23-0129 Mungu Wa Wakati Huu Mwovu

UJUMBE: 65-0801m Mungu Wa Wakati Huu Mwovu

PDF

pakua – m4a

pakua – amr 13MB (use Firefox to download)

Mpendwa kundi dogo Neno-Bikira wa Kristo,

Hatuwezi kuwa kitu kingine. Hatuwezi kusikia kitu kingine. Hatujui kitu kingine. Hatutaki kitu kingine. Palipo na Nyama mbichi, KUBONYEZA PLAY, ambalo ni Neno la majira haya, Hapo ndipo Tai watakapokusanyika. Neno linakuwa hai ndani yetu.

Sisi hatuko sawa na mtu mwingine yeyote ! Ninyi ni watu waliotengwa, watakatifu kwa Bwana, waliowekwa wakfu kwa Neno na Roho wa Mungu, kuzaa matunda ya ahadi Yake ya siku hii. Tunazidi kukomaa na kuivishwa kwa kusikia Sauti ya Mungu.

Nabii alituambia turejee kwenye kanda hizi. Kama una kinasasauti, kusanya kundi la watu pamoja na ukaicheze, na msikilize kwa makini. Kusikiliza Sauti Yake, kile anachotuambia. Neno la Mungu halihitaji kufasiriwa; Yeye hujifasiria Mwenyewe. “Mimi ni Sauti ya Mungu kwenu.”

Nalo ndilo Hili, Biblia, neno moja lisiongezwe Kwake au kuondolewa Kwake. Dumuni waaminifu tu kwa Sauti hiyo. “Mgeni hawatamfuata,”

Anawezaje mtu yeyote kutoona Njia ya Mungu iliyoandaliwa kwa ajili ya siku hii? Lakini utukufu kwa Mungu, tunaweza kuiona, kwa sababu tumechaguliwa kuiona . Hatuta, na hatuwezi kudanganywa, kwa sababu sisi ni Neno Lake lililodhihirishwa.

Ndugu na dada, hebu hilo nalizame ndani kwa dakika moja, SISI NI NENO LILILODHIHIRISHWA!! Mungu Mwenyewe, akinena kupitia midomo ya mwanadamu, anatuambia SISI NI NENO. Hatuna chochote cha kuogopa. Kila kitu tunachohitaji ni chetu.

Kila wiki tuko chini ya matarajio makubwa ya Bwana kutuzuru. Hatuna nafasi hapa ya kuketi kila mmoja, wala kila mmoja hawezi kuja Jeffersonville, kwa hiyo inatubidi tu kuwatumia Neno kupitia njia ya mtandao.

Tuko majumbani mwetu, makanisani mwetu, kwenye magari yetu, tumekusanyika kuzunguka vipaza sauti vyetu vidogo kutoka ulimwenguni kote, tukingojea Kuja kwa Bwana.

Wamekusanyika pamoja nasi huko katika Afrika, wakingojea Kuja kwa Bwana. Wamekusanyika pamoja nasi huko Mexico, wakingojea Kuja kwa Bwana. Huko Ulaya, Skandinavia, Australia, Mashariki ya kati, Amerika ya Kusini, kutoka pembe nne za dunia, wakingojea Kuja kwa Bwana.

Nasi tumekusanyika hapa kwenye kanisa la nyumbani, maskani, tukingojea Kuja kwa Bwana. Tuko umbali wa masaa mengi, Bali tuko pamoja kama JAMII MOJA, waamini, tukisikiliza Sauti ya Mungu, tukingojea Kuja kwa Masihi.

SISI NDIO watu walioitwa na waliochaguliwa na Mungu kutoka katika wakati huu mwovu kwa ajili ya Jina Lake. Tunajaribiwa na kuthibitishwa kwa Shetani kwamba sisi ni Neno. Sisi ni sehemu ya ule Mti wa Bibi-arusi wa Asili. Tunatazama maisha yetu yakidhihirishwa na Neno hilo.

