22-0807 Wa Kipekee

UJUMBE: 64-0614E Wa Kipekee

PDF

pakua – m4a

pakua – amr

BranhamTabernacle.org

Mpendwa Bibi-arusi wa Utukufu wa Shekina,

Jinsi gani mioyo na nafsi zetu zilivyoinuliwa hadi kufikia viwango vipya tulipokuwa tumekusanyika pamoja kutoka duniani kote, tukisikiliza Sauti ya Mungu ikizungumza kupitia mjumbe Wake na kutuhakikishia kwa mara nyingine tena, sisi ni nani.

Naye Anajifunika leo, katika vyombo vya udongo, pamoja na Shekina. Nje wanaonekana kana kwamba ni kundi la watakatifu wanaojifingirisha, ngozi za kale za pomboo, lakini ndani yake zinaficha Utukufu wa Shekina.

Utukufu kwa Mungu! Ndani yetu unajificha Utukufu wa Shekina. Tumeenda nyuma ya pazia nasi tunaweza kumwona Kristo waziwazi.

Leo hii, Mungu hatendi kazi akiwa ndani ya mwanadamu, Anatenda kazi kupitia mwanadamu. Yeye Alikuwa akitenda kazi akiwa katika mwanadamu wakati huo, Yesu. Sasa, Yeye anatenda Kazi kupitia mwanadamu ambaye yeye amemchagua kwa kusudi hili. Mungu, katika umbo la mwanadamu; Yeye Alijibadilisha kutoka katika umbo la Mungu, akawa katika umbo la mwanadamu.

Mungu Mwenyewe alijitokeza katika umbo la mwanadamu , kwa uzao wa kawaida wa Ibrahimu, kabla ya yale maangamizi, na Yesu alisema litakuwa ni jambo lile lile kwa Uzao huu wa kifalme kabla ya kurudi kwa Mwana aliyeahidiwa.

Mungu amejitokeza kwa mara nyingine tena katika umbo la mwanadamu, kama alivyoahidi angefanya. Ni Mungu aliyefichwa nyuma ya pazia la mwili uitwao William Marrion Branham. Isipokuwa uende nyuma ya pazia hilo na kuona Mungu, na si mwanadamu, umeukosa mpango wote wa Mungu.

Baadhi ya watu husema, “Ninyi watu mnamfanya Ndugu Branham kuwa mungu”. Vema, jambo hilo liko sawa kwa Namna fulani . Tunajua wanajaribu tu kutulaumu. Tunajua sisi hatukufanya hivyo. Bali pia tunajua hawalifahamu hilo, kwa maana wao wako upande wa pili wa ngozi, hawajaja nyuma ya pazia.

Tunaweza kusema waziwazi, “Vema, jambo hilo haliko mbali sana na Neno la Mungu sivyo? Tunawataka tu wajue kwamba hatujapotea. Tunajua tunaposimama. Tunajua tumetweka matanga ya namna gani, Na ni upepo wa namna gani unaoyavumia. Tunajua Hesi zetu zilivyo, na Nati yetu ni ipi . Nasi tunajua jinsi tunavyosimama.

Mungu alipodhihirishwa ulimwenguni, Yeye alikuwa amejificha nyuma ya pazia, nyuma ya ngozi ya Mtu aliyeitwa Yesu. Yeye alikuwa ametiwa utaji na kujificha nyuma ya ngozi ya mtu aliyeitwa Musa, nao walikuwa miungu, si Mungu ; bali walikuwa Mungu, yule Mungu mmoja, akibadilisha kinyago Chake tu, akifanya jambo lile lile kila wakati, akileta Neno hili.

Tumeingizwa kwenye Neno, Ujumbe na nabii wa wakati huu, na unatuvuta na kutupeleka kwenye Makao yetu ya Mbinguni. Sisi ni Wa Kipekee kwa ulimwengu, lakini Mungu ametutumia Nati ambayo inamtoa Bibi-arusi Wake atoke katika mchafuko huu, imwingize katika Uwepo wa Mungu. Sisi ni nati tuliyotiwa hesi kwa Neno.

Mungu, aliye na ngozi! Linaweza likasikika kama nati, kwa ulimwengu, bali linawavuta watu wote Kwake.

Ujumbe huu ni Mana itokayo Mbinguni, Chakula cha waamini ambacho ni kwa ajili yetu tu, nacho Kinamvuta Bibi-arusi Wake Kwake. Utukufu wa Shekina, juu ya Mkate wa Wonyesho, uliufanya usiharibike.

Mungu ameandaa Njia kwa ajili ya siku hii, Ujumbe huu na mjumbe wake; Mungu aliyefunikwa Aliye na ngozi . Sasa ni Mungu akijificha Mwenyewe ndani yetu, Bibi-arusi Wake, anayeweza tu kujilisha Sauti safi ya Mungu iliyothibitishwa na Nguzo ya Moto.

Sisi Hatupingani na huduma tano, Mungu apishe mbali, Mungu amewaita kuhudumu. Wanafuata na kufanya jinsi Roho Mtakatifu anavyowaongoza. Na sisi Tunafanya tu jinsi Roho Mtakatifu anavyotuongoza kufanya naye anatuongoza na kutuelekeza kushikilia hizo kanda peke yake.

Kwa hiyo, sasa , sikiliza kila Neno . Likamate. Na—na iwapo mnaunasa Huo kwenye kanda, ama cho chote kile , basi shikilieni kabisa Mafundisho hayo ya kanda . Msiseme kitu ila kile kanda hiyo inachosema. Semeni tu yale hasa kanda inayosema .

Kwetu sisi, NJIA PEKEE YA KUSIKIA: “KILA NENO,” “ SI KINGINECHO BALI YALE KANDA ZINACHOSEMA,” “ YALE HASA KANDA ZINACHOSEMA,” NI KUBONYEZA PLAY NA KUZISIKILIZA KANDA.

Kwa hiyo tunakualika uje kusikiliza yale hasa kanda zinachosema Jumapili saa 06:00 SITA MCHANA , saa za Jeffersonville, ( Ni saa 1:00 MOJA JIONI Ya Tanzania) na uwe Wa Kipekee pamoja nasi tunaposikia Ujumbe: Wa Kipekee 64-0614E .

Ndugu. Joseph Branham

Maandiko ya kusoma kabla ya kusikiliza Ujumbe :

I Wakorintho 1:18-25
2 Wakorintho 12:11