22-0403 Kimulimuli Chekundu Cha Dalili Ya Kuja Kwake

Ujume: 63-0623E Kimulimuli Chekundu Cha Dalili Ya Kuja Kwake

PDF

pakua

BranhamTabernacle.org

Sisi Wote ndani,

Utukufu kwa Mungu, ni siku ilioje tunayoishi. Tunasikiliza Ujumbe ambao umethibitishwa, kwa kila tendo, kuwa ni Yesu Kristo yeye yule jana, leo, na hata milele. Umefanya mambo yale yale aliyofanya alipokuwa hapa duniani; aliponya wagonjwa, alijua mawazo ya nia, akaonyesha mambo ambayo yangetukia, Aliwafufua wafu, na kila wakati, imekuwa kamilifu.

Maji yameosha udongo wote kutoka juu ya kilele kwenye mlima. Hakukuwa na kitu kilichobaki isipokuwa Mwamba. Kulikuwa na Maandishi ya Ajabu juu ya Mwamba, kwa hiyo Mungu akatutumia nabii wake mwenye nguvu ili kufasiri hayo Maandishi kwa Bibi-arusi Wake. Sasa Biblia imefasiriwa kikamilifu kabisa.

Akampeleka malaika wake mwenye nguvu juu ya mlima na akaweka UPANGA WA BWANA MKONONI MWAKE. Kisha malaika wake akakata kilele cha mlima ule na kukiinua juu. Ndani yake kulikuwa na mwamba mweupe, kitu kama namna ya jiwe gumu jeupe ambalo hata halikuwa limeandikwa.

Yeye Alituambia tuangalie Huu wakati alipokwenda Magharibi. Kisha alitwaliwa katikati ya Malaika Saba na akarudi na kutufunulia YOTE YALE HATA HAYAKUWA YAMEANDIKWA NDANI YA MWAMBA.

“ Huyu ni mtumishi Wangu. Nami nimemwita kuwa nabii kwa wakati huu, kuwaongoza watu kama tu Musa alivyofanya. Naye amepewa mamlaka, angeweza kunena kitu kiwepo.” Au kitu kama hicho, kama Musa alivyofanya, kama kunena watokee inzi. Nasi tunajua kuhusu wale kindi, na kadhalika, na mambo ambayo tayari yamekwisha kutukia. Maskini Hattie Wright nyuma kule, nadhani mnajua lililotukia kule nyumbani .

W-I-L-L-I-A-M M-A-R-R-I-O-N B-R-A-N-H-A-M ndiye mtu ambaye Mungu Amemchagua kumwongoza Bibi-arusi Wake leo hii. Yeye ni mwili aliouchagua kuzungumza nasi kama alivyofanya alipokuja katika mwili miaka 2000 iliyopita. Kila Andiko linathibitisha Hilo. Roho Mtakatifu amelifunua jambo hilo . Sasa kuna uhakikisho wa kwamba tunao UFUNUO WA KWELI wa Yeye ALIKUWA Nani, YEYE NI NANI na sisi NI NANI: Bibi-arusi wake Kipenzi Aliyechaguliwa .

Tunajua tuko katika Mapenzi yake makamilifu kwa kudumu na Neno Lake. Inaleta Furaha na shangwe kweli. Haiwezekani kuelezea kwa maneno tu kile inachomaanisha kwetu.

Daima tumejua ndani ya mioyo na Nafsi zetu kwamba kulikuwa na kitu tofauti hapo. Tulijua, hata bado tulipokuwa katika dhambi, kulikuwa na kitu pale ambacho hatukuweza kuelezea, lakini kilikuwa pale tu. Sasa TUNAJUA. Hatujawahi kuhisi hivi hapo awali, hakuna mashaka tena, hakuna kushangaa tena, hakuna kuuliza tena, Imechongwa na kuandikwa katika nafsi zetu. UTUKUFU KWA MUNGU!!

Sisi ndio kizazi kile ambacho hakitapita hadi mambo haya yote yatimie. Sisi ndio kizazi kile kinachoona ule ukengeufu ukifanyika mbele ya macho yetu. Wakati umekaribia. Kile Kimulimuli Chekundu cha Kuja Kwake kiko hapa. Onyo lake la mwisho linafanyika.

Mauti na Maangamizi vimetuzunguka pande zote. Tunaishi katika Sodoma na Gomora. Uchafu, dhambi, moyo wa mwanadamu unakufa kwa hofu, mabomu ya atomiki, dhiki kati ya mataifa, na wakati wote tunaungana na kuketi pamoja katika Ulimwengu wa Roho wakati Mungu mwenyewe akituambia, MSIOGOPE, NINYI NDIYO KIPENZI CHANGU. Hakuna kinachoweza kuwapata ninyi . Hebu tu mioyo yenu iwake ndani yenu ninapozungumza nanyi njiani na kuwaambia, NINYI NI BIBI-ARUSI WANGU.

Njoo uungane nasi Jumapili hii saa 6:00 Sita Mchana , saa za Jeffersonville, ( Ni Saa 1:00 Moja Jioni ya Tanzania), Wakati kuna makelele yanayosikika. Selo imeshuka. Kimulimuli Chekundu kimeanza kumemetesha . Iwapo unatarajia kuondoka pamoja nasi, afadhali utupe chini kifurushi hicho cha njugu karanga , uache kupiga domo , uchukue makasha yako, ukajitayarishe la sivyo utaachwa,  sababu litasimama hapo kwa muda mfupi tu. Limekuja kusema: Kimulimuli Chekundu Cha Dalili ya Kuja Kwake 63-0623E.

Ndugu. Joseph Branham

Maandiko ya kusoma kabla ya Ujumbe:

Mathayo Mtakatifu 5:28 / 22:20 / Sura ya 24 yote

2 Timotheo Sura ya 4 yote

Yuda 1:7

Mwanzo Sura ya 6 yote