23-0101 Kumtendea Mungu Kazi Bila Mapenzi Yake

Ujume: 65-0718M Kumtendea Mungu Kazi Bila Mapenzi Yake

PDF

pakua – m4a

pakua – amr 12MB (use Firefox to download)

BranhamTabernacle.org

Mpendwa Bibi-arusi anayeelekea kwenye nchi ya Ahadi,

Je, ni kitu gani kinachoenda kutukia Mwaka huu Mpya?

Bibi-arusi amejiweka mwenyewe tayari kwa kukaa na Neno. Tumefanya Ushirika, tumeweka ile Ishara kwenye nyumba zetu, na kujitia muhuri wenyewe kwa Neno la kweli, lililothibitishwa. Hatujapatana, bali tumejiweka wenyewe mabikira kwa Sauti ya kweli ya Mungu.

Ni wakati wenye fahari vipi tunaoishi. Ni wakati ambao manabii wote walitamani kuuona; saa hii. Twajua kwa mambo ya asili kwamba Kanisa linajiweka tayari kuondoka. Saa za mwisho za kufunga zinawadia nasi tunafifia katika Umilele. Ni lazima tukae kwenye mstari na kuyaweka macho yetu kwenye Njia ya Mungu iliyoandaliwa kwa ajili ya wakati wetu: Neno Lake, nabii Wake, ambaye ndiye Neno la wakati wetu.

Alimletaje Kristo hapa? Kwa Neno la manabii. Sivyo? Angeleta Bibi-arusi Wake hapa jinsi gani? Kwa Neno la manabii.

Ifanyweje? Tutafanya nini? Alitueleza jambo litupasalo kufanya: tumtake shauri nabii, Biblia, ambapo hatuwezi kuongeza au kupunguza. Kama tukifanya hivyo, Mungu atatuondoa katika Kitabu cha Uzima.

Muda umeenda sana, ili sisi kuwa Bibi-arusi wake lnatubidi tuwe katika Mapenzi yake makamilifu . Hatutaki kamwe Kumtendea Mungu Kazi bila Mapenzi yake, haijalishi inasikika nzuri vipi. Mungu alifanya ahadi jinsi angetenda leo. Mungu amelinena papa hapa katika Neno Lake jinsi angelitenda.

Atachukuaje Bibi-arusi Wake? Kwa Neno, sio kwa gari jipya, si kwa wazo la mwanatheologia, lakini kulingana na Neno Lake atamtambulisha. Usiweke kitu kimoja katika hilo au kuondoa kitu kimoja toka hilo sasa. Liache jinsi lilivyo. Unaona?

Kwa watu wengine, inaweza kuwachanganya sana kwani kuna manabii wengi wapakwa mafuta wasemao kuwa Mapenzi ya Bwana ya wakati huu ni yapi. Wanasema: “Ni makosa kucheza kanda kanisani, Ndugu Branham hakuwahi kamwe kusema jambo hilo. Wahudumu ndilo jambo lililo muhimu zaidi kwa sasa , na ndio njia iliyoandaliwa na Mungu kwa wakati huu. Kaa na mchungaji wako.”

Kwa hiyo, je, ni sawa kusikiliza kanda, lakini si kanisani? Je, Hatupaswi kuamini kila Neno lililo kwenye kanda, ila yale tu Roho Mtakatifu atuambiayo kipi ni Neno na kipi si Neno? Je, Kuwasikiliza wahudumu ndiko kutamkamilisha Bibi-arusi? Nisipokaa na mchungaji wangu siwezi kuwa Bibi-arusi? Je, Kama nikicheza tu kanda, niko nje ya Mapenzi makamilifu ya Mungu?

Kila mwamini anataka kufanya yaliyo sahihi na kuwa katika Mapenzi makamilifu ya Mungu. Hakuna anayetaka kuwa makosani au kuwa katika Mapenzi Yake yakuruhusia. Lazima kuwe na njia iliyo sahihi na ya kweli.

Ni wahudumu gani tunaopaswa kuwasikiliza…je, ni wote? Je! yatubidi kuchunguza yale wanayosema ikiwa ni Neno tunaporudi nyumbani kwa kusikiliza kanda, au tunapaswa tu kuchukua neno lao kwa jambo hilo? Yakini ni nini basi, je, ni neno la mchungaji wetu, ama ni yale Ndugu Branham aliyosema kwenye kanda?

Wanapaswa kuhubiri Neno, amina. Wanapaswa kuweka Neno mbele ya watu, amina. Lakini hawapaswi kuchukua mahali pa nabii wa Mungu. Wao si muhimu zaidi kuliko Sauti ya Mungu iliyothibitishwa. Wanaweza TU KUSEMA YALIYO KWENYE KANDA. Hiyo ndiyo Yakini ya Bibi-arusi.

