24-0310 Sikukuu Ya Baragumu

UJUMBE: 64-0719M Sikukuu Ya Baragumu

PDF

pakua – m4a

pakua – amr

BranhamTabernacle.org

Wapendwa Watoto wa Nuru,

Tunayo shukurani jinsi gani kuwa tunatembea katika Nuru Yake. Kuwa sehemu ya Nuru hiyo, kutambulishwa na Nuru Yake. Kuitwa na kuchaguliwa Na Yeye. Sisi ni Bibi-arusi wa Kristo, tumetambulishwa pamoja Naye. Hao wawili sasa ni Mmoja.

Nisingeweza kuliandika mara nyingi sana. Hatuwezi kulisema vya kutosha. Ujumbe huu unamaanisha KILA KITU kwetu. Kujua kuwa tunao Ufunuo wa kweli wa Neno Lake ni zaidi ya chochote tungeweza kuweka kwa maneno.

Kuishi katika siku hii na kuwa sehemu ya kile kinachotendeka, ndio heshima iliyo kuu ambayo Mungu angeweza kutupa. Jinsi lilivyokuwa jambo kuu kuketi katika mikutano katika Maskani ya Branham, kuona na kumsikia malaika wa Mungu akizileta Jumbe hizi, ni KUU hata na zaidi kule kuishi katika siku hii, na wakati huu, na kuwa ule utimilifu wa Neno hilo.

Mungu, katika Mpango Wake mkuu, ameandaa Njia ambayo tungeweza kukusanyika kutoka ulimwenguni kote, kuisikiliza Sauti ya Mungu sote kwa wakati mmoja, ili kukamilishwa na Neno Lake. Kusubiri kusikia katika sekunde yoyote malaika-mjumbe wetu wa saba aseme;

“Tazama Mwana-Kondoo wa Mungu aichukuaye dhambi ya ulimwengu!”

Hakujawahi kuwa na kitu chochote kama Hicho tangu mwanzo wa wakati. Kule Kumalizika kwa Mpango mkuu wa Mungu kunatukia, SASA HIVI, na sisi tu sehemu Yake. Ile Siku kuu ya Bwana imekaribia.

Siri zote zimefunuliwa kwa Bibi-arusi na malaika-mjumbe wa Mungu. Ile Mihuri, zile Nyakati, Ngurumo, Imani ya Kunyakuliwa, Mvuto wa Tatu…KILA KITU kimekwishanenwa na kiko kwenye kanda ili Bibi-arusi aweze kuzisikia tena na tena, nayo INATUKAMILISHA.

Roho Mtakatifu amerudi Kanisani tena; Kristo, Mwenyewe, akifunuliwa katika mwili wakibinadamu, wakati wa jioni kama alivyoahidi.

Sikiliza kwa makini sasa ewe Bibi-arusi, likamate.

Tumeitwa na Neno; Kristo mwenyewe ametuita. Amejiweka mwenyewe dhahiri kwetu; Waebrania 13:8, Luka 17:30, Malaki 4, Waebrania 4:12, Maandiko haya yote aliyoahidi.

Ni Yesu, Mwana wa Mungu, ambaye amejifunua kwetu kwa Maandiko haya ambayo yaliyochaguliwa tangu zamani kwa ajili ya siku hii, YAISHI TENA.

Na, kuamini Hilo, ndio dhihirisho la Roho Mtakatifu.

Mungu alimtuma nabii Wake kumwita Bibi-arusi Wake atoke. Neno linatuambia nabii ni Neno lililo hai la Mungu, lililodhihirishwa. Ndio ishara ya mwisho ambayo ulimwengu utakayopata; Yehova akinena katika umbo la mwanadamu.

Mtu katika mwili wa kibinadamu, kama nabii, hata hivyo ilikuwa ni Elohimu akilitambua wazo lililokuwa katika moyo wa Sara, nyuma Yake. Naye Yesu alisema, “Kama ilivyokuwa katika siku za Lutu, ndivyo itakavyokuwa katika ukamilifu wa dahari, wakati Mwana wa Adamu,” si Mwana wa Mungu, “wakati Mwana wa Adamu atakapokuwa akifunua.”

Bibi-arusi anajua isipokuwa uwe daima katika Neno, hutajua Yeye ni nani. Wao wanajua umuhimu wa kuiweka Sauti hiyo mbele zao kila siku kwa Kubonyeza Play.

Sasa Bibi-arusi hana budi kuondoka jukwaani, na kwenda juu, ili wale manabii wawili wa Mungu katika Ufunuo waweze kutokea jukwaani ili kupiga Baragumu ya Saba. Kuwajulisha Kristo.

Njoo uwe sehemu ya unabii uliotimia Jumapili hii saa 6:00 SITA MCHANA, saa za Jeffersonville, ( ni saa 1:00 MOJA JIONI ya Afrika Mashariki ) wakati nabii wa Mungu anapoleta Ujumbe, Sikukuu ya Baragumu 64-0719M, na kuzungumza na Baba na kusema,

Yawezekana kuwe na baadhi huko nje katika mataifa, ulimwenguni kote, ambao hata kanda hii ingewakuta manyumbani mwao au makanisani mwao. Tungeomba, Bwana, kwamba wakati ibada inaendelea, pale—pale…au kanda inachezwa, au nafasi yo yote tunayoweza kuwamo, au—au hali, yule Mungu mkuu wa Mbinguni na aheshimu huu unyofu wa mioyo yetu asubuhi hii, na kuponya wahitaji.

Ndugu. Joseph Branham

Maandiko ya kusoma kabla ya kusikiliza Ujumbe:

Walawi 16 yote
Walawi 23:23-27
Isaya 18:1-3
Isaya 27:12-13
Ufunuo 10:1-7
Ufunuo 9:13-14
Ufunuo 17:8