24-0407 Mabirika Yavujayo

UJUMBE: 64-0726E Mabirika Yavujayo

PDF

pakua – m4a

pakua – amr

BranhamTabernacle.org

Wapendwa Wanywaji Wa Kisima Kinachofoka Maji,

Bibi-arusi kamwe hatakuwa yeye yule tena baada ya wikendi ya Pasaka iliyo kuu ambayo Bwana aliyotupa. Tulikuwa tumefungiwa ndani pamoja Naye, tukishirikiana na kumwabudu Yeye wikendi yote. Uwepo wake ulizijaza nyumba zetu na makanisa yetu.

Tulikuwa chini ya matarajio makubwa kweli. Tulijua haya yalikuwa Mapenzi ya Bwana kwetu. Mungu alikuwa anajitayarisha kufanya jambo fulani. Tukafunga ulimwengu na vizubaishi vyake vyote. Tuliungana kutoka kote ulimwenguni kwa nia moja. Tulikuwa tumeketi pamoja katika mahali pa mbinguni, Tukijitayarisha vile ANGEZUNGUMZA NASI njiani.

Mioyo yetu ilikuwa ikilia, “Bwana, nifanye nifanane na Wewe zaidi. Nitayarishe kwa ajili ya huku kuja Kwako hivi karibuni. Nipe Ufunuo zaidi. Roho Wako Mtakatifu akijaze kila kiungo cha utu wangu.”

Wakati kila ibada ilipoanza, tulijiambia wenyewe, “Inawezekanaje? Nimezisikia Jumbe hizi maisha yangu yote, lakini sasa hivi zote zinaonekana kuwa mpya, kana kwamba sijawahi kuzisikia hapo awali. Yeye alikuwa akilifunua Neno Lake mioyoni na nafsini mwetu zaidi ya hapo awali”.

Ufunuo ufurikao ukaja tena ndani ya mioyo yetu… Ni Yeye… YEYE. Ni Roho Mtakatifu Mwenyewe AKIONGEA NASI MOJA KWA MOJA.

Sio mimi! Yeye! Yeye Ndiye! Ndio kwanza niwaambie, Yeye aliuchukua tu mwili wangu. Yeye huuchukua tu ulimi wangu, anayachukua macho yangu, kwa sababu Yeye alijua ningeyasalimisha Kwake, kwa hiyo Yeye alikuja tu na kunifanya nifanye hivyo. Kwa hiyo si mimi! Ni Yeye! Wala si mimi huko nje pamoja nanyi, ni Yeye huko nje pamoja nanyi. Yeye ndiye Ufufuo na Uzima. Loo, Mungu, Mungu; liamini. Loo, enyi watu: Mwaminini. Mwaminini. Yeye yupo hapa.

Yeye ametupa Ufunuo wa kujua HIZI KANDA ndiyo Sauti ya Mungu inayonena nasi leo hii. Hizo Kanda ndio Maneno Yake, Sauti Yake…SAUTI YAKE, iliyorekodiwa na KUHIFADHIWA ili tuweze KUMSIKIA YEYE akinena nasi Maneno ya uzima wa Milele. Hizo ndiyo njia Yake iliyoandaliwa kwa ajili ya Bibi-arusi Wake.

Ni matamu, masafi, Maji ya kisima yakibubujika na kububujika. Kadiri tulivyokunywa, ndivyo tulivyozidi kupaza sauti, “Zaidi Bwana, ZAIDI. Kijaze kikombe changu Bwana, kijaze Bwana”. Naye akakijaza! Kadiri tunavyozidi kunywa, ndivyo ANAVYOZIDI KUTUPA.

Kisha shetani akatamkwa ameshindwa kwa nguvu za Injili. Kwa Mungu wa Mbinguni Yule Aliyemchagua na Kumtuma Malaika Wake Atuhubirie Injili. Kwa Mungu Yule Aliyeliandika Neno na Kumtuma Malaika Wake ambaye Aliyekuwepo Kulithibitisha Neno Lake. “Toka ndani ya hawa watu, katika Jina la Yesu Kristo”.

