22-0327 Kusimama Katika Pengo

Ujume: 63-0623M Kusimama Katika Pengo

PDF

pakua

BranhamTabernacle.org

Wapendwa Walio Waaminifu,

Wiki hizi zilizopita zimekuwa wakati wa utukufu zaidi katika maisha yetu yote.
Imekuwa mojawapo ya mambo makuu zaidi kuungana na Bibi-arusi Wake ulimwenguni kote, kumsikiliza Mungu akifunua ile Mihuri Saba.

Je, sisi sote tuliungana pamoja kusikiliza kitu gani pia?

“Kule ndani ya hiyo piramidi, kulikuwako na Jiwe jeupe ambalo halikuwa limeandikwa.” Hiyo ndiyo sababu ilinibidi kwenda magharibi, kuungana na Ujumbe wa Malaika hawa, kurudi hapa na kuufunulia kanisa .

Ilimbidi aende magharibi ili kuungana na wale Malaika 7, ili arudi kutufunulia yale ambayo hata hayakuwa yameandikwa; lakini sasa, kwa Ufunuo, yamefunuliwa kwetu na yanatupa Imani ya Kunyakuliwa.

Tumezisikia Jumbe hizi maishani mwetu mwote, lakini sasa zimefunuliwa kuliko hapo awali; hii ndiyo siku yenyewe , huu ndio wakati wenyewe. Tunaona na kusikia yale aliyotuambia yangetukia, ulimwenguni na katika Ujumbe huu, na sasa yanadhihirishwa mbele ya macho yetu kabisa.

Je, Malaika_Mjumbe wetu wa 7 alikuwa ni nabii tu kama manabii wa kale? Hapana, Yeye aliitwa kwenye huduma ya juu zaidi kuliko manabii wote waliomtangulia. Kwa maana ilikuwa ni Mwana wa Adamu akijifunua Mwenyewe katika mwili wa mwanadamu kama tu alivyofanya miaka 2000 iliyopita. Nabii wetu aliitwa KUONGOZA BIBI-ARUSI mpaka kwenye Makao yetu mapya, kisha atatukabidhi kwa Bwana.

Yeye Alituambia huduma yake ilifananisha maisha ya Musa kikamilifu. Musa alipokuwa katika safari yake akiifuata Nguzo ya Moto, watu waliinuka na kumkabili. Watu hawa walikuwa wameitwa na walikuwa njiani kuelekea kwenye nchi ya ahadi. Walimpinga Musa kwa kusema alijitwalia madaraka mno; hakuwa mtakatifu pekee yake aliyeitwa, wao pia walikuwa watakatifu na walihitaji kuhubiri kitu fulani pia.

Alisema walikuwa watu watakatifu, na ya kwamba kweli walikuwa na jambo Fulani la kufanya, Lakini Mungu alikuwa amemwita YEYE, MUSA, MTU MMOJA, kuwaongoza watu.

Wao Walikuwa na nafasi yao. Walitiwa mafuta. Walikuwa wakifanya kile walichoitiwa na kuagizwa kufanya kwa kuwaambia watu, “msikilizeni Musa”, Lakini walitaka kusema KITU FULANI ZAIDI, AU KUFAFANUA KILE MUSA ALICHOKUWA ANASEMA . Hawakuridhika kuwaelekeza tu watu wamsikilize Musa. Walitaka wao wawaongoze watu. Walitaka kufanya jambo fulani zaidi, au tofauti, kuliko lile waliloagizwa kufanya.

Ukiwahi kutilia shaka Niani mwako kile nabii wetu alicho, au aliitiwa kufanya Nini, ninakualika uende magharibi kutazama safu ya milima ambayo Mungu Mwenyewe aliifanya kama ishara ya milele duniani, kwa kuweka jina la nabii wetu, B-R-A-N-H-A-M. , kwenye mlima huo.

Wewe ni Bibi-arusi wa Yesu Kristo. Alikuchagua na kukuteua tangu awali. Neno lake linaishi na kukaa ndani yako. Wewe ni Neno lililo hai lililofanyika mwili. Alikupa Ufunuo wa Neno Lake. Shetani hana nguvu juu yako. Ile Imani ya Kunyakuliwa inaishi na kukaa ndani yako.

Roho Mtakatifu anamwongoza Bibi-arusi Wake kwa njia Yake pekee aliyoiandaa kwa ajili ya wakati huu, Neno Lake lililonenwa na nabii Wake malaika wa Saba. Nabii huyo ndiye Mchungaji wetu.

Mchungaji wetu alituahidi kwamba ujumbe wowote mpya wa kanda ungetoka kwanza kwenye Ghala, mpaka Bwana alibadili . Kwa maana hapo ndipo kanda zilizowekwa kwenye ghala zingenasiwa.

Yeye Pia alimwelekeza mchungaji msaidizi wake Ndugu Neville, na wakati huu kwa Neema Yake, mimi mwenyewe, kile tunachopaswa kufanya kanisani.

Ninaomba ya kwamba utamsaidia mchungaji wetu mpendwa, Ndugu Neville. Mfanye, Bwana, kujaa neema na kujaa nguvu, na pamoja na ufahamu, apate kuchukua Chakula hiki Kilichowekwa kwenye ghala na kuwalisha kondoo wa Mungu.

Kanda hizi ni za wale ambao nabii aliitiwa kuwachunga. Ikiwa unataka kusikia BWANA ASEMA HIVI, njoo usikilize pamoja nasi Jumapili saa 12:00 Sita Mchana , saa za Jeffersonville, ( Ni saa 1:00 Moja jioni ya Tanzania), ili: Kusimama Katika Pengo 63-0623M , tunaposikia Chakula kilichowekwa kwenye ghala ambacho kimeandaliwa kwa ajili ya Bibi-arusi.

Tutauanza Ujumbe huu kuanzia kwenye namba ndogo (paragraph) ya 27.

Ndugu. Joseph Branham

Maandiko ya kusoma kabla ya kusikiliza Ujumbe :

Hesabu 16: 3-4