22-0320 Muhuri Wa Saba

Ujume: 63-0324e Muhuri Wa Saba

PDF

BranhamTabernacle.org

Mpendwa Bibi-arusi Mwaminifu,

Hata alipoifungua muhuri ya saba, kukawa kimya mbinguni kama muda wa nusu saa .

  • Lakini hapa kuna Ngurumo Saba mfululizo, moja baada ya nyingine: moja, mbili, tatu, nne, tano, sita, saba, hiyo namba kamilifu. Ngurumo Saba mfululizo, zilitoa sauti, si… zikifanya tu—tu moja, mbili, tatu, nne, tano, sita, saba, mfululizo. Ndipo, Mbingu hazingeweza kuandika jambo Hilo. Mbingu haziwezi kujua juu ya jambo Hilo, hakuna jambo lingine lo lote, maana hakuna jambo linaloendelea. Ilikuwa ni wakati wa kupumzika. Ilikuwa ni kuu sana, mpaka, ikafichwa Malaika.
  • Hata ngurumo saba zilipotoa sauti zao, nalikuwa tayari kuandika:…
    Kulikuwa kumenenwa kitu. Haikuwa ni kelele tu. Kitu fulani kilinenwa. Alikuwa tayari kuandika .
    Nami nilisikia sauti kutoka mbinguni ikisema,
    Angalia mahali zile sauti zilikokuwa katika zile Ngurumo. si Mbinguni, Nchini! Zile Ngurumo hazikutoa sauti kamwe toka mbinguni , zilitoa sauti toka Nchini.
  • Saba, nambari ya Mungu iliyo kamilifu. Saba moja kwa moja tu mfululizo . Ngurumo Saba zililia mfululizo pamoja , kana kwamba zilikuwa zikiendeleza herufi za kitu fulani .

Shauku ya mioyo yetu ni kuwa mwana au binti wa kweli wa Mungu; kuwa tayari kwa Unyakuo Wake unaokuja hivi karibuni. Kwa hiyo ni lazima tumuulize Bwana: “Ni kitu gani kitakachompa Bibi-arusi Imani ya kunyakuliwa anayohitaji”?

  • Nami naamini ya kwamba, kupitia Ngurumo hizo Saba, zitafunuliwa katika siku za mwisho ili kumkusanya Bibi-arusi pamoja kwa ajili ya kupata imani ya kunyakuliwa .
  • Nazo Ngurumo Saba papa hapa katika ufunuo, hapa, wa Yesu Kristo, ni siri fulani. Biblia haisemi kwamba ” huu ni ufunuo wa Yesu Kristo” ? Vema, kuna siri fulani yake iliyofichwa. Ni nini? Zile Ngurumo Saba zina hiyo siri. Kwa maana Yohana alikuwa tayari kuandika, na sauti ilishuka kutoka Mbinguni ikasema, “Usiliandike. Bali litie muhuri; litie muhuri. Liweke kwenye upande wa nyuma wa kile Kitabu .” Lapaswa lifunuliwe. Ni zile siri .

Je! Roho Mtakatifu, atamfunulia Bibi-arusi Wake Ufunuo wa zile Ngurumo Saba utakaowapa imani ya Kunyakuliwa kupitia hizi huduma ?

  • Sasa mjumbe huyu wa Malaki 4 na Ufunuo 10:7 atafanya mambo mawili . Moja : Kulingana na Malaki 4 ataigeuza mioyo ya watoto iwaelekee baba zao . Pili : Atafunua siri za ngurumo saba katika Ufunuo 10 ambazo ni mafunuo yale yaliyo ndani ya zile muhuri saba.
  • Muhuri hizi ziko nyuma ya kile Kitabu, na wakati yule Malaika wa Saba atakapopiga baragumu, siri zote ambazo zimeandikwa katika Kitabu
    zimekamilishwa. Na mara tu, Kitabu ambacho kilikuwa kimefunguliwa na kuandikwa ndani, kinafungwa, “Siri za Mungu zimetimizwa.” Na hizi ndizo siri za Mungu: kunyakuliwa kwa Kanisa, na mambo haya yote mengine. “Siri zimekwisha.”
    Wakati yule malaika wa saba anapiga baragumu ya kila siri , imekwisha. Hata awe nani. Hata iwe nini. Neno la Mungu haliwezi kushindwa .

NI RAHISI HIVI:

Siri kupitia hizo Ngurumo Saba zitampa Bibi-arusi Imani ya Kunyakuliwa . Ni Mungu PEKE YAKE , kupitia malaika Wake wa Saba, atakayefunua zile NGURUMO SABA kwa Bibi-arusi.

Ukitaka zile Ngurumo Saba zifunuliwe kwako, kukupa Imani ya Kunyakuliwa , hakuna njia nyingine ya kuupokea Ufunuo huo ila kuupata kutoka kwenye Sauti pekee ya Mungu iliyothibitishwa kwa ajili ya siku yetu; si kutoka kwangu, si kutoka kwa mchungaji wako wa mahala, mwinjilisti, au mwalimu, Bali kutoka kwa mchungaji wa Mungu kwa ulimwengu wote, kwa KUBONYEZA PLAY.

Njoo usikie siri zote zikifunuliwa; kupokea Imani ya Kunyakuliwa na ujaze Taa yako Mafuta, Jumapili saa 6:00 Sita mchana, saa za Jeffersonville, (ni saa 1:00 Moja jioni ya Tanzania), tunapomsikia Mungu akizungumza na kujifunua Mwenyewe katika urahisi na kutuletea: Muhuri wa Saba 63-0324E .

Ndugu. Joseph Branham

Maandiko ya kusoma kabla ya kusikiliza Ujumbe:

Kumbukumbu la Torati 29:16-19

1 Wafalme 12:25-30

Ezekieli 48:1-7, na mstari wa 23-29

Mathayo 24:31-32

Ufunuo sura 7 yote

Ufunuo 8:1

Ufunuo 10:1-7

Ufunuo sura 14 yote