23-0205 Matukio Yakidhihirishwa Na Unabii

Ujume: 65-0801e Matukio Yakidhihirishwa Na Unabii

PDF

pakua – m4a

pakua – amr 11MB (use Firefox to download)

BranhamTabernacle.org

Wapendwa Watu wa Wakati huu,

Baba, tunakupenda sana. tunawezaje kuanza kueleza jinsi tunavyojisikia? Ulituchagua, ukatukusudia tangu zamani, nawe ukafanyika Mwanadamu aliye hai ili kutoa Maisha Yako kwa ajili yetu.

Ulituandikia mawazo Yako yenyewe kwetu kupitia manabii Wako, ili tupate Neno Lako. Ndipo, kama ulivyoahidi, ulikuja tena , ukijifunua Mwenyewe katika mwili wa mwanadamu kwa matukio yanayodhihirishwa na unabii, kufasiri na kufunua Neno Lako.

Kwa kujichagulia wewe mwenyewe, ulimchagua William Marrion Branham kuwa mtu wa wakati huu. Ulimchagua ili kuvutia usikivu wetu. Uliongoza mikono yake. Uliongoza macho yake katika maono. Hakuweza kusema kitu cho chote ila kile ulichokuwa unamwonyesha.

Hakuweza kusema kitu cho chote ila kile ulichoweka kinywani mwake. Ulitawala kabisa ulimi wake, vidole vyake, na kila kiungo cha mwili wake. Yeye Alikuwa katika utawala wako mkamilifu .

Kisha, kwa kuchagua Kwako kwa mara nyingine tena, ulituchagua tuwe watu wa wakati huu. Kundi lako dogo la walio wachache limekusanyika kwa upako wa Neno Lako, likidhihirisha tena maisha ya Yesu Kristo. Sisi ni Neno Lako tukiungana na Neno. Hatuwezi kufanya kitu kingine .

Baba, tunataka kuwa katika Mapenzi yako makamilifu; hakuna kitu kingine muhimu kwetu. Hatutaki mawazo yetu, fikra zetu, au kile mtu mwingine ye yote asemacho, mapenzi Yako tu.

Tumeliendea Neno Lako ili kuona kile ulichosema tunapaswa kufanya ili kuwa Bibi-arusi Wako. Ulisema utauhukumu ulimwengu siku moja kwa Neno Lako. Ulituambia Neno Lako huwajilia manabii Wako PEKE YAO , ambao walichaguliwa tangu awali na kuamriwa tangu zamani na Wewe.

Ulituambia halimjii kamwe mwanatheolojia wala kundi la watu, bali kwa nabii Wako. Yeye Atakuwa mfasiri wako pekee wa kiungu wa Neno. Si mawazo yake, fikra zake, fasiri yake, bali Wewe ukinena kupitia kwake, ukilifasiri Neno Lako Mwenyewe.

Katika kila wakati, watu wanawaachilia watu waweke fasiri yao wenyewe kwenye Neno Lako, na inawafanya kuwa vipofu . Inafanya jambo lile lile lililofanyika kwa Mafarisayo na Masadukayo. Hiyo ndiyo sababu watu wanashindwa kulipata leo hii. Wao Wanasikiliza kile mtu mwingine anachosema juu Yake, badala ya kusikiliza Neno kama vile nabii Wako alivyowaambia wafanye.

Ulisema, kwanza Ninatuma Neno Langu, halafu kama watu hawataamini Neno Langu, basi Ninawapelekea wahudumu. Pia ulisema katika kila wakati wahudumu hupotoka ; si wote, bali wengi wao, na kuwaongoza watu kwao. Sisi tunataka kuwa katika Mpango Wako wa asili.

Inachanganya sana, wahudumu hawawezi kukubaliana wao kwa wao. Ndugu X hawezi kukubaliana na Ndugu Y; Ndugu Y hawezi kukubaliani na ndugu Z. Hawawezi kukubaliana  wao kwa wao. Wanaonekana kukubaliana juu ya jambo moja tu, hatupaswi kucheza kanda kanisani.
Ni Babeli tena, inachanganya sana. Tunaamini kuna Mchoro mmoja tu na ni lazima tujichonge wenyewe ili kueneana na Mchoro huo, sio kujaribu kukata Mchoro huo ili utuenee.

Kumekuwa na huduma nyingi sana ambazo zimeibuka na mawazo yao wenyewe, fasiri zao wenyewe na mafundisho. Wote wamekuwa si kitu. Kumekuwa na wahudumu wakubwa waliowekwa wakfu waliyoinuka wanaosema wanahubiri na kunukuu Ujumbe wa wakati huu, na huduma yao ndio Njia iliyoandaliwa na Mungu kwa ajili ya wakati huu, na sio kanda.

Wana watu waaminifu wanaoenda kwenye makanisa yao, wakiwasikiliza kwa miaka mingi. Wana wahudumu wengi wanaowatembelea, mikutano, miamsho, mahubiri, wakisema wanachosema wao ndio Njia Yako iliyoandaliwa, na sio kanda. Ndipo siku moja wanasema, Ujumbe huu si kweli.

