22-1009 Maswali na Majibu #2

Ujume: 64-0823E Maswali na Majibu #2

PDF

pakua – m4a

pakua – amr 16MB (use Firefox to download)

BranhamTabernacle.org

Mpendwa Bikira Safi aliyeposwa,

Mungu anatupenda sana hata akamfanya nabii wake ajibu maswali yetu YOTE, na akaweka majibu kwenye kanda. Wakati Tunapoyahitaji, yote tunayopaswa kufanya ni KUAMINI NA KUBONYEZA PLAY.

Je, ninaye Roho Mtakatifu?

Ishara ya Roho Mtakatifu, Mungu anapokufunulia na unaliona, BWANA ASEMA HIVI na kulikubali.

Basi ninaye Bwana, ulivyonifunulia Ujumbe huu na nimeukubali kama Bwana Asema Hivi !

Lakini, inaonekana kama ninakosea sana…na vipi kuhusu maisha yangu ya nyuma?

Si vile ulivyo, vile ulivyokuwa, au lo lote lile, ni yale Mungu amekufanyia wewe sasa. Hiyo ndiyo ishara.

Bwana, huyaoni maisha yangu ya nyuma na hata huyaoni makosa yangu mengi, mengi sasa, Unasikia sauti yangu tu; Utukufu Bwana, NINAYE ROHO MTAKATIFU.

Ndugu Branham, najua ulisema wewe siye changarawe pekee pwani, lakini ni nani atakayekuwa akimuongoza Bibi-arusi wa Kristo katika wakati wa mwisho?

Kwa msaada wa Mungu, naamini kuwa ninamuongoza Bibi-arusi wa Yesu Kristo.

Nina mambo mengi moyoni mwangu, nifanye nini?

Hakuna kilicho muhimu sasa ila kuwakusanya watoto wote wa Mungu pamoja na kusema, “Haya twendeni.”

Asante Bwana, tunafanya hivyo tu. Hakuna kitu kingine kilicho muhimu kwetu ila Neno Lako. Roho Wako Mtakatifu anatuongoza kupitia nabii Wako na tunakusanyika kulizunguka Neno Lako kutoka ulimwenguni kote, nasi tuko tayari Kwenda.

Nina maswali mengi, ninahitaji mwongozo, msaada, na majibu. Nitayapata wapi hayo?

Niko hapa kujaribu kuwasaidia, kwa sababu nawapenda. Ninyi ni watoto wangu niliomzalia Kristo. Nadai kila mmoja wenu. Nadai ninyi usiku huu; nadai ninyi wakati wote; mimi kila mara huwadai ninyi kisha—kama ndugu yangu na dada.

Tunakupenda pia Ndugu Branham. Tunajua Mungu alikutuma utuongoze na kutuelekeza. Tumelichunguza kwa Neno nalo linajipanga kikamilifu.

Ni nani Aliye Baba yangu katika Injili?

Ninyi ni watoto wangu; mi—mimi ni baba yenu katika Injili, si baba kama vile kasisi angalikuwa, mimi—mimi ni baba yenu katika Injili kama Paulo alivyosema pale.

Tunajua ni Roho Mtakatifu akuongozaye wewe kutuongoza, Ndugu Branham. Unasema kama vile tu Paulo alivyosema katika Biblia, kufuata hasa kabisa yale uliyosema, kwa kuwa ni Kweli, nasi hatupaswi kubadili yodi moja au nukta moja.

Utafanya nini Ndugu Branham?

Nimewazaa ninyi kwa Kristo, na sasa na—nawaposea ninyi Kristo; hilo ni kufanya ninyi muweke nadhiri ya ndoa kwa Kristo kama bikira wasafi. Msiniaibishe! Msiniaibishe! Ninyi iweni bikira safi.

Umetuposa sisi kwa Kristo kama mabikira kwa Neno Lake. Hatuwezi, na hata hatutavutiwa na mwingine. Tunakagua kila kitu tunachosikia na tunachofanya kwa Neno Lako lililohifadhiwa.

Je, ni jambo gani muhimu zaidi ninaloweza kufanya ili kuwa Bibi-arusi Wake, Ndugu Branham?

Kaa moja kwa moja na Neno.

Majibu yote kwa maswali yetu yanaweza kufupishwa kwa maneno haya:

KAA MOJA KWA MOJA NA NENO.

Ujumbe huu NI Neno la wakati wetu. Ndugu Branham ndiye Sauti ya Mungu kwa Wakati wetu. Kila kitu lazima kiendane na Neno. Neno halihitaji Kufasiriwa kwokwote. TUNAPOBONYEZA PLAY, YOTE TUNAYOHITAJI YANATOLEWA HAPO, KWENYE HIZO KANDA.

Je, Una jambo fulani moyoni mwako unalohitaji jibu? Njoo uungane nasi Jumapili
saa 6:00 SITA MCHANA , saa za Jeffersonville, (Ni Saa 1:00 MOJA JIONI Ya Tanzania) tunapopata majibu yetu yote tunaposikia : 64-0823E – Maswali Na Majibu #2.

Ndugu. Joseph Branham