24-0505 Maswali na Majibu #2

UJUMBE: 64-0823E Maswali na Majibu #2

PDF

pakua – m4a

pakua – amr

BranhamTabernacle.org

Mpendwa Bibi-arusi Neno-kamilifu,

Tunangojea tu kule Kuja kwa Bwana. Tukizitengeneza taa zetu, huku zikiwa zimejaa Mafuta, tukilisikiliza Neno lililofunuliwa mchana na usiku. Tukiomba vya kutosha, kila saa; si kila siku, kila saa. Tunajiweka tu wenyewe tayari kwa kukaa ndani, na kuamini, KILA NENO.

Tunatazamia, kila dakika, kwa wale waliolala katika mavumbi ya nchi waamshwe kwanza. Mara moja, tutawaona; baba, mama, waume, wake, kaka na dada. Hao hapo, wakisimama mbele zetu. Tutajua mara moja, tumewasili, wakati umefika. Imani ya kunyakuliwa itazijaza Roho zetu, akili na miili yetu. Ndipo miili hii iharibikayo itavaa ile isiyoharibika katika Neema ya kunyakuliwa ya Bwana.

Na kisha tutaanza kukusanyika pamoja. Sisi tulio hai na tuliosalia tutabadilishwa. Miili hii ipatikanayo na mauti haitaonja mauti. Kwa Ghafula, itakuwa kama upepo uvumao juu yetu … tutabadilishwa. Toka kwa mzee kuwa kijana, toka kwa mkongwe kuwa msichana.

Baada ya muda, tutasafiri kama wazo na wale waliokwisha fufuliwa tayari. KISHA…UTUKUFU…tutanyakuliwa pamoja nao ili kumlaki Bwana hewani.

Ni wakati ulioje ambao unaokuja kwa ajili yetu. Adui ANAJARIBU kutuweka chini, kutuhuzunisha, na kutuvunja moyo, lakini Mungu atukuzwe, hawezi. Tunao Ufunuo wa Yeye ni Nani; Ni yupi ambaye Yeye aliyemtuma kutuita sisi tutoke; sisi ni nani, si tutakuwa nani, SISI NI NANI. SASA limetia nanga katika NAFSI zetu, AKILI NA ROHO zetu, na hakuna kitu kinachoweza kuliondoa hilo kutoka kwetu. Tunajuaje? Mungu alisema hivyo!

Haya sio makao yetu, yote ni yako, Shetani, unaweza kuyachukua. Hatutaki sehemu yake na hatuyahitaji tena. Tunayo Makao ya Baadaye ambayo yamejengwa kwa ajili yetu. Na hata hivyo, shetani, tumepata taarifa, YAKO TAYARI. Ujenzi umekamilika. Nakshi zote za kumalizia zimekwisha kuwekwa mali pake. Nami ninayo habari fulani zaidi kwa ajili yenu, HIVI KARIBUNI SANA, Anakuja kutuchukua sisi ili tuweze kuwa na Fungate lisiloingiliwa kwa miaka 1000 pamoja Naye, nanyi hamjaalikwa, na hamtakuwepo.

Ni mambo tukufu jinsi gani ambayo Ujumbe huu unayotufunulia kila mara tunapo bonyeza Play. Mungu Mwenyewe alishuka, na kunena kupitia midomo ya mwanadamu ili aweze kutuambia mambo haya yote. Alituchagua na kutupa Ufunuo wa kweli na MZIMA wa Yeye Mwenyewe.

Yeye alikuwa Neno lililofanyika mwili, si lile Neno la siku za Musa, Musa alikuwa siku hiyo—Neno; si lile Neno la siku za Nuhu, Nuhu alikuwa Neno kwa siku hiyo; si siku ile—Neno lile la siku za Eliya, Eliya alikuwa Neno la siku hiyo; lakini Yeye alikuwa Neno la wakati uliopo, nao walikuwa wakiishi katika yaliyopita.

Je! Mko tayari?….Hili hapa linakuja. Ni pipa mara dufu na mzigo mzito, nasi tunalipenda Hilo sana!!

Jambo lile lile lajirudia! Hiyo ndiyo ishara ya Roho Mtakatifu, Mungu anapokufunulia na unaliona, BWANA ASEMA HIVI na kulikubali. Si vile ulivyo, vile ulivyokuwa, au lo lote lile, ni yale Mungu amekufanyia wewe sasa. Hiyo ndiyo ishara.

Haleluya, alipigilia msumari ndani. SASA hebu na tumsikie Yeye akiukaza.

Yeye alitupea ishara ya Roho Mtakatifu, Yohana 14. Yeye alisema, “Ninayo mengi ya kuwaambia. Sina wakati wa kuwaambia, lakini Roho Mtakatifu atakapokuja, Yeye atawaambia, atawakumbusha yote niliyowaambia, na mambo yajayo atawapasha habari zake.” Hamwoni? Hiyo ndiyo ishara. Huko ni kutabiri na kuwa— kuwa na fasiri ya Kiungu ya Neno lililoandikwa. Sasa, si hiyo ndiyo ishara ya nabii?

Roho Mtakatifu ndiye nabii wa kila kizazi. Yeye ni nabii wa kizazi chetu. Neno linakuja kwa nabii huyo TU. Ni Mungu akizungumza na kujidhihirisha Mwenyewe kupitia nabii Wake. Yeye ndiye Neno la siku hii. Ujumbe huu, KWENYE KANDA, ndio fasiri kamilifu ya Neno, lenye thibitisho la Kiungu.

“Ijapo ile iliyo kamili, iliyo kwa sehemu itabatilika.” Kwa hivyo mambo haya yote madogo madogo ya kuruka juu na chini kama mtoto, kujaribu kunena kwa lugha, na mambo haya yote, ijapo ile iliyo kamili… Nasi tunayo siku hizi, kwa msaada wa Mungu, ile fasiri kamilifu ya Neno na thibitisho la Kiungu! Basi ile iliyo kwa sehemu imebatilishwa. “Nilipokuwa mtoto mchanga, nilisema kama mtoto mchanga, nilifahamu kama mtoto mchanga;tokea hapo nilipokuwa mtu mzima, nimeyabatilisha mambo ya kitoto.” Amina!

Ile iliyo kamili imekuja; ile fasiri kamilifu ya Neno. BONYEZA PLAY. Hayo tu ndiyo yote Bibi-arusi Wake anayohitaji, na yote Anayotaka.

Njooni na Mbonyeze Play pamoja nasi Jumapili hii saa 06:00 SITA MCHANA, saa za Jeffersonville,( ni saa 1:00 MOJA JIONI ya Afrika Mashariki ) na kusikia NENO KAMILIFU, LENYE ILE FASIRI KAMILIFU, LENYE THIBITISHO LA KIUNGU wakati tunaposikia:

Maswali na Majibu #2 – 64-0823E

Ndugu. Joseph Branham