndugu Branham aliyosema wangekuja. Wako hapa kati yetu, kama tu walivyosema.

Hapa kuna kipande kidogo cha barua iliyoandikwa kutoka kwa mhudumu . Matunda yao yanajaribu kutilia shaka juu ya nabii wa Mungu. Wanawaonya watu wao kuwa sisi ni miungu watu kwa sisi kumfuata nabii na Kubonyeza Play.

Sikiliza jinsi hili lilivyodanganyifu.

Nimekerwa kwamba pepo huyu amepenya tabaka zetu za ujumbe hivi kwamba sasa tunaita vitabu vya mahubiri ya William Branham SAUTI YA MUNGU. William Branham hakuwa sauti halisi ya Mungu , bali ni sauti ya mwanadamu ambayo Mungu aliyotumia. Biblia haisemi kamwe kwamba Yeye alikuwa ni sauti ya Mungu, bali Biblia inamtambulisha kama sauti ya malaika wa 7. ( Ufu 3:14; 10:7 ).

Hebu twende kwenye NENO na tumwache nabii wa Mungu ayaanike wazi mafundisho haya ya uongo.

Ikiwa kwa kusema hivyo niliwakera, mnisamehe, lakini, nilihisi kwamba hilo laweza kuchukiwa, lakini, MIMI NI SAUTI YA MUNGU KWENU .

Sasa utamwamini nani, nabii huyu wa uongo aliyetiwa mafuta, au MALAIKA-MJUMBE WA SABA WA MUNGU ALIYETHIBITISHWA ? Unawezaje kukaa chini ya mhudumu yeyote ambaye anayeamini au anayekufundisha mambo kama hayo? Afadhali uingie katika Neno wakati ungalipo.

Kosa la kutisha limefanywa na jumuia ya ujumbe katika kumfanya William Branham kuwa mungu kwa kumfanya kuwa yakini. William Branham hakuwa kamwe yakini! Neno la Mungu ndilo Yakini.

Amina, Neno la Mungu NDIYO Yakini yetu. Neno lilikuja kwa nani, kwako wewe au kwake YEYE? Ni nani aliye mfasiri wa kiungu wa NENO LA MUNGU, wewe au YEYE? Ni nani ambaye Nguzo ya Moto ilimthibitisha kuwa Bwana Asema hivi, wewe au YEYE?

Kwa sababu ukiwa na watu wawili, una maoni mawili.

Hatuhitaji watu wawili wala maoni yao, tunahitaji tu kile nabii wa Mungu alichosema kwenye kanda.

Yapasa kuwe na Yakini moja thabiti , na Yakini yangu ni Neno, Biblia .

Hilo hapo, kama vile ulivyosema, Biblia ni Yakini yake na yetu, lakini kisha anasema:

Najua ninyi ni Ndugu , mnanichukua mimi kama Yakini Yenu .

Kwa hivyo subiri kidogo, hilo linasikika kinyume na ULICHOSEMA. Alisema kwamba tunamchukua yeye kama Yakini Yetu.

Mradi ninamfuata Mungu kama Paulo alivyosema katika Maandiko , “ Mnifuate mimi kama ninavyomfuata Kristo .”

Je, huyo si aliyetiwa mafuta? Je, hakujua alichokuwa anazungumzia?

Hivi Nabii wa Mungu alituambia nini wiki iliyopita?

Tunaona ya kwamba mtu anapokuja, ametumwa kutoka kwa Mungu, amechaguliwa na Mungu, akiwa na BWANA ASEMA HIVI ya kweli, ujumbe huo na mjumbe huyo ni mmoja na kitu kimoja .

Alisema huwezi kuwatenganisha, ni kitu kimoja, lakini unasema tunapaswa kuwatenganisha?

William Branham hana tofauti na mwanadamu ye yote apatikanaye na mauti, kwa maana alikuwa mtu wa tabia moja na Eliya alivyokuwa .

Amina, alikuwa mwanadamu tu hakika, lakini alikuwa NDIYE MTU ambaye Mungu alimchagua kufunua Neno Lake lote kwake , na kutuongoza kwenda kwenye Nchi ya Ahadi. Yeye ndiye ambaye Mungu alisema, wafanye watu WAKUAMINI.

Kitu kile kile, wametiwa mafuta, wakihubiri Injili ya Pentekoste, bali wakiikana ahadi ya siku hii ya Neno kuthibitishwa , “ Yesu Kristo yeye yule jana, leo, na hata milele .”

Tutajuaje tofauti ikiwa wao ni wapakwa mafuta wa kweli wa Roho Mtakatifu? Anatupa mifano ili tujue kati ya manabii wa uongo na nabii wa kweli.

Balaamu na Musa. Mikaya na Zedekia. Yeremia na
Hanania. Katika kila kisa wote wawili walikuwa manabii waliotiwa mafuta wa Mungu, lakini alituambia tufanye nini, TUDUMU NA NABII WA MUNGU ALIYETHIBITISHWA. Hiyo ndiyo njia PEKEE ya kuwa na uhakika kwamba unafuata Njia ya Mungu iliyoandaliwa, na uko katika mapenzi Yake makamilifu.

Mimi ndiye tu ninayekuwa karibu wakati anapoyafanya. Mimi nilikuwa tu sauti aliyoitumia Yeye, kusema jambo Hilo. Haikuwa yale niliyojua; ni yale niliyojitolea kwake tu , aliyozungumza kupitia .

Hayo ndiyo yote Bibi-arusi anayotaka na anayohitaji. Sauti Moja. Nabii mmoja. Ujumbe Mmoja. Mjumbe mmoja.

Ee Baba, jinsi tunavyoshukuru kwa neema na rehema zako kwetu. Ulituambia hakuna lisilowezekana kwako. Hakuna lisilowezekana kwetu sisi. Kwa maana yote yanawezekana kwao waaminio, nasi TUNAAMINI.

Njoo uungane nasi Jumapili saa 06:00 SITA MCHANA , saa za Jeffersonville, (ni Saa 2:00 MBILI USIKU ya Tanzania na Kenya pia.) tukiwa na Sauti iliyochaguliwa ya Mungu ikituambia yote kuhusu  Watiwa-Mafuta katika Wakati wa Mwisho 65-0725M.

Ndugu.  Joseph Branham