22-1231 Lile Shindano & Ushirika

Ujume: 62-1231 Lile Shindano

PDF

pakua – m4a

pakua – amr 13MB (use Firefox to download)

BranhamTabernacle.org

Wapendwa kundi wenyeji,

Ningependa tuwe na Ushirika kwa mara nyingine tena katika nyumba zetu katika Mkesha wa Mwaka Mpya, tarehe 31 Desemba. Maelekezo ya jinsi ya kupata divai, na jinsi ya kuoka mkate wa ushirika yanaweza kupatikana katika anuani zilizo hapa chini. Anuani yakupakua Sauti ya Ibada itapatikana hivi karibuni kwenye tovuti yetu. Au, unaweza kucheza sauti ya ibada kutoka kwenye programu ya Lifeline.

Kwa wenyeji katika eneo la Jeffersonville, mnaweza kutwaa divai ya Ushirika Ijumaa, tarehe 30 Desemba, kati ya saa 7:00 saba mchana – saa 10:00 kumi jioni, chini ya dari la VGR.

Tutasikiliza 62-1231 Lile Shindano , kuanzia Saa 11:00 Kumi na moja jioni, Majira ya Mashariki ya Kati ( ambayo ni saa Saba Usiku ya Tanzania) siku ya Jumamosi, tarehe 31 Desemba . Baada ya Ndugu Branham kuleta Ujumbe wa Mkesha wa Mwaka Mpya, tutasimamisha kanda na kuwa na takriban dakika 10 za Nyimbo za Kuabudu tunapojiandaa kwa ajili ya Meza ya Bwana. Kisha tutabonyeza kuendeleza tena kanda hiyo mahali ambapo Ndugu Branham anaanzisha ibada ya Ushirika. Kwenye kanda hii, anaacha sehemu ya ibada ya kutawadhana miguu, ambayo nasi tutazingatia hilo pia ( Hatutatawadhana miguu pia) .

Tunapogeukia mwaka mwingine katika Huduma Yake, hebu na tuyaweke wakfu maisha yetu upya Kwake kwa kulisikiliza Neno kwanza, na kisha kushiriki Meza Yake. Ni nafasi nzuri jinsi gani tuliyo nayo kwa mara nyingine tena ya kufanya nyumba zetu kuwa mahali Patakatifu ili kumkaribisha Mfalme wa Wafalme aje kujumuika nasi.

Mungu awabariki,

Ndugu Joseph