22-0414  Kutoka kwa Tatu na Kutawadhana Miguu

Ujume: 63-0630m Kutoka kwa tatu

PDF

pakua

BranhamTabernacle.org

Mpendwa BIBI-ARUSI ALIYEUNGANA Ambaye Anayenena NENO,

Huu ni wakati mzuri zaidi wa maisha yangu marafiki zangu! Tunaona Neno likitimizwa mbele ya macho yetu kuliko wakati mwingine wowote. Inasisimua jinsi gani kutambua Yeye ni Nani, mjumbe Aliyemtuma ni nani, na kisha KUJUA SISI NI NANI! Asante Baba. Hatukufikiri kamwe matukio haya yangetukia namna hii, lakini haya hapa yanatukia papa hapa mbele ya macho yetu, jinsi kabisa nabii Wako alivyosema kwenye kanda.

Niko chini ya matarajio makubwa kuona Roho wake Mtakatifu akituleta karibu Naye kuliko hapo awali kabla ya wikendi hii ya Pasaka. Ningependa kuwaalika kila mmoja wenu kushiriki nasi kwenye Ujumbe huu, pamoja na Bibi-arusi Wake ulimwenguni kote.

” Basi wakati jambo lo lote ndogo linapozuka, mbona unatenda kama mtoto? Inakupasa kuwa mtu mzima. Nena na watu! Amina. “Kisha mwendelee mbele.” Amina. Ndivyo hivyo “Usilie, nena!” Amina. Jamani, napenda hilo. “Mbona unanililia? Nena tu na watu, kisha songeni mbele kwa shabaha yenu.” Cho chote kile, kama ni magonjwa, cho chote kile, kama ni kufufua wafu ama cho chote kile, nena! Nilithibitisha hayo. Nena na watu! ”

Ni fursa iliyoje tuliyo nayo ya kuchangamsha imani yetu, hivyo sisi pia tunaweza Kunena NENO. Njoo ukusanyike pamoja na Bibi-arusi katika wikendi ya Pasaka, tunapojitayarisha kwa ajili ya Kutoka kwa mwisho. Maisha yetu lazima yaistahili Injili, kwa maana kizazi hiki kiko chini ya Shtaka. LAKINI SASA hakuna sababu ya Bibi-arusi wake kulialia, BALI KUNENA! Songeni mbele kwa shabaha yenu. Jina la Bwana lihimidiwe!

Kama kawaida yetu tufanyavyo kwa wikendi ya Pasaka, Hebu tujifungie mbali na ulimwengu kadri tuwezavyo kwa kuzima simu zetu isipokuwa kupiga picha, kusikia Nukuu ya Siku, na kucheza kanda kwenye programu ya Lifeline au kutoka kwenye anuani ya kupakua. Hebu na tumtolee Bwana wikendi hii takatifu kikamilifu, na tusiifanye Pasaka hii kuwa jambo la kijamii, bali kujiweka wakfu kwenye Neno, katika nyumba zetu. Ningependa sisi sote tuungane pamoja wikendi hii kwa ratiba ifuatayo, kwa Saa za kutwa za Mashariki (EDT) isipokuwa kama ifahamike vinginevyo.

ALHAMISI

Ilikuwa ni Alhamisi usiku ambapo Bwana Yesu alikula Karamu ya Mwisho na wanafunzi wake katika ukumbusho wa Pasaka kabla ya kutoka kwa wana wa Israeli. Ni fursa iliyoje ya kufanya ushirika na Bwana katika nyumba zetu, kabla ya wikendi yetu takatifu, na kumwomba atubariki sisi na familia zetu, na kutupa sisi sote kile tunachohitaji katika safari yetu.

Baba wa Mbinguni, tunashukuru kwa ajili ya jambo hili, wakati mwingine wa kukusanyika pamoja, upande huu wa Umilele. Na tunatarajia asubuhi ya leo kuhuishwa upya kwa nguvu kuja kutoka Kwako, zipate kututia moyo kwa ajili ya safari iliyoko mbele. Tumekusanyika kama wana wa Kiebrania walivyofanya asubuhi na mapema, kuokota mana iliyokuwa imetolewa kwa ajili yao usiku kucha, kuwapa nguvu kwa ajili ya siku ijayo. Tunakusanyika kwa ajili ya Mana ya kiroho, asubuhi ya leo, ipate kutupa nguvu kwa ajili ya safari.

