22-1225 Kuonea Haya

UJUMBE: 65-0711 Kuonea Haya

PDF

pakua

BranhamTabernacle.org

Mpendwa Rebeka Bibi-arusi,

Baba amemtuma mtumishi Wake mwaminifu, Eliezeri, kumwinda Bibi-arusi Rebeka Wake . Tumemtambua, malaika-mjumbe Wake wa saba, William Marrion Branham, ambaye Yeye amemwagiza: Kumwita, Kumkusanya, Kumwongoza na hatimaye Kututambulisha sisi , Kwake.

Ametumiminia Nguvu Zake za Kuhuisha nyingi na ametuleta katika utambuzi wa mahali petu, nafasi yetu, na wajibu wetu, tukiwa watu walioitwa, waliotengwa na ulimwengu, waliowekwa wakfu kwa Mungu. Anatuongoza na kutuelekeza katika mambo tunayofanya na kuyanena, na kuleta heshima na utukufu kwa Jina Lake.

Hakuna kitu, popote, kinachoweza kututenganisha na Hicho, HAKUNA CHOCHOTE. Tumelindwa Milele katika Ufalme wa Mungu. Baba amepiga Muhuri Wake juu yetu hadi mwisho wa safari yetu.

Shetani anatupiga konde mchana na usiku. Yeye anatusema kila kitu, na kutushtaki, na kujaribu kutufanya tufikiri ya kwamba sisi si Bibi-arusi huyo. Anatupa kila kitu njiani mwetu kujaribu kutuvuruga, kama ugonjwa na huzuni, lakini hatumsikilizi. Hiyo Nguvu ya Kuhuisha imo SASA HIVI ndani yetu nasi tumetiwa muhuri na moyo wetu upo kwenye Neno hilo. Tunaruka juu ya ngamia wetu, tukimkimbilia Yeye tukielekea kwenye Karamu yetu kuu ya Harusi.

Hatuonei haya kile tunachoamini; kinyume chake, tunataka ulimwengu ujue, SISI NI WATU WA KANDA TUNAOAMINI KILA NENO LILILOSEMWA NA NABII WAKE MWAMINIFU ELIEZERI aliyemtuma kumwita BIBI-ARUSI REBEKA WAKE atoke na kumwongoza. Hatuongezi kwake au kuondoa hata Neno MOJA. Ujumbe huu ni Yakini yetu.

Yawezekanaje Mtu ambaye amejazwa na Roho Mtakatifu, amejaa Nguvu za Mungu, na upendo wa Mungu moyoni mwake, anawezaje kuongea na mtu kwa dakika chache tu na asitaje jambo fulani kuhusu Ujumbe ambao ametoka kuusikia kwenye Kanda?

Unapokutana na watu wanaodai kuwa waamini katika Ujumbe huu wa wakati wa mwisho, unaweza kuzungumza nao kwa dakika chache tu na unaweza kujua pale wanaposimama kuhusu kucheza kanda. Wao ni aidha Watu wa Kanda ama sio.

Haliwaziki kwamba wanaona kuwa ni aibu, au hata ni kosa, ikiwa unasema unacheza kanda kanisani mwako au nyumbani mwako. Wanahisi ni kinyume cha Neno na si Njia ya Mungu iliyoandaliwa . Unadharauliwa kwa sababu unasema wewe ni “Mtu wa Kanda”.

Wahudumu wanaocheza kanda katika makanisa yao wanadhiakiwa, na hata kuitwa wavivu. Na iwapo unasikiliza kanda ile ile kwa wakati mmoja , vema, wewe hata si mhudumu, wewe ni dhehebu, ama mwabudu mtu.

Nadhani wale watu wote kabla yetu ambao waliyokuwa kwenye mawasiliano ya simu katika makanisa yao na majumbani mwao, wakimsikiliza Ndugu Branham wote kwa wakati mmoja, yawezekana walikuwa ni madhehebu pia. Huenda walikuwa nje ya Mpango wa Mungu. Hawakuonea haya NA WALA SISI PIA HATUONEI HAYA.

