24-0303 Kile Kipeo

UJUMBE: 64-0705 Kile Kipeo

PDF

pakua – m4a

pakua – amr

BranhamTabernacle.org

Wapendwa Familia Iliyo Kipeo,

Jinsi gani Jumbe hizi za mwisho zimekuwa Kamilifu kabisa kwa Bibi-arusi wa Kristo. Mungu, akijifunua Mwenyewe mbele zetu, akijifunua Mwenyewe waziwazi. Ulimwengu hauwezi kuliona Hilo, lakini kwetu sisi, Bibi-arusi Wake, Hilo ndilo tuonalo.

Tumelipenya pazia na kumwona Yeye waziwazi kabisa. Mungu, nyuma ya ngozi ya mwanadamu. Neno limefanyika mwili, kama vile hasa Yeye alivyoahidi katika Luka 17 na Malaki 4. Amejificha Mwenyewe katika pazia la mwanadamu, katika nabii Wake na katika Kanisa Lake.

Sisi ndio watu wenye furaha kuliko wote ulimwenguni wakati tunapomsikia Mungu akinena kupitia malaika-mjumbe Wake na kutuambia,

Ninashukuru sana kwa ajili yenu. Nina furaha sana kushirikiana pamoja nanyi. Nina furaha sana kuwa mmoja wenu. Mungu awe nanyi.Atakuwa nanyi. Yeye hatawaacha kamwe. Hatawapungukia. Yeye hatawaacha. Tayari mmekwisha pita katika ile pazia.

Tumekuwa watu wa kipekee kwa kila mtu, hata katika nyadhifa zetu wenyewe, lakini tunajivunia, na kushukuru sana, kwa Ufunuo Ambao Yeye ametupa wa Neno Lake wa siku hii. Kuwa wapumbavu kwa ajili ya Kristo na Neno Lake lililodhihirishwa.

Tumeweka imani yetu pamoja na imani ya nabii Wake, nasi tumeungana pamoja, tukifanya UMOJA mkuu wa Mungu. Yeye Hawezi kitu bila sisi; sisi hatuwezi kufanya lolote bila nabii huyo; wala hatuwezi kufanya lolote bila Mungu. kwa hiyo sote pamoja, TUNAFANYA KITU KIMOJA, Ule Muungano; Mungu, nabii Wake, Bibi-arusi Wake. Tumekuwa Kipeo Chake.

Ilimchukua Yeye miaka elfu nne kutengeneza Kipeo Chake cha kwanza. Sasa, imemchukua Yeye miaka elfu mbili kutengeneza Kipeo Chake kingine, SISI, Bibi-arusi Wake, familia Yake kuu iliyo Kipeo, Adamu wa Pili na Hawa wa Pili. Sasa tuko tayari kwa ajili ya ile bustani, ule Utawala wa Miaka Elfu. Ametufinyanga tena na sasa tuko tayari.

Sisi ndiye Bibi-arusi Wake Neno Kamilifu, sehemu ya ule Uumbaji Wake ASILI. Ubua, kishada, na ganda, sasa vinakusanyika katika ile Mbegu, tayari kwa ufufuo, na tayari kwa mavuno. Alfa imekuwa Omega. Ile Mbegu iliyoingia ndani, imepitia hatua fulani na imekuwa Mbegu tena.

Ile mbegu iliyoanguka katika bustani ya Edeni kisha ikafa kule, ilirudi. kutoka kwa ile mbegu isiyo kamilifu iliyokufia kule, ikarudi ikawa Mbegu kamilifu, Adamu wa Pili.

Sisi sasa tumekuwa Adamu wa Pili, Bibi-arusi wa kweli, ile Mbegu, amerudi na Neno la asili tena. Na lazima tuwe na Neno lote kusudi tupate kuwa ile Mbegu. Hatupaswi kuwa na nusu ya Mbegu; hatuwezi kukua, lazima tuwe Mbegu nzima.

Kuna jambo moja tu lililosalia, mavuno yamefika. Tumeiva kabisa. Tuko tayari kwa kule Kuja. Ni wakati wa mavuno. Ile Mbegu imeirudia hali yake ya asili. Ile Familia ilio Kipeo imekuja tena, Kristo na Bibi-arusi Wake.

Ili kumtia moyo nabii Wake na Bibi-arusi Wake, Bwana alimpa malaika wake ono kuu. Alimpa kuonekana kimbele kwetu SISI, Bibi-arusi Wake. Tulipopita karibu naye, alisema, tulikuwa wanawake wadogo walio wazuri mno. Alisema sote tulikuwa tukimtazama, tulipokuwa tukipita.

Mwishoni, wengine walikuwa wametoka kwenye mstari, nao walikuwa wakijaribu wawezavyo kurudi mstarini. Kisha aliona kitu fulani muhimu sana, walikuwa wakiangalia mahali pengine, Hawakuwa wakimtazama Yeye. Walikuwa wakiliangalia hilo kanisa lililoingia katika machafuko. Jinsi gani ninavyojivunia na ninavyoshukuru kusema, sio SISI, Hao waliokuwa mbele, sisi hatukutoka nje ya hatua ama kuyaondoa macho yetu Kwake Yeye.

Kwa hiyo kile Kipeo na Mwana wa Mungu—Kipeo na Bibi-arusi, Naye ni sehemu Yake, ambayo ni lazima iwe kutimizwa kwa Neno. Neno limekwishatimizwa, nasi tuko tayari kwa kule Kuja kwa Bwana.

Tunayoshukrani jinsi gani kujua, sisi ndio ile Familia iliyo Vipeo Vyake, Bibi-arusi Wake wa kweli. Neno limekwishatimizwa, nasi tuko tayari kwa kule Kuja kwa Bwana.

Ninawaalika mje muungane nasi Jumapili hii saa 06:00 SITA MCHANA, saa za Jeffersonville, ( ni saa 2:00 MBILI USIKU ya Afrika Mashariki ) ili kusikia Neno pamoja nasi, na kuwa sehemu ya ile Familia iliyo Kipeo cha Mungu, tunapomsikia nabii akituletea Ujumbe: Kile Kipeo 64-0705.

Ndugu. Joseph Branham

Maandiko ya kusoma kabla ya ibada:

Isaya 53:1-12
Malaki 3:6
Mathayo 24:24
Marko 9:7
Yohana Mtakatifu 12:24 / 14:19