Hebu na tuanze wote saa 12:00 kumi na mbili JIONI . kwa masaa ya nchi zetu, na tumsikie Yeye akituambia kwamba tuko katika Kutoka kwa mwisho, tunapokusanyika kukizunguka Kiti Chake cha Enzi ili kusikia Ujumbe: Kutoka kwa Tatu 63-0630M .

Sambamba Tunaposikiliza Ujumbe, tutakusanyika na familia zetu katika nyumba zetu na kushiriki Meza ya Bwana.

Hivi punde tutakuwa na Anuani ya kupakua kanda na ibada ya Ushirika, au, itapatikana kwa muda ulioratibiwa wa ibada kwenye Voice Radio, kwenye app ya Lifeline.

IJUMAA
Hebu na twende kwenye maombi na familia zetu saa 3 :00 Tatu ASUBUHI ( Ni saa 10:00 Kumi jioni ya Tanzania) ., na kisha tena saa 6:00 Sita MCHANA, ( Ni Saa 1:00 Moja Jioni ya Tanzania) Kumualika Bwana awe pamoja nasi na Bibi-arusi wake kutoka ulimwenguni kote katika wikendi hii ya kipekee sana; na ajaze nyumba zetu kwa Roho wake Mtakatifu tunapojitolea kumwabudu.

Hebu Fahamu zetu na zirudi nyuma hadi siku ile pale Kalvari, zaidi ya miaka 2000 iliyopita, na kumwona Mwokozi wetu akining’inia msalabani, kisha tujitoe vivyo hivyo kufanya daima yale yanayompendeza Baba.

Sasa angalieni. Wakati alipokuja ulimwenguni, wakati kulikuwapo na zaidi, kutokuamini kwingi duniani wakati huo kadiri kulivyowahi kuwa, hata hakukumpunguzia mwendo. Aliendelea moja kwa moja kuhubiri vivyo hivyo, na kuponya vivyo hivyo. Hakukumsumbua. Kulikuwako na wakosoaji. Mtu huyo alikosolewa tangu alipokuwa mtoto mchanga mpaka alipokufa msalabani. Je! hilo lilimzuia? La, bwana. Lengo Lake lilikuwa ni nini? “Kufanya sikuzote yale Baba ameandika. Kufanya daima yale yanayompendeza .”
.

Kisha saa 6:30 Sita na Nusu MCHANA . (Ni saa 1:30 Moja na Nusu jioni ya Tanzania) hebu na tufikirie kwa dhati juu ya swali muhimu sana katika maisha yetu, tunapokusanyika kukizunguka Kiti Chake cha Enzi ili kusikia Ujumbe: Je, Maisha Yako Yanaistahili Injili? 63-0630E .

Kisha Hebu na tuungane pamoja Tena katika maombi saa 9:00 Tisa ALASIRI (Ni saa 4:00 Nne Usiku ya Tanzania) . katika ukumbusho wa kusulubiwa kwa Bwana wetu.

JUMAMOSI

Hebu na Tuungane pamoja kwa mara nyingine tena katika maombi saa 3:00 Tatu ASUBUHI ( Ni Saa 10:00 Kumi jioni ya Tanzania) ., na saa 6:00 Sita MCHANA .,( Ni Saa 1:00 Moja Jioni ya Tanzania) na tuitayarishe mioyo yetu kwa ajili ya mambo makuu atakayotutendea kati yetu,

“ Baada ya kulileta shtaka hili dhidi ya marafiki wa—wangu wahubiri huko, na yanibidi niseme mambo haya magumu; lakini Bwana, niliyatenda kwa punzi Yako. Najisikia kuwa Wewe uliniambia nitende hili. Sasa, haumo mabegani mwangu, Bwana. Ni—ninafuraha umeniondokea. Na wao watende nao lo lote wapendalo, Baba. Naomba kuwa wataupokea. Naomba kuwa Wewe utamwokoa kila mmoja, Bwana. Na humo kutokee ufufuo wa wenye haki na Uweza mkuu uje kati ya Kanisa kabla tu ya kuondoka Kwake. Si vigumu kuomba hayo, kwa maana Wewe uliyaahidi. Nasi twatazamia, Bwana, huo mvuto wa tatu tunaojua kuwa utatenda mambo kati yetu .”

