UJUMBE: 65-0725M Watiwa Mafuta Katika Wakati Wa Mwisho
- 24-0804 Watiwa Mafuta Katika Wakati Wa Mwisho
- 23-0115 Watiwa Mafuta Katika Wakati Wa Mwisho
- 21-0919 Watiwa Mafuta Katika Wakati Wa Mwisho
- NUKUU YA LEO KWA KISWAHILI
- 20-0405 Watiwa Mafuta Katika Wakati Wa Mwisho
- 18-1021 Watiwa Mafuta Katika Wakati Wa Mwisho
- 17-0115 Watiwa Mafuta Katika Wakati Wa Mwisho – Preliminari
Wapendwa Walaji wa Mana Iliyofichwa,
Mungu alimtuma malaika-mjumbe wake wa saba amwongoze Bibi-arusi Wake; si mtu mwingine, si kundi la watu, bali MTU MMOJA, kwa maana Ujumbe na mjumbe Wake ni kitu kile kile. Neno la Mungu halihitaji kufasiriwa. Alilinena kwa Bibi-arusi Wake kupitia midomo ya mwanadamu nasi tunaliamini Hilo jinsi vile tu Yeye alivyolisema.
Ni lazima tuwe waangalifu sana leo ni sauti gani inayotuongoza, na inatuambia nini. Kikomo chetu cha milele kinategemea uamuzi huo hasa; kwa hiyo ni lazima tuamue ni sauti gani ndio sauti iliyo muhimu zaidi ambayo tunayopaswa kuisikia. Ni Sauti gani ambayo imethibitishwa na Mungu? Ni Sauti gani iliyo na Bwana Asema Hivi? Haiwezi kuwa sauti yangu, maneno yangu, fundisho langu, lakini lazima liwe Neno, kwa hiyo ni lazima tuende kwenye Neno kuona kile Linachotuambia.
Je! linatuambia kwamba Yeye atainua huduma tano ituongoze mwishoni? Tunaweza kuona waziwazi katika Neno wao wana mahali pao; mahali muhimu sana, lakini Je, Neno linasema MAHALI POPOTE kuwa wao ndio watakaokuwa na sauti zilizo muhimu zaidi TUNAZOPASWA kuzisikia ili kuwa Bibi-arusi?
Nabii alituambia kutainuka watu wengi katika siku za mwisho watakaojaribu kumtendea Mungu kazi bila ya kuwa Mapenzi Yake. Ataibariki huduma yao, lakini sio njia Yake kamilifu ya kumwongoza Bibi-arusi Wake. Alisema Mapenzi yake makamilifu ni, na daima yamekuwa, ni kuisikia na kuiamini Sauti ya nabii wake aliyethibitishwa; kwa maana ni Hiyo, na hiyo peke yake ndio iliyo na Bwana Asema Hivi. Ndioamana alimtuma malaika Wake. Ndiomaana alimchagua yeye. ndiomaana Yeye aliirekodi. Ni Chakula Cha Kiroho Kwa Wakati Wake, Mana Iliyofichwa, kwa Bibi-arusi Wake.
Kwa kuwa saba kati ya nyakati saba, sijaona kitu ila watu wakiliheshimu neno lao wenyewe kuliko Langu. Kwa hiyo mwishoni mwa wakati huu ninawatapika mtoke katika kinywa Changu. Yote yamekwisha. Nitazungumza basi. Naam, niko hapa katikati ya Kanisa. Amina wa Mungu, aliye mwaminifu na wa kweli atajifunua Mwenyewe na itakuwa KWA NJIA YA NABII WANGU.” Loo! ndiyo, hivyo ndivyo ilivyo.
Saba kati ya nyakati saba watu wanaliheshimu neno lao wenyewe kuliko Langu. Unatakiwa kujiuliza mwenyewe, Je, jambo hili halifanyiki kati yetu hivi sasa? “Usicheze kanda kanisani, bali lazima umsikie mchungaji wako, zicheze tu kanda nyumbani kwako”. Wao hawaiweki Sauti Yake iliyo kwenye kanda kuwa ndio Sauti iliyo muhimu zaidi, bali sauti yao.
Wanawaelekeza watu kwao wenyewe, na umuhimu wa huduma YAO; Wito WAO kulileta Neno, kumwongoza Bibi-arusi; Lakini Bibi-arusi hawezi kulivumilia hilo. Hawatalikubali. Hawatalifanya jambo hilo. Hawatapatana kuhusu Hilo; ni Sauti ya Mungu na si kitu kingine.
Hivyo ndivyo Neno linavyosema.
Swali lililo niani mwa watu siku hizi ni: Ni nani ambaye Mungu alimchagua kumuongoza Bibi-arusi Wake, Je, ni kanda au ni huduma tano? Je, wahudumu watamkamilisha Bibi-arusi? Je, wahudumu watamwongoza Bibi-arusi? Kulingana na Neno la Mungu, hiyo haijawahi kamwe kuwa Njia Yake.