Je, hawakuwa wanachunguza alichokuwa anasema kwa kutumia kanda hizo? Je! walikuwa wakichukua tu kile alichosema kuwa ni Neno, Njia iliyoandaliwa na Mungu kwa ajili ya wakati huu? Kama angalizicheza kanda, Sauti Yako iliyothibitishwa kwa watu, badala yake wao wenyewe wakijiweka kama sauti iliyo muhimu sana, wangejua waliyekuwa wakimsikiliza ni mpakwa mafuta wa uongo katika mafundisho ya wakati wa mwisho.

Hiyo haimaanishi kuwa huhitaji mchungaji. Haimaanishi wote ni wachungaji watiwa mafuta wa uongo. Hilo Halimaanishi kuna wengi wanaohubiri kile hasa Ndugu Branham alichosema. Bali inamaanisha jambo lililo muhimu sana unalopaswa kusikia ni Ujumbe uliyo kwenye kanda; Ndio BWANA ASEMA HIVI PEKEE.

Ni Mwongozo. Ni Yakini. Ni Neno la mwisho. Ndilo Neno Kamilifu pekee. Isipokuwa mchungaji, kiongozi wako wa kiroho, anasikiliza Neno hilo safi pamoja na watu wake, kuna kitu kitaenda kombo.

Kwa nini wahudumu hawataki kucheza Sauti Yako iliyothibitishwa katika makanisa yao? Wanawezaje kusema ni makosa huku wanadai wanaamini kuwa ni Neno? Kwa nini wanatoa kila aina ya visingizio na kusema huduma yao ndiyo Njia Yako iliyoandaliwa kwa ajili ya Wakati huu, na sio Sauti Yako iliyothibitishwa kwenye kanda?

Kwa nini wanawatisha watu kwa kusema kwa sababu tunasema “BONYEZA PLAY” ili kuisikia Sauti yako, tunamwabudu mtu na sio Wewe unenaye kupitia mtu huyo?

Sisi tunakuabudu WEWE TU BABA. Tunalikagua kwa Neno lako tena na tena. Unatuambia kupitia nabii Wako kwa kila Ujumbe tunaosikia kwenye kanda: Ndiyo Njia Yako pekee iliyoandaliwa kwa ajili ya Wakati huu.

Wapi pengine ambapo Bibi-arusi Wako angeweza kwenda isipokuwa kuongoza moja kwa moja kwenye Neno Lako. Sisi ni Bibi-arusi- Neno Bikira wako. lazima tudumu na Nguzo Yako ya Moto. Ndipo mahali pekee tunapoweza kuridhika na kusema amina kwa kila Neno tunalosikia.

Baba, tunakuona Wewe ukiwa nje ya kanisa lako ukijaribu kuingia ndani, na hilo linaivunja mioyo yetu. Komeo liko kwa ndani nasi tumekufungulia mlango uingie. Hatujui kitu kingine . Hatutaki kitu kingine. Hatuwezi kuchukua kitu kingine. Tumetiwa mimba na Neno lako.

Asante Baba kwa Ufunuo wa Neno Lako. Hatumpingi yeyote, tuko kwa ajili ya Neno lako tu lililodhihirishwa na unabii. Tutasimama mbele zako siku moja kwenye hukumu. Kwa mioyo yetu yote tunataka kusema, “Baba, tumedumu na Neno Lako.”

Mtie moyo mchungaji wako, kiongozi wako wa kiroho, Kubonyeza Play Jumapili hii kusikia Sauti ya Mungu. Utahukumiwa siku moja kwa yale Neno la Mungu lisemayo kwenye kanda. Unawezaje kukipa nafasi kitu kingine cho chote?

Umealikwa kuja kuuungana nasi Jumapili hii saa 06 :00 SITA MCHANA , saa za Jeffersonville, ( Ni saa 2:00 MBILI USIKU ya Tanzania na Kenya pia ), kusikia: Matukio Yakidhihirishwa Na Unabii 65-0801e , Mungu anapozungumza kupitia midomo ya mtu aliyejichagulia. Yule ambaye alimpa tabaka yake, karama zake. Alimpa tabia yake, mwenendo wake, na cho chote kile, jinsi anavyojieleza, cho chote afanyacho. Yeye Alimfanya William Marrion Branham mtu wa wakati huu ili kuwashika watu wa wakati huu, nasi ndio WATU WA WAKATI HUU.

Ndugu. Joseph Branham

Maandiko Ya Kusoma Kabla Ya Kusikiliza Ujumbe :

Mwanzo 22:17-18
Zaburi 16:10 / Sura ya 22 yote / 35:11 / 41:9
Zekaria 11:12 / 13:7
Isaya 9:6 / 40: 3-5 / 50:6 / 53:7-12
Malaki 3:1 / sura ya 4 yote
Yohana Mtakatifu 15:26
Luka Mtakatifu 17:30 / 24:12-35
Warumi 8:5-13
Waebrania: 1:1 / 13:8
Ufunuo: 1:1-3 / Sura ya 10 yote