23-0910 Muhuri Wa Saba

UJUME: 63-0324E Muhuri Wa Saba

PDF

pakua – m4a

pakua – amr

BranhamTabernacle.org

Mpendwa Bibi-arusi wa Kanda,

Ni siku ya namna gani tunayoishi! Ni wakati mkuu jinsi gani! Zile siri, mafumbo, yote yanayofunuliwa kwetu kila siku. Hatuoni tu yale ambayo tumeyapita, tunajua ile saa hasa tunayoishi na yale hasa yaliyo mbele.

Tunaambiwa mstari kwa mstari kile kitakachotokea. Yeye anatuambia waziwazi sisi ni nani, ni akina nani watakaokuwapo kule, na hata kile tutakachofanya. Wale Wayahudi 144,000, lile kanisa lililotakaswa kwa Dhiki, watenda kazi katika mashamba ya mizabibu ambao watakaoleta heshima na utukufu wao katika mji ule.

Lakini basi anatuambia huyo hatakuwa wewe…loo la, wewe ni Bibi-arusi Wangu, uko pamoja Nami katika Mji ule. Wewe hutakuwa huko nje ukifanya kazi katika mashamba ya mizabibu, wewe ni kipenzi changu. Wewe u Malkia Wangu pamoja Nami, Mfalme wako. Ninyi ndio wale moja ya mia ya hao moja kwa tano niliyowachagua kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu. Nimepatengeneza Mahali hapa KWA AJILI YENU TU…NA JINSI TU MNAVYOLIPENDA.

Kuwazia tu, tunakusanyika kuizunguka Meza yake anapozungumza nasi wiki baada ya wiki, siku baada ya siku, saa baada ya saa, akitufunulia Neno Lake lote la ajabu. Yeye anatuambia tena na tena sisi ni nani; jinsi gani Yeye anavyotupenda; kile kilichokuwa, kile kilicho sasa, na kile kitakachotukia.

Hakuna maneno ya kuelezea jinsi inavyomaanisha kwetu, ama jinsi tunavyojisikia wakati tunapomsikia Yeye akituambia mambo haya. Wakati Tunapobonyeza Play na kuisikia Sauti hiyo, tunaondoka katika ulimwengu huu na mara moja tunaketi katika ulimwengu wa Roho pamoja Naye. Nafsi zetu zinafarijiwa. Tunajisikia Roho Mtakatifu akijaza utu wetu wote kwa Roho Wake. Ni furaha isiyoweza kuelezeka. Mungu anazungumza NASI. Kila Neno lililonenwa kwenye kanda hizo, Yeye alinena kwa ajili yetu. Yeye anajua hasa kile ambacho tungehitaji kusikia na wakati ambao tuliyohitaji kulisikia… na mara nyingi tunahitaji kulisikia tena na tena…. na kila wakati HUFURIKA NAFSI ZETU.

Sisi hatuchoki kumsikia yeye akituambia kuhusu Maono, Ndoto, Bwana Asema Hivi, ng’ambo ya pazia, akituona sisi tumevaa nguo ndefu nyeupe, Mvuto wa Tatu, kuwaumba kindi, Ule Upanga wa Mungu uliyoenea mkononi mwake barabara, chakula kilichohifadhiwa, tukiwa tumewekwa kwa Mkuu wa Meza, Ngurumo, Malaika wenye nguvu wakija na kumtwaa juu, yule malaika wa saba wakipekee aliyemaanisha kitu cha zaidi kwake, ishara ya milele ya vilele saba vya milima vinavyoendeleza herufi BRANHAM, semeni tu hasa yale yaliyo kwenye kanda hizo, ninayo Maneno ya kutoweza kukosea, Yeye ameitiwa wito wa juu zaidi, nitawaambia UFUNUO WANGU, Mimi ni Sauti ya Mungu kwenu, shikilieni kabisa hayo mafundisho ya kanda, nitawaita BIBI-ARUSI, aiko, iyo, dafuta… sisi tunayapenda YOTE.