Kuna watu wengi sana leo wanaosema wameufuata na kuuamini Ujumbe huu kwa miaka na miaka, lakini sasa wanaiweka huduma YAO kuwa ndio sauti iliyo muhimu zaidi unayopaswa kuisikia.
Utaifuata huduma ipi basi? Utaweka kikomo chako cha Milele kwenye huduma ipi? Wote wanasema wameitwa na Mungu kuhubiri Ujumbe. Sikatai ama kulihoji hilo, lakini baadhi ya wahudumu wenye ushawishi mkubwa katika vyeo vya huduma tano wanasema, “Hiyo siyo Sauti ya Mungu, ni sauti ya William Branham tu”. Wengine wanasema, “siku za Ujumbe wa mtu mmoja zimepita”. “Ujumbe huu sio Yakini”. Je, Huyo ndiye anayekuongoza?
Wanaume ambao wamehubiri katika mamia ya makusanyiko yao, viongozi wakubwa wa huduma tano, SASA wanaukana Ujumbe na KUSEMA “Ujumbe huu ni wa uongo”.
Nyingi kati ya huduma zote husema, “Hampaswi kusikiliza Sauti ya malaika wa Mungu kanisani, isipokuwa tu majumbani mwenu.” “Ndugu Branham hakusema kamwe kuzicheza kanda kanisani.”
Hilo halisadikiki. Siamini ndugu ama dada wanaosema wanaamini Ujumbe huu; kwamba Ndugu Branham ndiye malaika-mjumbe wa saba wa Mungu, ni Mwana wa Adamu anayezungumza, angeangukia kwenye kauli ya udanganyifu kama hiyo. Hilo lingepaswa kukuchefua tumbo. Ikiwa wewe ni Bibi-arusi, LITAKUCHEFUA.
Mungu hajawahi kamwe kubadilisha Nia Yake kuhusu Neno Lake. Daima Yeye amemchagua mtu mmoja kuwaongoza watu wake. Wengine wana mahali pao, lakini wao wanapaswa kuwaongoza watu kwa yule mmoja ambaye YEYE amemchagua kuwaongoza watu. Amkeni, enyi watu. Hebu jaribuni kusikiliza kile hawa wahudumu wanachowaambia, Nukuu hizo wanazotumia kuiweka huduma yao mbele ya ile ya nabii. Inawezaje huduma ya mtu ye yote kuwa ndio muhimu zaidi kuisikia kuliko Sauti ya Mungu iliyothibitishwa ambayo Yeye ameihakikisha na kuithibitisha kuwa Bwana Asema Hivi?
Yeye ametuambia, na kutuambia, kunaweza kuwa na watu waliotiwa mafuta kweli, na Roho Mtakatifu wa kweli juu yao, ambao ni wa uongo. Kuna NJIA MOJA tu ya kuwa na hakika, KUKAA NA NENO LA ASILI, kwa maana Ujumbe huu na mjumbe ni kitu kile kile. Kuna Sauti moja tu ambayo Mungu aliichagua kuwa Bwana Asema Hivi…MOJA.
Huduma ya kweli itakuambia kwamba HAKUNA KITU kilicho muhimu zaidi kuliko kulisikia Neno la Mungu kutoka kwenye Sauti ya Mungu iliyo kwenye kanda. Wao wanaweza kuhubiri, kufundisha, au chochote walichoitiwa kufanya, LAKINI LAZIMA WAIWEKE SAUTI YA MUNGU KUWA NAFASI YA KWANZA; LAKINI WAO HAWAFANYI HIVYO, BALI WANAIWEKA HUDUMA YAO KUWA NDIO NAFASI YA KWANZA. Matendo yao yenyewe yanathibitisha kile wanachoamini.
Wanakwepa kujibu swali kuhusu kuiweka Sauti ya Mungu kwenye mimbara zao kwa kusema, “Ndugu Joseph haamini katika wahudumu. Haamini katika kwenda kanisani. Wao wanamwabudu mtu. Wanafuata fundisho hilo la Joseph. Yeye anatengeneza dhehebu kwa kucheza na kusikiliza wote kanda ileile.” Wakiwakengeusha tu watu kutoka kwenye swali kuu hasa, lakini matendo yao yanathibitisha kile wanachoamini kwa kile wanachowafundisha watu wao: HUDUMA YAO NDIO NAFASI YA KWANZA.
Wanasema, kuwafanya watu wasikilize wote kanda ile ile kwa wakati mmoja ni dhehebu. Je! Hivyo sivyo hasa alivyofanya Ndugu Branham Wakati yeye alipokuwa hapa; kuwaunganisha watu kwa simu ili wasikie Ujumbe wote kwa wakati mmoja?
Wewe jiulize, kama Ndugu Branham angekuwepo hapa leo katika mwili, Je! hangewafanya Bibi-arusi wote KUJIUNGANISHA KWA SIMU ili wamsikie yeye wote kwa wakati mmoja? Je! asingejaribu kuwakusanya Bibi-arusi pamoja katika HUDUMA YAKE kama vile yeye alivyofanya kabla Mungu hajampeleka nyumbani?
