22-1218 Je! Mungu Hubadilisha Nia Yake Kuhusu Neno Lake?

Ujume: 65-0418E Je! Mungu Hubadilisha Nia Yake Kuhusu Neno Lake?

PDF

pakua – m4a

pakua – amr 13MB (use Firefox to download)

BranhamTabernacle.org

Wapendwa Masihi Wadogo,

Sisi ni watiwa-mafuta wa Mungu; waliotiwa mafuta na Roho Wake yule yule, kwa kazi zile zile, kwa Nguvu zile zile, kwa ishara zile zile. Imetoka tai hadi tai, kutoka Neno hadi Neno mpaka utimilifu wa Yesu Kristo udhihirishwe katika kila mmoja wa miili yetu kwa hitaji la kimwili , kiroho, au hitaji lolote tunalohitaji. Hizo Nguvu za kuhuisha zinaishi na kukaa ndani yetu. Sisi ni Masihi wadogo wa Mungu.

Kila wiki Ufunuo wa Ujumbe huu; sisi ni nani, wapi tunatoka, na wapi tunakoenda, unakuwa mkubwa zaidi na zaidi. Twajiuliza kwa matarajio makuu, lawezaje kuwa tukufu zaidi? Laweza kuwa wazi zaidi kiasi gani? Lakini kwa kila kanda mpya tunayosikia, Mungu ananena nasi mdomo kwa sikio na kutufunulia zaidi Neno Lake, na kutuhakikishia, SISI NI NANI.

Shauku kubwa ya moyo wa kila mwamini ni kuwa katika MAPENZI MAKAMILIFU ya Mungu. Kamwe hatutaki kuwa katika mapenzi Yake ya kuruhusia. Mioyo yetu huvunjika na kupondeka ikiwa tunahisi tumefanya jambo lolote ambalo litamchukiza. Tunajua Mungu anayo Mapenzi makamilifu, nasi tunataka tu kuwa katika MPANGO WA MAPENZI YAKE MAKAMILIFU.

Katika maisha yangu, nimekuwa na msimamo mkali kwa kusema ninaamini jambo lililo muhimu zaidi ambalo kila mshiriki wa Bibi-arusi analoweza kufanya, washirika na wahudumu vilevile , ni KUBONYEZA PLAY . Ninaamini ndiyo Sauti ya Mungu PEKEE iliyothibitishwa kwa ajili ya Siku yetu ambayo lazima usikie na kutii kila Neno.

Nimesema ninaamini wahudumu wanahitajika kumrudisha Ndugu Branham kwenye mimbara zao na kucheza kanda katika makanisa yao, kwa kuwa Ndiyo Sauti moja muhimu sana iliyopo ambayo watu hawana budi kuisikia.

Nimepokea shutuma nyingi maishani mwangu kwa kuchukua msimamo huu kwa kile ninachoamini kuwa Mpango Wake na Mapenzi yake Makamilifu. Imeeleweka vibaya na kusemwa kwamba siamini katika huduma tano ya Waefeso 4.

Nimeeleza mara nyingi, nyingi sana huo ni uongo. Sijawahi kamwe kusema, wala sijawahi kuamini jinsi hiyo. Kuna wengi ambao wamepindisha maneno yangu na kuwaambia watu mambo ambayo sijawahi kusema ama kuamini, lakini hilo ni jambo la kutarajiwa.

Lazima kuwe na Kweli ya Neno la Biblia. Ikiwa unadai unaamini Ujumbe huu, basi hatuna budi kuchukua yale nabii aliyosema, kwani ndiyo fasiri halisi hasa ya Neno la Mungu. Kwa maana yeye ndiye mfasiri PEKEE wa Neno hilo.

Ikiwa ningewauliza kila mmoja wenu, “Ni nani anayetaka kuwa katika mapenzi makamilifu ya Mungu?”
Kila mmoja wenu angesema, “NDIYO, hiyo ndiyo haja ya moyo wangu.” Hivyo ni lazima tuangalie kwenye kile nabii alichosema ni Mapenzi Makamilifu ya Mungu.

KUMBUKA: Ikiwa Ujumbe huu ulio kwenye kanda si Yakini yako, na huamini kila Neno, ACHA KUSOMA BARUA HII. Kwangu mimi, wewe si mwamini, kwa hivyo sio kwa ajili yako. Mimi Ninaweza tu kukaa na yale Mungu aliyosema kwenye kanda.

Tunataka alichosema Yeye; si kile kanisa lilisema, kile alichosema Daktari Jones, kile alichosema mtu mwingine. Tunataka kile BWANA ASEMA HIVI ilichosema, kile Neno lilichosema.

Inatupasa kujikabidhi wenyewe kwenye mapenzi Yake na kwenye Neno Lake. Hatupaswi Kulitilia swali. Yatubidi Kuliamini tu. Usijaribu kutafuta njia ya kuliepa. Lichukue tu jinsi lilivyo.

Watu wengi wanajaribu kuepa, kupitia njia nyingine. Nawe unapofanya jambo hilo, Mungu atakuwa akikubariki, bali unafanya kazi katika mapenzi Yake ya kuruhusia wala si mapenzi Yake makamilifu, ya Kiungu. Mungu atakuruhusu kufanya jambo fulani, na hata akubariki katika kulifanya, bali hata hivyo si mapenzi Yake makamilifu.