Kisha saa 6:30 Sita na Nusu MCHANA.( Ni Saa 10:30 Kumi na Nusu jioni ya Tanzania). sote tutakusanyika pamoja ili kusikia NENO: Lile shtaka 63-0707M . Hii itakuwa SIKU ILIYO KUU jinsi gani kwa Bibi-arusi Wake ulimwenguni kote.

Kisha Hebu na tuungane pamoja tena katika maombi saa 9:00 Tisa ALASIRI. ( Ni Saa 4:00 Nne Usiku ya Tanzania) katika ukumbusho wa kusulubiwa kwa Bwana wetu.

JUMAPILI

Ni siku nzuri jinsi gani ya kutolialia tena, Bali KUNENA! Ni asubuhi iliyoje ya ufufuo! Hebu na tuamke mapema kama vile Ndugu Branham alivyofanya asubuhi ile wakati rafiki yake mdogo, robin, alipomwamsha Saa 11:00 Kumi na moja ALFAJIRI ( ni Saa 6:00 Sita Mchana ya Tanzania) .. Hebu na tumshukuru tu Bwana kwa kumfufua Yesu kutoka kwa wafu:

“ Saa kumi na moja asubuhi ya leo, rafiki yangu mdogo mwenye kifua chekundu aliruka dirishani akaniamsha. Ilionekana kana kwamba moyo wake mdogo ungepasuka, akisema, “Amefufuka.”

Saa 3:00 Tatu ASUBUHI Saa za Jeffersonville ( ni Saa 10:00 Kumi jioni ya Tanzania) Hebu na tuungane kwa dhati kwa mara nyingine tena katika Maombi yetu ya mnyororo , kuombeana mmoja kwa mwingine na tukijitayarisha wenyewe kuisikia Sauti ya Mungu.

Saa 6:30 Sita na Nusu MCHANA saa za Jeffersonville ( Ni saa 1:30 Moja na Nusu Jioni ya Tanzania) tutakusanyika pamoja ili kusikia Ujumbe wetu wa Pasaka: Mbona unalialia? Nena! 63-0714M .

Baada ya Ibada hii, Hebu na tuungane tena katika maombi, Kumshukuru kwa WIKENDI YA AJABU ALIOTUPATIA PAMOJA NAYE NA PAMOJA NA BIBI-ARUSI WAKE ULIMWENGUNI KOTE.

Kwa ndugu na dada zangu walio nchi za ng’ambo, ningependa kuwaalika kuungana nasi kwa matukio haya kwa masaa ya Jeffersonville, kwa masaa yote ya maombi kwenye ratiba hii na kwa kanda itakayochezwa Jumapili asubuhi. Ninatambua, hata hivyo, kwamba kucheza Kanda hizi za Alhamisi, Ijumaa, na Jumamosi alasiri kwa masaa ya Jeffersonville ingekuwa vigumu sana kwa wengi wenu, kwa hivyo tafadhali jisikie huru kucheza Jumbe hizo wakati wowote wa siku husika unaokufaa. Ningependa, hata hivyo, sote tuungane pamoja Jumapili saa 6:30 Sita na Nusu MCHANA za Jeffersonville, ( Ni Saa 1:30 Moja na Nusu Jioni ya Tanzania) ili kusikia Ujumbe wetu wa Jumapili kwa pamoja.

Ningependa pia kukualika wewe na watoto wako kuwa sehemu ya karatasi za creations, mafunzo , na maswali ya YF, ambayo familia yako yote inaweza kufurahia pamoja. Tunafikiri mtayapenda kwa kuwa yote yanahusu NENO ambalo tutakalosikia wikendi hii.

Kwa ratiba ya wikendi, Taarifa kuhusu kujiandaa kwa ajili ya ibada ya Ushirika, nyenzo zitakazohitajika kwa ajili ya kazi za creations , Maswali ya Pasaka, na taarifa nyinginezo, tazama anuani zilizo hapa chini.

Ni heshima kubwa kwangu kukualika wewe na familia yako kuungana pamoja na Bibi-arusi duniani kote kwa wikendi iliyojaa KUABUDU , SIFA NA UPONYAJI. Ninaamini kweli ni wikendi ambayo itabadilisha maisha yako milele.

Ndugu Joseph Branham