Ni rahisi kwa kila mtu kuamini kwamba Yesu alikuwa jawabu la moja kwa moja kwa kila unabii uliokuwa utimie ndani Yake, kwa sababu wanatazama nyuma kuona hayo yakitukia. Lakini katika wakati huu mwovu uliopo sasa, wanafanya jambo lile lile walilofanya wakati huo, kwa kulifasiri kwa njia nyingine, na wamewafanya watu waingie katika nguvu za upotevu wauamini uongo. Laiti wangetambua ni Neno lile lile la wakati huu likidhihirishwa.

Kuna jambo moja tu linaloweza kumleta Bibi-arusi pamoja, Ujumbe huu. Kuna jambo moja tu ambalo sote tunaweza kukubaliana kwalo, Ujumbe huu. Kuna Sauti moja tu ambayo imethibitishwa kuwa Bwana Asema hivi, Sauti ya Mungu kwenye kanda.

Sasa, makanisa tu baridi, ya kawaida, magumu, na kadhalika, ya theolojia za kujitengenezea, hayo hayangeweza; walio Wateule wasingewajali. Lakini ni kule juu karibu sana na jambo lililo halisi. Kuacha tu Neno moja ndivyo tu unavyopaswa kufanya. Lililoahidiwa kwa wakati huu; wakati mkuu sana!Enyi Wakristo, kila mahali, jihadharini na saa tunayoishi! Andikeni, na someni, na msikilize kwa makini.

Mungu wa wakati huu mwovu anafanya yote awezayo kuwadanganya watu kwa kuizuia Sauti Yake iliyothibitishwa isiwafikie. Anajaribu kuwafanya wasiamini Neno moja tu, kama alivyomfanyia Hawa hapo mwanzo.

Lakini Bibi-arusi-Neno wa Kristo anakuja kilipo Kichwa. Tunaungana tena kwa Mwenzi wetu pale tulipoanzia. Wakati wa kutoka umefika. Mungu anakuja kwa ajili Bibi-arusi Wake yule anayedumu na Neno Lake.

Roho Mtakatifu yuko hapa akimwita Bibi-arusi wa Kristo atoke. Yeye anafanya hivyo kwa kumthibitishia Neno Lake la ahadi Kwake, kwa ajili ya wakati huu, akionyesha ya kwamba Hilo ni Kristo.

Hakuna jambo lililo kuu kuliko kuungana na Bibi-arusi ulimwenguni kote, Kusikiliza Sauti ya Mungu ikinena nawe moja kwa moja. Hakuna haja ya kutumaini, kushangaa au hata kuomba ikiwa kile unachosikia ni kweli. Kwa maana Ndiyo SAUTI PEKEE ILIYOTHIBITISHWA YA BWANA ASEMA HIVI.

Njoo uungane nasi ukasikilize:

Baada ya hayo naliona malaika mwingine, akishuka kutoka mbinguni, mwenye mamlaka kuu; na nchi ikaangazwa kwa utukufu wake.

Saa 6:00 SITA MCHANA , saa za Jeffersonville,( ni Saa 2:00 MBILI USIKU YA Tanzania na Kenya pia) tunaposikia: Mungu wa Wakati Huu Mwovu 65-0801M.

Ndugu. Joseph Branham

Maandiko ya kusoma kabla ya kusikiliza Ujumbe:

Mathayo Mtakatifu sura ya 24 yote /27:15-23
Luka Mtakatifu 17:30
Yohana Mtakatifu 1:1 / 14:12
Matendo 10:47-48
1 Wakorintho 4:1-5 / sura ya 14 yote
2 Wakorintho 4:1-6
Wagalatia 1:1-4
Waefeso 2:1-2 / 4:30
2 Wathesalonike 2:2-4 / 2:11
Waebrania sura ya 7 yote
1 Yohana Sura ya 1 yote / 3:10 / 4:4-5
Ufunuo 3:14 / 13:4 / Sura ya 6-8 na 11-12 zote / 18:1-5
Mithali 3:5
Isaya 14:12-14