Hili ndilo ono langu. Sauti ya Mungu iliyo kwenye kanda ndio Mapenzi makamilifu ya Mungu, MWISHO WA MANENO. Kuzicheza kanda ndio Mapenzi makamilifu ya Mungu, MWISHO WA MANENO. Wewe unaweza kuwasikia wahubiri, waalimu, mitume, manabii, wachungaji, LAKINI kanda ndizo, na zinatakiwa kuwa, Sauti iliyo muhimu sana unayotakiwa kuisikia, MWISHO WA MANENO. Sauti iliyo kwenye kanda ndio Sauti pekee ambayo Mungu Mwenyewe aliyosema, MSIKIENI YEYE, MWISHO WA MANENO.

Ndugu na dada zangu, simpingi mtu ye yote, Mimi niko kwa ajili ya Sauti hiyo tu. Inatupasa, na mimi, nawapenda wote wanaotangaza kwamba wanapenda na kuamini Ujumbe huu. Hata kama mnajisikia kwamba ninawaambia watu vibaya kuwaambia kubonyeza play, Ninawapenda na ninaamini mnanipenda. Sote tunataka kuwa katika Mapenzi yake Makamilifu. Tafadhali endelea kufanya yale Mungu aliyokuitia kufanya; hubiri, fundisha, kuwa mchungaji, wewe liambie tu kundi lako ni Sauti gani iliyo muhimu sana wanayotakiwa kuisikia.

Ni Sauti hiyo tu iliyo kwenye kanda isemayo jambo lile lile KILA WAKATI. Haibadiliki kamwe. Bibi-arusi anaweza TU KUSEMA AMINA kwa kila Neno lililo kwenye kanda, lakini Bibi-arusi hawezi kusema AMINA kwa kila neno ambalo mwanadamu ye yote asemalo, MWISHO WA MANENO.

Kama huamini jambo hilo, wewe si Bibi-arusi. Ikiwa unaamini jambo hilo, basi hutakuwa na shida kuwaambia kundi lako kwamba kuzisikiliza kanda ndiyo Sauti iliyo muhimu zaidi wanayotakiwa kuisikia.

Kwa Mimi kutoa kauli hizi nimesikia kutoka kwa wahudumu wengi tofauti ambao wanasema kwamba ninawaambia watu wasiwasikilize wachungaji wao na kuyaacha makanisa yao, HIYO SI KWELI. Siwezi kusema jambo hilo na siamini jambo hilo.

Ni kweli wengi wanasema mambo ambayo sijawahi kamwe kusema, wala kuamini. Siwezi kuwajibishwa kwa ajili yao, lakini tu kwa yale niliyosema na yale ninayoamini. Nimezungumza waziwazi na kuyaweka katika mfumo wa barua yale ninayoamini. Wao / ninyi mnapindisha kwa manufaa yenu yale ninayosema /na ninayomaanisha.

Bibi-arusi wote watakuwa wakisema jambo lile lile. Hakuna watu wawili wasemao jambo lile lile. Sauti Moja. Nabii mmoja. Bibi-arusi Mmoja.

Mimi Siamini kwamba yakubidi kuusikia Ujumbe kwa wakati mmoja kabisa, kama wanavyofanya waamini wengi ulimwenguni kote, ili uwe Bibi-arusi Wake, lakini Naamini unapaswa kuisikia Sauti ya malaika-mjumbe wa saba Jumapili asubuhi…ipe hiyo sauti nafasi ya KWANZA.

Unaalikwa kusikiliza pamoja nasi: Muhuri wa Saba 63-0324E, Jumapili saa 06:00 SITA MCHANA, saa za Jeffersonville, ( ni saa 1:00 MOJA JIONI ya Afrika Mashariki) Wakati sehemu ya Bibi-arusi kutoka kote ulimwenguni watakaposikia Sauti hiyo kwa wakati mmoja kabisa.

Ndugu. Joseph Branham

Maandiko ya kusoma kabla ya Kusikiliza Ujumbe:

Kumbukumbu la Torati 29:16-19
1 Wafalme 12:25-30
Ezekieli 48:1-7, 23-29
Mathayo 24:31-32
Ufunuo 7 yote
Ufunuo 8:1
Ufunuo 10:1-7
Ufunuo 14 yote