24-0324 Kutambua Siku Yako Na Ujumbe Wake

UJUMBE: 64-0726M Kutambua Siku Yako Na Ujumbe Wake

PDF

pakua – amr

BranhamTabernacle.org

Wapenzi Watu Wathamani na Wapendwa,

Inapendeza sana jinsi gani kujua sisi ndio Bibi-arusi Wake mpendwa na Wathamani. Tumefanyizwa kutoka ulimwenguni kote, tukikusanyika pamoja kulizunguka Neno Lake, tukisikiliza Sauti ya Mungu ikizilisha nafsi zetu.

Tumelikubali katika ukamilifu wake, na katika nguvu ya kuthibitishwa kwake na ufunuo wake. Tumekuwa sehemu Yake. Ni kitu ambacho kiko ndani yetu. Ni zaidi ya uhai kwetu.

Tumetambua: Malaika-Mjumbe Wake wa Saba.
Tumetambua: Ujumbe wa Nuru ya Jioni.
Tumetambua: Sisi ni Nani.

Mungu amechukua Neno la nabii Wake na kutubangua. Ametukata kwa Malaki 4, kama alivyoahidi angefanya. Tunaamini kila Neno kwa mioyo yetu yote.

Kuna uamsho mkubwa unaoendelea miongoni mwa watu. Wao pia wanatambua umuhimu wa kuisikia Sauti hiyo. Wanataka kurudi na kuzicheza kanda katika makanisa yao.

Wamejulishwa na Roho Mtakatifu, kwamba hii ndiyo Njia iliyoandaliwa na Mungu kwa ajili ya siku hii. Wanatambua kuwa hii ndio Sauti wanayohitaji kuisikia. Ndicho Chakula cha Mungu kilichohifadhiwa kwa ajili ya kumkamilisha Bibi-arusi Wake.

Neno liliahidi jambo Hilo. Kanda zinalitangaza. Wao wanaliamini.

Ilifanyaje? Iliwasumbua makuhani, kuona hao watu wakiondoka makanisani na kwenda zao. Akasema, “Kama yeyote wenu akihudhuria mikutano Yake, mtatengwa na ushirika. Tutawafukuza moja kwa moja kutoka katika dhehebu.”

Haliaminiki, lakini hilo limekuwa ni jambo lile lile leo hii. Watakufukuza katika makanisa yao ukisema, “Tafadhali, chezeni kanda.” Je! Hivi tumewahi kamwe kuwazia huenda hiki ndicho kinachowatenganisha watu? Kuicheza Sauti ya Mungu katika makanisa yetu?

Kanisa limesahau manabii wao. Wao “hawawahitaji tena,” ndivyo wanavyodai. Bali Mungu anajua hana budi kuwa nao; Yeye huwakata watu Wake kwa Neno Lake. Lakini kwao Hilo limepitwa na wakati sana katika siku hii.

Tutakaa na nabii wetu. Tunaamini kuwa ndio Sauti inayomwita Bibi-arusi Wake. Kwetu sisi, hakuna kitu chochote kilicho muhimu zaidi ya KUBONYEZA PLAY.

Loo, enyi kondoo za Mungu, sikilizeni Sauti ya Mungu! “Kondoo Wangu huisikia Sauti Yangu.”

Njoo uisikie na uitambue Sauti hiyo pamoja nasi, Jumapili saa 6:00 SITA MCHANA, saa za Jeffersonville,( Ni saa 1:00 MOJA JIONI ya Afrika Mashariki ) tunaposikia,  Kutambua Siku Yako na Ujumbe Wake 64-0726M.

Ndugu. Joseph Branham