21-0822 Kuchagua Bibi-Arusi

Ujumbe: 65-0429e Kuchagua Bibi-Arusi

PDF

pakua – m4a

pakua – amr

BranhamTabernacle.org

Tai wanakusanyika Pamoja.

Mpendwa Bibi-arusi aliyechaguliwa na Mungu,

Baba alimchagua Bibi-arusi Wake kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu. Alitaka Bibi-arusi atakayeonyesha tabia Yake. Alitaka Bibi-arusi ambaye angevutia usikivu Wake kwa kushika Neno Lake.

Bibi-arusi ambaye angejitolea sana Kwake na kwa Neno Lake lililoahidiwa, hata Nia ile ile iliyokuwa ndani Yake ingekuwa ndani yao. Wangekuwa mwili Wake uleule, mifupa ile ile, Roho yule yule, kila kitu kile kile, wamejengwa sawa sawa kabisa mpaka hao wawili wangekuwa Mmoja.

Alitaka kuunda tabia Yake hasa ndani yao, kwa maana Anatakiwa awe kama tu Yeye . Amengojea tangu alipoweka Adamu na Hawa wake wa kwanza duniani ili kumrejesha Bibi-arusi wake mkamilifu. Amekuwa akimfikiria sana, kumrudisha katika Dhihirisho lake kamilifu; kwa maana watakuwa Bibi-arusi _Neno Lililonenwa wake.

Alipomwona bibi-arusi, Alifurahi sana, Hatimaye alikuwa na Bibi-arusi ambaye hatapatana hata kwa Neno moja. Bibi-arusi ambaye hangetilia shaka hata moja wapo ya hilo , bali Atalichukua vile tu lilivyo. Wangeuambia ulimwengu Halihitaji Fasiri yo yote, kwa maana ni Sauti Safi Ya Mungu.

Alipokuwa akimwangalia Mke wake kipenzi mdogo mkamilifu , Alijisifia kwa ajili yake, Ilibidi tu amwonyeshe wazi. Kwa hivyo alimwita malaika wake wa 7 mwenye nguvu, ili aweze Kumkagua huyo bibi-arusi kimbele . Alimtaka amwone bibi-arusi, na amwonyeshe wazi, ili aweze kumwelezea huyo Bibi-arusi jinsi alivyo mzuri. Kwa hivyo angeweza kumtia moyo bibi-arusi na kumfanya atambue kwamba yeye Anamjua bibi-arusi ni nani.

Kwa hivyo Alimchukua malaika Wake na kumweka mahali pa juu ili aweze kumkagua bibiarusi kimbele. Alipotazama, Roho wa Mungu akamwambia kusema, “ Huyo hapo Bibi-arusi.” Akatazama, na akawaona NINYI pale. Moyo wake Ulifurahi.

Kila mmoja WENU alikuwa amevaa vazi la kitaifa la huko ambapo mnakotoka: Uswizi, Ujerumani, kote ulimwenguni, kila taifa. Nywele ndefu zilizotengenezwa vizuri huku nyuma, nguo zenye mikono mirefu, na sketi ndefu Nadhifu. NANYI mlikuwa Mkipiga Hatua Taratibu, ” Twendeni, Askari Wakristo, tukitembea kama waendao vitani.” Alipotazama, Tulianza kupiga hatua hata Angani; Tulikuwa Neno.

Asante Baba. Jinsi gani jambo hilo linavyotutia moyo mioyo yetu leo hii. Tunakupenda wewe na Neno lako kwa yote yaliyo ndani yetu. Tunaamini kila Neno. Ujumbe huu unatutoshea kama glavu mkononi.

Tunataka kuwa Bibi-arusi-Neno wako Mkamilifu. Hatujui njia nyingine ya kufanya jambo hilo ila kukaa na Neno lako, hii manna iliyohifadhiwa uliyomwachia Bibi-arusi wako ili ajifanye Mwenyewe tayari.

Tunaona wakati huo umekaribia. Ulimwengu unatetemeka chini yetu kwa Matetemeko ya ardhi. Malaika wako wapelelezi wote wanazunguka karibu . Ulimwengu umepinduliwa-juu-chini. Vita, mapigano, mauaji, virusi na magonjwa kila mahali. Adui anakasirika bila kukoma, anajaribu kumtesa Bibi-arusi Wako, lakini Mke wako kipenzi aliyechaguliwa yuko THABITI akishikilia Neno Lako.

Tusaidie Baba tusitoke nje ya hatua. Hebu na tukuangalie wewe na kushikilia Mkono Wako usiobadilika. Ongeza IMANI yetu, utupe kile tunachohitaji. Njoo uwe na Bibi-arusi wako Jumapili hii, saa 8:00 Nane mchana, saa za Jeffersonville,( ni saa 3:00 Tatu usiku ya Tanzania) tunapokusanyika kuizunguka Sauti Yako kwa ajili ya siku hii na kukusikia Ukinena: Kuchagua Bibi-arusi 65-0429E.

Haya ni Maombi yetu Baba:

Ee Mungu wa Mbinguni, hurumia ulimwengu wenye dhambi na watu wenye dhambi, Bwana, kama tulivyo usiku wa leo. Mungu, ninajaribu kusimama pengoni na kuomba rehema ya Kiungu, kwamba utalizungumzia kundi hili usiku wa leo na kumhamasisha Bibi-arusi Wako, Bwana, akapige hatua taratibu si kwa ishara za kanuni zozote za imani, bali kwa sauti ya Injili ya Bwana Yesu Kristo. Tujalie, Ee Mungu. Na ijulikane, usiku wa leo, ya kwamba Wewe ni Mungu, na Neno Lako ni Kweli. Huku, kwa uchaji, mbele ya macho ya watu hawa, tunawahamasisha Neno Lako.

Ndugu. Joseph Branham

Mwanzo 24: 12-14
Ufunuo 21: 9