Ujumbe: 62-1014M Kimo Cha Mtu Mkamilifu
- 26-1011 Kimo Cha Mtu Mkamilifu
- 25-0601 Kimo Cha Mtu Mkamilifu
- 20-1004 Kimo Cha Mtu Mkamilifu
- 18-1125 Kimo Cha Mtu Mkamilifu
- 16-1023 Kimo Cha Mtu Mkamilifu – Preliminari
Mpendwa Kimo cha Mtu Mkamilifu,
Ni mafunzo jinsi gani ambayo tumekuwa nayo. Sauti ya Mungu imekuwa ikinena na kutufundisha, Neno kwa Neno kwa Neno, jinsi ya kumshinda kabisa kila adui. Yeye ametufunulia na kutia nanga mioyoni mwetu, SISI NI NENO. Kwa hivyo, hatuwezi kushindwa.
Wakati adui anapotufuatia, sisi tunampiga tu na kumpiga tena na tena kwa bomu letu la atomiki, Neno Lililonenwa la Mungu, ambalo huishi na kukaa ndani yetu.
Kweli, vita viko tayari, bali sasa hatuna hofu tena; hakuna wasiwasi tena. Hatuzisikilizi dhamiri zetu. Hatuzisikilizi kumbukumbu zetu. Hatuyasikilizi matakwa yetu. Tumezifunga akili zetu kwa mambo haya na kuweka Roho wa Neno Lake mioyoni na rohoni mwetu. Tumekilipua kila kitu kilicho kinyume na Neno Lake.
Kila shaka imetoweka. Kila hofu imetoweka. Kila hisi ya shaka imetoweka. Kila hisi imetoweka. Hakuna kitu kinachosimama hapo ila Neno la Mungu linaloishi na kukaa NDANI YETU, naye Shetani hawezi kupigana na Hilo.
Tunafanyika Maskani iliyo hai ya Mungu aliye hai. Ni Mungu akiishi ndani yetu, akitufanya tufanane na Yeye, akiuakisi Utu Wake ndani yetu.
Tunapachukua mahali pa Kristo, tukiiendeleza huduma Yake. Yeye anaishi katika umbo la mwanadamu kama Yeye anavyojiakisi ndani yetu. Sasa tunayo ibada kamilifu pamoja Naye! Ni Mungu akijidhihirisha ndani yetu, tukiwa Maskani Yake.
Ni upi msingi wetu usiotikisika wa kuyaamini mambo haya? IMANI. Nayo imani yetu haihitaji chochote; kwa maana imani yetu inaliamini Neno la Mungu. Kwa maana imani huja kwa kusikia, na kusikia Neno la Mungu, nalo Neno la Mungu huja kwa nabii peke yake, na tunaweza tu KUMSIKIA nabii kwa Kubonyeza Play…PIGA!!
Kwa kuisikiliza Sauti Yake, tumwekwa kwa mrija Wake wa kutilia Nguvu Zake nasi tumekufa kwa mawazo yetu wenyewe. Imani yetu imekuwa imani halisi, nao Uhai Wake umewekwa ndani yetu. Tumekuwa viumbe hai vya Mungu, makao ambapo Roho Mtakatifu anaweza kutuma miali ya baraka Zake za upendo kupitia humo.
Sauti hiyo iloyo kwenye kanda inafanya nini?
Kristo alinituma kuwajenga watu binafsi wafikie kiwango cha Yesu Kristo, kusudi wapate kuwa kituo cha nguvu na makao ya Roho Mtakatifu, kwa Neno Lake. Kwa Neno Lake, unaona, kumjenga mtu binafsi afikie mahali hapo.
Kwa kuisikia Sauti Yake, na kuamini na kulifuata Neno Lake, imetujenga kufikia vimo vya Yesu Kristo; makao ya Roho Wake. Sisi ni nguvu hai, maarifa hai, saburi hai, utauwa hai, Nguvu iliyo hai, zitokazo kwa Mungu aliye hai, zinatufanya kuwa mtu aliye hai, sanamu hai, katika kimo cha Mungu.
Lakini Mwili uliniwekea tayari,” Mwili ambao Mungu anaweza kuishi ndani yake, Mungu anaweza kutembelea, Mungu anaweza kuona nao, Mungu anaweza kuzungumza humo, Mungu anaweza kufanya nao kazi. Amina! Chombo kilicho hai, Mungu, Mungu akitembea kwa miguu miwili, ndani yako. Utukufu! “Hatua za mwenye haki huongozwa na Mungu,” Mungu akitembea ndani yako. “Kwa maana ninyi ni waraka uliandikwa, unaosomwa na watu wote.”
Utukufu…!!! Kwa hivyo, hatujali kama tunaishi katika hema au kibanda, tuishi ama tufe, tuzame au tufe maji. Jambo hili ndilo tu tunalotaka, UJUMBE HUU, SAUTI HII, NENO LA MUNGU. Ndio Ufalme wa Mungu. Ndio njia ya Mungu iliyoandaliwa ya siku hii. Inajenga Kimo cha Mtu Mkamilifu, ambaye NDIYE SISI!
Hebu na tukutanike pamoja na kuyachunguza maisha yetu tunapomsikia Mwalimu wetu akitufundisha kile tunachopaswa kufanya, na jinsi gani tunavyopaswa kuishi, ili kufanyika wana na binti za Mungu W-A-K-A-M-I-L-I-F-U
Tutamwahidi Bwana kwamba kwa msaada Wake na kwa neema Yake, tutamwomba na kumtafuta Yeye kila siku bila kukoma, mpaka tutakapojisikia kila moja ya mahitaji Yake yanatiririka katika miili yetu. Tutakaa hapo mpaka tuweze kuwa dhihirisho la Kristo aliye hai.
Kila wiki msisimko na matarajio kwa yale Bwana atakayofanya na kutufunulia sisi yapita maneno kuelezea. Jinsi gani ninavyotaka ulimwengu mzima uungane nasi kwani hakuna kitu kilicho kuu zaidi, au kikamilifu zaidi kuliko kukaa katika uwepo wa Sauti ya Mungu na kuwa Kimo Kikamilifu cha Bibi-arusi Neno Wake Mkamilifu.
Ndugu Joseph Branham
Ujumbe: Kimo cha Mtu Mkamilifu 62-1014M
Muda: saa 6:00 MCHANA Masaa ya Jeffersonville, IN.
Maandiko:
Mathayo Mtakatifu 5:48
Luka Mtakatifu 6:19
Yohana Mtakatifu 1:1 / 3:3 / 3:16 / 5:14 / 14:12
Matendo 2:38 / 7:44–49 / Sura ya 10 / 19:11 / 28:19
Waefeso 4:11-13
Wakolosai Sura ya 3
Waebrania 10:5 / 11:1 / 11:32-40
Yakobo 5:14
2 Petro Mtakatifu 1:1-7
Isaya 28:19