Mungu alimtuma malaika-mjumbe wake wa saba duniani kumwita Bibi-arusi Wake atoke . Tunaamini ilikuwa ni Mwana wa Adamu akijifunua Mwenyewe katika mwili wa mwanadamu. Ni Sauti yenyewe hasa ya Mungu ambayo imerekodiwa na kuhifadhiwa kwa ajili ya Bibi-arusi Wake.

Mungu mwenyewe alimwambia nabii wake, ukiwafanya watu WAKUAMINI , hakuna kitakachosimama mbele zako. Alikuwa ndiye aliyechaguliwa na Mungu kumwongoza Bibi-arusi Wake. Hakuna anayeweza kupachukua mahali pake. Haidhuru ni akina Kora wangapi walioinuka, ama Dathani wangapi, ilikuwa ni William Marrion Branham ambaye Mungu alimwita kumwongoza Bibi-arusi Wake. Huu ndio Mpango wa Mungu na MAPENZI YAKE MAKAMILIFU.

Iwapo watu hawatatembea katika mapenzi Yake makamilifu, Yeye ana mapenzi ya kuruhusia atakayokufanya uende kwayo.

Sasa, Mungu ni mwema…Yeye hutuma Neno Lake . Kama hutaamini Neno Lake, Basi ndipo anaweka katika Kanisa ofisi tano tofauti : Kwanza, mitume, manabii, walimu, wachungaji, wainjilisti. Ni kwa ajili ya kulikamilisha Kanisa.

Kwa hivyo, wahudumu waliinuliwa tu kwa sababu watu katika nyakati zote hawakukubali MPANGO WA MAPENZI MAKAMILIFU ya Mungu; Neno Lake lililonenwa na nabii Wake. Tunapaswa kuamini tu Neno ambalo nabii wa Mungu alilonena. Hatuhitaji mtu mwingine yeyote au kitu kingine chochote.

Basi kazi ya wahudumu ni KUWARUDISHA watu kwenye Mpango wa Mapenzi Yake Makamilifu, ambao ni: KAENI NA HIZO KANDA, KWA MAANA NI MAPENZI MAKAMILIFU YA MUNGU. Kisha weka MPANGO HUO WA MAPENZI MAKAMILIFU mbele zao kila wakati kwa: KUBONYEZA PLAY.

Huna budi kurudi na kuanzia mahali ulipoanzia, ama mahali ulipoachia, na kuchukua kila Neno la Mungu.

Kwa hivyo unapaswa kufanya nini ili uwe katika MAPENZI YAKE MAKAMILIFU : Kubonyeza Play .

Wachungaji wanapaswa kufanya nini ili wawe katika MAPENZI YAKE MAKAMILIFU: Kubonyeza Play.

Nabii wa Mungu alikuwa anafanyaje akienda kwenye mikutano? Kuombea tu wagonjwa, na kila kitu namna hiyo? Angesema mambo kwa njia isiyo dhahiri ambayo kondoo wangesikia, kwa sababu tunajua kile anachozungumzia. Ama kweli, ilikuwa tu ni chambo kwenye ndoano. Aliwaonyesha ishara kama utambuzi, na alijua siri za mioyo yao, ili tu kuwachochea watu. Lakini kisha akasema jambo muhimu zaidi lilikuwa ni :

Muda si muda, kanda inaangukia nyumbani mwao. Imelenga penyewe, basi. Kama yeye ni kondoo, anakuja moja kwa moja Nalo. Kama yeye ni mbuzi, anapiga hiyo kanda teke.

Je, Wewe ni kondoo au ni mbuzi? Kundi dogo la Mungu moyo wake uko kwenye Neno hilo. Tuko katika Mapenzi Yake Makamilifu kwa Kubonyeza Play kwa kuwa huo ulikuwa, na ndio, Mpango wake wa asili.

Kaa moja kwa moja na Neno Lake, maana hilo ndilo litakalotokea mwishoni, lile Neno, Neno kwa Neno. “Ye yote atakayeondoa Neno moja Kwake, ama kuongeza neno moja Kwake!” Halina budi kudumu, Neno hilo.

Ninamshukuru sana Bwana kujua, kwa Ufunuo wa kiroho, ya kwamba niko katika Mapenzi Yake Makamilifu kulingana na Neno Lake. Siongezi fasiri yangu Kwake, ama ufahamu wangu Kwake, bali ninasikia kwa masikio yangu BWANA ASEMA HIVI na Mapenzi Yake Makamilifu ni kitu gani .

Ninakualika uje Ukatafute madini pamoja nasi Jumapili hii saa 6:00 SITA MCHANA , saa za Jeffersonville,(Ni saa 2:00 MBILI USIKU ya Tanzania ) tunaposikia: Je! Mungu Hubadilisha Nia Yake Kuhusu Neno Lake? 65-0418E . Kuna vito vingi vya thamani sana katika Ujumbe huu, utakuwa TAJIRI katika Roho wake Mtakatifu tukimaliza.

Ndugu. Joseph Branham

Maandiko ya Kusoma Kabla ya Kusikiliza Ujumbe :

Kutoka sura ya 19 Yote
Hesabu 22:31
Mathayo Mtakatifu 28:19
Luka 17:30
Ufunuo sura ya 17 yote