26-1018 Kiongozi

Ujumbe: 62-1014E Kiongozi

PDF

BranhamTabernacle.org

Mpendwa Kituo Cha Nguvu,

Mungu aliahidi kumtumia Bibi-arusi Wake kiongozi katika siku hizi za mwisho ili Yeye aweze kujifunua Mwenyewe katika mwili, kama vile alivyofanya wakati alipokuja duniani katika Mwanawe, Yesu. Alituambia katika Neno Lake kwamba Yeye angemtuma Eliya nabii, ambaye angekuwa Mwana wa Adamu akijifunua Mwenyewe katika mwili wa kibinadamu; kwa maana Yeye angali bado anayo mambo mengi ya kunena na kutufundisha.

Kwa maana hatanena kwa shauri lake mwenyewe, lakini yote atakayoyasikia atayanena, na mambo yajayo atawapasha habari yake. Yeye atanitukuza mimi; kwa kuwa atatwaa katika yaliyo yangu na kuwapasha habari.

Yeye alimtuma William Marrion Branham kulitimiza Neno Lake na kutujenga sisi kama watu binafsi kuwa Kimo cha Yesu Kristo; mtu mkamilifu ambaye angeweza kumshinda kila adui, na ambaye angekuwa kituo cha nguvu na makao ya Roho Mtakatifu kuishi ndani yake.

Mungu daima hajawahi kamwe kushindwa kuwatumia watu Wake kiongozi. Bali ili uwe Bibi-arusi Wake, huna budi kumkubali kiongozi huyo. Huna budi kuamini jambo hilo. Huna budi kupitia njia anayosema la sivyo utapotea. Haidhuru tunafikiri nini, yale yanayoonekana ni ya maana, ama yanayoonekana ya kipuuzi, hatuwezi kupambanua jambo hilo, kiongozi ndiye tu anayeweza.

Unasema, Ndugu Joseph, huyo ni Roho Mtakatifu wa kutuongoza, si Ndugu Branham. Maneno aliyosema NI Roho Mtakatifu na si Ndugu Branham; bali yeye ndiye aliyechaguliwa na Mungu kumfunua Roho Mtakatifu ndani yake, na kuwa kiongozi wetu wa duniani.

Na sasa Mungu daima amewatuma viongozi Wake, Yeye daima hajakosa kuwa na kiongozi, katika nyakati zote. Mungu daima amekuwa na mtu fulani aliyemwakilisha katika dunia hii, katika nyakati zote.

Tunapaswa kumtambua ni nani huyo kiongozi wa duniani anayemwakilisha Yeye hapa duniani; hapo ndipo ulipo Ufunuo wa kweli wa Neno Lake.

Tunajua Roho Mtakatifu ndiye Kiongozi Mkuu ambaye Baba alimtuma kumwongoza Bibi-arusi Wake, lakini hapa Mungu alisema kwamba daima Yeye humtuma mtu kuwa kiongozi wa kumwakilisha Yeye Mwenyewe na kumwongoza Bibi-arusi Wake.

Kiongozi wetu alituambia kwamba Kornelio alikuwa mtu mashuhuri na mheshimiwa aliyejenga makanisa. Alitoa sadaka na aliomba kila siku. Bali wakati Roho Mtakatifu alipokuja, alihitaji Kiongozi.

Mungu alimtumia Roho Mtakatifu. Alimtuma katika utu wa Petro, “Bali Petro alipokuwa anasema Maneno haya, Roho Mtakatifu akamshukia.” Mungu alimtumia Kiongozi kupitia kwa Petro. Alimtumia, kwa sababu Yeye alimwongoza Kornelio kwenye njia sahihi.

Wakati petro alipokuwa angali akinena, Roho Mtakatifu akawashukia hao. Petro akasema,

“Mtu anaweza kukataza maji, kwamba watu hawa wasibatizwe?” Mnaona, Kiongozi angali anazungumza, si Petro.

