The Seventy Weeks of Daniel Series banner

26-1129 Sababu Sita Za Kusudi La Gabrieli Kumzuru Danieli

UJUMBE: 61-0730E Sababu Sita Za Kusudi La Gabrieli Kumzuru Danieli

PDF

BranhamTabernacle.org

Mpendwa Unayependwa Sana,

Kuna mambo mengi makubwa yanayotendeka na yaliyo mbele yetu. Mungu analifunua Neno Lake na kulitimiza kila siku. Tunagundua ni lini tutapanda juu, nasi tunajitayarisha. Tumeelekeza nyuso zetu kwa Mungu kupitia maombi na dua, naye anatufunulia saa tunayoishi. Wakati umekwisha; Yeye anakuja kutuchukua, Bibi-arusi Wake Anayependwa Sana.

Bali kwanza, Mungu anapiga kelele kupitia malaika Wake kuwaonya watu Wake kwamba yawapasa wamsikie Yeye. “BWANA ASEMA HIVI, Mungu hatalishughulikia Kanisa Lake hadi lirudi katika nchi ya uenyeji wao, Ujumbe wa wakati huu. Rudini kwenye la asili!”

Ninapenda tu jambo hilo. Wakati ninapoweza kumsikia nabii akisimama akiwa na BWANA MUNGU ASEMA HIVI, ndugu, ndivyo ilivyo. Kwangu mimi, hilo linatosha. Ni hayo tu.

Loo, jinsi gani tunavyolipenda hilo pia. Linatosha kwetu sisi. Tunafanya vile hasa Yeye alivyotufundisha kufanya. Kwa kweli, hatujawahi kamwe kuliacha Neno Lake la asili, tumedumu na SAUTI YA MUNGU ILIYO KWENYE KANDA, kwani ni BWANA ASEMA HIVI!!

Huenda tusiweze kuyaelewa yote yanayonenwa na kufunuliwa kwetu, bali tunajua jambo moja, tunaamini kila Neno lililo kwenye kanda. Hicho ndicho kipimo cha kweli cha kujua wewe ni Bibi-arusi Wake.

Sisi ndio lile kundi la watu wale ambao nabii aliowaona Ng’ambo ya Pazia la Wakati.

Zilikuwa ni sauti zetu zilizopiga kelele, “Tunategemea kila Neno ulilonena.”

Tunangojea kwa hamu na kuomba huku macho yetu yakielekezwa Mbinguni, tukikutazamia Kuja Kwake.

Kama vile Danieli, Yeye ameyasikia maombi yetu na ameshuka kufunua kile alichokikusudia kwa Wayahudi na Yerusalemu, hata mwisho wa yote; jambo hilo lote. Yeye alimwambia Danieli, “Yafunge Maneno haya na ukakitie muhuri Kitabu hata wakati wa mwisho.”

Hiyo siku ya mwisho ni sasa. Tumewasili. Sisi ndio Bibi-arusi Wake Anayependwa Sana ambaye Yeye amekuwa akimsubiri. Ni Wakati wa Kanisa la mwisho. Ujumbe na mjumbe ni Mmoja nao wanafunua MAMBO YOTE. Ule ufunuo wa kweli wa Yesu Kristo, uliotiwa muhuri hadi wakati huu, SASA UMEFUNULIWA.

Si Nafsi ya tatu, si Nafsi ya pili, si Nafsi ya tatu, lakini ni ile Nafsi ya Mungu. Siri hizi nyingine zote za Mungu zitafunuliwa, kwa sababu zimeandikwa hapa katika kitabu Hiki, na kufunuliwa kwa kizazi cha wakati wa mwisho.

Neno la Mungu linafunuliwa kuliko wakati wowote ule ili kuliweka Kanisa katika utaratibu kwa ajili ya Unyakuo na kwenda Nyumbani!! Kanisa halina budi LIRUDI KWENYE KANDA. Rudini kwenye nchi ya uenyeji, mwanzoni. RUDINI KWENYE UJUMBE WA WAKATI HUU, RUDINI KWENYE SAUTI YA ASILI ILIYOWAITA. RUDINI KWENYE BWANA ASEMA HIVI.

Jumapili hii, mwambie mchungaji wako, “Hebu na tuisikie Sauti ya Mungu ya asili leo. Ndio Sauti ambayo Mungu aliyoichagua kunenea Mwenyewe. Ndio Sauti ambayo itakayotutambulisha kwa Bwana Yesu wakati atakapokuja. Ndio Sauti pekee ambayo Mungu Mwenyewe alisema, Mimi ni Sauti ya Mungu Kwenu.”

Hakuwezi kuwa na Sauti KUU KULIKO Sauti hiyo. Sauti ambayo sote tunaweza kusema AMINA kwayo kwa kila Neno.

Karibu uungane na sehemu ya Bibi-arusi ulimwenguni kote wakati Mungu anaponena na kuufunua wakati wenyewe hasa wa Kuja Kwake. Utakuwa upako ulio mkuu kuliko uliopata kusikia.

Tutakusanyika saa 06:00 MCHANA, masaa ya Jeffersonville, kusikia: 61-0730E – “Sababu Sita Za Kusudi La Gabrieli Kumzuru Danieli”

Ndugu Joseph Branham