Ndani ya dakika chache tu unapozungumza na watu, watakujulisha mara moja papo hapo ni upi msimamo wao: Ndiyo, Tunabonyeza Play. Ndiyo, tunasikiliza kanda Jumapili Kanisani mwetu ama majumbani mwetu. Ndiyo, kanda ile ile, kwa wakati mmoja.

Kwa nini wengine husema, “Tunaenda kanisani Jumapili asubuhi, Jumapili usiku, na Jumatano usiku. Tunaye mchungaji mzuri sana; analiweka wazi sana na kwa dhairi sana kwetu sisi kuelewa. Anaufafanua Ujumbe ili niweze kuuelewa. Unahitaji kuwa na mhudumu ili uwe Bibi-arusi. Ndugu Branham hakusema kamwe kucheza kanda kanisani.”

Ni kipi basi unachosema ndilo jambo lililo muhimu zaidi? je, ni kile Wahubiri wasemacho, ni kile Ndugu Joseph asemacho, ama ni kile isemacho Sauti hasa ya Mungu mwenyewe kwenye Kanda? Yakini yako ni nini? ni kile kilicho kwenye Kanda , au ni kile mtu fulani asemacho?

Wahudumu ni wazuri, na katika Neno. Tunawahitaji. Lakini ni kipi MUHIMU ZAIDI , kuhubiri au Kanda?

Ikiwa Kanda hizi si jambo lililo muhimu zaidi katika maisha yako ya kibinafsi, katika maisha yako ya kanisa, basi kuna kasoro fulani . Umetoka kwenye Mpango wa Mapenzi makamilifu ya Mungu. RUDI KWENYE MSTARI.

Mtu anapokutana na Mungu; si katika kuuchochea mhemko, shauku fulani, ama fundisho fulani la kidini, katekismo fulani ama kanuni ya imani, ama fundisho la sharti ambalo amelikubali kwa ajili ya kuji—kujifariji, lakini wakati kweli anapofikia mahali kama vile Musa alivyopafikia, upande wa nyuma ya jangwa, akutane uso kwa uso na Mwenyezi Mungu, nawe unaiona hiyo Sauti ikisema nawe, imeambatana kabisa na Neno na ahadi ya wakati huo , kuna kitu inachokufanyia! Unaona, huionei haya, inakufanyia kitu fulani.

Katika siku yetu hii, utaji huo wa mapokeo umepasuliwa. Na hii hapa Nguzo ya Moto imesimama, ikidhihirisha Neno la siku hii. Uungu uliofunikwa katika mwili wa mwanadamu. Utukufu wa Shekinah kwa siku yetu ya leo. Mungu akisimama na kunena mbele zetu, amefunikwa katika mwili wa mwanadamu.

Musa alikuwa na Neno. Sasa kumbukeni, baada ya Neno kudhihirishwa, Musa alikuwa ni Musa tena. Mnaona? Lakini wakati Neno hilo lilipokuwa ndani Yake lipate kutolewa, yeye alikuwa ni Mungu; vema, yeye hakuwa ni Musa tena. Yeye alikuwa na Neno la Bwana kwa ajili ya wakati huo.

Ni sherehe ya KRISTO iliyoje ambayo sisi akina Rebeka tutakayokuwa nayo Jumapili hii. Siku nzima, kwa masaa tofauti siku nzima. Tutakuwa tukimsikia Eliezeri wetu akimwita Bibi-arusi wake atoke nasi tutakuwa tukimwambia hatuonei haya.

Bwana na awape sherehe ya KRISTO ya kupendeza, iliyojaa “UWEPO WAKE.”

Ndugu. Joseph Branham

Ujumbe: 65-0711 Kuonea Haya

Maandiko ya kusoma Kabla kusikiliza ujumbe :

Marko Mtakatifu  8:34-38