22-0731 Kufunuliwa Kwa Mungu

UJUMBE: 64-0614M Kufunuliwa Kwa Mungu

PDF

pakua – m4a

pakua – amr

BranhamTabernacle.org

Mpendwa Neno lililoandikwa,

Kila wiki inakua kuu zaidi na zaidi. Jumapili, tulipata fursa ya kutazama, na kuamua, TULIONA NINI? Je, tuliona mhudumu , HAPANA! Je, tuliona mchungaji wetu, HAPANA! Tulipotazama nyuma ya pazia la mwili wa mwanadamu tulimwona Yesu Kristo akijifunua Mwenyewe na kujidhihirisha Mwenyewe.

Wakati tumekuwa tukizisikiliza hizo kanda kama zijavyo, Imekuwa dhahiri zaidi na zaidi, kama unayo masikio ya kusikia na macho ya kuona. Sasa tunamwona Mungu waziwazi. Pazia limepasuka, nasi tunamwona Mungu akisimama waziwazi mbele zetu, Yule Nguzo ya Moto Akijidhihirisha Mwenyewe waziwazi.

Imewapofusha wengine, Lakini kwetu sisi, Imefunua ile Kweli. Mungu amemtukuza mjumbe wake mbele zetu, kama alivyomtukuza Musa.

Hamko nyuma ya pazia hilo tena, enyi Watoto wadogo. Mungu anaonekana wazi kabisa kwenu.

Ni kitu gani? Uungu uliofunikwa katika mwili wa mwanadamu. Mungu, katika umbo la mwanadamu, akijificha Mwenyewe wasimwone. Wanaweza tu kumwona mwanadamu na kusema Nabii wa Mungu anakosea, hata alisema hivyo yeye mwenyewe, akijaribu kuwafundisha watu ya kwamba kuna makosa kwenye hizi kanda . Lakini kwetu sisi, Bibi-arusi Wake Aliyechaguliwa tangu Awali, tunamwona Mungu na kumsikia na hakuna makosa.

Mmoja aliona mwanadamu, huyo mwingine alimwona Mungu. Unaona? Na ilikuwa ni Mungu nyuma ya pazia la mwanadamu, ikiwafanya wote wawili kuwa sahihi, lakini imani yako katika yale usiyoyaona.

Kwetu sisi, tutaamini na kufuata makosa ya nabii wa Mungu aliyethibitishwa, kama kungekuwepo na yoyote , kabla hatujachukua na kuamini Bwana Asema hivi yao.

Musa hakupaswa kuupiga Mwamba mara ya pili. Roho yuleyule angalisema katika siku hiyo, “Ona, Musa anakosea.” Lakini maji yalitoka hata hivyo, na ikiwa hukunywa kutoka kwenye kile kinachoitwa kosa la musa, ulikufa. Ndivyo ilivyo leo hii. Mashtaka mengi sana.

Musa alikuwa na Neno. Sasa kumbukeni, baada ya Neno kudhihirishwa, Musa alikuwa ni Musa tena. Mnaona? Lakini wakati Neno hilo lilipokuwa ndani Yake lipate kutolewa, yeye alikuwa ni Mungu; vema, yeye hakuwa ni Musa tena.

Ndugu Branham alikuwa na Neno. Baada ya Neno kudhihirishwa, Ndugu Branham alikuwa Ndugu Branham tena, Lakini wakati Neno hilo lilipokuwa ndani yake lipate kutolewa kwa watu kwenye kanda, yeye alikuwa ni Mungu; hakuwa Ndugu Branham. Hivyo tunajifunza, yaliyo kwenye hizi kanda ni Maneno ya Mungu, na hakuna makosa katika Maneno ya Mungu.

Sisi sio tu kwamba tunaliamini, bali tunaliishi. Wakati hao wengine wote wanaliondokea, sisi tunadumu Nalo! Tunaliamini! Haijalishi kile mtu ye yote anachofanya ama anachosema , sisi tunaliamini na kisha tunalitendea kazi. Kama wewe hufanyi hivyo, basi huliamini.

Nasema vivyo hivyo katika Jina la Yesu Kristo. Usiongeze kitu. Usiondoe—kuliwekea mawazo yako. Wewe sema tu yaliyosemwa katika kanda hizo. Tenda sawasawa kabisa na vile Bwana Mungu amekuamuru kutenda. Usiongezee Kwake!