Sisi hatuongozwi na mtu; tunaongozwa na Roho Mtakatifu, ANAYENENA KUPITIA MTU HUYO MUNGU ALIYECHAGUA KUWA KIONGOZI WETU WA DUNIANI.

Roho Mtakatifu akizungumza kupitia malaika-kiongozi Wake daima atanena Neno. Yeye alituambia, “Nina mambo mengi ya kuwaambia. Hamwezi kuelewa na jambo Hilo sasa, bali Yeye ajapo, atawaongoza kwenye Hilo.”

Yohana aliongozwa alipoandika Ufunuo. Aliongozwa na yule Kiongozi. Pia aliongozwa na yule Kiongozi kusema, “Mtu yeyote atakayeondoa Neno moja kutoka Kwake, ama kuongeza neno moja Kwake, yeye ataondolewa, sehemu yake, kutoka katika Kitabu cha Uzima.”

Roho Mtakatifu pia alimwongoza Ndugu Branham kusema tunapaswa kusema tu kile kilicho kwenye kanda; tusiongeze kwake au kuondoa. Na Yeye ameiandaa njia tunayoweza kufanya kile hasa yeye alichotuagiza kuwa ni lazima tukifanye, Bonyeza Play.

Naam, utabadilishaje kitu fulani kwa Neno la Mungu, na bado useme unaongozwa na Roho Mtakatifu?

Tunaongozwa na Roho Mtakatifu ambaye ametupa Ufunuo wa Yeye ni nani, ni yupi Yeye aliyemtuma kama kiongozi Wake wa duniani kumwita Bibi-arusi Wake atoke, na sasa lile jiwe la kifuniko: Ufunuo wa sisi ni nani. Yapita maneno ya kibinadamu kupata kuelezea.

Tazama kile Yeye alichotutendea, katika wiki hizi chache zilizopita. Alitufundisha jinsi gani ya kumshinda kila adui anayekuja mbele yetu; jinsi ya kuuchomoa Upanga wetu wa IMANI na kumpiga hadi kufa. Hatuna cha kuogopa. Hakuna kinachoweza kusimama mbele yetu.

Jinsi gani Yeye alivyokihifadhi Chakula kwa ajili ya Bibi-arusi Wake apate kula. Hata wakati mjumbe Wake yuko mbali, bado tungali tunaye Kiongozi ambaye ulimwengu haujui lolote kumhusu; bali kwa Bibi-arusi Wake, Ni Chakula cha Kiroho kwa Wakati Wake, Mana Iliyofichwa tunayoila siku kwa siku.

Ametujenga kufikia vimo vya watu wakamilifu ili Yeye aweze kuishi na kukaa ndani ya kila mmoja wetu. Alitutumia Roho Wake Mtakatifu na kujifunua Mwenyewe katika mwili, kama alivyofanya miaka 2000 iliyopita, kuwa Kiongozi wetu, akiishi na kunena kupitia kiongozi Wake wa duniani.

Ninawaalika kila mmoja wenu mje na muisikie, “Honk-honk, honk-honk!” Yake, ambapo Bibi-arusi watakuja moja kwa moja kwenye Honk hiyo. Yeye atafanya, “Honk-honk, honk-honk!” nako kutakuwa na yubile ya aina yake ulimwenguni kote. Kwa nini? Bibi-arusi wanaijua Sauti ya Kiongozi wao.

Ikiwa hutaki kupotea, njoo umsikilize Kiongozi wetu anenapo kupitia kiongozi Wake wa duniani Yeye aliyemteua Jumapili hii saa 06:00 MCHANA, masaa ya Jeffersonville.

Ndugu. Joseph Branham

Ujumbe:
62-1014E —Kiongozi

Maandiko:
Marko Mt.16:15-18
Yohana Mt.1:1 / 16:7-15
Matendo 2:38
Waefeso 4:11-13 / 4:30
Waebrania 4:12
2 Petro 1:21
Kutoka 13:21