24-0317 Kuenda Nje Ya Kambi

UJUMBE: 64-0719E Kuenda Nje Ya Kambi

PDF

pakua – m4a

pakua – amr

BranhamTabernacle.org

Wapendwa Askari Wakristo,

Wazieni jambo hilo! Ni mwisho wa wakati, Haleluya! Tumewasili. Ile Siku kuu ya Kuja kwa Bwana kumchukua Bibi-arusi Wake imekaribia. Tunakusanyika wenyewe pamoja kutoka ulimwenguni kote, tukikamilishwa kwa kusikiliza Sauti ya Mungu. Tunatazamia na kungojea wapendwa wetu watokee… ni siku yoyote sasa.

Kitu pekee ambacho tumeagizwa kufanya ni “Dumuni na Neno”. Yote tuyaonayo ni Yesu, na Yeye ni Neno lililofanyika mwili. Huo ndio Ufunuo wa siku yetu. Hiyo ndio Kambi ya Mungu kwa ajili ya Bibi-arusi Wake.

Ujumbe huu, Sauti hii, kanda hizi, ndicho kila kitu tunachohitaji kwa ajili ya Unyakuo. Hatuhitaji kitu kingine chochote. Tumeitwa tutoke, tumetengwa na kila kitu kingine isipokuwa ile Sauti. Tumeshawishika kuwa Sauti hiyo ndiyo Njia ya Mungu iliyoandaliwa kwa ajili ya siku hii.

Wazieni jambo hilo, Yeye ametupatia nabii mkuu wa nyakati zote. Yule ambaye Nguzo ya Moto Mwenyewe alipiga picha naye ili aweze kuuambia ulimwengu, “Huyu ni malaika wangu mwenye nguvu. Yeye ni Sauti Yangu kwenu. Yale Anenayo duniani Mimi nitarudisha mwangwi mbinguni. Hakuna aliye kama yeye”.

“Nimemkabidhi yeye, na yeye peke yake, siri Zangu zote nilizozificha tangu kuwekwa misingi ya ulimwengu. Yeye ndiye niliyemchagua tangu awali kuwaita NINYI mtoke katika ulimwengu huu mje Kwangu. Yeye ndiye niliyemchagua kuwatangulia, kuwaongoza, na kuwaelekeza. Nawatangazieni, msikieni Yeye, kwa maana si yeye anenaye, NI MIMI, YULE MIMI NIKO ALIYE MKUU.

Nimewaweka wakfu watu wakuu na kuwaita kuutangazia ulimwengu na kuuambia , “Leo maandiko ya Malaki 4, Ufunuo 10:7 na Luka 17:30 yametimia mbele ya macho yenu. Yule Malaika wake mwenye nguvu amewasili, kama jinsi Maandiko yalivyotangaza. Mungu yuko hapa miongoni mwetu, akijifunua Mwenyewe katika mwili wa mwanadamu kama alivyosema angefanya.”

Ni Yesu Kristo yeye yule jana, leo na hata milele. Tumeitwa kuwaelekeza ninyi kwake yeye, malaika wa Mungu. Yeye ndiye ambaye Roho Mtakatifu alimchagua kuongoza na kumwita Bibi-arusi Wake atoke. Msihojiane, msibishane, msigombane na kushindana ni nani atakayekuwa kuhani mkuu; nani anayetakiwa kuwa hili, lile, ama linginelo. DUMUNI NA SAUTI HIYO. Kwa maana kuna SAUTI YA MUNGU moja tu iliyothibitishwa na jina lake ni William Marrion Branham.

Yatupasa kuwa waangalifu sana kudumu na hiyo Sauti, kwa kuwa kuna wengi wanaotaka kuwaongoza kwingineko. Mapokeo yao yanaiweka Sauti hiyo ya kweli mbali na watu. Yeye amekuwa mgeni kwa wengi wao. Sauti yao imepachukua mahali pa Sauti hiyo, hata wakati Mungu, kwa njia ya kanda, anapowazuru, Yeye ni mgeni.

Ule uwepo mkuu wa Agosti u pamoja nasi. Mtu yeyote mwepesi wa kuhisi Roho anaweza kujua Sauti hiyo ni Sauti ya Mungu. Ndio ile Kambi ya Mungu kwa ajili ya siku hii.

Kila mtu anayedai kuwa Bibi-arusi wa Kristo lazima aamue ni Kambi gani aliyomo. Ni lazima wajiulize swali hili rahisi: Hivi ni Sauti gani ambayo Bibi-arusi wote wanaweza kusema “AMINA” kwayo?

Kama kweli wewe ni Bibi-arusi wa Kristo, mwenye Ufunuo wa kweli wa Neno la siku hii, kuna jibu moja tu: Sauti ya Mungu iliyo kwenye Kanda. Bila shaka Shetani anajaribu kuliendesha hilo kwa njia nyingi tofauti, lakini hakuna jibu lingine kwa Bibi-arusi. Ni rahisi jinsi hiyo.

Sote tunajua kwamba Shetani anatumia jibu hilo ili kutugawanya. Lakini Neno linatuambia Bibi-arusi hana budi KUUNGANA… TUMEUNGANA, kwa SAUTI PEKEE INAYOTUUNGANISHA.

Njoo uungane nasi, kwa maana ile saa imechelewa sana.

“Nataka kwenda nje ya kambi. Haidhuru itanigharimu nini, nitautwaa msalaba wangu na kuubeba kila siku. Nitatoka nje ya kambi. Hata watu waseme nini juu yangu, nataka kumfuata nje ya kambi. Niko tayari kwenda.”

Ikiwa unataka kuwa katika ile Kambi ya Mungu ya siku hii, LAZIMA UAMINI Sauti ya Mungu iliyo kwenye kanda ndio Sauti iliyo muhimu sana unayopaswa kuisikia.

Njoo uungane na sehemu ya Bibi-arusi Jumapili hii saa 6:00 SITA MCHANA, saa za Jeffersonville,( ni saa 1:00 MOJA JIONI ya Afrika Mashariki ) tunapoisikia ile Sauti ambayo Mungu aliyoichagua kumwongoza Bibi-arusi Wake, anapotuletea Ujumbe, Kuenda Nje ya Kambi 64-0719E.

Sio “kambi fulani”; ni “ILE KAMBI”.

Ndugu. Joseph Branham

Maandiko ya kusoma kabla ya Ibada :

Waebrania 13:10-14
Mathayo 17:4-8