24-0218 Kufunuliwa Kwa Mungu

UJUMBE: 64-0614M Kufunuliwa Kwa Mungu

PDF

pakua – m4a

pakua – amr

BranhamTabernacle.org

Mpendwa Bibi-arusi Aliye Nyuma ya Pazia,

Kwa nini ninaendelea kuwaambia tena na tena, “KUBONYEZA PLAY ndilo jambo lililo muhimu zaidi mnalopaswa kufanya”? Kwa nini ninaendelea kuwaambia wachungaji, “Mrudisheni Ndugu Branham kwenye mimbara zenu”?

Ni rahisi tu namna hii. Kule kuisikiliza Sauti ya malaika-mjumbe wa saba kwenye kanda, ni kusikiliza NENO LILILO HAI.

Mbele za watu, Mungu alijitia utaji tena na kumthibitisha Musa, kwa utaji, kwa kujitia utaji kwa Moto ule ule, Nguzo ile ile ya Moto ilishuka. Tangu—tangu wakati huo…Kutoka kwao, kwa hiyo wangeweza tu kusikia Neno la Mungu. Mnalipata? Neno pekee, waliisikia Sauti Yake. Kwa kuwa, Musa alikuwa, kwao, Neno lililo hai.

Nena kuhusu Mhudumu aliye Hai! Sauti tunayoisikiliza kwenye kanda ndio Sauti ya Neno lililo Hai la siku yetu. Hakuna nyingine iliyo kuu kuliko Hiyo.

Katika siku za Musa, ni wana wa Israeli tu waliokuwa kambini ndio wangeweza kuisikia Sauti Yake. Lakini leo, Mungu alitaka ULIMWENGU uisikie Sauti Yake, KWA HIYO AKAIREKODI KWENYE KANDA, ili Bibi-arusi Wake aweze kuisikia Sauti ya Neno lililo Hai.

Mungu alikuwa amejificha nyuma ya pazia la nabii Wake, apate kuwaambia Neno Lake. Hilo ndilo alilokuwa amefanya. Musa alikuwa ndiye hilo Neno lililo hai kwa watu, lililotiwa utaji kwa Nguzo ya Moto.

Kama huna Ufunuo wa jambo hilo kwa ajili ya siku yetu, huwezi kuwa Bibi-arusi wa Yesu Kristo. Kama unao, basi wewe NI Bibi-arusi wa Yesu Kristo na itakubidi kusema, “hakuna jambo lililo muhimu zaidi kuliko kuzisikiliza kanda, kwa maana ni Sauti ya Mungu ikinena nawe mdomo kwa sikio.”

Wengi wanajaribu kuwatisha watu na kusema tunamsifu sana nabii; tunamuabudu. Enyi marafiki, Yeye ndiye aliyesema mambo haya, si mimi. Mimi nina nukuu tu Neno.

Kama ilivyofanyika katika kila wakati, Uungu ukitiwa utaji katika mwili wa binadamu. Angalieni, Yeye alifanya hivyo. Manabii walikuwa ni Uungu, umetiwa utaji. Walikuwa ni Neno la Mungu (hiyo ni kweli?) lililotiwa utaji katika mwili wa binadamu. Kwa hiyo wala hawakumwona Musa wetu, mnaona, Yesu.

Hatumwabudu mwanadamu, bali Mungu, Ambaye ametiwa utaji na anayejifunua Mwenyewe kupitia nabii. Ili kuelewa na kuamini hilo, yakubidi ufanye hivi.

Hamko nyuma ya pazia hilo tena, enyi Watoto wadogo. Mungu anaonekana wazi kabisa kwenu.

Hatuko nyuma ya pazia hilo tena, tunaweza kuona Ni Mungu anayejifunua Mwenyewe waziwazi. Imefunuliwa ya kwamba kusikiliza Sauti hiyo kwenye kanda ni Mungu akizungumza na Bibi-arusi Wake. Tunaamini ndiyo Njia Yake iliyoandaliwa kwa ajili ya siku hii.

Tunaweza tu kusema AMINA kwa Sauti hiyo, si kingine. Sauti hiyo itahubiri, itafundisha na kutufunulia kila kitu tunachohitaji kujua. Sauti hiyo itatutambulisha sisi kwa Bwana wetu Yesu Kristo. Sauti hiyo ndiyo yote tunayotaka na tunayohitaji.

Tunashukuru kwa huduma 5 ambayo Mungu anayoitumia kuwaelekeza watu kwenye Sauti hiyo; kwa ajili ya wachungaji ambao wamelipata lile ono na walio na ufunuo kwamba kuzicheza kanda katika makanisa yao ndilo jambo kubwa sana wanaloweza kufanya kwa ajili ya watu wao.

Tunawaalika mje msikilize pamoja nasi ile Sauti yenye nguvu ya Neno lililo Hai Jumapili hii saa 06:00 SITA MCHANA, saa za Jeffersonville,( ni saa 2:00 MBILI USIKU ya Afrika Mashariki ) tunapoisikia ikifunua:  Kufunuliwa Kwa Mungu 64-0614M.

Ndugu. Joseph Branham