Bonyeza play na uamini KILA NENO kama vile Mungu alivyotuamuru kutenda. Ni Mungu akinena mdomo kwa sikio na Bibi-arusi Wake.

Mbele za watu, Mungu alijitia utaji tena na kumthibitisha Musa, kwa utaji, kwa kujitia utaji kwa Moto ule ule, Nguzo ile ile ya Moto ilishuka. Tangu—tangu wakati huo…Kutoka kwao, kwa hiyo wangeweza tu kusikia Neno la Mungu. Mnalipata? Neno pekee, waliisikia Sauti Yake. Kwa kuwa, Musa alikuwa, kwao, Neno lililo hai .

Mungu habadilishi, na hawezi kubadilisha mpango Wake. Yeye Ni Yesu Kristo yeye yule jana, leo na hata milele. Kwa hiyo, kwetu sisi, nabii Wake aliyethibitishwa, William Marrion Branham ndiye Sauti yetu ya Mungu, na Neno lililo Hai la wakati wetu.

Sasa si Neno tu lililoandikwa kwetu, ni kitu halisi. Tuko ndani Yake. Sasa tunafurahia. Sasa tunamwona Yeye. Sasa tunamwona, lile Neno, akijidhihirisha Mwenyewe. Limefichwa, huko nje, kwa sababu (kwa nini?) Limetiwa utaji katika mwili wa binadamu. Mnaona?

Haidhuru nini, wao hawalioni. Kwa nini? Haikutumwa kwao .

Kwa sababu unaliona, je, uko tayari kumsikia yeye akikuambia kwa mara nyingine tena WEWE NI NANI? Anapotazama chini kutoka kwenye ngome za Utukufu na kukuona, Yeye Anamwona nani?

* Ninaona Neno likidhihirishwa. Yale aliyosema angeyafanya katika siku hizi za mwisho, ninaliona likikua. Ninaona watoto wakila huo Mkate wa Shekina unaotoka kwenye kule kuiva kwa hilo Neno, ambao wanaliamini. Amina!

* Basi, sisi, ndipo tunakuwa sehemu Yake, kwa kuwa wewe ni utaji unaomficha Yeye. Wewe ni sehemu Yake, mradi Kristo yumo ndani yako, kama vile Kristo alivyokuwa wa Mungu. Kwa kuwa Mungu alikuwa ndani Yake, ilimfanya Mungu. Na kwa kuwa Kristo yumo ndani yako, tumaini la Utukufu, unakuwa sehemu ya Kristo.

* “Ninyi,” Hilo lilisema, “ninyi ni nyaraka zilizoandikwa,” ama, “ninyi ni Neno, ambalo limeandikwa, lililodhihirishwa,” hakuna kitu kinachoweza kuongezewa Kwake. Huwezi kusema, “Mimi ni waraka ulioandikwa,” na kuishi namna nyingine mbali na vile Hii imeandika tayari, kwa maana hakuna kitu kinachoweza kuongezwa wala kuondolewa .

Jina la Bwana Yesu Kristo litukuzwe. YEYE ANATUONA SISI. SISI TUNAMWONA YEYE. Sisi ni Neno Lake lililodhihirishwa leo hii.

Njoo uungane nasi Jumapili saa 06:00 SITA MCHANA , saa za Jeffersonville, (Ni Saa 1:00 MOJA JIONI Ya Tanzania), Mungu akisimama mbele zetu; ile Nguzo ya Moto ikiwa imefichwa katika mwili wa mwanadamu, nayo inazungumza nasi Neno tunalopaswa kuishi kwalo katika siku hii. Ni Utukufu wa Shekina unaotuivisha. Mkate wa Wonyesho kwa mwamini.

Kufunuliwa Kwa Mungu 64-0614M

Ndugu. Joseph Branham

Maandiko ya kusoma kabla ya kusikia Ujumbe:

Mathayo 24:24
Luka Mtakatifu 17:28-29
Yohana Mtakatifu 14:14
1 Wakorintho 12:13
2 Wakorintho 3:6 – 2 Wakorintho 4:3
Wafilipi 2:1-8
1 Timotheo 3:16
Waebrania 13:8
Ufunuo 10:7 & 19:13
Kutoka sura ya 19 yote & sura ya 20 yote
Yoeli 2:28
Malaki 4:5