Lazima zako tano ndizo hizo. Lazima iwe hivyo; wakati Wake; majira Yake wakati aliposema itakuwa; na mtu yule aliyemchagua, na lazima ije kwa nabii; na nabii yule lazima awe nabii aliyethibitishwa.

Mimi Sijaribu kushutumu Wahudumu ama kusema hawana mahali, Mungu apishe mbali. Ninasema tu, kuwachezea watu Sauti ya Mungu iliyo kwenye kanda ndilo jambo lililo muhimu sana ambalo wahudumu wanalopaswa kufanya. Chochote ninachosema, au mhudumu anachosema, au hata mshirika wakanisa anachosema, lazima yawe neno kwa neno yale nabii wa Mungu aliyosema.

Ninachukia kwamba unanikasirikia na unafikiri ninapingana na mchungaji wako, hilo silo lililo moyoni mwangu. Mimi Ninataka tu Bibi-arusi aungane pamoja kwa kitu KIMOJA PEKEE tunachoweza kuungana kwacho, UJUMBE HUU.

Katika wakati wa migawanyiko kama huu, mkanganyiko, tofauti kati ya watu, ninaamini Ujumbe huu tunaokwenda kuusikia Jumapili ni mojawapo ya Jumbe zilizo muhimu sana kwa wakati wetu.

Hebu na tufungue mioyo yetu na tuone kile Mungu analosema kwa kanisa, kwa watu wanaosikiliza kanda, na watu waliounganishwa kwa redio wanaosikiliza katika mataifa yote.

Kabla hatujaingia katika Nchi ya ahadi, kuna jambo tunalopaswa kufanya. Sauti ya Mungu inatutaka tusikilize kwa makini sana na tusikose kuelewa anachosema.

Alisema kama vile tu wakati Musa alipokuwa akizungumza na Israeli, baada ya yeye kuthibitishwa na Mungu na ile Nguzo ya Moto, na kujua alithibitishwa kuwa mtumishi wa Mungu kuwaongoza watoke . Lakini kabla hawajaenda katika nchi ile, aliwaambia: “ Naita mbingu na nchi kushuhudia dhidi yenu. Msiongeze kitu moja kwa yale niliyosema au kuondoa neno moja toka kwake.”

Nasema vivyo hivyo katika Jina la Yesu Kristo. Usiongeze kitu. Usiondoe—kuliwekea mawazo yako. Wewe sema tu yaliyosemwa katika kanda hizo. Tenda sawasawa kabisa na vile Bwana Mungu amekuamuru kutenda. Usiongezee Kwake.

Huyo ni BWANA MUNGU wetu akituamuru kwamba tunaweza KUSEMA TU YALIYOSEMWA KATIKA KANDA. Hatuwezi kuongezea kwake, kuondoa, kuweka mawazo yetu, fikira zetu, au fasiri yetu kwake. Sema tu yaliyosemwa katika kanda.

Ikiwa unaamini maneno haya yaliyonenwa na nabii wa Mungu aliyethibitishwa kuwa ni kweli, basi kwa nini KUBONYEZA PLAY kusiwe ndilo jambo lililo muhimu zaidi ambalo Bibi-arusi analoweza kufanya?

Alimtambulishaje alipokuja? Kwa mtu aliyekuwa na roho ya Eliya juu yake akitokea jangwani. Atamtambulishaje Bibi-arusi Wake? Aliahidi katika Malaki 4 kitu kile kile kabla ya kuiharibu dunia kama ilivyokuwa katika siku za Sodoma.

Mpendwa Bibi-arusi wa nchi ya Ahadi, unao UFUNUO wa kweli. Uko katika Mapenzi Makamilifu ya Mungu. Umejitambua wewe ni nani. Uko katika Mpango wa Mungu kwa Kubonyeza Play. Wewe ni Neno. Wewe ni sehemu ya Bwana arusi. UTUKUFU!!!

Ni njia gani ya kuanza Mwaka Mpya. Bibi-arusi waliungana pamoja, wakifuata amri ya Mungu kwa, Kubonyeza Play .

Njoo ujiweke Mwenyewe tayari kwa Unyakuo pamoja nasi Jumapili saa 6:00 SITA MCHANA , saa za Jeffersonville,( ni Saa 2:00 MBILI USIKU ya Tanzania na Kenya pia ) tunaposikia: 65-0718M ” Kumtendea Mungu Kazi Bila Mapenzi Yake .”

Ndugu. Joseph Branham

Maandiko ya Kusoma kabla ya Kusikiliza Ujumbe :

Kumbukumbu la Torati 4:1-4 / 4:25-26
1 Mambo ya Nyakati 13
1 Mambo ya Nyakati 15:15
Zaburi 22
Marko 7:7
Yoeli 2:28
Amosi 3:7
Malaki 3
Mathayo 11:1-15
1 Wakorintho 13:1