24-0428 Maswali na Majibu #1

UJUMBE: 64-0823M Maswali na Majibu #1

PDF

pakua – m4a

pakua – amr

BranhamTabernacle.org

Wapendwa Wasikilizaji Wa Kanda,

Siwezi tu kulisema vya kutosha, HAKUNA kitu kilicho kikubwa kuliko kuisikia Sauti ya Mungu ikisema nasi kupitia malaika-mjumbe Wake aliyethibitishwa kwa ajili ya siku yetu. Ufunuo baada ya Ufunuo Bwana anatufunulia. Hakuna mwisho Wake. Kila Ujumbe ni kama hatujawahi kuusikia hapo awali. Ni Neno la Uzima, Mana Safi, Chakula cha Mungu Kilichohifadhiwa kwa ajili ya Bibi-arusi Wake, na yote tunayopaswa kufanya ni KUBONYEZA PLAY.

Tunasikia kila kitu kuhusu Unyakuo WETU unaokuja hivi karibuni. Tunaenda…UTUKUFU, TUNAKWENDA kwenye Karamu ya Arusi. Yeye alituchagua SISI tangu zamani kuwa Huko kwa kujua Kwake tangu zamani, na hakuna kitakachozuia jambo hilo. Neno hapa linaungana na mtu, na hao wawili wanakuwa Mmoja. Linamdhihirisha Mwana wa Adamu. Neno na Kanisa wanakuwa Mmoja. Lolote Mwana wa Adamu afanyalo, Yeye alikuwa Neno, Kanisa linafanya jambo lile lile.

Kabla sijaendelea mbele, mnaweza kutaka kulisoma hilo tena!! Tunawezaje kumwacha shetani atushushe? Sikilizeni kile sisi tunachotarajia. Sikilizeni sisi ni nani. Sikilizeni kile kinachoendelea SASA HIVI.

Tunaenda wapi? Kwenye Karamu YETU ya Arusi ambayo sisi tumechaguliwa tangu zamani kwenda huko kwa kujua Kwake tangu zamani, ambapo SISI, Neno Lake na Kanisa Lake, tunakuwa MMOJA NAYE, na lo lote afanyalo Mwana wa Adamu, TUNAFANYA JAMBO LILE LILE!!

Kisha tukasikia kila kitu kuhusu Makao YETU ya Baadaye. Mjenzi wa Kiungu ameubuni Mji WETU Mpya, ambamo Yeye ataishi pamoja NASI, Bibi-arusi Wake. Ameujenga na ameweka kila kitu kidogo kulingana na sisi TUNAVYOPENDA hasa; jinsi tu SISI tungetaka. Ambamo hapatakuwa na haja ya nuru, kwa kuwa Mwana-Kondoo atakuwa ndiye Nuru yetu. Ambamo nabii ataishi jirani karibu nasi; atakuwa jirani yetu. tutakula hiyo miti, na tutatembea kwenye barabara hizo za dhahabu kwenda kwenye chemchemi na kunywa. Tutatembea katika paradiso za Mungu, huku Malaika wanarukaruka kuizunguka dunia, wakiimba nyimbo za sifa. Utukufu! Haleluya!

Akithibitisha Neno Lake kwetu; Yeye, ile Nguzo ya Moto, alipiga picha Yake pamoja na malaika-mjumbe Wake ili kuthibitisha na kuuambia ulimwengu, “Msikieni Yeye.” Hatupaswi kutilia shaka Neno moja, kwa maana Si neno la nabii, ni Neno la Mungu lililonenwa kwa Bibi-arusi Wake. Kisha akatuambia, tuna uwakilisho kwa kuchaguliwa tangu awali, kutuhakikishia. Yeye hatuoni sisi, anasikia tu sauti yetu kupitia Damu ya Yesu. Sisi ni wakamilifu machoni pake.

Kilindi kinaita kilindi kuliko wakati wowote ule. naye Baba anatujaza kwa Neno Lake lililofunuliwa. Kila kitu tunachohitaji kujua kimerekodiwa na tumepewa SISI. Ni kwamba tu hakuna mwisho kwa Ujumbe huu wa Neno la Uzima. Hakuna kitu kikubwa kuliko kujua SISI ni Bibi-arusi Wake. Hakikisho la kujua kwamba kusikiliza Sauti hiyo, Kubonyeza Play, ndio Mapenzi makamilifu ya Bwana; Mpango Wake aliyouandaa.

Kuna mengi zaidi yajayo! Ni Neno lisiloisha la Maji ya Uzima kwa ajili ya Bibi-arusi Wake. Hatujawahi kuwa na kiu zaidi katika maisha yetu yote, lakini hatujawahi kuburudika sana tunapokunywa na kunywa yote tunayotaka.

Kila Jumapili, Bibi-arusi anasisimka sana kukusanyika pamoja na sehemu ya Bibi-arusi kutoka ulimwenguni kote, ili kusikia kile kinachofuata ambacho Yeye anaenda kukifunua. Alituambia kama hatuwezi kuja hapa Maskanini, tutafute kanisa fulani mahali fulani; twende kwalo.

Hatuwezi sote kukusanyika pamoja kwenye kituo cha nyumbani cha nabii; makao yake makuu ambako yeye ameimarika, bali tunaweza kuyageuza makanisa yetu, ama Nyumba zetu kuwa makanisa, ambapo tunamweka yeye mimbarani. Ambapo tunaweza kulishwa NENO KAMILIFU JINSI TU VILE LILIVYOFUNULIWA.

Hakuna kukusanyika kukuu, hakuna upako mkuu, hakuna mahali pazuri zaidi pa kuwa kuliko kuketi pamoja katika ulimwengu wa roho, tukiisikiliza Sauti ya Mungu.

Ninawaalika mje kuisikia Sauti ya Mungu iliyothibitishwa pamoja nasi Jumapili hii saa 06:00 SITA MCHANA, saa za Jeffersonville,( Ni saa 1:00 MOJA JIONI ya Afrika Mashariki ) anapozungumza nasi kwa mara nyingine tena kupitia malaika-mjumbe Wake, na kuyajibu maswali yote tuliyo nayo mioyoni mwetu, na kutuhakikishia kwamba sisi ni Bibi-arusi Wake.

Ndugu. Joseph Branham

Ujumbe wa Jumapili:

Maswali na Majibu #1 64-0823M