24-0421 Kuthibitisha Neno Lake

UJUMBE: 64-0816 Kuthibitisha Neno Lake

PDF

BranhamTabernacle.org

Mpendwa Kanisa-Bibi-arusi,

Mwana wa Adamu amekuja na kujifunua Mwenyewe katika mwili wa mwanadamu kwa Bibi-arusi Wake. Amelisema, tunaliamini, na Yeye amelithibitisha. ni Bibi-arusi Wake. Sisi ndio Kanisa-Bibi-arusi Wake tuliojiweka tayari kwa kusikiliza na kuamini kila Neno lililotoka katika kinywa Chake.

Kutakuweko na ufufuo wa wafu. Yeye atathibitisha hilo. Kutakuweko na Kunyakuliwa kwa Kanisa. Atathibitisha hilo. Kutakuweko na ule Utawala wa Miaka Elfu. Atathibitisha hilo. Kutakuweko na Mbingu mpya na nchi mpya. Atathibitisha hilo, kwa sababu Neno Lake lilisema hivyo.

Sisi ndio tutakaokuweko huko. Atathibitisha hilo. Sisi ndio wale ambao tumekwisha kufanywa sehemu ya Neno hili. Alituchagua SISI tangu zamani kuwa Huko. Kutakuweko na Unyakuo kwa kujua kwake tangu zamani na hakuna kitakachozuia jambo hilo, tutakuweko huko!

Shetani amejaribu kwa muda mrefu kuwafanya watu watilie shaka Neno moja tu lililonenwa. Usifanye hivyo. Amini tu kila Neno. Huna budi kuamini kila Neno ili kuweko huko. Si neno la nabii, ni Neno la Mungu ambalo limerekodiwa na kuhifadhiwa kwenye Kanda.

Kuhani mkuu, askofu, kardinali, mchungaji?” Mungu! Kila Neno litokalo kinywani mwa Mungu. Tunajuaje ni Neno la Mungu? Yeye husema hivyo, kisha akalithibitisha. Yeye hulithibitisha Neno Lake.

Ni LAZIMA uamini kila Neno litokalo katika kinywa cha Mungu. Amethibitisha ni Neno Lake lililo kwenye Kanda. Amethibitisha kwamba William Marrion Branham ndiye malaika-mjumbe Wake wa saba; ndiye Sauti ya Mungu kwa ajili ya siku yetu. Wote wasiouamini Ujumbe na mjumbe wataangamia.

Sasa, siongei hasa na wasikizi hawa. Haya yananaswa, mnaona, na yanaenda ulimwenguni kote. Je, mnafahamu, watu wa ulimwengu, ya kwamba Neno moja, Neno moja, si fungu moja la maneno, si aya moja, Neno moja, hilo tu ndilo Hawa alikosa kuamini.

Yeye ni Neno, nasi tulikuwa sehemu ya Neno Lake. Na hiyo ndiyo sababu tuko hapa, kuhakikisha mahali petu maishani. Kuamini kila Neno. Kukaa na Neno. Kumwelekeza Bibi-arusi kwa kila Neno lililo kwenye Kanda.

Katika siku yetu, yule Mwana wa Adamu amefunuliwa. AME liunganisha Kanisa kwa kile Kichwa; ameunganisha arusi ya Bibi-arusi. Ule Wito wa Bwana Arusi umekuja. Mwana wa Adamu amekuja katika mwili wa mwanadamu kuwaunganisha hao wawili pamoja. Yeye ni Neno. Sisi ni Neno Lake, na hao wawili wanaungana pamoja.

itachukua dhihirisho la kufunuliwa kwa Mwana wa Adamu… Si kasisi… Yesu Kristo, atashuka katika mwili wa mwanadamu kati yetu, naye atafanya Neno Lake dhahiri sana hata litaunganisha Kanisa pamoja Naye kama mmoja, Bibi-arusi, kisha ataenda Nyumbani kwenye Karamu ya Arusi. Amina.

Dhihirisho la Neno litamuunganisha Bibi-arusi. Linamdhihirisha Mwana wa Adamu tena, si wanathelogia wa kanisa. Mwana wa Adamu! Neno na Kanisa wanakuwa mmoja. Lo lote afanyalo Mwana wa Adamu, Yeye alikuwa Neno, Kanisa litafanya jambo lile lile.

Tumeunganishwa na Roho Mtakatifu, Neno Lake, Sauti Yake, nasi tunajitayarisha kwenda kwenye Karamu ya Arusi. Neno limetuunganisha, na hao wawili wanakuwa MMOJA.

Tunasema KANDA, KANDA, KANDA. Mnapaswa kuzicheza Kanda majumbani mwenu, makanisani mwenu. Tunashutumiwa kwa sisi kutilia mkazo sana kuhusu kuzicheza Kanda. Kwa nini tunasema hivyo? Ni nani anayenena NASI kwenye Kanda?

Sasa, kumbuka, huyo hakuwa Yesu akinena na Ibrahimu pale, ambaye angeyatambua mawazo rohoni mwa Sara nyuma yake. Huyo hakuwa Yesu, hakuwa amezaliwa bado. Bali alikuwa mtu katika mwili; ambaye Ibrahimu alimwita “Elohim, yule Mkuu Mwenyezi.”

Ikiwa mnaamini kwamba Mwana wa Adamu amefunuliwa katika siku yetu; Mungu akinena kupitia midomo ya mwanadamu, Anawezaje basi mtu ye yote kutokuona umuhimu wa kuiweka Sauti hiyo kuwa ndio SAUTI ILIYO MUHIMU KULIKO ZOTE MNAYOPASWA KUISIKIA?

Siwashutumu wengine ambao hawaoni na kuamini kile tunachoamini; wao ni ndugu na dada zetu, lakini Mimi NIMERIDHIKA VYA KUTOSHA, NIMEJAA TELE, NINA HAKIKISHO LA KUTOSHA hii ndiyo njia iliyoandaliwa na Mungu kwa ajili ya Bibi-arusi Wake. Siwezi kufanya vinginevyo. Mimi na nyumba yangu, Kubonyeza Play ndiyo NJIA PEKEE.

Kwa mara nyingine tena ninaualika ulimwengu wote kuja kuungana nasi Jumapili saa 06:00 SITA MCHANA, saa za Jeffersonville,( ni saa 1:00 MOJA JIONI ya Afrika Mashariki ) tunaposikia:  Kuthibitisha Neno Lake 64-0816.

Ndugu. Joseph Branham

Maandiko ya kusoma kabla ya ibada:

Mathayo Mt 24:24
Marko Mt 5:21-43 / 16:15
Luka Mt 17:30 / 24:49
Yohana Mt 1:1 / 5:19 / 14:12
Warumi 4:20-22
I Wathesalonike 5:21
Waebrania 4:12-16 / 6:4-6 /13:8
1 Wafalme 10:1-3
Yoeli 2:28
Isaya 9:6
Malaki 4