22-0410 Kiongozi

Ujume: 62-1014e Kiongozi

PDF

pakua

BranhamTabernacle.org

Wapendwa Wana-Kondoo Wanaoongozwa,

Vita vya mwisho vimekaribia. Tunaenda mahali ambapo hatujawahi kufika hapo awali. Tunapita katika nyika, nasi tumo njiani kuelekea mahali fulani, nasi hatuwezi kuendelea bila Kiongozi. Msiwe na wasiwasi enyi kundi dogo, Mungu ametoa Kiongozi wa kutuongoza.

Kiongozi huyu atatufunulia mambo, naye atatuambia mambo aliyosikia; Anaweza kurudia maneno yetu moja kwa moja na kusema tuliyosema. Hatuna budi kumfuata Kiongozi huyu, kwa maana Yeye ndiye peke Yake ajuaye njia.

Wakati Yesu alipokuwa duniani, aliwaambia wanafunzi wake kwamba alikuwa na mambo mengi zaidi ya kusema na kutufunulia, hivyo angetutumia huyo Roho wa kweli, naye atatuongoza atutie kwenye kweli hizi zote. Yeye Alisema Bibi-arusi Wake angemtambua kwa kuwa angejifunua na kujithibitisha Mwenyewe kama tu alivyofanya alipokuja katika mwili mara ya kwanza.

Atajua kila wazo lililo moyoni mwetu. Atatujua sisi ni nani na tumefanya nini. Atajua kila kitu kutuhusu sisi. Yeye ni Kiongozi wa Mungu, Roho Mtakatifu akiishi na kujidhihirisha Mwenyewe katika mwili wa mwanadamu.

Kama vile Yesu Mwenyewe alivyosema, “ Si Mimi nizifanyaye zile kazi; ni Baba Yangu anayekaa ndani Yangu. Amini nawaambieni, Mwana hawezi kufanya neno kwa nafsi Yake Mwenyewe; bali lile analomwona Baba akifanya, ndilo analofanya Mwana vile vile. Baba anafanya kazi, Nami ninafanya kazi vile vile .”

Vivyo hivyo malaika wake hatanena kwa shauri lake mwenyewe, Lakini yote atakayoyasikia atayanena. Atatwaa haya yote kutoka kwa Baba, na ndipo atatupasha Habari . Atafunua siri zote zilizofichwa katika Neno.

Baba alituambia ya kwamba angekuwa na MTU ambaye angemwakilisha yeye hapa duniani, Kiongozi, na kwamba Bibi-arusi Wake atamtambua waziwazi na kumfuata .

Yeye atamtukuza Mungu tu. Yeye atasema waziwazi, Si yeye, yule malaika wa saba, ni kudhihirishwa kwa Mwana wa Adamu. Ni siri ya Mungu iliyofunuliwa. Si mwanadamu, ni Mungu. Yeye si Mwana wa Adamu; yeye ni mjumbe kutoka kwa Mwana wa Adamu. Mwana wa Adamu ni Kristo, Yeye Ndiye tunayejilisha.

Wengi watasema wao ndio waliotiwa mafuta ili kumwongoza Bibi-arusi, lakini Mungu hataki utegemee Akili zako mwenyewe ama mawazo yako mwenyewe , wala mawazo yoyote yaliyotungwa na mwanadamu. Mungu hutuma Kiongozi, naye Mungu anataka mkumbuke ya kwamba huyo ni Kiongozi Wake aliyemchagua.

Kiongozi wetu hatampeleka mmoja huku na mwingine kule na kusema: yakubidi umsikilize mhubiri huyu, kisha yakubidi umsikilize mhubiri yule;
Wao hata hawakubaliani wao kwa wao. Hilo linawezaje kukukamilisha?

Kuna NENO MOJA Tu LILILOKAMILIFU litakalotukusanya na kutuweka pamoja, NENO LA SAUTI YAKE ILIYOTHIBITISHWA KIKAMILIFU KWENYE KANDA .

Wao Wanasema leo hii Roho Mtakatifu anamuongoza kila mmoja wetu kama mtu binafsi, ambalo ni kweli. Basi kwa nini uwe na mhubiri ikiwa Roho Mtakatifu anakuongoza? Jisikilize mwenyewe: Ni afadhali niwe na mhubiri aniongoze na anifundishe badala ya nabii aliyethibitishwa wa Mungu? Afadhali nipate fasiri yake ya Neno kuliko kulisikia moja kwa moja kutoka kwa Sauti ya Mungu Mwenyewe jinsi yeye anavyoweza kulifafanua vizuri zaidi?

Mimi Sijaribu kushutumu hizo huduma, au kusema ni za uwongo, au kwamba hupaswi kuzisikiliza hizo huduma. Tafadhali nisamehe ikiwa silitamki ipasavyo . Ninasema tu haziwezi kuwa Mkataa wako, neno la mwisho, Kiongozi wako. Watu hawawezi kukubaliana kamwe. Kila mtu ana wazo tofauti, uongozi tofauti. Hilo linawezaje kumkamilisha Bibi-arusi? Ikiwa unawasikiliza wote, na kujua wote hawawezi kukubaliana na kile wao wanachosema kuwa ni Neno kamilifu la Mungu, hilo linawezaje kumkamilisha Bibi-arusi? Je, hilo Linawezaje kuwa kiongozi wako?

Na kama tutamwacha tu Roho Mtakatifu atuweke pamoja na Neno Lake, ni kwamba Wote tutakuwa na moyo mmoja, nia moja, na katika umoja, kwa Roho mmoja; Roho Mtakatifu, Kiongozi wa Mungu atakayetuongoza atutie kwenye Kweli yote. Lakini hunabudi kumfuata Kiongozi wako.

Usishindane kamwe na Neno la Kiongozi wako. Mfuate Yeye. Kama humfuati, utapotea. Pia, kumbuka, unapomwacha, uko peke yako, kwa hiyo tunataka kuwa karibu na yule Kiongozi.

Roho Mtakatifu anatuongoza kumfuata Kiongozi wake, ambaye ni Roho Mtakatifu anayenena kupitia Malaika-Mjumbe wake wa saba . Si Neno la mwanadamu, Ni Sauti ya Mungu kwa Bibi-arusi Wake na NDILO JAMBO PEKEE LINALOWEZA KUMKAMILISHA BIBI-ARUSI .

Njoo tuwe pamoja Jumapili saa 6:00 Sita MCHANA , saa za Jeffersonville, (Ni saa 1:00 Jioni ya Tanzania), tunapoianza wiki yetu ya Pasaka kumsikiliza Kiongozi wetu. Anaenda kutuongoza mahali ambapo hatujawahi kamwe kufika hapo awali.

62-1014E Kiongozi

Ndugu. Joseph Branham

Maandiko ya kusoma kabla ya ibada:

Marko Mtakatifu 16:15-18

Yohana Mtakatifu 1:1 / 16:7-15

Matendo 2:38

Waefeso 4:11-13 / 4:30

Waebrania 4:12

2 Petro 1:21

Kutoka 13:21