22-1211 Ni Kuchomoza Kwa Jua

Ujume: 65-0418M Ni Kuchomoza Kwa Jua

PDF

pakua – m4a

pakua – amr 14MB (use Firefox to download)

BranhamTabernacle.org

Mpendwa Hekalu la Nguvu za Utendaji ,

Mwanadamu daima ametamani moyoni mwake kuwa kama Ibrahimu alipokuwa ameketi nyumbani kwake karibu saa 11:00. Aliiinua macho na kuwaona wanaume watatu wakija kwake wakiwa na vumbi kwenye mavazi yao. Akawakimbilia upesi, na kusema, “Bwana Wangu.” Aliyesimama pale mbele zake, katika mwili wa mwanadamu akinena, alikuwa ni Melkizedeki Mkuu.

Jumapili hii, shauku hiyo katika mioyo yetu itatimia kwa kila mmoja wetu. Sisi sote tutakusanyika pamoja kutoka ulimwenguni kote, tukimsikiliza Melkizedeki yule yule mkuu akizungumza NASI. Mtu ambaye hakuwa na baba, wala mama, hana mwanzo wa siku zake au mwisho wa uhai, Mungu,  en morphe , akizungumza nasi kupitia midomo ya mwanadamu, kama jinsi Alivyofanya siku hiyo kwa Ibrahimu.

Hakuna njia nyingine ya kusikia Sauti hiyo isipokuwa UBONYEZE PLAY. Hakujawahi kuwa na wakati katika historia ambapo Bibi-arusi ameungana kutoka kote ulimwenguni kuisikia Sauti ya Melkizedeki ikinena kwa wakati huohuo mmoja . Mungu anamuunganisha Bibi-arusi Wake kwa Sauti hiyo.

Tumekuwa, kwa miaka, na Neno la Mungu. Sasa tunaye Mungu wa Neno, mnaona, na papa hapa akiliishi Neno Lake. Kwa hiyo ni kweli, moja ya ishara kuu za mwisho zilizoahidiwa Kanisa kabla ya Kuja kwa Bwana.

Jumapili hii, Bibi-arusi atakuwa na Ujumbe wa Pasaka Desemba hii; na ni Ujumbe ulioje tutakaosikia.

Mitambo. Nguvu za utendaji. Nguvu za kuhuisha. Kristo aliyefufuka. Wana wa Mungu Waliodhihirishwa. Roho yule yule aliyekaa ndani ya Kristo anakaa ndani yetu. Uhai ule ule, nguvu zile zile, baraka zile zile, alizokuwa nazo, tunazo. Hati ya kumiliki. Ile Mbegu ya kwanza iliyopevuka inatikiswa mbele ya watu. Sisi sasa tu nyama ya nyama yake, mfupa wa mfupa Wake; uhai wa uhai wake, Nguvu za Nguvu Zake! Sisi ni Yeye!

Yesu Kristo aliyefufuka; Melkizedeki Mwenyewe, atatoa mlio na kutuambia, “Nilirekodi Sauti yangu na kuiweka kwenye kanda ya sumaku ili niweze kuwavuta ninyi kwangu, nami ningeweza kusema nanyi kama vile nilivyomfanyia Ibrahimu. Ninawataka msikie moja kwa moja kutoka Kwangu .”

Ninyi ndilo Kanisa langu lililochaguliwa na kukusudiwa tangu zamani! Miili yenu ni hekalu la Nguvu za Utendaji , kwa sababu tangu mwanzo mlikuwa sehemu ya ile Mitambo.

Huo ni ule ufunuo wa Kiungu wa Neno lililofanyika mwili. Kama lilikuwa mwili katika siku hiyo kwa njia ya Mwana, Bwana Arusi, ni mwili leo kwa Bibi-arusi. Mnaona?

Hizo Nguvu za Kuhuisha zinaishi ndani yetu. Hatupaswi kuogopa KITU. Roho yule yule aliyekuwa ndani Yake, sasa yu ndani yetu na anaihuisha miili yetu ipatikanayo na mauti. Hatutumaini hivyo, TUNAJUA HIVYO. Tayari tumefaulu, yeye alifaulu kwa ajili yetu.

Kisha, ili kuhitimisha alasiri, Melkizedeki atazungumza kwa mara nyingine tena na kusema;

Watu hawa, ambao ni raia wenzangu wa Ufalme, wenye kumiliki Nguvu za kuhuisha, lihuishe kwao, Bwana, sasa hivi . Naomba Roho aende kutoka tai hadi tai, kutoka kwenye Neno hadi Neno, mpaka utimilifu wa Yesu Kristo udhihirishwe katika kila mmoja wa hiyo miili, kwa ajili ya haja za kimwili, za kiroho, ama haja zo zote walizo nazo, tunapowekeana mikono. Katika Jina la Yesu Kristo.

Kutoka tai hadi tai, Neno hadi Neno, utimilifu wa Yesu Kristo utadhihirishwa katika kila mmoja wa miili yetu. UTUKUFU!!

Hili linaweza tu kutukia kwa KUBONYEZA PLAY, kwa hivyo njoo uungane nasi na ushiriki katika Yubile ya mlo bora wa Chakula kilichohifadhiwa , tunaposikia Sauti Hiyo, Jumapili saa 6:00 SITA MCHANA , saa za Jeffersonville, ( ni saa 2:00 MBILI USIKU ya Tanzania ) ikituletea Ujumbe, Ni Kuchomoza Kwa Jua 65-0418M .

Ndugu. Joseph Branham

Maandiko ya kusoma Kabla ya Kusikiliza Ujumbe :

Mambo ya Walawi 23:9-11
Mathayo 27:51 / 28:18
Marko 16:1-2
Luka Mtakatifu 17:30 / 24:49
Yohana Mtakatifu 5:24 / 14:12
Matendo 10:49 / 19:2
Warumi 8:11
1Wathesalonike 4:16
Waebrania 13:8
Ufunuo 1:17-18