22-1030 Mtu Anayejiepusha Na Uso Wa Bwana

Ujume: 65-0217 Mtu Anayejiepusha Na Uso Wa Bwana

PDF

pakua – m4a

pakua – amr 9MB (use Firefox to download)

BranhamTabernacle.org

Wapendwa Wana-kondoo wa Bwana,

Jinsi mioyo yetu inavyotamani siku hii kila wiki tunapoweza kuungana pamoja kutoka ulimwenguni kote ili kusikia Sauti ya Mungu ikizungumza nasi Neno la Uzima wa Milele. Hakuna kitu kingine kinachoshibisha nafsi zetu na kukata kiu yetu ila Sauti ya Mungu.

Ulituambia, Baba, kwamba mashamba Makubwa ya mavuno ni meupe, yameiva, na nafaka iko tayari sasa kwa ajili ya ule wakati mkuu wa kupura. Nafaka sasa inakaa katika Uwepo wa Mwana na ikiiva kwa ajili ya Ufalme wa Mungu.

Baba, Tunatetea tunayoamini kuwa ni Kweli; Sauti Yako kwenye kanda ndiyo Sauti PEKEE ambayo itatukamilisha sisi, Bibi-arusi Wako.

Ni ngumu kwani tunaeleweka vibaya sana kwa ndugu na dada zetu. Tunawasihi na kuwaomba wasijiepushe na Uwepo Wake, bali wakimbilie kuingia katika Uwepo Wake.

Tunajua kuna watu wengi watiwa-mafuta uliowachagua na kuwaweka waangalie kundi Lako, wanaopenda Ujumbe huu kwa mioyo yao yote, Lakini Baba, wanashindwa kuweka Sauti Yako iliyothibitishwa kwenye kanda mbele yao. Wanashindwa kuwaambia kwamba huu ni Ujumbe wa mtu mmoja na kwamba Wewe ulimchagua mtu huyo kumwongoza Bibi-arusi Wako. Wanashindwa kuwaambia kwamba Sauti Yako ndiyo Sauti PEKEE itakayomunganisha na kumkamilisha Bibi-arusi Wako.

Lazima “Nipige kelele juu yake.” Nipige kelele juu ya kila kitu, na kila mtu, ambaye anapinga kucheza Kanda Zako katika makanisa yao. Nipige kelele juu ya matendo yao, nipige kelele juu ya kanisa lao, nipige kelele juu ya manabii wao, nipige kelele juu ya wahudumu wao, nipige kelele juu ya makasisi wao. Lazima nipige kelele juu ya kitu hicho chote!

“Aisee, nimeshuka kuja kujiunga nanyi enyi jamaa. Mnajua, naamini nitawaambia nitakachofanya. Nina kitu kidogo tu hapa naamini ninaweza kuifanya ninino…kutuunganisha sote pamoja, na kufanya hivi, vile, ama vinginevyo.”

Lazima nipige kelele juu ya jambo hilo, kwani Neno Lako pekee, lililonenwa na nabii Wako, ndilo linaloweza kutuleta PAMOJA. Mahubiri yao yanawezaje? Wote hawakubaliani mmoja kwa mwingine na wanaona mambo kwa njia tofauti mmoja kwa mwingine, isipokuwa jambo moja, wote wanalokubaliana kwalo… KUTOCHEZA KANDA KATIKA MAKANISA YAO. Hilo lawezaje , Baba?

Ulituambia ni lazima tuwe na YAKINI MOJA, ambayo ni Neno lako. Ulituambia Neno Lako humjia nabii Wako, PEKE YAKE. Ulituambia yeye ndiye Mtu PEKEE anayeweza kulifasiri Neno Lako. Ulituambia kwamba kila mhudumu, kila mshiriki wa kawaida, kila mwanadamu, anaweza TU KUSEMA ALICHOSEMA. Sauti Yake ndiyo SAUTI PEKEE ambayo imethibitishwa na Nguzo Yako ya Moto kuwa Bwana Asema Hivi .

Sisemi kwamba ni wa uwongo au hawapaswi kuhubiri. Wala sisemi Bwana hayuko pamoja nao, au hawajatiwa mafuta na kuitwa kuhubiri, Lakini lazima niwapigie kelele wakati hawatawaambia watu wao kwamba kusikiliza kanda ndilo jambo muhimu zaidi wanaloweza kufanya.

Kubadilisha yodi moja au nukta moja ni kifo. Umeandaa njia kwa ajili ya Bibi-arusi wako kusikia Bwana Asema hivi kwa masikio yao wenyewe. Wanawezaje Kutowahubiria watu wao kwamba huu Ndio Ujumbe uliyo muhimu sana uwapasao Kusikia? Ndio Ujumbe pekee ninaoweza kusema AMINA kwa kila Neno, kwa kuwa si Neno la mwanadamu, au fasiri ya mwanadamu ya Neno Lako, ni Neno Lako Safi.

Ulisema Ujumbe na mjumbe ni kitu kimoja . Nabii wako alinena Hilo nawe ungelitimiza. Neno Lako lililonenwa na nabii Wako HALIHITAJI fasiri kwa kuwa ni Mwana wa Adamu akizungumza moja kwa moja na Bibi-arusi Wake.

Yanipasa niwasihi watu, rudini kwenye upendo wenu wa kwanza. Rudini kwenye kile mnachojua ni BWANA ASEMA HIVI. Ikiwa umekuwa unajiuliza ni njia gani ya kwenda au nini cha kufanya, njoo, ingia katika Merikebu pamoja nasi usiku wa leo. Tunashuka kwenda Ninawi, ili kupiga kelele. Tuna wajibu mbele za Mungu, huo ni Ujumbe huu kwenye kanda.

Tunaamini ya kwamba Kuja kwa Bwana kumekaribia, Naye atakuwa na Bibi-arusi, nasi tunajitayarisha. Hatutaki chochote ila Neno Safi la Mungu lililonenwa na nabii Wake. Tunaenda Utukufuni, njoo tuungane katika Merikebu yetu.

Ikiwa unaamini Ujumbe huu ni Kweli, na unaostahili kuuishia, unaostahili kuufia, njoo uungane nasi Jumapili hii saa 06:00 SITA MCHANA , saa za Jeffersonville, (Ni saa 1:00 MOJA JIONI Ya Tanzania), tunaposikia Ujumbe tunaoamini ni muhimu na wa haraka kwetu kuusikia: Mtu Anayejiepusha Na Uso Wa Bwana 65-0217.

Ninyi ni wana-kondoo wangu. Mwaonaje? Ninyi ni wana-kondoo wa Bwana ambao ameniruhusu kuwalisha .

Ndugu. Joseph Branham.

Maandiko ya kusoma kabla ya Kusikiliza Kanda :

Yona 1:1-3
Malaki sura ya 4 yote
Yohana Mt. 14:12
Luka 17:30