ILIMBIDI ibilisi kumwacha kila mgonjwa, kila mtu anayeteseka. Sasa nguvu za Mungu zimetufufua tumepata afya njema na nguvu tena.

Kisha, kutoka ndani ya kilindi cha mioyo yetu tulisema:

“Mimi sasa nakubali ya kwamba Yesu Kristo, kama Mwana wa Mungu aliyefufuka, Yeye ni Mwokozi wangu, Yeye ni Mfalme wangu, Yeye ni Mponya wangu. Sasa nimepona. Nimeokoka. Nitamwishia Yeye aliyenifia. Nitasimama kutoka hapa katika upya wa maisha, nipate kusonga mbele nikafanye vizuri niwezavyo Kwake…kwa ajili Yake Yeye aliyefufuka kwa ajili yangu. Haleluya!”

Hiki ni Kisima Kinachofoka Maji tunachokinywea kila siku. Ndicho kisima pekee kinachotoka moja kwa moja kutoka Mbinguni kinachotiririka daima. Kinajitegemea chenyewe. Daima ni matamu na masafi. Hayajakufa na kuoza. Ni Maji ya uzima yanayobadilika kila wakati, yakifunua jambo jipya kwa Bibi-arusi kila wakati.

Daima kinabubujika. Haitubidi kuyavuta kwa mashine, kuyavuta kwa winchi, kuyapindisha, ama kujiunga nayo. Ni chemchemi ya Mungu ya Maji ya uzima, nasi hatuwezi kufikiri kunywa kitu kingine chochote.

Tunasikia leo, “Maji yetu ndio maji bora unayopaswa kunywa. Tumeyaweka kwenye mchakato wetu wa uchujaji wa hatua ya 7. Kisha tumeongeza madini yote TULIYOYACHUJA tumeyarudishamo tena katika maji tunayodhani mnahitaji kuongeza maji mwilini.

Utukufu kwa Mungu, haitupasi kubahatisha au kuhoji ikiwa kile tunachokunywa ama kile kilichoongezwa ama kuchujwa. KILA KITU tunachohitaji kiko katika Maji yetu.Tunachotakiwa tu kufanya ni KUBONYEZA PLAY na kunywa kama kibubujikavyo.

Ni faraja iliyoje kuyanywa Maji haya. Tungetoka kwenda maili nyingi ili tu kunywa kwenye hilo, lakini haitupasi kufanya hivyo. Tunalibeba kila mahali tuendapo. Majumbani mwetu, makanisani mwetu, kazini, tuendeshapo katika magari yetu, tuendapo matembezini… TUNAKUNYWA, NA KUNYWA, NA KUNYWA.

Ee ulimwengu, njooni mnywe kutoka kwenye Chemchemi iliyotolewa na Mungu. Ndio mahali PEKEE huhutaji kuwa na wasiwasi na kusema, “Naomba Roho Mtakatifu atanilinda ili nisije nikanywa kitu chochote nisichotakiwa kunywa.” LOTE NI NENO SAFI LILILOTHIBITISHWA LIKITIRIRIKA KUTOKA KWENYE CHEMCHEMI ZA MBINGUNI.

Hakuna mahali pengine Panapofaa Bibi-arusi Wake kunywa!

Njoo Unywe pamoja nasi kwenye Kisima chetu Kinachofoka maji Jumapili hii saa 06:00 SITA MCHANA, saa za Jeffersonville,( Ni saa 1:00 MOJA JIONI ya Afrika Mashariki ) tunaposikia: Mabirika Yavujayo 64-0726E.

Ndugu. Joseph Branham

Maandiko ya kusoma kabla ya kusikiliza Ujumbe:

Zaburi 36:9
Yeremia 2:12-13
Yohana Mtakatifu 3:16
Ufunuo Sura ya 13