Hebu niingize kitu fulani hapa. Wakosoaji watasema, unaona, anafanya yale yale, kumsifia huyo mtu sana; wao wanamfuata mtu, William Marrion Branham!! Hebu tu tuone kile Neno linachosema kuhusu hilo pia:
Katika siku za mjumbe wa saba, katika siku za wakati wa Laodikia, mjumbe wake atafunua siri za Mungu kama zilivyofunuliwa kwa Paulo. Yeye atanena, na hao watakaompokea nabii huyo katika jina lake mwenyewe watapokea matokeo mema ya huduma ya nabii huyo.
Hili litamkasirisha shetani zaidi ya chochote kile naye atanishambulia hata na zaidi, lakini enyi watu, afadhali mlichunguze hili kwa Neno. Si kwa sababu mimi nimelisema, hapana, basi ningekuwa kama mtu yeyote yule; bali ifungueni mioyo yenu na nia zenu na mlichunguze hilo kwa Neno. Si kile mtu mwingine ye yote anachosema au anachowafasiria, bali kile nabii wa Mungu alichosema.
Baada ya barua hii wao watawapa nukuu baada ya nukuu baada ya nukuu, nami nasema AMINA kwa kila nukuu, LAKINI VIPI KUHUSU JAMBO LILILO KUU? Je! wanazitumia nukuu kuwaambia kuwa kumsikia nabii ndilo jambo mnalopaswa kufanya, au HUDUMA YAO? Wakisema Ujumbe, nabii, basi waambieni waiweke hiyo Sauti KUWA NAFASI YA KWANZA katika kanisa lenu.
Juu ya msingi wa tabia za wanadamu peke yake, mtu ye yote anajua ya kwamba palipo na watu wengi kuna hata na maoni yasiyopatana juu ya mambo madogo-madogo ya fundisho muhimu ambalo wote wanashikilia pamoja.
Hilo hapo. Hii nukuu moja tu inawaambia haiwezi na HAITAKUWA kundi la watu. Si wahudumu watakaowaunganisha watu kwa sababu ya tabia za wanadamu peke yake; wamegawanyika juu ya maoni ya mambo madogo-madogo ya mafundisho muhimu. Wote hawawezi kukubaliana, kwa hivyo mnapaswa kurudi kwenye NENO LA ASILI.
Ni nani basi atakayekuwa na mamlaka ya kutokosea ambayo itarudishwa katika wakati huu wa mwisho, kwa kuwa wakati huu wa mwisho utarudi kwenye kumdhihirisha Bibi-arusi wa Neno Halisi?
NI NANI atakayetuongoza? SAUTI MOJA, iliyo na mamlaka ya kutokosea ndio itamwongoza Bibi-arusi.
Hiyo inamaanisha tutakuwa na Neno tena kama lilivyotolewa kikamilifu, na kueleweka kikamilifu katika siku za Paulo.
Utukufu… Limetolewa kikamilifu na kueleweka kikamilifu. Halihitaji fasiri, kwa vile lilivyotolewa kikamilifu, na sisi, Bibi-arusi, tunalielewa kikamilifu na kuamini kila Neno.
Hilo hapo. Yeye anamtuma nabii aliyethibitishwa.
Anatuma nabii baada ya karibu miaka elfu mbili.
Yeye anamtuma mtu fulani aliye mbali sana na madhehebu, elimu, na ulimwengu wa dini hivi kwamba kama vile Yohana Mbatizaji na Eliya wa kale,
Yeye ata-sikia tu kutoka kwa Mungu
Ata-kuwa na “Bwana asema hivi” na kunena kwa niaba ya Mungu.
Yeye atakuwa kinywa cha Mungu
NAYE, KAMA INAVYOTANGAZWA KATIKA MAL. 4:6, ATAIGEUZA MIOYO WA WATOTO IWAELEKEE BABA ZAO.
Atawarudisha wateule wa siku za mwisho nao watamsikiliza nabii aliyethibitishwa akitoa kweli halisi kama vile ilivyokuwa kwa Paulo.
Atairudisha kweli kama walivyokuwa nayo.
Na hao wateule walio pamoja naye katika siku hiyo watakuwa ndio wanaomdhihirisha Bwana kwa kweli na watakuwa ndio Mwili Wake na kuwa sauti Yake na kutenda kazi Zake. Haleluya! Unaliona hilo?
Tunaliona hilo. Tunaliamini hilo. Tunalitegemea jambo HILO.
Umealikwa kuja kuungana nasi wakati tunapokisikia kinywa cha Mungu, Sauti ile itakayo muunganisha Bibi-arusi wa Yesu Kristo, Nabii wake aliyethibitishwa, anapotupa ukweli halisi, saa 06:00 SITA MCHANA, saa za Jeffersonville,(Ni saa 1:00 MOJA JIONI ya Afrika Mashariki)
Ndugu. Joseph Branham
65-0725M Watiwa Mafuta Katika Wakati Wa Mwisho